Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Musukuma awavaa Chadema, asema hawana ubavu wa kumfukuza Lowassa

0
0
Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma amesema kwamba viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanapiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Lowassa kwenda Ikulu lakini hawana mabavu ya kumfukuza uanachama kwani yeye ndiye mwenye chama.

Msukuma amedai kwamba, Mbowe ambaye anaaminiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA tayari alikwishauza chama kwa Lowassa muda mrefu ndiyo maana hana sauti ya kumuwajibisha.

Aidha Msukuma hajaishia hapo ambapo pia amemtaka Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho aoneshe nguvu yake ndani ya chama kwa kumwambia Lowassa aombe radhi  na siyo waombane wao kwa wao kwani kutakuwa ni kuwapumbaza wanachama na wafusi wao bali hadharani watu waone.

"Lowassa ndiye mwenye Chama. Wewe mbowe uliuza chama sasa wewe kama msemaji toa kauli ya kumfukuza chama Lowassa. Tunashangaa kuanza kuchafuliwa kwa mtu ambaye mlituaminisha kuwa anafaa kuwa Rais. Muite Lowassa umhoji mitandaoni tuone akikuomba radhi. Na hata akikuomba radhi sasa hivi tutajua siyo kwa mapenzi yake," Msukuma.

Ameongeza kuwa, "Mbowe kusema kuwa Lowassa alikurupuka ni kumkosea adabu kwanza, Lowassa ni mtu mzima kwake na yeye bado ni kijana. Na  ninaamini kwamba wewe Mbowe Lowassa hakuombi msamaha kwa kuwa yeye ndiye mmiliki".

DAWASCO yakubali kulipa fidia Nyumba Iliyoungua Moto

0
0
Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Dar es salaam DAWASCO imesema itamlipa fidia mmiliki wa nyumba iliyoungua moto jana maeneo ya Buguruni kutokana na moto uliosababishwa na shughuli za mamlaka hiyo.

Akiongea  kwenye eneo la tukio Mkurugenzi mtendaji wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema ofisi yake inaongea na mmiliki huyo ili kuona namna ya kumlipa kutokana na uharibifu uliotokea.

''Tunaongea naye kuona jinsi gani tutamlipa fidia kwa uharibifu huu uliotokea  ili aweze kuendelea na maisha yake na familia kama kawaida'', amesema Luhemeja.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala Salum Hamduni amesema zoezi la kuziba bomba la gesi la Songasi ambalo liliungua juzi  usiku limefanikiwa na hali kwa sasa ni shwari baada ya kufanikiwa kuziba 'valve' zilizopasuka.

Tukio hilo la moto lilitokea juzi jioni katika eneo hilo la Buguruni Mnyamani baada ya mafundi wa DAWASCO kupasua kwa bahati mbaya bomba la gesi la Songasi ambalo lilisababisha kulipuka kwa moto huo.

Wanaovaa Nusu UCHI Arusha Waanza Kushughuliwa

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo ametangaza rasmi kuanza oparesheni ya kukamata watu wanaovaa nguo zisizo na heshima kulingana na maadili ya Tanzania na kuwafikisha mahakamani.

Mkumbo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya Usalama  kwa mwaka jana.

”Hizi nguo hazipendezi na si maadili  yetu, mnaiga wenzenu wanaovaa kwa sababu ya hali ya hewa ya kwao sasa tunatangaza kuanza msako mwaka huu na tutakayemkamata tunamchukua hivyo hivyo hadi mahakamani bila kumpa nguo ya kujifunika ili ndugu zake wamuone’’. Amesema Mkumbo.

Mkumbo amefikia uamuzi huo kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na ulawiti tofauti na matukio mengine ambayo yamepungua kutoka na jitihada za jeshi la polisi.

Ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka 2016 matukio ya ubakaji yalikuwa 144 huku mwaka 2017 yameongezeka na kuwa 149, wakati matukio ya ulawiti kwa mwaka 2016 ni 58 na kuongezeka kwa mwaka 2017 na kuwa 62.

