Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Majaliwa ahamasisha uliamaji wa mazao matano makuu ya biashara

$
0
0
Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo  jana Bungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na utafutaji wa masoko ya Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo mwaka huu.

“Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi,” alisema Waziri Mkuu.

Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.

Pia, Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu alisema, Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.

“Baada ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu,” alisema Mhe. Majaliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na misitu, alisema Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikisha wanavijiji na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa mipaka hiyo.

Hata hivyo alisema ikiwa kijiji kitaonekana kiko ndani ya mipaka ya msitu au pori, tathmini itafanyike na baadae watapewa elimu ya kutoingia ndani ya mipaka ya misitu na mapori ya Serikali Kuu

Misitu yote ya Serikali Kuu inahifadhiwa kisheria na mipaka hiyo inaonekana ili kuondoa migogoro na wananchi.


Serikali yatenga fedha kumaliza migogoro sugu ya ardhi kwenye maeneo ya jeshi

$
0
0
Na Regina Mkonde
Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeahidi kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wananchi na jeshi kwa kulipa fidia wananchi ambao ardhi zao zimechukuliwa na Jeshi bila kulipwa kwa muda mrefu.

Ahadi hiyo imetolewa jana Februari 8, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la Mbunge wa Dimani Juma Ally Juma lililohoji mpango wa serikali katika kutatua mgogoro wa muda kati ya Jeshi na Wananchi wa eneo la Kisakasaka, visiwani Zanzibar.

Dkt. Mwinyi alisema wizara yake imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wanaostahili hasa wale waliochukuliwa maeneo yao na Jeshi pasipo kulipwa fidia.

“Kambi nyingi ambazo zina migogoro ya ardhi, iko ya aina nyingi kuna migogoro ambayo Jeshi limechukua ardhi  ya wananchi hawajalipa fidia, wananchi wamevamia maeneo ya kambi na kadhalika, tumeweka fedha kwenye bajeti ya wizara ili kwenye maeneo ambayo fidia zinahitajika tuweze kulipa fidia, ili kumaliza migogoro, mwaka wa bajeti haujaisha na ni mategemeo yetu fedha zikipatikana tuanze kulipa fidia kwa wanaostahili kulipwa fidia maana wengine wapo wamevamia hawastahili kulipwa fidia,” alisema.

Kuhusu mgogoro wa Kisakasaka, alisema serikali inautambua mgogoro huo uliokuwepo tangu mwaka 1979, na kwamba kilichokwamisha utatuzi wa mgogoro huo ni ukosefu fedha jambo ambalo wizara yake imetenga fedha ili kuleta suluhisho la kudumu kwenye mgogoro huo.

“Wizara ya ulinzi inatambua uwepo wa mgogoro wa ardhi kati ya jeshi na wananchi katika eneo la kisakasaka, katika kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huu, makao makuu ya jeshi imeridhia kurekebisha mpaka wa kambi ya kisakasaka ili kuwaachia wananchi eneo la mgogoro na hivyo kuleta suluhisho la kudumu kwenye mgogoro huo. Zoezi hilo halijafanyika kutokana na ufinyu wa bajeti, hata hivyo katika mwaka huu wa fedha wa mwaka 2017/18 tunategemea kutekeleza zoezi hilo,” alisema.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewasihi wananchi wa Kisakasaka kuwa wastahimilivu wakati serikali inachukua hatua stahiki ili kuzuia madhara yoyote yanayoweza kutokea, endapo wataendelea na shughuli za kilimo na mifugo katika eneo hilo. 

Panya wamkera Mkuu wa Mkoa, atoa maagizo kwa viongozi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuulia panya wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya.

Amesema kuwa ameisikia changamoto hiyo ya uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya kutoka kwa vijana mbalimbali wanaojishughulisha na mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya changamoto za kuendeleza misitu.

“DC tafuta dawa ya panya, wauliwe huko mashambani, ili panya wasiwepo na miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa panya tutawaua kwa sumu huko mashambani wasiwe chanzo cha mioto ambayo mnachoma huko kuwatafuta hawa panya ili wafie huko huko mashimoni msiwapate,” alisisitiza.

Agizo hilo amelitoa katika muendelezo wa kampeni ya upandaji miti mijini na vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, kata ya Mpwapwa, Wilayani Sumbwanga baada ya kuwauliza wananchi wa Kijiji hicho juu ya changamoto aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya, japo wananchi walikataa.

Pia katika kuongezea hilo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha anasimamia sheria ya hifadhi ya mazingira na kuwawajibisha wote wanaohusika na uharibifu wa mazingira.

Nae akisoma taarifa Mkurugenzi wa H/W ya Sumbawanga Nyangi Msemakweli alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto ni muitikio mdogo wa uhifadhi wa mazingira pamoja na mila na tamaduni za wananchi za uwindaji wa panya hali inayosababisha uchomaji wa misitu wakati wa kiangazi.

