Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Benard Membe amchokonoa Edward Lowassa kiaina ....Adai kuwa ikitokea kada yeyote wa CCM mwenye PESA akawa Rais, lawama zote zitaelekezwa kwa waandishi wa habari

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutoruhusu mtu yeyote kununua urais kama njugu.   Alitahadharisha kuwa kama itatokea kada yeyote wa CCM amepata urais kwa kununua kama njugu, waandishi wa habari nchini watakuwa wa kwanza kulaumiwa kwa kuwasaidia kuwaingiza madarakani watu wa aina hiyo.   Ingawa Waziri Membe hakutaja

Lulu Michael ayakumbuka mapenzi ya Steven Kanumba katika "siku ya wapendanao"

$
0
0
WAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo aliyetangulia mbele za haki. Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa

Kodi ya ving`amuzi kushuka......Lengo ni kuhamasisha kampuni nyingi zaidi kujitokeza kuuza vifaa hivyo kwa wananchi

$
0
0
Serikali imesema inatarajia kuwa kodi ya ving'amuzi itashuka ili kuhamasisha kampuni nyingi zaidi kujitokeza kuuza vifaa hivyo kwa wananchi, tofauti na sasa. Hayo yalisemwa mjini hapa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, wakati  akifunga mkutano wa jukwaa la kujadili mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali,

Hamisa Mobeto alikana penzi la Diamond...“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema Sepetu"

$
0
0
Mrembo aliyewahi kushiriki miss Tanzania Hamisa Mobeto a.k.a Hamisa kadomo amekanusha tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii kipenzi cha kinadada Naseeb Abdul a.k.a Daimond Platnumz na kusema kuwa anamuheshimu kama shemeji yake.   Hamisa ambaye pia amewahi kuonekana katika video ya msanii Quick Rocka ‘My baby’, ameiambia Global Publishers kuwa maneno yanayosemwa  si

Ndege ya Ethiopian Airlines yatekwa na Rubani wake, Abadili uelekeo na kutua Uswis ili kuomba hifadhi ya kisiasa

$
0
0
Rubani msaidizi wa ndege ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikienda Roma toka Addis Ababa ameteka ndege hiyo mapema leo na kuilazimisha itue Geneva, Uswisi, polisi wameieleza AFP.    Rubabi huyo alitenda kitendo hicho cha ajabu kama njia ya kujaribu kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Uswisi. “Anadai anaishi kwa hofu nchini kwake mwenyewe, hivyo anataka hifadhi

Picha za kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika jana ikiwa ni siku yake ya pili chini ya mwenyekiti wake, Rais Kikwete

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili ukumbini kuendesha Kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma jana, Feb 16, 2014.  Wajumbe wa NEC, na Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Daladala zagoma jijini Mwanza zikidai nauli IPANDE.... Abiria nao waamua kutumia Malori, baiskeli, Toyo Kilimo na pikipiki kusafiria

$
0
0
Madereva  wa  daladala  jijini  Mwanza  leo  wameamua  kugoma  kutoa  huduma  hiyo  muhimu  kwa  jamii  wakiishinikiza  serikali  kupandisha  nauli  na  kupunguza  faini  pindi  wanapokamatwa  na  askari  wa  usalama  barabarani.... Baada  ya  mgomo  huo  kuanza, abiria     walimua   kutumia  Malori, baiskeli, Toyo Kilimo  na  pikipiki  kama  njia  mbadala  ya  kusafiria.

Mkutano mkuu wa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi waanza leo mjini Moshi.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akisalimiana na makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya ndani kwenye ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo cha taaluma ya Polisi Moshi. Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima akisalimiana na

Mahabusu afariki dunia baada ya KUJINYONGA kwa kutumia tambala la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi

$
0
0
MAHABUSU, Vumi Elias (30), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tambala la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi Tunduma.   Elias, mkazi wa Maporomoko-Tunduma, aliyetuhumiwa kwa unyang’anyi wa kutumia nguvu katika eneo la Tunduma wilayani Momba, alifariki dunia jana, saa 12 asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Afya Tunduma

Godbless Lema anusurika kukamatwa na jeshi la Polisi kutokana na WARAKA wake unaomhusu Rais Kikwete aliouposti kwenye mtandao wa kijamii

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema jana alinusurika kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi ili kuhojiwa kutokana na ujumbe wake aliouposti kwenye mtandao wa kijamii akiandika: “Rais Kikwete mbona umeamua kuliangamiza taifa.”   Akizungumza na gazeti  la  Mwananchi  jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la Katiba, Lema

Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali aiomba mahakama kuu iitupilie mbali kesi ya kikatiba inayomkabili waziri mkuu, Mizengo Pinda

