Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Moja ( 21 )

0
0
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Yaani kaka yangu hapa sijui nifanyaje nimeomba ruhusa ya kumuuguza mume wangu ila hata hamu ya kwenda huko hospitalini sina”
Habibi alizungumza huku taratibu akijisogeza nilipo huku akiendelea kulia na taratibu kichwachake akakilaza kwenye mapaja yangu na mkono wangu mmoja nikauweka kwenye ziwa lake na kuliminya kumfanya astuke na kunitazama kwa jicho kali la hasira

 ENDELEA
“Ohh samahani dada yangu”
Nilizungumza huku nikiutoa mkono wangu kwenye ziwa lake na taratibu Habiba akajinyanyua kutoka alipo jilaza kwenye mapaja yangu na kukaa kitako
“Samahani tena dada yangu kwa kukushika......”
“Usijali kaka yangu ila kwa sasa ninaomba mimi niondoke”
“Sawa hakuna shaka”

“Naomba unipe namba yako ya simu”
Nikamtajia Habiba namba zangu kisha na yeye akataja zake nikajaribisha kuzipiga kabla hajatoka na simu yake ikaita
“Kaka hivi nisave nani?”
“Save Eddy”
“Mmmmm”
“Mbona unaguna”
“Yaani majina ya Eddy sina imani nayo kabisa tangu mume wangu aniafanyie hili tukio nimetokea kuyachukia kupita maelezo”
“Kwani anaitwa nani?”
“Ana mjina mbaya kama huo wako wa EDDY”
    Nikabaki nikicheka Habiba akajiweka sawa nguo zake na kutoka chumbani na kuniacha nikijiliaza chali kitandani huku nikiikariri namba yake kwa kwichwa ili isiwe rahisi kuisahau.Nikanyanyuka na kufunga mlango kwa funguo kisha nikarudi kitandani huku nikijitahidi kuutafuta usingizi kwa juhudi zote.

Nikachukua mto mmoja nikaukumbatia huku nikiuwekea mguu kwa juu ndani ya dakika tano nikaanza kuhisi nilicho kikumbatia sio mto ila kinaendana na umbo la mtu.Nikakurupuka na kujitoa mikononi mwa msichana mzuri aliye kaka kitandani huku akiwa na night dreas tu na katika kumbu kumbu zangu nilimuona huyu msichana siku yangu ya kwanza alipo nitokea Olvia Hitler na alikuwa ni miongoni mwa wasichana aliye kuwa akimpepea na kitu kinacho fanana na mkia wa Simba
“Usiniogope kwani sikuja kwako kwa mabaya”
“Wewe ni nani?’
“Unanfahamu ila itanibidi nijitambulishe jina langu”
“Sasa jamani mutanniua mimi”
“Huwezi kufa.....kwanza mimi ninaitwa Vicky ni jina ninalo litumia nikiwa ulimwenguni ila nikiwa nyumbani nina jina langu”
Sikuweza kuogopa sana kutokana nimesha wazoea hawa viumbe ambao wananiandama tangu nilipo hamia katika nyumba yangu mpya

“Mtakatifu Olvia Hitler amenituma nije kukupa ujumbe huu”
“Ujumbe gani?”
“Yeye kwa sasa hayupo katika maeneo unayo ishi amekwenda nchini kwetu kwa ajili ya mazungumzo na baba yake mzazi”
“Haya nashukuru.....Jibadilieshe na uniachie mto wangu”
“Hapana kuna kitu nahitaji kutoka kwako”
    Vicky akanifwata kwa kasi na ndani ya dakika moja nikajikuta nipo kama nilivyo zaliwa kisha taratibu akaanza kuninyonya mdomo wangu hapo ndipo nikagundua ladha iliyopo kwenye mate ya mwanadamu na jini.Vicky akaivua nightdreas yake na kuimalizia nguo ya ndani kisha akanipandisha kitandani
“Unataka unione kama nani?”
“Kivipi?”
“Unataka unione katika muonekano kama wa  msichana gani unaye mpenda duniani?”
“Mmmmmm Angelina Jolie”
Ndani ya sekunde kadhaa Vicky akageuka na kuwa kama Angelin Jolie mwan mke mwenye mvuto wa kudumu duniani ambaye ni mcheza filamu maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla na nikabaki nimeduwaa

 

Katibu Mkuu CHADEMA aongoza Viongozi Wenzake Kuripoti Polisi

0
0
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na viongozi wengine wa chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi leo asubuhi Machi 5, 2018.

