Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Klabu ya Galatasaray Yamuonea Huruma Eboue na Kumpa Dili Hili

$
0
0
Baada ya nyota wa zamani wa Ivory Coast Emmanuel Eboue kupoteza fedha zake kwa mke wake wa zamani hatimaye klabu ya Galatasaray ya Uturuki imempa nafasi ya kuwa kocha.

Eboue ambaye amewahi kutamba na klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Arsenal amepewa nafasi ya kuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 14 (U-14) ya klabu ya Galatasaray.

Galatasaray imemtaka Eboue kushughulikia leseni yake ya kufundisha soka ili aweze kuanza kibarua rasmi ndani ya timu hiyo ili kuokoa hali yake ya kimaisha.

Klabu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu soka ya Uturuki, imemwahidi mshahara mnono ili kusaidia kurejesha hali yake nzuri ya kimaisha.

Eboue amejikuta kwenye wakati mgumu wa maisha baada ya mahakama kuamuru mali zote kukabidhi kwa mke wake. Eboue na mke wake waliachana huku akiwa ameandika jina la mkewe katika sehemu kubwa ya mali zake ikiwemo nyumba za kifahari alizokuwa amezinunua kutokana na malipo yake kama mchezaji.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Disemba 26

Wanacha Wengine 1200 wa CHADEMA Watimkia CCM

$
0
0
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezidi kumomonyoka baada ya wanachama wao zaidi 1,200, wakiwemo viongozi wakuu wa Wilaya ya Ngorongoro, kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa viongozi waliohama ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya Ngorongoro, Samweli Ole Nakumbale, aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2015, Elias Ngorisa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVITA) Wilaya ya Ngorongoro, Wiliam ole Telele.

Wakizungumza baada ya kuomba kurudi CCM na kupokewa wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM za ubunge katika Jimbo la Longido juzi, walisema kuwa ubinafsi ndani ya Chadema umekithiri na vyeo katika chama hicho hutolewa kwa kuangalia sura na ukabila.

“Nilikuwa kada wa CCM nikachukuliwa na mafuriko ya mwaka 2015 nimekaa huko hakuna kipya ni usanii mtupu. Chama hakina hata ofisi ya wilaya kwenye baadhi ya mikoa lakini baada ya kulinganisha nikaona kweli nimepotea njia,” alisema Nakumbale.

Naye Ngorisa alisema mwanaume mwenye busara, ni yule anayejitafakari na kujitathimini katika maamuzi yake. “Nimekaa nimetafakari kwa kina, nikaona kweli kuna mahali nilikosea na ndiyo maana nikaamua kurudi CCM, kwa kuwa ilani yake inatekelezeka kwa vitendo na wananchi wanafurahia utendaji wa Rais John Magufuli”.

Alisema kibaya zaidi amekuwa akiandikwa vibaya kila siku kwenye mitandao ya kijamii kwa mambo ya uongo na uzushi yasiyokuwa na tija, hali ambayo imemfanya arudi CCM. 

“Nimetuhumiwa sana kwenye mitandao nikiitwa msaliti wakati si kweli, lakini sasa kutokana na tuhuma zao ambazo hazikuwa na mashiko nimeamua kurudi CCM.

“Nimekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa miaka 10 kupitia CCM na ukweli kuna mahali tulikosea baadhi ya viongozi, tulikuwa na maslahi binafsi badala ya kuhangaika na kero za wananchi, lakini Mungu ametupa Rais mzalendo aliyejitoa sadaka kwa ajili ya kupambana na mafisadi na kusimamia rasilimali za nchi,” alisema.

Kwa upande wake, mfanyabiashara maarufu katika Wilaya ya Longido ambaye pia ni Laigwanani wa mila ya jamii ya Kimasai, Eliya Malari alisema wazee wa mila walilala kwake siku 10 wakimuomba arudi CCM, na baada ya kutafakari utendaji wa Rais Magufuli, alikubali ombi la wazee hao na kuamua kurudi CCM na wafuasi wake

Afrika Imeamua.....Marais Afrika Nzima Kukutana January Kwa Ajili ya Mageuzi Makubwa

$
0
0
Wakuu wa nchi na Serikali za Afrika, wakiwemo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mapema mwakani wanatarajiwa kusaini makubaliano ya kuanzishwa kwa eneo huru la biashara la bara hilo (CFTA).

