Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Baba ashikiliwa kwa mauaji ya mwanae

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora  linawashikila watu watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto Leokadia Maganga, mwenyekiti pamoja na mtendaji wa kata ya Ndala wilaya ya Nzega mkoani Tabora, kwa tukio la mauaji ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka 11.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP), Wilbroad Mutafungwa amesema mtoto huyo inadaiwa aliuwawa na kutumbukizwa kwenye kisima cha maji katika kijiji cha Budushi kata ya Ndala wilayani Nzega Mkoani Tabora.

"Ni kweli tulipokea taarifa za tukio hilo la mtoto kukutwa katika kisima cha maji na baadae kuzikwa, tuliamua kwenda mahakamani kuomba hati ya kufukua maiti ili tufanye uchunguzi, baba mzazi wa mtoto huyo bado tunamshikila  kwa ajili ya upelelezi", amesema Kamanda Mutafungwa.

Sambamba na hilo Kamanda Mutafugwa amewaomba wananchi wawe wavumilivu katika kipindi hiki  ambacho Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi, ili kubaini chanzo zaidi cha mtoto huyo kufariki, na mara utakapokamilika watatoa taarifa zaidi ya tukio hilo.

Mbarawa: Ukitozwa Nauli Isiyo Rasmi Ripoti Vyombo Husika

$
0
0
WaziriI wa Kazi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, pamoja na kuwatakia Watanzania heri ya sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya ameagiza pia kuwaripoti mara moja kwa vyombo husika watu wanaowatoza nauli  isiyo rasmi na kuwataka wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini barabarani.

Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter,  akisema ipindi hiki cha sikukuu kimekuwa na changamoto kubwa za usafiri, ikiwemo kutozwa nauli ya juu, na kuwataka kutoa taarifa mara moja kwa vyombo husika.

“Napenda kuwatakia Watanzania wote kila la kheri katika msimu wa sherehe za Xmas & mwaka mpya 2018,wito wangu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri ni kuzingatia sheria na kanuni za barabarani, kwani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu kumekuwa na changamoto ya usafiri,  hivyo kwa abiria endapo utatozwa nauli za juu ya viwango vilivyowekwa usisite kuripoti kwenye vyombo husika kwa wakati”, ameandika Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni kumekuwa na tatizo la wamiliki wa vyombo vya usafiri kuongeza nauli kutokana na wingi wa watu wanaofanya safari zao kuelekea mikoani kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kusababisha ugumu wa usafiri.

Familia yasema Babu Seya, Papii Kocha walitabiriwa kutoka gerezani

$
0
0
Familia ya mwanamuziki  Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’  imeeleza jinsi  mchungaji wa Kanisa la Life in Christ Ministries  Zoe,  lililopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaam  alivyotabiri kutoka gerezani kwa wanamuziki hao.

Akizungumza  leo Jumapili Desemba 24 katika ibada ya  kumshukuru Mungu kwa miujiza aliyoitendea familia hiyo iliyofanyika katika kanisa hilo, mtoto wa Babu Seya Michael Nguza 'Nabii Nguza’ amesema utabiri huo sasa umekuwa kweli.

Amesema mchungaji wa kanisa hilo Nabii Joseph alitabiri mara tatu kuwa ndugu zake hao wataachiwa huru.

Babu Seya na Papii Kocha wamekaa gerezani miaka 13 na miezi minne wakikabiliwa na kosa la kubaka na kulawiti watoto 10 wa kike ambao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.

Waliachiwa huru Desemba 9, mwaka huu kufuatia msamaha wa wafungwa, ukiwahusisha waliofungwa maisha na waliohukumiwa kunyongwa uliotolewa na Rais John Magufuli,  muda mfupi baada kutoka gereza la Ukonga walikwenda katika kanisa hilo na kuombewa na Nabii Joseph kwa takribani saa tano.

Amesema nabii Joseph alitabiri kwa mara ya kwanza mwaka 2012 na mara ya pili mwaka 2014.

“Utabiri wa tatu ulikuwa Mei 21 mwaka huu. Nabii Joseph alisema amepokea neno la Mungu lenye ujumbe kuwa watu wawili ambao ni baba na mwanaye wataachiwa huru, mmoja atakuwa kijana na mwingine mzee,” amesema na kuongeza,

"Haya mambo si ya kutunga ni ya uhalisia kwa sababu naamini Mungu yupo na nilimuamini sana Nabii Joseph kwa kile alichokuwa akitabiri na nilikuwa naipelekea familia yangu ujumbe gerezani na iliupokea.”

