Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Nchemba amwagiza IGP kufanya uchunguzi wa mauaji ya kiongozi wa Chadema

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji ya Daniel John ambaye alikuwa ni Katibu wa kata ya Hananasifu (Chadema) yaliyotokea Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Waziri Mwigulu amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake nini na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

“Mataifa mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapotepotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu kama jambo la kawaida tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili,” alisema Waziri Mwigulu.

Ameongeza kusema kuwa maswala ya demokrasia huamukiwa kwa peni na karatasi na si kwa panga,lungu wala mkuki.

Wananchi Wamkataa Mkuu Wa Wilaya Mbele Ya Waziri Mkuu

$
0
0
WANANCHI wa wilaya ya Kwimba wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Mtemi Msafiri baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Wametoa ombi hilo jana (Ijumaa, Februari 16, 2018) walipozuia msafara wa Waziri Mkuu alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya Kwimba zilizopo Ngudu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Wananchi hao walimkataa mkuu wao wa wilaya Bw. Msafiri kupitia ujumbe wa mabango 17, ambapo Waziri Mkuu amewataka wananchi hao wawe watulivu wakati Serikali inafanyia kazi malalamiko yao.

Wananchi hao wanadai kwamba Mkuu huyo wa Wilaya anatabia ya kuamrisha polisi wawakamate kwa kisingizio cha uzururaji na kisha wanawekwa mahabusu, ambapo baada ya muda wanatolewa na kwenda kulima kwenye shamba lake.

Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kila mtumishi atambue majukumu yake na ayatekeleze. “Hakuna atakayeonewa, haki zenu zote tunazitekeleza nanyi mnatakiwa kutenda haki kwa kuwatumikia wananchi.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka Mkuu huyo wa wilaya Bw. Msafiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Bibi Pendo Malebeja na wakuu wote wa Idara wajitathmini kama kweli wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kuwatumikia wananchi.

“Mkurugenzi katika kipindi chako chote cha utendaji kuanzia mwaka 2013 hadi leo, fedha nyingi za Serikali zilizoletwa Kwimba zimepotea na hazijulikani zilipo huku miradi mingi bado haijakamilika na muda wote huo Halmashauri imekuwa inapata hati chafu.”

Pia Waziri Mkuu amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba wabadilishe mienendo yao na wawatumikie vizuri wananchi pamoja na kuishi nao vizuri.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, FEBRUARI 16, 2018.

Serikali kutoa viwanja kwa ajili ya Mabalozi kujenga ofisi na makazi Dodoma

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiongea katika kikao na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wa hapa nchini kuhusu Mpango Mkuu wa mji wa Serikali mjini Dodoma ambao utakuwa na eneo kwa ajili ya wanadiplomasia

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf  Mkenda amewahakikishia Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini kuwa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwapatia viwanja vya ukubwa wa ekari 5 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na makazi ya Balozi mjini Dodoma itatekelezwa kama ilivyoahidiwa.

Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo katika sherehe  za  kufungua mwaka wa 2018 ya wanadiplomasia zilizofanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam tarehe 09 Februari 2018.

Prof. Mkenda alitoa kauli hiyo kwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakati wa kuwasilisha mada kuhusu Mpango Mkuu wa Mji wa Serikali mjini Dodoma.

Mada hiyo ilitolewa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Manispaa ya Dodoma kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) leo Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mada hiyo, mji wa Serikali mjini Dodoma utajengwa pembeni ya Barabara ya Dar Es Salaam hadi Dodoma, kilomita 17 kutoka katikati ya mji wa Dodoma na unakadiriwa kugharimu Shilingi za Kitanzania trilioni 10 hadi unakamilika.

Mji huo ambao umesanifiwa kwa asilimia 100 na wataalamu wa Kitanzania umezingatia mahitaji yote muhimu ambayo mji wa kisasa unastahili kuwa nayo. Miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na miundombinu ya kutosha ikiwemo barabara, maji safi na maji taka, nishati ya umeme, TEHAMA na dampo kwa ajili ya taka ngumu ambalo ujenzi wake umeshakamilika na juhudi zinaendelea za kutafuta mwekezaji kwa ajili ya kubadilisha taka kwa matumizi mengine (recycling).