Februari 27, 2018 viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye leo hayupo kwa maelezo kuwa ni mgonjwa, walifika kituoni hapo na kuhojiwa kwa takribani saa tano, kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena leo.

Viongozi hao wakiongozwa na Dk Mashinji ambaye Februari 27, 2018 hakufika kuhojiwa kutokana na kuwa nje ya nchi, mpaka saa 2:15 asubuhi walikuwa wamewasili wote kituoni hapo.

Mbali na Mashinji, viongozi wengine waliofika kituoni ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Viongozi hao wameambatana na wakili Frederick Kihwelo na Alex Massaba pamoja na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.

Massaba amesema kuwa Mbowe hatoweza kufika kwa kuwa ni mgonjwa.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 23 na 24)

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                       
ILIPOISHIA  

Raisi alizungumza kwa kubabaika sana, kitendo kilicho nishangaza hata mimi mwneywe.
“Hapana dhiara yoko iwe pale pele muheshimiwa, ila ninacho kuomba uweze kuondoka Dar es Salaamu kupitia botii usiku wa leo. Ondoka na walinzi wako unao waamini ukisha fika Tanga mimi ndio ninakaye kupokea katika ufukwe wa Mwambani”
“Sawa sawa kijana nitafanya hivyo na msafara wangu wa kesho je?”
“Awepo raisi feki ambaye anaweza hata kuvalishwa sura ya bandia”
“Basi nitafanya hivyo kijana asante sana na Mungu akubariki”
“Asante muheshimiwa”
Simu ikakatwa, Olvia Hitler akaachia tabasamu pana kisha akanyanyuka kitandani na kunisokela sehemu nilipo simama, akalifungua taulo langu na kunishika jogoo wangu na kumninya taratibu, kitu kilicho ufanya mwili wangu mzima kusisimka kupita hata nilivyo wahi kushikwa na mwanamke yoyote kwenye maisha yangu.

ENDELEA
“Unajisikiaje?”
Olvia Hitler aliniuliza kwa sauti laini huku akiendelea kumchua jogoo wangu.
“Ra…rahaaa”
“Ok baadae kafanye kazi kwanza”
Olvia Hitler akaniachia na kusogea pembeni yangu, tukatazamana kwa sekunde kadhaa kisha akaotoka mlangoni pasipo kuufungua, kitendo kilicho nishangaza sana. Nikabaki nikiwa nimesimama kwa sekunde kadhaa huku macho yakiwa yamenitoka nikikilifikia tukio  la Olvia Hitler kutoka kwenye mlango huu. Mlio wa simu yangu ndio ukanistua na kujikuta nikiitazama ni nani anaye piga. Nikakuta ni K2, nikashusha pumzi nyingi kisha nikaipokea simu.

“Dany za asubuhi mpenzi wangu?”
“Salama za kwako?”
“Safi vipi kuna taarifa yoyote ambayo imetokea?”
Nikataka kumuambia ndio, ila nikasita kidogo na kufikiria, kitu ambacho nimekizungumza na raisi.
“Dany”
“Eheee”
“Vipi mbona kimya?”
“Ahaa hakuna kitu, kidogo usingizi ndio unanipitia pitia hapa”
Ilinibidi kuongopea japo usiku mzima sikuweza kulala, ila uchovu wangu wote umweweza kuniondoka kutokana na maajabu niliyo weza kuyaona kwa mara yangu ya kwanza kwenye maisha yangu.
“Ahaa ina maana bado umelala mpenzi wangu?”
“Yaa baby, nimechoka sana. Ila hakuna kitu kilicho jitokeza”
“Ok sawa ngoja nikuache upumzike kipenzi changu mwaya”
“Asante sana baby”   

