Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Milipuko miwili ya mabomu yautikisa mji wa Zanzibar...

$
0
0
Milipuko  miwili  inayosadikiwa  kuwa  ni ya  mabomu imetokea  katika  maeneo  mawili  tofauti  mjini  Zanzibar  na  kusababisha  hofu  kubwa  kwa  wananchi.... Mlipuko  wa  kwanza  umetokea  katika  hoteli  ya  Mercury  iliyopo  Forodhani  na  wa  pili  umetokea  kanisa  la  Anglikana  eneo  la  Mkunazini... Habari  zaidi  zitakuijia  hivi  punde. <!-- adsense -->

Madai ya Wajumbe wa Bunge la Katiba kutaka nyongeza ya posho yagonga MWAMBA .....

$
0
0
Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba.     Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.  

Wananchi watishia kuwachoma moto wanajeshi wastaafu wa JWTZ wilayani Arumeru

$
0
0
Zaidi ya wakazi 300 wa kitongoji cha Olmapinuu katika kijiji cha Bwawani  wilaya ya Arumeru,  juzi waliwashikilia kwa saa sita askari  wanne wastaafu wa Jeshi la Wananchgi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa na trekta lao wakidai kuwa wamevamia eneo la shamba la wanakijiji hao.  Wananchi hao waliwatishia wastaafu hao kuwa watawateketeza kwa moto endapo wataendelea kulima shamba hilo. Sakata

Picha kutoka bungeni: Waziri mkuu akiwa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba mjini Dodoma leo

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Zamani wa Morogoro, Shamim Khan, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Februari 24, 2014. Kulia ni mbunge wa Sumve Richard Ndassa. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Zamani wa Morogoro, Shamim Khan, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma

Picha za milipuko ya mabomu iliyotokea Zanzibar leo mchana

$
0
0
  Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu cha mlipuko katika eneo la mkunazini, na kuleta mtafaruku  katika majira ya mchana..Katika mlipuko huo hakuna mtu aliyepata majeraha na uharibifu wa majengo katika eneo hilo.     Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la

Lady JayDee aeleza sababu za kujifunza Karate...Anataka kumkabili nani? Bofya hapa umsikilize

$
0
0
Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.   Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani

"Mbunge anayeona posho haimtoshi afungashe virago aondoke"....Mwigulu Nchemba

$
0
0
Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.    Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya  madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, kugonga mwamba baada

Baraza la Mitihani latoa ufafanuzi jinsi alama na MADARAJA ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2013 yalivyopangwa

$
0
0
Baraza la Mitihani nchini limetoa ufafanuzi wa alama na madaraja yalivyopangwa kutokana na matokeo ya mtihani wa watahiniwa walioitimu Kidato cha Nne 2012/13 baada ya malalamiko yaliyotokana na mkanganyiko wa utaratibu huo mpya ambao haukuwepo katika miaka ya nyuma. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde amesema

Daktari FEKI akamatwa hospitali ya Muhimbili......Hili ni tukio la tatu kutokea katika hospitali hiyo

$
0
0
Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya

Mwanafunzi wa chuo cha afya Bugando ajishindia gari ya kampuni ya beforward kupitia mtandao wa facebook

$
0
0
Bwa.Marco Hingi akifurahia mara baada ya kujishindia gari hilo aina ya Noah kutoka kampuni ya Be Forward  **** Kampuni ya uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka JAPAN ya BEFORWARD imeendesha shindano la kuwapata washindi 25 duniani kote waliojielezea jinsi wanavyoweza kuitumia kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambapo

Kijana anusurika kuuawa baada ya kunaswa akiiba ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.

