Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Agizo la Waziri Nchemba kama huna kitambulisho cha utaifa

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa Tanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari na kwamba ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambuliwa.

Amesema hayo akizindua zoezi la kujiandikisha kupata kitambulisho  cha Taifa na kugawa vitambulisho katika Mkoa wa Ruvuma na kukagua zoezi hilo linaendaje kwa mikoa ya Nyanda za Kusini hasa iliyoko mipakani mwa nchi.

Waziri Nchemba amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania.

Mh. Nchemba amewagiza viongozi wa wilaya na vijiji kutokuunganisha zoezi la kuandikisha wananchi kupata vitambulisho vya uraia na zoezi lingine lolote akitolea mfano baadhi ya viongozi kuchangisha fedha za kijiji kwa kuwaambia kuwa hutopata kitambulisho mpaka utakapo lipa fedha unazo daiwa na kijiji.

"Hili zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye nchini, ni kosa kubwa kama wewe ni raia ukaamua kukaidi ikiwa Rais wetu Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote.

“Hili ni jambo la Nchi na ni kubwa hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote, baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali”
–Dr Nchemba

Dk. Shika ( 900 Itapendeza ) Atangaza Kuihama Tanzania

$
0
0
Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani.

“Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu halafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa  Bara la Afrika, sasa ni world wide, ofisi itakuwa New York, nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR.

“Hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, hizi ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Rais Vladimir Putin”, amesema Dkt. Shika.

Dkt. Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina lake kupitishwa ikiwemo na Marekani.

TCRA Yatangaza Bei Mpya Za Kupiga Simu, Yaitoza Startimes Faini

$
0
0
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetangaza bei mpya za mwingiliano wa mitandao ya simu hapa nchini kwa dakika moja kuanzia Januari mosi, mwakani huku ikizitaka kampuni za mitandao kuongeza dakika za maongezi kwa wateja wao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kiliba, alisema uamuzi wa Serikali kutoa viwango vipya vitakavyodumu kwa miaka mitano (2018/2022), ni baada ya kufanya utafiti wa gharama za kampuni –fanisi (efficient operator) za uendeshaji wa mitandao ya simu namba tano wa mwaka huu.

Alisema mbali na kufanya utafiti, pia walikusanya maoni ya wadau husika kama ilivyoelekezwa katika kifungu namba 18(2) cha sheria ya namba 12 ya TCRA ya mwaka 2003 na kuunda jopo la wataalamu la kupitia maoni ya wadau juu ya gharama za mwigiliano zilizopendekezwa na TCRA.

Kiliba alisema kuanzia Januari mosi,  gharama ya mwigiliano kwa dakika moja itakuwa Sh 15.60, mwaka 2019 itakuwa Sh 10.40, mwaka 2020 itakuwa Sh 5.20, mwaka 2012 itakuwa Sh 2.60 na mwaka 2022 itakuwa Sh 2.00.

Alisema Serikali imeamua kushusha viwango hivyo zaidi tofauti na miaka mitano iliyopita ambapo kwa mwaka 2013 ilikuwa ni Sh 34.92,  mwaka 2014 ilikuwa ni Sh 32.40, mwaka 2015 ilikuwa ni Sh 30.54, mwaka 2016 ilikuwa ni Sh 28.57 na mwaka 2017 ilikuwa ni Sh  26.96.

Kiliba alisema kabla ya viwango hivyo, Serikali ilitoa ruhusa kwa wenye kampuni za mitandao ili kukaa na kupendekeza bei lakini walishindwa kuelewana kutokana na mvutano wa biashara yao ndipo ilipoamua kufuata sheria na kufikia kutangaza bei hizo.

“Kushuka kwa gharama za mwingiliano kutasababisha ongezeko la dakika za maongezi na hivyo kuongezeka kwa mapato ya watoa huduma na ya Serikali kutokana na ongezeko la matumizi ya huduma mbalimbali za mawasiliano.

“Kama TCRA inatarajia kwamba, kupungua kwa gharama za mwingiliano kutasababisha kushuka kwa gharama za kupiga simu kwenda mitandao mingine na hivyo kupunguza ulazima wa wateja kuwa na laini zaidi ya moja kwa kuhofia gharama kubwa kwenda mitandao mingine.

“Awali nimewaeleza laini zinazotumika hadi sasa zimefikia zaidi ya milioni 40, hivyo kuongezeka kwa matumizi ya huduma za mawasiliano kutawezesha na kuongeza ufanisi katika shughuli za sekta nyingine kiuchumi na kijamii, wito wetu kama mamlaka ni kuwataka watoa huduma kuzingatia viwango vipya, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake,” alisema.

Pia alisema gharama zilizotolewa ni bei za jumla ambazo kampuni za simu hulipana ili kufidia gharama ya kupokea simu inayotoka mtandao mwingine na kuifikisha kwa mteja aliye ndani ya mtandao unaopigwa na viwango hivyo si bei ya rejereja anayotozwa mteja anapopiga simu.

