Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbaroni kwa kutapeli fedha za Rais

$
0
0
Kijana mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamedy Msangi (28) mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa jambo hilo na kusema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa na askari walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya kosa hilo kwa kuomba mkopo katika taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Matei amedai kuwa kijana huyo alipoomba mkopo huo aliorodhesha majina ya vijana wengine wanne akijifanya kuwa vijana hao wamejiunga kwenye kikundi hicho kisha kupatiwa mkopo huku hao vijana aliowaorodhesha wakiwa hawana taarifa yoyote.

Mbali na hilo Kamanda Matei alitoa rai kwa wananchi wa Morogoro na kuwataka wananchi kuacha wizi "Tuache huu wizi kwa kutumia vyombo vinavyotoa mikopo kwani mikopo hii imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa chini na hilo ndiyo lengo la Serikali kuwaondolea watu umasikini ili waweze kufungua viwanda vidogo vidogo na kujipatia kipato, lakini wapo watu wanatumia vibaya vikundi hivi" alisema  Matei

Meneja TBA Kigoma akamatwa

$
0
0
Jeshi la polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari Kigoma.

Meneja huyo alikamatwa akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana.

Mhandisi Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika

Prof. Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea. Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo.

Orodha ya wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo watakaosakwa kuanzia Januari 8

$
0
0

Orodha ya wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo watakaosakwa kuanzia Januari 8

Viwanda Vitano vya Samaki Vyapigwa Faini ya Milioni 180 na Wanakiwa Kuilipa Ndani ya Masaa 24

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewaamuru wamiliki wa viwanda vitano vya kuchakata minofu ya samaki vilivyoko jijini Mwanza kulipa faini ya shilingi milioni 180 ndani ya saa 24 baada ya kubainika kupokea na kuchakata samaki wasioruhusiwa kwa kukiuka Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009  sambamba na Sheria ya usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004

Pia Waziri Mpina amechukizwa na kitendo cha viwanda hivyo kufadhili uvuvi haramu na kueleza kuwa ni bora kutokuwa na kiwanda hata kimoja cha samaki kuliko kuendelea kuwa na viwanda vinavyofadhili uvuvi haramu na kutishia kuvifunga viwanda vyote sambamba na kutaifisha samaki, magari na boti zinazobeba samaki wasioruhusiwa.

Waziri Mpina amesema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara kutembelea viwanda vinavyochakata samaki jijini Mwanza ambapo pia alimuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.  Yohana Budeba kuwasimamisha kazi maofisa watatu wa Kitengo cha Udhibiti wa Usalama na Ubora wa Mazao ya Uvuvi Kituo cha Mwanza kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kulisababishia Taifa hasara kubwa.

Maofisa hao ambao Waziri Mpina ameagiza wasimamishwe kazi na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ni pamoja na Philemon Mugabo,Dorina Mlenge na John Bosco Rubajuna

Waziri Mpina ametaja viwanda vilivyokutwa vikichakata samaki wasioruhusiwa wakiwemo samaki wazazi na samaki wachanga  na idadi ya kilo zilizokamatwa kwenye mabano kuwa ni pamoja na Nile Perch Fish (920), Victoria Fish (131), Nature Fish (150), Omega Fish (580), Tanzania Fish Processing (842) huku magari 41, boti 15, Nyavu haramu 294 wakiwa na samaki wachanga na wazazi ambapo sheria inakataza kuvuliwa samaki chini sentimita  50 na juu ya sentimita 85 .

Majina ya viwanda hivyo na faini zao walizotozwa Nile Perch sh milioni 25, Tanzania Fish Processing sh. milioni 50, Victoria Perch Milioni 30, Nature Fish milioni 25, Omega Fish Ltd milioni 50 ambapo amesisitiza kuwa adhabu hiyo ni ya kwanza na ya mwisho na kwamba ikithibika tena wenye viwanda waendelea kufadhili uvuvi haramu hatua za kuvifunga viwanda na kutaifisha mali ikiwemo mitumbwi, boti na magari yatakayokuwa yanabeba samaki hao itafuata.

Waziri Mpina amesema ukanda wa Ziwa Victoria ulikuwa na Viwanda 13 vya kuchakata samaki vilivyokuwa na uwezo wa kuchakata tani 1,065 kwa siku lakini kutokana na kushamiri kwa uvuvi usiongatia sheria kumesababisha viwanda 5 kufa kutokana na kukosekana malighafi na kwamba viwanda 8 vilivyobaki sasa vinachakata tani 171 tu kwa siku huku ajira zikiwa zimeporomoka kutoka ajira 4, 088 na kufikia 2,179 tu.

