Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tido Muhando Kaachiwa kwq Dhamana

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amepata dhamana baada ya kukidhi masharti na kutakiwa kurejea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23, mwaka huu.
 
Tido alifikishwa mahakamani hapo saa 5:22  asubuhi na aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kabla ya kusomewa mashtaka matano.
 
Leo Januari 26, mwaka 2018 wakili wa Takukuru, Leonard Swai amedai mbele ya hakimu mkazi mkuu wa makahama hiyo,  Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano.

Swai amesema Juni 16, 2008 katika maeneo ya Dubai, United Arab Emirates (UAE), Tido akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 group Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume  na sheria ya manunuzi na kuisababishia BVl kupata manufaa.
 
Shtaka la pili, Tido anadaiwa Juni 20, 2008  katika maeneo ya utekelezaji wa kazi yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano (wakuu wa makubaliano) kwa utangazaji wa digital duniani kati ya TBC na BVl.
 
Shtaka la tatu, Agosti 11, 2008  na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Tido anadaiwa kutumia  vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.
 
Shtaka la nne, Tido anadaiwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai, United Arab Emirates alitumia vibaya madaraka yake kwa kusini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT broadcast infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.
 
Katika shtaka la tano, Tido anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 katika maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887, 122,219.19.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Tido ambaye anatetewa na wakili Ramadhani Maleta alikana mashtaka yote.
 
Swai alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
 
Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Mbali na sharti hilo, pia awe na wadhamini wawili ambapo watasaini hati ya dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh500 milioni na asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
 
Mshtakiwa alikamilisha masharti hayo kwa kuwasilisha hati za mali na wadhamini wawili nyakati za saa sita mchana na kuondoka.
 
Kesi imeahirishwa hadi Februari 23, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).
Kuhusu dhamana hiyo, DPP alipeleka hati ambayo inaipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuisikiliza kesi hiyo.
 
Mhando ni miongoni mwa waandishi wa habari na watangazaji mahiri na wakongwe ndani na nje ya nchi ambaye amewahi kufanya kazi Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC).
 
Pia amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanspoti na The Citizen na sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 27

Jibu la Polisi baada ya kuagizwa na Waziri kuwakamata watuhumiwa ndani ya siku 7

$
0
0
Jeshi la Polisi limesema limepokea agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla la kuwachukulia hatua watu wanne ndani ya siku saba kwa madai wanashiriki katika mtandao wa ujangili, lakini halifanyi kazi kwa shinikizo.
 
Msemaji wa Jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa amesema polisi wanafanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Jeshi hilo.
 
Juzi,  Kigwangalla mbali na kutoa agizo hilo, amesema watu hao wanne pia walipanga njama za kumuua mwanaharakati, Wayne Lotter na kwamba polisi wakishindwa kuwakamata atawashtaki kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mwakalukwa amesema jukumu lao ni kukamata wanapopata shitaka la kuwapo kwa kitu kisicho cha kawaida, kuchunguza na kupeleka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine.
 
“Kazi yetu ni kukamata, kuchunguza na kupeleka kwa  DPP kwa ajili ya taratibu nyingine, hatufanyi kazi kwa matamko ya bungeni,” amesema na kuongeza;
 
“Alichokisema mheshimiwa Kigwangalla nimekisoma kwenye vyombo vya habari akihusisha na suala la mwanaharakati aliyeuawa, sisi hatufanyi kazi kwa kufuata vyombo vya habari vimeandika nini au limetolewa tamko gani au kuna shinikizo gani, tunafanya kwa kufuata taratibu zilizopo.”

Taarifa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB)

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa  wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz  hadi tarehe 31 Januari, 2018.

Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo:
•    Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz
•  Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha.
•    Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020
•   Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet”
•    Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe.
•   Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka.
•    Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150
•    Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hawatahusika kwenye zoezi hili kwa vile taarifa zao ziliwasilishwa wakati wa kuomba mikopo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 26/01/2018

Lowassa avaa gwanda kwa Mara ya Kwanza na kumnadi Mgombea wa CHADEMA

$
0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa leo  amepokewa kwa nderemo na wafuasi wa chama hicho.

