Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wanajeshi FEKI wawili wakamatwa Dar es Salaam

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kutumia sare za Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ) kufanya matukio mbali mbali ya kihalifu.

Wakati akizungumza na wanahabari jana Disemba 22, 2017 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Lainon Fratenus (20) na Noel Cleophace Wagesa (30) wote wakazi wa Kigogo.

“Jeshi la Polisi mnamo Disemba 15, 2017 majira ya saa sita usiku maeneo ya Lugalo Kawe polisi wakiwa dolia walifanikiwa kukamata wahalifu wawili wakiwa wamevalia sare za JWTZ na kisu kimoja huku wakitumia gari namba T 306 CRU Toyota Carina rangi ya fedha, wanatuhumiwa wanasadikiwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya uporaji jijini Dar es Salaam,” amesema.

SACP Mambosasa amesema watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima na matukio yote waliyowahi kufanya na baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa watapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 23

Mwanajeshi Aliyeshambuliwa DRC Congo Afariki Dunia

$
0
0

Askari wa Tanzania aliyejeruhiwa katika shambulizi lililoua wengine 14 walio katika vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ameripotiwa kufariki dunia.

Kifo hicho kinaongeza idadi na kufikia waliouawa katika shambulizi hilo kufikia 15. Askari 44 walijeruhiwa.

Umoja wa Mataifa (UN) umeelezea shambulizi hilo ni tukio baya zaidi lililovikumba vikosi vyake katika kipindi cha miaka 25.

Pia, UN imetuma rambirambi kwa Serikali ya Tanzania na ndugu waliopoteza wapendwa wao.

Katika ujumbe wa Twitter, ujumbe maalumu wa UN ulio DRC (Munusco) umesema askari huyo ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika shambulizi la Desemba 7,2017.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa mbali ya kueleza kuwa, “Umoja wa Mataifa umehuzunishwa na kusikitishwa kutokana na mauaji hayo.”

Mashambulizi hayo yanadaiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la ADF waliojichimbia katika misitu ya Congo.

Umoja wa Mataifa umeanza uchunguzi kwa kina kuhusu shambulizi hilo na umeahidi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo.

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix amesema uchunguzi unafanywa kwa kuzingatia vigezo vyote vya kimataifa.

Amesema baada ya kukamilika wataalamu watafanya uchambuzi na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuzuia mauaji kama hayo kujirudia.

“Uchunguzi utafanyika kwa mbinu ambazo zinatakiwa. Hitimisho na mapendekezo yatachambuliwa kwa kina na kuzingatiwa kwa hali ya juu na kwa haraka iwezekanavyo,” amesema baada ya kutembelea kambi ya Semuliki iliyoko Kivu Kaskazini.

Tanzania yasisitiza kuzidisha ushirikiano DRC

$
0
0
Waziri wa ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi akipokea maelezo katika kambi ya MONUSCO Beni 

Waziri wa ulinzi wa Tanzania, Hussein Mwinyi ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazo shiriki katika kuleta amani mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mwinyi alitoa wito huo siku ya Ijuma alipowatembelea wanajeshi wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa shambulizi la Disemba 7, 2017.

Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuwawa na wengine 44 kujeruhiwa walipo shambuliwa na waasi wasiojulikana hadi hii leo katika kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Beni, Waziri Mwinyi alisema amefika kuwapa pole wanajeshi wa Tanzania na kuwatembelea walojeruhiwa pamoja na kuwapa moyo kuendelea na jukumu lao la kurudisha amani katika eneo la mashariki ya Kongo.
Akizungumzia uchunguzi unaoendelea kuhusu shamblizi hilo, Mwinyi amesema hadi sasa hawana habari zaidi, "sasa hivi ni mapema sana kusema fulani amefanya hivi. Hatuna uhakika, UN pia haina uhakika na ndiyo maana tunasema ni lazima uchunguzi ufanyike."