Mpina amesema tayari Rais Dk John Magufuli ameshatoa maagizo kwa wavuvi kuachana na uvuvi haramu sambamba na wenye viwanda kutofadhili uvuvi huo huku pia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye akisisitiza jambo hilo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikikemea vikali huku Sheria za nchi nazo zikikataza  jambo hilo lakini wenye viwanda kwa makusudi wameamua kudharau maagizo ya viongozi wakuu wa nchi jambo ambalo Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya uongozi wake Waziri Mpina haliwezi kukubalika kamwe.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dk. Yohana Budeba amesema kama watumishi wa wizara yake wangesimamia majukumu yao kikamilifu mambo hayo aliyobaini Waziri Mpina yasingejitokeza huku akikiri kupokea maagizo yake yote na atayasimamia kwa haraka kuona yanatekelezwa.

Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC), Mhandisi Boniphace Guni amesema wenye viwanda hivyo wamekutwa na makosa ya kupatikana na samaki waliochini wa ukubwa, kukutwa na samaki wachanga kinyume cha Sheria ya Usimamizi Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 ambapo wamekiuka kifungu namba 58(I)(a)  hivyo wamestahili adhabu hiyo ya kulipa faini ya milioni 180 ndani ya saa 24  
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akimbeba samaki aina ya sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu alipokuwa katika ukaguzi wa mazao ya uvuvi katika Kiwanda cha Nature Fisheries Limited Jijini Mwanza, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Yohana Budeba na kulia ni Afisa Uvuvi Mkuu Bw. Boniface Shatila.
Samaki mzazi aina ya Sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu(alikuwa na urefu wa sentimita 120), samaki ambaye akiachwa ziwani kwa muda  wa miezi mitatu ana uwezo wa kuzaa samaki milioni tatu, na kuongeza idadi kubwa ya jamii
hiyo ya samaki katika ziwa Victoria.

Samaki chini ya sentimita 50 na mwenye zaidi ya sentimita 85 hawaruhusiwi kisheria kuvuliwa.

Baba Amuua Mwanae Kwa Kumpiga Mateke Akidai Mkewe Alimbambika

$
0
0
Watu  wawili wameuawa wilayani Kalambo mkoani Rukwa katika matukio tofauti, likiwamo la mtoto kuuawa kwa kupigwa ngumi na mateke tumboni na baba yake.

Katika tukio la kwanza lililotokea Januari 1 saa 4 usiku, mtoto Benedicto Salumu (13), mkazi wa Kitongoji cha Saint Maria Kata ya Matai wilayani humo, inadaiwa alipigwa na baba yake hadi kufa baada ya ugomvi kuzuka kati ya mama na baba wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Rafael Sinyangwe, kwa muda mrefu kumekuwapo ugomvi baina ya baba wa mtoto, Pius Salum (46) na mkewe, Hilda Mpangamila (37), akimtuhumu mkewe kuwa mtoto huyo si wa kwake.

Mwenyekiti huyo alisema Salum mara kadhaa amekuwa akiwalalamikia ndugu zake kuwa mkewe alibeba ujauzito wa mtoto huyo wakati akiwa amekwenda kutafuta maisha na aliporudi alihisi mkewe ni mjamzito.

Sinyangwe aliongeza kuwa tofauti hizo zilisababisha mvutano mkubwa wa mara kwa mara kati ya wanandoa hao.

Mwenyekiti Sinyangwe alidai siku ya tukio hilo mtuhumiwa akiwa ametoka kusherehekea Mwaka Mpya, aliingia chumbani na kukuta mtoto huyo akiwa amelala kisha kuanza kumpiga na ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo tumboni hadi kusababisha kifo chake.

Aliendelea kudai kuwa baada ya kumua, alimpiga pia mke wake akidai amemsababishia kulea mtoto asiyekuwa wake kwa muda mrefu, hali mbayo ilikuwa ikimuudhi na kumkosesha amani.

Katika tukio jingine lililotokea Januari 1 majira ya jioni, mkazi wa Kijiji cha Kafukoka kata ya Kisumba wilayani Kalambo mkoani Rukwa Kalasto Katanti (40) aliuawa na ndugu zake baada ya kipigo kikali wakidai kuchukizwa na madeni aliyonayo.

Kabla ya kuuawa kwa kipigo Katanti alikuwa anadaiwa shilingi 64,000, deni ambalo lilikuwa ni la muda mrefu kiasi ambacho alionekana ameshindwa kulilipa.

Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Frank Sichalwe, alisema ndugu zake wawili ambao ni Florens Zunda (38) na Dafusi Zunda (35) ndipo walipoamua kumpiga hadi kumuua wakidai wamechoshwa na tabia yake ya kukopa fedha wakati anajua hana uwezo wa kulipa, kitendo kinachodhalilisha ukoo wao.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na Kuongeza kuwa watuhumiwa wanashikiliwa na polisi na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0

🎁OFFER SPECIAL MWAKA MPYA🎁
    PENDEZA SASA KWA PUNGUZO KUBWA LA BEI. 
       KATIKA KUSHEREHEKEA MSIMU WA SIKUKUU  @natural2162 TUNA  PUNGUZO LA 20% KWA BIDHAA ZETU ZOTE, IKIWA NI SHUKRANI KWA KUTUUNGA MKONO.