Aidha, usanifu wa mji huo umezingatia vigezo vya uendelezaji endelevu wa miji duniani ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na urithi wa asili, kuepuka uchafuzi wa hali ya hewa na urahisi wa kufikika.
 
Wasanifu wa mji huo wakisisitiza kuhusu uendelezaji endelevu wa miji, katika usanifu wao wamezingatia hali ya hewa ya Dodoma ambayo ni ya joto na upepo mkali, hivyo, wametenga maeneo kwa ajili ya upandaji miti itakayopunguza kasi ya upepo na ujenzi wa vyanzo vya maji kwa ajili ya kupoza joto.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza katika mji wa Dodoma katika miradi mbalimbali ikiwemo mashule, hospitali, mahoteli, maduka makubwa na miundombinu mingine.
 
“Tumetenga eneo kubwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambalo limegawanywa katika ukubwa tofauti tofauti kutegemea na mahitaji ya mwekezaji, hivyo wahimizeni wafanyabiashara kutoka katika nchi zenu waje kuwekeza Dodoma”. Bw. Kunambi aliwaambia Mabalozi.

Bw. Kunambi alieleza kuwa Mpango Mkuu wa mji wa Dodoma ulisanifiwa tangu mwaka 1976 na kufanyiwa mapitio mwaka 2010 na sasa wataalamu hao ambao wamepata uzoefu kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Nigeria, Malaysia, China na Malawi ili kusanifu mji unaozingatia mahitaji ya sasa.

–Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 
16 Februari 2018

Waziri Mkuu Akemea Vitendo Vinavyoharibu Ubora Wa Pamba .....Awataka Wasiweke Mchanga Wala Maji Ili Kuongeza Uzito

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa pamba kutochanganya pamba na mchanga au maji kwa sababu watakosa wanunuzi.

Pia amesema Serikali itapambana na watu wote wanaotaka kuvuruga zao hilo, hivyo amewataka wakulima waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Waziri mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Februari 16, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Kwimba.

“Wakulima msichezee pamba kwa kuichanganya na chochote ili kuiongezea uzito kwa sababu mtaharibu sifa nzuri ya pamba ya Tanzania ndani nan je ya nchi.”

Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima wasiokuwa waaminifu ambao kabla ya kuipeleka pamba sokoni wanachanganya na maji au mchanga.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kuona tija tangu ilipoagiza Maofisa Kilimo katika mikoa inayolima pamba wasimamie kilimo hicho kuanzia ngazi za awali.

Akizungumzia kuhusu suala la wanunuzi wa pamba, Waziri Mkuu alisema tayari Serikali imeweka mikakati ya kutosha itakayowezesha pamba yote kununuliwa.

Kuhusu suala la bei alisema wataangalia katika soko la Dunia na kisha watawashawishi wanunuzi wanunue kwa bei nzuri itakayowanufaisha wakulima.

Alisema Serikali itaendelea kusimamia zao hilo kuanzia hatua za maandalizi ya shamba kwa kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi masoko.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mashamba ya mfano ya pamba katika kijiji cha Kilyaboya na Igumangobo ambapo alisema ameridhishwa mashamba hayo.

Pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kadashi, mradi ambao ulioibuliwa na Diwani wa Kata ya Maligisu, Bw. Tabu Mapembe.

Kata ya Maligisu yenye vijiji vine ina zahanati moja tu, kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia kupunguza tatizo la utoaji wa huduma za afya.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, FEBRUARI 17, 2018.

Mtulia: Nitakubaliana na Matokeo Yoyote

$
0
0
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulid Mtulia amefunguka na kudai atakubaliana na matokeo yoyote yatakayo tangazwa jioni ya leo na Tume ya Uchaguzi Taifa (NEC) pindi zoezi la kuhesabu kura litakapomalizika.