“I love you Dany”
“I love you too baby”
K2 akakata simu na kujikuta taratibu nikikaa kitandani huku kichwa changu kikiandamwa na mawazo ni kitu gani ninaweza kukifanya kuingia katika ofisi ya Meya na kuichukua Nyaraka ambazo ni mali ya mama. Sikuona kama ninaweza kuendelea kukaa hotelini hapa, nikaingia bafuni na kuchukua tisheti yangu ambayo bando ni mbichi. Nikaivaa hivyo hivyo japo nina tambua ina madhara kwenye kidonda changu mgongoni, nikaivaa suruali yangu, pamoja na viatu. Nikachukua kila kilicho changu ndani ya chumba hichi na kutoka.

Nikaeleka sehemu nilipo liacha gari la mama, nikafungua na kuingia. Nikaondoka hotelini hapa taratibu na kuanza kueleka katika ofisi za Meya zilipo. Uzuri wa jiji la Tanga, hakuna magari mengi kiasi cha kufanya kuwa na foleni kama Dar es Salaam. Sikuchukua muda mwingi  kuweza kufika katika ofisi za meya huyo.

Nikaisimamisha gari yangu mbali kidogo na ofisi hiyo kwa mana gari hili ni la mama na nina hisi kwamba ni watu wengi wanalifahamu, japo yapo mengi hapa mjini ila mtu anaweza kufahamu namba za usajili wa gari. Kabla sijashuka simu yangu ikaita na kukuta ni mama, nikaipokea na kuiweka sikioni huku nikiacha gari likiwa bado linawaka.

“Shikamoo mama”
“Marahaba, umefikia wapi?”
“Sasa kuna kazi nina ifanya nitakufahamisha”
“Sawa, ila nataka kwenda ofisini leo kuna kikao cha maandalizi ya mwisho ya kumpokea raisi”
“Mmmm, huoni kama inaweza kuwa ni hatari kwako?”
“Hapana haiwezi kuwa na hatari, kwa maana nitatumia gari la baba yako mkubwa hapa”
“Sawa mama kuwa makini, na usiache kunitaarifu kwa chochote kitakacho endelea na nyaraka zako by saa nne nitakuwa nazo”
“Nitakushukuru sana mwangu, kwa maana hapa ninakwenda ofisini ila sina hata amani”
“Usijali mama kila kitu kitakuwa salama”
“Sawa, ila kuwa maniki Dany, usije na wewe ukaingia kwenye matatizo”
“Usijali hilo mama yangu”
“Ok asubuhi nje”
“Nawe pia mama”
Nikakata simu, nikazima gari na kuchomoa funguo. Nikashuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea kwenye ofisi hizo za Meya, kwa bahati nzuri nikamkuta msichana ambaye amevalia mavazi ya sectretary akifungua ofisi hiyo.

“Habari yako dada”
“Salama, kaka habari ya wewe”
“Safi tu, naonao ndio unafungua ofisi?”
“Yaa ndio mida yetu ya kufungua ofisi”
“Ahaa sawa sawa. Meya huwa anafika saa ngapi?”

“Saa mbili na nusu huwa ndio muda wake”



Watu 9 wakamatwa na Jeshi la Polisi

0
0
Watu tisa wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuingia nchini Kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika eneo na Nyashishi Wilayani Msingwi Mkoani humo wakiwa wamejificha katika vichaka kwa ajili ya kwenda kuchukuliwa kwa ajili ya kuendelea na safari yao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kukamatwa kwa raia hao kunafuatia taarifa za raia mwema aliewatilia shaka na kisha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao waliojificha katika kichaka hicho.

Katika hatua nyingine Kamanda Ahmed Msangi amewataka wananchi kutanguliza uzalendo kwa kuwafichua watu wanaoshi nchini bila ya kuwa na vibali maalumu na kinyume cha sheria.