Wanatarajiwa kuwa na mkutano wa 30 wa kawaida Januari 28 na 29 mwakani katika ukumbi wa Nelson Mandela uliopo kwenye Kituo kipya cha Mikutano (AUC) jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huo utakaokuwa nakaulimbiu; “Kushinda Vita Dhidi ya Rushwa: Mwelekeo Endelevu wa Mabadiliko Afrika,” utatanguliwa na mkutano wa 35 wa Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu (Januari 22-23) na mkutano wa 32 wa kawaida wa Baraza la Utendaji (Januari 25-26).

CFTA itakuwa soko la zaidi ya watu bilioni 1.3 na wanatarajiwa kufika takribani bilioni mbili ifikapo mwaka 2025. Yatakaposainiwa, makubaliano hayo ya kibiashara yatakuwa makubwa zaidi barani humo yakizihusu nchi zote 54 za Afrika, na yatakuwa ya pili kwa ukubwa duniani. Makubaliano makubwa zaidi duniani ni ya Shirika la Biashara la Dunia (WTO) yaliyosainiwa mwaka 1994.

Kwa sasa Afrika ina masoko mawili makubwa yanayozihusu baadhi ya nchi, ikiwemo Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).

EAC yenye nchi sita wanachama za Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Tanzania na Kenya, ina zaidi ya watu milioni 170. Mkutano wa 18 wa kawaida wa wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia Januari 2012, uliamua kuwa hadi mwaka 2017 CFTA iwe imeanzishwa. Majadiliano kuhusu uanzishwaji huo yalianza rasmi Juni 2015.

Juni mwaka huohuo, wakati wa mkutano wa 25 wa wakuu wa nchi za AU uliofanyika Afrika Kusini, viongozi hao walikubaliana lianzishwe eneo huru la biashara ifikapo mwaka 2017 kupitia makubaliano na biashara huria za bidhaa na huduma.

Kwenye mkutano wa nne wa mawaziri wa biashara kutoka nchi za Afrika, uliofanyika hivi karibuni Niamey, Niger viongozi hao waliidhinisha muundo wa makubaliano na kuzingatia maendeleo, yaliyofikiwa kwenye majadiliano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano ujao wa wakuu wa nchi na serikali. CFTA itatoa uhakika wa mazingira ya uwekezaji, maendeleo ya viwanda na ongezeko la thamani ya bidhaa na huduma, hivyo kutengeneza fursa za ajira na vipato vya familia.

Hivi karibuni, wakati anafungua mkutano wa mawaziri mjini Niamey, Rais wa Jamhuri ya Niger Issoufou Mahamadou alipongeza maendeleo yaliyofikiwa katika majadiliano kuhusu makubaliano hayo.

CFTA na makubaliano mengine yakiwemo ya Kuharakisha Maendeleo ya Viwanda Afrika (AIDA), Programu ya Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP), Mpango wa Programu ya Maendeleo ya Miundombinu Afrika (PIDA) vitaiwezesha Afrika kufanikiwa katika malengo ya mabadiliko.

Makubaliano ya kuanzisha eneo huru la biashara Afrika, yanaweka ajenda kwa ajili ya mijadala kuhusu biashara ya bidhaa, biashara ya huduma na utatuzi wa migogoro. CFTA itashughulikia itifaki mbili, ikiwemo ya biashara ya bidhaa na itifaki ya biashara ya huduma. Makubaliano hayo yanatarajiwa kuboresha biashara baina ya nchi za Afrika.

Malengo makuu ya CFTA ni kuiwezesha Afrika kuwa na soko moja la bidhaa na huduma, litakalotoa uhuru kwa wafanyabiashara na uwekezaji na hivyo kutoa fursa ya kuongeza kasi ya kuanzisha umoja wa forodha barani humu.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
🎁OFFER SPECIAL MWAKA MPYA🎁
    PENDEZA SASA KWA PUNGUZO KUBWA LA BEI. 
       KATIKA KUSHEREHEKEA MSIMU WA SIKUKUU  @natural2162 TUNA  PUNGUZO LA 20% KWA BIDHAA ZETU ZOTE, IKIWA NI SHUKRANI KWA KUTUUNGA MKONO.

