Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ramaphosa Aongoza Jahazi Kumung'oa Zuma Madarakani, Ampa Saa 48

$
0
0
Chama Tawala Nchini Afrika Kusini (ANC) kimempa masaa 48 rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kujiuzulu katika nafasi yake ya urais.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, vimesema kuwa hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kuwepo kwa mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala nchini humo ANC.

ANC kilifanya mazungumzo ya kina na baadaye kutuma ujumbe wa watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba achague moja ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Aidha, Chama hicho kimeona kuwa njia hiyo ni rahisi zaidi kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Hata hivyo, Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa ndiye anayeongoza shinikizo la kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, huku akiahidi kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama hicho, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.

Diamond Platnumz, Hamisa warudi tena Mahakamani

$
0
0
Nyota wa muziki wa Bongo fleva na Rais wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao.

Diamond na Mobetto wamefika Mahakamani hapo, ikiwa ni wiki moja baada ya kufika na kusuluhishwa.

Hamisa Mobetto akizungumza nje ya Mahakama  amesema; “Maamuzi nimeridhika nayo na tumekubaliana kuhusu matunzo ya mtoto, Pande zote mbili tulikaa na kukubaliana, nashukuru kila mtu tumekubaliana na tumeridhika, hivyo yamekwisha.”

Naye Diamond Platnumz amesema mara ya mwisho ilikuwa ni usuluhishi haikuwa Kesi na leo tumeweka rekodi sawa ili kutunza kumbukumbu na kuweka vitu sawa ili yasije kuzushwa mengine ya uongo na kweli.

“Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani. Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz

Zitto Kabwe amemtembelea Samatta Ubelgiji

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe leo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amewajulisha watanzania kuwa amefanikiwa kufika nyumbani kwa nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta.

Zitto amefika nyumbani kwa Samatta nchini Ubelgiji katika mji wa Genk na kumjulia hali na amethibitisha kuwa Samatta anaendelea vizuri.

==>Huu ni ujumbe wa Zitto Kabwe
Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.

Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi. Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Genk
Ubelgiji
Februari 13, 2018




RC Makonda apiga marufuku ukamataji wa bodaboda kwa kuvamia

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa onyo kali kwa kampuni zinazofanya kazi ya kukamata pikipiki (bodaboda) kwa mtindo wa kuvamia kitendo kinachohatarisha usalama wa dereva na abiria.

Makonda amesema zipo baadhi ya kampuni zimekuwa zikivizia madereva wa bodaboda kisha kuwavamia na kuwakamata na wakati huohuo kuwapiga kitendo ambacho amesema hawezi kukiruhusu kiendelee kwenye mkoa wake.

Makonda ametoa onyo hilo wakati wa kikao na madalali wanaotekeleza hukumu za mahakama na benki kilicholenga kuwatambua na kupitia nyaraka zinazowapa mamlaka ya kufanya kazi hiyo ili wasionekane matapeli na waweze kupata ushirikiano wa serikali.

Uamuzi wa Makonda kukutana na madalali hao ni manyanyaso na ukandamizaji unaofanywa na baadhi ya madalali wanaopiga minada nyumba, magari, viwanja, mashamba, ofisi na mali za watu bila kufuata taratibu na kusababisha maumivu makali kwa wananchi.

Amesema zipo kampuni za udalali zinazofoji nakala za hukumu, mihuri, sahihi za mahakama, ofisi ya Mkoa, wilaya na mitaa na wakati mwingine kufanya minada bila kufuata taratibu.

Kutokana na hilo Makonda amezitaka kampuni zote za udalali Dar es salaam kuwasilisha nakala za nyaraka ya usajili kwa mwanasheria wa mkoa zipitiwe na kujiridhisha ili wapewe ushirikiano na serikali.

Nao madalali wamemshukuru Makonda kwa uamuzi wa kuwatambua ili wapate ushirikiano wa serikali kwakuwa wapo baadhi ya madalali waliokuwa wakifanya kazi hiyo kinyume na sheria na kuwachafulia kazi wale wenaofata taratibu za kazi hiyo.

Mwanasheria mkuu Kenya ajiuzulu

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai amejiuzulu nafasi hiyo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka sita. Na tayari Rais Uhuru Kenyatta amemteua Jaji Paul Kihara Kariuki kushika wadhifa huo.

Kwa upande wake, Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa namna alivyolitumikia Taifa kwa weledi katika nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Profesa Muigai alitangaza leo kujiuzulu wadhifa huo alioteuliwa Agosti 27, 2011.

"Nimepokea kwa masikitiko uamuzi wa mwanasheria mkuu Githu Muigai. Namshukuru kwa huduma yake katika kipindi cha miaka sita na nusu. Nimemteua Jaji Paul Kiharara Kariuki,” Rais Uhuru Kenyatta alichapisha katika mtandao wake wa Twitter.