IDADI YA SIMU ZA MIKONONI, MEZANI
Pia alisema Tanzania imeendelea kupata mafanikio katika sekta ya mawasiliano ambapo idadi ya watoa huduma na watumiaji imeendelea kuongezeka na kukuwa kwa biashara na ujasiriamali.

“Kwa upande wa mawasiliano ya simu, idadi ya simu za mezani imeongezeka kutoka 16,238 mwaka 1961 hadi 127,976  Septemba, mwaka huu, kila mwaka kulikuwa na ongezeko fulani lakini kasi ipo juu kwa upande wa watumiaji wa simu za mkononi kwa sababu zimeongezeka kutoka laini 2,963,737 kwa mwaka 2005 hadi laini 40,002,364 kufikia Septemba, mwaka huu.

“Katika upande wa simu za kufanya miamala za kifedha, huduma hii nayo imekuwa tangu mwaka 2008 kwa sababu ilikuwa ni kampuni moja tu lakini hadi leo zimefikia kampuni sita ambazo ni Airtel, Tigo, Halotel, TTCL, Vodacom na Zantel, watumiaji wa miamala walikuwa 17,639,349 kwa mwaka 2015, lakini hadi Septemba, mwaka huu wamefikia 21,611,855.

“Watumiaji wa intaneti wameongezeka kwa kasi kutoka 1,681,012 kwa mwaka 2005 lakini hadi Septemba, mwaka huu  wamefikia 22,841,903, hili ni ongezeko kubwa la muda mfupi. Serikali tunaendelea kuboresha miundombinu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia,” alisema.

Kuhusu mitandao ya kijamii, alisema kuna watu wanaitumia isivyo kwa kuweka vitu ambavyo si vyake kweli na vingine vinakwenda kinyume na maadili ya Watanzania ikiwamo picha za utupu na aliliomba Jeshi la Polisi kuwa makini kwa kuwakamata wahusika.

“Sisi TCRA tunatoa miongozo na kudhibiti watumiaji lakini hatuwezi kukamata ila tunasaidiana na polisi kuwakamata wahusika, hivyo kila mnachokiona kinakwenda kinyume huwa tunahusika na wengine wamekamatwa, si kwamba kila kitu tutakisema hatua zilizofikiwa, tunaomba ushirikiano hasa waandishi wa habari,” alisema.

FAINI STAR TIMES
Akizungumzia faini za chaneli za bure za televisheni, alisema baadhi ya kampuni zenye ving’amuzi zimekuwa zikikiuka kanuni ya 14 (2)(a) ya mwaka 2011 kwa kushindwa kuonyesha chaneli tano za bure huku zikiwatoza wateja wao.

Alisema baada ya ufuatiliaji wa kampuni hizo, TCRA ilibaini Kampuni ya Star Media Tanzania Ltd inayomiliki king’amuzi cha Star Times haionyeshi chaneli hizo huku ikiwatoza watazamaji wake ndipo Desemba 22, mwaka huu Serikali iliamua kuitoza faini ya Sh milioni 100 kwa kitendo hicho.

Alisema zipo kampuni nyingine za ving’amuzi zinaendelea kufuatiliwa kwa ukaribu na kuwataka Watanzania kutoa taarifa pale chaneli tano ambazo ni TBC 1, ITV, EATV, Channel Ten, Star TV na Clouds TV zitakaposhindwa kuonekana ili sheria ziweze kuchukuliwa haraka.

Vanessa aanika alivyovuta ‘Pumzi ya Mwisho’ Akiwa Polisi

$
0
0
Mwanamuziki Vanessa Mdee anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi amesema kwamba alitamani kukata tamaa mwezi wa tatu alipokuwa kituo cha polisi lakini Rappa JohMakini alikuwa naye pamoja nyakati za usiku akimtembelea na kuhakikisha hakati tamaa.

Akizungumza kwenye usiku wa uzinduzi wa Albamu yake ya 'Money Mondays', Vanessa amefunguka na kusema kwamba hata baada ya kutoka kituo cha Polisi aliusikia wimbo wa Pumzi ya Mwisho uliofanywa   studio na alivutiwa na na ujumbe uliokuwepo kwenye wimbo huo.