Lowassa ambaye kwa mara ya kwanza leo Jumamosi Januari 27,2018 amevaa gwanda tangu ajiunge na Chadema mwaka 2015 aliwasili ofisi za chama hicho kanda ya Pwani zilizoko Magomeni, ambako yalianza maandamano kuelekea Mwananyamala ulikofanyika mkutano wa hadhara wa kampeni.

Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Ali Mapilau, Mwananyamala .

Akiongea katika mkutano huo, Lowassa amefunguka na kuwataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kuacha kumtaja taja mgombea Ubunge wa CCM Kinondoni Maulid Mtulia kwani mtu huyo ni wa hovyo hastaili kutajwa tajwa kwani kufanya hivyo ni kumpa kichwa.

"Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka kusema saizi tujiandae kulinda kura zetu" alisema Lowassa

Mbali na hilo Lowassa alimnadi Salum Mwalimu kwa kusema kuwa ni kijana safi ambaye anastahili kwenda Bungeni kuwasemea wananchi wa Kinondoni 

 
Akizungumzia hatua ya Lowassa kuvaa Gwanda, Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Kinondoni, Rose Moshi amesema anadhihirisha kuwa ni kamanda na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi naye.

"Tulikuwa na hofu alipokwenda Ikulu, kuvaa kwake gwanda kunaonyesha kuwa ni mwenzetu," amesema.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Jerome Ulomi amesema Lowassa amedhihirisha kuwa ni mwana Chadema.

January Makamba: Taasisi za umma tumieni gesi kupikia

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba ameziagiza taasisi za umma, kuacha kutumia mkaa kupikia vyakula badala yake zitumie gesi ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.

Waziri January alitoa kauli hiyo jana kwenye shughuli za upandaji miti zilizofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma alikokwenda kumwakilisha Makamu wa Rais.

Alisema wakati wowote kuanzia sasa ataandika waraka katika taasisi zote kubwa ikiwamo majeshi na vyuo vikuu vyote kwa kuwa mamlaka hiyo anayo kisheria.

“Wengine mtajiuliza nachukua wapi mamlaka hiyo kutoka wapi, natumia sheria ya mazingira kifungu cha 13 ambacho kinanipa mamlaka hayo kwa taasisi yoyote nitakayoona inaharibu mazingira.

“Sheria inanipa nguvu hata kama kuna sheria nyingine hapa inayotoa tafsiri nyingine, inasema sheria hii itakuwa juu yake,” alisema January.

Awali, Naibu Waziri wizara hiyo, Kangi Lugola alisema Serikali haitamsamehe mwekezaji yeyote wa viwanda atakayeharibu, kutiririsha maji au kemikali kwa kisingizio cha uwekezaji wa viwanda.

Lugola alisema kumekuwa na kelele nyingi na visingizio vya Serikali ya viwanda kwa kuanzisha viwanda bila ya kufuata sheria ya mazingira.

Alisema mwekezaji yeyote atakayevunja sheria hiyo hakutakuwa na msamaha badala watamlinda mtu atakayefuata sheria ya viwanda na mazingira.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa alizitaka halmashauri zote kutunga sheria kali kwa ajili ya kulinda hifadhi ya mazingira ikiwamo miti inayopandwa.

Mwigulu Nchemba Awachana Wapinzani Wakati Akimnadi Mgombea wa CCM

$
0
0
MBUNGE wa Iramba Magharibi, Singida na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameongoza jahazi la makada, wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uzinduzi wa kampenzi za uchaguzi mdogo wa ubunge kwa Jimbo la Kinondoni.

Katika uzinduzi huo ambao umefanyika katika Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, CCM wamemnadi Maulid Mtulia na kuwaomba wananchi wa Kinondoni wampe kura za kutosha ili aweze kuwawakilisha vilivyo bungeni ikiwa ni pamoja na kutatua kero zao, kushirikiana na serikali bega kwa bega katika kuleta miondombinu ya maendeleo kwa jimbo hilo.

Mwigulu nchemba akizindua kampei za CCM katika Viwanja vya Biafra Kiondoni, Dar.

“Msije mkaenda kupiga kura ya uchaguzi mdogo kwa kiwango kidogo, mkapige kura kwa kiwango cha uchaguzi mkuu, kila mmoja akawe kampeni meneja wa mgombea wetu, aje na wapiga kura siku ya kupiga kura Februari 17, na hiyo ndiyo faida ya mtandao wa chama chetu .