Profesa Muigai atakumbukwa kwa namna alivyokuwa mstari wa mbele kuwatetea watuhumiwa dhidi ya uhalifu wa binadamu uliotokana na vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007 na kuendelea hadi 2008.

Vurugu hizo zilifunguliwa kesi kwenye Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) iliyopo The Hague nchini Uholanzi na aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu, Luis Moreno-Ocampo.

Orodha ya watuhumiwa hao iliyofahamika kama ‘Ocampo six’ ni Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto wakati huo alikuwa waziri wa Elimu, mawaziri wengine wa zamani Henry Kosgey, Francis Kirimi Muthaura, aliyekuwa mkuu wa polisi Mohammed Hussein Ali na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang.

Pia, Profesa Muigai aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari vya Kenya akimtaka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda kuliheshimu Taifa la Kenya kwa kuonyesha weledi wakati wa kuendesha kesi iliyomkabili Rais Uhuru na wenzake, kwamba Kenya siyo Taifa lililoshindwa kutekeleza wajibu wake.

Hata hivyo, Profesa Muigai mwaka 2016 alipata changamoto baada ya muungano wa makanisa ya Kipentekoste kumtaka kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kuishauri Serikali kuhusu masuala ya kidini.

Muungano wa makanisa hayo ulitoa hoja hiyo kufuatia kusajiliwa kwa kikundi cha watu waliokuwa wakidai hawamuamini Mungu, kwa madai anakwenda kinyume na katiba inayotambua uwapo wa Mungu.

Rais Zuma akubali kujiuzulu Lakini kwa Masharti

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali kuachia madaraka ya kuongoza nchi hiyo, baada ya wito uliotolewa na chama chakle ANC kumtaka kujiuzulu ndani ya masaa 48.

Makubaliano hayo ya kujiuzulu yamekuja na sharti kwamba atafanya hivyo baada ya miezi mitatu mpaka sita kuanzia sasa, na bado uongozi wa ANC haujatoa jibu kama umeridhia ombi hilo.

Hapo jana chama cha ANC kikiongozwa na Cyril Ramaphosa ambaye alichukua wadhifa wa Zuma wa kukiongoza chama hiko, kilituma ujumbe maalum kumtaka rais huyo kuachia madaraka, kutokana na harakati nyingi za kumtaka afanye hivyo tangu mwaka jana.

Jacob Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa, na Bunge la nchi hiyo kujaribu kupiga kura za maoni ili kumuondoa lakini ilishindikana, na ndipo chama kuamua kuchukua uamuzi huo mgumu wa kumtaka afanye hivyo, la sivyo kitamtoa kwa nguvu.

Iwapo Zuma atafanya hivyo atakuwa amefuata nyayo alizopita rafiki yake mkubwa Robert Mugabe ambaye alikuwa Rais wa Zimbabwe, aliyetakiwa kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka 2017 na jeshi la nchi hiyo, la sivyo lingetumia nguvu kumng'oa, na hatimaye kuachia madaraka.

Waziri Mkuu: Bahari Kuu, Viwanja Vya Ndege Vyabainika Kupitisha Dawa Za Kulevya

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini kwamba maeneo ya bahari kuu, bandari, vituo vya mabasi na viwanja vya ndege yanayotumika sana katika kupitisha dawa za kulevya.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya wameendelea kukamatwa, lengo ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 13, 2018) wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga  kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Amesema mbali na kukamata meli, pia Serikali imewakamata wasambazaji pamoja na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya sambamba na watumiaji, lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kizazi chenye uwezo wa kuzalisha mali. 

Waziri Mkuu amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulenya, ambapo hivi karibuni imekamata meli nyingi, moja ilikiwa inatokea pwani ya Msumbiji na ilikamatiwa maeneo ya Mtwara ikiwa na dawa nyingi za kulevya.

“Niwakati wa Serikali kuendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na leo hii tunawakabidhi gari hili jipya kabisa ili iweze kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo.”

Pia Waziri Mkuu amewataka Watanzania waachane na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na  kazi ya kusambaza, kuzalisha na kutumia na watakaokamatwa wakijihusisha nayo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa sasa Serikali inajenga maabara ambayo itatumiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa wanazozikamata.

Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa mara wanapowabaini wafanyabiashara, watumiaji na wasambazaji wa dawa hizo. Pia wahakikishe wanawalinda vijana ili wasijihusishe na dawa za kulevya.

Kwa upande wake Siyanga aliishukuru Serikali kwa kuipatia mamlaka hiyo gari, ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waachane na biashara ya dawa za kulevya. Alisema wanapambana kuhakikisha dawa za kulevya ili zisiingie nchini.

Alisema mbali na kudhibiti biashara hiyo, pia wanatoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya vikiwemo vitendo viovu vinavyofanywa na watumiaji ili wachukie na waache kutumia dawa hizo.