        BIDHAA ZETU ZOTE ZIMETENGENEZWA KWA MIMEA NA MATUNDA HAZINA KEMIKALI WALA MADHARA.
    KWA WANAUME TUNATIBU👇👇
☆Kukosa hamu ya tendo.
☆Kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo.
☆Maumbile madogo ya uume.
☆Kuchoka sana wakati wa tendo na uume kusinyaa  nk.
      @natural2162 tumeandaa tiba bora kabisa kama ifuatavyo:-
 
1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @220,000/=
2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @130,000/=
3VigRX  CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @170,000/=
4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @140,000/=
5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @220,000/=
6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @140,000/= 
 
     PIA KWA WANAWAKE WANAOPENDA KUWA NA MUONEKANO MZURI ZIPO ZA👇👇👇
1.Kuongeza hips, makalio na mapaja @180,000/=
2.Kushepu mguu (CHUPA YA BIA) @130,000/=
3.Kuwa mweupe bila sugu kwa:-
(a)mafuta @130,000/=
(b) Vidonge @150,000
4.Kurefusha nywele na kutokukatika ovyo @130,000/=
5.Kuongeza hips, makalio na mapaja kwa vidonge (YODI PILLS ORIGINAL) @200,000/=
6Kupunguza au kuongeza maziwa kuyasimamisha @130,000/=
7.Kubana uke na kuondoa uchafu ukeni @120,000/=
8.Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
        NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri na garantii ili kukuhakikishia ubora na usalama wa bidhaa za NATURAL BEAUTY CO

    Wasiliana nasi Popote
  ulipo duniani kwa (+255)
           0659618585 na
           0759029968
        UTAPATA HUDUMA.
👉🏻OUR WEBSITE:- www.naturalworldbeauty.og
👉🏻INSTAGRAM PAGE:-
@natural2162
@natural2162
@natural2162

         < WELCOME ALL>

Nyumba ya Rais Kabila yachomwa moto`

$
0
0

Nyumba ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila imechomwa moto katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na waasi, ambapo askari mmoja aliuwa.

Tukio hilo limetokea Desemba 25, 2017, ambapo taarifa zinasema kuwa waasi wa kundi lijulikanalo Mai Mai walijaribu kuiba mali kutoka makazi hayo ya rais yaliyoko eneo la Musienene, katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Wakati wa tukio Rais Kabila hakuwa kwenye nyumba hiyo ambayo iko kijijini maili 1,680 Mashariki mwa mji wa Kinshasa, huku kundi la Mai Mai na kundi la waasi wa ADF wakiwa washukiwa wa kwanza juu ya tukio hilo.

Hivi karibuni Rais Kabila amekuwa akipingwa na wanasiasa mbali mbali kwa kitendo chake cha kutaka kugombea nafasi ya urais kwa muhula mwingine.

PICHA: Tundu Lissu akiwa amesimama kwa miguu kwa mara ya kwanza

$
0
0
Hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika na ameanza rasmi kufanya mazoezi ya viungo katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma mnamo Septemba 7, 2017.

Picha kutoka Hospitali ya Nairobi imemuonesha Lissu akifanya mazoezi ya kusimma kwa msaada wa madaktari wa hospitali hiyo. Lissu ameanza mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze kutembea.

Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema “Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba  madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.

“Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni.

“Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu accordingly, Wasalaam,”  Mhe. Tundu Lissu.

Habari Ziloizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 27


Chadema Yapata Pigo Jingine, Diwani Siha Ajiuzulu na Kuhamia CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Siha ambaye pia ni diwani wa Gararagua, Zakaria Lukumay amejiuzulu uanachama wa (Chadema) na kujiunga na CCM.
 
Lukumay ametangaza kujiuzulu siku kadhaa baada ya aliyekuwa mbunge wa Siha (Chadema), Dk Godwin Mollel kujivua ubunge na kujiunga na CCM.
 
Sawa na Dk Mollel, diwani huyo amesema uamuzi wake unatokana na kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kutetea na kulinda rasilimali za Taifa.
 
Katika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha inayoonyesha iliandikwa Desemba 24,2017 Lukumay amesema anajiunga na CCM kwa sababu ndicho chama kinachogusa mahitaji ya Watanzania wote.
 
Aliyekuwa diwani wa Chadema wa Donyomurwak wilayani Siha,  Lwite Ndossi maarufu Nsonuu Desemba 19,2017 alijivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM.

Taarifa iliyotolewa na idara ya itikadi na uenezi ya CCM Desemba 19,2017 ilisema Ndossi alieleza sababu za kujiunga na CCM ni kuwa amejiunga na watu wanaofanya siasa za kufanya kazi za maendeleo na si kulumbana na maneno matupu.