Mtulia ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anafanya mahojiano ya mubashara kutokea katika kituo alichopigia kura cha Friends Corner, Kata ya Ndugumbi na kusema zoezi hilo linakwenda salama mpaka hivi sasa na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili washiriki katika zoezi hilo ambalo ni haki yao ya kimsingi.

"Chama changu sio cha ulalamishi na hata kama kikiona hakikutendewa haki huwa kinafuata njia za kisheria kwa kufungua kesi Mahakamani kulalamikia matokeo lakini tutayakubali matokeo yeyote yatakayo kuja jioni", amesema Mtulia.

Jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini leo yameingia katika zoezi la kupiga kura za kuchagua wabunge watakaoweza kuwakilisha shida za wananchi wa majimbo hayo Bungeni.

Mkuu wa shule amzaba kofi mwalimu mbele ya wanafunzi

$
0
0
Katika  hali isiyo ya kawaida Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabwe iliyoko mwambao mwa Ziwa Tanganyika, Nkasi mkoani Rukwa, Jackson Mussa, amemtandika kofi mwalimu mwenzake, Emmanuel Mbemba, mbele ya wanafunzi wake.

Akizungumzia tukio hilo, Mratibu Elimu Kata ya Kabwe, Geofrey Mtafya, alisema tukio la kupigwa kofi mwalimu huyo, lilitokea juzi asubuhi majira ya saa 4:00 asubuhi na kusababisha taharuki kubwa kwa wanafunzi na walimu wengine wa shule hiyo.

Mtafya alisema siku ya tukio hilo, Mwalimu Mbemba alikwenda ofisini kwa Mkuu wa shule kuomba ruhusu ili awapeleke wanafunzi kwenye ziara ya mafunzo kwa kutembelea fukwe za Ziwa Tanganyika.

Mkuu huyo wa shule alimtaka mwalimu huyo aandike barua ya kiofisi na alifanya hivyo. Aliipokea barua hiyo na kumwahidi mwalimu huyo kuwa baada ya muda si mrefu atampatia majibu kwa maandishi.

Alisema baada ya kusubiri kwa muda bila majibu, Mwalimu Mbemba ambaye anafundisha Kidato cha tatu somo la Jiografia, alimfuata mkuu wake wa shule na kumkumbusha kuwa bado anasubiri. Mkuu wa shule alijibu kuwa alikuwa bado hajaandika barua ya ruhusa kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine.

Baada ya muda mrefu tena kupita, mwalimu huyo wa Jiografia alimfuata Mkuu wa Shule ikiwa ni mara ya tatu na kumweleza kuwa anachelewa kwenda kwenye ziara ya mafunzo na wanafunzi, kitendo kilichomkasirisha mkuu huyo wa shule, ndipo alipomfuata na kumkaba koo Mwalimu Mbemba mbele ya wanafunzi na akaanza kumzaba vibao mfululizo.

Taarifa kutoka shuleni hapo zinaeleza kuwa wanafunzi wa shule hiyo walishuhudia tukio hilo huku baadhi yao walianza kupiga kelele hatua iliyosababisha walimu wengine kwenda kuamua na kuwaachanisha walimu hao waliokuwa wamekwidana mashati.

Mwalimu Mbemba alitoa taarifa kwa kiongozi wa Chama Cha Walimu (CWT) mahali pa Kazi, Elia Elia ambaye alimwarifu Ofisa Mtendaji Kata ya Kabwe, Geoffrey Kuzumbi ambaye aliitisha kikao cha dharura shuleni hapo.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Mkuu wa Shule huyo alikana kumpiga kofi mwalimu mwenzake bali alidai kuwa alimkaba koo tu. Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Nkasi, Abel Ntupwa, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kukemea kitendo hicho kuwa ni utovu wa nidhamu huku akiahidi kutolea uamuzi wiki ijayo baada ya kupatiwa ripoti kamili.

Dereva Aliyetoa Rushwa ya Elfu 5 Kwa Trafiiki Naye Asakwa Na Jeshi La Polisi

$
0
0
Jeshi  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamsaka dereva aliyempa rushwa ya Sh. 5,000 askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye amefukuzwa kazi, kwa ajili ya kukamilisha upelelezi.