Anasema uchunguzi ukifanyika utawawezesha kujipanga vyema zaidi ili tukio kama hili lisitendeke tena au likitendeka wawe tayari kukabiliana nalo, akitoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya pande zote zinazohusika na shughuli za kulinda na kurudisha amani mashariki ya Kongo.

IGP Sirro Atoa ONYO Zito kwa Waliojipanga Kufanya Uhalifu Msimu Huu wa Sikukuu

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amefunguka na kuwataka watu wanaofikiria kutaka uharifu waache mara moja kwani wasipofanya hivyo wanaweza kujikuta wameishia gerezani au kukatishwa uhai wao na wakashindwa kusherehekea sikukuu.

Simon Sirro ametoa kauli hiyo mkoani Lindi, alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari. 

Kamanda Sirro amesema mtu yeyote anayefikiria kufanya vurugu au vitendo vya uhalifu wa namna mbalimbali,ikiwemo wa kutumia siraha ni vema akaacha, vinginevyo anaweza akaishia gerezani au kupoteza maisha kabla ya hata hajashehelekea sikukuu hizo.

"Nasema tumejipanga vyema karibu timu zetu zote, zikiwemo za upelelezi, za kiinterijensia na timu zetu za operesheni nazo zimejipanga kwa ajili ya doria zikiwemo za helkopta, majini kila mahali kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani na utulivu ndani ya Taifa lao" Alisema Sirro.

Aidha Sirro alisema kuwepo kwa amani na utulivu kutawafanya wananchi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara kutekeleza majukumu yao vizuri katika kujiletea maendeleo ndani ya nchi yao.

Mbali na hilo IGP Sirro, ameonya kwa kusema wale wanaofikiria kutumia silaha waachane na mpango huo  mara moja , kwa kuwa ni vigumu kumkamata mtu aliye na silaha na hivyo kitakachotokea ni ama mmojawapo kukatishwa uhai wake, huku akiwataka waalifu kujiuliza mara mbili kabla ya kuchukuwa silaha kwa lengo la kufanya uhalifu.

Ndugai akosoa upangaji vituo vya kazi kwa walimu

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwa nini inapoka madaraka ya halmashauri.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23,2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji Tamisemi ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni Tamisemi hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.

Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.

Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.

"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.

Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.

Polisi yanasa wasichana wanaotumika kama “Chambo” kupora pikipiki

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia wasichana wawili kwa kosa la kujihusisha na upangaji njama wa wizi wa pikipiki.

Wakati akizungumza na wanahabari jana  Disemba 22, 2017 jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo, SACP Lazro Mambosasa alisema wasichana hao wanaofahamika kwa majina ya Fatuma Jumanne (19) na Nasra Bakari (19), hutumika kama chambo kukodisha pikipiki kisha kuzipeleka kwa wakabaji.

“Watuhumiwa hawa walikamatwa baada ya askari kupokea taarifa ya tukio la unyang’anyi huko Ukonga Mazizini ambapo Mussa Hosea dereva wa bodaboda alikodiwa na wasichana hao kwa lengo la kuwapeleka mazizini, na wakati wanatoa pesa walijitokeza vijana watatu na kumkaba dereva wa pikipiki na kisha kutoroka nayo huku wasichana hao wakitoroka eneo hilo katika mazingira yasiyo eleweka,” alisema.

SACP Mambosasa alisema polisi walipowahoji wasichana hao, walionyesha nyumba ilikofichwa pikipiki hiyo, huko Ukonga Mazizini kwa Kapteni Mstaafu wa JWTZ Egno Paul (66).

Katika tukio lingine, SACP Mambosasa amesema mnamo Novemba 11 mwaka huu maeneo ya Vijibweni na Mbagala Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata walinzi watatu wa kampuni ya Supreme International Guard waliokuwa zamu siku ya tukio la wizi wa mashine ya boti HP 85 Yamaha mali ya Wizara ya Mifugo na uvuvi yenye thamani ya milioni 18, iliyokuwa imeegeshwa kwenye ofisi ya TAFICO Kigamboni.

“Watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na tukio hilo na kwamba mashine hiyo wameiuza Ilala kwa Bwana Katanga kwa bei ya Tsh milioni 2.5. Katanga alipokamatwa alieleza kuwa boti hiyo imesafirishwa kwenda Kigoma na ndipo yakafanyika mawasiliano na mashine hiyo kurudishwa jijini Dar es Salaam,” amesema.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Ramadhan Omary (41), Mohamed Abdallah (40), Rahis  Faiya (29) na Mikidadi Hussein (40). Amesema upelelezi kwa watuhumiwa wote unaendelea na ukimalizika watapelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.

Mwanamke achomwa moto na mpenzi wake kwa kukataa kuchumbiwa naye

$
0
0
Mwanamke mmoja ajulikanaye kama Sandhya Rani mwenye umri wa miaka 25 huko Kusini mwa nchini India ameuawa kwa kuchomwa moto na mpenzi wake baada ya kukataa kuchumbiwa naye.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo, mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona mwanaume huyo akifuata mwanamke huyo na wakaanza kuzungumza kwa kubishana na ndipo mwanaume huyo alipochukua mafuta ya taa aliyokuwa ametembea nayo na kummwagia binti huyo kisha kumuwasha moto.

Inaelezwa kuwa watu walijaribu kumwokoa binti huyo lakini alikuwa ameungua sana na alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali. 

Inaelezwa pia kuwa wawili hao wamewahi kufanya kazi ofisi moja. Polisi jimboni humo tayari wamemkamata mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina la Karthika Vanga.

Mwalimu akamatwa kwa kubaka wanafunzi 9 wa darasa la kwanza

$
0
0
Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya mkoani Mara limemkamata na kumfikisha mahakamani Mwalimu wa Shule ya Msingi Itiryo kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi 9 wa darasa la kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, alithibitisha kuwa wamemkamata Mwalimu Swamwel Daniel ambaye anatuhumiwa kuwabaka wanafunzi wa darasa la kwanza wenye umri kati ya miaka 7 hadi 9.

Kamanda Mwaibambe alisema kuwa mwalimu huyo anadaiwa kutenda kitendo hicho kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 30 Novemba hadi tarehe 6 Disemba. Aidha amesema walimkamata mtuhumiwa huyo alipokuwa akijiandaa kutoka nje ya nchi.

Mwalimu hiyo alifikishwa mahakamani Disemba 12 mwaka huu na kufunguliwa kesi ya jinai namba 682 ambayo inatarajiwa kutajwa Disemba 28 mwaka huu.

Aidha, Mwaibambe alisema kuwa ushahidi na vitu vyote vinavyotakiwa katika kesi hiyo vimekamilika na hivyo ameiomba mahakama kama itawezekana kesi hiyo isikilizwe ndani ya muda mfupi.

Urasimu waiondoa kampuni ya umeme Kenya , yajipanga kuhamia Tanzania

$
0
0
Kampuni ya nchini Sweden iliyotaka kujenga mtambo mkubwa zaidi Afrika Mashariki wa kufua umeme kwa kutumia upepo huko Malindi, Kenya,  kwa gharama ya shilingi za kitanzania 253 billioni, imehamishia uwekezaji huo nchini Tanzania, kufuatia kutokuwepo kwa maelewano mazuri na serikali ya Kenya.

Mwaka jana kampuni ya VR Holding AB ilieleza lengo lake la kujenga mitambo ya kufua umeme kwa kutumia upepo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 600, katika rasi ya Ngomeni mjini Malindi, lakini Wizara ya Nishati nchini Kenya ikalikataa mbi lao kwa madai ya kutokuwepo kwa mfumo wa miradi ya nishati mbadala ya kiwango hicho pamoja na uhitaji wa umeme kuwa mdogo nchini hapo.

Wakurugenzi wa kampuni hiyo wameeleza kuwa, kwa sasa wamebadili mtazamo wao na kuiangalia zaidi nchi ya Tanzania ambayo pia iko katika ukanda huo huo wa Bahari ya Hindi.

