Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kakobe Asema Yuko Tayari Kuchunguzwa Utajiri Wake

0
0
Askofu  mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe,  amesema hahofii kuchunguzwa na serikali kuhusiana na ukwasi anaoumiliki na kuongeza kuwa fedha alizonazo ni zaidi ya fedha zinazomilikiwa na serikali nyingi duniani.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili kanisani hapo, Askofu Kakobe amesema  hana wasiwasi wa kuchunguzwa utajiri wake na kuongeza kuwa kwa sasa anamiliki pesa nyingi zaidi ya serikali za China na Marekani.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwajibu watu wote waliokuwa wakihoji uraia wake.

 " Wanaosema Kakobe amekimbia nchi nawashangaa sana nipo na wala siendi popote, kipindi Fulani walikuja kuchunguza uraia wangu lakini wakaambulia patupu, tutabanana hapa hapa.

" Watu wanasema Niko kimya sana wala sipo kimya tatizo wanataka nizungumze wanayoyataka wao, sasa Mimi sio mtu wa namna hiyo, ukiniona nimesimama katika madhabau Hays basi ujue nina kibali cha Mungu, mtu ukiitwa Mbwa kwani wewe ndio utakua Mbwa? Sasa nashangaa unaogopa nini kuitwa Mbwa wakati wewe sio Mbwa"
-Kakobe

Akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi wiki iliyopita, askofu huyo alisema yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania.

Katika mahubiri ya leo,  Askofu Kakobe amewaambia waumini wake kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni zaidi ya serikali nyingi duniani.

PPF wazungumzia kukamatwa kwa mfanyakazi wao na mirungi

0
0
Mfuko wa Pensheni wa PPF umesema mfanyakazi wake, Anitha Oswald, wa ofisi ndogo ya Moshi aliyekamatwa wiki hii akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi huko Moshi, Kilimanjaro, alikuwa kwenye likizo ya dharura na kwamba alikamatwa akiwa kwenye gari lake binafsi na nje ya eneo la kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na PPF vyombo vya habari na Meneja Uhusiano  leo, shirika hilo limesema tuhuma hizo zinamkabili mfanyakazi huyo yeye binafsi na si PPF.  Vilevile limelaani vitendo vya aina hiyo na linaunga mkono juhudi za serikali za kupiga vita madawa hayo.

Shirika pia limemchukulia hatua mfanyakazi huyo kwa kuzingatia sera za wafanyakazi wake.

Kauli MPYA ya Mbowe kuhusu madiwani na wabunge wa CHADEMA wanaohamia CCM

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewashangaa viongozi na wanachama wa chama hicho wanaohama na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa madai kwamba wanamuunga mkono Rais, na kusema haona sababu ya viongozi hao kuipongeza serikali.

Mbowe ameyasema hayo leo Disemba 31, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu matukio mbalimbali yanayoendelea nchini na kusema kuwa watu wanakufa hovyo, vyuma vimekaza, hivyo anawashangaa wanaosema kwamba wanaiunga mkono serikali.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai ametoa mifano kadhaa akionyesha matendo ambayo serikali hii inayetenda na kusema kwa kiongozi mwenye akili timamu hawezi kuhama na kuunga mkono serikali.

“Ni bora basi wanaohama wakatoa na sababu nyingine yenye akili. Mnapohama wote na wimbo mmoja kama kasuku, inatufanya tujiulize kwanini hawa wote wanaohama wanafurahia tu bwana mkubwa anapiga vita ufisadi?”

“Aliyesema ajenda za siasa ni ufisadi peke yake ni nani? Uchumi unaporomoka, vyuma vimekaza nchi nzima, wewe unampongeza Rais kwa lipi? Vyombo vya habari vinafungiwa, wewe unampongeza Rais kwa lipi? Miili ya watu waliouawa inaokotwa inaelea bahari, wewe unaipongeza serikali kwa lipi? Wewe Mbunge na Diwani mwenye akili timamu unaipongeza serikali wakati Lissu ana majeraha ya risasi 16?” alihoji Mbowe.

Mbowe amesema kwamba, wanasiasa waliohama kwa sababu hizo, wanawatakia kila la heri na kwamba wanaamini wataifika salama kwa sababu walipokuwa hawakuwa sehemu sahihi.