“Changamoto nyingine ni baadhi ya viongozi wa serikali ya Kijiji kujihusisha na uuzajia wa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya hifadhi ya Kijiji na usimamizi mdogo wa sheria ndogo za vijiji katika utunzaji wa misitu,” Alimalizia.

Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na upandaji kiti wa kibiashara Julius Magaga alimweleza Mh. Wangabo kuwa chnagmoto inayowakatisha tamaa vijana wengi ni kutokana na uwindaji wa panya uliokithiri na kusababisha hasara katika misitu.

Kwa msimu wa 2017/2018 hadi 30/1/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga imepanda miti 830,527 ambayo ni sawa na 55.4% na ina misitu 92 yenye ukubwa wa jumla ya Hekta 49,179.6. Huku Mh. Wangabo akigawa miche 850 kwa kaya 850 za Kijiji cha Mpwapwa, Wilayani Sumbawanga

Polisi watakiwa kuweka mikakati endelevu ili kuboresha afya za wanaowahudumia

$
0
0
Wataalamu wa afya wa Jeshi la Polisi wametakiwa kujiweka tayari katika kujadili changamoto na kuibua mikakati endelevu ili waweze kuboresha huduma za afya kwa watu wenye uhitaji, askari pamoja na familia zao.

Hayo yamesemwa katika hoteli ya SG Resort iliyopo jijini hapa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili ya wakuu wa vituo tiba vya Polisi Tanzania pamoja na wafanyakazi na watumishi wa JSI kuhusiana na uboreshaji utoaji wa huduma za afya katika kukabiliana na jukumu la kupambana na uzuiaji wa maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Alitoa wito kwa Madaktari, Wauguzi na watumishi wengine wanaofanya kazi katika Zahanati na vituo vya afya kuendelea kuwatambua wenye maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa kuwapima, kuwaanzishia dawa na kuhakikisha wote walioanza matibabu wanaendelea kutumia dawa kwa kipindi chote cha uhai wao.

Kamanda Mkumbo aliendelea kuwakumbusha washiriki wa mkutano huo kuendelea kuwahudumia wananchi kwa uadilifu na utunzaji mkubwa wa siri za wateja wanaopatiwa huduma za VCT/CTC ikiwa ni sehemu ya kiapo chao juu ya taaluma yao.

Naye Mganga mkuu wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Msenga, alisema kwamba lengo la semina hiyo ambayo inawezeshwa na JSI/AIDS FREE ni kujitathmini namna ya utoaji huduma bora kwa askari, familia zao pamoja na wananchi wengine wanaotumia vituo hivyo.

Alisema kwamba ubora wa huduma ambao wanatoa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku ambapo wataalamu hao wa afya wamekuwa wakihakikisha kwamba wagonjwa wote wenye matatizo wanapatiwa dawa na walioacha dawa wanafuatiliwa na kuendelea kuhudumiwa.

 Alisema vituo vyao vya Afya vimekuwa vikitoa Ushauri Nasaha na Kupima (VTC) lakini pia kwa wagonjwa wamekuwa wakipata huduma za Uangalizi pamoja na kupewa dawa (CTC) hali ambayo imesaidia watu wengi kujitokeza kupima na kufahamu afya zao.

Awali akizungumza katika Semina hiyo iliyojumuisha washiriki 50 kutoka vituo mbalimbali vya afya vya Polisi nchini, Mkurugenzi wa AIDS FREE Dr. William Nyagwa, alisema kwamba shirika hilo lisilo la kiserikali linataka siku za usoni UKIMWI uwe historia na kuwataka wana semina hao kuendelea kujitoa kufanya kazi hiyo huku akiwahakikishia kwamba wao wapo nyuma yao.

Aidha alitoa wito kwa askari pamoja na familia zao kujitokeza kwa wingi kupata huduma kupitia vituo hivyo vya afya kwani kwa mgonjwa itakuwa rahisi kuhudumiwa na kuwahakikishia kwamba wataalamu wanaotoa huduma katika vituo vya afya wamekula kiapo hivyo wasiwe na wasiwasi juu ya usiri.

Dr. Nyagwa alisema Semina hiyo pia itatoa uhuru kwa washiriki wote kuelezea changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili ziweze kutatuliwa.

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Dawa ya Asili ya Vidonda vya Tumbo, Pumu, Nguvu za Kiume, Korodani kuvimba

$
0
0
Super Muhi Mix Power:  Ni dawa ya nguvu za kiume kutoka Congo, inatibu na kuponesha kabisa tatizo la nguvu za kiume, itakufanya uweze kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka. Itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 20- 25, huimaliha misuli iliyolegea na kusinyaa. Dawa hii imechanganywa na mizizi 11.