Hata hivyo amesema kuwa sababu kubwa ya kuongezeka kwa matukio hayo ni kutokana na mila potofu, imani za waganga wa kienjeji na ukosefu wa elimu.

Aidha amewataka watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa makosa  hayo hayafai na yana adhabu kubwa ya kifungo cha miaka 30 au cha maisha.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

0
0
MAMBO MAPYA 2018
  Ktk kusajiliwa kwa kampuni ya  @natural_beauty_prod
Kwanza tunawatakia kheri ya mwaka mpya kwa wote. Pia tunakukalibisha tena kwenye kampuni yetu yenye bidhaa mpya zilizoingia kuanzia tar 01/01/2018. 

     Bidhaa hizi MPYA zimefanyiwa maboresho makubwa zaidi hivyo zina matokeo ya haraka kuliko ilivyokuwa awali.
  NI PAMOJA NA  HIZI👇🏼
☆Kutengeneza shepu (hips, makalio na mapaj) @200,000/=
☆Kurefusha nywele @130,000/=
☆Kuongeza urefu na upana wa uume @200,000/=
☆Kung'arisha mwili mzima na kuondoa sugu @150,000/=
☆Kupunguza unene na manyama uzembe @180,000/=
☆Kuongeza nguvu za kiume  hata kwa mwenye kisukari (diabetic) @180,000/=
☆Kuondoa mvi moja kwa moja na zisiludi tena milele @150,000/=
☆Kuongeza unene, uzito na hamu ya kula @150,000/=
☆Kutengeneza miguu (Chupa ya bia) na kuondoa kigimbi @150,000/=
☆Kubana uke na kuondoa uchafu @150,000/=
☆Kuongeza au Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @140,000/=
☆Kuondoa michirizi ya uzazi  au unene @130,000/=
N.K
     Bidhaa hizi zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda. Hazina kemikali wala madhara kwa mtumiaji.
    NB: MATOKEO NI UHAKIKA NA GARANTII NA HAKIKISHA UNAPATA RISITI YENYE MUHURI HALISI WA NATURAL BEAUTY
 
    Wasiliana nasi kwa no
         (+255) 0759029968
                0659618585
  Popote ulipo utapata huduma
   Follow us on
GOOGLE👉 natural beauty
INSTAGRAM@natural_beauty_pr
YOU TUBE 👉natural beauty
         <<WELCOME ALL>>

Watano washikiliwa sakata la kuunganisha bomba la mafuta

0
0
Jeshi la Polisi limewakamata watu watano, akiwemo mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kisiwani Kigamboni, Lebeka Nganji kwa kujihusisha na uuzaji wa mafuta ya dizeli yanayosadikiwa yalitoka katika bomba lililounganishwa kwa wizi.

Inadaiwa kuwa bomba hilo liliunganishwa na Samwel Kilanglani (63), ambaye nyumba yake iko umbali wa takribani mita 20 kutoka lilipo bomba kuu la mafuta la Tanzania na Zambia (Tazama).

Kilanglani anadaiwa kujichotea mafuta kutoka katika bomba hilo alilolipitisha chini ya ardhi.

Imedaiwa kwamba mfanyakazi huyo mstaaafu wa Tazama alianza kutoboa bomba la kwanza na kukuta lina mafuta ghafi na kuliziba, kisha kutoboa jingine lililokuwa na dizeli na kujiunganishia hadi nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Bariki Dickson, Christon Kapinga na Farhan Ahmed ambao wote wanaishi Kigamboni.

Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na Kilanglani kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuwataja wenzake ambao huchukua na kuuza mafuta hayo.

“Huyu mtuhumiwa alisema hayupo peke yake hivyo ana wenzake wanashirikiana dili hilo, ndiyo akawataja hao wanne akiwemo mwalimu wa Shule ya Msingi Kisiwani,” alisema.

“Tuliwakamata watuhumiwa sehemu mbalimbali za Kigamboni ambao wote wanafanya dili hilo la kunyonya na kuuza mafuta ya dizeli kutoka kwenye bomba kuu,” alisema Kitalika.

