Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TLS Wammwagia Sifa Rais Magufuli

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amepongeza Rais  John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.

 Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama.

Pia, ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili, tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale inapostahili."

Ametoa wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani  na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa  kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Pia  kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu anapenda uadilifu na imeandikwa katika vitabu vitakatifu, kulinda na kuhifadhi misingi ya kitaaluma na kujifunza kwa kufuata makosa yaliyotokea hapo nyuma

Ngwilimi ametoa  wito akisema: " Kama sehemu ya watanzania, tusitumie mahakama vibaya, kusumbua wengine, kuonea wengine, kama sehemu ya majaribio, siyo maabara , kama jumba la kamari.

Mnyika Ampa Makavu Mtulia....."Msaliti huwa haachi usaliti"

$
0
0

Mbunge wa Kibamba kupitia Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amewatahadharisha wananchi wa jimbo la Kinondoni kwa kutomchagua mgombea wa CCM, Maulid Mtulia kwa madai ni msaliti na hawezi kuacha hiyo tabia.

Mnyika ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo wa kumpigia kampeni mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Salum Mwalimu kupitia tiketi ya CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA.

"Mtulia alianza usaliti tangu siku ya kwanza alipotangazwa kuwa Mbunge mwaka 2015, maana siku ile matokeo yalipokuwa yanatangazwa na tume, aliposikia jina lake tu kuwa ameshinda alikimbia na kuwaacha watu waliokuwa wakipigania atangazwe na hakutaka kusikia matokeo ya Urais", alisema Mnyika.

Pamoja na hayo, Mnyika aliendelea kwa kusema "msaliti huwa haachi usaliti, hivyo kama wananchi wakikosea na kumpa Mtulia ridhaa ya kuwa Mbunge basi atakuja kuwasaliti tena".

Kwa upande mwingine, mpaka sasa zimebakia takribani siku 16 ili wananchi wa jimbo la Kinondoni  na Siha kuweza kushiriki kupiga kura katika majimbo hayo ambayo yapo wazi kwa sasa.

Ijue Afya Yako: Pata Tiba Asili ya Busha, Maumbile Madogo na Nguvu za Kiume

$
0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaayhiri watu  wengi sana baada ya kujiona wako tofauti na watu wengine .Kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na maumbile  nchi-6-7 .Matatizo haya yanasababishwa na punyeto) kisukari) presha) naulevi wakupita kiasi pia na msogo wa mawazo, homoni za toka kuzaliwa 

MOMLA ni dawa inayotibu kinacho sababisha tatizo,kama vile sukari, presha, magonjwa ya zinaa, misuli kulegea na kusinyaa kwa kwasababu ya kujichuwa au punyeto na akili kudumaa kwaajili ya tendo bila kushiriki 

MBEPE nikwa wenye maumbile mafupi na membamba kwa matatizo hayo ni dozi ya siku 5 unapona kabisa 

DAGULA hii nikwaajili ya wenye busha iwe ya maji au ya utumbo kushuka inatibu bila opresheni , kuuga mifupa kwwaliopata ajari yoyote inayo sababisha uvujifu wa mifupa inatibu kwa mda wa siku 14 tayali kwa mazoizi 

LUKOMOLO ni dawa ya mvuto wa mpenzi biaashara ata kama mme mke mchumba atakutafuta mwenyewe na kutekeleza yote unayotaka mfanye akutafute mwenyewe pia tunatibu kiuno miguu aina yote tumbo la uzazi kwa kina mama na kina baba nk 

KWA WAKAZI WA DSM TUNAPATIKANA MBANGALA RANGI TATU MKABALA NA KISUMA BAA. 

KWAMIKOA YOTE MTAPATA HUDUMA HILI KWA MAWASILIANO PIGA 0767131395, 0712757594, 0787131395 MUONE DR MWANGARA

Chanzo cha Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume na Tiba Yake

$
0
0

Tendo la ndoa limengawanyika katika makundi matatu baadhi yake makudi hayo niuhanisi, kufanya tendo la ndoa maramoja na kushidwa kurudia tena 

sababu zinazo pelekea ni ugonjwa wa kisukari, kujichuwa, maumivu ya mgongo na kiuno, tumbo kuuguruma na kujaa gesi, msogo wa mawazo, presha, kutokuwa nyama sehemu ya haja kubwa yani mgoro, ulevu wa kupidukia, kuadhilika na madawa ya kulevya 