Sub 3Mix; Hii ni dawa ya mvuto wa mapenzi, huvuta mume, mke, mchumba na atatimiza ahadi zote alizokuahidi. Pia mkufu na pete ya bahati vipo.

Pata pia dawa ya pumu, ngiri, kisukari, kaswende, vidonda vya tumbo na korodani kuvimba

Mawasiliano: 0659874143-Dr. Hussein Omary

Huduma hii utaipata popote ulipo. Tupo Mbagala Dar es Salaam kwa sasa

Godbless Aibua Upya Sakata la Matibabu ya Tundu Lissu Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amehoji sababu za Bunge kutogharamia matibabu ya Tundu Lissu aliyepo nchini Ubelgiji tangu Januari 7, 2018 akipatiwa tiba ya mazoezi.

Lema ametoa kauli hiyo  jana  Februari 8, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za Bunge za Utawala na Serikali za Mitaa, Katiba na Sheria na Sheria Ndogo.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari lililokuwa nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7 mwaka jana, kupatiwa matibabu Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo siku hiyo hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Alipelekwa Ubelgiji Januari 7 kwa ajili ya tiba ya mazoezi na mara kadhaa familia yake imelishutumu Bunge kuwa kimya kuhusu matibabu ya mbunge huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Katika mchango wake, Lema alianza kwa kutoa pole kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyedai kuwa yupo nchini India kwa matibabu.

“Mheshimiwa Spika anatumia fedha za Serikali kupata matibabu na mbunge Lissu tumeendelea kumtafutia fedha za matibabu mitaani tena kwa mkopo,”alisema Lema.

Alibainisha kuwa kitendo cha Ndugai kutibiwa na fedha za Serikali huku Lissu ambaye ni mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni akishindwa kupewa msaada na Bunge ni jambo ambalo halikubaliki.

Wakati akieleza hayo, alikatishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akimtaka ajielekeze kwenye hoja tatu za taarifa za kamati huku mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi akisema bima walizonazo wabunge zinawawezesha kupata matibabu.

“Kama hawana mawasiliano mazuri na Bunge nawashauri na nawapa taarifa wawasiliane na ofisi ya Bunge,” alisema Nchambi.

Kauli ya Nchambi iliibua mvutano bungeni, huku mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche akisikika akisema kauli ya mbunge huyo wa Kishapu ni sawa na kucheza na uhai wa mtu.

Kufuatia hali hiyo, Chenge aliingilia kati na kuwatuliza wabunge hao kwa kuwataja kwa majina, akiwemo Heche na mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.

Mwenyekiti huyo alipomtaka Lema kuendelea na mchango wake, mbunge huyo aliendelea kuzungumzia matibabu ya Lissu na kubainisha kuwa suala hilo linahusu utawala bora, si vinginevyo kama inavyodaiwa na Nchambi.

“…, Huyu (Nchambi) anasimama anaongea mzaha kuna watu wamepotea mmoja anaitwa Ben Saanane (msaidizi wa mwenyekiti wa Chadema-Freeman Mbowe) haya ni mambo yanayohusu utawala bora na sheria,” alisema Lema.

Alisema kujadili matibabu ya Lissu na masuala ya utekaji hawana lengo la kushutumu, bali ni kutaka mambo yarejee katika mstari.

Licha ya Lema kuendelea kuchangia taarifa hizo za kamati huku akikatishwa mara kwa mara,  muda wake ulipomalizika alitakiwa na Chenge kuketi ili kumpisha mchangiaji mwingine.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 9, 2018

$
0
0
Fuatilia hapa yanayojiri Bungeni Dodoma moja kwa moja kutoka Dodoma muda huu katika Bunge la 11, Mkutano wa kumi leo Februari 9, 2018. 

==>Tazama hapo chini

PICHA: Lowassa alivyofika kwenye msiba wa Tambwe Hizza

$
0
0
Waziri mkuu Mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa jana jioni aliungana na baadhi ya viongozi wa chama hicho nyumbani kwa aliyekuwa Mwanachama wa chama hicho na Mwanasiasa mashuhuri Marehemu Richard Hizza Tambwe eneo la Mbagala kuwapa pole wafiwa kutokana na msiba wa mwanasiasa huyo uliotokea  jana.

Maamuzi ya mahakama katika kesi ya Diamond na Hamisa Mobeto

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond amesema mazungumzo katika kesi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto kati yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto,  imekwenda vizuri.

“Niseme tu mambo yameenda vizuri na kama mnavyojua mambo ya mahakamani ikitokea ninahitajika nitakuja,” amesema.

Diamond alifika mahakamani hapo jana Februari 8, 2018  kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul iliyofunguliwa na Mobeto.

Amesema yeye na Mobeto hawana shida yoyote, ila kuna watu waliokuwa wakizungumza maneno na kumchochea Mobeto.