“Sababu zote za msingi za ushindi tunazo sisi, wao wamebaki na hoja moja tu kwamba Mtulia amehama kwa nini? Ilani ya uchaguzi iliyochaguliwa ni ya CCM na itatekelezwa hadi mwaka 2020, asitokee mtu ambaye atawadanganya, kumpigia kura mtu wakati hana ilani inayotekelezeka ni sawa na kupigia kivuli wakati kuna mtu,” alisema Mwgulu wakati akiwasihi wananchi kumpigia kura Mtulia.

Aidha katika mkutano huo, wanachama wengi wa upinzani wamerudisha kadi na kujiunga na CCM.

Wassira: CHADEMA Ndo Shetani Wetu

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika serikali ya awamu ya nne na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM, Stephen Wasira amedai hawawezi kufanya siasa bila ya kukitaja chama cha CHADEMA kwa kuwa ndio shetani wao

Wasira amebainisha hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba baada ya kusikia kauli ya mgombea Ubunge wa Jimbo hilo katika 'televison' kuwa CCM hawawezi kufanya siasa bila ya kuitaja CHADEMA.

"Nimemshangaa kiukweli mgombea huyo, maana hata Maimamu na Wachungaji huwa hawawezi kumaliza ibada bila ya kumtaja shetani maana shetani ndio mpinzani wao na endapo wasipotaja wana kuwa hawajamaliza ibada yao. Hivyo asishangae sana na sisi tunapokuwa katika siasa kuitaja CHADEMA kwa maana ndio shetani wetu hapa", alisema Stephen Wasira.

Kwa upande mwingine, Wasira amesema tokea mwaka 2015 kumekuwa na siasa za kishetani nchini Tanzania hasa upande wa upinzani ambazo zimetawaliwa na uongo unaofanana na giza kwa kusema uongo katika kampeni zao na kudanganya wananchi.

Kubenea: Mchagueni Salum Mwalimu...Yeye Ndo Tundu Lissu Mdogo!

$
0
0
Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amefunguka na kusema mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.

Kubenea amesema hayo leo Januari 27, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha.

Kubenea amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini ambao wanapaswa kufika Bungeni kuwatetea wananchi wa Kinondoni.

"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo makubwa sana na kutetea hadhi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine, mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea

Mbali na hilo Kubenea aliwataka wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi.

PICHA 5 :Alikiba alivyomtembelea mama yake Rais Magufuli

$
0
0
Leo January 28,2018 Staa wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba amepost picha kupitia ukurasa wake wa Instagram na kushukuru kwa baraka alizozipata baada ya kumtembelea mama mzazi wa Rais Magufuli  akiwa  Wilayani Chato.

Mume amteka mkewe.....aamuru rafiki yake ambake kisha kammwagia tindikali

$
0
0
Binti wa miaka 24 mwenye mtoto mmoja ambaye ni raia wa Kenya, ameuawa kikatili baada ya kutekwa na mume wake ambaye alikuwa na rafiki yake kisha kumwambia rafiki yake huyo ambake binti huyo na baada ya mateso hayo kwa kushirikiana wakamwagia tindikali.

Lucy Ndungu aliwekewa dawa za kulevya na mumewe na ndipo alipoweza kumteka akiwa na rafiki yake, na baada ya kumbaka na kummwagia tindikali waliutupa mwili wake kando ya barabara.

Familia ya marehemu imeeleza kuwa ilimkuta Lucy anamajeraha ya kuungua kwa 75% ya mwili mzima huku hali yake ikiwa mbaya sana na hivyo akawahishwa katika Hospitali ya Taifa Kenyatta kupatiwa matibabu lakini hata hivyo akiwa kwenye matibabu hayo alifariki dunia.

Inaelezwa sababu ya mume huyo kufanya hivyo ni kwamba, walikuwa kwenye ugomvi na Lucy akaamua kuachana naye na kuondoka nyumba waliokuwa wanaishi pamoja na kukataa kurudiana na mumewe huyo jambo ambalo linadaiwa kumkasirisha mwanaume huyo.