        BIDHAA ZETU ZOTE ZIMETENGENEZWA KWA MIMEA NA MATUNDA HAZINA KEMIKALI WALA MADHARA.
    KWA WANAUME TUNATIBU👇👇
☆Kukosa hamu ya tendo.
☆Kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo.
☆Maumbile madogo ya uume.
☆Kuchoka sana wakati wa tendo na uume kusinyaa  nk.
      @natural2162 tumeandaa tiba bora kabisa kama ifuatavyo:-
 
1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @220,000/=
2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @130,000/=
3VigRX  CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @170,000/=
4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @140,000/=
5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @220,000/=
6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @140,000/= 
 
     PIA KWA WANAWAKE WANAOPENDA KUWA NA MUONEKANO MZURI ZIPO ZA👇👇👇
1.Kuongeza hips, makalio na mapaja @180,000/=
2.Kushepu mguu (CHUPA YA BIA) @130,000/=
3.Kuwa mweupe bila sugu kwa:-
(a)mafuta @130,000/=
(b) Vidonge @150,000
4.Kurefusha nywele na kutokukatika ovyo @130,000/=
5.Kuongeza hips, makalio na mapaja kwa vidonge (YODI PILLS ORIGINAL) @200,000/=
6Kupunguza au kuongeza maziwa kuyasimamisha @130,000/=
7.Kubana uke na kuondoa uchafu ukeni @120,000/=
8.Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
        NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri na garantii ili kukuhakikishia ubora na usalama wa bidhaa za NATURAL BEAUTY CO

    Wasiliana nasi Popote
  ulipo duniani kwa (+255)
           0659618585 na
           0759029968
        UTAPATA HUDUMA.
👉🏻OUR WEBSITE:- www.naturalworldbeauty.og
👉🏻INSTAGRAM PAGE:-
@natural2162
@natural2162
@natural2162

         < WELCOME ALL>

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls 0658316976
0755911233
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Wastara amlilia Rais Magufuli baada ya kutapeliwa milioni 80 na kampuni ya simu

$
0
0
Msanii wa filamu Wastara Juma amepaza sauti yake ya kutaka kusaidiwa pesa ya matibabu na Rais John Pombe Magufuli baada ya kutapeliwa na kampuni moja ya simu ambayo ilimteua kama balozi wa bidhaa zao.

Muigizaji huyo amedai ametapeliwa zaidi ya tsh milioni 80 na kampuni hiyo ya simu pesa ambayo amedai alikuwa anajichanga kwaajili ya matibabu ya mguu wake nchini India.

Taarifa ya Wastara.

    “RAIS MHE MAGUFULI
    MAKAMO MHE SAMIA SULUHU
    WAZIRI MKUU MHE KASIM MAJAALIWA
    MKUU  WA MKOA MHE POUL MAKONDA
    WATANZANIA WENZANGU

Mim Wastara juma muigizaji wa filamu tanzania naandika ujumbe huu mfupi sina budi sina jinsi nahitajika kurudi hosptal india Sifael hosptal tokea tal 12/02/2017 ambapo nilitakiwa nifanye matibabu kwa mda wa miaka 2 chini ya uwangilizi wa hosptal hiyo kabla ya kufanya maamuzi ya kufanyiwa operetion ya mgongo hivyo kila tal 12/ 2 natakiwa kurudi hosptal nimejitahidi kupambana peke yangu kutafuta pesa ya kunirudisha hosptal nimeshindwa

Mwezi 1 wachina wenye kampun ya simu ya KZG wamenikimbia nikiwadai milion 80 mwezi wa 2 muzambiq nimepoteza mzigo wa milon 19 kwenye vurugu la kufukuzwa watanzania
 
Mwezi wa 3 nimeenda nchini sweden kufanya filamu nimerudi mikono mitupu mwezi wa 4 nimedai pesa yangu steps tumeishia kwenda mahakamani bila kulipwa nilivyokuwa natarajia tokea hapo chchote ninachofanya kinachohusu pesa lazima tuishie polisi au mahakamani silipwi vile tunavyokubaliana na baya zaidi ninaofanya nao kazi awajui kuwa tokea nimerudi nchini toka sweden ninahaha kutafuta pesa ya matibabu,,

silali kwa maumivu makali ya mgongo na ninazimia kila mda hii imetokana na kuchelewa kurudi hosptal kufanya tiba ya mgongo na kubadilisha soberly skoner inayowekwa kwenye mguu kama tiba kuu ya kurudisha mgongo wangu ukae sawa matokeo yake mguu unavimba na kuchanika kila mara mgongo unauma kitu ambacho kinanikosesha raha kabisa na kuona sasa naathirika kiakili kwa maumivu sababu mda mwingi nakunywa dawa za maumivu bila kujua kama nimemeza dawa mara ngapi kwa siku hii sio nzuri kiafya