"Kuna baadhi ya meseji sikuwahi kufikiria kuziweka kwenye Albamu yangu.  Pumzi ya Mwisho ni wimbo ambao sikuwahi kufikiria kuwepo kwenye Albam yangu ila baada ya kupitia changamoto za kukaa kituo cha polisi kwa siku kadhaa ilibidi meseji hii pia niiweke kwenye wimbo huu ambao nimeshirikiana na Johmakini pamoja na Casper Nyovest". Vanessa Mdee

Ameongeza kwamba; "Nisamehe Joh nakuuza lakini naombeni niseme kwamba Johmakini, Juma Jux pamoja na Benpol ni watu waliokuwa kila siku wanakuja kituoni na kunitia moyo. Namshukuru sana na naweza kusema kwamba ndoto yang katika maisha ya muziki ilikuwa ni ndoto yuangu ya  kufanya kazi na msanii Johmakini"

Mbali na hayo Vanessa Mdee amekiri kwamba albamu yake isingekamilika bila mpezi wake Jux kuwepo karibu kwani ni mtu ambaye alikuwa akimsukuma kuitoa kazi hiyo.

Breaking News: TRA kumchunguza Askofu Kakobe baada ya kumsikia akisema ana hela kuliko Serikali

$
0
0
Siku chache baada ya kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zachary  Kakobe kusema kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato nchini TRA imejipanga kuanza kufuatilia ulipaji wake wa kodi.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema mamlaka yake imeipokea kwa furaha kauli ya Askofu Kakobe na inataka kujiridhisha vyanzo vya utajiri huo.

Kichere amesema TRA inafahamu kuwa shughuli za kidini hazitozwi kodi lakini inataka kufahamu kama fedha hizo za Askofu Kakobe zinatokana na sadaka pekee au kuna shughuli nyingine za kiuchumi.

"Tumefuatilia hakuna kumbukumbu za Askofu Kakobe kulipa kodi, sasa tumeona tumfuate maofisa wetu wakajiridhishe kama fedha hizo anazozizungumzia zinatokana na sadaka,"

"Na kama hana shughuli zozote za kiuchumi ikiwa ina maana utajiri huo unatokana na sadaka ni jambo la kushtua kidogo lakini sisi tutaishia hapo,"

Amesema katika taarifa za mamlaka hiyo wapo watu wengi wenye fedha nyingi na kumbukumbu zao za kodi zipo lakini Askofu Kakobe si miongoni mwao.

Kichere amemwomba Askofu Kakobe kutoa ushirikiano kwa maofisa wa TRA watakaomtembelea kwa ajili ya shughuli hiyo ya ukaguzi.

Kuhusu kwanini uhakiki huo umekuja sasa Kichere amesema ni baada ya kusikia ana fedha nyingi kuliko Serikali wakati anafahamika ni kiongozi wa taasisi ya dini.

Habari Mbaya: Ofisa wa polisi ajiua kwa kujinyonga

$
0
0
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kituo cha Nansio wilayani Ukerewe, John Kalongola amejinyonga kwa kipande cha chandarua nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.

Amesema baada ya uchunguzi na utaratibu kukamilika mwili utasafirishwa kwa mazishi mkoani Iringa.

Kamanda Msangi amesema mwili huo ulibainika baada ya harufu kutoka ndani ya nyumba yake na mlango ulipovunjwa ulikutwa ukining’inia.

Mwili wa askari huo uligunduliwa jana Ijumaa Desemba 29,2017. Amesema kipande cha chandarua kilifungwa juu ya dari.

BREAKING: Serikali Imetoa Tamko Kuhusu Matumiizi ya Fedha za Kigeni Hapa Nchini

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katika  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kuwa utekelezaji wake uanze  tarehe 1 Januari, 2018.  Maagizo hayo ni kama ifuatavyo: –
  1. Bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi ya nyumba za kuishi na maofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.
  2. Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi. Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni.
  3. Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vile vya soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.
  4. Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yeyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.
Aidha Dkt. Mpango ameviagiza vyombo vya dola viwachukulie hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo haya ya Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Mahakama ya Katiba yalitaka bunge kumshtaki Rais

$
0
0
Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imebaini kwamba bunge la nchi hiyo lilishindwa kutimiza wajibu wake kwa kushindwa kumuwajibisha rais wa nchi hiyo Ndg. Jacob Zuma juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Uamuzi huo wa Mahakama ya Katiba ukiongozwa na Jaji Chris Jafta nchini humo umeainisha kwamba bunge hilo ni lazima lianze mchakato wa taratibu za kumfungulia mashitaka ingawa haikuwa wazi kwamba mchakato huo utaweza kumuondoa madarakani kwa kupigiwa kura.

Mahakama hiyo ilikuwa ikisikiliza kesi  iliyofunguliwa na kambi ya upinzani ambayo ilitaka bunge la nchi hiyo kuanza mchakato wa kumshitaki Rais Zuma.

Rais Zuma anatuhumiwa kutumia fedha za umma kuendeleza makazi yake binafsi.

Alichokiandika mke wa Kafulila baada ya kuonana na Tundu Lissu leo

$
0
0
Leo December 30, 2017 Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Singida Jesca Kishoa alikuwa Nairobi Kenya ambapo alienda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi akiwa nyumbani kwake Dodoma na watu wasiojulikana.