Mbowe ameeleza kwamba, kama wanaohama wangekuwa wanatoa sababu mbalimbali, mfano mwingine aseme uchumi upo vizuri, kilimo kimewekewa mikakati madhubuti au ajira na mishahara imeongezwa, ingekuwa afadhali kuliko kumsifia bwana mmoja ambaye nchi nzima inaugulia kwa sababu yake.

“Ili mti ukue, lazima majani ya zamani yapukutike, ili mengine mapya yachipue,” alisema Mbowe.

Nape aponda hamahama ya wanasiasa

0
0
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amehoji sababu za vyama vya siasa kuhangaika kupokea wanachama wa vyama vingine, badala ya kushughulika na Watanzania wasio na vyama.

Akizungumza leo Jumapili Desemba 31,2017 katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam, Nape amesema siku zote amekuwa na msimamo tofauti na wanachama wanaovihama vyama vyao kwa maelezo kuwa unawajenga wanaohama, si vyama.

"Kama tunataka kujenga vyama viwe vya kitaasisi ni lazima kuhamahama lisiwe suala la kawaida. Yaani mtu mpaka anahama watu waseme kweli huyu alistahili kuhama," amesema Nape.

Amesema, "Watanzania wapo zaidi ya 50 milioni, wenye uwezo wa kujiunga na vyama kikatiba wanaweza kuwa zaidi ya 30 milioni, waliopo kwenye vyama wanaweza wasifike 10 milioni. Kwa nini tunakwenda kuhangaika na wanachama wa vyama vingine badala ya kushughulika na Watanzania wasio na vyama. Tushughulike kuwashawishi hawa."

Katika kipindi hicho, mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro na mwanahabari mkongwe, Dk Gideon Shoo waliungana na Nape kukosoa vitendo vya wanachama kuvihama vyama vyao.

Kwa mtazamo wao, hamahama ya wanasiasa ni miongoni mwa kasoro zilizojitokeza mwaka 2017.

Kigwangalla:Tukimpeleka Askofu Kakobe Mahakamani Atatushinda

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa ukimpeleka mahakamani Askofu Zacharia Kakobe atashinda kwasababu watu wanasema inawezekana anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.

Kigwangalla ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo ameeleza kuwa ugonjwa unaotajwa kuwa huenda unamsumbua Kakobe dalili zake ni kujisifia.

Kigwangalla amefafanua aina ya ugonjwa huo wa akili ambao inawezekana unamsumbua Askofu Kakobe kuwa ni 'Bipolar Disorder: Currently Mania’. Pia amesisitiza kuwa hata ukimpeleka mahakamani anaweza akashinda kwa kigezo hicho.

''Kuhangaika na mtu kama KAKOBE  ni kupoteza muda bure. Kuna watu wanasema inawezekana akawa na ugonjwa wa akili ‘Bipolar Disorder: Currently Mania’ ambao katika dalili zake ni ‘delusions of grandeur’ . Akipelekwa mahakamani anaweza kutetewa kwa kigezo hiki na akashinda!'' ameandika Kigwangalla.

Tundu Lissu kupelekwa Ulaya kwa matibabu Januari 6

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe ameeleza kuwa hali ya Mbunge Tundu Lissu anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, imeimarika na hivi karibuni atahamishiwa katika hospitali nyingine kwa ajili ya mazoezi ya viungo.

“Tiba zote ameshamaliza kinachoendelea sasa ni mazoezi,” amesema Freeman Mbowe.

Mbowe amesema hayo leo, Disemba 31, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa tarehe 6 Januari, 208 Tundu Lissu atasafirishwa kupelekwa katika nchi moja ya Ulaya ambayo hakuitaja kwa kile kilichotajwa kuwa ni kwa sababu za kiusalama.

“Kwa sasa siwezi kuitaja nchi anakokwenda kwa ajili ya usalama,” amesema Mbowe.

Amesema gharama zilizotumika hadi sasa kumuuguza ni dola 300,000 za Marekani sawa na zaidi ya Sh 600 milioni.

Ikiwa ni siku zaidi ya 100, tokea Mbunge Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi eneo la nyumbani kwake, Area D, Dododma, majira ya saa 7 mchana, akiwa anatokea kazini, kwa sasa hali yake imeimarika ambapo picha za mwisho kutumwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, zilimuonyesha akiwa amekaa mwenyewe juu ya kitanda cha Hospitali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya January 1 , 2018.....Ni Mwaka Mpya !....

Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi Rais wa Kenya kufuatia ajali ya barabarani

0
0
"Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na roli katika barabara ya Nakuru - Eldoret nchini Kenya.
 
Msiba huu umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.
 
Kwa niaba ya Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.
 
Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone haraka na Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina".
 
Hizi ni salamu za rambirambi alizozitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu takribani 36 baada ya basi la abiria kugongana na roli katika barabara ya Nakuru - Eldoret nchini humo tarehe 31 Desemba, 2017.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Desemba, 2017

Lipumba ataka mjadala wa kitaifa kuhusu uchumi

0
0
Mtaalamu wa Uchumi, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu uchumi na mustakabali wa Taifa.

Profesa Lipumba ameyasema hayo jana Jumapili Desemba 31,2017 wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam kujadili hali ya uchumi kwa mwaka 2017.

Alisema kuna haja ya kujadili sera za kiuchumi, namna ya kujenga uchumi unaoongeza ajira kwa wananchi na kutafuta suluhisho la matatizo yanayowakabili Watanzania.

“Tuitishe mjadala wa kitaifa tuje kujadili, tutazame upya sera za kiuchumi, namna ya kujenga uchumi unaoongeza ajira utakaoleta manufaa kwa wananchi wote. Tujadili kimsingi na tutoke na sera ambazo tunaweza kuishauri Serikali nini cha kufanya,” alisema Profesa Lipumba.

Katika mjadala huo, Profesa Lipumba alisema Serikali haiwezi kufanikisha mapinduzi ya viwanda kama haijafanikisha ya kilimo kwa sababu ukuaji wa kilimo ndiyo ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi.

Alisema robo tatu ya Watanzania wanategemea kilimo lakini ukuaji wa sekta hiyo ni mdogo kutokana na Serikali kukiacha nyuma kilimo na kukumbatia sekta nyingine.

Profesa Lipumba alisema kuna changamoto kubwa kwenye kilimo ambazo zinatokana na ukweli kwamba, Serikali haijawekeza vya kutosha kwenye utafiti wa kilimo, mafunzo kwa wakulima na usambazaji wa pembejeo.

“Tujifunze kwa nchi za Asia kama vile China, India na Malaysia, wao wamewekeza kwa wakulima wadogowadogo,” alisema Profesa Lipumba.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeshiriki mjadala huo, alisema mfumo wa elimu wa sasa wa Tanzania unamwandaa mtu kuwa tegemezi badala ya kujitegemea kama ilivyokuwa zamani.

Alisema kuna umuhimu wa kufumuliwa upya kwa mfumo huo tegemezi ili kujenga utakaowafanya vijana wajifunze kujitegemea au ujasiriamali.

Bashe alisema Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa idadi kubwa ya mifugo lakini hakuna dira ya wazi ni wapi pajengwe viwanda.

Akichangia mada ya hali ya uchumi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Dk Bravious Kahyoza alisema Tanzania haijazalisha ajira za kutosha kwa wananchi kwa sababu ya kusinyaa kwa uchumi.

Alisema Serikali imekuwa ikishindana kukopa na sekta binafsi jambo lililosababisha sekta binafsi kubaki nyuma na kushindwa kuajiri watu wengi kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi.

lietaka kuwepo uwiano kati ya sera za kifedha na zile za kibajeti ili kuleta matokeo mazuri kwenye uchumi.

“Wataalamu wetu wanapaswa kukaa chini na kuangalia kama tuko kwenye njia sahihi kuelekea mpango wa maendeleo wa miaka mitano na uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. Kama hatuko sahihi basi ni vyema tukabadilisha mbinu tunazotumia kufika huko,” alisema.

Chadema Yawataka Viongozi Wa Dini Kuendelea Kuikosoa Serikali

0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini kwani ndio wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu nchi ilipopata Uhuru.

Mbowe ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.

“Lakini viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na hawa ndio kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.

“Sisi wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”

“Ukisikia Kakobe amezungumza, tafakari kwanza kabla ya kumkabili,”

0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amejibu hoja zinazotolewa dhidi yake, baadhi zikitolewqa na Serikali akisema anapozungumza ni lazima kutafakari kabla ya kumkabili.

Askofu Kakobe alizungumza jana wakati wa ibada katika kanisa la FGBF lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

“Ukisikia Kakobe amezungumza, tafakari kwanza kabla ya kumkabili,” alisema.

Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni siku moja baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutangaza kuanzakufuatilia ulipaji wake wa kodi.

Uamuzi wa TRAulitangazwa juzi na Kamishna Mkuu, Charles Kichere mbele ya waandishi wa habari baada ya hivi karibuni Askofu Kakobe kusikika akisema ana fedha nyingi kuliko Serikali.

TRA ilisema uamuzi huo unatokana na kiongozi huyo wa kiroho kutokuwemo katika kumbukumbu za ulipaji kodi za mamlaka hiyo. Mamlaka hiyo ilisema kama utajiri wake unatokana na sadaka pekee litakuwa jambo la kushtua.

Jana, Askofu Kakobe alitumia ibada hiyo kuwajibu TRA na pia alizungumzia mambo mengine mawili; uraia wake na onyo la Serikali la kuwataka viongozi wa dini kutokuzungumzia masuala ya siasa.

“Tangu nilipoitika wito huu miaka 30 iliyopita, sijawahi kufanya biashara yoyote zaidi ya hii na kanisa hili halina mradi wowote wa kiuchumi. Kakobe hana mradi wowote na kama yupo anayejua ajitokeze aseme nitampa zawadi,” alisema Askofu Kakobe.

“Akaunti yetu iko Benki ya NBC na iko chini ya Bodi ya Wadhamini, bodi ambayo imesajiliwa Rita (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini). Kwa hiyo, hao wanaotaka kujua zaidi waende Rita wakaulize wajumbe wa bodi hii ni akina nani na waende NBC kuona vyanzo vyetu vya mapato kama ni tofauti na sadaka.”

Huku akishangiliwa na waumini, alisema tatizo kubwa lililojitokeza nchini ni watu kutafasiri wanavyojua na kujikuta wakipotoka. Alisema hilo ni tatizo watu kutopenda kusoma Biblia kwa undani na kwa upana zaidi.

“Wamemsikia Kakobe anazungumza hapa, anazungumza mambo ya rohoni kuhusu haya ya utajiri. Unaweza kusikia maneno ukatafsiri kivyako kwa sababu haya tunayozungumza hapa ni mambo ya rohoni, wewe unayatafsiri kisiasa,” alisema Kakobe.

“Wanasema wewe una hela kweli kuliko Tanzania sema... ninaweza kuvunja hekalu na kulisimamisha kwa siku tatu. Mtu anajiuliza hekalu gani hili? Hekalu hili ni mwili wake. Maana yake niueni, nisulubisheni, lakini nitakufa na siku ya tatu nitafufuka, hii ndio hekalu, unatafsiri kwa akili.”

Kwa sauti ya juu na yenye msisitizo, Askofu Kakobe alisema: “Kimsingi, mimi si mtu tu tajiri kuliko Serikali, bali ni tajiri kuliko Serikali zote duniani. Kwa hiyo ukisikia Kakobe amezungumza, tafakari kwanza kabla ya kumkabili.”

“Hela yote ya Serikali ya Tanzania au dunia nzima haiwezi kununua tiketi hata moja ya Mbinguni. Mimi ni tajiri kuliko Serikali ya Magufuli (Rais John Magufuli) au Serikali ya Trump (Rais wa Marekani Donald Trump),” alisema.

Alisema nyumba anayoishi iliyopo Kijitonyama karibu na Kituo cha Polisi Mabatini jijini Dar es Salaam aliijenga miaka ya sabini na tangu wakati huo hajawahi kujenga kokote na gari lake ni la kawaida.

Askofu Kakobe alisema maisha yake si ya kifahari kama wasemavyo watu.

Uraia wake
Kuhusu uraia, Askofu Kakobe alisema wazazi wake walikuwa wakiishi Kakonko mkoani Kigoma na baada ya kufariki walizikwa huko, huku uraia wake ukifuatiliwa na ilibainika ni raia halali.

“Baba yangu alikuwa mwalimu kwa kipindi kirefu, amefanya kazi Tanga, Sumbawanga, Usukumani kwa Wanyamwezi, Tabora na Shinyanga. Miongoni mwa watu tuliocheza pamoja katika utoto wetu ni Christopher Chiza, huyu alikuwa waziri,” alisema Kakobe.

“Ukitaja kwa jumla familia yetu, inajulikana miaka mingi. Walikwenda kuchunguza uraia wangu na kujiridhisha pasina shaka na kusema huyu ni Mtanzania. Kuna kipindi watu walikwenda mara tatu kijijini kwangu Kakonko kuchunguza uraia.”