Kikubwa ninachoomba kutoka kwenu ni mim nirudi kwenye apointment yangu ya hospital sababu siwezi kurudisha mguu wangu kama zamani lakini ninaweza kuyakwepa maumivu kutokana na tiba ninayoweza kupata kupitia tatizo langu

Sihitaji msaada wa mtu nikiwa mahututi nikiwa siwezi kuandika sms kupokea sim au kumtambua mtu nahitaji sasa ninayo nguvu kidogo ya kuelewa hta nataka kutibiwa nin staki nisaidiwe kwa mtu kunisemea matatizo yangu wakati huo mim nimeshashindwa hta kuongea tena please watanzania wenzangu mficha uchi hazai sio mim mwenye matatizo pekee wapo wengi ila wanaona aibu najua mtajiuliza kiasiku wastara anauza nguo why?

anataka msaada sio kweli kuwa biashara ya mtandao inakidhi mahitaji yetu nimekuwa nikipost bidhaa kwa fujo bila kupost hta picha zangu nikiamini nitauza sana ili nirudi hosptal lakini sio kweli kabisa watu wanataka kuniona mim mitandaoni na sio mashati na magauni ninayouza ndio maana sifanyi vizuri upande huo ninaumia sana kuona mashabiki nawanyima haki ya kuniona lakini ninayo shida nahitaji niwe na afya njema nitembee vizuri nifurahi na watoto wangu na mashabiki zangu

afya yangu mim inauzwa tena kuanzia dollar 18000 pia mtajuliza why sioni aibu kusema shida zangu au kuomba msaada wakati mimi ni msanii na tafsir ya walio wengi wasanii ni watu wenye pesa sana sio kweli sanaaa yetu ndio kwanza inakuwa nimechoka kupost nikilalamika naumwa huku kesho mtu ananiona mzima nacheza mziki kumbe najilazimisha tu kuficha mateso yangu staki tena kuficha maumivu yangu natembea nanenepa huku nina maumivu makali

natamani nimmpe mtu huu mwili na ili jina ili niwe huru kwenye mateso ya kujificha huku naumia
 
nimejaribu sana kuongea na marafiki zangu wa karibu wanajua natania ninavyosema naumwa nahitaji msaada mtu aamini hata nikimwambia nichangie elfu 50 anaona nina pesa nyingi sana nadanganya No kabla haujafa haujaumbuka

nikiuza nyumba gari na chchote nilichonacho alafu nikafa watoto wangu wataishi wapi nin kitawasaidia mpka wapate pesa za kujikimu?? Jibu hakuna japo nimejaribu kunadi kilakitu nilichonacho ili mladi nipate pesa nirudi hosptal lakin mda umepita sana na naendelea kuumia mwili na kiakili pia sijafanikiwa please usinitafsir vibaya wala kunikejili wakati huna uwezo wa kunisaidia mim nimeamua kuwa muwazi kuwa nahitaji msaada ili niendelee na majukumu yangu watoto na watanzania waendelee kuniona

Pili ninaomba serikali inisaidie nipate pesa ninazowadai wachina mpka sasa zaidi ya milion 400 maana nilisain mkataba wa miaka miwili mpka leo ni mwaka 1 na miezi 2 na awajasitisha huo mkataba mpka leo kitu kinachoniuzia mim kufanya kazi na kampuny nyingine ya kuuza sim mpka mkataba wao uishe na awajanipa hta shilingi mia mpka sasa….

please wamenitoroka sina mkono mrefu wa kuwakamata zaidi ya huruma yenu na wanacho kiwanda kikubwa tu uko kwao china cha KZG kwasasa ninachohitaji kuliko chochote ni afya yangu kwanza
 
    Ukiguswa kwa chchote nipo na unanipata kwa no hii.
    0768666113
    0768666113

Auwa familia kwa wivu wa mapenzi

$
0
0

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule ambaye ni Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, amechukua uamuzi wa kuua familia yake kutokana na wivu wa mapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Benedict Kitalika amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kusema kuwa muuaji alifanya tukio hilo usiku wa jana huko nyumbani kwao Kimara jijini Dar es salaam, na kisha kutokomea kusikojulikana.

“Ni kweli mwanaume mmoja ambaye anafanya kazi ya uhasibu katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule, ameua mke, mtoto na shemeji yake, inasemekana kulikuwa na ugomvi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa huyu mtoto mdogo sio wake na anajihusisha na mapenzi na wanaume wengine, hivyo aliamua kuwaua kwa jembe na kukimbia”, amesema Kamanda Kitalika.

Kamanda Kitalika ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo marehemu aliacha ujumbe kuwa polisi wasihangaike kwani yeye ndiye kafanya mauaji.

Jeshi la Polisis limesema taarifa za tukio hilo walizipata kutoka kwa majirani baada ya kugundua hakuna dalili ya kuwepo watu kwenye hiyo nyumba na kuanza kuchunguza, ndipo walipogundua hayo na kuita polisi kuvuja mlango.