ARRBERA 1 Ni dawa ya asili ambayo imefanyiwa tafiti kwa hali ya juu isiyo na kemikali yoyote kwa mtumiaji ambayo humfanya mtumiaji kufanya tendo la ndoa maratatu bila kuchoka 

Pia ARRBERA 2 ni dawa asili abayo huimalisha ukuaji wa umbile la kiume lililo sinyaa na kunenepesha saizi upedayo. sihayo tu upade wa wamatatizo kisukari yakushuka na kupada kuna dawa ya kutumia siku saba na kufanya sukari ibaki nomo balasi abayo ni 4-5-6 vilevile kwaupade wa kina mama matatizo ya uzazi na hedhi kuvurugika na kutokwa maji maji sehemu za sili fagasi na kifafa cha mimba kwa kina mama waja wazito na kifafa cha kawaida 

FIKA OFISINI KWETU MBANGALA RAGI TATU ASIYE KUWA NA NAFASI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO KWA KWA KAZI WA DSM muone dr kabero simu 0758078280 au 0713 293 988 wote mnakalibishwa
No automatic alt text available.

Rais Magufuli: "Sitalalamika tena,najua nitakavyofanya"

$
0
0
Rais John Magufuli amewapa pole Majaji kwa changamoto wanazokumbana nazo pindi wanapo shughulikia mashitaka yanayopelekwa na serikali na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kabla ya mwezi Februari kuisha kwa madai ameshajifunza vya kutosha.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipohudhuria kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo yeye binafsi ndio alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo akiongozana na viongozi wengine wa serikali.

"Kwa kuadhimisha siku hii ya sheria maana yake ni kwamba nchi yetu inatambua umuhimu wa sheria katika kusimamia haki, kudumisha amani na kuleta maendeleo ya nchi. Maadhimisho haya ya siku ya sheria ni muhimu kwa vile yanatoa fursa kwa vyombo vinavyohusika na masuala ya sheria na utoaji haki", alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mkuu), na ndio maana muda mwingine inawapelekea kuwapa changamoto kubwa Majaji.

"Najua mnapata shida sana mnapo-dili na mashitaka yanayoletwa na serikali mnauona kabisa ushahidi upo lakini watetezi hawajitokezi hadharani kuutetea. Mwaka jana nililalamika lakini mwaka huu nitalishughulikia vizuri. Sitalalamika tena ninajua nitakavyofanya kwa sababu nimeshajifunza vya kutosha na nimejua wapi kuna 'weakness' na wala huu mwezi wa Februari hautoisha", alisisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewataka viongozi wengine wanaosimamia vyombo vya sheria kufuata mfano mzuri aliyouanzisha Profesa Ibrahimu Juma kwa kutowafumbia macho wahalifu wa aina yeyote ile.

Hii hapa orodha ya mikoa iliyoongoza kwa kiwango cha ufaulu kidato cha nne 2017

Kampuni ya simu TTCL yabadilishwa Rasmi

$
0
0
Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo Februari 1, 2018 imefanya mabadiliko na kuibadili kampuni ya simu ya TTCL kuwa shirika la Umma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametangaza maamuz hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa mabadiliko hayo hayawezi kuathiri wateja wa TTCL

"Sasa tunatoka kwenye TTCL kampuni na kuwa shirika la Umma tunaamini saizi mtajipanga zaidi kwenye mambo ya usalama na uimarishaji mambo ya uchumi. Pia napenda kuwajulisha Watanzania kuwa mabadiliko haya hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa na kampuni ya simu ya TTCL, huduma zote zilizokuwa zikitolewa kuanzia kwenye simu za mkononi, data, enternet, TTCL Pesa zote zitaendelea sasa kwa kiwango kikubwa zaidi" alisema Mbarawa

Mbali na hilo Mbarawa amewataka TTCL sasa kufanya jitihada za kwenda kukusanya madeni yake kwa wananchi mbalimbali ambao wanatumia huduma zao na kusema kuwa Serikali inatambua ina deni kwa TTCL na kuwa wao watalipa na wako tayari kulipa ila wanapaswa kuanza kwenda kudai fedha zao kwa wananchi mbalimbali na makampuni ambayo pia yanadaiwa na TTCL.