$
0
0
NAIBU Mwanasheria Mkuu, Mhe George Masaju (pichani) amedai mahakamani katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi  ya  Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba kwa mujibu wa katiba mamlaka ya mahakama kuingilia mwenendo wa bunge yameondolewa.   Pia, Mhe Masaju amedai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi

Lulu Michael akiri mahakamani kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba, akana mashitaka ya kuua bila kukusudia na kueleza kilichotokea

$
0
0
Mwigizaji maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta, amekiri mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba na pia kuwa ugomvi na Kanumba siku ya tukio la kifo cha mwigizaji huyo, lakini akakana mashtaka ya kumuua bila kukusudia.    Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi hiyo katika

"Fedha chafu zinachochea uhalifu nchini "...Hii ni kauli ya naibu waziri wa mambo ya ndani wakati akifungua mkutano wa maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Perreira Ame Silima, amesema uwepo wa fedha chafu nchini umechangia kuendelea kukua kwa uhalifu.  Kwa mujibu wa naibu waziri huyo, matendo hayo ya uhalifu ni usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara ya binadamu na mitandao ya kigaidi nchini.   Akifungua mkutano wa siku sita wa wakuu na maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi kwenye ukumbi wa

Mchawi wa ungo adondoka jijini Arusha ....Baada ya watu kujaa, abadilika ghafla na kuwa kuku mweupe

$
0
0
  HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji la Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika  kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo.... Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu

Rais wa Rwanda, Paul Kagame aifanyia ukachero Tanzania....Jeuri yake yadaiwa kujengwa na ushirika wake wa kiintelijensia alioupandikiza ndani ya mfumo wa serikali ya Tanzania

$
0
0
JEURI ya wazi inayoonekana kuwemo ndani ya taarifa ambazo zimekuwa zikichapishwa mara kwa mara na vyombo vya habari  vya  serikali ya Rais Paul Kagame wa Rwanda dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na serikali yake, inaelezwa kujengwa na ushirika wake wa kiintelijensia  alioupandikiza ndani ya mfumo wa  serikali  na taasisi mbalimbali hapa nchini,MTANZANIA limedokezwa.  Taarifa zilizolifikia gazeti

Mwanamke atiwa mbaroni baada ya kumfunga MINYORORO mtoto wa kaka yake na kuanza kumtumia KISHIRIKINA

$
0
0
KATIKA hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Dorah Joseph (34) anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kumfunga mnyororo mtoto wa kaka yake aitwaye Happy Joseph (13) na kumtelekeza bila kumpatia huduma muhimu, ikiwemo chakula. Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda, kisa cha mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili, ni katika harakati zake za

Vigogo sita wa CCM waliohojiwa na kamati ya maadili ya chama hicho wapewa adhabu ya ONYO KALI

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kati ya tarehe 13/02/2014  na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama. Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013. Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni

Mheshimiwa Pandu Amir Kificho ashinda nafasi ya Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba

$
0
0
Spika wa Bunge la Wawakilishi Zanzibar na Mbunge wa Bunge maalum la Katiba, Pandu Amir Kificho  amechaguliwa na wajumbe wa Bunge hilo kuwa Mwenyekiti wa muda.    Kutokana na ushindi huo Kificho sasa atakuwa na kazi  kuandaa kanuni ambazo zitatumika kwa ajili ya kumchagua mwenyekiti wa kudumu wa bunge hilo na kusimamia vikao vyake.   Muda wa mwenyekiti

Habari njema kwa akina dada: Mchumba mwaminifu anahitajika haraka sana. Vigezo na masharti ya huyo muoaji, bofya hapa

$
0
0
   Mimi ni kijana wa kitanzania ambaye nimekulia katika maadili ya kidini na malezi mazuri ya kifamia, napenda nichukue fursa hii nitangaze nafasi ya mchumba ambaye kama ata kidhi vigezo vyangu atakuwa ndio mke wangu wa ndoa. Kifupi mi ni mtaalam wa IT naishi Dar es salaam.Mchumba ninaye mtaka ni vema awe amekulia malezi ya kidini kwa sababu mimi ni mcha Mungu na napenda kusali kwa hiyo napenda

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Jumbe Mangu aongoza mkutano mkuu wa maafisa wakuu wa jeshi la polisi mjini Moshi leo

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Jumbe Mangu akisisitiza jambo kwenye mkutano Mkuu wa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika Chuo cha Taluma ya Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mkutano huo umebebwa na kauli mbiu isemayo “Zingatia Weledi katika Kutoa Huduma Bora Kwa Jamii”. Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Paul Chagonja
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images