RPC Shanna: Atakaefunga Barabara Na Kuchoma Matairi Mkesha Wa Mwaka Mpya Kukiona

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kufunga barabara kwa kuchoma matairi katika mkesha wa mwaka mpya na kupelekea usumbufu kwa watuamiaji wengine wa barabara kuacha kufanya kitendo hicho .

Amesema atakaejaribu kuchoma moto matairi kwenye mkesha huo,jeshi la polisi mkoani hapo litamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kiusalama inavyoendelea hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu ya mwisho wa mwaka ,kamanda Shanna alisema wanazidi kuimarisha doria katika pande zote za mkoa huo.
 
Alisema kipindi cha sikukuu ya x-mas hali ilikuwa shwarii hivyo wanaendelea na misako ya miguu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na doria hizo zitakuwa mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha watu waishi kwa amani .
 
Akielezea kuhusiana na hali ya uhalifu katika kipindi cha Januari hadi disemba mwaka huu ndani ya mkoa huo ,kamanda Shanna alisema wamefanikiwa kupunguza idadi ya makosa kwa kiwango kikubwa.
 
Kamanda huyo alisema,matukio ya makosa ya uvunjaji yamepungua kutoka 771 kipindi kama hicho 2016 na kufikia 233 mwaka huu ikiwa ni tofauti ya matukio 538.
 
Makosa mengine ni yale ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambayo yamepungua kutoka 31 mwaka jana hadi nane kwa mwaka 2017  tofauti makosa 23.
 
“Unyang’anyi wa kutumia nguvu  yameripotiwa makosa 43 ,kipindi kilichopita ilikuwa 112 tofauti makosa 69,:;na mauaji makosa yaliyoripotiwa januari hadi disemba mwaka huu ni 34 ,mwaka uliopita ilikuwa 126  tofauti ni makosa 92.” alifafanua kamanda Shanna.
 
Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo mara wanapotilia shaka kundi ama mtu ni mhalifu ,kwani kila mmoja ana wajibu wa kudhibiti vitendo vya uhalifu .
 
Kamanda Shanna ,alisema Pwani yenye utulivu,amani ,yenye kushikamana inawezekana endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.

Mbunge aliyejiuzulu Awapa Makavu CHADEMA....." Waulizeni milioni 360 za Ruzuku walimpa nani?”

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Molel amewataka wananchi wa Siha kutoogopa akisema ametazama mbali hadi kuhama Chama hicho na kudai kuwa hawatajuta.

Akiwa kwenye Kampeni Longido Mollel amesema amehoji kama CHADEMA hawanunui watu huwa wanapeleka wapi Tsh Milioni 360 za ruzuku wanayopata kama chama kwa mwezi.

Mollel amesema kwamba; "Niwaambie watu wangu wa Siha. Msiogope. Mliponichagua kuwa Mbunge nilitakiwa kulitetea taifa na kuitetea Siha. Cheo ni zaidi ya maslahi ya taifa na Siha. Msiogope nimetazama mbali na nimeona mbali hivyo hamtajuta. Nataka kuwamba Rais aliyoko madarakani analitetea taifa".

Godwin Mollel alijivua ubunge Disemba 14 mwaka huu kwa kusema kwamba; “Nimeona nia ya dhati ya Serikali CCM kutetea rasirimali za Taifa, nikaona niweze kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge ili niweze kwenda kujiunga kwa vitendo katika kulinda rasirimali za Taifa letu, aminini watu wangu wa Siha nimeona mbali katika maamuzi haya".

Marekani yawawekea vikwazo wataalamu wa makombora Korea Kaskazini

$
0
0
Marekani imewawekea vikwazo maafisa wawili wa Korea Kaskazini ambao inasema kuwa wamechangia kuundwa makombora ya nchi hiyo.

Wizara ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na kusema kuwa wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya masafa marefu wa Korea Kaskazini.
 
Baraza la ulianzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa marefu. Korea Kaskazini ilisema kwa hatua hiyo ni kama ya vita.

Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume hao wawili zinazofanywa nchini Marekani, na hata kutwaliwa kwa mali zao zilizo  nchini Marekani.

Wanaume hao wawili wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora.

Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo inasema kuwa yanaweza kufika nchini Marekani.