Pia wanafanya kazi ya kuwahudumia watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya, hivyo aliwaomba wananchi kutowanyanyapaa waathirika na badala yake wawapeleke katika vituo maalumu vya kutolea huduma za methadone.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 13, 2018.

Waziri Lukuvi Apiga Marufuku Wathamini Wanaofanya Uthamini Nje Ya Serikali

$
0
0
Na Florah Raphael.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi leo amezindua rasmi bodi ya wathamini ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria ya uthamini na usajili wa wathamini ya mwaka 2016 ambayo imeanza  kutumika rasmi Januari mwaka huu.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa sheria wajumbe wa bodi ni lazima kutoka katika taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, ofisi ya Rais TAMISEMI, vyuo vikuu, vyama vya kitaluma vya wathamini, ofisi ya mwanasheria mkuu, taasisi ya mabenki, na bodi ya wakaguzi na wahasibu(NBAA) na kuongeza kuwa kwa muundo huo bodi inahitaji mpana mkubwa wa uwakilishi ili kutekeleza majukumu yake kwa urahisi.
 
Pia amesema kuwa serikali iliona umuhimu wa kuwa na chombo madhubuti kwa ajili ya kusimamia taaluma ya uthamini baada ya kuonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la udanganyifu katika kazi ya uthamini hasa kwenye miradi ya serikali na ya mikopo katika mabenki baada ya Kazi hiyo ya uthamini kuwa chini ya Baraza la wapima ardhi na wathamini (NCPS).
 
Aidha ameweka wazi kwamba tasnia ya uthamini ni ya muhimu sana kwa ustawi wa uchumi kwa ujumla kwani Kazi za wathamini zunahusiana na ukadiriaji wa Mali kwa malengo mbalimbali ikiwemo kuweka rehani za mikopo kwenye mabenki, kodi za ardhi na majengo, mahesabu ya makampuni binafsi na taasisi za serikali hivyo kama Kazi hiyo haitafanywa kwa umakimi na uadilifu inaweza kuchangia kuanguka kwa uchumi na hata watu kupoteza mali sambamba na kusababisha migogoro ya ardhi.
 
Pia amebainisha masuala ambayo yanatakiwa kufanyiwa Kazi kwa haraka ili kufuta dosari zilizopo na kusema kuwa ni kudhibiti kazi ya uthamini kufanywa na watu wasiosajiliwa na bodi na wale wasio ma taaluma ya uthamini, kudhibiti udanganyifu wa thamani kwa ajili ya uthamini kwa ajili ya fidia, kodi na mikopo ya benki, kutoa na kusimamia mafunzo ya Mara kwa Mara kwa wathamini pamoja na kuandaa viwango na miongozo ya uthamini.
 
Pia Waziri ametoa onyo kwa wathamini wanaotumia udanganyifu pindi wanapofanya tathimini pamoja na wale wanaofanya kazi ya uthamini nje ya kazi au miradi ya serikali na kuwaomba wathamini wote kujisajili kwenye bodi ya wathamini ili watambulike na kupata usajili unaotambulika.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa wathamini Dkt.Cletus E.Ndjovu amesema kuwa bodi ya wathamini ni muhimu sana katika suala la maendeleo na kuahidi kwamba watafanya kazi kwa weledi na kwa kufuata sheria ya bodi ya uthamini bila kumwonea mtu aibu ili kuleta heshima katika taaluma ya uthamini.

Waziri Mkuu Azindua Mpango Mkakati Wa Afya Moja

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa mahala safi na salama kwa kuishi na kufanya kazi za kimaendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 13, 2018) wakati akizindua mpango mkakati huo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo amesema dhana ya Afya Moja inafaa kutumika zaidi katika nchi zinazoendelea.

Waziri Mkuu amesema mbali na mpango kufaa kutumika katika nchi zinazoendelea pia hata kwa nchi zinazokaribia maeneo ya wanyama pori kama Tanzania kutokana na kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa rasilimali.

Amesema kwa upande wa nchi za Afrika hali ni hatarishi zaidi kwa kuwa Bara hilo, lina sehemu nyingi zinazokaribia mapori makubwa ya wanyama kama Bonde la Mto Kongo, ambalo mazingira yake yamekuwa ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa (RVF), Marburg na mengineyo.

Waziri Mkuu amesema kwa kutambua hilo, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) na wadau wengine wa Maendeleo, imeendelea kutekeleza agenda ya Afya Moja nchini tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mjini Arusha na  Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

“Utekelezaji wa Mpango huu unakwenda sambamba na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2015-2020) ya kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora itakayowawezesha kuzalisha mali na kutoa huduma mbalimbali ambayo ni muhimu sana katika kufikia azma ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda.”

Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema uzinduzi wa mkakati huo ni ngao tosha kwa nchi katika kuzuia na kudhibiti magonjwa.