Kupitia account yake ya Instagram aliandika jumble usemao….”Shauku yake ya kulitetea taifa hili imeongezeka mara 100000000000….. Aisee ni kama kuzima moto kwa petrol… Wasiojulikana wamemfanya awe jasiri zaidi.Glory to the Almighty God.Aluta Continua“

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 31

Kanusho la taarifa inayosambazwa kumuhusu Makamu wa Rais

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuwa atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018. 

Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa.

Ikumbukwe kuwa siku ya tarehe 15-12-2017 wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo itaratibiwa na Ofisi yake .

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia matangazo, taarifa na ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya upandaji miti Dodoma.

 Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma

 30 Desemba, 2017.

Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Ya Ccm Mkoa Wa Arusha Robert Pjn Kaseko Amjibu Askofu Zacharia Kakobe.

$
0
0
Askofu Kakobe Umekosea sana kuigeuza nyumba ya Ibada takatifu na kuifanya kama Uwanja wa kuongelea mambo yahusuyo Siasa. Ni kweli  kila mtanzania  ana Uhuru wa kuongea na kutoa maoni yake lakini pia tufahamu wakati sahihi na mahala Sahihi pa kuwasilisha jambo fulani na wewe  kama Kiongozi na Mtumishi wa Mungu  tambua  MUKTADHA ama Ujumbe wako na Mazingira ya kuongelea jambo fulani, haikuwa mahala sahihi kuongelea mambo yahusuyo Siasa tena unayemlenga hayumo humo kanisani.

Kwa Uelewa wangu mdogo, kanisa kama eneo ama jengo ni mahala ambapo watu hukusanyika ili kupewa mahubiri/ mafunzo ya maneno matakatifu ya Mungu. Kanisani ni sehemu takatifu ya Kumwabudu Mungu, ni sehemu ya kuwaambia waumini waliokusanyika humo maovu yao ili  wayaache na kumrudia Mungu. Sasa huwezi kuacha kuhubiri habari za  Yesu Kristo ukaanza kuwahubiria  waumini habari za Siasa na wakati wamekuja kujifunza neno la Mungu.  

Tukumbuke  Kuna namna nzuri ya kuwasilisha ujumbe wako baada ya kumtambua vizuri uliyemkusudia kumpelekea huo Ujumbe wako. Mimi siwezi nikaanza kukusema wewe kakobe mtumishi wa Mungu kwa kupayuka tu na wakati natambua wewe ni nani katika Taifa hili na vivyo hivyo unatambua John Pombe Magufuli ni Kiongozi Mkuu wa Nchi katika Taifa hili kwa nini usingeomba appointment ya kuonana na Rais Magufuli na kumweleza ya moyoni. Hata vitabu vitakatifu pia vinazungumzia habari ya kuheshimu watawala halali wa Nchi, sasa kuheshimu ni pamoja na kumtambua mtawala halali wa Taifa lako ambaye amepata kibali kutoka kwa Mungu. Kama unataka kumkosoa basi yule si kama mimi ambaye unaweza kufanya ulivyofanya yule ni Mtawala na Kiongozi Mkuu wa Nchi mfuate umueleze na kumshauri vizuri. Muombe msamahama Rais Magufuli na waumini wako hata wao hukuwatendea haki.

Aidha Askofu Zacharia  Kakobe nikushauri kama umeamua kuwa mwana siasa fuata taratibu za Nchi kusajili Kanisa lako kuwa Chama Cha Siasa au Ubaki kuwa Mtumishi wa Mungu  na ufuate dhumuni hasa la Kanisa lako maana ulichokifanya ni kukiuka dhumuni la kuanzishwa kwake. 

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI NA KUWAHEKIMISHA VIONGOZI WETU WA DINI, MUNGU BARIKI RAIS WETU WA TANZANIA.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
December 29, 2017.

Waziri Mkuu amwagiza Ofisa madini aitishe kikao na wananchi.......Ni baada ya kupokea mabango ya wananchi wakidai kunyanyaswa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Kanda ya Kusini, Bw. Ogesa Charles Tale afike eneo la mgodi wa dhahabu wa Namumgo na kuitisha kikao cha wananchi leo (Jumapili) saa 4 asubuhi.

“Sasa hivi natoka kwenda Matambare, twende wote, lakini kesho (leo) saa 4 asubuhi uje hapa Namungo, uitishe mkutano wa hadhara na uwasikilize hawa wachimbaji wadogo na kisha uniletee maelezo ofisini kwangu,” alisema.

Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Desemba 30, 2017), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Namungo, wilayani Ruangwa baada ya kupokea mabango mawili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo. Waziri Mkuu yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, na ameamua kukagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi katika wilaya hii.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya awamu ya tano imejikita kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na alipomuuliza afisa huyo kama ameshawahi kupata nafasi ya kuwasikiliza wachimbaji wadogo, alijibiwa kwamba hajawahi kufanya hivyo.