Magufuli ambadilikia Waziri na Mwanasheria Mkuu

$
0
0
Rais  Dkt. Magufuli leo Februari 1, 2018 amewabadilikia Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi mambo ya msingi.

Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria na kusema yeye ameubwa kusema ukweli hivyo ataendelea kuusema hata kama kuna watu unawaumiza

"Kinachoshangaza pamoja na hatua nzuri ya Serikali kupeleka 'Legal Aid Act' ya mwaka 2017 na mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini 'regulation' mpaka saizi hazijaletwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria, tena ni Profesa, AG yupo, Deputy AG yupo 

"Jamani mtanisamehe sana mimi ndivyo nilivyo nawasema hapa hapa, kwa hiyo wewe Profesa Juma na majaji na mahakimu hamna 'Instrument' za kuweza kutoa uamuzi. Wabunge wao wamepitisha sheria, mimi nikaletewa nikasaini lakini regulations mpaka leo miezi tisa imepita.

"Watu wapo wanakula tu mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi wanapata shida na muda mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi haki kumbe ni Serikali watendaji wake hawatoi haki kwa Watanzania.

" Ndiyo maana nawaambia changamoto zingine zipo ndani ya Serikali lazima na mimi nijitathimini ninachaguaagaje hawa watu ambao wanachelewesha chelewesha, hiyo ndiyo tathimini ambayo ninaanza kujifanyia kuanzia leo" alisema Rais Magufuli

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FULL POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Idara ya uhamiaji yakanusha taarifa zilizosambazwa kuihusu

Chadema Walimwa Barua.....wadaiwa kukiuka maadili ya uchaguzi Kinondoni

$
0
0
Wakati kampeni za uchaguzi jimbo la Kinondoni zikiendelea, Chadema wamepewa barua mbili za malalamiko na  msimamizi  wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli kikidaiwa kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.

Akizungumza leo Februari 1, 2018 Mkurugenzi  wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema wamepokea barua hiyo jana, yenye malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF).

Katika barua hiyo, CUF inalalamika kuwa Januari 28, Chadema walifanya kampeni nyumba kwa nyumba  katika eneo la Kigogo Mbuyuni hadi London Bar badala ya siku hiyo kuwa kata ya Ndugumbi kama ratiba inavyoonyesha.

Malalamiko mengine ni Chadema kudaiwa kutumia salama ya CUF katika majukwaa ya kampeni sambamba na kupamba bendera za chama hicho.

"Madai mengine ni kwamba viongozi  wa CUF  wanakuja katika mikutano yetu  na kukaa meza kuu na kupanda katika majukwaa. Pia CUF wanadai Chadema inawatumia viongozi  wao kupita nyumba kwa nyumba kuiombea kura Chadema  wakiwa na sare za CUF,” amesema Kigaila.

Kwa mujibu wa barua hizo Chadema wanatakiwa kutoa maelezo ya utetezi kwa maandishi  kuhusu tuhuma hizo ndani ya saa 48 baada ya kuzipokea.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya February 2

Breaking: Rais Magufuli Amtumbua Mwanasheria Mkuu wa Serikali

$
0
0
Rais Magufuli amefanya uteuzi mpya kwa kumteua Dk Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli pia amewateua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, kuanzia leo.

Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St.Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority- PURA).

Taarifa ya Ikulu imeeleza pia kuwa, Naibu Mwanasheria Mkuu Paul Ngwembe kabla ya uteuzi, alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA).

Wateule wote wanatarajiwa kuapishwa Jumamosi asubuhi tarehe 3 Februari 2018.

Awali katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli katika hotuba yake, aliwanyooshea vidole Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi, na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Naibu wake Gerson Mdemu wameshindwa kuandaa kanuni za msaada wa kisheria.

Rais Magufuli alitoa mwezi mmoja kwa viongozi hao, kukamilisha kanuni za msaada wa kisheria, huku akiongeza kuwa  usimamizi wa sheria na utoaji wa haki, bado una changamoto, kwani wapo wachache, uadilifu wao na matendo yao yanachafua vyombo nyeti.

Breaking News: Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia

$
0
0
Habari tulizozipokea hivi punde zinasema kuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.

 
Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali  zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali

Rais Magufuli Amjulia Hali Mzee Majuto Hospitalini, Afunguka Alivyomtabiria Makubwa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa.

Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.

“Mimi ndiyo mtu wa kwanza kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli. Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu bwana, tumepata Rais sio masihara watu wote sasa hivi wana adabu zao wanajua nini maana ya kazi”, alisema Majuto.

Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ;“sisi wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye msimamo”.

Kwa upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt. John Magufuli.

Nape Nnauye aipa changamoto Serikali

$
0
0
Mbunge Nape Nnauye leo Bungeni ameipa changamoto Serikali juu ya gharama za kuunganisha umeme na kuishauri kuendelea kuchaji elfu 27,000 hata baada ya mradi wa REA kupita ambapo wataanza kuchaji 177,000 kuunganisha umeme.

Nape Nnauye ametoa ushauri huo alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwenda kwenye Wizara ya Nishati

"Kwanza niipongeze Serikali chini ya Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri wanayofanya ya usambazaji mzuri wa umeme vijijini hasa REA awamu ya 3, kwa kuwa gharama za kuunganisha umeme wakati mradi unaendelea ni elfu 27,000 na mradi ukipita ni 177,000 na kwa kuwa idadi kubwa na nzuri ya watumiaji wa umeme ni biashara nzuri kwa TANESCO kwanini bei hii isiwe moja ya elfu 27" alisema Nape Nnauye

Hata hivyo Nape Nnauye aliendelea kusisitiza kuwa kama jambo hilo halitawezekana basi REA waendelee na uwekaji wa nguzo na miundombinu na TANESCO wafanye kazi moja ya kupeleka umeme na kukusanya kodi baada ya kupeleka umeme.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati alijibu hoja hiyo na kudai kuwa amepokea ushauri huo wa Mbunge wa Mtama na kuwa atapeleka katika ngazi zingine na kuona Serikali nini itafanya

"Wazo alilosema Kaka yangu Nape Nnauye linapokelewa na litafanyiwa kazi kwani ni la msingi kwa sababu Wizara yetu na shirika letu la TANESCO na wadau wengine wa nishati tunauza bidhaa hii hivyo ni vema tunapouza tupate wateja wengi ili tupate mapato na kuendesha shughuli mbalimbali na uwekezaji mpya wa maeneoya nishati"

TAMISEMI yaagiza Shule ya Sekondari Njombe kuchunguzwa baada ya wanafunzi wote kupata 0

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi, Joseph Kakunda ameagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Njombe kufanya uchunguzi wa matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viziwi Njombe.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana Jumanne Januari 30,2018 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), shule hiyo katika matokeo ya mtihani uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana watahiniwa wote 21 wamepata daraja sifuri (0).

Naibu Waziri Kakunda ametoa agizo la kufanyika uchunguzi leo Jumatano Januari 31,2018 bungeni alipojibu swali la mbunge wa Buyungu (Chadema), Samson Bilago.

Bilago alitaka kujua ni kwa nini shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu zinafanya vibaya kwenye mitihani.

Akizungumzia hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema walimu waliosoma elimu maalumu watapata ajira bila kikwazo cha kusubiri.

Mkuchika amesema wanasubiri kupelekewa orodha ya walimu hao.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini aliyetoa mfano wa shule ya Viziwi Njombe ya wanafunzi wa mahitaji maalumu iliyofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne akisema ni kutokana na kukosa walimu hao.

Mbunge aliyesimamia kiapo cha Raila Odinga Akamatwa

$
0
0
Mbunge wa Ruaraka Tom J Kajwang’, ambaye alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park Jumanne amekamatwa.

Mbunge huyo amekamatwa leo Jumatano mchana na maofisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi.

Alikamatwa muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho.

Kajwang’ na mwanasheria mwingine Miguna Miguna, ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa matukio ya kwenye viwanja vya Uhuru Park yaliyomalizikia kwa “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa watu’.

Wakati wa sherehe za kiapo Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi na alishangiliwa sana na wafuasi wa Nasa.

Odinga alikula “kiapo” huku Kajwang’ akiwa amesimama nyuma yake japokuwa wajibu wake katika tukio hilo bado haujafahamika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 1

Waziri Mpina Akamata Meli Ya Malaysia , Aipa Siku Saba Kulipa Faini Milioni 770/-

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekamata meli ya uvuvi mali ya Kampuni ya Buah Naga 1 ya nchini Malaysia na kuitoza faini ya Dola za kimarekani 350,000 sawa na Sh.milioni 770 kwa kosa la kukutwa na mapezi ya samaki aina ya papa yenye uzito wa kilo 90 bila miili yake.