Breki zilivyosababisha vifo 6 na majeruhi 6

0
0
WATU sita walifariki dunia jana na wengine sita kujeruhiwa baada ya lori la kokoto walilokuwa wakisafiria kufeli breki na kugongana na gari la taka la Manispaa ya Dodoma, katika gema la Mlima Ntyuka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ilikuwa majira ya saa tisa alasiri.

Alisema ajali hiyo, imehusisha magari mawili ambapo moja ni lori la kokoto lenye namba T236 DHF na la taka la Manispaa.

Akizungumza kuhusu ajali hiyo, mmoja wa mashuhuda ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema lori hilo la kokoto lilipinduka katika mlima huo likiwa limebeba abiria ambao ni wapakia kokoto.

"Hili gari lilikuwa na abiria zaidi ya 10 ambao ni wapakiaji kokoto na lilikuwa likiendeshwa na Baraka Malata ambaye yupo mahututi kwa sasa," alisema shuhuda huyo. "Huyu Baraka huwa ni utingo wa hilo lori, dereva mwenyewe hakuwepo leo."

Alisema lori hilo lilikuwa likishuka na kokoto kutoka kwenye mlima huo na kwamba breki zake zilifeli na kugongana uso kwa uso na gari la taka ambalo lilikuwa likipandisha.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Dodoma, Dk. Caroline Damian alithibitisha kupokea miili sita ya watu waliofariki na kwamba baadhi ya majeruhi wapo katika hospitali hiyo na wengine Hospitali ya DCMC.

Nape: Viongozi Afrika kunga’ang’ania madaraka ni ushetani

0
0
Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amesema ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani.

Kupitia ukurasa wake wa twitter leo Machi 5, 2018, Nape ameandika kuwa ni lazima ushetani huo upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla haujaota mizizi na kusambaa.

Nape ambaye amewahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya kuvuliwa wadhifa huo na Rais John Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Harrison Mwakyembe amekiri kuwa twitter ni yake ingawa hakuwa tayari kufafanua zaidi.

“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa!” unasema ujumbe huo wa twitter.

Katibu Mkuu CHADEMA Ahojiwa na Kuachiwa Kwa Dhamana

0
0
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amehojiwa na polisi kwa saa mbili na kuachiwa kwa dhamana.

Wakati Mashinji akihojiwa, vigogo wengine watano wa chama hicho alioambatana nao hawakuhojiwa, badala yake wote kwa pamoja wametakiwa kuripoti tena Kituo Kikuu cha polisi Machi 13, 2018.

Mmoja wa mawakili wa viongozi hao Alex Massaba amesema Dk Mashinji amehojiwa kwa tuhuma za kusababisha mkusanyiko isivyo halali.

Mashinji amehojiwa kuanzia saa 5:30 asubuhi hadi saa 7:30 mchana.

Februari 27, 2018 viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye leo hakuwepo baada ya kuugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, walifika kituoni hapo na kuhojiwa kwa takribani saa tano, kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena leo.

Leo viongozi hao wakiongozwa na Dk Mashinji ambaye Februari 27, 2018 hakufika kuhojiwa kutokana na kuwa nje ya nchi, mpaka saa nane mchana walikuwa wameondoka kituoni hapo.

Mbali na Mashinji, viongozi wengine waliofika kituoni ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Kwa mujibu wa Massaba, wengine walioambatana na Mashinji hawakuhojiwa.

"Awali Mashinji  hakuwepo wakati wenzake wanahojiwa lakini leo amefika na amehojiwa kwa kosa moja la kufanya mkusanyiko usio halali,” amesema Massaba.

Amesema ikiwa Machi 23, viongozi hao hawatapelekwa mahakamani, hawataripoti tena kituoni hapo kwa mdai kuwa utakuwa usumbufu.

Amesema hilo linatokana na baadhi ya viongozi hao kuwa wabunge, hivyo wanahitaji kushiriki vikao vya Bunge vitakavyoanza mapema Aprili, 2018.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.