Maadhimisho miaka 54 ya Mapinduzi kugharimu Sh1.2 bilioni

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itatumia zaidi ya Sh1.2 bilioni kwa maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kilele chake kitakuwa Januari 12 mwakani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed amesema hayo leo Jumapili Desemba 24,2017 ofisini kwake Vuga mjini Unguja alipotoa taarifa ya maandalizi ya sherehe hizo.

Amesema fedha hizo zinatarajiwa kutumika katika maandalizi ya siku ya kilele, ufunguzi wa miradi 49 ya maendeleo ya kiuchumi, miradi ya maji, majengo ya shule, umeme na barabara.

Waziri amesema miradi 33 itazinduliwa baada ya kukamilika na 16 itawekwa mawe ya msingi. Miradi hiyo ni ya taasisi za umma, jamii na ya wawekezaji.

Waziri Mohamed amesema Serikali imepiga hatua katika kufanikisha huduma za kijamii na maendeleo sambamba na lengo la Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kuunga mkono jitihada za Serikali katika kufanikisha maadhimisho hayo ambayo yatazinduliwa Desemba 30,2017 kwa kufanya usafi wa mazingira.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk Idriss Muslim Hijja amesema miradi iliyopendekezwa kuingizwa katika maadhimisho imefuatiliwa na kutolewa taarifa kwa sekretarieti ya halmashauri ya sherehe na maadhimisho ya kitaifa.

Amesema katika uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi ya miradi, viongozi wa kitaifa wa Serikali zote mbili wamejumuishwa wakiwemo marais, mawaziri na wastaafu wa pande zote mbili.

Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa Januari 12,2018 katika Uwanja wa Amani mjini Unguja ambako Rais Ali Mohammed Shein atakuwa mgeni rasmi.

Sumatra kusaka Mwarobaini wa usafiri mwishoni mwa mwaka

$
0
0
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Johansen Kahatano amesema kuanzia mwakani wataandaa mkakati wa mabasi kufanya kazi saa 24 na kupandisha nauli wakati wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Kahatano amesema hayo leo Jumapili Desemba 24,2017 alipozungumza na waandishi wa habari eneo la Ubungo kuhusu hali ya usafiri.

Amesema kumekuwa na changamoto ya usafiri takriban kila mwisho wa mwaka na kusababisha kero kwa abiria.

“Tumeliona hilo na sisi Sumatra tumeandaa mpango ambao tunafikiri unaweza ukawa suluhisho la adha ya usafiri hapa Ubungo; kwanza tunafikiria kuruhusu mabasi kufanya kazi saa 24 wakati wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka,” amesema.

Amesema pia wataweka nauli kubwa wakati wa msimu wa sikukuu ili abiria wasafiri kipindi ambacho nauli itakuwa ndogo.

Kahatano amesema mpango huo utaanza kufanyiwa kazi mwakani kwa kukaa na wadau wa usafiri na wananchi kuujadili.

Akizungumzia hali ya usafiri kituoni Ubungo amesema iko shwari kulinganisha na jana ambapo abiria walikuwa wengi na mabasi yalikuwa machache.

“Tumejitahidi kusaidia kupunguza adha hii kwa leo baada ya kuruhusu watu wenye magari yenye uwezo wa kupakia abiria kuja na kupatiwa vibali hapa Ubungo,” amesema.

Waliokufa maji Ziwa Tanganyika idadi yaongezeka

$
0
0
Ofisa  Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) mkoa wa Kigoma,  Amaniel Sekulu amesema miili sita ya watu waliozama katika ajali ya boti kugonga mtumbwi katika Ziwa Tanganyika imeopolewa.

Mpaka sasa idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Ijumaa iliyopita imefikia 19 kutokana na awali kuopolewa miili 13.

Akizungumza leo Jumapili Desemba 24, Sekulu amesema miili hiyo sita imeharibika kutokana na kukaa majini zaidi ya saa 50.

Amesema uopoaji wa miili hiyo ilikumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo wazamiaji kukumbana na hali mbaya ya hewa, mvua za mara kwa mara, mawimbi makubwa na kina kirefu cha maji.