Waumini wakiwa kimya wakimsikiliza, Askofu Kakobe alisema, ‘’ Nimezaliwa Tanzania, wazazi wangu wamezaliwa Tanzania, mimi ni Mtanzania kwa hiyo sitoki hapa, tutabanana hapa hana.”

“Baada ya kuona, yote hayo, mara waende huku, waende huko waulize wazazi wangu ambao wamefariki hivi karibuni na makaburi yapo kijijini na niliwaambia makaburi wayaweke barabarani ili anayechunguza uraia wangu aanzie pale,” alisema.

Alisema, ‘’Kila jambo chini ya mbingu kuna kusudi, kuna kusudi la Mungu mimi kuzaliwa Tanzania, kwa hiyo wanaosema nimetoroka hawanisumbui kichwa.”

Kuhusu taarifa za kutoroka nchini alisema: “Ninapokwenda na kurudi washirika wa hapa wanajua. Kwa mfano safari ya mwisho ilikuwa Agosti (mwaka jana) na tangu hapo sijasafiri. Niko hapa na haya mengine nayasikia nimetoroka, hayanisumbui, ukiitwa majina si yako unasumbukia nini?”

Agizo la Waziri MKuu Kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Kilimo kutoka mikoa inayolima korosho, washirikiane kupata takwimu mpya za wakulima wa zao hilo.

Ametoa agizo hilo jana  mchana (Jumapili, Desemba 31, 2017) wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

“Maafisa kilimo na maafisa ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na kusimamia kwa umakini upatikanaji wa takwimu za wakulima na maeneo yanayolimwa, haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu,” alisema.

“Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi, na je ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani?” alisema.

“Pia nilikwishawaagiza maafisa ushirika na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) mpaka chama kikuu cha ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Mwenyekiti wa Kijiji, kwa sababu wao wana idadi kamili za watu wanaowaongoza,” alisema.

“Ninaamini tukifanya hilo tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wakulima wake, na tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji yao,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alipanda mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha akagawa miche kwa wakulima 10 kutoka vijiji vya Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao waliwawakilisha wenzao.

Mapema, kabla ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu na ya pili ni ile iliyotokana na vikonyo (grafting).

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka jimboni kwake.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki zoezi hilo.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, DESEMBA 31, 2017.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ammwagia sifa Rais Dkt Magufuli

0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, kwa kuiongoza nchi vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017.

Seif ametoa pongezi hizo katika salamu zake za mwisho wa mwaka ambapo alisema kwamba, kwa mwaka 2017, Rais Magufuli ameweza kuiongoza nchi vizuri kwa kudhibiti rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma.

Akitolea ufafanuzi suala la makinikia, Seif alisema kuwa, Rais Magufuli ameweza kupigania rasilimali za nchi hasa madini ili kuhakikisha wananchi wote wanafaidika, hatua ambayo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kiongozi huyo wa upinzani alisema, licha ya kuwa rushwa bado haijaisha, lakini juhudi zilizofanywa haziwezi kubezwa kwani imepungua ikilinganishwa na kipindi cha serikali ya awamu ya nne.

Pia, aliwataka wanasiasa kutokuona shida kusifia mazuri ambayo yamefanywa na serikali wakati wakifanya tathmini ya mwaka 2017. Seif alieleza namna serikali ilivyowafikisha mahakamani vigogo wa rushwa, kurejesha nidhamu ya fedha lakini pia kuokoa fedha zilizokuwa zikipotea kwa kuwalipa watumishi hewa.

Mbali na hayo, Seif pia alizungumzia changamoto za mwaka 2017 na kusema kuwa, uhuru wa kufanya siasa nchini umebanwa kufuatia kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa pamoja na maandamano.

Lakini akielezea suala la Zanzibar, alisema, ubaguzi katika visiwa hivyo bado ni changamoto kubwa kwani hata ajira zinatolewa kwa kufuata mrengo wa kisiasa badala ya utaalamu wa mtu.