Juzi mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa alieleza kuwa Kilanglani alibainika baada ya mafuta yaliyokuwa yanavuja kuanza kusambaa barabarani.

Mgandilwa alisema Januari 6, walipelekewa taarifa kuwa mafuta yamesambaa kwenye njia ya mabomba ya Tazama yanayopita Tungi, Kigamboni.

Alisema baada ya kupewa taarifa hizo walienda hadi eneo hilo na kuamua kuchimba ili kubaini tatizo.

“Awali tulihisi bomba kubwa limepasuka. Tuliamua kuchimba ili kuyakabili mafuta yasiweze tena kuvuja na kuwasababishia athari wananchi,” alisema.

Alisema wakati wakiendelea na kazi hiyo, walikuta mabomba makubwa matatu ya mafuta, mawili yalikuwa yametobolewa; moja likipitisha mafuta ghafi ambalo lilionekana kuwa limezibwa.

“Bomba jingine ambalo lilikuwa la mafuta ya dizeli lilikuwa limeunganishwa kwa chini ya bomba jingine dogo kwa kutumia koki, tulivyofuatilia tukabaini limeelekea nyumbani kwa Kilanglani,” alisema.

“Huyu mtuhumiwa ni mtaalamu sana. Mtu  wa kawaida hawezi kuunganisha chini kwa chini, ndiyo maana alipogundua bomba la kwanza linatoa mafuta machafu akaziba na kutoboa jingine lililokuwa na mafuta ya dizeli.

“Mafuta yanaposhushwa kwenye meli hupita katika mabomba kwa kusukumwa na mashine kuelekea kituo cha kuhifadhia cha Tazama. Mabomba hayo yamepita karibu na nyumba yake.”

Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata kuwa Balozi

0
0
Rais John Magufuli ameteua mabalozi wapya wawili ambao ni Alphayo Kidata na Meja Jenerali Mstaafu, Simoni Mumwi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa Kidata umeanza jana Jumatano Januari 10.

Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vyao vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.

BREAKING NEWS | Bavicha wanazungumza na waandishi wa habari ......Nini kinajili? Bofya Hapa

0
0
Bavicha wanazungumza na waandishi wa habari nini kinajili?...Tazama Hapo Chini

Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne

0
0
Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne
 
Kutana Maajabu ya Mtabibu MAALIM MOHAMEDI MASUDI Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..
MAALIM MOHAMEDI MASUDI ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
 
Je unasumbulia na Mapenzi..?
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na MAALIM MOHAMEDI MASUDI Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
Wasiliana na MAALIM MOHAMEDI MASUDI Kwa Majibu ya Maswali yako..

Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA.

Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.
Wasiliana nae kwa namba
0655516982
0688856265
0621898709(Whatsapp)

BREAKING: Lowassa Akutana na Freeman Mbowe Kumpa Mrejesho wa Ikulu

0
0
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amekutana na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho wa alichozungumza na Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na waraka na taarifa nyingi za kupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.

“Taarifa zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh Lowassa. Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na mwenyekiti wa chama chake, Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.”

“Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki , taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala wao,”

“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”

============================

Bavicha Washtushwa na Lowassa Kwenda Ikulu

0
0
Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limesema limeshtushwa na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa kumpongeza Rais John Magufuli.

Akizungumza leo Alhamisi Januari 11, Katibu wa Bavicha, Julius Mwita amehoji Lowassa anapata wapi ujasiri wa kumpongeza Rais wakati nchi inakabiliwa na matukio mengi ya uvunjaji wa haki za binadamu.

"Unampongezaje Magufuli wakati serikali yake bado haijatoa tamko lolote tangu Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alivyopigwa risasi," amesema.

"Unampongeza vipi Magufuli wakati serikali yake imezuia mikutano ya vyama vya siasa."

Mwita amesema kitendo cha Lowassa kumpongeza Rais Magufuli kimewasikitisha hasa kutokana na mazingira ya kisiasa yalivyo hapa nchini.