“Hawa ndiyo nguvukazi ya mgodi, hawa ndiyo wanaingia kule chini kuchimba udongo, hawa ndiyo wanapata machungu ya kazi ya uchimbaji, kwa hiyo uje uwasikilize na uniletee taarifa kesho mchana,” alisisitiza.

Baada ya kuyasoma mabango yao, Waziri Mkuu aliwaita wakazi ambao waliyaleta mabango hayo na kuwataka waeleze kwa undani ni matatizo gani yanayowakabili. Bango la kwanza lilisema wananchi wananyanyaswa na viongozi kwa maslahi binafsi ya viongozi na la pili lilisema wamekatazwa wasiseme matatizo yao kwenye mkutano huo wa Waziri Mkuu.

Mkazi wa kijiji cha Mtondo, kata ya Nambilanje, Bw. Mussa Omari Kimatilo, alisema wananyanyaswa na uongozi wa kijiji pamoja na uongozi wa wenye machimbo ya dhahabu na kwamba wananyimwa uhuru wa kujieleza kila wanapokutana na viongozi hao.

“Tunanyanyaswa na uongozi wa machimbo, tunanyanyaswa na uongozi wa kijiji na tukilalamika hakuna wa kutusikiliza. Tumekaa na Rajani (mmiliki wa mgodi) amekubali kutulipa lakini wananchi hatuna uhuru wa kujieleza,” alisema.

Alidai hata Naibu Waziri wa Madini alipotembelea mgodi huo mapema mwezi huu, hakupewa fursa ya kukutana na wachimabji wadogo, na badala yake alipitishwa kijijini hapo na kuingizwa mgodini kisha akaondoka.

Naye Bahati Mikael, mkazi wa kijiji cha Namungo alisema kumekuwa na ukiritimba wa kutoa leseni kuhusu mgodi huo na kwamba tangu ilipotolewa rasmi mwaka 2014, bado hawajalipwa malipo yao.

“Hapa pana ukiritimba wa kutoa leseni ya uchimbaji. Mwekezaji amekuwa akichimba kinyemela; tangu mwaka 2006 alikuwa hajapewa leseni hadi mwaka 2014 ndipo alipopewa,” alisema.

Alipoitwa na Waziri Mkuu atoe ufafanuzi juu ya madai ya wakazi hao, Kaimu Afisa Madini wa kanda hiyo alisema eneo wanalodai wakazi hao ni la Mzee Kishor Rajani na inaeleweka hivyo na kwamba miaka ya nyuma walichimba kwa maelewano tu bila mikataba yoyote.

“Yale ya nyuma yalishapita kwa sababu hamkuwa na mkataba naye, mlifanya naye kazi kwa makubaliano ya mdomo tu. Sasa hivi mmeanza kuwekeana mikataba, zamani alikuwa anachukua asilimia kubwa lakini sasa hivi anachukua asilimia 17.5 na inayobaki amewaachia ninyi,” alisema Bw. Tale.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara ya jimboni kwake.

Rais Magufuli Asali Ibada Ya Familia Takatifu Katika Kanisa La Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya  Familia Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.

Katibu Bunge afunguka Zitto Kabwe kuanika utajiri wake facebook

$
0
0

Siku  moja baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) kuanika mali zake na madeni kwenye mitandao ya kijamii na kuwataka viongozi wengine wafanye hivyo, Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai, amesema jambo hilo ni uamuzi binafsi wa mtu, hivyo ofisi yake haiwezi kuingilia.

Pia katibu huyo  alisema kuwa bado hajauona muswada anaodai Zitto kuwa tayari amewasilisha zaidi ya mara moja kutaka kuwapo kwa sheria itakayowalazimisha wabunge na mawaziri kuweka wazi kwa umma taarifa juu ya mali wanazomiliki pamoja na madeni yao na si taarifa hizo kuishia tu kwa Kamishna wa Maadili.

Juzi, kupitia kurasa za akaunti zake za mitandao ya kijamii ya facebook na tweeter, Zitto aliweka hadharani tamko lake juu ya mali zote anazomiliki pamoja na madeni, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuliwakilisha na kupokewa kwenye Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Jana ndiyo iliyokuwa siku ya mwisho kisheria kwa kila kiongozi kuwasilisha tamko lake kwenye sekretarieti hiyo.

Katika tamko lake hilo, Zitto alitaja mali zake zinazoweza kuchukuliwa na Watanzania walio wengi kuwa ni utajiri kutokana na hali halisi ya kipato kwa wengi wao.

Mali hizo ni pamoja na fedha taslimu Sh. milioni 55.2 zilizotokana na mshahara; Sh. milioni 21.8 alizoingiza kupitia posho ya kujikimu; Sh. milioni 102 zilizotokana na posho ya ubunge huku posho ya vikao ikiwa sifuri kutokana na ukweli kuwa huwa hachukui.

