Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mgufuli akagua ujenzi wa nyumba 851 za serikali zinazojengwa Mabwepande jijini Dar

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za Serikali zipatazo 851 zilizopo katika eneo la Mabwepande, Kinondoni,jijini Dar es Salaam zinazosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Huu ni muendelezo na mikakati ya Wizara ya Ujenzi ya kuwajengea na kuwauzia watumishi wa Serikali nyumba kwa bei nafuu. Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe

CHADEMA wamvaa Rais Kikwete , Wampa siku 3 za kuifuta kauli yake....Nape Nnauye ajibu mapigo, adai kuwa Rais Kikwete hawezi kuifuta kauli hiyo, asisitiza kuwa dawa ya moto ni moto

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempa siku tatu Rais Jakaya Kikwete awe amefuta kauli yake aliyoitoa Februari 15 mwaka huu, mjini Dodoma baada ya kufunga Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Kauli hiyo ni ile iliyowataka wanachama wa CCM kuacha unyonge badala yake wajibu mapigo ya wapinzani hasa wanaoendesha siasa za vurugu katika kampeni za uchaguzi. Rais Kikwete

Baby Madaha atangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na maisha ya presha

$
0
0
  IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza,  staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha. Akiongea  na  mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.  

Juma Nature Akana Madai ya Kumponda Diamond kwenye Nyimbo yake Mpya…Adai ‘Dada Mondi’ ni Msanii tofauti.

$
0
0
Hatimaye Juma Nature, amezungumzia utata ulioibuka kwenye wimbo wake mpya Kama Jana, unaohusiana na kama kweli amemdiss Diamond.   Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter, Juma Nature aka Kiroboto amesema jina la ‘Dada Mondi’ lililofanya wengi waamini kuwa ni version yake ya Diamond, ni jina la msanii mwingine kabisa.     “Hamna diss ya kumdiss Diamond, Diamond   hajadisiwa,”

Video ya Nape akisimulia UNYAMA wa CHADEMA ulioilazimisha CCM iwatangazie wanachama wake kuacha unyonge na kujibu mapigo

$
0
0
Hii  ni  Video  fupi  ya  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Bw. Nape Nnauye  akisimulia  unyama  na  ukatili  unaofanywa  na  chama  pinzani  cha  CHADEMA  kiasi  cha  kuilazimu  CCM  nayo  kuwatangazia  wanachama  wake  waache  unyonge  na  badala  yake  wajibu  mapigo  ya  ukatili   huo.... VIDEO  IKO  HAPO  CHINI

Mkuu wa IGP Ernest Mangu na Chagonja wakemea uhalifu na mauaji nchini....Wadai kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio haya

$
0
0
  Na Frank Geofray wa  Jeshi la Polisi, Moshi. Jeshi la Polisi Nchini litaendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na vitendo vya mauaji yanayosababishwa na Imani za kishirikina kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu katika mkutano mkuu wa maofisa wakuu waandamizi unaoendelea

Ajali mbaya: Lori la mafuta ladondoka mlima Sekenke na kuua watu wanne papo hapo

$
0
0
  LORI la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne papohapo.   Chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki lori hilo kukamata moto wakati lilipokuwa linashuka milima hiyo. Shuhuda wa ajali hiyo, bwana Julius Chacha alipoongea na Dj Sek Blog amesema kuwa lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.  

Taarifa ya serikali kuhusu baraza la maaskofu wa kipentekoste Tanzania kutokuwa na uwakilishi katika bunge maalumu la katiba

$
0
0
TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU BARAZA LA MAASKOFU WA KIPENTEKOSTE TANZANIA (PENTECOSTAL COUNCIL OF TANZANIA) KUTOKUWA NA UWALIKILISHI KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA 1.  Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba unafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo

Facebook yanunua application ya 'WhatsApp' kwa jumla ya dola bilioni 19

$
0
0
  Facebook wanazidi kujitanua zaidi kibiashara katika ulimwengu huu wa dijiti ambapo wameweza kufanya makubalino na waanzilishi wa ‘WhatsApp’, Jan Koum na Brian Acton kuinunua kwa makubaliano ya jumla ya dola bilioni 19 pamoja na hisa.   Mwanzilisihi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa walianza kuzungumzia hatua hiyo siku 11 zilizopita ili waweze kuimiliki WhatsApp ambayo hivi sasa

Mtandao mkubwa wa wizi wa fedha za serikali katika wizara ya fedha....Ni akina nani wameiba hizi bilioni 480 ?