Amesema Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)  na wananchi wenye ujuzi wa kuogelea ndio waliofanikisha kupatikana kwa miili hiyo.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa ikihusisha boti la Atakalo mola lililokuwa linatoka Kigoma mjini kwenda Kalya na mtumbwi wa MV Pasaka uliookuwa ukitoka kijiji cha Kalilani kwenda Sunuka.

MV Pasaka ilikuwa imebeba waumini wa Kanisa la Pentekoste waliokuwa wanakwenda kwenye mkutano wa injili na sherehe za sikukuu Krisimasi katika kijiji cha Sunuka.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 25

Majaliwa Mwiba Mchungu.....Avunja Mfuko wa Kuendeleza Pamba na Kuagiza wahusika wachunguzwe

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Pamba (CDTF) na amegiza wahusika wote wachunguzwe ili kubaini fedha walizokusanya zimetumikaje.

Alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki (Ijumaa, Desemba 22, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao alichokiitisha mkoani Shinyanga kufanya ufuatiliaji wa maagizo ambayo alikwishakuyatoa. Waziri Mkuu alishafanya vikao vitatu na wadau mbalimbali wa zao hilo.

Alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watendaji wa mfuko huo hawajatekeleza majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo lakini pia majukumu yao yanaingiliana na yale ya Bodi ya Pamba Tanzania (TCB).

“Kuna CDTF katika zao la pamba lakini hakuna inachofanya ambacho kinawalenga wakulima moja kwa moja. Tunaiondoa CDTF na kazi zake kuanzia sasa zifanywe na Bodi,” alisema.

“Waziri wa Kilimo peleka timu ya ukaguzi kuona wamefanya nini hadi sasa. Tunataka Bodi ifanye kazi na iulizwe maswali kuhusu zao hili. Endapo kuna jambo halijafanyika, Bodi iwe na uwezo wa kutoa majibu si kusubiri tena mtu wa chombo kingine aje kutoa majibu,” alisema Waziri Mkuu.

“Kwa muundo huu, Mkurugenzi wa Bodi anakaa tu, wakati akisubiri kazi yake ifanywe na CDTF,” aliongeza.

Mfuko wa CDTF unaundwa na wajumbe sita ambao ni wawakilishi wa wakulima wawili, wawakilishi wa wenye viwanda vya kuchambua pamba wawili, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba na Mkurugenzi wa Mazao kutoka Wizara ya Kilimo.

Mfuko huu uliundwa mwaka 1999 na Bodi ya Pamba (TCB) ili uwashirikishe wadau wa zao hilo kuondoa matatizo yaliyojitokeza kwenye sekta hiyo baada ya Serikali kujitoa kwenye uendeshaji wa moja kwa moja wa mazao nchini ikiwemo uzalishaji na biashara kutokana na mfumo wa soko huria.

Desemba mwaka jana, Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba alifikia uamuzi kama huo na kuamua kusimamisha shughuli zilizokuwa zinafanywa na Mfuko wa Kuendesha Zao la Korosho Nchini (CIDTF) ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.

Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam, Waziri Tizeba alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mfuko huo kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu pamoja na kuwapo kwa malalamiko ya muda mrefu kuhusu utendaji wa mfuko huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Dr. Shein: Wala Rushwa CCM Wajadiliwe, Watimuliwe

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa chama kutosita kuwajadili wanachama ambao wanakiuka maadili ya chama hususan vitendo vya rushwa.

Pia, amesema wanachama hao wakishajadiliwa hawatasita kufukuzwa ndani ya CCM na kwamba imefikia hatua baadhi ya watu hao ambao wanafanya vitendo hivyo wanaonewa haya.

Hayo ameyasema jana , katika sherehe za kumpongeza kuchaguliwa tena nafasi ya Makamu Mwenyekiti, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa Mjini ,ambapo aliwataka viongozi hao kutofumbia macho vitendo hivyo ndani ya CCM.

Katika maongezi yake Dk.Shein aliongeza kuwa vitendo hivyo vya rushwa si jambo jipya ndani ya CCM na kwamba inaharibu sana maadili ya chama.

“Vitendo hivi vya rushwa ndani ya CCM si suala jipya lakini tunaoneana huruma, tunafichiana na baadae tunalalamikiana wakati chama ni ya wanachama hivyo lazima tushirikiane,”alisema.