Kadhalika, Zitto alisema kwa ufupi, tamko lake la mwaka 2017 unaomalizika leo halina tofauti sana na mwaka 2016 isipokuwa katika baadhi ya maeneo ikiwamo kuongezeka kwa deni jipya kutoka Benki ya Azania kiasi cha Sh. milioni 104 na deni la mtu binafsi kiasi cha dola za Marekani 2,300.

Pia kupungua kwa madeni ya benki ya CRDB kutoka Sh. milioni 214 hadi kufikia Sh. milioni 143 na NSSF kutoka Sh. milioni 191 hadi kufikia Sh. milioni 142 baada ya kuyalipa kwa mwaka mzima uliopita; kuongezeka kwa rasilimali ambazo ni hisa 60,000 za kampuni ya Vodacom na kupimwa kwa ardhi eneo la Mangamba Manispaa ya Mtwara Mikindani lenye vitalu 42 vya ukubwa tofauti.

Kuhusiana na uamuzi wa Zitto wa kufichua maslahi yake kwenye kurasa za facebook na tweeter, Kigaigai alisema mbunge huyo hawezi kuzuiwa kufanya hivyo kwa sababu ni uamuzi wake binafsi.

“Hata wewe (mwandishi) ukiamua kufanya hivyo ili mimi nijue, sioni kama kuna tatizo… yeye kaamua (kwa utashi) binafsi na sidhani kama hilo lina kizuizi,” alisema Kigaigai.

Kuhusiana na madai ya Zitto kuwasilisha zaidi ya mara moja muswada wa sheria ya kuwalazimisha wabunge na mawaziri kuweka hadharani tamko la mali zao na madeni kwa nia ya kuimarisha maadili na kufanikisha zaidi dhana ya utawala bora, Kigaigai alisema yeye hajaona muswada huo na wala haufahamu.

“Huo muswada mimi sijauona na wala siujui … katika ofisi hii sina muda mrefu ,” alisema Kigaigai ambaye aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Katibu wa Bunge Oktoba 7, mwaka huu.

Mahakama Kuu yakataa ombi la mjane aliyemlilia Rais Magufuli

$
0
0
Mahakama Kuu imetupa maombi ya Swabaha Mohamed aliyeangua kilio mbele ya Rais John Magufuli akidai kudhulumiwa mirathi ya mumewe, baada ya kujiridhisha kuwa sababu alizotoa hazikuwa na ukweli.

Katika maombi hayo, Swabaha alitaka ateuliwe kuwa msimamizi wa mirathi.

Mama huyo anayedai ni mjane wa Mohamed Shosi Yusufu wa mkoani Tanga alikuwa akiomba kuongezewa muda wa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya Wilaya Tanga.

Mahakama ya Wilaya Tanga ilitupilia mbali rufaa yake ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo Tanga kumteua Saburia Shosi ambaye ni mtoto wa marehemu kuwa msimamizi wa mirathi hiyo badala yake.

Mahakama Kuu katika uamuzi uliotolewa Jumatano na Jaji Amour Khamis, imeyatupa maombi hayo baada ya kuridhika kuwa sababu zake za kuomba kuongezewa muda si za kweli.

Katika uamuzi huo, Jaji Khamis alikubali hoja za Saburia kupitia kwa wakili wake, Abdon Rwegasira kuwa mwombaji (Swabaha) hakutoa sababu za msingi za kustahili kuongezewa muda wa kukata rufaa na kwamba sababu ya ugonjwa na kulazwa aliyoitoa si ya kweli.

Hii ni mara ya pili kwa Swabaha kufungua maombi mahakamani hapo akiomba kuongezewa muda wa kukata rufaa.

Ombi la awali lilitupwa kutokana na kutokuwa na sababu za msingi kisheria za kuchelewa kukata rufaa.

Awali, alifungua maombi mwaka 2016 akidai alichelewa kupata nakala ya mwenendo wa kesi na hukumu aliyokuwa anataka kuikatia rufaa.

Oktoba 2016 Mahakama Kuu katika uamuzi uliotolewa na Jaji Khamis iliyatupilia mbali maombi hayo.

Mapema mwaka huu alifungua tena maombi hayo mahakamani hapo na akatoa sababu nyingine, akidai alichelewa kukata rufaa kwa kuwa alikuwa amelazwa hospitalini kutokana na kuwa mgonjwa.

Aliwasilisha mahakamani kadi ya kuruhusiwa kutoka Tanga Central Health Centre, ikionyesha alilazwa Oktoba 9, 2016 na akaruhusiwa Oktoba 16, 2016.

Wakili Rwegasira aliwasilisha mahakamani barua na kiapo cha mkurugenzi wa kituo hicho aliyejitambulisha kuwa ni Dk H. I. Ngayomela, akikana mama huyo kulazwa hospitalini kwake.