CCM yamjibu Askofu Kakobe baada ya kuikashifu serikali

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la FGBF lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam amekosa hekima na busara kwa kugeuza madhabahu ya kanisa kuwa jukwaa la kisiasa na kuanza kukashifu viongozi wa serikali akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Frank Kamugisha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Aksofu Kakobe kukosoa namna serikali inavyotenda mambo yake, akisisitiza kwamba Tanzania si nchi ya chama kimoja kama ambavyo viongozi wanataka kuigeuza na hivyo kuwataka viongozi wa serikali waanze kutubu.

Kamugisha amesema kuwa, wao kama viongozi wa CCM hawaweza wakakaa kimya wanapoona chama kinachafuliwa na viongozi wake ambao wanafanya kazi kwa niaba ya watanzania wakikashifiwa.

Aidha, alisema kuwa, siasa ni kwa ajili ya wanasiasa, na kama kiongozi wa dini ana jambo lolote analotaka kuzungumzia, kuna busara za kutumia na sio kutumia kanisa kusema hayo.

==>Msikilize Kamugisha hapa chini akizungumza,

Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu Uchi

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania.

Waziri Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika.

"Pale tunapoona kuna ukiukwaji, tufumbe macho tusijali malalamiko yanavyokuja kutolewa, maana ukiwagusa wasanii walikuwa wanakuja juu sana, lakini tunashukuru mkuu wa nchi kulisemea hilo, basi na sisi tumeongezewa nguvu basi hatutaachia suala hilo kuendelea kuharibu vizazi vyetu", amesema Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho.

NEC yathibitisha mgombea wa Chadema kujitoa kwa Nyalandu

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imethibitisha kumtoa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Singida Kaskazini mgombea kwa tiketi ya Chadema, David Djumbe.

Mgombea huyo ameondolewa kwenye orodha baada ya kutimiza masharti ya kujitoa katika uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema jana kuwa Djumbe alifuata maelekezo kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

“Kama Sheria inavyosema Kifungu cha 49(1)(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 mgombea anaweza kujitoa kwa kuandika barua na kuisaini yeye mwenyewe pamoja na ahadi ya kiapo cha sheria alichoapa mbele ya hakimu.

“Tume haimkubalii wala haimkatalii sababu ni hiari yake. Amewasilisha taarifa hizo na Tume imemfuta katika orodha ya wagombea,” alisema Kailima alipoulizwa jana kuhusu hatima ya mgombea huyo.

Desemba 20, Djumbe aliwasilisha nyaraka za kujitoa katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani akieleza kuwa jina lake lilipelekwa kimakosa.

Mkanganyiko ndani ya Chadema ndiyo uliosababisha jina la Djumbe kupelekwa NEC na kupitishwa kuwa mgombea ubunge Singida Kaskazini.

Wakati Chadema ngazi ya Taifa ikisema haitashiriki katika uchaguzi huo mpaka NEC itakapokutana na wadau kujadili changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa udiwani katika kata 43, uongozi wa chama hicho mkoani Singida ulipeleka Tume jina la Djumbe kuwa mgombea.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Shaban Limu alisema Djumbe aliteuliwa kugombea na kamati ya utendaji ya wilaya.

Alisema wakati anateuliwa uongozi wilaya na mkoa ulikuwa haujawasiliana na makao makuu kujua msimamo juu ya uchaguzi huo.

Jimbo la Singida Kaskazini liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, Lazaro Nyalandu kujivua uanachama wa chama hicho hivyo kupoteza nyadhifa zote ukiwamo ubunge. Alijiunga na Chadema.

Uchaguzi pia unafanyika katika majimbo ya Longido ambako matokeo ya uchaguzi wa ubunge ya mwaka 2015 yalibatilishwa na Mahakama; na Songea Mjini ambako aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, Leonidas Gama alifariki dunia.

Taarifa ya serikali kuhusu kuzimwa kwa 'chaneli' za bure kwenye ving'amuzi

$
0
0
Kufuatia uwepo wa malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu kukosa huduma ya runinga za bure pindi vifurushi katika visimbusi (ving’amuzi) vyao vinapomalizika, serikali imetolea ufafanuzi suala hilo kwa kueleza namna mfumo wa utendaji unavyotakiwa kufanya kazi.

Akijibu maswali ya watumiaji mbalimbali wa mtandao wa Twitter kuhusu urushwaji wa runinga za bure, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Abbas alisema, kwa mujibu wa sheria iliyopo sasa, vituo vyote vya runinga ambavyo vimepewa leseni ya FTA (Free to Air) vinapaswa kuonekana hata baada ya kifurushi kwenye kisimbusi kwisha.