PICHA: Moto Ulivyoteketeza Bweni Korogwe Girls

0
0
Moto umeteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe iliyoko mkoani Tanga na kuwaacha wanafunzi hao katika hali mbaya kufuatia mshtuko wa kupoteza vifaa vyao vyote.

Moto huo ulitokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi takribani 40 wanaoishi katika bweni hilo wakiwa darasani wakijisomea.

Hata hivyo licha ya moto huo kutekeza bweni, hakuna madhara ya kimwili kwa upande wa wanafunzi hao isipokuwa kwa wale waliopata mshituko na kuzimia ambao wamelazwa katika Hospitali ya Magunga na Majengo wilayani humo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Credit: GPL

Shilingi Trilioni 1 Zatengwa Kulipa Madeni Mbalimbali Mwaka wa Fedha 2017/2018

0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1 mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali ya watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Umma.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameeleza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi na ahadi mbalimbali za Serikali.

“Kati ya shilingi Trilioni 1 zilizotengwa kulipia madeni kwa mwaka huu wa fedha, shilingi Bilioni 896.3 zimeshalipwa kwa watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Serikali,” alisema Dkt. Abbasi.

Amesema hesabu hiyo inajumuisha shilingi Bilioni 43 ambazo zimelipwa Februari, 2018 ikiwa ni malimbikizo ya wafanyakazi  wa sekta ya Umma.

“Madeni mengine uhakiki unaendelea na yataendelea kulipwa siku zijazo na tutawajulisha,” alifafanua Dkt. Abbasi.

Vile vile amesema, Serikali katika kuwaondolea adha ya usafiri kwa wananchi wa maziwa makuu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria. 

Kwa upande wa Ziwa Victoria,  mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwezi huu kwa ajili utengenezaji wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400.

Kwa upande wa Ziwa Tanganyika zabuni kwa ajili ya utengenezaji wa meli mpya ya abiria na mizigo itatangazwa mwezi huu. Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na italeta mapinduzi makubwa katika usafiri ziwani hilo.

Aidha Dkt. Abbasi amesema Julai mwaka huu nchi itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo Boeing Dreamliner na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa, Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi kote nchini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 6

Ufaransa Yaipongeza Tanzania Kwa Kupambana Na Rushwa

0
0
SERIKALI ya Ufaransa imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mapambano dhidi ya rushwa na inaamini fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali zitatumika kama ilivyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa jana (Jumatatu, Machi 05, 2018) na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Bw. Frederic Clavier alipomtembelea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Balozi Clavier alisema Ufaransa imeridhishwa na mapambano ya rushwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wataendelea kushirikiana nayo katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pia Balozi huyo alisema Septemba mwaka huu wanatarajia kufungua ofisi ya Shirika la Kimataifa la Misada ya Maendeleo la Ufaransa (AFD) jijini Dar es Salaam ili kurahisisha utoaji wa huduma. 

Kwa sasa ofisi za AFD zipo Nairobi nchini Kenya.Shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo na ya maji safi na maji taka kwenye mikoa ya Simiyu, Mwanza, Musoma na Morogoro.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema Serikali imeweka kipaumbele katika uwajibikaji na kupambana na rushwa ili kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zinatumika vizuri pamoja na wananchi kupata haki.

Alisema mapambano dhidi ya rushwa yataiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, uwekezaji, kilimo na utalii, hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ufaransa ili waje kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda, kilimo, madini na miundombinu mbalimbali.

Pia Waziri Mkuu alisema Serikali itashirikiana na Ufaransa katika kuandaa mikutano mbalimbali itakayowakutanisha wadau wa sekta binafsi kutoka nchi zote mbili ili kuwapa mbinu za namna ya kukuza uchumi.

Rais Magufuli atoa kibali cha kuendelezwa ujenzi wa msikiti wa Sumbawanga......Serikali ya mkoa wa Rukwa yachangia Milioni 5.7 kuumalizia

0
0
Uongozi wa Waislamu Mkoani Rukwa umepokea kwa furaha mchango wa Shilingi Milioni 5.7 uliotolewa na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha maridhiano juu ya ujenzi wa msikiti uliosimama kwa muda.