Makamu Mwenyekiti huyo Dk.Shein alisema utaratibu wa chama kinajielekeza wanachama ambao wanakiuka maadili wanapaswa kujadiliwa kuanzia ngazi za tawi na baadae inawasilishwa kwenye uongozi wa juu na kuchukuliwa hatua.

Alieleza chama kipo kwa wanachama ikiwemo kwenye mashina na matawi na taratibu zinafafanua kuwa ngazi hizo ndipo mambo hayo yanazungumzwa kwamba mwanachama akikiuka maadili anajadiliwa kwenye tawi.

“Anajadiliwa kwenye kamati ya tawi na shina, kamati ya jimbo, kamati ya wilaya, Halmashauri ya wilaya ndipo wanapojadiliwa huku kwamba anafaa ama hafai hachukuliwe hatua za kufukuzwa ama asichukuliwe,”alisema.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema utaratibu unaeleza kuwa baada ya kujadiliwa wanachama hao taarifa itapelekwa kwenye ngazi za juu na kufanya maamuzi ya kumfukuza.

“Nachotaka kueleza kuwa kazi hii ni ya wote na kwamba jukumu kubwa ni kuhakikisha CCM inashinda mwaka 2020 msiwafiche watu ambao wanataka kuharibu chama, na kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwa ndumi la kuhili tunayoyasema sio tunayoyafanya,”alisema  Makamu Mwenyekiti.

Alifafanua kuwa kazi ya siasa ya kipindi hiki lazima kuongeza kasi ambapo kuna mambo zaidi ya kuyafanya na hata Mwenyekiti Dk.John Magufuli alisisitiza kwenye mkutano mkuu uliofanyika Desemba 18, mwaka huu mjini Dodoma.

Mbali na hilo, Dk.Shein aliwataka viongozi wa serikali kutambua na kuheshimu CCM kutokana na kuwa wanafanya kazi ya utekelezaji wa chama hivyo hawanabudi kukithamni.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Dk.Abdallah Juma Saadalla(Mabodi), alisema wanachama kutoka visiwani humo wanatarajia kusimamia vyema ibara ya tano ya kuhakikisha CCM inashinda mwaka 2020.

Aliongeza kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na mawimbi makubwa sana lakini watu walioshiriki walikuwa wanastahili.

“Bado tunafanya juhudi za kutoa elimu kwa viongozi wa chama kuhusu suala la kuzingatia kanuni na maadili ili kuhakikisha wanasongesha gurudu la uchaguzi wa mwaka 2020″alisema.

Dk.Mabodi ameeleza  kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa wagombea wote ambao wamepita kwenye uchaguzi huo asilimia kubwa wana maadili ya kutosha.

Ray C awapasha wanaokaa uchi

$
0
0
Mkongwe kwenye muziki wa bongo fleva Rehema Chalamila Ray C amewafungukia mavideo Vixen ambao wamekuwa wakitokea kwenye video mbalimbali za muziki huku sehemu ya miili yao ikiwa nusu utupu.

Ray amefanguka kuwa tabia ya kukaa uchi katika video haitokani na maoni ya waongozaji bali, hata tabia za mavideo vixen wenyewe hutaka na hutengeneza mazingira ya kukaa uchi jambo ambalo si zuri kwa afya ya muziki wa Bongo fleva.

“Nina wafahamu vizuri mavideo vixen wa bongo, baadhi yao hutengeneza mazingira ya wao kuonesha maumbo yao na kwa kujiweka utupu, si maoni ya waongozaji tu, bali hata video Queen wenyewe ni tatizo,” alisema Ray C

Godbless Lema Awakumbuka Wafungwa....Amuomba Rais Magufuli Aingilie Kati la Wakili Mwale

$
0
0
Leo  ikiwa ni sikukuu ya Krismasi, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema amewatakia kheri wafungwa na mahabusu nchini.

Lema ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) katika salamu alizotoa jana Jumapili Desemba 24,2017 amekumbusha kilichomtokea sikukuu ya Krismasi mwaka jana akitaka wenye mamlaka kusimamia haki kwa weledi.

‘’Wakati ninawakumbuka na kuwatakia heri ya Krismasi mahabusu na wafungwa wote nchini ni muhimu watu wote mlioko kwenye vyombo vya sheria mjue wajibu wenu, unapokosa utu na upendo maana yake ni kuumiza watu na kutesa watu mahali fulani,” amesema Lema.

