Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

RC Makonda Atokwa Na Chozi, Ni Baada Ya Kujionea Maisha Ya Wastaafu Waliodhulumiwa Nyumba

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana  ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.

RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote. 
 
Story ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyohuzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu  anamdhulumu Mali yake.
 
Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Bank, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.
 
Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha. 
 
Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.
 
Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanyonge.

Baada ya Rais Magufuli, Rais Shein atoa msimamo wake kuhusu muda wa kukaa madarakani

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amesema hayupo tayari kuongeza muda wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya Zanzibar.

Dkt Shein amesisitiza kwamba, aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar hivyo hawezi kubadilisha muda wa uongozi na hakuna mtu atakayemfanya abadilishe au amvutie yeye kuendelea kukaa madarakani.

Rais Dkt Shein ameyasema hayo jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baaada ya kurejea kutoka kwenye ziara ya wiki moja katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) alipokua ameambatana na mke wake, Mama Mwanamwema Shein.

“Mimi naheshimu katiba ya Zanzibar, na nina heshimu sheria za Zanzibar. Muda wangu ukifika nitaondoka haraka sana. Hakuna atakayenilazimisha mimi nikae, au atakayenivutia mimi nikae” alisema Rais Dkt Shein.

Aidha, Dkt Shein amesema kuwa, alisikia wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi wakizungumza hilo, lakini hawazuiwi kujadili kwani wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, lakini yeye hayuko tayari kuongeza muda.

“Hilo walizungumza wawakilishi barazani, wana haki ya kuzungumza, kwa mujibu wa taratibu zao na sheria zao na yeyote mwingine anaweza kuzungumza. Mimi nilisikia wakati wananzungumza, Mwakilishi mmoja akasema kwamba kuna baadhi ya nchi duniani zina miaka mitano nyingine saba, sasa kwanini na sisi tusiwe na miaka saba!”

Rais Dkt Shein amesema kuwa, suala la miaka saba labda linaweza kuwepo baada ya yeye kutoka lakini hadhani kama kuna jambo kama hilo.

“Mie sijalisema, sitolisema, na hakuna atayanilazimisha niliseme” alihitimisha Rais Dkt Shein, huku akitilia mkazo kwamba, muda wake ukiisha atamchukua mkewe na kumwambia waondoke.

Waziri Lukuvi Atangaza Kiama

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kutoa muda hadi April 30 mwaka huu kuhakikisha wanalipa kodi hiyo.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo kwenye ziara mkoani Mwanza alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya jiji la Mwanza na kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo la ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi linakamilika kwa wakati.

Amewataka wakuu wa idara za ardhi nchini kusajili hati za viwanja kwa wanaohitaji ardhi kwa kutumia majina yanayotambulika kwenye vitambulisho vya taifa NIDA ili kuepuka udanganyifu ambapo kodi hiyo ipo kisheria.

Waziri Lukuvi pia amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanapima maeneo yote yakiwemo mamlaka za viwanja vya ndege, hifadhi za wanyama na misitu taasisi zinazomiliki ardhi na wizara zote kupimwa.

Chanzo cha Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume na Tiba Yake

$
0
0

Tendo la ndoa limengawanyika katika makundi matatu baadhi yake makudi hayo niuhanisi, kufanya tendo la ndoa maramoja na kushidwa kurudia tena 

sababu zinazo pelekea ni ugonjwa wa kisukari, kujichuwa, maumivu ya mgongo na kiuno, tumbo kuuguruma na kujaa gesi, msogo wa mawazo, presha, kutokuwa nyama sehemu ya haja kubwa yani mgoro, ulevu wa kupidukia, kuadhilika na madawa ya kulevya 

ARRBERA 1 Ni dawa ya asili ambayo imefanyiwa tafiti kwa hali ya juu isiyo na kemikali yoyote kwa mtumiaji ambayo humfanya mtumiaji kufanya tendo la ndoa maratatu bila kuchoka 