"Vyama vya upinzani vina malalamiko mengi hatukutegemea kiongozi kusimama na kumpongeza mtu anayevikwamisha vyama vya siasa," amesema.

TCRA Yamtosa Mrema Sakata la Kuzushiwa Kifo

0
0
Baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini, Mh. Agustino Lyatonga Mrema kusema anaenda kufungua kesi ya madai ya mabilioni ya shilingi TCRA  kwa watu waliomzushia taarifa za kifo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imemuelekeza kiongozi huyo  kuanzia kituo cha polisi kabla ya kufika kwenye ngazi hiyo.

Akizungumza baada ya Mrema kuwasilisha malalamiko yake katika Mamlaka hiyo Naibu Mkurugenzi - Huduma za Bidhaa na Mawasiliano  Bw. Tadayo Joseph amesema kuwa Kabla ya Mrema kufika katika mamlaka hiyo alitakiwa kuanzia ndani ya jeshi la polisi kwani malalamiko hayo yanahusu kosa la jinai.

"Mzee Mrema na wananchi wengine wanaoleta taarifa za malalmiko  tunawapongeza kwa hatua hiyo. Suala ambalo alilileta ni linahusu kosa la jinai. Mamlaka hii na jeshi la polisi zinafanya kazi kwa ukaribu sana. Ameshauriwa kwanza akaripoti huko kisha atapatiwa wapelelezi kabla ya kufika kwenye mamlaka hii,".

Mrema ambaye alizushiwa kifo na watu wasofahamika siku ya Jumanne, aliahidi jana kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kwamba  angekwenda  kufungua kesi TCRA na kisha kudai Bilioni 20  kutokana na matatizo pamoja na usumbufu uliosababishwa na mzushaji wa taarifa hizo.

Mbali na hayo  Mheshimiwa Mrema jana alisema  alisema kitendo cha kuzushiwa kifo kilimsaidia kujua ni watu gani wanampenda kweli na kina nani hawampendi, kutokana na reaction zao baada ya taarifa feki za kifo chake.

BAVICHA Wamshambulia Kwa Maneno Katibu Mkuu UVCCM Baada ya Kudai Tundu Lissu ni Muongo na Anatafuta Umaarufu

0
0

Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Julius Mwita amefunguka na kusema kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka huenda ana matatizo ya akili.

Mwita amesema hayo leo Januari 11, 2018 katika Mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu tuhuma alizotoa kiongozi huyo wa UVCCM dhidi ya Tundu Lissu ambapo alisema kuwa Tundu Lissu ni muongo na hapaswi kuaminiwa kwani atafuta tu umaarufu.

Kufuatia kauli hiyo ya Shaka ndipo hapo viongozi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA walipoaamua kujitokeza na kuzungumzia juu ya kauli hizo za kijana wa CCM na kusema kuwa;

 "Tumetafakari kauli ya Shaka kwa kina na tumejaribu kufikiri kama Shaka ana akili timamu au ni kichaa? Kwa sababu kama chama chake chenyewe wamekiri pamoja na Serikali hawawezi kuzungumza suala la Lissu kwa sababu ni mgonjwa na yupo hospitali, Shaka anapata wapi ujasiri wa kuja kuzungumza mambo yanayomuhusu Tundu Lissu tena kwa kuzungumza mambo ya uongo na ushahidi usio na tija yoyote na anawadanganya Watanzania kuwa katika nchi hii Lissu siyo wa kwanza kupigwa risasi" alisema Mwita

Aidha kiongozi huyo wa BAVICHA amemtaka Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka alisimame na kusema mpaka sasa Tundu Lissu ametibiwa kwa fedha ya Serikali shilingi ngapi.

"Tulitegemea umoja wa vijana wa chama ambacho kinaendesha Serikali watoke wawaambie Watanzania kwamba tunakitaka chama chetu yaani kiiagize Serikali kutibu mgonjwa ambaye yupo hospitali na ameshambuliwa katika majukumu yake ya Ubunge lakini Shaka anatoka kupotosha kwa maneno ya kejeli na ya kihuni. 