$
0
0
Ugumu uliopo hapa ni kwamba haijulikani kama fedha hizo zilizopotea zilitokana na kodi za wananchi au wafadhili ambao walichangia Sh842 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13. Tangu gazeti la The Citizen lichapishe mwishoni mwa wiki habari za upotevu wa Sh480 bilioni katika Wizara ya Fedha, Serikali imekaa kimya kama vile wizi huo ni tukio la kawaida, hivyo halihitaji

CHADEMA yamwekea pingamizi mgombea wa CCM kalenga ikidai kuwa si raia wa Tanzania

$
0
0
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA, Grace Tendega, amemuwekea pingamizi mgombea mwenzake kupitia CCM, Godfrey Mgimwa, kwa kile kinachodaiwa kuwa si raia wa Tanzania.   Tendega alichukua fomu ya kumwekea pingamizi hilo juzi wakati zoezi la kusitisha fomu za wagombea ukiwa umefikia kikomo. Jana majira ya mchana mgombea huyo alirudisha fomu ya pingamizi kwa msimamizi wa uchaguzi

Wabunge waikataa posho ya sh 300,000 kwa siku....Wanadai eti ni ndogo sana na haiendani na hadhi zao

$
0
0
WAKATI mjadala wa kihistoria wa kuunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiwa katika hatua ya kupata kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, baadhi ya wajumbe wameamua kuelekeza nguvu kudai posho nono.  Wajumbe hao wanapinga posho ya sasa ya Sh 300,000 kwa siku, ambayo kwa wananchi wa kawaida inaonekana ni kubwa, lakini vielelezo vyao ni taarifa, kwamba wajumbe ambao wanatoka

Ombi la kesi ya Sheikh Ponda kusikilizwa Februari 26 mwaka huu....

$
0
0
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imesema itasikiliza maombi ya kufanya marejeo kuhusu kuliondoa shitaka la kukaidi amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (pichani) Februari 26, mwaka huu. Hatua hiyo  imefikiwa jana mahakamani hapo  baada ya Sheikh

Bunge la Katiba: Wadau walaumu mume na mkewe kuteuliwa kukiwakilisha chama.... Ni chama cha NLD ambapo mwenyekiti wake alijiteua yeye na mkewe.

$
0
0
Habari kwa mujibu wa gazeti la MWANANCHI — Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano. Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji

Watoto mapacha waliopelekwa kutenganishwa nchini India warejea jijini Dar

$
0
0
  Watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha wakiwasili nchini Tanzania kutokea nchini India walipokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya watoto ya Appolo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe,

Familia ya watu watatu yahamishia makazi yake chooni

$
0
0
FAMILIA ya watu watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka saba imelazimika kuhamishia makazi chooni baada ya paa la nyumba waliyokuwa wakiishi kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita katika Wilaya ya Hai.   Familia hiyo ya Aziza Mohamed (55), mwanae wa kiume, Sikujua  Aloyce (40)  na mjukuu wake wakazi wa Kitongoji cha Kijiweni, Kijiji cha

Baada ya wabunge kuikataa posho ya sh. 300,000 kwa siku, Mwenyekiti ameamua kuunda tume ya watu 6 itakayotazama jinsi ya kuboresha viwango vya posho hizo.

$
0
0
Suala la posho limezidi kuwa kaa la moto katika vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma leo, hali iliyomlazimu mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho ateue timu maalum ya watu 6 kutazama jinsi ya kuboresha viwango vya posho hizo.    Timu hiyo inatarajiwa kuyachunguza kwa undani mahitaji ya wajumbe wa Katiba, kisha kuisaidia serikali kutafuta jinsi ya kuongeza posho hizo

Uganda yapiga marufuku vimini, vitopu na mavazi mengine ya nusu uchi.....Atakaye kaidi, atafungwa jela miaka 10 mpaka 15

$
0
0
RAIS Yoweri Museveni amesaini sheria ambayo inaharamisha mavazi yasiyo ya heshima na picha za utupu.  Pia, wanawake wamepigwa marufuku kuvaa nguo fupi - vimini na blauzi fupi – vitopu, ambavyo vinashawishi hisia za ngono, isipokuwa kama vivazi hivyo vitatumika kwa madhumuni ya kutoa elimu au matibabu au kutumika kwenye michezo na utamaduni.   Akizungumza na waandishi wa habari katika

Baada ya CHADEMA kuweka pingamizi, CCM yamwaga VIELELEZO Kuthibitisha kuwa Godfrey Mgimwa ni Raia wa Tanzania

$
0
0
Bw. Godfrey Mgimwa akiwa ameshika Passport yake aliyokuwa akiwaonesha waandishi wa habari leo katika ofisi kuu za CCM mkoa wa Iringa alipokutana na waandishi wa habari   *** Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha madai yaliyotolewa kwenye pingamizi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba mgombea wao (CCM) katika Jimbo la Kalenga, Godfrey William Mgimwa, siyo Mtanzania

Umoja wa Mataifa waiomba Tanzania kupeleka wanajeshi ( JWTZ ) Sudan Kusini kwa ajili ya kulinda amani.....Hii ni kutokana na ubora uliotukuka wa jeshi letu

$
0
0
Serikali inatarajia kupeleka kikosi kimoja cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Sudan Kusini kwa ajili ya kulinda amani kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea.    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Dar es Salaam jana kwamba Serikali imekubali kupeleka batalioni moja baada ya kuombwa na Umoja wa Mataifa (UN).  
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images