Pia ARRBERA 2 ni dawa asili abayo huimalisha ukuaji wa umbile la kiume lililo sinyaa na kunenepesha saizi upedayo. sihayo tu upade wa wamatatizo kisukari yakushuka na kupada kuna dawa ya kutumia siku saba na kufanya sukari ibaki nomo balasi abayo ni 4-5-6 vilevile kwaupade wa kina mama matatizo ya uzazi na hedhi kuvurugika na kutokwa maji maji sehemu za sili fagasi na kifafa cha mimba kwa kina mama waja wazito na kifafa cha kawaida 

FIKA OFISINI KWETU MBANGALA RAGI TATU ASIYE KUWA NA NAFASI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO KWA KWA KAZI WA DSM muone dr kabero simu 0758078280 au 0713 293 988 wote mnakalibishwa
No automatic alt text available.

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Dawa Bora Ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE YA UMME MDOGO "Arrabela" FIKA NJOMBE MJINI, TUPO MTAA WA MPECHI KWA TABIBU MABULA HERBAL CLINIC.                                                    

 75%Ya Wanaume hukabiliwa na upungufu wa Nguvu za Kiume kwa sababu mbalimbali za matatizo ya Kiafya na Kibailojia hasa MTU ambaye anakuwa na Matatizo ya Ugonjwa wa KISUKARI, Zinaa, maumivu ya mgongo na kiuno, Tumbo kajaa gesi na kuunguruma, mshipa wa ngiri, Bawasiri au Mgoro, Au ugonjwa wowote unaochukua muda mrefu bila kupona hufanya kupungua kwa hormones za kichocheo kwa tendo la ndoa. 

Pia Matumizi ya dawa za kulevya ,Pombe,na utafunaji wa milungi.lakini wakati mwingine hutokana na sababu za Kimfumo wa kimwili na kuasilika kisaikolojia kwa kuwa na msongo wa Mawazo.

Lishe duni,upungufu wa protini mwilini na Madini.Kwa Huduma Bora za Matibabu ya KISUKARI, Nguvu za Kiume, maumbile ya umme MDOGO ,Matatizo ya kimaisha,muwasho sehemu za siri, Uzazi, Vidonda vya Tumbo,kikohozi kigumu,Magonjwa nyemelezi, mahusianona Tambazi

 FIKA KWENYE KITUO CHETU CHA TABIBU MABULA HERBAL CLINIC NJOMBE MJINI MTAA WA MPECHI

 KWA WALIOPO NJE NA MKOA WA NJOMBE HUDUMA YA DAWA ITAWAFIKIA KWA KUTUMIWA KWA MABASI ,SIMU 0768351097/0767488895 NYOTE MNAKARIBISHWA

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda Vya Tumbo, Busha, Nguvu Za Kiume, Kisukari

$
0
0

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni 3Power,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

FINA Power Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR SHEIKH OMARY
Anapatikana dar magomeni moroco hotel
SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

Rais Dkt. Magufuli Asali Ibada Ya Jumapili Katika Kanisa Katoliki La Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa kusali pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  mara baada ya wote kwa pamoja kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli. Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika  katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta akihubiri katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka Kanisani pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli mara baada ya Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Nakala za CD ya kwaya kutoka Chuo cha Ardhi mara baada ya Ibada. Kushoto ni Mke wake Mama Janeth Magufuli akifurahia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda mara baada ya kupewa na moja ya Waumini wa Kanisa hilo mara baada ya Ibada ya jumapili.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Nchini Ethiopia,kumwakilisha Rais Magufuli Katika Kongamano La Viongozi Wakuu Wa Umoja Wa Nchi Za Afrika

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, kwenye ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke Ethiopia, katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, Waziri Mkuu, anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, wakati alipo wasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Addis Ababa, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU Nchini Ethiopia. Januari 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisainiwa kitabu cha kumbukumbu, cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Kiongozi huyo, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Mahakama ya Rufaa Yawakana CHADEMA

$
0
0
Mahakama ya Rufaa imesema hakuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido iliyopo mahakamani hapo.