$
0
0
  Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo  kizito  baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini

CHADEMA Majanga tena: Madiwani wake wawili wajiuzulu, Wachana kadi za chama na kuhamia CCM

$
0
0
Madiwani  wawili wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  katika Manispaa ya Shinyanga wametanganza kujiuzulu nyadhifa zao wakidai uongozi ngazi ya taifa  wa chama hicho unaendekeza majungu na  kudhalilisha baadhi ya viongozi kwa kuwaita wahaini au wasaliti bila kuchambua ukweli. Madiwani hao, Sebastiani Peter  kutoka kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo,

Dr. Slaa adai kuwa Kiongozi anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi .....Asema hata wakibaki watatu, chama chao HAKITAKUFA

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa mbunge au diwani anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi msaliti wa chama.   Dk. Slaa alitoa msimamo huo jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa CHADEMA jimboni Kalenga, Grace Tendega, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mnadani,

Magari yatekwa jijini Mbeya, Abiria wajeruhiwa kwa mapanga na marungu.....Watu 10 wakamatwa na jeshi la polisi kwa mahojiano

$
0
0
WATU wasiofahamika majina wala makazi yao, juzi walifunga Barabara Kuu ya Mbeya-Njombe, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya kwa kuweka mawe, magogo, kuteka magari na kujeruhi abiria waliokuwa katika magari hayo.  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mbeya jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Robert Mayala, alisema tukio hilo lilitokea saa 1:30 usiku, Kijiji cha Machimbo, Kata

Polisi wafafanua jinsi milipuko minne ya mabomu ilivyotekea huko Zanzibar na kuua mtu mmoja

$
0
0
JESHI la Polisi Zanzibar, jana limetoa ufafanuzi wa matukio ya milipuko iliyotokea katika maeneo manne tofauti. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Hamdani Omari Makame, alisema tukio la kwanza lilitokea Februari 23 mwaka huu, saa saba mchana eneo la Pangawe. Alisema mlipuko huo ulitokea baada ya waumini wa dhehebu la Evengilistic kumaliza ibada na haukuleta madhara

Ujumbe wa Ray C kwenda kwa watumiaji wa dawa za kulevya

$
0
0
  Ray C   ni  Miongoni mwa mastar  wa Bongo ambao waliingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya ingawa baadae alikuja kuacha baada ya kuanza kutumia dozi rasmi ya kuacha matumizi ya dawa hizo.  Habari  njema  kutoka kwake  kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa taarifa kuhusu kufungua asasi ya kuwaelimisha vijana na jamii kuhusu madhara ya utumiaji wa dawa hizo za kulevya.     Huu  ni 

Ali Kiba aeleza sababu ya ukimya wake, ujio wake mwaka huu na kazi aliyofanya na Mwana Fa na Ay

$
0
0
Kwa kipindi kirefu mkali wa ‘Single Boy’ Ali Kiba amekuwa kimya bila kutoa kazi yake binafsi huku ukimya wake ukizua maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa muziki Tanzania.   Lakini  February 25 Ali Kiba amezua maswali mengine kwa mashabiki wake baada ya kuweka kwenye Instagram picha inayomuonesha akiwa na AY na Mwana Fa na kuandika ‘@Aytanzania&007#mj record #wait for it bonge

Togolani Mavura ateuliwa kuwa msaidizi wa Rais ( Hotuba )

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Togolani I. Mavura (pichani) kuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) kuanzia Februari 8, mwaka huu, 2014. Taarifa iliyotolewa Jumanne, Februari 25, 2014, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Bwana Mavura anachukua nafasi ya Bwana Msafiri Marwa ambaye amehamishimiwa

Sheikh Ponda agonga mwamba tena Mahakamani.....Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) awasilisha pingamizi akiitaka mahakama itupilie mbali mbaombi yake

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ameendelea kuweka pingamizi dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda akipinga maombi yake ya kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.    Sheikh Ponda anakabiliwa na kesi ya jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, akidaiwa kufanya uchochezi maeneo mbalimbali mkoani humo na kukaidi amri ya

Mavazi ya nguo fupi za kubana ( Vimini ) na mengine ya nusu uchi ni marufuku kuingia nayo ndani ya Bunge maalum la Katiba

$
0
0
Wajumbe wanawake wa Bunge Maalumu la Katiba na wageni wa jinsi hiyo watakaovaa nguo fupi ‘vimini’ au nguo za kubana, hawataruhusiwa kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge.    Hayo yamo katika mapendekezo ya rasimu ya kanuni za uendeshaji wa Bunge hilo, zilizowasilishwa katika semina mahsusi ya kupokea rasimu hizo, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati Maalumu, Profesa Costa Mahalu.  
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images