Dk Ngayomela alisema ingawa kadi inaonekana ni ya hospitali yake, lakini hajui aliipataje, huku akisema tarehe ya kulazwa na kuruhusiwa pamoja na namba ya jalada vinavyoonekana katika kadi hiyo ni vya mgonjwa mwingine tena wa kiume.

Alisema mwandiko kwenye kadi haufanani na wa daktari yeyote kituoni kwake, huku akidai haina saini.

Siku chache baadaye, Swabaha aliwasilisha maelezo mengine mahakamani ambayo hata hivyo, yalikuwa yameandikwa kwenye karatasi bila kubainisha kuwa imeandikwa kwa nani, akidai inatoka kwa Dk Ngayomela akikiri kumtambua na kwamba kuna makosa yalifanyika wagonjwa wawili wakapewa namba moja ya jalada.

Maelezo hayo yalisababisha wakili Rwegasira aiombe Mahakama mama huyo afike mahakamani kuhojiwa kuhusu mkanganyiko huo na alishindwa kutoa maelezo ya kuiridhisha Mahakama.

Jaji Khamis katika uamuzi wake alisema amebaini kuwa kuna ufa wa wazi katika madai ya mama huyo ya kuugua na kulazwa, kutokana na kushindwa kutaja hata jina la daktari au muuguzi aliyemhudumia kwa siku saba.

Alisema hata barua ya pili ya Dk Ngayomela inayoeleza kumtambua haiwezi kufafanua na kuondoa shaka ya tuhuma alizotoa mwanzoni kwenye kiapo cha upande wa mjibu maombi.

Jaji Khamis alisema Swabaha katika mahojiano mahakamani hakuweza kufafanua utata huo na kwamba, majibu yake wakati wa madodoso, akihojiwa na wakili Rwegasira yalikuwa ni ya kujikanganya.

“Mwombaji alishindwa hata kutaja majina ya madaktari na wauguzi waliokuwa wakimhudumia kwa muda wa siku saba alizodai alilazwa hospitalini hapo. Alimtaja Dk Ngayomela tu kama anayeweza kumkumbuka katika orodha ya madaktari waliomhudumia katika ugonjwa wake,” alisema.

Jaji Khamis alisema, “Kwangu hili haliwezi kuwa kweli kwa sababu kama angekuwa amemhudumia kama alivyodai asingeweza (Dk Ngayomela) kushindwa kutambua mwandiko wake katika kadi ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, kwa kiwango cha kukana uhalali wake kwa kiapo.”

Alisema maombi hayo hayana mashiko hivyo kuyafuta na kuamuru Swabaha kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo.

Lema atabiri majibu ya Kakobe kwa TRA

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri wake wa majibu ambayo Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe atawapa Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu mali na utajiri wake.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jana ilisema kuwa inataka kufanya uchunguzi mali za Askofu huyo ili kujua chanzo halisi cha utajiri wake kufuatia Askofu huyo kudai kuwa ana fedha kuliko Serikali. 

Alichoandika Jux kwenda Vanessa wakiwa pamoja Kenya

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Juma Jux ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Utaniua' amefunguka na kumpa neno mpenzi wake Vanessa Mdee kuwa katika mwaka 2017 amepambana sana na kufanya kazi kubwa mno katika maisha yake.

Jux na Vanessa kwa sasa wapo pamoja nchini Kenya ambapo leo Vanessa Mdee anategemea kufanya show Kenya na huuu ndiyo ujumbe wa mpenzi wake Jux kwake

"Umepambana sana mwaka huu baby. 'Am so proud of what you have done' pumzika leo (jana) Kesho (leo) tukaweke historia nyingine" aliandika Jux

Kamishna wa Magereza azungumzia msongamano wa wafungwa

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa amesema jeshi hilo linakabiliwa na msongamano wa wafungwa kutokana na kuongezeka vitendo vya uhalifu na makosa ya kijinai.

Dk Malewa amesema hayo leo Jumapili Desemba 31,2017 katika Gereza Kuu la Mkoa wa Mbeya akiwa ziarani kukagua magereza na kuzungumza na askari wa jeshi hilo.

Amesema msongamano unatokana na majengo yanayotumika kuwahifadhi wafungwa ni yaliyojengwa enzi za mkoloni.

Hata hivyo, amesema wamejipanga kuendelea kuongeza idadi ya magereza kwa kila wilaya licha ya baadhi ya wananchi kutopendezewa na jambo hilo.

“Wakati tunapata Uhuru watu tulikuwa kama 10 milioni, hadi sasa majengo kama yameongezeka basi ni mawili lakini ni yaleyale; pia kuna makosa mapya ya uhalifu yameongeza ambayo zamani hayakuwepo,” amesema.

Amesema makosa ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha yamejitokeza; huku mauaji yakiongezeka.

Pia, amesema msongamano unasababishwa na kesi zinavyoendeshwa mahakamani ambako zipo zinazochukua muda mrefu upelelezi kukamilika.