Amesema, “Krismasi mwaka jana nilikuwa nimeshikiliwa kama mahabusu Gereza Kuu Arusha kwa kunyimwa dhamana, tukiwa gerezani mimi na wenzangu tulikuwa tunaandaa sikukuu ya Krismasi.”

Lema amesema anawakumbuka rafiki zake wengi aliokaa nao vizuri ambao wengine wamefungwa na baadhi bado wako mahabusu.

“Kwa kweli zaidi namkumbuka sana wakili Median Mwale ambaye amekuwa mahabusu kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita. Ninamuomba Rais aingilie kati suala la Mwale, kwa kweli huyu mtu inatosha kuwepo magereza kwa zaidi ya miaka sita bila kuhukumiwa. DPP najua unajua watu wengi wako magereza, nguvu uliyopewa na sheria inapokosa upendo basi nguvu hiyo inakuwa ni ukatili,” amesema Lema.

Amesema Krismasi mwaka jana alikuwa gerezani baada ya ibada iliyoongozwa na Askofu Lebulu (Josephat - Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha) walifanya maandalizi ya kula chakula ambacho familia zao  ziliwapelekea.

“Tukiwa tunakula wakili Mwale alisema, Lema wewe utatoka na mimi na wenzangu namuomba Mungu Krismasi inayokuja niweze kuwa nje, kwa bahati mbaya wakili Mwale na rafiki zake bado wameshikiliwa gerezani.”

Amesema kwa kipindi alichokuwa gerezani ameelewa huzuni za familia na watuhumiwa, ndiyo sababu Rais alipowasamehe wafungwa na hasa wenye makosa makubwa alimshukuru kwa sababu anajua huzuni ya kukosa uhuru.

Rose Muhando atema cheche kwa wanaomkebehi baada ya kujiunga CCM

$
0
0
Msanii wa muziki wa Injili nchini Tanzania, Rose Muhando ameamua kufunguka ya moyoni baada ya kupokea maoni mengi ya watu wakimponda kuhusu maamuzi yake ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

Rose Muhando amesema wanaomponda na kumkebehi anawachukulia ni watu wa kawaida kwani hawezi kujifunza kwa watu walioshindwa huku akidai ameshazoea kusemwa.

“Watu wengine hawaelewagi nini wanachoongea, wanaongea ili waonekane nao wanaongea. Mimi ni mtu ambaye ninayejitambua sawa eehhh!! mimi hata sijali, nimeshazoea kutukanwa kwahiyo hata sihangaikagi na maneno yao. 

"Mimi ni funzi kwa walioshindwa na nimeondoka kwa walioshinda, walioshindwa wana maneno mengi kutokana na nilishaimba uoga wako ndio umasikini wako, Mimi siwezi kuishi kwa uoga kwenye nchi yangu kwani ni maamuzi yangu na sijavunja sheria ya nchi na ningeogopa zaidi kama ingekuwa ni dhambi.”amesema Rose Muhando kwenye mahojiano yake na E-Gospel ya Radio E-FM.

Mapema mwezi huu kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma, Rose Muhando alialikwa kutumbuiza kwenye mkutano huo na kabla ya kukaribishwa Jukwaani, Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema Rose na Kundi lake wamekuja na maombi mawili likiwemo la kujiunga CCM na kutumbuiza huku akisema kuwa vyote vimekubaliwa.

Awali Rose Muhando hakuwa kwenye upande wowote wa vyama vya kisiasa na amesema kujiunga CCM au Chama chochote ni maamuzi yake na sio dhambi wala kosa kisheria.

Neno la Rais Magufuli kwa Watanzania Katika Sikuu ya X-Mass

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwatakia heri Watanzania wote katika kusherehekea siku ya Christmas na mwaka mpya.

Magufuli ametoa salamu zake hizo kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ambapo rais amewataka Watanzania kusherehekea sikukuu hizo kwa utulivu na amani na kuwataka Watanzania mwaka 2018 kuwa pamoja ili nchi iweze kufanikiwa zaidi na zaidi.

Mbunge Hussein Bashe awaomba radhi watanzania

$
0
0
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amewaomba radhi wananchi wa jimbo lake na watanzania kwa ujumla kama atakuwa aliwakosea kwa namna moja ama nyingine wakati akitekeleza majukumu yake kwa mwaka 2017.