Fedha hizo zilizochangwa zilijumuisha ahadi, fedha taslimu pamoja na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa kwa umoja wa viongozi wa serikali kuonesha mshikamano uliopo kati ya serikali na wananchi bilaya kujali itikadi, dini wala rangi huku Mh. Wangabo akichangia milioni 1.5

Kabla ya maridhiano hayo Mh. Wangabo alitoa salamu za rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya kuuendeleza msikiti huo na kunukuu kuwa Mheshimiwa Rais ametoa kibali cha kuuendeleza msikiti hio na yupo tayari kuweka jiwe la msingi ama kuuzindua msikiti huo.

“Mh. Rais ameniagiza niseme yafuatayo kuwa ametoa kibali cha kuendelea kujenga msikiti huu ahdi umalizike, ameyafikiria mambo mengi sana mpaka kuja kufikia maamuzi haya, ili yalete muskabali wa maridhiano, ilete amani, ilete utulivu, mshikamano, maoelewano na umoja ili Rukwa yetu iweze kusonga mbele kama kitu kimoja., la pili alisema kuwa yupo tayari kuweka jiwe la msingi ama la kuzindua msikiti huu,”

Kwa kuongezea hilo Mh. Wangabo aliuomba uongozi wa uislamu mkoa kuendelea kushirikiana na kudumiasha amani na kuhakikisha wanajenga Rukwa moja isiyoyumbishwa na tofauti yoyote kwani ushirikiano huo umekuwa wa muda mrefu hovyo asingependa pawepo na tofauti.

Pia alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha vikwazo vyote vianondolewa na kumtaka kamishna wa ardhi nyanda za juu kusini kufanya haraka kupitisha kibali ili msikiti huo upatiwe hati.

Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali amesifu maamuzi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na kukubali ombi lake la kutaka kuja kuweka jiwe la msingi ama kuuzindua msikiti huo na kuwa waislamu wataendelea kuungana nae na kumuombea amalize vipindi vyake salama.

“Mh. Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya waislamu wa mkoa wa Rukwa kwanza tunatoa shukrani za dhati kwa Mh.Rais wa nchi Mh. Dk. John Magufuli, nimeamini kama alivyosema kuwa yeye ni msikivu na yeye anatuomba kila siku tumuombee dua na sisi mwisho wa khotuba yetu kila ijumaa tunadua huwa tunaiomba, Eee Mola wetu linda amani ya nchi yetu na uwalinde viongozi wetu,” Shekh Akilimali alimalizia.

Uongozi wa mkoa wa Rukwa uliowajumuisha kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa halmashauri, Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga pamoja na kaimu Kamishna wa Ardhi nyanda za juu kusini.

Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Hamphrey Polepole wapata ajali mkoani Kigoma

0
0
Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la Kijiji cha Nyamidato, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Vx yenye namba za usajili T150 CWE iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Polepole amewasili  mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu.

Mangula Aonya Viongozi Wa Dini, Wanasiasa Wanovuruga Amani Nchini

0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Philipo Mangula amewataka Watanzania kujenga na kuilinda amani nchini na kushangazwa na viongozi wa dini wanaobariki chuki kuwa wanamkosea Mungu.

Pia aliwaonya wanasiasa wanaochochea chuki na kusababisha vurugu na kuwashauri waache kwa kuwa siasa ni uvumilivu na kuvumiliana.

Mangula alitoa kauli hiyo juzi mjini Musoma alipozungumza na viongozi na wana wana chama wa CCM kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama mjini humo.

Alisema kuwa turufu kubwa iliyobaki kwa CCM na watanzania ni amani iliyodumu nchini kwa miaka dahari na hivyo wakati wote wazungumzie taratibu na kutunza amani ya nchi ili kue[uka machafuko vurugu na migogoro inayosababishwa na kuchochewa na wanasiasa.