Katikati ya wiki, video fupi iliyokuwa ikionyesha askari huyo akipewa rushwa na dereva wa gari ndogo ilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusababisha Polisi kumchukulia hatua trafiki huyo.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, aliwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam "video ile" iliwashutua na walichukua hatua mara moja za kumfukuza kazi na sasa ni raia wa kawaida.

Juzi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi Jumanne Murilo, alisema askari huyo alifukuzwa tangu Jumanne.

Kamanda Murilo alisema askari huyo hadi anafukuzwa kazi ndani ya Jeshi la Polisi alikuwa amefanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

"Tukio hili lilifanyika eneo la Mwenge na baada ya kulibaini tulianza uchunguzi wetu ambao juzi (Jumanne) ulikamilika na kubaini tukio hilo lilikuwa la kweli (kwamba) amepokea rushwa. Hivyo tumemuondoa kazini," alisema juzi Kamanda Murilo.

Kamanda Murilo ambaye hakumtaja jina askari huyo aliwakumbusha trafiki kuzingatia maadili ya kazi na taratibu za kijeshi zilizowekwa.

Akirejea taarifa hizo, Mambosasa alisema upelelezi wa shauri hilo unaendelea .

"Kwa sasa upelelezi unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ambaye kwa sasa si askari tena," alisema Kamanda Mambosasa.

"Lakini kama ambavyo sheria za rushwa zinavyoelekeza ni lazima tumpate na aliyehusika kutoa rushwa ili kupata ushahidi wa kesi hiyo," alisema Mambosasa.

Alieleza zaidi kuwa ingawa wanamsaka mtuhumiwa huyo namba mbili, pia wanamshukuru kwa ushirikianao uliowezesha kupatikana kwa askari huyo na hatua kuchukuliwa dhidi yake.

"Badala ya raia kulalamika na kusema Jeshi la Polisi halifanyi kazi ni vyema mkatoa taarifa kama alivyotoa huyu aliyerekodi video, aliyewezesha kumnasa aliyekuwa askari wetu na tukambaini kweli na kosa la kuomba rushwa ya Sh. 5,000 wakati serikali inapambana na matukio kama hayo," alisema.

Katika tukio hilo, dereva aliyeombwa rushwa alimrekodi askari huyo kupitia simu ya mkononi wakati akimpatia rushwa hiyo iliyowekwa chini ya leseni.

Uchaguzi Kinondoni: Mkurugenzi Afafanua Mawakala Kuzuiwa Kuingia

$
0
0
Wakati baadhi ya vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa jimbo la Kinondoni mawakala wa vyama vya siasa wamezuiwa kuingia kwa madai kuwa barua zao za viapo zimekosewa, msimamizi wa uchaguzi huo, Aron Kagurumjuli amesema uchaguzi huo unakwenda vizuri.

Baadhi ya mawakala hao katika kituo cha Lasko kilichopo kata ya Tandale wamezuiwa kwa madai kuwa hati zao za uthibitisho walizopewa zimekosewa.

Akizungumza leo Februari 17, 2018 msimamizi wa mawakala wa CUF kata ya Tandale, Abdul Zain amesema wamefika vituoni tangu saa 12 asubuhi lakini mawakala wao wamezuiwa kuingia ndani ya vituo hadi hati zao zitakapobadilishwa.

Amesema kuwa wamefuatilia suala hilo ofisi za Kagurumjuli na kupewa fomu nyingine ambazo pia zimekataliwa.

Katika ufafanuzi wake, Kagurumjuli amesema mawakala wengi hawakuwa na barua kutoka NEC zinazowatambulisha kuwa ni mawakala ambazo walitakiwa kupewa na viongozi wa vyama vyao na badala yake wanatumia barua za viapo alizodai kisheria haziwezi kuwa utambulisho pekee wa kuwa mawakala.

Amefafanua kuwa barua hizo za viapo hazitumiki kuwahalalisha, kwamba vituo vyote katika kata tano wameshatatua tatizo hilo.