Ambapo hiyo ni kinyume cha Kanuni ya 66 ya kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.

Meli hiyo ilikamatwa Januari 26 mwaka huu baada ya kufanyika ukaguzi uliosimamiwa na kikosi maalum cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao yake wakati ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara.Pamoja na kukutwa na mapezi hayo ya papa, meli hiyo ilikutwa pia na bastola aina ya Bereta ikiwa na risasi 10 bila ya kuwa na nyaraka za umiliki wake.

Akizungumza mjini Mtwara ambako meli hiyo ndiko inakoshikiliwa na Serikali Waziri Mpina ameagiza fedha hizo zilipwe ndani ya siku saba huku akitoa onyo kali kwa wamiliki wa meli waliopewa leseni za uvuvi wa Bahari kuu kufuata masharti ya vibali vyao na katika zama hizi za utawala wa Rais, Dk.John Magufuli watachukuliwa hatua kali zaidi.

"Enzi za Serikali ya Awamu Tano ya Rais Magufuli mtakaguliwa na kupekuliwa kuliko wakati wowote, hivyo ni vizuri mkatii sheria za nchi kwa mujibu wa leseni zenu,"amesema Mpina huku akisilizwa na Kapteni wa meli hiyo Han Ming Chuan  raia wa Taiwan.

Mpina amesema meli hizo zimekuwa zikitumika pia kufadhili biashara nyingine haramu ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya ,usafirishaji haramu wa  binadamu na biashara ya silaha.Pia zinatumika kutorosha nyara za Serikali ikiwemo meno ya tembo, samaki na madini.

Aidha Waziri Mpina amesema kitendo cha wamiliki wa meli hiyo kuwakata samaki hao mapezi na kisha kutupa miili yao baharini kimeleta athari kubwa kwa Taifa kwani samaki hao wangeweza kutumika kwa matumizi mengine ya binadamu na kuchochea uchumi wa nchi.

Hivyo, ameridhia faini hiyo iliyotozwa na Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Sh.milioni 770 na kuagiza kilo 90 za mapezi ya samaki na samaki wasioruhusiwa wataifishwe na kugawiwa kwa wananchi wa maeneo jirani ya Manispaa ya Mtwara. "Siku nyingine Serikali ikikamata meli iliyofanya makosa ya aina hiyo itataifishwa pamoja na vitu vyote vitakavyokuwemo kwa mujibu wa Sheria za nchi,"amesisitiza.

Waziri Mpina ameagiza wenye meli hizo kuzingatia masharti ya leseni zao zinazotaka kuwepo na asilimia 10 ya mabaharia wa kitanzania ndani ya meli zinazoingia kuvua katika Bahari kuu upande wa Tanzania.

Kwa upande wa Kamishna wa Oparesheni wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya, Luteni Kanali Fredrick Milanzi amesema meli hiyo baada ya kukaguliwa imekutwa na mapezi kilo 90 ya samaki aina ya papa na bastola yenye risasi 10 ambayo inaendelea kushikiliwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mtwara hadi hati za umiliki zitakapowasilishwa.

Pia mwenye meli atatakiwa kuhakikisha anawasafirisha mabaharia kurudi nchi zao kwa madai hawataki kuendelea kufanya kazi kutokana na kukiukwa kwa mikataba yao ya kazi.Aidha samaki wasioruhusiwa kuvuliwa kwa mujibu wa leseni ya uvuvi iliyopewa meli hiyo ( Bychatch) watabaki kuwa ni wa Tanzania na watauzwa kwa mnada na fedha zitakazopatikana kiasi cha sh milioni 12 zitaingizwa kwenye Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu, Hosea Mbilinyi amesema hatua zinachukuliwa kwa sasa zimelenga kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi na kwamba operesheni hizo ni endelevu na hazitambakiza mtu hata mmoja.

Wakati huohuo, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Divisheni ya Mashtaka Makao Makuu Dar es Salaam, Wankyo Simon amesema makosa hayo adhabu yake ni kubwa na wanapaswa kuzingatia muda uliotolewa na Waziri wa kulipa faini.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images