NEC Yatoa Maamuzi Ya Rufaa Ya Mgombea Ubunge wa CHADEMA Na Rufaa 5 Za Wagombea Udiwani

$
0
0
MAAMUZI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU RUFAA MOJA YA MGOMBEA UBUNGE NA RUFAA TANO ZA WAGOMBEA UDIWANI

Kwa kuzingatia masharti ya Kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) akipinga maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kuhusu pingamizi alilomuwekea Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aidha, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ikisomwa pamoja na Kanuni za 28 na 29 za Kanuni za Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa tano (5) za Wagombea  Udiwani  kutoka katika Kata ya Isamilo – Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakipinga Maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo.  Rufaa tatu (3) ni za wagombea walioondolewa kwenye kugombea ili warejeshwe na Rufaa mbili (2) zinaomba Tume itengue uteuzi wa mgombea Udiwani aliyeteuliwa katika Kata hiyo.

Katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 26 Januari 2018 siku ya Ijumaa, Tume ilipitia Rufaa hizo na kuamua kama ifuatavyo:

Mosi, kuhusu Rufaa ya Mgombea Ubunge, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo Mgombea aliyekatiwa Rufaa wa CHADEMA anaendelea kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kinondoni.

Pili, kuhusu Rufaa za Wagombea Udiwani Kata ya Isamilo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kupinga kuondolewa kugombea Udiwani katika Kata hiyo, Tume imewarejesha kuwa Wagombea Udiwani wawili wa vyama vya CHADEMA na CUF.

Tatu, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ya kumuondoa katika orodha ya wagombea Udiwani mgombea wa Chama cha UDP. Hivyo hatakuwa mgombea katika kata hiyo

Nne, Tume imekataa rufaa mbili zilizokuwa zinapinga uteuzi wa mgombea wa CCM aliyeteuliwa katika Kata hiyo na hivyo, mgombea wa CCM anaendelea kugombea Udiwani katika kata husika.

Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatie wahusika maamuzi hayo.

Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya January 28

CCM yazidi kupunguza Madiwani wa CHADEMA Dar

$
0
0
CCM yazidi kupunguza Madiwani wa CHADEMA Dar

Madiwani Watatu wa CHADEMA Kilimanjaro Watimkia CCM

$
0
0
Katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Rombo, Katibu wa NEC Mwenye dhamana ya Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole ameujulisha umma wa wananchi wa Rombo kuwa baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani na kutambua uwepo wa kero kubwa ya Maji, amewasiliana na Uongozi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwamba ukosefu wa kiasi cha shilingi Milioni 130 kilichokuwa kinakosekana ili kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa kuvuta maji kutoka Ziwa Chala sasa zitatolewa na Wizara ili tatizo la upungufu mkubwa wa maji Wilaya ya Rombo limalizike.

Aidha Ndg. Polepole akawaelekeza watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kufanya mawasiliano ya haraka na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kupata fedha hizo na kuhakikisha mchakato wa kuvuta maji kutoka Ziwa Chala unaanza maramoja.

Wakati Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Wilaya na Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi kikiendelea madiwani watatu wa Chadema walifika eneo la kikao na kuomba wapewe fursa ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pamoja na maelezo waliyoyatoa Madiwani hao wa Chadema katika kikao Cha Halmashauri Kuu ya Wilaya juu ya sababu zilizopelekea kujitoa kwao Chadema na kujiunga na CCM, wameelezea pia siri ya kudorora kwa Maendeleo Wilaya ya Rombo kuwa ni mpasuko uliopo kati ya Madiwani wanaomwunga mkono Mbunge wa Jimbo la Rombo Ndg. Joseph Selasini na madiwani wanaomwunga mkono Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Ndg. Evarist Silayo sababu ikiwa ni vita ya Ubunge mwaka 2020.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Rombo kwa kauli moja wamewapokea wanachama hao wapya na Ndg. Polepole akaelekeza uongozi wa Wilaya kuwapitisha katika program ya mafunzo ya Imani, Itikadi, Siasa, Masharti ya Mwanachama, Ahadi za Mwanachama na Sera za Maendeleo za CCM.

Madiwani waliojitoa CHADEMA na kujiunga na CCM leo ni Ndg. Juliana Malamsha na Martha Ushaki wa Viti Maalum pamoja na Frank Lubega wa kata ya Kelamfuamokala.