Mahakama imetoa kauli hiyo wakati Chadema ikiilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo kwa madai kwamba kuna kesi mahakamani hapo.

Uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema, Onesmo ole Nangole ushindi wake kutenguliwa na Mahakama Kuu.

Mara kadhaa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Ole Nangole wamekaririwa na vyombo vya habari wakidai kwamba kuna rufaa katika Mahakama ya Rufani.

Viongozi hao wamekuwa wakiilalamikia NEC kuwa iliendesha uchaguzi mdogo katika jimbo hilo wakati rufaa ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomvua ubunge Ole Nangole ikiwa haijatolewa uamuzi.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa imesema uchaguzi mdogo uliofanyika Longido ulikuwa halali kwa kuwa hakuna rufaa yoyote iliyoko mahakamani hapo.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Elizabeth Mkwizu amesema hakuna rufaa yoyote kupinga hukumu ya uchaguzi wa Longido iliyoko mahakamani hapo, bali kuna maombi.

“Hapa hatuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido, bali kuna maombi ya kuongezwa muda wa kuwasilisha ‘notice of appeal’ (taarifa ya kusudio la kukata rufaa). Walileta notice of appeal lakini ikatupiliwa mbali, sasa wanaomba muda ili waiwasilishe tena,” alisema na kuongeza:

“Maombi si rufaa, kwa hiyo haya maombi yasingeweza kusimamisha shughuli za uchaguzi.”

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Mahakama ya Rufaa, maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na Jaji Jacob Mwambegele Februari 5.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, mwombaji kupitia kwa mawakili wake atalazimika kutoa sababu za kuiridhisha Mahakama ni kwa nini alichelewa kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Ikiwa Mahakama haitaridhika na sababu zake, itatupilia mbali maombi hayo lakini ikiridhika nazo itamruhusu kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, atasubiri kupata kumbukumbu za rufaa, yaani nyaraka zitakazohusika kwenye rufaa yake, ikiwamo hukumu anayoilalamikia, mwenendo wa kesi ya msingi na vielelezo vilivyotumika.

Akipata nyaraka hizo, ndipo atakapowasilisha rufaa kamili, yaani sababu za kwa nini anapinga hukumu iliyomvua ubunge wa jimbo hilo, na upande wa pili (wajibu rufaa) nao utawasilisha hoja zake na baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote ndipo itatoa hukumu.

Ole Nangole alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Juni 29, 2016 kutokana na kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Dk Steven Kiruswa akipinga ushindi wake.

Baada ya Mahakama kumvua ubunge, Ole Nangole kupitia mawakili John Materu na Dancan Oola aliwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa ilitupiliwa mbali na Mahakama kutokana na kasoro za kisheria.

Baada ya kutupiliwa mbali, kwa kuwa muda wa kisheria wa siku 14 za kuwasilisha kusudio la kukata rufaa ulikuwa umeshaisha, waliwasilisha maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha taarifa hiyo.

Maombi hayo pia yalitupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ndipo wakapeleka maombi Mahakama ya Rufani.

ACT- Wazalendo Kuzunguka Mikoa 6

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Dorothy Semu, anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara akiambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Ziara hiyo ya siku nane itaanza tarehe 30 Januari 2018 hadi Februari 6, 2018 kwenye mikoa ya Kahama ambao ni Mkoa Maalum wa Kichama, Kigoma, Katavi, Shinyanga, Tabora na Kigoma.

Aidha taarifa ya Chama hicho imebainisha kuwa katibu ataambatana na Ndg. Wilson Mshumbusi ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee Taifa, Ndg. Janeth Rithe ambaye ni Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa pamoja na Katibu wa Sera na Utafiti Ndg. Idrisa Kweweta.

Moja ya majukumu ambayo Dorothy Semu atayafanya ni kukagua uhai wa Chama, kutoa maelekezo ya ujenzi wa chama, kusikiliza Kero na changamoto za wanachama na kuzipatia ufumbuzi.