“Wakala anapaswa kuapa kwanza na barua ya kiapo napaswa kuwa nayo mimi ili wakifanya kosa niwachukulie hatua. Kiapo si mali yao ndiyo maana tuliwapa nakala, hakuna sheria ya kupewa barua ya kiapo kuna sheria inayosema wakala ataapa siku saba kabla ya uchaguzi na ndivyo ilivyofanyika,” amesema.

“Barua ya utambulisho ndiyo kitu muhimu wanapaswa kuwa nazo ambazo zimetolewa na ofisi ya Mkurugenzi. Barua ya kiapo siyo suluhisho la kuingia nayo kwenye kituo ila barua ya utambulisho ndiyo inahusika.”

Kuhusu matokeo kutangazwa amesema, “Tunatarajia  hadi saa sita usiku matokeo yatakuwa yameshajulikana iwapo kura zitapigwa vizuri na kuhesabiwa bila vurugu.”

Salumu Mwalim Alia Mawakala wa Chama Chake Kuzuiwa Kuingia

$
0
0
Mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chadema, Salum Mwalimu amelalamikia uchaguzi huo kuwa mawakala wa chama hicho wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kwa wakati.

Akizungumza leo Februari 17, 2018 amesema mawakala wa chama hicho kikuu cha upinzani wamechelewa katika baadhi ya vituo kwa saa mbili hadi tatu.

Mwalimu alitolea mfano Kata ya Hananasifu kuwa mawakala hao wameingia saa 2 asubuhi wakati vituo vyote 613 vya kupigia kura vimefunguliwa saa 1 asubuhi.

Mwalimu ambaye alitembelea kituo cha Hananasifu B, amesema mawakala hawa wamezuiwa baada ya kuelezwa kwamba hawana fomu za halmashauri na wengine zile za kiapo.

"Cha ajabu nimeingia kituo kimojawapo halafu wakala wa chama cha UMD anazo barua zote tangu saa 12 asubuhi wakati huohuo wakala wa Chadema hana barua na nilipohoji wananiambia mbona wakala wa CCM pia hana barua na hajaingia,” amesema Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar,

"Sasa mtu anapoanza kukuuliza mbona na wa CCM hana unaanza kujiuliza maswali mengi kwanini? Mle ndani walivyokaa wamejipanga kufanya wanachokifanya na wao wanajua wanafanya kazi kwa maelekezo ya nani.”

Amedai tatizo kama hilo pia limewahi kujitokeza kata ya  Saranga na kusababisha upigaji kura kutozingatia haki na taratibu.

Mwalimu amesema baadhi ya wananchi wameshindwa kupiga kura kutokana na majina yao kutoonekana vituoni wakati katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, walipiga kura katika vituo hivyo hivyo.

Mwenyekiti NEC atembelea vituo
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage ametembelea kituo cha kupigia kura  cha Leaders Club kuangalia upigaji kura unavyoendelea.

Amesema vituo vimefunguliwa kwa wakati na wapigakura wanaendelea kupiga kura katika kata nane na majimbo mawili yenye marudio ya uchaguzi.

Kuhusu malalamiko kwenye baadhi ya vituo vya kupiga kura amesema hadi sasa hajapokea malalamiko hayo na kwamba mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wanashirikiana vyema.

"Hadi sasa nimepokea malalamiko ya wakala mmoja kuwa na viapo viwili. Wakala anayemwakilisha mgombea mmoja hawezi kuwa na viapo viwili,” amesema Jaji Kaijage.

Alipoulizwa kuhusu viapo kucheleweshewa kwa mawakala wa vyama vya siasa amesema wakala anatakiwa kuwa na kiapo kabla ya muda wa uchaguzi kuanza ambapo wakala atatakiwa kuwa na barua ya utambulisho pamoja na kitambulisho.