Huu ni muendelezo wa ziara za ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhuisha dhana ya Chama kushika hatamu na kuhakikisha kinaisimia Serikali katika kushughulika na shida za wananchi.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), ROMBO, KILIMANJARO

Ujenzi wa reli ya kisasa watarajiwa kuanza Machi mwaka huu

$
0
0
 Serikali imesema ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Morogoro hadi Makutopora mkoani Dodoma ambao utaanza kabla ya Machi mwaka huu, utagharimu dola 1.923bilioni za kimarekani (sawa na Sh4.3 trilioni).

Meneja Mradi huo wa Kampuni Hodhi ya Raslimali za Reli (Rahco) Mhandisi Maizo Mgedzi amesema mradi huo unatarajia kuanza wakati wowote kabla ya Machi.

Amesema  treni hiyo ina uwezo wa kwenda kilometa 160 kwa saa itahifadhi mazingira na kwamba itaweza kubeba mzigo mkubwa kwa zaidi ya mara tano ya reli ya sasa.

“Pia itaweza kubeba watu na mizigo kwa usalama kwa maana  hakutakuwa na ajali zinazosababishwa na ubovu wa miundombinu,” amesema

Meneja wa Kampuni ya Yapi Merkezi iliyopewa zabuni ya mradi huo, Abdullah Kilic amesema kuwa jiwe la msingi la mradi huo litawekwa wakati wowote kuanzia sasa.

“Tunachosubiri ni utaratibu wa Ikulu lakini jiwe la msingi tutaliweka wakati wowote kuanzia sasa,”amesema.

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde amesema Serikali ingependa mradi huo ulete matokeo chanya kwa watu wa Dodoma na si laana.

“Matokeo haya yasiwe laana kwa maana tusije kuiacha reli hii ipite tu hapana. Sisi tunataka kwa watu wa Dodoma reli hii iwe kichocheo cha kwanza cha uchumi ikiwezekana kubadilisha mji,”amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Deogratius Ndejembi amesema viongozi watawapa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha miaka mitatu cha ujenzi wa reli hiyo na kurekebishana kwa baadhi ya mambo.

“Wamesema asilimia 80 (watu 3000) watachukua watu wa Dodoma kwa hiyo ni jambo kubwa sana. Hii ni fursa kubwa hata kipindi hiki cha ujenzi,”amesema.

Wanachama wahofia kufilisiwa shamba, wampigia magoti Rais Magufuli

$
0
0
Wanachama wa chama cha Ushirika cha Uru Kati Mawela, wamemuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati mgogoro wa ardhi wakihofia kufilisiwa shamba walilopewa na Serikali lenye ukubwa wa hekari 213.

Wasiwasi huo unatokana na kushindwa kesi waliyoifungua dhidi ya kampuni ya mwekezaji, Laitolya Tours & Safaris, ambayo imejenga hoteli ya kitalii ya Kilemakyaro Mountan Lodge ndani ya hekari 27.54.

Hayo yamejitokeza katika mkutano mkuu maalum wa wanachama ulioitishwa jana Januari 27, mahsusi kujadili hukumu hiyo iliyotolewa Ijumaa ya Januari 19 na Jaji Benedict Mingwa wa Mahakama Kuu Moshi.

Katika hukumu hiyo, Jaji Mingwa amesema  hekari hizo 27.45 ni mali ya Laitolya Tours and Safaris na kuutaka ushirika huo kukabidhi hati namba CT10663 ili kampuni imilikishwe hekari hizo 27.54.

Mbali na kuamuru hati hiyo ikabidhiwe kwa msajili wa hati, lakini Jaji Mingwa ameamuru pia kuwa wana ushirika hao watalazimika kulipa gharama za kesi hiyo ya madai namba 10 ya mwaka 2015.

Hata hivyo, Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa Kilimanjaro, Henjewele John, ameliwaambia wanachama hao kuwa mwekezaji huyo amempibu Rais Magufuli na kwamba atampigia simu.

“Niwaahidi kwamba tutatumia njia zote kuhakikisha kuwa wananchi wa Uru wanapata haki yao. Hapa tutamwambia Ushirika leteni hati yenu ya kumiliki na huyu mwekezaji alete hati zake,”amesema.