Mbali na hayo Katibu Mkuu huyo pia atakagua maendeleo ya zoezi la uchaguzi wa ndani ya chama. Ziara hiyo pia imeelezwa kuwa itawalenga wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo wa maeneo hayo.

January Makamba: Taasisi za umma tumieni gesi kupikia

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba ameziagiza taasisi za umma, kuacha kutumia mkaa kupikia vyakula badala yake zitumie gesi ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.

Waziri January alitoa kauli hiyo jana kwenye shughuli za upandaji miti zilizofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma alikokwenda kumwakilisha Makamu wa Rais.

Alisema wakati wowote kuanzia sasa ataandika waraka katika taasisi zote kubwa ikiwamo majeshi na vyuo vikuu vyote kwa kuwa mamlaka hiyo anayo kisheria.

“Wengine mtajiuliza nachukua wapi mamlaka hiyo kutoka wapi, natumia sheria ya mazingira kifungu cha 13 ambacho kinanipa mamlaka hayo kwa taasisi yoyote nitakayoona inaharibu mazingira.

“Sheria inanipa nguvu hata kama kuna sheria nyingine hapa inayotoa tafsiri nyingine, inasema sheria hii itakuwa juu yake,” alisema January.

Awali, Naibu Waziri wizara hiyo, Kangi Lugola alisema Serikali haitamsamehe mwekezaji yeyote wa viwanda atakayeharibu, kutiririsha maji au kemikali kwa kisingizio cha uwekezaji wa viwanda.

Lugola alisema kumekuwa na kelele nyingi na visingizio vya Serikali ya viwanda kwa kuanzisha viwanda bila ya kufuata sheria ya mazingira.

Alisema mwekezaji yeyote atakayevunja sheria hiyo hakutakuwa na msamaha badala watamlinda mtu atakayefuata sheria ya viwanda na mazingira.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa alizitaka halmashauri zote kutunga sheria kali kwa ajili ya kulinda hifadhi ya mazingira ikiwamo miti inayopandwa.

Mwigulu Nchemba Awachana Wapinzani Wakati Akimnadi Mgombea wa CCM

$
0
0
MBUNGE wa Iramba Magharibi, Singida na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameongoza jahazi la makada, wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uzinduzi wa kampenzi za uchaguzi mdogo wa ubunge kwa Jimbo la Kinondoni.

Katika uzinduzi huo ambao umefanyika katika Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, CCM wamemnadi Maulid Mtulia na kuwaomba wananchi wa Kinondoni wampe kura za kutosha ili aweze kuwawakilisha vilivyo bungeni ikiwa ni pamoja na kutatua kero zao, kushirikiana na serikali bega kwa bega katika kuleta miondombinu ya maendeleo kwa jimbo hilo.

Mwigulu nchemba akizindua kampei za CCM katika Viwanja vya Biafra Kiondoni, Dar.

“Msije mkaenda kupiga kura ya uchaguzi mdogo kwa kiwango kidogo, mkapige kura kwa kiwango cha uchaguzi mkuu, kila mmoja akawe kampeni meneja wa mgombea wetu, aje na wapiga kura siku ya kupiga kura Februari 17, na hiyo ndiyo faida ya mtandao wa chama chetu .

“Sababu zote za msingi za ushindi tunazo sisi, wao wamebaki na hoja moja tu kwamba Mtulia amehama kwa nini? Ilani ya uchaguzi iliyochaguliwa ni ya CCM na itatekelezwa hadi mwaka 2020, asitokee mtu ambaye atawadanganya, kumpigia kura mtu wakati hana ilani inayotekelezeka ni sawa na kupigia kivuli wakati kuna mtu,” alisema Mwgulu wakati akiwasihi wananchi kumpigia kura Mtulia.

Aidha katika mkutano huo, wanachama wengi wa upinzani wamerudisha kadi na kujiunga na CCM.