Watu 120 wamekamatwa wakiwemo Mapadri nchini DRC Congo

0
0
Zaidi ya Makanisa 150 yaliandamana nchini DRC Congo December 31, 2017 wakimtaka Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani katika maandamano hayo imetolewa taarifa na Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Florence Marchal

Katika taarifa iliyotolewa imesema watu saba wameuawa mjini Kinshasa na mmoja katika mkoa wa Kananga, katikati mwa Congo na kuongeza kuwa watu 82 wamekamatwa wakiwemo mapadri, katika mji mkuu Kinshasa, na 41 katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake ya kumaliza mwaka, Kabila amesisitiza kuwa kutangazwa  kwa ratiba ya uchaguzi wa December 2018, kumefungua njia ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Polepole atumia Facebook Kuwachana Wapinzani na Kuelezea Mafanikio ya CCM

0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kujibu moja kwa moja maswali aliyoulizwa na wananchi.

Kupitia mtandao huo jana, Polepole alieleza mafanikio ya CCM yaliyopatikana kwa mwaka 2017.

Katika kipindi hicho kilichoanza saa 12:00 jioni, Polepole alikuwa akisoma maswali anayoulizwa na kuyajibu, huku akiviponda vyama vya upinzani kutokana na madai kuwa wanaohamia chama hicho wanahongwa na kuliingiza Taifa gharama za uchaguzi.

Akizungumzia mafanikio ya CCM, alisema yanatokana na mabadiliko makubwa ya muundo wake kwa kupunguza idadi ya vikao na wajumbe wa ngazi zote.

Katika mabadiliko hayo, wajumbe wa Halmashauri Kuu wamepunguzwa kutoka 388 hadi 158. Pia kikao hicho kimepunguza idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu kutoka 34 hadi 24.

“Alihama Nyalandu (Lazaro-aliyekuwa mbunge wa CCM- Singida Kaskazini) kwenda upinzani wakasifia kuwa demokrasia nzito, nzuri tusimseme ana haki na tuheshimu mawazo yake lakini Dk Mollel (Godwin-aliyekuwa mbunge wa Chadema -Siha) kaondoa kurudi CCM wanasema ni gharama ya uchaguzi,” alisema.

Alisema Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chadema lakini hawakulalamika

“Kwa kazi nzuri ambayo Rais John Magufuli anafanya sijui kama atabaki mtu, Dodoma watu wamehamia CCM, huko Tarime chama kinaitwa ACT viongozi wake wote wamehamia chama tawala, mpaka tukaanza kujiuliza majengo yao itakuwaje,” alisema.

Alisema hivi sasa chama hicho kina orodha ya makada wa vyama mbalimbali wanaowaelewa.

“Wanatuelewa maana wanaoongoza kupiga vita ufisadi ni CCM, kama ulisikia mafisadi hawashikwi, CCM ndio inawashika. wanaoongoza kutoa elimu bure ni CCM na Serikali yake. Sasa huko upinzani mnafanya nini. upinzani una kazi moja tu kukosoa,” alisema.

Zitto Kabwe ametaja lengo la waliotaka kumuua Tundu Lissu

0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameuzungumzia mwaka 2017 huku akiukaribisha mwaka mpya 2018, kwa kusema kuwa tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu lilimgharimu.

==>Hapo chini ni ujumbe wa Zitto Kabwe
Tunawatakia heri ya mwaka mpya 2018. Mwaka 2017 ulikuwa na changamoto lukuki lakini pia mafanikio makubwa kwetu kama chama. Mkutano wa miaka 50 ya Azimio la Arusha jijini Arusha ilikuwa mafanikio ya juu kiitikadi. Kwangu Mimi Hotuba ya Arusha ilikuwa bora kimaudhui na ilipaswa tutoe kitabu cha Hotuba ile.

Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia Jijini Mwanza kuhusu Maendeleo bila kupoka Uhuru wa watu ulitusaidia kuweka msimamo wetu kuhusu ubinywaji wa haki na Uhuru unaoendelea nchini.

Tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia. Ilinigarimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani tukio lile. Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema zaidi.

Kuondoka wanachama waandamizi ilikuwa pigo. Pigo hili limetupa funzo kubwa Sana na hivyo Tutaendelea kuwepo na imara zaidi mwaka 2018.

Chama chetu kinawatakia heri ya mwaka 2018. Tunamshukuru Mungu kwa mwaka 2017

Salamu za Mwaka Mpya kutoka kwa Rais Magufuli

CHADEMA Kuja na Mikakati Mipya 2018....Isome Hapa

0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza mikakati ya chama chake kwa mwaka 2018, akisema kitapigania upatikanaji wa Katiba Mpya ikiwemo uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema licha ya kutambua kuwa mwaka 2017 ulikuwa mgumu kwa vyama vya upinzani, mwaka huu watahakikisha wanapambana ili kurudisha mchakato wa Katiba mpya.