“Sasa hivi nataka niwaambie majumba ya watu yanabomolewa. Si mnaona? Kwa hiyo huyu mzee wetu amebipi sasa akibipu sisi tutapiga. Zama zimebadilika na kwa hili tutalifikisha kwa Rais,”amesisitiza.

Mwenyekiti wa Ushirika huo, Richard Kimaro, amesema wao hawakuwahi kumpa mwekezaji huyo eneo hilo la ardhi, bali walimkodishia lakini aliwazunguka kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi.

“Katika kipindi chote cha mkataba tangu 1998 hakuwahi kulipa kodi ya pango ambayo kwa mujibu wa mkataba ilikuwa Dola 700 za Marekani (sawa na Sh1.6 milioni) kwa mwezi,”alidai mwenyekiti huyo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, ni kutokana na kutolipa kodi hiyo na kujimilikisha ardhi yao, walifungua kesi ya madai wakitaka ushirika ulipwe malimbikizo ya kodi yanayofikia Dola 153,600.

Mbali na kudai fedha hizo, lakini waliiomba mahakama itamke kuwa mwekezaji huyo ni mvamizi na ameingia kwa jinai katika shamba lao na pia imuamuru alipe fidia ya jumla ya Sh80 milioni.

Akizungumza katika mkutano huo, mmoja wa wanachama wa Ushirika huo, Francis Moshi, alisema wamekanganyikiwa waliposikia wameshindwa kesi na kudaiwa kuwa wao ndio walivuruga mkataba.

“Tunajiuliza hivi ni nani hapa alivuruga mkataba kati yetu na Laitolya ambaye hakulipa kodi ya pango kwa mujibu wa mkataba? Ulikuwa mkataba wa miaka 10 akaongeza sifuri ukawa miaka 100,”amedai.

Makamu Mwenyekiti wa Ushirika huo, Emanuel Mushi, alisema kilichojificha ni kuwa baadhi ya viongozi walishiriki kughushi muhtasari wa vikao mbalimbali kwa maslahi ya mwekezaji huyo.

Wajumbe wa mkutano huo waliazimia kwa kauli moja, kwamba bodi ya uongozi ya chama hicho ikate rufaa kupinga hukumu hiyo na pia ilipeleke suala hilo ngazi za juu Serikalini kupitia kwa Mrajisi.

Hata hivyo mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joachim Minde alipotafutwa jana, alisema anawashangaa wanachama hao kufanya mkutano badala ya kukata rufaa kama hawakuridhika na uamuzi.

“Wao kama wanataka kwenda kwa Rais sijui Waziri wa Ardhi wao waende. Kama mimi nina haki yangu si lazima nitalalamika? Wao kama nao wanaona wana haki walalamikie mahakama,”amesema.

“Huwezi kulalamika kuwa unamtaka Rais sijui unamtaka Waziri. Hili jambo sio la leo. Alishakuja Waziri wa Ushirika na pia akaja Waziri wa Ardhi hapa. Sio jambo geni kabisa,”amesisitiza Minde.

Minde amedai kuwa kinajitokeza ni kwamba wamekuja baadhi ya viongozi wa Ushirika ambao ni wageni wanaosumbuliwa na njaa na atafurahi sana kama siri ya mgogoro mzima ujulikane.

Mkurugenzi huyo alisema huu ni wakati wa kujua mapato na matumizi ya shamba hilo na kwamba kwa sasa anajiandaa kufungua kesi nyingine ya madai kwa jinsi walivyopata hasara tangu 1998.

Mbowe: Moleleli ni Daktari Asiye na Uwezo na Alikuwa ni Mtu wa Kujikomba CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kukanusha taarifa alizotoa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Siha, Dkt Mollel kuwa aliamua kuhama CHADEMA na kwenda CCM kwa kuwa alizuiwa kuongea na viongozi wa CHADEMA.

Mbowe amesema hayo juzi katika uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Siha, Elvis Mosi na kudai kuwa Molle hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na ni mtu ambaye amekuwa akijikomba kwa watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

"Mollel hajazuiliwa na mtu bali ni Dk. asiye na uwezo, hana uwezo wa kujenga hoja ni mwanaume anajikomba komba kwa watu wa CCM

".... niwambie watu wangu wa Siha mnapokuwa mnachagua viongozi sisi kama chama tunawapima kila mwaka, huyu uchaguzi unaokuja ataturudishia jimbo au atatunyima jimbo? 