Wassira: CHADEMA Ndo Shetani Wetu

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika serikali ya awamu ya nne na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM, Stephen Wasira amedai hawawezi kufanya siasa bila ya kukitaja chama cha CHADEMA kwa kuwa ndio shetani wao

Wasira amebainisha hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba baada ya kusikia kauli ya mgombea Ubunge wa Jimbo hilo katika 'televison' kuwa CCM hawawezi kufanya siasa bila ya kuitaja CHADEMA.

"Nimemshangaa kiukweli mgombea huyo, maana hata Maimamu na Wachungaji huwa hawawezi kumaliza ibada bila ya kumtaja shetani maana shetani ndio mpinzani wao na endapo wasipotaja wana kuwa hawajamaliza ibada yao. Hivyo asishangae sana na sisi tunapokuwa katika siasa kuitaja CHADEMA kwa maana ndio shetani wetu hapa", alisema Stephen Wasira.

Kwa upande mwingine, Wasira amesema tokea mwaka 2015 kumekuwa na siasa za kishetani nchini Tanzania hasa upande wa upinzani ambazo zimetawaliwa na uongo unaofanana na giza kwa kusema uongo katika kampeni zao na kudanganya wananchi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya January 29

Rais Magufuli alivyotoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Robert Kisanga

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 28 Januari, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga (pichani) nyumbani kwa marehemu Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 

Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu. 
 
Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam jana Jumapili Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam jana Jumapili Januari 28, 2018.

Tanzania yaibuka kinara Afrika uchumi jumuishi....Watalaamu Waitabiria Makubwa Zaidi

$
0
0
Baada ya Tanzania kuibuka kinara wa Uchumi Jumuishi barani Afrika, baadhi ya Wataalamu wa masuala ya uchumi nchini wameelezea kuwa hatua zinazochikuliwa na Serikali kuwawezesha wanachi kuwekeza katika shughuli za kiuchumi na utoaji bora wa huduma za jamii vitaufanya uchumi wa Tanzania kuendelea kukua zaidi.

Wakitoa maoni yao juu ya dhana ya uchumi jumuishi, baadhi ya wataalamu hao wamesema kuwa madiliko ya sera na sheria zinawawezesha wananchi wengi kumiliki uchumi ni sehemu ya vigezo vya kuufanya uchumi kukua huku ukigusa maisha ya wananchi walio wengi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi, Bi. Bengi Issa ameielezea dhana ya uchumi jumuishi kuwa ni ile ambayo shughuli za kiuchumi zinawajumuisha moja kwa moja wananchi na kwamba mabadiliko ya sheria katika sekta ya madini na katika umiliki wa makampuni ya simu yametoa fursa kwa watanzania wengi kushirikikatika uchumi.

Amesema kuwa utekelezaji wa sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne, kuimarishwa kwa huduma za afya, maji, umeme pamoja na mapambano dhidi ya rushwa, hifadhi ya jamii na utekelezaji wa miradi ambayo inawapa fursa wananchi kushirikikatika shughli a kiuchumi ni miongoni mwa sifa zinazoifanya Tanzania kushika nafasi ya juu.

“Serikali inaweka mazingira bora ya wananchi kushiriki shughuli za kiuchumi katika miradi mbalimbali. Tunahakikisha kila mradi unaoingia nchini basi wafanyabiashara wa Tanzania wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo”, alifafanua Bi. Bengi.

Amesema kwa upande wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi wamekuwa wakishiriki katika kuweka mipango na sera ili kuhakikisha Watanzania wengi wanashiriki shughuli zakiuchumi ikiwemo kumiliki ardhi ili iwasaidie katika kutafuta mitaji ya biashara.

Nae Mtaalam wa Uchumi wa Kilimo ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo anaeleza kuwa mfumo bora wa utawala nchini umewezesha Tanzania kuwa na Uchumi Jumuishi kutokana na wananchi kuanzia ngazi ya kijiji kushirikishwa katika kupanga mipango ya maendeleo jambo ambalo linawafanya waangalie vipaumbele muhimu katika maeneo yao.