"Lakini tumkumbushe Shaka, Amani Abed Karume hakuuawa kwa sababu za kisiasa na wala hajawahi kuwa mpinzani, wala hajawahi kuwa mkosoaji wa Serikali iliyopo madarakani kwa wakati huo useme kwamba alishambuliwa kwa sababu ya ukosoaji wake bali kulikuwa na sababu zingine tofauti zilizopelekea Karume kushambuliwa"

Siku kadhaa zilizopita Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alifunguka na kuishtumu Serikali ya awamu ya tano kuhusika katika kushambuliwa kwake baada ya kali hiyo Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka naye amlijibu Tundu Lissu na kusema kuwa mwanasiasa huyo ni muongo na anatafuta umaarufu.

Video: Kibao kipya cha Barnaba ft Aslay ”Ngoma”

0
0
Barnaba ameachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha msanii toka kundi la ya moto band lililovunjika tangu mwaka jana, dogo Aslay ambaye amekuwa tishio kwa wanamuziki kwa kutoa nyimbo nyingi, kali na nzuri zinazotamba mtaa kwa mtaa.

Wimbo huo umechezwa katika mazingira ya kijijini huku mpendezesha video akiwa mwanadada maarufu Tunda.

Tazama video hiyo hapo chini

Ofisa Ardhi Mwanza na Wenzake Watiwa Mbaroni Kwa Utapeli wa Viwanja

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu sita akiwemo Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Ilemela, Alex Nyabange (30), kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utapeli wa viwanja, kutengeneza vyeti bandia vya kitaaluma pamoja namba za mlipa kodi za (TIN), za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Alhamisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kati ya Desemba 30, 2017 na Janauari 9 mwaka huu.

Msangi aliwataja waliokamatwa kwa tuhuma za kuwatapeli watu kwa madai ya kuwauzia viwanja kuwa ni Aloyce Nyabange (30) ambaye ni ofisa Ardhi wa  Manispaa ya Ilemela, Alex Josephat(41) ambaye ni mfanyabishara, Juma Malulu (60) mkazi wa mta wa Ilemela.

Wengini ni Katibu Mhatasi wa kampuni ya Nyambale Civil Works, Getruda Peter (42) mkazi wa Nyegezi na mchora ramani Deodatus Bety (51) mkazi wa Usagara ambao wote walikamatwa Desemba 30, 2017 kwa nyakati tofauti.

“Tulipata taarifa hizi baada ya mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Barnabasi Ibengo (39) mfanyabishara wa Kiseke kuwa ametapeliwa na watu waliosema wana viwanja viwili eneo la Nyasaka na kwamba vinahitaji Sh45 milioni, lakini akawa ametanguliza Sh10 milioni akiamini kuwa ni ukweli kutokana na nyaraka zote walizomuonyesha,” amesema Msangi.

Hata hivyo Msagi amesema mfanyabishara huyo, aligundua kuwa ametapeliwa baada ya kwenda eneo vilipo viwanja hivyo na kuonana na mwenyekiti wa mtaa huo na kuaambiwa hakuna jambo la namna hiyo ndipo alitoa taarifa polisi na kuanza kufuatilia kukamatwa mmoja baada ya mwingine.

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na komputa inayotumika kutengenezea nyaraka mbalimbali na baadhi ya nyaraka zinazoonyesha viwanja kwa ajili ya kuuzwa.

Kuhusu vyeti feki Kamanda Msangi amesema walimkamata Evancy Wilson (33) katika mtaa wa Buzuruga Ilemela akiwa na vifaa vya kughushi vyeti vya taaluma mbalimbali.

Amesema tukio hilo lilitokea Janauri 9, mwaka huu saa 11:00 jioni ambapo mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuchunguzwa kwenye kompyuta yake walikuta namba inayofanana na TIN ya TRA na vyeti hivyo vya taaluma vya kughushi.

Amesema walikuta vyeti vya kughushi vya, stashahada, shahada, vyeti, vitambulisho vya mpigakura, nyaraka zinazoonyesha kuwa ni za kuombea mikopo benki, leseni za biashara na flash ambazo zimejazwa vitu hivyo.