“Tumeamua kutafuta ufumbuzi kwa ajili ya Tanzania” alisema Victoria Rikede, Mkurugenzi katika kampuni hiyo.

“Kenya imeonekana kuwa na ugumu kiasi na pia haitoweza kutumia kiasi chote cha umeme utakaozalishwa katika gridi hiyo. Hivyo kwa sasa ufumbuzi kwao ni kujenga gridi ndogo,” aliongeza.

Nchi ya Kenya inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa Afrika Mashariki imeonakana kupoteza baadhi ya fursa kubwa za uwekezaji kama vile bomba la mafuta ambalo limehamishiwa Tanzania.

Wizara ya Nishati nchini humo ilieleza kuwa kujengwa kwa mtambo huo mkubwa wa kuzalisha umeme, kungeifanya nchi hiyo kuwa na umeme mwingi kuliko mahitaji na hivyo  kuwafanya wananchi wake kulipa gharama kubwa za umeme ambao hautotumika.

Taarifa zinaeleza kuwa nchi ya Kenya iliitaka Kampuni hiyo kujenga mtambo mdogo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 50.

Wolper: Sijawahi Kutambulisha Mwanaume Kwetu, Tunafanya Mapenzi Kujifurahisha T

$
0
0
Staa wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hajawahi kumpeleka mwanaume yeyote nyumbani kwao kumtambulisha licha ya kuwa kwenye na mahusiano na wanaume tofauti kwa nyakati tofauti tangu kuwa staa.

Wolper ameanika hayo wakati akifanya interview na Global TV Online usiku wa kuamkia leo katika shoo yake ya House of Stylish iliyofanyika katika Ukumbi wa High Spirit Lounge, jijini Dar es Salaam.

Diva huyo wa filamu ambaye amewahi kukiri mwenyewe kubanjuka na mastaa wakiwemo wa Bongo Fleva alisema mastaa wengi wanafanya mapenzi kujifurahisha tu wala si kwa ajili ya kutengeneza familia ama ndoa.

“Kwa kuwa nafanya vitu vya kijamii naepukana na baadhi ya mambo, mahusiano ya mnayoyaona kwenye mitandao ni kujifurahisha tu, ndo maana najiachia, lakini mama yangu angeuwa anatumia mitandao nisingejaribu kufanya hivyo, lazima niwaheshimu wazazi wangu.

“Sijaolewa na hamna aliyepeleka mahali nyumbani kwetu, kwa nini nimtambulshe mwanaume? Siwezi!” alisema Wolper.

Waziri Mkuu Awatoa Hofu Wakazi Wa Songea

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wakazi 1,000 wa Manispaa ya Songea wanaoidai fidia ya sh. bilioni 3.8 ya eneo lao ambalo limechukuliwa na kuwa eneo la kiuchumi mkoani Ruvuma (Ruvuma SEZ) kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Manispaa hiyo.

Amesema Serikali ya awamu ya tano inatambua kilio chao ambacho alisema ni cha muda mrefu na kwamba alishawahi kupata ombi maalum kutoka kwa mbunge wao wa zamani, Bw. Leonidas Gama ambaye sasa ni marehemu.

“Alipotoka kutibiwa India alikuaja ofisini kwangu na kunieleza kwamba ana mambo mawili ambayo nikifanya ziara mkoani Ruvuma anaomba niyatafutie ufumbuzi. La kwanza lililkuwa ni hili la fidia kwa wakazi wa Mwengemshindo na la pili lilikuwa ni la ujenzi wa kituo cha mabasi cha mabasi cha mjini Songea,” alisema.

“Leo nimefanya ziara maalum kwa ajili yenu kwa sababu serikali ya awamu ya tano iko kwa ajili yenu na hasa wananchi wanyonge. Na tatizo hili inalijua. Kabla sijafika hapa, nilipita kwenye eneo husika na afisa mipango miji akanionyesha ramani ya eneo lenu hili,” alisema.

Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba eneo hilo limetengwa na Manispaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambapo wawekezaji watatu tayari wamekwishajitokeza na wanataka kujenga viwanda vitatu.

“Kutakuwa na kiwanda cha kusindika mahindi, kutengeneza pumba za kuku na ng’ombe na mbolea. Kiwanda cha pili kitakuwa ni cha kusindika kahawa na cha tatu kitakuwa ni cha kukamua mafuta ya mbegumbegu,” alisema na kuongeza kwamba reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbaba Bay inatarajiwa kupita kwenye eneo hilo.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa amlipo yao, Waziri Mkuu alisema kwamba katia ya wawekezaji hao watatu aliyekwishalipa fidia ni mmoja tu, na kwamba kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji, fidia inapaswa kulipwa na mnunuzi wa eneo husika.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alikiri kuwepo kwa mapungufu wakati wa ulipaji kwa sababu walifuata orodha ya majina (kialfabeti) badala ya kutoa malipo kwa wakazi wa eneo husika. “Sasa hivi mwekezaji anataka kuanza ujenzi, lakini ndani ya eneo lake kuna watu ambao bado hawajalipwa, kwa hiyo hawawezi kutoka hadi wale waliobakia nao walipwe. Serikali itawafuatilia hawa wawekezaji wengine ili nao walipe fedha zao haraka ili waliobakia waweze kulipwa,” alisema.

Jumla ya watu 2,179 walifanyiwa uthamini mwaka 2008 na gharama yao kubainika kuwa ni sh. 3,254,737,622. Kuanzia Juni 8-19, 2015, Serikali iliwalipa wakazi 1,179 sh. 1,920,242,121 ambapo kati ya hizo, sh. 1,210,078,261 zilikuwa ni malipo ya thamani ya mali za wananchi na sh. 710,163,860 zilikuwa ni riba kutokana na malipo hayo kuchelewa kufanyika.

Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 2,033 (sawa na ekari 5,000) lilitwaliwa na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Ruvuma na Manispaa ya Songea tangu mwaka 2007. Eneo hilo linajumuisha mitaa ya Luwawasi (Mkuzo), Mwengemshindo na Luhira.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Afisa Ardhi wa Manispaa ya Songea, Bw. Kundaeli Fanuel Ndemfoo afuatilie suala la Bibi Monica Joseph Miti na wanae ambao walidhulumiwa nyumba ya urithi na aliyekuwa mwanasheria wa manispaa hiyo.

Ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mwengemshindo baada ya kupokea bango lililoandikwa na Bibi Miti kuomba arejeshewe umiliki wa nyumba ya marehemu muwewe.

Alipopewa nafasi ya kueleza tatizo lake, Bibi Miti ambaye alimtaja mwanasheria huyo kwa jina moja la Bw. Mwakasungura, alidai kuwa mwanasheria huyo alighushi hati ya nyumba, na kuwatoa ndani ya nyumba yeye na watoto wa marehemu.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu aeleze alipo huyo mwanasheria wa manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bibi Tina Sekambo alijibu kwamba alishahamishiwa wilaya ya Ukerewe.

Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na Afisa Ardhi wa Manispaa wafuatilie suala hilo na wampe majibu mapema iwezekanavyo. Pia amemuomba Bibi Miti na wanawe wafike kuonana naye Januari 3, mwakani atakapokuwa Songea kwa mapumziko mafupi ya mwisho wa mwaka.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku moja mkoani Ruvuma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kanisa Anglikana lapata mrithi wa Askofu Mokiwa

$
0
0
Mchungaji Jackson Sosthenes amechaguliwa kuwa askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kura 110 kati ya 185 zilizopigwa na wajumbe wa sinodi wa kanisa hilo.

Mchungaji Sosthenes amemshinda Mchungani Patrick Bendera aliyepata kura 74, huku moja ikiharibika.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 23,2017 katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam la Mtakatifu Albano lililopo Posta wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Ofisa habari wa dayosisi hiyo, Yohana Sanga amesema uchaguzi umelenga kumpata askofu wa tano wa Dayosisi ya Dar es Salaam anayechukua nafasi ya Dk Valentino Mokiwa.