Chanzo cha Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume na Tiba Yake

$
0
0

Tendo la ndoa limengawanyika katika makundi matatu baadhi yake makudi hayo niuhanisi, kufanya tendo la ndoa maramoja na kushidwa kurudia tena 

sababu zinazo pelekea ni ugonjwa wa kisukari, kujichuwa, maumivu ya mgongo na kiuno, tumbo kuuguruma na kujaa gesi, msogo wa mawazo, presha, kutokuwa nyama sehemu ya haja kubwa yani mgoro, ulevu wa kupidukia, kuadhilika na madawa ya kulevya 

ARRBERA 1 Ni dawa ya asili ambayo imefanyiwa tafiti kwa hali ya juu isiyo na kemikali yoyote kwa mtumiaji ambayo humfanya mtumiaji kufanya tendo la ndoa maratatu bila kuchoka 

Pia ARRBERA 2 ni dawa asili abayo huimalisha ukuaji wa umbile la kiume lililo sinyaa na kunenepesha saizi upedayo. sihayo tu upade wa wamatatizo kisukari yakushuka na kupada kuna dawa ya kutumia siku saba na kufanya sukari ibaki nomo balasi abayo ni 4-5-6 vilevile kwaupade wa kina mama matatizo ya uzazi na hedhi kuvurugika na kutokwa maji maji sehemu za sili fagasi na kifafa cha mimba kwa kina mama waja wazito na kifafa cha kawaida 

FIKA OFISINI KWETU MBANGALA RAGI TATU ASIYE KUWA NA NAFASI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO KWA KWA KAZI WA DSM muone dr kabero simu 0758078280 au 0713 293 988 wote mnakalibishwa
No automatic alt text available.

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FULL POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

OFA : Jipatie Riwaya Kali za Kusisimua Kwa Punguzo

$
0
0
OFA OFA YA SIKU YA KUZALIWA KWANGU
Namshukuru Mungu kwa kuzaliwa leo 17th feb 2018. Miaka 25 iliyo pita mama yangu aliweza kunileta duniani. Kwa kusherekea siku yangu ya kuzaliwa na mashabiki wangu wote ndani na nje ya TANZANIA. NIna toa punguzo la bei kwa asilimia 40. Hadithi zangu zote na hadithi hizi ninaziuza kupitia
1.Whatsapp 06657072588 au 0768516188.
2. Email eddazariaM@gmail.com
3. Facbook kupitia ukurasa wangu wa @StoryZaEddy-tz.

HADITHI ZILIZOPO KWENYE OFA YA SIKU YA LEO NI
1. SEX DEALER sh 2000/=
2. HARD DAY sh 3000/=
3. SHE IS MY WIFE sh 4000/=
4. SORRY MADAM sh 5000/=
5. MY MOM'S FRIEND sh 6000/=
6. SORRY MADAM D.F.E sh 6000/'=
7. AM NOT A DOCTOR sh 7000/=
8. MY LIFE sh 8000/=
9. POWER sh 10000/=
10. AIISSII YOU KILL ME LEGACY sh 10000/=
11. AIIISSIII YOU KILL sh 15000/=

Hadithi mpya za SIN na TANGA RAHA season two. Zinapatikana katika group langu la hadithi watsapp na ada yake ya mwenzi ni sh 4000 tu.Sherekea nami kwa kuniunga mkono katika kipaji changu hichi.

HAPPY BIRTH TO ME na KARIBUNI SANA

Zari Amlipua Diamond.....“Utakoma tu mwenzangu”

$
0
0
Ikiwa leo ni siku ya tatu toka Zari atangaze rasmi kuachana na mzazi mwenzake Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa instagram, Leo February 17,2018 kupitia mtandao wa Snapchat wa Zari ameandika caption ambayo inatafsirika ni ujumbe kwa Diamond Platnumz.

Zari the boss lady ameandika “Utakoma tu mwenzangu” akiwa anaangalia wimbo wa Sikomi wa Diamond Platnumz kwenye Tv.

Sanduku la Kupigia Kura Laibiwa Kinondoni

$
0
0

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA) Salum Mwalimu amedai sanduku la kupigia kura katika mtaa wa Idrisa Magomeni Jijini Dar es Salaam limeibwa huku watu wakishuhudia kitendo hicho kikifanyika na hakuna hatua zozote za kisheria zilizofanyika

Salum Mwalimu amebainisha hayo pindi alipokuwa anazungumza mubashara kutoka katika kituo hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa mmoja wa wakala wake aliyempigia simu kumtaarifu kwamba kuna mtu ameiba sanduku la kupigia kura akiwa na gari na kutokomea pasipo julikana.