"Tunahitaji kuweka mambo sawa. Tunahitaji kuwa katika mstari kwa sababu vitu vidogo vinaharibu upande wa mama na upande wa baba kwa hiyo tulikuwa tunaweka mambo sawa ili kesho na keshokutwa yasilete sintofahamu baina yetu,” amesema na Diamonda na kuongeza:

“Ikitokea kuna mtafaruku baina ya mtoto, kila mtu anakuwa na mawazo yake, kwa hiyo ni lazima kumjenga mtoto na kuhakikisha kuwa mtoto anajengwa na kulelewa  katika malezi bora.”

Alipoulizwa ni kiasi gani cha fedha anachoweza kumudu kutoa kwa ajili ya matunzo ya mtoto huyo, amesema kiasi cha fedha kinazungumzwa zaidi lakini mtoto anahitaji matunzo mengi.

"Kiasi cha pesa tunachoandika sehemu kama hizi tunazungumza tu. Mtoto ana mahitaji mengi wakati mwingine mtoto wako unaweza kumpa hata Sh100 milioni. Huwezi kusema siwezi kumpa kwa sababu niliandikisha nitampa Sh100,000. Tumeweka mazingira mazuri ya kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora,” amesema.

Msanii huyo amesema kupitia kesi hiyo amejifunza vitu vingi na kwamba,  mazungumzo yao ndani ya mahakama hiyo ni siri yao: “mambo yamekwisha.”

Amesema atahakikisha mtoto huyo anakuwa katika mazingira mazuri, kumsomesha kadri ya uwezo wake utakavyoruhusu kwa maelezo kuwa maisha ni kupanda na kushuka.

“Kuna wakati unakuwa hauna unasema leo mie sina basi mambo yanakuwa Bundasiliga leo mnakula mihogo maisha ndivyo yalivyo,” amesema.

Ugonjwa wa Aveva Wasababisha Kesi Kupigwa Kalenda

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, na makamu wake, Geofrey Nyange, ambao wanakabiliwa na shauri la utakatashaji wa fedha, kutokana na Aveva kuwa mgonjwa.

Kutokana na hali hiyo, Mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo ya kutakatisha Dola za Marekani 300,000 hadi Februari 22, mwaka huu.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, aliieleza mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa, wakati shauri hilo lilipofikishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai alieleza Aveva ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa kwa ajili ya kutibiwa ugonjwa wa figo.

Alidai wamepata taarifa mshtakiwa ameshatoka hospitali,lakini ameshindwa kufikishwa mahakamani kwa sababu afya yake haijawa ya kuridhisha.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 22, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15, 2016 wakionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva wakati si kweli.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa Machi 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe Ilala, Aveva akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.

Ilidaiwa katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kati ya Machi 15 na Juni 29,2016 jijini Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata Dola za Marekani 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.

Katika shtaka la nne, Aveva anadaiwa kati ya Machi 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola za Marekani 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Katika shtaka la tano, Nyange anadaiwa Machi 15,2016 katika benki ya Baclays tawi la Mikocheni alimsaidia Aveva kujipatia Dola za Marekani 300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi

Bashe awahenyesha mawaziri watano, wakutana kwa dharura

$
0
0
Mawaziri watano jana walilazimika kufanya kikao cha dharura bungeni baada ya uongozi wa Bunge kuagiza serikali itoe majibu kutokana na hoja ya Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe.

Mawaziri waliokutana kutokana na hoja hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati,Dk. Medard Kalemani na naibu mawaziri wa fedha, Dk. Ashatu Kijaji na wa maji, Jumaa Awesso.

Mbunge huyo aliwashtaki mawaziri kwenye chombo hicho cha kutunga sheria akieleza kuwa wamekuwa chanzo cha mateso na mahangaiko kwa wananchi wa Nzega.

Huku akitumia Kanuni ya 47 kuliomba Bunge liahirishe shughuli zake za jana na kujadili jambo la dharura, Bashe aliwataja hadharani Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Tamisemi, Selemani Jafo, ambao alidai wamesababisha wananchi wa jimbo lake kukosa maji kwa siku ya 13 mfululilo hadi kufikia jana.

Alisema huduma hiyo haiko jimboni kwake kwa kipindi hicho cha wiki mbili kutokana na mamlaka ya maji kukatiwa umeme kutokana na serikali kutolipa malimbikizo ya madeni kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Mbunge huyo alisema amekuwa akiwasiliana na serikali lakini hakuna kinachoendelea na wahusika wamekaa kimya ilhali wananchi wa jimbo lake hilo wanapata taabu.

“Ndugu zangu wabunge na hasa wabunge wa CCM, naombeni mniunge mkono katika jambo hili. Nzega ni siku ya 13 sasa hatuna maji, wanawake wanateseka bila maji na kunilazimu ninunue maji kwa ajili ya hospitali,” alisema Bashe aliyeonekana kuzungumza kwa hisia kali.