Wakati huohuo, Dk Malewa amesema katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuongeza uzalishaji wa chakula kwa lengo la kujitegemea ifikapo mwaka 2022 wametenga magereza 10 yatakayotekeleza mpango wa uzalishaji.

Amesema chakula kitakachozalishwa kitatumika ndani ya magereza hayo na kulisha Taifa litakapokabiliwa na uhaba.

“Kwa sasa Jeshi la Magereza linaitegemea Serikali kwa asilimia 100 ilhali ina rasilimali watu ya kutosha kuzalisha chakula. Hivyo, tumeanza utekezaji kwa magereza 10 na lengo ni hadi kufika miaka mitano ijayo tuwe tunajitegemea kwa asilimia 100 bila Serikali,” alisema Dk Malewa.

Kanisa Katoliki yaitisha maandamano ya amani Kongo

$
0
0
Kuna wasi wasi wa kukosekana utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayokabiliwa kwa sasa na mgogoro wa kisiasa kufuatia kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo kuitisha maandamano ya amani.

Kabila ambaye waandaaji wa maandamano hayo wanamtaka atamke wazi kuwa hatawania muhula wa tatu wa uongozi, amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 wakati aliposhika madaraka ya urais baada ya baba yake Laurent Kabila kuuawa.

Kabila alikataa kujiuzulu bada ya kumalizika  kipindi chake cha pili na cha mwisho  Desemba 2016 hatua iliyosababisha maandamano pamoja na machafuko.

Tangu kipindi hicho maanadamano yamekuwa yakipigwa marufuku licha ya wakati mwingine waandamanaji kukiuka amri ya serikali na kuendelea na maandamano hali ambayo pia imekuwa ikisababisha umwagaji wa damu.

Hatua ya kanisa Katoliki kuitisha maandamano  ya leo Jumapili licha ya serikali kuyazuia yasifanyike inawafanya baadhi ya wachambuzi kuonya juu ya uwezekano wa kukosekana utulivu.

“Maandamano ya leo Jumapili nchini Kongo yanaweza kuwa makubwa zaidi kuliko yale ya mwaka jana” ameandika kupitia ukurasa wa twitter Jason Stearns  mchambuzi aliyebobea katika masuala ya siasa za Kongo kutoka chuo kikuu cha New York kinachohusika na mahusiano ya kimataifa.

Anasema vyama vyote vikubwa vya upinzani, asasi za kiraia, makundi ya vijana wanaharakati pamoja na kanisa Katoliki yanaunga mkono maandamano hayo ya leo Jumapili.

Uchaguzi ulipaswa kufanyika mwaka huu
Uchaguzi ulikuwa ufanyike mwishoni mwa mwaka huu chini ya makubaliano yaliyoasimamiwa na kanisa  katika juhudi za kuzuia machafuko kwenye  taifa hilo kubwa lenye utajiri wa madini ambalo halijawahi kushuhudia mabadilishano ya madaraka kwa njia ya amani tangu lijipazie uhuru wake kutoka Ubeligiji mwaka 1960.

Baada ya kuahilishwa mara kadhaa hasa kutokana na vurugu katika mkoa wa  Kasai  uchaguzi huo uliocheleweshwa sasa umepangwa kufanyika  Desemba 23, mwakani.

Kiasi ya makanisa 150 ya kanisa Katoliki yametoa mwito kwa waumini wao kuitikia wito wa kuandamana  leo Jumapili mjini Kinshasa  wakiwa na biblia mkononi ili kushinikiza kutekelezwa kwa makubaliano yaliyotiwa saini mwaka mmoja uliopita  yaliyokuwa na lengo la  kurejesha uthabiti nchini humo ikiwa ni pamoja na kumtaka Kabila kuondoka madarakani.

Si baraza la maaskofu nchini humo au mwakilishi wa serikali ya mjini Vatican  amezungumzia lolote kuhusiana na maandamano hayo.

Gavana wa mji huo Andre Kimbuta wenye watu milioni 10 amesema jana Jumamosi kuwa maandamano hayo  yasiyo na kibali hayawezi kuendelea kwa maelezo kuwa mji huo hauna maafisa wa polisi wa kutosha kusimamia maandamano  ya leo.

Hata hivyo msemaji wa waratibu wa maandamano  Leonie Kandolo alisisitiza kuwa licha ya kauli hiyo ya serikali maandamano ya leo yatafanyika na kuwa maafisa wa mji huo pamoja na polisi wanalazimika kutimiza wajibu wao kuwalinda raia na mali zao.

Waandaaji wa maanadamano  wametoa mwito kwa waumini kukusanyika baada ya misa ya asubuhi kwa ajili ya kushiriki maandamano leo.

Katiba ya Kongo inamzuia Kabila kuwania muhula wa tatu wa uongozi lakini makubaliano yaliyofikiwa yanamruhusu kusalia madarakani hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI  DW
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images