Amesema walioshiriki uchaguzi huo ni wajumbe wa sinodi ambao ni mapadri, mashemasi, walei, wajumbe wa vikao vya sinodi na wa idara katika dayosisi.

"Baada ya Dk Mokiwa kuamriwa kujiuzulu nafasi hii ilishikiliwa na kasisi mkuu, Jerome Napera ambaye leo amemkabidhi Canon Sosthenes,” amesema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 24

Mtwara: Mwanamke Amfungia Mumewe Ndani na Kisha Kumchoma Moto

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zuhura Ismail (29) kwa tuhuma za kumuua mume wake baada ya kumfungia ndani na kisha kuichoma nyumba kwa petroli.

Taarifa hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Lucas Mkondya, ambapo amesema kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, baada ya mwanamke huyo kugundua kuwa aliyekuwa mume wake anaishi na mke mwingine, na kuamua kumvizia nyumbani kwake kisha kuichoma moto na kusababisha kifo chake.

"Ni kweli Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka mwanamke mmoja ayefahamika kwa jina la Zuhura Ismail kwa tuhuma za kuichoma nyumba aliyokuwa anaishi mume wake na mwanamke mwingine, kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya Zuhura kugundua kuwa mumewe anaishi na mke mwingine, na kuamua kwenda kuchoma nyumba hiyo moto na kuwasababishia majeraha makubwa, ambapo mumewe alipelekwa hospitali lakini kutokana na majereha hayo makubwa alifariki dunia, lakini mwanamke aliyekuwa nae anaendelea vizuri", amesema Kamanda Mkondya.

Aidha Kamanda Mkondya amesema mara baada ya tukio hilo mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Zuhura Ismail alitoroka na kwenda kusikojulikana, na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka na pindi atakapopatikana watatoa taarifa.

Agizo la serikali kwa wanaodaiwa mikopo ya elimu ya juu

$
0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amewataka wote wanaodaiwa mikopo ya Elimu ya Juu kuirejesha mikopo hiyo mara moja pasipo kungoja kuchukuliwa hatua za kisheria.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Waziri Ndalichako alisema kuwa kila aliyepata mkopo wa Elimu ya Juu ana wajibu wa kuulipa ili wanafunzi wanaoomba mikopo nao waweze kupata na kwamba serikali haitosita kuchukua hatua stahiki kwa wale ambao hawatozirejesha ikiwamo kushtakiwa mahakamani.

Waziri Ndalichako alisema kwa wale waliokuwa wakinufaika na mikopo hiyo na kwa sasa wamejiajiri wenyewe na ambao bado hawajapata ajira wanapaswa kufika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo ili wapewe utaratibu wa namna gani ya kuanza kurejesha.

Hata hivyo Prof. Ndalichako alisema kwamba, idadi ya wanufaika wa mikopo waliojitokeza kwa hiari kuanza kurejesha mikopo yao imeongezeka na kuwataka ambao bado hawajaanza kufanya hivyo wawaige wenzao walioanza tayari.

Novemba 2016, Bodi ya Mikopo ilitoa orodha ya majina ya wadaiwa sugu takribani 20,000 ambao walitakiwa kuanza kurejesha mikopo yao ndani ya siku 30.

Hapo awali Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdulrazaq Badru alieleza kuwa watachapisha orodha ya majina ya wadaiwa sugu takribani 142,470, wanaodaiwa jumla ya kiasi cha shilingi za kitanzania 239.3 billioni.

Hata hivyo Prof Ndalichako aliwataka wale wote watakaoanza kurejesha mikopo yao kwa Bodi ya Mikopo, kulipa fedha hizo kupitia akaunti ya benki ya Bodi na siyo kulipa fedha taslimu kwa mtu yeyote yule. Alisisitiza hilo ili kuepusha usumbufu ikiwemo utapeli ambao unaweza kufanyika wakati wa ufanyaji wa malipo hayo.