Alibainisha kuwa yuko tayari kwa jambo lolote kwa kuwa ni wananchi wake wanaoumizwa na serikali kwa kukatiwa maji katika kosa ambalo serikali ndiyo mhusika mkuu wa deni hilo.

Alisema wananchi wake wanapata mateso lakini serikali haijawahi kupeleka majibu ya aina yoyote kuhusu mateso hayo na bado inaonekana kutojali licha ya Bunge kutaka mawaziri wakutane naye kujadiliana.

"Waheshimiwa wabunge, naomba tusaidiane katika kumsaidia Rais wetu, hali ni mbaya. Wapendwa leo ni Nzega, lakini itakuwa kesho kwa mwingine, lolote litalotokea huko litakuwa juu ya mawaziri hao,” alisema Bashe na kutoa hoja.

Kutokana na hoja hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyekuwa anaongoza kikao cha jana, alisimama na kueleza ukubwa wa tatizo la maji kuwa ni la nchi nzima, hivyo halitakiwi kuupuzwa na akaomba kuwatendea haki wananchi katika maeneo yote.

Kwa uzito huo, Chenge alimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, kueleza hatua ambazo zimechukuliwa na serikali kutatua changamoto hiyo.

Waziri huyo aliagiza mawaziri wanaohusika na maji, nishati na fedha kukutana kwa dharura kwenye moja ya kumbi za Bunge mara moja pamoja na Bashe baada ya kuahirishwa kwa shughuli za chombo hicho jana mchana.

Kutokana na majibu hayo, wabunge wengi walisimama na kuomba miongozi huku Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), akieleza kuwa tatizo la maji kuwa ni kubwa na hata katika wilaya yake ambako watumishi walikula fedha za mradi wa maji lakini wakahamishwa na kuacha mradi ukiwa haujakamilika.

Nje ya Bunge, Bashe alisema kuwa kikao baina yake na mawaziri hao kilifanyika kwa nusu saa kwenye moja ya kumbi ndogo zilizoko ndani ya jengo la Ukumbi wa Bunge na akabainisha kuwa katika kikao hicho waliazimia serikali iji-commit' kulipa deni la umeme na mamlaka ya maji irudishiwe huduma ya umeme haraka.

Shahidi akana kuona mkojo wa Wema Sepetu

$
0
0
Kesi ya msanii  Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa jana February 8, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille aliieleza Mahakama kuwa hakuwepo wakati Wema akichukuliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali.

Shahidi huyo aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipoulizwa maswali na Wakili wa Wema, Alberto Msando.

Katika ushahidi wake, Inspekta Wille, alidai hakuwahi kupeleka sampuli za mkojo  za washtakiwa wenzake Wema ambao ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Shahidi  huyo alidai kuwa aliijaza fomu ya kupeleka sampuli ya mkojo wa Wema saa nne asubuhi akiwa ofisini kwake na kuandika maneno  mkojo uko ndani ya chupa ya plastiki.

==>Mahojiano kati ya wakili Msando na shahidi yalikuwa hivi:

Wakili: Katika hii fomu shahidi umejaza kuwa mkojo ulikuwa ndani ya chupa ya plastiki. Nataka kujua je uliuona huo mkojo kama ni wa Wema?

Shahidi:  Nilijaza fomu kutokana na uzoefu wangu wa miaka 15.

Wakili: Ulijaza fomu ya kisheria ya kupima sampuli kabla ya mshtakiwa kufika kwa Mkemia Mkuu wa Serikali?

Shahidi: Ndio uzoefu wangu.

Wakili: Mkojo uliokabidhi uliupata wapi?

Shahidi:Kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakili: Je ulikuwapo wakati mshtakiwa anachukuliwa sampuli ya mkojo?

Shahidi : Sikuwapo.

Wakili: Inawezekana ukasema hujui kilichokuwa ndani ya chupa ya plastiki kwa vile haukuwapo?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Wakati Mkemia Mkuu unamkabidhi mkojo  chupa ya plastiki ilikuwa imewekwa lakiri?

Shahidi: Ndiyo

Wakili: Je, ulikaa muda gani katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali?

Shahidi: Niliondoka baada ya kukabidhi fomu, ilikuwa kama saa 5:00 asubuhi.

Wakili: Ulihusika kwenda kukagua nyumbani kwa mshtakiwa wa kwanza?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Je, ulipekua chumba anacholala mshtakiwa wa kwanza?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Je, vitu mlivyokuta katika upekuzi wenu vilikutwa sehemu gani?