Bashe ametoa rai hiyo kupitia salamu za Christmas na Mwaka Mpya alizozitoa ambapo pia ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwa miradi ambayo imetekeleza jimbo kwake.

Isome hapa chini barua ya salamu za Christmas iliyotolewa na mbunge huyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Apata Ajali na Familia Yake

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Juma Kilimba amepata ajali ya gari lake kupinduka leo akiwa na familia yake, wamepelekwa katika hospital ya Wilaya ya Kiomboi kwa ajili ya matibabu.

Mke wake na watoto wawili wamepewa rufaa, lakini yeye na wanae wengine wawili wapo Hospitali ya Wilaya Kiomboi. Mtoto mmoja hawezi kusafirishwa sababu hali yake sio nzuri.

Taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu

Barnaba Aamua Kuachana na Muziki

$
0
0
Ikiwa zimebaki siku sita tu kabla ya kuumaliza mwaka 2017 na kuingia 2018, staa wa Bongofleva Barnaba Classic ametangaza kuwaaga mashabiki wake kwa mwaka huu na atakuwa kimya kimziki kwa muda.

Mkali huyo wa sauti na uandishi kwenye kiwanda cha mziki Bongo, ameweka wazi kuwa ukimya wake utaanzia kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kujipanga namna ya kuuanza kwa kishindo mwaka 2018.

“Nikiwa najitoa kwenye mitandao ya kijamii kidogo, ningependa kuwatakia mashabiki, marafiki na familia yangu Heri ya Christmas na Mwaka Mpya”, amefunguka Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Pamoja na kujitoa kwake nyota huyo anayetemba na ngoma yake ya Mapenzi Jeneza ameongeza kuwa anajiweka vizuri kuanzia mwonekano mpaka sound ya hit zake zijazo.

“Ninapumzika kidogo ili kuweka mipango yangu vizuri kwaajili ya mwaka 2018. Nitawaletea Barnaba mpya mwenye kila jipya kimuziki na hata Sound” ameongeza.

Kardinali Pengo Awataka Watanzania Wamuunge Mkono Rais Magufuli

$
0
0
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo amewataka wananchi kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kufufua uchumi.

Akihubiri wakati wa ibada ya mkesha wa Krismasi jana Jumapili Desemba 24,2017 katika Kanisa la Mtakatifu Maurus lililopo Kurasini, Kardinali Pengo amesema wananchi wamuunge mkono Rais kwa kufanya kazi badala ya kuwa walalamikaji.

"Magufuli na wasaidizi wake tuwaunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo," amesema.

Kardinali Pengo amesema watu wanapofanya kazi kwa bidii nchi inakuwa na amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo.

"Wakati umefika wa watu kufanya kazi usiku na mchana, hilo likifanyika nchi itaendelea kuwa na amani. Muda wote uwe wa kufanya kazi bila kujali ni usiku au mchana, tupumzike kidogo kwa ajili ya kupata usingizi," amesema.

Kardinali Pengo amesema amani ya kweli duniani haitokani na viongozi waliopo madarakani bali wananchi wenyewe.

Amesema kila mtu afahamu kwamba chimbuko la amani ni kufanya kazi halali inayopendeza machoni mwa Mungu.

Amewataka wananchi kuliombea Taifa na viongozi wake ili waendelee kusimamia ujenzi wake.

Askofu Gwajima Ahubiri Mafanikio na Namna ya Kuwa Juu Kimaisha

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema hakuna mtu anayeweza kupata mafanikio kwa kuanzia juu.

Askofu Gwajima amesema hayo leo Jumatatu Desemba 25,2017 akihubiri katika ibada ya Krismasi. Amesema anayeanzia juu ipo siku atashuka chini.

Amesema kwa kawaida mafanikio ya mwanadamu yeyote duniani ni lazima yaanzie chini.

"Hata Yesu alizaliwa kwenye hori la ng'ombe, sehemu ya chini kabisa lakini ndiye aliyetukomboa na dhambi. Ogopa kilichozaliwa kwenye hori, ukiona mtu ameanzia juu jua kuna siku atashuka," amesema.

Askofu Gwajima amesema ingewezekana Yesu kuzaliwa sehemu ya heshima lakini Mungu alitaka iwe hivyo kudhihirisha utukufu wake kwamba, kilichozaliwa kwenye hori la ng'ombe ni kikuu.

Amesema chochote kinachoonekana kinyonge na kidhaifu leo, kisidharauliwe kwa sababu ipo siku kitaheshimiwa.