Alisema pamoja na kutekeleza kanuni za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ambazo zinahitaji ushirikiano  wa sekta mbalilmbali kwa kutumia dhana ya afya moja, mpango mkakati huo unaleta msukumo katika Ofisi ya Waziri Mkuu  kuendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali kudhibiti magonjwa.

Bibi Jenista alisema uratibu wa afya moja unakwenda sambamba na matakwa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (IOE) na Shirika la Kimataifa la Chakula la Kilimo (FAO) ambayo yanashirikiana katika kudhibiti magonjwa yanayoambukiza na usugu wa dawa.

Benki ya Dunia Yakana Kuishinikliza Serikali kusimamisha zoezi la bomoa bomoa Dar

$
0
0
Benki ya Dunia (WB) ofisi ya Tanzania imekanusha madai ya kwamba iliishinikiza Serikali kusimamisha zoezi la bomoa bomoa ya makazi ya watu kwenye hifadhi ya barabara ya Morogoro.

Madai hayo ambayo yaliripotiwa na chombo kimoja cha habari, kabla ya kusambaa kwenye mitandao ya jamii yalibainisha kwamba WB walishinikiza kusimamishwa kwa bomoabomoa kwa kuwa ndio wafadhili wa mradi wa barabara hiyo.

Ilidaiwa na vyombo hivyo kuwa WB ilitishia kusimamisha utoaji wa fedha kwa ajili ya upanuzi wa barabara hiyo, ambayo itakuwa na miundombinu ya barabara ya mwendokasi (BRT) pamoja na barabara kuu kuelekea Morogoro, mpaka hapo fidia itakapolipwa.

Akitolea ufafanuzi madai hayo leo Februari 13, 2018  msemaji wa ofisi ya WB Tanzania,  Loy Nabeta amesema ofisi yake haijatoa taarifa yoyote ya kuitaka Wakala wa Barabara (Tanroads) kisitisha bomoa bomoa hiyo.

“Tunaelewa kwamba gazeti lilifanya mahojiano na baadhi ya wamiliki wa nyumba. Benki ya dunia inathamini sera na utaratibu unaotakiwa kufuatwa kutekeleza mradi wowote ule inaoufadhili,” amesema msemaji huyo.

“Hizi ni nyaraka za kisheria ambazo tulisaini na Serikali kwa kila mradi tunaoufadhili na huwa tunahakikisha kwamba utekelezaji wake unafuata utaratibu.”

 Msemaji huyo aMEsema wamepokea malalamiko mengi mwaka jana kutoka kwa wamiliki wa nyumba zilizojengwa pembezoni mwa barabara ya Morogoro ambao walipewa notisi ya kubomoa na Tanroads.

“Tuliwawasilisha malalamiko serikalini. Desemba 22, 2017, tulipata barua toka kwa katibu mkuu wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi kwamba watasimamisha ubomoaji wa nyumbakwenye kipande cha kuanzia Ubungo hadi Kimara,” amesema kwenye taarifa hiyo.

Amesema bomoa bomoa hiyo ambayo ilitekelezwa kuanzia Kimara hadi Kiluvya, ni mwendelezo wa utekelezaji wa upanuzi wa barabara ya Morogoro, haihusiani na mradi wowote unaofadhiliwa na WB.

Bomoa bomoa hiyo inahusisha nyumba na mejengo 1,300 ambavyo vinadaiwa kujengwa kwenye hifadhi ya barabara  ambayo ni meta 121.5 toka katikati ya barabara ya sasa. Hata hivyo, nyumba 1,000 zimekwisha bomolewa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, upanuzi wa barabara ya Morogoro (kutoka Kimara hadi Kiluvya) unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

LHRC Yamvaa Makonda kuingilia mahakama

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeponda kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kusimamisha shughuli za mabaraza ya kata na kuingilia utendaji kazi wa mahakama.

Kimesema kuwakusanya wananchi kusikiliza kero zao za ardhi maana yake ni kutatua kero hizo bila sheria.

Akizungumza leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko dhidi ya ukiukwaji wa utawala wa sheria, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Felista Mauya amesema watendaji wa Serikali wanapaswa kuheshimu utaratibu wa utendaji kazi, kuacha kuingilia majukumu ya taasisi na mihimili mingine.

Huku akinukuu alichokisema Makonda Februari 10, 2018 jijini Dar es Salaam, Mauya amesema, “ Makonda alisema ‘mahakama haitaki kuguswa kwa kisingizio cha mhimili mwingine, wamechukua nafasi ya Mungu na mimi ni mteule wa Mungu lazima niwaseme’. Huku ni kushambulia utendaji wa mahakama kinyume cha Katiba aliyoapa kuilinda.”

Februari 10, 2018 Makonda alipokea ripoti kutoka kwa wanasheria waliosikiliza kero za wananchi kwa uratibu wa ofisi yake.