Dkt. Abbas alisema kwamba, hadi sasa kuna vituo 16 vya runinga vya ndani ya nchi vilivyopewa leseni hizo, vikiwemo vituo vya ITV, Clouds TV na Channel 10.

Aidha, alifafanua kuwa, ili mtumiaji aweze kutazama hata baada ya kufurushi chake cha malipo kwisha, kituo cha runinga (mfano ITV) kinapaswa kuwalipa warushaji wa masafa (mfano Azam) ili ITV iweze kuonekana kwa wananchi hata ambao hawajalipia visimbusi vyao.

“… mfumo uko hivi: ili wewe uone bure hizo channeli kuna mzalishaji wa vipindi ambaye ni kituo cha TV na msafirisha masafa mfano StarMedia. Ili wewe uone bure kuna gharama huyo wa kwanza anatakiwa kulipia kwa wa pili. Asipolipia akakatiwa huduma hautaona. Kwa sasa ndio mfumo.”

Pia, Dkt. Abbas alitahadharisha kuwa, endapo kituo cha runinga hakutawalipa wasafirishaji wa masafa, watakatiwa huduma na hivyo kuwafanya wananchi washindwe kuweza kutazama runinga bure.

Kuhusu TBC kuonekana katika visimbusi vyote hata bila malipo, msemaji alifafanua kuwa, kila kisimbusi kinatakiwa kuweka TBC kupitia sera ya ‘must carry’ ambayo inaiwezesha kuonekana kwa wananchi bila malipo yoyote.

“Unapata TBC mda wote kwa sababu TBC anahadhi inayoitwa “must carry” ambaye mrusha masafa yeyote Tz lazima aioneshe TBC. Kama hupati channeli zingine za FTA muulize mtoa huduma wako. Majibu atakayokupa nijulishe na unipe jina la mtoa huduma wako,” aliandika Dkt. Abbas.

Alisema kuwa, kwa sasa serikali haina mfumo wa kuwaadhibu wamiliki wa vituo vya runinga wenye leseni za FTA lakini hawawalipi warusha masafa ili wananchi waweze kuona runinga hizo bure, badala yake, warusha matangazo hayo wanatawakati huduma kama hawajalipwa.

“…kwa kanuni iliyoanza Machi mwaka huu, mtoa huduma za TV asipolipa kwa msafirisha masafa anaweza kukatiwa huduma.”

Kuhusu Dstv na Azam kukata matangazo ya runinga za ndani baada ya kifurushi kwisha, Dkt Abbas alisema suala hilo lipo Baraza la Ushindani hivyo wananchi wasubirie majibu, na kwamba asingependa kulizungumzia kwa sasa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 28

Viongozi wa umma watakiwa kukabidhi orodha ya mali zao kabla ya Desemba 31

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho
 Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewahimiza Viongozi wa Umma kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kabla ya Disemba 31 mwaka huu.

Ametoa kauli hiyo jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inayomtaka kiongozi wa umma kupeleka tamko kwa maandishi lililo katika hati rasmi linaloorodhesha mali au rasilimali za kiongozi na familia yake kwa Kamishna wa Maadili kila mwisho wa mwaka.

Jaji Mstaafu Nsekela amesema kuwa fomu za tamko hilo zinapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya maadili ambayo ni www.ethicssecretariat.go.tz hivyo ametoa wito kwa viongozi ambao hadi sasa hawajapata fomu kutumia tovuti hiyo kupata fomu kwa urahisi.

“Kwa kuzingatia kifungu cha 9 (1) (a) na (c) cha Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma, viongozi wapya wanaochaguliwa au kuteuliwa wanatakiwa kujaza fomu hizi ndani ya siku thelathini baada ya kupewa wadhifa fulani pia anapofika mwisho wa kutumikia wadhifa huo anapaswa kujaza fomu na kuzirejesha katika ofisi yetu,” alisema Jaji Mstaafu Nsekela.

Jaji Mstaafu Nsekela amefafanua kuwa fomu hizo zinatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma zilizopo Jijini Dar es Salaam au katika ofisi zao za Kanda zilizopo katika Mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha, Mtwara, Tabora, Pwani na Mbeya.

Kwa upande wake Afisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo, Filotheus Manula amesema kuwa kujaza fomu hizo ni takwa la kikatiba hivyo Viongozi wa Umma wahakikishe wanajaza fomu hizo bila kudanganya.