Shahidi: Katika upekuzi msokoto wa bangi na rizza ya kusokotea bangi ilikutwa jikoni juu ya kabati la vyombo na walikuta msokoto wa bangi uliotumika ukiwa ndani ya kiberiti dirishani katika chumba wanacholala wafanyakazi wake.

Wakili: Je, kwenye hicho chumba mlichokuta msokoto ni wa mshtakiwa wa pili au wa tatu?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Je, huo msokoto ni wa mshtakiwa wa kwanza?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Je mshtakiwa wa pili na watatu alipimwa sampuli ya mkojo?

Shahidi: Hapana.

 Mahakama iliipokea hati ya ukamataji mali iliyojazwa katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Wema Sepetu  kama kielelezo.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 26 na 27, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Tiba Asili ya Kuondoa Chunusi, Kupunguza Tumbo, Maziwa Makubwa na Nguvu za Kiume

$
0
0
Asilimia 90 ya wanaume hushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya  kama vile kisukari, punyeto ambayo huathiri mfumo mzima wa wa misuli inayozalisha vichocheo ashiki , kutopata choo vizuri hali ambayo huchakiwa na kula chakula kisicho na asili,tumbo kuunguruma, kujaa gesi,kiuno kuuma, mgongo na miguu kufa ganzi

SUPER HOLO; Ni dawa itokanayo na miti shamba, ipo katika mfumo wa vidonge na unga. Hutibu na kumaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa muda mfupi tu.,SUPER HOLO hurudisha heshima ya ndoa, itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-30. Itakupa hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3. Pia itaimarisha misuli iliyosinyaa na kulegea. Dawa hii hutumiwa kwa watu wa umrii wa miaka 20- 80

NZOGIWE ni dawaya maumbile.Hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo urefu wa nchi 4-8 na unene wa sentimita 2-4 za upenyo

NZOGOMA ni dawa asili ya miti shamba, huboresha mbegu za uzazi...huzibua mirija na kusafiisha ili kuweza kushika mimba au kutia mimba.

Pia tunayo dawa ya kupunguza tumbo, unene, maziwa makubwa, kuongeza hips, makalio na kutoa chunusi

TUNAPATIKANA MTONI MTONGANI. KANA HAUNA NAFASI YA KUFIKA UTALETEWA ULIPO. WASILIIANA NA DR. MBUSI.  PIGA SIMU NAMBA:   0718 431222

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Waziri Mkuu Atoa Maagizi Mazito Wizara ya Maliasili na Utalii

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii irudi kwenye maeneo yote yenye migogoro ya mipaka na iungane na Halmashauri za wilaya ili waweze kutoa majibu kwa wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Alhamisi, Februari 8, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Urambo, Bibi Margaret Sitta wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.

Bibi Sitta alitaka kujua Serikali imeweka taratibu na mikakati gani ya kumaliza migogoro ya mipaka inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya hifadhi za misitu nchini kwa kuwa wananchi wanahitaji maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo.

Waziri Mkuu amesema Serikali iliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iweke vigingi kwenye maeneo yote yanayozunguka hifadhi za misitu ili kuweka alama zitakazopunguza migogoro ya kuingiliana kati ya wananchi walioko kwenye vijiji na wahifadhi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu hiyo.

Amesema maagizo hayo yalitolewa baada ya kugundua kuwa kuna migogoro mingi kati ya wananchi walioko katika vijiji vya jirani na misitu iliyohifadhiwa kisheria ambayo ina ramani.

“Lakini tunatambua kwamba wanapoendelea na zoezi hilo la uwekaji alama, inaweza kutokea kijiji kikajikuta kipo ndani ya mipaka ya hifadhi na inaweza kusababisha kutoelewana kati ya wanakijiji na wenye mamlaka ya hifadhi.”

“Tuliwasihi wanakijiji wakati zoezi hili linaendelea na hata kama kijiji kitajikuta kimezungukwa na hizo alama, wanakijiji watulie ili kazi ya awali ikamilike na pale kwenye mgogoro, Serikali itarudi tena kuja kuangalia mgogoro huo na kufanya tathmini ya kina.”

Amesema Serikali iliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii inapofanya kazi hiyo ya kuweka vigingi lazima ishirikishe mamlaka za halmashauri na kijiji husika na wao washiriki katika zoezi hilo ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi izitumie ranchi za NARCO na kugawa katika vitalu ili kubaini ukubwa wa eneo iliyonayo ndipo iweze kufanya uamuzi wa kugawa vitalu hivyo kwa wafugaji.

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nkenge, Balozi Dkt. Diodorus Kamala aliyetaka kujua taarifa ya kamati iliyoundwa na Serikali kufuatilia migogoro ya ranchi zilizokuwa chini ya NARCO na wafugaji, itapelekwa lini bungeni ili iweze kujadiliwa.