Waliouawa kwenye tukio hilo wametajwa kuwa ni Upendo Lukule ambaye ndiye mke, Magreth Samuel ambaye ni shemeji mtu na mtoto mdogo ambaye umri wake ni chini ya mwaka mmoja.

Wateja benki zilizofilisiwa kulipwa si zaidi ya Sh1.5 milioni

$
0
0
Bila kujali ni kiasi gani walitunza, wateja kwenye benki tano zilizotangazwa kufilisika, wataambulia si zaidi ya Sh1.5 milioni ya amana zao kwa mujibu wa sheria.

Jana, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu aliwaaga Watanzania baada ya kuiongoza taasisi hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa kwa miaka 10 mfululizo na kueleza kuwa tayari benki zilizofilisika zimekabidhiwa katika Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kwa taratibu za kisheria.

Kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo, Richard Malisa alimhakikishia Profesa Ndulu kuwa taratibu za malipo hayo zitafanyika haraka iwezekanavyo huku kiwango cha juu kitakacholipwa kwa wateja kikiwa ni Sh1.5 milioni.

“Mwenye amana za Sh100,000 atalipwa kiasi hicho na mwenye Sh50,000 atalipwa hiyo ila kiwango cha mwisho ni Sh1.5 milioni. Kwa hiyo, kama wewe una Sh5 milioni utakacholipwa ni Sh1.5 milioni,” alisema.

Taasisi tano zilizotangazwa kufilisiwa ni Benki ya Wanawake Convenant na Efatha. Nyingine ni benki za wananchi; Njombe na Meru pamoja na Benki ya Wakulima Mkoa wa Kagera (KFCB) ambazo zinaungana na FBME, Twiga Bancorp na Benki ya Wananchi Mbinga zilizofilisika na kufutiwa leseni mwaka jana.

Nyingine tatu zimewekwa chini ya uangalizi ambazo ni Benki ya Ushirika Kilimanjaro, Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na Benki ya Wananchi Tandahimba ambazo, endapo zitashindwa kukidhi vigezo, baada ya muda, nazo zitafilisiwa.

Kuhusu athari za kufungiwa na kufilisiwa kwa benki hizo Profesa Ndulu alisema jumla ya amana za benki zote nane ni Sh67.6 bilioni ambazo ni sawa na asilimia 0.38 ya benki zote 58 zilizopo nchini hivyo kutokuwa tishio.

“Hakuna athari zozote za kiuchumi zinazoweza kujitokeza kutokana na kufungiwa kwa benki hizi. Lakini, endapo tungeziacha ziendelee kujiendesha hivyohivyo, madhara yake yangekuwa makubwa,” alisema.

Profesa Ndulu alitaja sababu za benki ndogo kutofanya vizuri kuwa ni kutokana na kukosa mtaji, wigo mdogo wa biashara, ukubwa wa bodi zinazozisimamia pamoja na gharama kubwa za uendeshaji.

“Tumewashauri waungane, wawe shirikisho halafu hizo benki nyingine ziwe matawi kusaidia mfumo wao wa undeshaji uwe mmoja kupunguza gharama lakini utekelezaji umekuwa mgumu,” alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Benki za Kijamii (Cobat), Lukwaro Senkoro alikiri kupewa ushauri huo na BoT lakini akasema muda haukuwa rafiki kwao kuutekeleza ingawa hatua za makusudi zilichukuliwa.

Alisema katika jitihada hizo za kukamilisha mchakato wa kuziunganisha benki za wananchi, chama hicho kilianza kwa kukutana na bodi za wakurugenzi wa benki husika ambazo ziliafiki ushauri huo na kuahidi kwenda kuzungumza na wanahisa wao.

“Huko ndiko kulikosumbua,” alisema. “Benki sita zilikubali kuungana lakini tatu wanahisa wake wanahitaji muda wa ziada kufikiri kuhusu suala hilo,” alibainisha.

Alisema kwenye mkakati wao, walishafanikiwa kumpata mwekezaji atakayeiwezesha Benki ya Taifa ya Wananchi ambayo ingeanzishwa lakini baada ya benki tatu kutangazwa mufilisi, mchakato huo utakuwa umefika mwisho.

Alisema ushauri wa BoT ni wazo jipya lililohitaji kujadiliwa na wadau kabla ya kuridhia kuungana na kujiendesha chini ya mwamvuli mmoja hivyo kuhitaji muda wa kutosha wa uelimishaji.

“Ushauri ulitolewa Juni na tulipewa mpaka Oktoba tuwe tumekamilisha taratibu ili Novemba mwaka jana tuungane. Tumepambana mpaka mwisho lakini hatujafanikiwa. Kwa sasa mpango huo hautekelezeki,” alisema kwa masikitiko.