“Ni kosa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(c) cha Sheria za Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kiongozi kushindwa kutoa tamko bila sababu ya msingi kwani sheria hizi hazimzuii kiongozi kumiliki au kuwa na mali nyingi bali mali hizo zinatakiwa kutolewa maelezo ya chanzo cha upatikanaji wake,” alisema Manula.

Aidha, Manula amefafanua kuwa kosa hilo linaweza kumpelekea muhusika kuonywa au kupewa adhabu ya kushushwa cheo, kusimamishwa, kufukuzwa kazi pamoja na kupelekwa Mahakamani.

Vile vile Manula amesema kuwa kwa sasa hali ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma inaridhisha kwani ukiukwaji wa maadili umepungua kwa kiasi kikubwa.

Makatibu Wakuu wajadili utekelezaji mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge

$
0
0
Na Veronica Simba
 Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, hivi karibuni walifanya kikao kujadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge.

Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

Aidha, kikao hicho pia kilijadili majukumu ya kila Wizara husika katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi huo.

Akifungua kikao hicho, Dkt. Mwinyimvua alieleza kuwa mahitaji ya umeme nchini kwa sasa ni makubwa kutokana na kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda hali inayosababisha huduma ya umeme wa uhakika kuhitajika zaidi ya muda mwingine wowote.

“Serikali ya Awamu ya Tano inaelekeza nchi kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, hatua za makusudi za kuongeza uzalishaji wa umeme kwa ajili ya viwanda zinahitajika.”

Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, akielezea umuhimu wa Mradi huo kwa Taifa alisema kuwa umeme wa uhakika unahitajika ili pamoja na mambo mengine kukidhi mahitaji ya mkakati wa kusambaza umeme vijijini ambao unaendelea nchini kote.

Awali, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi husika katika kikao hicho, Msimamizi wake, Mhandisi Leonard Masanja alieleza kuwa, Desemba 19 mwaka huu, Wizara ya Nishati ilitangaza zabuni ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi huo ambao utekelezaji wake unakadiriwa kuanza mwishoni mwa mwezi Februari 2018.

Alisema kuwa, mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, Rais John Magufuli aliamua kuanza utekelezaji wa ujenzi wa Mradi huo ambao ulibuniwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere miaka ya 1970.

Mhandisi Masanja aliongeza kuwa, timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), iliundwa ili kufanya maandalizi ya Mradi na baadaye kusimamia ujenzi mara baada ya Mkandarasi kupatikana. “Timu hiyo iliungana na timu ya wataalam kutoka Ethiopia katika utekelezaji wa jukumu hilo.”

Makatibu Wakuu walioshiriki au kuwakilishwa katika kikao hicho ni kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wengine ni kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.


Trump aitaka Zimbabwe kuacha kutumia Dola ya Marekani

$
0
0
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema utawala wake uko tayari kufanya kazi na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe lakini amesisitiza kuwa hilo litawezekana iwapo taifa hilo litaacha kuendelea kutumia Dola ya Marekani.

Amelitaka kutotumia dola hiyo na badala yake lianzishe mfumo utakaohakikisha linatumia sarafu yake ya Zimbabwe. Kwa miaka mingi Zimbabwe ilikoma kutumia sarafu yake na kutumia ile ya Marekani hali ambayo ilikosolewa vikali na wanauchumi.

Duru za habari zimenukuu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika, Don Yamamoto akisema Zimbabwe anapaswa kudhibiti uchumi wake na siyo kuendelea kutegemea sarafu ya nje.

“ Hivi leo hali ya uchumi wa Zimbabwe ni mbaya. Taifa hili linaagiza chakula kutoka nje, taasisi zake za kiuchumi hazipo katika hali nzuri. Wamelazimika kutumia Dola ya Marekani. Hawapaswi kutegemea sarafu ya Marekani au taifa lingine lolote la kigeni. Haya ndiyo mageuzi tunayopenda kuona yakifanyika sasa,” amenukuliwa waziri huyo akisema.

Amesema Marekani iko tayari kusaidia magaeuzi ya kiuchumi na kisiasa nchini Zimbabwe ili kurejesha taifa hilo katika hali yake ya kawaida. Hatua hiyo imekuja huku Rais Mnangagwa akiyataka mataifa ya magharibi kuliondolewa vikwazo taifa lake vilivyowekwa wakati wa utawala wa mtangulizi wake, Robert Mugabe.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images