Akitoa mfano amesema hata yeye alianzia chini kwa kuuza mihogo na barafu.

Amewatia moyo waumini walio hatua ya awali ya maisha akiwataka kutokata tamaa kwa sababu kuna wakati wa kuinuliwa.

"Niwaambie tu msiogope, aliyeanza kwa udhaifu atamaliza kwa heshima," amesema.

Amewataka kujenga tabia ya kuwasikiliza hata wale aliowaita waropokaji kwa sababu kuna wakati Mungu anaweza kuwatumia wakawa na ujumbe wenye kujenga.

Nyota wa Mpira, Emmanuel Eboue Atamani Kujiua Baada ya Kufilisika

$
0
0
Staa wa soka wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama Arsenal na Galatasaray ya Uturuki Emmanuel Eboue amedai  kufilisika  baada ya talaka, iliyompa mali zote mkewe Auerilie Bertrand

Eboue kwa sasa ana umri wa miaka 34 na anaitumikia adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja na FIFA kwa kushindwa kumlipa wakala wake.

Eboue licha ya kutokea katika maisha magumu Ivory Coast alifanikiwa kutengeneza pesa nyingi akiwa katika Ligi Kuu England akiitumikia Arsenal kwa miaka saba.

Beki huyo wa zamani wa Arsenal kwa sasa yupo katika maisha magumu na analala chini kwa rafiki yake huku akishindwa kulipia pesa nguo zake ziende dry cleaner, hivyo analazimika kufua kwa mikono. Eboue anatajwa kuelekea kufilisika kutokana na kutalakiana na mkewe.

Hali hiyo imemfanya Eboue kuwa masikini  kutokana na utajiri wake wote kumuandikisha mkewe. 

Kisheria wakiachana mali zote zitakuwa za mwanamke ambaye amezaa nae watoto watatu, jambo ambalo Eboue linamfanya aumie kichwa na kuweka wazi kuwa mara kadhaa linamjia wazo la kujiua kichwani kwake na anaomba Mungu aliepuke.

 Eboue ameichezea Arsenal kwa miaka saba kabla ya mwaka 2011 kuamua kujiunga na Galatasaray ya Uturuki.

“Pesa zote ambazo nilikuwa naingiza nilikuwa natuma kwa mke wangu kwa ajili ya watoto wetu, nikiwa Galatasaray Uturuki nilikuwa naingiza euro milioni nane na nilikuwa namtumia euro milioni 7, chochote alichokuwa anataka nisaini nilikuwa nasaini”-Eboue

Harmorapa Akiri Kwenda Kwa Mganga wa Kienyeji Kisa Penzi la Wema Sepetu

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kusema kuwa katika mwaka 2017 amehangaika kulipata penzi la mwanadada Wema Sepetu kiasi cha kuamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mara tatu ili aweze kumpata mrembo huyo.

Harmorapa akiongea  kwenye kipindi cha eNewz cha EATV amedai kuwa baada ya kuhangaika kwa marafiki zake Wema Sepetu na kugonga mwamba aliamua kwenda kwa babu (mganga) ambapo amedai kwa mara ya kwanza aliambiwa apeleke kuku mweupe, na alipeleka huyo kuku lakini aliporudi mjini Dar es Salaam mambo yake yakawa bado vile vile.

"Nimemuendea kwa babu Wema Sepetu mara tatu, nilipokwenda mara ya kwanza niliambiwa nipeleke kuku mweupe, nikapeleka zangu yule kuku mganga akafanya yake lakini niliporudi mjini sikuona mabadiliko yoyote yale, nikamfuata tena babu akaniambia nipeleke vitu vingine viwili ambavyo hapa nashindwa kuvisema" alisema Harmorapa

Harmorapa aliendelea kufunguka jinsi ambavyo amehangaika  kulitafuta penzi la Wema Sepetu na kudai ilifika wakati aliambiwa apeleke mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu au mchanga ambao mwanadada huyo ametemea mate, kitu ambacho Harmorapa amedai kilikuwa kigumu sana kwake kwa sababu hapati nafasi ya kukutana live  na Wema Sepetu.

Hata hivyo Harmorapa kwa sasa amesema amemwachia Mungu juu ya jambo hilo baada ya kuona harakati za kwa mganga wa kienyeji zinakwama.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images