Waziri Mkuu amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliunda tume ya kufuatilia maeneo yote ya ranchi za Taifa na kuyapima maeneo hayo lakini pia kujua ni akina nani wanayamiliki maeneo hayo, kubaini kama walipewa kihalali, na kama ni kweli wanamiliki mifugo yoyote kwenye maeneo tajwa.

Kuhusu kupelekwa bungeni kwa taarifa ya tume hiyo, Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Mifugo aikamilishe na kuiwasilisha Bungeni kama taratibu zinavyotaka ili kuwawezesha wabunge na wananchi wajue dira na mwelekeo wa Serikali wa namna ya kufuga mifugo hiyo kwa njia ambazo zitawaletea tija lakini kikubwa zaidi ni kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Serikali Yakataa Kuivunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)

$
0
0
Serikali imesema iko tayari kupokea ushauri wa namna bora yakuimarisha utendaji wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza Taasisi hiyo kwani bado inahitajika na madhumuni ya kuanzishwa kwake  yana  tija kwa Taifa.

Akizungumza wakati akijibu Hoja za Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma  na Maendeleo ya Jamii Waziri wa Elimu Sayansi na Teknplojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika hivyo Serikali inaangalia namna ya kuiboresha na si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

“ Taasisi ya Elimu ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wale waliokosa katika mfumo rasmi na pia kutoa mafunzo  endelevu hivyo bado kuna umuhimu wa kuendeleza Taasisi hii” Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Akifafanua  Prof. Ndalichako amesema kuwa Taasisi hiyo inaweza kuimarishwa zaidi ili  kuendana na mahitaji ya sasa  ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha na kukuza kiwango cha elimu nchini.

Akizungumzia mikakati yakuimarisha elimu nchini Profesa Ndalichako amesema kuwa kwa sasa Serikali inafanya ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini, vyuo vya Ualimu, na Ujenzi wa maktaba yakisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja hiyo ikiwa ni sehemu ya miradi yakuboresha elimu inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yalipendekeza kuwa TEWW ivunjwe ambapo Serikali imesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika na ina tija hivyo kitakachofanyika ni kuiboresha zaidi ili kukuza elimu hapa nchini na Si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

Taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 139 ya mwaka 1989 na iko chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

Habari Njema kutoka kwa Waziri Mwigulu kwa walionyang’anwa Pikipiki na Polisi

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dk Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatue haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi, walekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu

Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.

Aliyekuwa kamishna wa madini kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka

$
0
0
Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Bondo Samaje amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka.

Samaje amefikishwa katika mahakamani hiyo  jijini Dar es Salaam leo Februari 9, 2018.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa  kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, April 9, 2013  na Juni 21, 2013 Makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.

Amesema akiwa Kaimu Kamishna wa Madini, alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kuishauri Bodi ya Madini katika utoaji wa leseni ya madini ya Graphite na Marble kwa Kampuni ya Tanzaniteone Mining Limited na State Mining Corporation.

Katika shtaka la pili, April 16, 2013 makao Makuu ya Wizara ya Nishati iliyopo wilaya ya Ilala, akiwa Kaimu Kamishna wa Madini na Katibu wa Bodi ya Ushauri wa Madini kutoka wizarani, alitumia vibaya madaraka yake kwa kutoa maelekezo kwa msaidizi wake John Nayopa kuandaa leseni za madini ya Graphite and Marble, bila kufuata sheria ya madini.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili na mmojawapo kusaini bondi ya Sh 50milioni.

Pia mshtakiwa hatakiwi kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Mahakama.

Habari Njema kwa watumishi wote wanaoidai Serikali....Madeni Yote Yanalipwa Mwezi Huu

$
0
0
Serikali imetangaza neema kwa watumishi wake wote wanaoidai malimbikizo ya madeni kwa kueleza kuwa itaanza kuyalipa madeni hayo ndani ya mwezi huu wa Februri 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Fedha na Mipango ameeleza kuwa mwisho wa mwezi Februari 2018, serikali itawalipa kwa mkupuo mmoja watumishi wake wote malimbikizo ya madeni na madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi.

“Madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi Bilioni 16.25 kwa walimu 15,919, na Tsh. Bilioni 27.15 kwa watumishi 11,470 wasiokuwa walimu. Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya TZS Bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja,” amesema Waziri Mpango.

Ameongeza kuwa kwa malipo ya madai haya ambayo kwa baadhi ya watumishi yana muda wa zaidi ya miaka kumi, majina ya wadai yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho Jumamosi februari 10, 2018.

“Malipo ya madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka 10, majina ya walipwaji yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018,” amesema Waziri Mpango.

Waziri Mpango amesema madai haya yanajumuisha malimbikizo ya mishahara, nyongeza ya mishahara pamoja na tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu nafasi.

“Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara… Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi Bilioni 43.39 ikiwa ni 34% ya madai yote, yalihakikiwa na kuonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho” amesema.