Salamu za Krismas na Mwaka Mpya 2018 Kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mwigulu Ataja Sababu Za Upinzani Kugomea Uchaguzi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezindua kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo jimbo la Longido unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 na kusema kwamba wapinzani wameogopa kushiriki kwa sababu wataachwa mbali sana.

Akizindua kampeni hizo, Mwigulu amewataka wananchi wa jimbo la Longido kumchagua mgombea wa CCM, Dk. Steven Kiruswa awe mbunge wao kutekeleza ilani ya chama mapinduzi kwa kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.

Mwigulu amesema wapinzani wameogopa kuwa wataachwa mbali k baada ya kupima uitikio wa wananchi ambao wanakubali kazi za Rais John Magufuli na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na wananchi wanaona.

Aidha amewahakikishia wananchi wajitokeze siku ya kupiga kura kwani usalama ni wa uhakika wakati wa kupiga kura.​

Shein Awapa Kila Mmoja Kiwanja, Sh. Milioni Tatu Zanzibar Heroes

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa zawadi ya kiwanja kwa kila mchezaji wa Zanzibar Heroes  na shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji.

Dkt.Shein ametoa zawadi hizo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes baada ya kufanya vizuri katika michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

“Mmeonyesha kwamba mnaweza soka katika michuano ya CECAFA, kama serikali inabidi tuwatunuku zawadi, jumla mko thelathini na tatu pamoja na wachezaji  na viongozi wa timu, kwa hiyo natoa pesa shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji na viongozi wenu pamoja na kiwanja kwa kila mchezaji na kiongozi, na viwanja vyote vitakuwa sehemu moja mtaanzisha kijiji chenu,” amesema Shein

Zanzibar Heroes walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano ya CECAFA, huku wakiwa na rekodi nzuri baada ya kumtoa bingwa mtetezi Uganda  na kuwafunga ndugu zao Kilimanjaro Stars.

Rais Magufuli azidi kung'arishwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amezindua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Arusha mjini katika eneo la Njiro Kontena.

Akizungumza na wananchi ambao wamehudhuria shughuli ya uzinduzi wa hospitali hiyo, Gambo amesema kwamba anafuraha kushuhudia tukio hili kwani ni moja kati ya ahadi za Rais Magufuli.

“Nina furaha sana kushuhudia tukio hili litakaloacha alama katika maisha ya watu wetu wa Arusha, kwani wakati wa kampeni Mhe Rais Magufuli aliahidi na tunatekeleza kwa vitendo,” Gambo

 Hospitali hiyo inatarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya laki nne kutoka wilayani humo na maeneo ya jirani ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanasababisha hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kuelemewa. 
 
Mhandisi wa Majengo Jiji la Arusha akitoa maelezo ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) na mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe Fabian Daqqaro ( katikati).

Aidha Gambo ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa mapato yanayokusanywa na Jiji la Arusha kwa mwaka bado hayatoshelezi hata kulipa mishahara ya watumishi wake na kwa maana hiyo ni muhimu kuweka mifumo thabiti ya ukusanyaji wa mapato jijini humo.

 “Jiji la Arusha mapato yake ya ndani kwa mwaka hayazidi bilioni 12 na mishahara pekee ya watumishi wa halmashauri ni zaidi ya bilioni 40, sasa hapo ukilipa tu mishahara hela yote inakwisha na bado unakua na deni, sasa hata fedha za maendeleo zitatoka wapi zaidi ya kutegemea hela zinazoletwa na Magufuli?? Gambo alihoji.

 Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Arusha kwa awamu ya kwanza unafanyika katika moja ya maeneo ya wazi yaliyo kuwa yakimilikiwa kinyemelela na baadhi ya wajanja wachache na kwa sasa ujenzi umeanza ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 500 hii ikiwa ni jengo la Ghorofa moja kwa ajili ya wagonjwa wa nje.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images