Katika mkutano huo, mkuu huyo wa mkoa aliwaita jukwaa kuu wakuu wa idara ya ardhi na nyinginezo kutoka manispaa zote tano za Dar es Salaam na kuwahoji kuhusu idadi ya migogoro na changamoto katika maeneo yao ya kazi.

Katika maelezo yake ya leo, Mauya amesema ibara ya 107A ya Katiba inasema mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki Tanzania itakuwa mahakama.

“Wakati huohuo Ibara ya 107B inasisitiza uhuru wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa hiyo kwa mujibu wa ibara hii mihimili mingine ya dola na watendaji wake hawapaswi kwa namna yoyote ile kuingilia utendaji wa mahakama,” amesema Mauya.

Amebainisha kuwa kituo hicho kinawakumbusha viongozi wa Serikali na wanasiasa kuwa hawana mamlaka kisheria kuingilia utendaji kazi wa chombo hicho wala kuelekeza utendaji, badala yake wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu katika upatikanaji wa haki.

“Tumebaini mkutano wa mkuu huyo wa mkoa na wananchi wa jiji lake kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo yamekuwa yakifanywa na sio tu na Makonda, bali pia na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali,” amesema.

 Amesema sheria ya utatuzi ya migogoro ya ardhi inamtaja waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa na mamlaka juu ya mabaraza ya ardhi ya kata.

“Kifungu cha 10(1) cha sheria ya utatuzi wa migogoro ya ardhi namba 216 ya mwaka 2002 kinayatambua mabaraza ya kata kama mahakama ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa ngazi ya kata, hivyo kwa mujibu wa sheria hizi wakuu wa mikoa hawana mamlaka ya kusimamisha, kuendesha wala kuelekeza utendaji,” ameongeza Mauya.

Kwa upande wake, Mkurugezi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga amesema lengo la tamko hilo ni kutaka umma ufahamu kuwa kitendo cha wakuu wa mikoa kuingilia mahakama si sahihi.

Amesema pia wametoa tamko hilo ili wananchi waelimike na kutambua kuwa ili kufikia haki kuna utaratibu umewekwa kisheria.

“Kwanza wajue ni utaratibu upi uliopo kisheria kwani kuna mahakama kitengo cha ardhi, mabaraza ya kata lakini tukisema tuwakusanye kila mmoja aeleze shida yake tutakuwa tunatatua kero bila sheria,” amesema.

Habari Zilizopo Katika Magazetii ya Leo Jumatano ya February 14

Waziri Mkuu Akabidhi Gari Kwa Mamlaka Ya Kupambambana Na Dawa Zakulevya

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa( Aliye vaa miwani) jana  (Jumanne, Februari 13, 2018) amekabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga kwa ajili ya Mamlaka hiyo. Makabidhiao hayo yamefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Kiongozi CHADEMA Auawa....Mbowe Asimulia Alivyotekwa na Mwili Wake Kuokotwa Ufukwe wa Bahari

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 13,2018 alisema John alitoweka siku moja iliyopita.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.

Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi leo  Februari 14,2018.

Mbowe alisema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari.

Mbowe alisema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba, walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi.

Alisema mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kuashiria alipigwa na kitu kizito.

Kuhusu Mallya alisema alipigwa panga kichwani na alivunjwa mkono. Mbowe ametaka polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Mallya aliyekuwapo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari alisema walikuwa wakitembea na John ndipo waliposimamishwa na kuingizwa ndani ya gari.

Alisema alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipozinduka alijikuta ufukweni alikojikokota hadi barabarani ambako alipata msaada wa bajaji na alikwenda Hospitali ya Mwananyamala alikotakiwa kuwa na taarifa ya polisi ambayo aliipata Kituo cha Polisi Oysterbay.

Rufani ya Lema kusikilizwa Juni 15

$
0
0
Rufani ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, baada ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Sekela Mosha, kutokuwapo mahakamani hapo.

Katika kesi ya msingi, Lema alimkataa Hakimu Desderi Kamugisha, akisema hawezi kutenda haki katika kesi yake ya madai ya kumtukana Rais John Magufuli.

Alidai hakimu huyo aliwahi kumnyima dhamana hali ambayo ilimfanya asote mahabusu miezi zaidi ya  minne.

Akiahirisha rufani hiyo jana, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Angelo Rumisha, alisema itasikilizwa Juni 15, mwaka huu, saa 3:00 asubuhi mbele ya Jaji Mosha.

Katika rufani hiyo, Lema aliwasilisha hoja zake zikiwamo za kumkataa Hakimu Kamugisha kuendelea na kesi yake ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli kwa madai ya kuwa na upendeleo.

Hoja nyingine ni kuwa taarifa ya kukata rufani haianzishi kukata rufani kutokana na hakimu huyo kukataa kujitoa katika kesi yake, baada ya kumkataa.Katika rufani hiyo, Lema anatetewa na Wakili John Mallya.