“Hili lilitokana na taarifa tulizopata kutoka kwa raia wema kuhusu kuwapo kwa mtu anayetenegeza vitu hivyo ndipo tulianza kufuataili, watuhumiwa wote wapo polisi, upelelezi ukikamilika tutawafakisha mahakamani.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya January 12


Serikali Yakiri Kuingizwa Mkenge Ubinafsishaji TTCL.....Dr Mpango Akabidhi Ripoti ya Uchunguzi Kwa Rais Magufuli

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango jana tarehe 11 Januari, 2018 amewasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo tarehe 20 Desemba, 2017.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Mpango amesema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.

Kufuatia ukiukwaji huo Dkt. Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake.

“Lakini niwaambie Watanzania yale ambayo tumeyaona ni machafu sana, ni mambo ya hovyo kabisa, nchi yetu kwa kifupi tuliingizwa mkenge, ni fedha nyingi zimepotea kwa hiyo sisi katika majadiliano haya lengo letu litakuwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata haki yao” amesema Dkt. Mpango.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amepokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa tarehe 25 Novemba, 2017 wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi  (Mloganzila) kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Baadhi ya maagizo hayo ni kupunguza baadhi ya idara na madaktari katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kuhamishia Mloganzila na hospitali za mikoa kuhamishwa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mhe. Ummy Mwalimu amewasilisha taarifa hiyo akiwa ameongozana na  viongozi wakuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKHI), Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (MUHAS).

Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amekamilisha kanuni za sheria ya madini namba 7 ya mwaka 2017 na kuwasilisha vitabu vya kanuni hizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Akiwa na Naibu Mawaziri wa Madini Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo na Mhe. Doto Mashaka Biteko, Prof. Kabudi amesema kanuni hizo zimekamilika siku moja kabla ya tarehe ya mwisho iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli na kubainisha kuwa sasa sheria inaweza kuanza kutumika.

Kwa upande wao Naibu Mawaziri wa Madini wamewataka Watanzania na wadau wote wa sekta ya madini kushirikiana na Serikali kutekeleza sheria hiyo na wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msukumo wa kukamilishwa kwa kanuni hizo.

Wizara Ya Maliasili Na Utalii Yatangaza Rasmi Viwango Vipya Vya Ada Kwa Mawakala Wa Kusafirisha Watalii Nchini

0
0
Na Hamza Temba-WMU-Dar es Salaam
.......................................................................
Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza rasmi viwango vipya vya malipo ya ada kwa Mawakala wa kusafirisha watalii nchini baada ya kukamilika kwa marekebisho ya kanuni ya ada na tozo za biashara ya utalii yaliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana, 2017.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, imeeleza kuwa baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo ya kanuni, Tangazo la Serikali namba 506 la tarehe 29 Desemba, 2017, limeweka viwango vipya vya ada kwa mawakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters).

Taarifa hiyo imeeleza viwango hivyo kuwa ni shilingi sawa na dola za Kimarekani 500 kwa kampuni za wazawa zenye umiliki mkubwa wa raia wa Tanzania na zinazomiliki gari 1 hadi 3.

"Shilingi sawa na dola za Kimarekani 2,000 kwa kampuni zenye gari 4 hadi 10, shilingi sawa na dola za Kimarekani 3,000 kwa kampuni zenye gari 11 hadi 50 na shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000 kwa kampuni zenye kumiliki gari 51 na kuendelea", imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa kampuni za kigeni zenye umiliki mkubwa wa raia wa kigeni na zinazomiliki gari 10 hadi 30 zitalipa ada ya shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000, kampuni zenye gari 31 hadi 50 zitalipa shilingi sawa na dola za kimarekani 7,500 na na kampuni zenye gari 51 na kuendelea zitalipa shilingi sawa na dola  za Kimarekani 10,000.