“Jambo kubwa tunalopigania hapa ni kuwa na tume huru ya uchaguzi,” alisema.

Moja ya mambo yanayolalamikiwa kuwa chombo hicho hakina uhuru ni uteuzi wa viongozi wake kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, na muundo wake.

Kwa sasa, NEC ina wafanyakazi wa ofisi ya makao makuu tu, wakati katika ngazi za wilaya ambako uchaguzi huratibiwa, inategemea wakurugenzi wa halmashauri ambao pia ni wateule wa Rais na si waajiriwa wa chombo hicho.|

Katika mkutano wa jana, Mbowe alisema suala la ukosefu wa fedha ili kuendelea na mchakato huo halina mashiko kwa kuwa kinachohitajika ni dhamira ya dhati.

“Tumeshatumia fedha nyingi hadi kufikia mchakato wa Katiba mpya ulipoishia, kinachohitajika ni dhamira ya dhati ya kupata Katiba Mpya. Rais anatakiwa kutambua kuwa Katiba ni matakwa ya wananchi si mapenzi ya Rais,” alisema.

Aliwataka wadau kutoviachia vyama vya siasa pekee kudai Katiba mpya kwa kuwa ina manufaa kwa Watanzania wote.

Mbowe alisema watahakikisha wanatumia kila aina ya mbinu ili kufanikisha kuendelea na mchakato huo.

“Leo tunamaliza mwaka 2017 lakini kwetu ulikuwa mgumu kushinda yote tangu nchi iingie katika demokrasia ya vyama vingi miaka 25 iliyopita,” alisema.

Alisema licha ya kuijenga demokrasia kwa kipindi chote hicho, utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano umerudisha nyuma.

“Pamoja na kuwa mimi ni mwenyekiti wa Chadema siwezi kuitisha mkutano wa wanachama hapa Dar es Salaam,” alisema.

Mchakato wa Katiba Mpya ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2011 alipounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Hata hivyo, mchakato huo uliishia kwenye Bunge Maalumu la Katiba ambalo licha ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ambayo haijapigiwa kura ya maoni hadi leo, baadhi ya vyama vya upinzani vilijitoa na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kikiwemo Chadema na kupinga mchakato huo kwa maelezo kuwa ulivurugwa na chama tawala.

Vyama vya upinzani vimejikuta katika wakati mgumu tangu kuingia madarakani Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na kushindwa kufanya mikutano ya hadhara, viongozi wake kukamatwa kwa tuhuma za uchochezi, kufanya fujo na uharibifu.

Mbowe alisema wakati vyama vya upinzani vinakatazwa kufanya mikutano, chama tawala kinafanya.

“Hakuna usawa katika kufanya siasa, ni sawa na kumfunga mikono bondia halafu unataka apigane na mwenzake ambaye hajafungwa mikono,” alisema.

Mbowe alisema kama Serikali inaona hakuna umuhimu wa kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa ni bora vikafutwa kuliko kuvizuia visifanye siasa.

Ujumbe wa Lowassa kwa watanzania wanapoanza mwaka 2018

0
0
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, ametuma salamu za mwaka mpya kwa Watanzania, akiwasihi kuwa, wakati wanaposherehekea mwaka mpya wasikubali kugawanywa.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) amesema kuwa amani na mshikamano nndio nguzo muhimu kwa Watanzania.

“Tunapouanza mwaka huu mpya, niwaombe watanzania wenzangu tukatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile.
Umoja na mshikamano ndio nguzo yetu.”

Kwa siku za hivi karibuni, Lowassa ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini, amekuwa kimya, bila kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoibuka katika siasa za Tanzania.

Mke wa Naibu Waziri, Kangi Lugola afariki dunia leo

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Kangi Lugola amefiwa na mkewe Mary.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Mary amefariki dunia leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa utaratibu wa mazishi unaendelea kufanyika na taarifa zitatolewa baadaye.

Wakati huohuo, Ofisi ya Bunge katika taarifa kwa umma imesema Spika Job Ndugai amemtumia rambirambi Lugola kutokana na kifo cha mkewe.

Imeelezwa msiba upo Railway Club Gerezani jijini Dar es Salaam.

Ndugai ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images