Awali katika kesi hiyo, Oktoba 9, mwaka jana, Wakili Sheck Mfinanga, alijitoa kuendelea kumtetea Lema kwa kile alichodai kuomba mwenendo wa kesi zaidi ya mara tatu mahakamani hapo na kushindwa kupewa, ili aweze kukata rufani Mahakama Kuu, lakini Hakimu Kamugisha aligoma kutoa.

Wakili Mfinanga alimtaka Hakimu Kamugisha kujitoa kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Lema, licha ya mbunge huyo kumtaka afanye hivyo kwa kile alichodai aliwahi kufanya uamuzi wa hila na kusababisha kusota mahabusu zaidi ya miezi minne.

Hata hivyo, hakimu huyo aliamua kuendelea na shauri hilo, hata pale mawakili wa Lema walipowasilisha kwa mdomo kusudio la kukata rufani Mahakama Kuu kwa lengo la kupinga uamuzi huo wa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.


OFA ya Valentine...Jipatie Riwaya Kali za Kusimumua kwa Punguzo la Bei

$
0
0
NI SIKU YA WAPENDA NAO
Mimi na timu yangu ya @Storyzaeddytz TUNA PENDA kuwapatia ofa ya hadithi zetu zifwatazo kwa wasomaji wetu wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Hadithi zote zitakazo patikana katika ofa ya leo, tuna ziuza kupitia Whatsapp 0657072588 au whatsapp 0768516188. Pia una weza kuwasiliana nami muandishi kwa namba 0657072588 au 0768516188.

1.President wife(Muendelezo wa SORRY MADAM D.F.E) utaipata leo kwa sh 8000 tu.
2. AIIISS YOU KILL ME sh 15000
3. AIISSII YOU KILL ME LEGACY sh 10000.
4. SORRY MADAM Season one sh 5000
5. SHE IS MY WIFE sh 4000
6.AM NOT A DOCTOR sh 8000
7. POWER sh 15000
8. SEX DEALER sh 3000
9. HARD DAY sh 3500

Pia tuna kukaribisha ujiunge katika group la V.I.P STORIES ambapo utasoma hadithi mpya za SIN na TANGA RAHA SEASON TWO. Ili uweze kujiunga na group nitafute whatsapp kwa namba 0657072588.
Katika group ndani ya mwezi mmoja utasoma episode 48
Huduma zetu ni za haraka na tuna wajali wateja wetu karibuni sana
By Eddazaria G.Msulwa
C.E.O www.storyzaeddytz.com

Serikali Yatoa Masharti Mapya Kwa Mtu Anayetaka Kuingia Ndani ya machimbo ya Tanzanite

$
0
0
Serikali imetangaza utaratibu mpya wa kuingia katika machimbo ya Tanzanite yaliyopo Mererani ambapo kuanzia Februari 15 ni lazima mtu awe na kitambulisho maalumu.

Akizungumza na wachimbaji wa madini hayo  jana Februari 13  mjini hapa, Kamishna na Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma alisema vitambulisho vitakavyotakiwa ni vile vinavyotolewa na Wizara ya Madini.

Juma alisema hadi sasa ni vitambulisho 6,000 ambavyo tayari vimetolewa na katika machimbo hayo kuna wachimbaji zaidi ya 15,000.

"Baada ya ujenzi wa ukuta kukamilika sisi kama wizara tutaanza Februari 15 kudhibiti kuingia migodini," alisema.

Alisema wamiliki wa migodi yote, wachimbaji na madalali wa madini pamoja na watu wengine ambao watataka kuingia kwenye eneo lililozungushwa ukuta lazima wawe na vitambulisho.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula alisema  agizo hilo la Serikali halina utani, hivyo ni lazima wanaotaka kuingia migodini wafuate sheria.

Alisema  lengo ya mpango huo ni kuhakikisha madini hayatoroshwi na pia Serikali inapata stahiki zake kabla ya madini kutoka nje ya uzio.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (Marema), Sadiki Mnenei alisema wanaunga mkono mpango wa vitambulisho, lakini wanaomba muda zaidi wa kuzuia wasio na vitambulisho hadi Machi mosi.

"Ili kutoathiri kazi zetu tunaomba utaratibu mpya kuanza mwezi ujao kwani gharama za kitambulisho ni kubwa kwa kuwa kila mchimbaji anatakiwa kutoa Sh3,500 na mmiliki wa mgodi Sh5,000," alisema. 

Alisema  kwa wastani mgodi mmoja una zaidi ya wafanyakazi 100, hivyo wote kuwapa vitambulisho wakati mmoja ni vigumu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yawajibu CHADEMA

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezijibu hoja sita za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni.