Kufuatia marekebisho hayo, muda wa kutumika kwa leseni za mwaka 2017 za Wakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters) umesogezwa mbele hadi tarehe 31 Januari, 2018 ili kuwezesha maandalizi ya kuingia kwenye mabadiliko ya viwango hivyo vipya.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa  maombi ya usajili na leseni za biashara ya utalii na leseni za waongoza watalii kwa mwaka 2018  kwa wafanyabiashara wapya na wanaoendelea na biashara yanaendelea kupokelewa.

Waombaji wote wametakiwa kufuata masharti ya uombaji wa leseni hizo ikiwemo kuwasilisha nakala za hati za usajili wa magari zilizothibitishwa kisheria kwa Wakala wa kusafirisha watalii (wapya na wanaoendelea na biashara) na kivuli cha leseni ya mwaka 2017 kwa wafanyabiasbara wote.

"Ni kosa kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa leseni", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Desemba 10 na 11 mwaka 2017, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alikutana na wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha kwa lengo la kuwashirikisha katika mapendekezo ya viwango vipya vya ada kwa Wakala wa kusafirisha watalii ambavyo vilivyotolewa na Wizara yake.  Mapendekezo ya viwango hivyo yalilenga kuongeza mapato na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wenye gari kuanzia moja kuingia katika biashara hiyo.

Kheri James: Rais Magufuli Ameamua Kusafisha Nyumba Hakuna Mende Atakayebaki

0
0
 Na Mathias Canal, Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu utendaji wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi ya watanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa ziarani Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.

Kheri alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameamua kusafisha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu yeyote kusalia kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa maslahi ya Taifa.

Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka 2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.

Alisema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua Kali za kisheria dhidi ya yeyote atakayetaka kuvuruga ama kuleta uvunjifu wa amani Siku ya uchaguzi.

"Ndugu zangu wana Mrandarara nataka niwasihi na kuwahakikishia kuwa MTU yeyote atakayeleta masihara na mchezo mchezo Siku ya uchaguzi anapaswa kuchezewa yeye mchezo mpaka ashike adabu" Alikaririwa Kheri

Alisema kuwa Mara baada ya Mbunge kuchaguliwa tu anapaswa kusimamia vyema asilimia 5% za fedha za mfuko wa vijana zinazotolewa na Halmashauri sambamba na asilimia 5% kwa ajili ya wanawake ili kuendeleza chachu na imani ya vijana na wananchi kwa ujumla dhidi ya serikali yao.

Aliongeza kuwa kumchagua mbunge wa CCM itampendeza zaidi Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Magufuli kwani atakuwa amepata msaidizi kwa ngazi ya Jimbo atakayetekeleza vyema ilani ya CCM ambayo imeainisha mambo mengi muhimu na msingi kwa maslahi ya watanzania wote hasa wananchi wa Longido.

Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Longido na majimbo mengine matatu likiwemo Jimbo la Singida Kaskazini na Songea Mjini utafanyika tarehe 13 Januari 2018.

Wakati huo huo akiwa Kijijini Mairowa Kata ya Ngarenaibor Mwenyekiti Kheri amewataka mawakala wa CCM kote nchini kuwa waaminifu katika kusimamia vyema chaguzi mbalimbali kote nchini kwani wameaminiwa na Chama hivyo kutojihusisha na viashiria vya aina yoyote ya rushwa.

TANESCO Yatoa Siku Nne (4) Kwa Wadaiwa Sugu Wa Bili Za Umeme Wawe Wamelipa, Vinginevyo Huduma Zinasitishwa

0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.


Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.


Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.


mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

Mafuriko Yaleta Maafa Dodoma

0
0
Na Canal- Wazohuru
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha mafuriko na adhari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara.

Athari za mvua hizo zimejitokeza katika vijiji vya Olboloti,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuwa ndio vimeathiriwa zaidi na mafuriko hayo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji cha Olboloti  Abdalah Suti amesema kuwa mvua iliyonyesha katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960

Amiry Issa ni Mkuu wa zimamoto kituo cha Dodoma amesema kuwa kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka wananchi kutosogelea maeneo hatarishi

Akizungumzia hilo,Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, Simon Odunga amesema kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na milima huku akiwataka wananchi waliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images