“Siasa ni kuvumiliana na uvumilivu ndiyo hujenga umoja.Wanasiasa wanapoleta vurugu  wajue wanaoumia ni watoto na wanawake na hivyo tuache chuki tujenge amani ya nchi yetu bila kufanya hivyo hatuwezi kupata maendeleo,”alisema Mangula na kuongeza kuwa;

“Nashangaa na kushitushwa na viongozi wa dini wanapojiingiza na kubariki chuki, wanamkosea Mungu. Machafuko yakishatokea hakuna atakayesalimika kwa kusema mimi ni kiongozi wa dini."

Alieleza kuwa kazi ya serikali si kuwajengea nyumba bali  mazingira mazuri wananchi ili wajijenge na kujifanyia maendeleo.

Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM bara alieleza zaidi kuwa yapo mabadiliko makubwa ya maedeleo mkoani Mara na yote hayo yanafanyika kwa kuwa nchi ina utulivu kwani bila amani ni vigumu kupata maendeleo na hivyo amani kwanza taratibu na kanuni zifuatwe baadaye.

Alisisitiza wanasiasa kuwa wanapochochea chuki na vurugu wanakuwa na passports (hati za kusafiria) mikononi na yakichafuka wanaondoka na kuwaonya wana CCM wasijiingize kwenye migogoro  hasa vijana wa CCM wasijiingize humo.

Aidha, Mangula aliwapongeza wabunge wa CCM mkoani Mara walio karibu na wanaotekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi kwa wananchi na wapiga kura wao.

Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samuel Kiboye Namba Tatu alisema Mangula ni miongoni mwa viongozi waadilifu waliobaki ndani ya CCM na Tanzania.

Alimpongeza kwa kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais John Magufuli na kuiwezesha CCM kurudisha heshima kwa wananchi na akawataka wana CCM kumuombea maisha marefu.

“Nakupongeza kwa kumsaidia Rais Magufuli na sisi huku chini hatutamvumilia mtu yeyote asiye na nidhamu wala maadili.Wabunge wa CCM nao wamejitahidi kutekeleza ilani ya Chama hasa mbunge wa Musoma Mjini jimbo  ambalo ni gumu kisiasa,”alisema Namba Tatu.

Kwa mujibu wa habari za ndani ya chama hicho, Mangula atakuwa na ziara ya siku tatu katika wilaya za Tarime, Serengeti na Bunda ambako atafanya vikao na viongozi wa serikali na jumuiya za CCM.

Jumanne na Jumatano atakuwa Tarime, Alhamisi na Ijumaa  atakuwa Serengeti kabla ya kuhitimisha ziara yake jumapili wilayani Bunda.

Mkapa amteua Prof. Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) Kuchukua Nafasi ya Profesa Kikula

0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO    
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa ametangaza uteuzi wa  Profesa Egid Beatus Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Idris Suleiman Kikula.

Uteuzi huo umetangazwa rasmi  tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi   ya Mkuu wa UDOM, Mhe. Benjamin Mkapa.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Mubofu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kabla ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.

Profesa Idris Kikula ni miongoni mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani  na nje ya nchi kitaaluma kwa kushiriki katika tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii

Ameshiriki katika tafiti hizo kwa kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa nchini  kama REPOA, pamoja na taasisi ya UONGOZI.

UDOM ndio chuo kikuu pekee chenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi hapa nchini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 40,000, pia kina eneo la ukubwa wa hekari zaidi ya 6000.


Vipimo Vyakwamisha Kesi ya Nabii Tito

0
0
KESI inayomkabili mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45), ya kujaribu kujiua kwa kutumia wembe, imeahirishwa tena kuanza kusikilizwa hadi Machi 19, mwaka huu kutokana na ripoti ya vipimo vya akili kutokamilika.

Akiahirisha kesi hiyo jana, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Mwajuma Lukindo, alisema kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe hiyo kutokana na ripoti ya vipimo hivyo kutokamilika.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka katika Taasisi ya Afya ya Akili Mirembe Isanga kwa kawaida ripoti ya vipimo huchukua siku 42, hivyo kutokana na hali hiyo vipimo vya nabii huyo havijakamilika.