"Nimepigiwa simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini nikazungumza na msamamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambae ni msamimizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote tulikubaliana kuwa sanduku liliibwa na mtu ambae alikuja na kulipora japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo", amesema Salum.

Pamoja na hayo, Salum Mwalimu ameendelea kwa kusema "baada ya dakika kama 10 hivi sanduku likarudishwa. Sasa kinachonishangaza ni kwamba Polisi na Tume wanasema uchaguzi uendelee. Yaani kura zimeibwa na Polisi wapo na kuna mpaka wa vyeo vya juu kutoka katika Mkoa wa kipolisi Kinondoni"

Aidha, Mkuu wa kituo hicho alipofuatwa na muandishi kuulizwa juu ya sakata hilo alidai aruhusiwe kuongea jambo lolote kwa kuwa yeye hana mamlaka ya kuongea.

Kwa upande wake, Wakala wa CHADEMA katika kituo hicho, Msafiri Mussa amesema waliona gari aina 'Land Rover' na kushuka mtu mmoja akiwa na askari kisha akachukua sanduku hilo na kutokomea nalo.

TANGA RAHA- Sehemu ya Sita ( 6 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Nikanyanyuka na kwenda kuchungulia dirishani nikamuona Rahma akishuka kwenye gari la kifahari aina ya G8 VX na taratibu akaanza kupiga hatua kuja katika mlango wangu kitendo kilichozidi kunipa presh

ENDELEA
Rahma akagonga mlango taratibu nikajikuta ninaanza kujishauri juu ya kuufungua mlango huku mapigo yamoyo yakinienda mbio kama saa mbovu ya kichina inayoelekea kuisha muda wake wa matumizi.Nikajikaza na kujifuta kajasho kanacho nitoka kisha nikaufungua mlango taratibu na macho yangu yakakutana na Rahma akiwa amejiremba vizuri kama anakwenda harusini
"Karibu ndani"
"Asante baby"
Rahma akaingia huku akionekana kukichunguza chumba kwa umakini na kuzidi kuniogopesha.Nikahisi nimekanyaga kitu kwenye mguu wangu wa kushoto taratibu nikayashusha macho yangu kutazama ni nini nilicho kikanyaga.Nikajikuta nikihamaki hii ni baada ya kuikuta sidiria ya Mama Fety niliye lala naye jana usiku

Haraka haraka nikaisukumia chini ya sofa pasipo Rahma kuniona huku nikijitahidi kuweka tabasafu usoni mwangu ili Rahma asifahamu hofu niliyo kuwa nayo
"Sir kumependeza ndani kwako hadi raha"
"Asante mpenzi wangu karibu ukae"
Nikamshika kiuno Rahma na kumkalisha kwenye sofa kisha na mimi nikaa pembeni yake haku nikiwa ninazichezea nywele zake ndefu za kiarabu zilizo shuka hadi mgongoni huku zikiwa zimepakwa mafuta mazuri ya kunukia
"Sir yaani kila nikikuangalia najisikia hamu ya kufanya mapenzi yaani mwili mzima una nisisimka"
"Usijali mke wangu nipo kwa ajili yako"
Kwa kubabaika nikajikuta ninamuita Rahma mpenzi wangu nikasahau kuwa ni mwanafunzi wangu katika shule ninayo ifundisha

Rahma taratibu akaanza kuyalegeza macho yake huku vidole vyake akivisogeza katika kifua changu kilicho jaa nywele nyingi ambazo kwa mwanamke mwenye kuyajua mapenzi huwa hupata furaha anapoziona nywele hizo na.Rahma akaanza kuzichezea taratibu huku akionekana kuwa na raha ya ajabu kwa jinsi nilivyo choka wala asinge nishika kwani mpute mpute nilio upata kwa mama Fety ulinifanya kiuno na mgongo vyote kuniuma

Kauli ya polisi kufuatia Mtu Mmoja Kupigwa Risasi Kwenye Maandamano ya CHADEMA Jana

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi, wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walioandama jana Februari 16, 2018.