"Na kwa vigezo mbalimbali vya chama vilivyofanyika wananchi wa Siha mshukuru kwa sababu mlikuwa unatuchagulia gunia la misumari bila kujua, angebaki kwa miaka mingine mitatu kwenye nafasi yake ya Ubunge CHADEMA wananchi wa Siha mngeichukia" alisema Mbowe

Mbowe aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha Mollel kujivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge jimbo la Siha ni mpango wa Mungu na ni jambo zuri kwani lingefanya chama hicho kuchukiwa na wananchi.

"Huu ni mpango wa Mungu aliona wananchi wa Siha nikiwaachia hili gunia la misumari litakuwa si jambo zuri hivyo akamtia uchizi akaamua kuhama chama, kwa hiyo hatuna cha kulia kila kitu ni mpango wa Mungu, alijua kwamba Siha tumejitwisha gunia la misumari"

Nandy Afunguka Kuhusu Kukuwadiwa Wanaume

$
0
0

Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy ambae anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa 'kivuruge' amefunguka na kudai hakuna mtu yeyote atakaeweza kumuunganishia kwa wanaume wenye pesa (pedeshee) bali kama watamuitaji wataenda wenyewe kwake.

Nandy ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo tetesi za muda mrefu zinazodai kwamba msanii huyo amesababisha kuvunjika kwa kundi la 'LFLG' kutokana na aliyekuwa meneja wake ambae ni Petit Man kumkuwadia kwa 'vigogo' huku akifahamu tosha kwamba mrembo huyo anatoka kimapenzi na Bill Nas ambae pia alikuwa mmoja wa wasanii katika kundi hilo.

"Mimi mtu hawezi kunipeleka kwa mapedeshe kama kunifuata watanifuata wao wenyewe, hawezi mtu kunipeleka kwa mwanaume sijafikia hatua hiyo. Na sina mazoea na Petit ya kuunganishiana mizigo", alisema Nandy.

Kwa upande mwingine, Nandy amesema haoni umuhimu wa kuongelea mambo ambayo hayana msingi katika kipindi huku akisisitiza kwamba jambo la muhimu kwa sasa ni 'kivuruge' kushika namba moja Tanzania nzima pamoja na wimbo wao mpya na Aslay 'Subalkher'.

Mbowe Amvaa Mwigulu Nchema, Seleman Jafo kwa Ubaguzi

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kulaani vikali kitendo alichofanya Waziri wa Mambo ya ndani pamoja na Waziri wa TAMISEMI kumpigia kampeni mgombea wa Ubunge wa CCM jimbo la Siha na kusema kauli zao zimejaa ubaguzi wa wazi wazi

Mbowe amesema hayo juzi  wakati akizindua kampeni za wagombea wa Ubunge na udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Siha na kudai Mawaziri hao wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao.

"Kaja Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anawaambia kuwa lazima mchague CCM, anakuja Jafo Waziri wa TAMISEMI anawaambia wananchi wa Siha ili mpate maendeleo labda mumchague Mollel, huu ni utoto mtupu. 

"Tunapoongozwa na viongozi wa sampuli hizi, viongozi wabaguzi, viongozi waliopewa dhamana ya maisha yetu wakafikiri ni mali za baba zao na mama zao wanakuja kutuambia utoto watu wa Siha tunaakili, kujengwa kwa barabara si fadhila ya Rais" alisema Mbowe

Mbali na hilo Mbowe alisema kuwa katika uchaguzi huu wa sasa endapo wataona gari za Serikali zikitumika kwenye kampeni za wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zitakuwa halali yao.

"Mzee Mwambigija safari hii kama kufa tufe, safari hii kama noma na iwe noma tunaomba magari ya Serikali yatumike kwa kazi za Serikali hatutakuwa na ugomvi lakini magari ya Serikali na vyombo vya Serikali vikitumika kwenye kampeni za chama chochote ni halali yetu, kwa sababu nchi hii inaonekana siasa za kistaraabu haziwezekani" alisisitiza Mbowe
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images