Februari 5, mwaka huu mahakama hiyo iliagiza kutekelezwa kwa amri iliyotolewa na Mahakama hiyo ambayo iliamuru jana, kupelekwa kwa vielelezo vinavyoonyesha Nabii Tito ana matatizo ya akili na kufanyiwa vipimo katika Taasisi ya Afya ya Akili Mirembe Isanga.

Akitoa maelezo ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, Wakili wa Serikali, Beatrice Nsana, aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuwasilishwa kwa taarifa kutoka Isanga.

Hata hivyo, Hakimu Karayemaha alisema mshtakiwa huyo amewasilisha vielelezo vyake kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na mahakama inahitaji taarifa kutoka Taasisi ya Mirembe Isanga kama ilivyoagiza.

“Mahakama ilitoa amri apelekwe Taasisi ya Mirembe Isanga kwa mujibu wa kifungu namba 219 (2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,” alisema Hakimu Karayemaha.

Kifungu hicho kinasema kama mshtakiwa atabainika kuwa kweli ana matatizo ya afya ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili timamu, hivyo hana hatia.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Karayemaha alimuamuru Mkuu wa Magereza ya Isanga kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa ya kumpeleka kufanyiwa vipimo mshtakiwa huyo.

“Namuamuru Mkuu wa Magereza Isanga atekeleze amri ya mahakama, ili taarifa za mshtakiwa ziletwe Machi 5, mwaka huu, tutataja kesi na kupokea taarifa ya vielelezo vya vipimo vyake kutoka Isanga na mshtakiwa ataendelea kukaa rumande,” alisema hakimu huyo.

Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu katika mtaa huo wa Ng’ong’ona.

Rugemalira Asaka Dhamana Mahakama ya Rufaa

0
0
Mshitakiwa wa Kesi ya uchotaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, James Rugemalira amewasilisha maombi matatu katika Mahakama ya Rufaa ikiwemo ombi la kusudio la kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’.

Ombi lingine ni la kuitaka Mahakama hiyo kumuingiza katika maombi hayo, Mtuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, Habinder Sethi ambapo Rugemalira ameiomba Mahakama imuingize Sethi kama mtu muhimu katika kesi hiyo.

Maombi hayo yamewasilishwa  jana Machi 5, 2018 mahakamani hapo na Rugemalira mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Benard Luanda na Jaji Gerald Ndika.

Hata hivyo, kulikuwa na mvutano kati ya upande wa Jamhuri na upande wa mshtakiwa baada ya Jamhuri kuweka pingamizi kwa kuiomba Mahakama ya Rufaa kuyatupilia mbali maombi hayo kwa madai kuwa, muwasilishaji alitumia kanuni zisizo sahihi huku upande wa utetezi ukipinga pingamizi hilo kwa madai kwamba Jamhuri haikuwasilisha pingamizi hilo kwa maandishi.

Kufuatia mvutano huo, Jaji Luanda amesema wanaahirisha maombi hayo na watapanga tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Freeman Mbowe aruhusiwa kutoka hospitali. Daktari aeleza ugonjwa wake

0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) ameruhusiwa kutoka hospitali hapo baada ya madaktari kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika.

Mbowe alilazwa hospitalini hapo kuanzia juzi usiku ambapo alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.

Afisa Habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema kuwa Mbowe ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo, baada ya madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kuona afya yake inazidi kuimarika.

Mbowe alifikishwa KCMC Machi 4 akiumwa kichwa, na jana Machi tano aliruhusiwa kutoka hospitalini.

Bashe Ajilipua......Akabidhi hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ya kuchunguza matukio ya Mauaji na Utekaji Nchini

0
0
Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya uchunguzi.

"Leo asubuhi (jana) nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu", amesema Bashe.

==> Isome barua Hiyo hapo chini 


Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218 TUNAPATIKANA BUGURUNI SOKONI STENDI ya musanga
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images