Wafuasi hao wa CHADEMA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa uchaguziwa chama hicho.

Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa ukifanyika mkutano wa kampeni wa Chadema na yalipofika eneo la Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia

Kamanda Mambosasa amesema kuwa watu hao waliokuwa wakiandamana, walizuia mabasi yanayotoa huduma ya usafiri wa mwendokasi, na kuanza fujo kwa kurusha mawe, hivyo polisi waliingilia kati na kuwatawanya kwa kufyatua risasi kadhaa hewani, na kati ya risasi zilizofyatuliwa, moja ilimpata mtu.

“Walizuia mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu),” alisema.

Ufafanuzi huo wa Mambosasa licha ya kutoweka wazi kama mtu huyo aliyepatwa na risasi hiyo amefariki dunia ama la, umekuja huku ikidaiwa kuwa aliyepigwa risasi na kupoteza maisha ni mwanafunzi wa elimu ya juu.

Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilianza kusambaa tangu jana, Ijumaa jioni katika mitandao ya kijamii sambamba na kuwekwa picha yake huku ikieleza kuwa amepigwa risasi wakati akiteremka katika basi la daladala.

Mambosasa alipoulizwa kama mtu huyo ni mwanafunzi wa elimu ya juu amesema kuwa haijathibitishwa kama ni mwanafunzi nab ado uchunguzi unaendelea ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Haijathibitishwa hiyo, nipo kwenye pilika za uchaguzi, nadhani nitajibu hilo nitakaporejea ofisini na kupata taarifa,” alisema.

Aliyepigwa Risasi na Polisi na Kufariki Wakati wa Maandamano ya CHADEMA Ni Mwanafunzi wa NIT, Sio UDSM

$
0
0
Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) imepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha mwanafunzi Aqulina Akwilini ambaye inasemekana amepigwa risasi na polisi wakati wakikabiliana na waandamanaji wa Chadema jana.

Awali taarifa hizo zilimhusisha mwanafunzi huyo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lakini baada ya uchunguzi wa kina imebainika ni mwanafunzi anayesoma Chuo cha Usafirishaji (NIT) mwaka wa kwanza.

Daruso inalaani vikali kitendo hicho kilichotokea na kutumia nafasi hii kushauri polisi kujitafakari kama ni sahihi kupambana na raia wa Tanzania kwa kutumia silaha za moto.

Daruso pia amekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na cha kulaaniwa na kukemewa na kila Mtanzania yeyote bila kujali tofauti  za kisiasa.

‘’Pamoja na tofauti zetu nyingi kama vyama , dini ,ukabila na kadhalika , taifa letu limejengwa kwenye misingi ya undugu, umoja, mshikamano na si matumizi ya nguvu kupita kiasi au kukiuka sheria na taratibu za nchi yetu,’’ imesema barua hiyo ya Daruso kwa vyombo vya habari.

Mgombea Ubunge Kinondoni Salumu Mwalimu Akamatwa na Polisi

$
0
0
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu amekamatwa  na polisi katika kituo cha kupigia kura cha Idrisa kata ya Magomeni.

Tukio hilo limetokea Muda mfupi baada ya  baadhi ya wananchi wa kata hiyo kudai kuwa katika kituo hicho kuna mtu ametoroka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na polisi akiwa amelibeba sanduku hilo.

Mwalimu  aliyefika kufatilia undani wa tukiio hilo la kuibiwa Sanduku, alikamatwa nje ya kituo hicho na kupakizwa katika gari la polisi aina ya defender huku taarifa za awali zikidai kuwa alikwenda eneo hilo na kundi kubwa la watu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa Mwalimu amesema kuwa hana taarifa zozote.

Baada ya kufikishwa kituo cha polisi Magomeni, Mwalimu aliingizwa ndani na kukaa takribani robo saa na kuachiwa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images