CCM yamsaka diwani wake aliyeipa kura UKAWA

$
0
0
Wajumbe wa CCM wanaoingia kwenye Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam, wamesema wapo katika hatua za mwisho za kumpata mjumbe mwenzao aliyesababisha wao kushindwa uchaguzi wa naibu meya wa jiji hilo.

Uchaguzi huo uliokuwa na mchuano mkali kutokana na kila upande kuwa na wajumbe kumi na moja, ulifanyika juzi katika ukumbi wa Karimjee na Mussa Kafana wa CUF akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) aliibuka kidedea kwa kupata kura 12 dhidi ya 10 alizopata Mariam Lulida wa CCM.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mjumbe baraza hilo CCM, Abdallah Chaurembo alisema tayari wanao ushahidi na wameshaanza kumbaini mjumbe ambaye alisababisha chama chao kushindwa katika uchaguzi huo.

“Tunataka kuirahisishia kazi kamati ya siasa ya mkoa kwa kumpata kwanza mjumbe huyu, halafu wao ndiyo watakaokuwa na jukumu la kumtangaza na kumchukulia anazostahili kwa mujibu wa makosa yake,” alisema Chaurembo.

Chaurembo ambaye pia ni Meya wa Temeke alisema walishaanza kumbaini mjumbe huyo kabla ya kazi ya kuhesabu halijakamilika na kudai kwamba hakuwa na nia ya dhati na CCM.

“Tulishakijua alichokuwa akikifanya, kwanza alikuwa anatetemeka wakati anaenda kupiga kura. Wakati yupo katika eneo la kupiga yeye ndiyo alitumia takriban dakika tano wakati wenzake nusu dakika.

“Hivi mtu unachukua takriban dakika tano nzima katika kupiga kura, una nini wewe, ina maana hujui kusoma wala kuandika? Alihoji Chaurembo. Nawaambia WanaCCM tutampata mtu huyo very soon (muda mfupi).

Alisema wameamua kushughulikia jambo hilo, ili iwe funzo kwa madiwani wengine wasiokitakia mema chama hicho na kwamba, hiyo itakuwa njia ya kuwaondoa wale viongozi wasio na masilahi na CCM.

Alieleza kuwa wajumbe wa CCM katika baraza hilo, wana imani wameshindwa katika uchaguzi kwa hoja mbili ambazo ni Ukawa kutumia utemi wakati kura mbili ziliharibika, na mjumbe mwenzao kuharibu kura na siyo kumpigia kura mgombea wa upinzani.

Katika uchaguzi huo, Chaurembo na meya mwenzake wa Ubungo (Chadema), Boniface Jacob nusura wazichape wakati wa shughuli ya kuhesabu kura kama si wajumbe wa uchaguzi huo kuwatenganisha.

Chaurembo aliendelea kwa kufafanua kuwa mjumbe huyo akishapatikana wajumbe wa CCM wa baraza ndiyo watakaokuwa mashahidi kwenye kamati ya siasa ya mkoa.

Babu Seya, Papii, Warudi Rasmi Kwenye Muziki

$
0
0
Ngili  wa muziki wa dansi, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Jonhson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa mara ya kwanza tangu waachiwe huru Desemba 9 kwa msamaha wa Rais John Maguuli, leo Januari 5 wamekutana na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza pamoja na wanahabari ambapo wamepata fursa ya kueleza namna walivyojipanga kurudi kwenye tasnia ya muziki.

Akizungumza na wanahabari katika Studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge, Coca-cola, Naibu Waziri Shonza amesema wao kama wizara kazi yao kubwa ni kuwasaidia wasanii na kuhakikisha wanafanikiwa kufikia malengo yao, hivyo wameamua kuwakutanisha na wadau wa muziki wakiwemo Wanene ili kufanmikisha zoezi la nguli hao kurudi kwenye game.

“Sisi kama wizara kuna namna ambayo tunaitumia kuwasapoti wasanii, hatuwezi kutoa fedha, hivyo tumeamua kuwakutanisha Babu Seya, Papii Kocha na Studio ya Wanene ili waweze kuweka mipango sawa kwa ajiri ya kuendeleza muziki,” alisema Shonza.

Kwa upande wake Babu Seya alisema mashabiki wao watulie kwani mipango ndiyo inapikwa hivyo mambo yakikamilika kila kitu watakiweka hadharani.

“Baada ya shooting na recording tutaangalia namna ya kufanya lakini hatutakuwa na utaratibu wetu wa zamani wa kupiga shoo kila siku,” alisema Babu Seya huku papii Kocha akiachia kionjo cha moja ya wimbo wao wa zamani.

Aidha, Mmiliki wa Studio za Wanene, Dash alisema wao wamejipanga kutoa sapoti ya ainza zote kwa babu Seya na papii ili kuhakikisha wanarekodi kazi nzuri na kuzifikisha kwa jamii na mashabiki wao.

Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

$
0
0
Leo January 5, 2017 Mfanyabiashara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja.

Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

“Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea TAKUKURU washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” – James Rugemarila

Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Tofauti na hayo Rugemarila pia ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini India kwa sababu anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi aliiambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.

Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018.

Tundu Lissu kusafirishwa kesho Kutoka Kenya....Bofya Hapa Kumsikiliza Akisimulia Kila Kitu Tangu Apigwe Risasi

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amefunguka na kusema kuwa kesho Januari 6, 2018 atasafiri na kutoka nje ya Kenya kwenda kufanyiwa matibabu zaidi kufuatia shambulio la kupigwa risasi lililotokea mwaka jana.

Lissu amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa nje ya hospitali ya Nairobi na kusema kuwa amekuwepo hapo kwa takribani miezi minne akifanyiwa matibabu lakini sasa anakwenda kufanyiwa matibabu zaidi sehemu nyingine.

Mbali na hilo Tundu Lissu ameendelea kusema kuwa shambulio lake kupigwa risasi ni tukio la kisiasa ndiyo maana viongozi wa bunge wamekuwa wakishikwa na kigugumizi.

 Amesema Bunge limeshindwa kumhudumia na kumlipia matibabu kama ambavyo inapaswa kuwa lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa Bunge ambaye amethubutu hata kwenda kumuona.

"Leo nazungumza Bunge la Tanzania halijatoa hata shilingi moja wakati sheria ipo wazi, ndugu zangu wamewaandikia barua ya kuwaomba kupata haki ya matibabu lakini mpaka tunazungumza sasa hivi Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Bunge, Katibu wa Bunge wala hakuna kiongozi wowote wa Bunge aliyefika kuniona kwa miezi hii minne, walijua sitaweza kupona ndiyo maana hawakuwa na Plan ya kunitibu" amesema Lissu

Aidha Mbunge huyo ametoa maoni yake kuwa anaamini jaribio la yeye kutaka kuuawa mnamo Septemba 7, 2017 ni jaribio la kisiasa na amedai anaamini jeshi la polisi nchini Tanzania hawapelelezi juu ya tukio hilo.

"Maoni yangu kilichofanyika kilikuwa ni jaribu ya mauaji ya kisiasa moja kwa moja, mimi siyo mfanyabiashara, jeshi la polisi kwa maoni yangu hawapelelezi tukio hili kwa sababu sijawahi ona mtu anakuja kuniuliza, wanamtaka dereva wangu kwaajili ya kumkamata na sio kumhoji juu ya tukio hilo" amesema Tundu Lissu

Msemaji Mkuu wa Serikali amemjibu Tundu Lissu

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu-Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu, Dkt Hassan Abbas amesem kwamba Tundu Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa.

Dkt Abbasi ameeleza kuwa, kwa sasa serikali bado inaendelea kumuombea mbunge huyo ili aweze kupona haraka.

Maneno hayo yametolewa ikiwa ni mida mfupi tangu Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alipozungumza na waandushi wa habari akiwa Hospitalini jijini Nairobi na kuituhuma serikali kuhusu masuala mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Miongoni mwa mambo mengi ambayo Tundu Lissu ameituhumu serikali ni pamoja na jaribio la kutaka kumuua lililotokea Septemba 7 mjini Dodoma, ambapo Lissu amesema licha ya kuwa miezi minne imepita tangu aliposhambuliwa kwa lengo la kuuawa, hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyekemea tukio hilo.

Lissu ameelekeza malalamiko yake pia kwa Bunge ambapo amekosoa uamuzi wa Bunge kukataa kugharamia matibabu yake, na kuacha mzigo wote kwa chama na familia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 6

Waziri Mkuu Ahimiza Kilimo cha Kahawa

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la biashara.

Ametoa wito huo jana Januari 5, 2017 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990.

“Limeni kahawa ili mpate fedha sababu zao hili ni la biashara. Kahawa ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali ya awamu ya tano imeamua kuyawekea mkazo ili yaweze kuongeza tija kwa wakulima na kuinua uchumi wa Taifa,” alisema Majaliwa.

“Tumeamua kuweka mkazo kwenye mazao matano ya pamba, kahawa, chai, korosho na tumbaku kwa sababu yanaleta tija na kuliingizia Taifa fedha za kigeni,” alisema na kuongeza.

“Tumefanya tathmini na tumegundua udhaifu mkubwa mkubwa katika usimamizi wa mazao haya ndani ya Serikali kuanzia ngazi ya Halmashauri.”

Waziri Mkuu alisema ni lazima wananchi walime zao hilo na viongozi wahakikishe wananchi wananufaika na zao hilo. 

Hata hivyo, alionyeshwa kutoridhishwa na utendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea baada ya kuelezwa kuwa kampuni ya Aviv Tanzania imezalisha miche milioni moja lakini iliyochukuliwa na kusambazwa kwa wananchi ni miche isiyozidi 200,000.