Majibu hayo yametoka baada ya Chadema kuilalamikia tume na watendaji wake walioteuliwa kusimamia uchaguzi huo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, NEC ilidai haijapokea barua yoyote kutoka Chadema licha ya chama hicho kikuu cha upinzani bungeni, kuvieleza vyombo vya habari kwamba kimeiandikia barua tume kuhusu wakuu wa wilaya kushiriki mikutano ya kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na tume haijachukua hatua zozote.

Taarifa ya NEC ilibainisha kuwa hoja ya pili ya Chadema ni tume kuhamisha vituo 46 vya kupigia kura katika kata tatu za Kigogo, Mwananyamala na Kijitonyama bila kuishirikisha Chadema.

Hoja nyingine ni Msimamizi wa Uchaguzi kutoa uamuzi dhidi ya Chadema kwenye Kamati ya Maadili kwa uonevu na Chadema kuadhibiwa na Kamati ya Maadili kwa makosa yanayotuhumiwa kutendwa na mwanachama wa Chadema na kuwa makosa hayo ni ya kijinai na yalipaswa kushughulikiwa kijinai na si kukipa adhabu chama hicho.

Pia Chadema ilisema kikao hicho kiliendeshwa na mtu asiyepaswa kuwa Mwenyekiti wa Kamati.

Taarifa ya NEC ilieleza kuwa hoja nyingine ni kitendo cha malalamiko ya Chadema dhidi ya wakuu wa wilaya kushiriki kampeni za uchaguzi na Kamati za Maadili kutotenda haki kwa kuwa wenyeviti wake ni makatibu tawala wa wilaya.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani, ilifafanua kuwa tume haijapokea barua au karatasi yoyote kutoka Chadema inayoelezea malalamiko yao.

“Ukweli ni kwamba, Chadema hawajawasilisha barua kwa tume. Hata kama wangewasilisha barua za malalamiko yao, tume ingewaelekeza kusoma na kuelewa Maadili ya Uchaguzi, kwa kuwa lalamiko namba mbili hadi sita waliyoyataja kwenye vyombo vya habari yangeweza kushughulikiwa na Kamati za Maadili ambazo Chadema kama chama chenye wagombea ni sehemu ya wajumbe wa kamati husika,” alisema.

Kailima katika taarifa hiyo, alisema uhamishaji wa vituo umezingatia matakwa ya Kanuni ya 21 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura za mwaka 2008 kama zilivyorekebishwa mwaka 2014.

“Kanuni hiyo ikisomwa pamoja na kipengele cha 9.2(c) cha Kitabu cha Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ya mwaka 2015, vituo vya kupigia kura havitakiwi kuwa kwenye maeneo ya Kambi za Jeshi, Polisi, maeneo ya kuabudia kama vile misikiti na makanisa, nyumba za viongozi au mashabiki wa vyama vya siasa,” alifafanua katika taarifa hiyo.

Kailima pia alisema kuwa kwa kuzingatia matakwa ya kanuni na kipengele tajwa, Januari 31, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni, aliitisha mkutano wa vyama vya siasa vyenye wagombea ubunge na ajenda ilikuwa ni kuhamisha vituo vya kupigia kura.

“llifanyika hivyo kwa sababu mbalimbali zikiwamo baadhi ya vituo kuwa kwenye maeneo ya kuabudia, kuwa jirani mno na ofisi ya chama cha siasa, nyumba za watu binafsi, kwenye maeneo finyu,” alisema.

Alidai kuwa kikao hicho kilishirikisha wawakilishi 16 kutoka vyama 11 vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni.

“Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kinondoni, Mustapha Muro na Katibu wa Chadema wa Wilaya, Shabani Kirita,” Kailima alieleza katika taarifa hiyo.

Kuhusu malalamiko kwamba Msimamizi wa Uchaguzi alitoa uamuzi wa uonevu dhidi ya Chadema kwenye Kamati ya Maadili, Kailima alisema uamuzi hufanywa na Kamati ya Maadili na si Mwenyekiti wa Kamati.

“Tunaikumbusha Chadema sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi hayampi Mamlaka Msimamizi wa Uchaguzi kutoa maamuzi kwenye Kamati ya Maadili. Msimamizi wa Uchaguzi ni Mwenyekiti wa Kikao cha Maadili tu, na kwamba, maamuzi hufanywa na Kamati ya Maadili na siyo Mwenyekiti wa Kamati,” alieleza Kailima katika taarifa hiyo.

Kuhusu Chadema kuadhibiwa kwenye Kamati ya Maadili kwa makosa ya kijinai, Kailima alisema tume imekitaka chama hicho kama hakikuridhika na maamuzi kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.

Kuhusu malalamiko dhidi ya wakuu wa wilaya kushiriki kampeni za uchaguzi, Kailima alisema tume inaitaka Chadema kuwasilisha malalamiko yake kwenye mamlaka husika kwa kuwa sheria na kanuni zimebainisha mamlaka zinazoshughulikia masuala hayo.

Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa kuwahudumia wakimbizi ambao imekuwa ikiutoa kabla na baada ya uhuru, licha ya uchumi mdogo ilio nao. 
 
Waziri Mahiga ametoa wito huo  jana Jijini Dar Es Salaam katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani (World Refugees Council-WRF) kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia juzi kwenye Hoteli ya Hyatt Regecy, Kilimanjaro.
 
Waziri Mahiga alieleza kuwa Tanzania ilipokea wakimbizi kutoka Poland wakati wa vita ya pili ya dunia na mwaka 1959 ilipokea wakimbizi kutoka nchi ya Rwanda. Aidha, baada ya uhuru, Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi mara kwa mara na wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Tanzania ilipokea wakimbizi wengi zaidi duniani.
 
Aliendelea kueleza kuwa athari zinazotokana na kupokea wakimbizi wengi ni nyingi na kubwa hivyo, ni jukumu la Jumuiya ya Kimataifa kuzisaidia nchi zenye wakimbizi wengi, hususan zile zenye uchumi mdogo.

Katika kikao hicho, Waziri Mahiga alitoa ufafanuzi kuhusu msimamo wa Serikali ya Tanzania kujitoa katika mpango wa kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo la wakimbizi duniani (Comprehensive Refugees Response Framework – CRRF). Alisema katika mpango huo wa CRRF, Serikali imesikitishwa na mapendekezo ya mpango huo ya kuitaka Tanzania ikope fedha kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi na kugharamia ukarabati wa miundombinu iliyoharibika. 
 
Halikadhalika, CRRF inapendekeza kuwepo na utaratibu wa kuwapa uraia, ajira na ardhi wakimbizi wanaoingia nchini ili waweze kuwa huru na kujitegemea.
 
Alibainisha kuwa Serikali ilishatoa uraia kwa wakimbizi zaidi ya laki moja na nusu. Jumuiya ya kimataifa iliahidi kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia makazi na huduma nyingine kwa wakimbizi hao. Hata hivyo, Jumuiya ya Kimataifa haijatekeleza ahadi hiyo, badala yake inaitaka Serikali ichukue mkopo wenye riba kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi.

“Misitu, ardhi, mazingira na miundombimu mingine inaharibika kwa sababu ya wakimbizi, halafu tuchukue mkopo na kulipa deni kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi, nadhani sio utaratibu mzuri” Dkt. Mahiga alilalamika.
 
Dkt. Mahiga alieleza kuwa amewasilisha ujumbe wa Serikali kwenye Baraza hilo ili lifikishe kilio cha Tanzania katika Jumuiya ya Kimataifa kwa matumaini kuwa wao wanasikilizwa zaidi. 
 
Kwa upande wake, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, alitoa maelezo kuhusu dhamira ya kuanzishwa kwa WRC. 

Alisema WRC ilianzishwa mwaka 2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Canada na Taasisi isiyo ya kiserikali ya nchi hiyo. Lengo la chombo hicho ni kuangalia sababu zinazopelekea wakimbizi kuongezeka,  matatizo na changamoto zinazowakabili wakimbizi na kutoa maoni ya namna ya kutatua tatizo la wakimbizi duniani.
 
Baraza hilo linaongozwa na jopo la watu wanne wenye uzoefu wa masuala ya wakimbizi duniani ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Canada ambaye ni Mwenyekiti, Mhe. Lyord Axworthy, Mwenyekiti Mwenza ni Rais wa zamani wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti ni Mwanadiplomasia wa zamani wa Canada, Mhe. Paul Heinbecker na Mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza, Mhe. Hina Jilani. 
 
Baraza lilifanya kikao cha kwanza Geneva, Uswisi mwezi Juni 2017 na baadaye kutembelea nchi za Jordan na Ujerumani. Nchi hizo zimetembelewa kwa sababu Jordan ndio nchi inayopokea wakimbizi wengi kwa sasa duniani na Ujerumani kutokana na kuruhusu kupokea wakimbizi kulisababisha Serikali iliyopo madarakani kupata upinzani mkali katika uchaguzi uliopita.
 
Kikao cha pili kinafanyika Afrika na Tanzania imechaguliwa kutokana na uzoefu wake katika masuala ya wakimbizi. Aidha, kikao kijacho kitafanyika Bara la Asia katika nchi ya Thailand na kitafuatiwa na kikao kitakachofanyika Bara la Amerika Kusini.

Katika kikao kinachoendelea nchini, Nchi mbalimbali za Afrika zimealikwa zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya ambazo zieleza uzoefu wao kuhusu matatizo na sababu za kutoa wakimbizi.

Baraza hilo linatarajiwa kukamilisha ripoti yake mwaka 2018 na kuiwasilisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 13 Februari 2018

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images