Aidha amesema kutokana na zoezi la uhakiki lililofanyika, serikali imeweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na 66% ya madai yote zilizokuwa zilipwe kimakosa kutokana na uwepo wa watumishi wengi wenye vyeti feki.

“Zoezi la uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika, limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na 66% ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo… Kama tungekurupuka tu tukalipa, tungekuwa tumetumia vibaya fedha za watanzania shilingi bilioni 84.22,” amesema Waziri.

Vile vile amesema kuwa serikali itaendelea kulipa madeni yote ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuepukana na malimbikizo ambayo kwa namna moja au nyingine, yanaweza kuisababishia serikali hasara.

“Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza, ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili,” amesema.

Waziri Mkuu: Viwanja Zaidi Ya 15,000 Vimepimwa Dodoma, Kuanza kuuzwa Machi 30, mwaka huu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Manispaa ya Dodoma imekamilisha upimaji wa viwanja vipya zaidi ya 15,000 na vitaanza kugawiwa Machi, 30 mwaka huu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Februari 9, 2018) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 10 wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Aprili 3, mwaka huu.

“Kutokana na agizo la Serikali la kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma, mahitaji ya viwanja hadi Februari 2018 yalikuwa ni viwanja 24,602. Manispaa ya Dodoma hivi sasa inatekeleza mkakati wake wa kuzalisha viwanja 30,000 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Tayari upimaji wa viwanja vipya 15,316 umekamilika na vitaanza kugawiwa kuanzia tarehe 30 Machi 2018,” amesema Waziri Mkuu.

Amelieleza Bunge kwamba kiasi kilichobaki cha viwanja 14,684 kitakamilika ifikapo Juni, 2018 na wananchi watauziwa viwanja hivyo kwa bei elekezi itakayotolewa na Manispaa hiyo.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi na watumishi wa umma watakaohitaji viwanja kufuata taratibu za maombi ya viwanja pindi vitakapotangazwa rasmi na kusisitiza kuwa zoezi la kubadilisha hati zilizotolewa na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kupata hatimiliki za miaka 99 linaendelea. “Wenye hati za CDA mnasisitizwa kuendelea na taratibu za kuzibadilisha,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema jumla ya watumishi 3,829 kutoka wizara na taasisi mbalimbali za Serikali tayari wamehamia Dodoma akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

“Napenda kulifahamisha Bunge lako tukufu kuwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ofisi yake walihamia rasmi Dodoma tarehe 15 Desemba, 2017 kama ilivyopangwa,” amesema.

Kuhusu mpango wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kuifanya Dodoma iwe na ukanda wa kijani (Green Belt) kupitia mpango wa kuendeleza, kutunza na kuhifadhi maeneo ya msitu wa Mahomanyika wenye ukubwa wa hekta 2,000; msitu wa Chimwaga Nzuguni (hekta 300) na msitu wa Mbwenzelo (hekta 3,500) pamoja na vilima vya Image na Nyankali.

“Katika kutimiza malengo hayo ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, Serikali imeendelea kutoa elimu ya upandaji miti na uhifadhi wa misitu hususan miti adimu ya asili na makao ya wanyamapori mbalimbali katika kata nane za Ipala, Nzuguni, Kikombo, Ng’ong’ona, Chahwa, Zuzu, Hombolo na Kikuyu Kaskazini ambapo kila kata imepewa lengo la kupanda miti isiyopungua 40,000,” amesema.

Kuhusu zoezi la upandaji miti, Waziri Mkuu amesema miche 34,000 yenye thamani ya sh. milioni 34 ilitolewa bure katika kata mbalimbali na kupitia mradi wa TASAF miche mingine 138,000 inaendelea kusambazwa kwa wananchi. “Kwa sasa, Manispaa ya Dodoma inaendelea na maandalizi ya kuotesha miche mingine 200,000 kwa ajili ya msimu ujao,” ameongeza.

Ametumia fursa hiyo kuwashukuru Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Bonde la Wami Ruvu, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ambao kwa kushirikiana na Manispaa ya Dodoma wamefanikisha upandaji wa miche 79,000 katika maeneo ya UDOM, Mzakwe, Iseni Park, Nala na Mahomanyika.

Katika kuhakikisha zoezi la upandaji miti linakuwa endelevu, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini zihakikishe zinaandaa miche ya kutosha na kuweka utaratibu wa kila kaya kupanda na kutunza miti isiyopungua mitano.

“Taarifa za utendaji na maendeleo za Halmashauri zote zioneshe mafanikio yaliyopatikana kutokana na zoezi la upandaji miti. Utendaji wa Wakurugenzi na Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya, utapimwa kutokana na uendelezaji na utunzaji wa mazingira katika maeneo yao,” amesisitiza.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images