“Kampuni hii imeamua kutoa miche ya bure kwa wakulima, wamezalisha miche milioni moja lakini hadi sasa imechukuliwa 200,000 tu. Kuna miche zaidi ya 800,000, imebaki, na tena wawekezaji hawa wanatoa elimu bure ya kulima na kuitunza mikahawa yako,” alisema.

Amewataka wakulima hao watenge ekari moja hadi tatu kwa kila kaya ili waweze kulima zao hilo. “Wana Lipokela tengeni ekari moja hadi tatu za kulima kahawa, tukifanya hivyo suala la fedha kupitia kahawa litakuwa limekamilika,” alisema.

Amesema itabidi zao la kahawa liundiwe mfumo maalum wa ununuzi ambao ni wa ushirika kwa kuzingatia vyama vya msingi (AMCOS) vilivyokuwepo.

Mapema, akitoa taarifa juu ya shamba hilo, Meneja wa Aviv Tanzania, Bw. Medu Medappa alisema lengo la kuanzisha mradi huo lilikuwa ni kuhakikisha wanapata shamba kubwa la kahawa aina ya Arabica nchini Tanzania lenye viwango vya kimataifa.

Alisema wamekwishatoa ajira kwa Watanzania wapatao 3,000 zikiwemo za moja kwa moja na za msimu.

Alisema kampuni hiyo imeweza kuchangia miradi ya maendeleo kwenye vijiji vinne jirani vya Lipokela, Lusonga, Liganga na Selekano. “Hadi mwaka 2017 tuliweza kukamilisha ujenzi wa zahanatio katika kijiji cha Lipokela, nyumba ya mwalimu katika vijiji vya Liganga na Lusonga, uchangiaji wa madawati kwenye vijiji vya Lipokela na Lusonga,” alisema.

Alisema wameweza kuanzisha scheme ya wakulima wadogo wa nje (outgrowers scheme) kwa wakulima 2,000 ambao wamegawanyika kwenye vikundi 36 katika vijiji 31 ndani ya mkoa wa Ruvuma.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kutembelea wilaya ya Mbinga ambako atakagua miche kwenye taasisi ya TACRI, atatembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha Mbinga (MCCCO), kuzungumza na watumishi na madiwani na pia kuhutubia mkutano wa hadhara.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

BREAKING: Tundu Lissu aondoka Nairobi kwenda Ubeljiji kwa matibabu zaidi

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo Jumamosi asubuhi kwenda nchini Ubeljiji kwa matibabu zaidi ya kuurejesha mwili wake katika hali yake ya kawaida.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) ataondoka saa 2.30 asubuhi ya leo Jumamosi na Ndege ya Shirika la Kenya akiambatana na mke wake, Alicia.

Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma.

Mwanasiasa huyo amesindikizwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na watoto wake pacha, Augustino na Edward, ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.

"Nawashukuru sana madaktari wa hapa Nairobi na wale wa Dodoma wakiongozwa na Katibu Mkuu (wa wizara ya afya Profesa Mpoki Ulisubisya waliookoa maisha yangu," amesema Lissu kabla ya kupandishwa gari la wagonjwa

"Nakwenda Ubelgiji kwa matibabu, nikirudi mapambano yanaendelea, nawashukuruni nyote mlioniombea, nawashukuru Wakenya na serikali yao ambao kwa miezi minne nikiwa hapa walinipa ulinzi wakati wote."

Akizungumza kwa msisitizo  mbele ya wabunge na wanachama wa Chadema waliokuwapo amesema "Chapeni kazi, mimi nitarudi kuendeleza mapambano haya."

Kuhusu gharama, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema gharama za safari na matibabu zimegharamikiwa na Chadema na TLS.

Baadhi ya waliokuwapo hospitalini kumsindikiza Lissu uwanja wa ndege ni kaka yake Alute Mghwai, mdogo wake, Vinceti Mghwai na ndugu wengine.

Pia, Dk Mashinji, Naibu Makatibu Wakuu, John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar).

Wengine walikuwapo ni wabuge wa Chadema, Susan Kiwanga (Mlimba) na Godbless Lema(Arusha Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Rose Kamili (Viti Maalum), Anna Gideria (Viti Maalum).

Kwa niaba ya familia, Alute amesema "Tunamwomba Mungu ajalie huko anakokwenda akapate matibabu, kwani alivyokuja hapa sivyo anavyoondoka na tunawashukuru wananchi wa Tanzania na Kenya kwa ushirikiano wao."

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akitolewa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

BREAKING: Rais Magufuli aongeza baraza la mawaziri. ........Amteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Januari, 2018 amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Mhe. Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na  alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Kufuatia uteuzi huu Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.

Mhe. Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018

Breaking News: Rais Magufuli aenda kumjulia hali Kingunge Ngombale Mwiru

$
0
0
Rais  Magufuli akimjulia hali mzee Kingunge Ngombale Mwiru, katika wodi ya Mwaisela, Muhimbili. Mzee Kingunge amelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images