Dkt. Lunogelo anataja mradi ya TASAF, kuongezeka kwa mikopo kwa wanafunzi wa  elimu ya juu, kuanzishwa kwa vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) na kurahisishwa kwa huduma za kifedha ni miongoni mwa mambo yanaifanya Tanzania kuibuka kinara katika uchumi jumuishi.

Aidha, Dkt. Lunogelo anaeleza kuwa kutokana na kuendelea kuboreshwa kwa mifumo na juhudi za makusudi za Serikali za kuwasaidia Watanzania wengi zaidi kushiriki shughuli za kiuchumi kutaifanya Tanzania kung’ara zaidi katika suala la uchumi jumuishi ambao unafaidisha wananchi wengi.

“Uchumi jumuishi ndio msingi mkubwa wa kuleta amani na utulivu katika nchi kwani watu wanaguswa na matunda ya ukuaji wa uchumi”, alieleza Mtaalamu huyo wa Uchumi.

Dkt. Lunogelo anasisitiza kuendelea kufanya kuwashirikisha na kuwatafutia wananchi fursa zaidi za kiuchumi ili dhana hii ya Uchumi Jumuishi iwaguse Watanzania wengi zaidi.

Jaji Mkuu Awaonya Watumishi wa Mahakama

$
0
0
Na Lydia Churi-Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Watumishi wa Mahakama nchini kutoa huduma kwa kuzingatia Maadili, kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati pamoja na kuacha vitendo vya rushwa ili kuongeza imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Akizindua wiki ya Sheria na Maonesho ya Elimu ya Sheria jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu alisema kuwa nguvu ya Mahakama ni imani ya wananchi na imani hiyo itaongezeka ikiwa hakuna rushwa, kuna maadili mema na kesi zitamalizika kwa wakati.

Jaji Mkuu pia amewataka wananchi kuacha kuilalamikia Mahakama na badala yake wachukue hatua kwa kuwataja watumishi wasiozingatia maadili kwa uongozi wa Mahakama.

Aidha, amewashauri wananchi kujifunza na kuelewa taratibu za mashauri Mahakamani ili kurahisisha upatikanaji wa haki zao wanapozitafuta kwenye Mahakama mbalimbali nchini.

“Wananchi wengi wanakwenda kutafuta haki sehemu isiyohusika hivyo wanatakiwa kujifunza taratibu za Mahakama ili waweze kupata haki kwa wakati kwa kuwamuda mwingi unapotea  kwa  kutafuta haki mahali pasipostahili”, alisema Prof. Juma.

Alisema hivi sasa Mahakama inaingia kwenye matumizi ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano- TEHAMA hivyo matumizi haya yatamsaidia mwananchi kuweza kufahamu hatua zote za shauri lake lililopo Mahakamani.

Jaji Mkuu ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupata elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Mahakama na sekta ya sheria kwa ujumla.

Alisema, katika maonesho hayo, wananchi watapata nafasi ya kujifunza juu ya usuluhishi nje ya Mahakama,  Mahakama inayotembea (Mobile Courts) pamoja na changamoto  za upatikanaji wa haki zikiwemo upungufu wa Watumishi, Miundombinu, pamoja na vifaa.

Akizungumzia taratibu wa usuluhishi wa kesi nje ya Mahakama (Mediation), Jaji Mkuu amesema wakati sasa umefika kwa wananchi kutumia utaratibu huo unaorahisisha upatikanaji wa haki na kuongeza kuwa Haki bora hupatikana kwa usuluhishi majumbani.

Aidha, kabla ya kuzindua wiki ya Sheria, Jaji Mkuu aliongoza Matembezi waliyowashirikisha watumishi wa Mahakama, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla yaliyoanzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mpaka viwanja vya Mnazi Mmoja.

Matembezi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa wakati katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo  Prof. Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images