Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TANESCO yajipanga kuboresha vituo vya kupoozea umeme jijini Dar ili kupunguza adha ya kukatika kwa umeme nchini.

$
0
0
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema lipo katika mpango wa uboreshaji wa vituo vidogo vya usambazaji na upoozaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza na kumaliza adha ya kukatika kwa umeme nchini. Vituo hivyo ni pamoja na kile kilichopo katikati ya jiji pamoja na kituo cha Kurasini. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ziara

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa kuzuia uhalifu kwa njia ya mtandao

$
0
0
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wakimataifa utakaojadili uzuiaji wa uhalifu unaotokana na matumizi ya njia ya mtandao, unatarajia kufayika Jijini Dar es Salaam, Machi 27 hadi 28 mwaka huu. Mkutano huo unatokana na kuwa Tanzania ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazokabiliwa na changamoto za uhalifu huo kwa njia ya mtandao. Akizungumza na wandishi wa habari jijini

Muuza magazeti ajitokeza kuwania ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CHADEMA

$
0
0
Bw. Aidan Pugili WAKALA wa magazeti mjini Iringa Aidan Pugili (34),  amejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Uchaguzi mdogo wa kujaza kiti hicho kilichoachwa wazi na Dk William Mgimwa aliyefariki Januari 1, mwaka huu, utafanyika Machi 16, mwaka huu. Akitumia umaarufu wake wa kuuza magazeti mjini hapa, Pugili

Wema Sepetu awashangaa wanaomponda Jokate Mwegelo kwa kumaliza ugomvi wa kugombania penzi la Diamond

$
0
0
Mwigizaji Wema Sepetu, amewashangaa wanaomponda Jokate Mwegelo kwa kumaliza tofauti baina yao akisema kuwa hawatendi haki na wanaingilia uhuru wa wasanii hao.   Kauli ya Wema imekuja siku chache baada ya Jokate kufika kwa kushtukiza katika onyesho lililofanywa na Wema mkoani Arusha hivi karibuni na kumaliza tofauti zao.  

Uchaguzi wa madiwani: CCM yapata ushindi wa kishindo ....Yashinda kata 24 kati ya 27, CHADEMA waambulia kata 3 tu

$
0
0
WAKATI Chama Cha Mapinduki (CCM),ikishinda Kata 24 Kati ya Kata 27 ambazo Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Umefanyika jana Kote Nchini, mjini Kigoma katika jimbo la Mbunge wa Chadema Zitto Kabwe ushindi umekwenda kwa CCM.   Hatua ya Chadema kushindwa katika kata ya Mkongoro inatokana na mgogoro ulioikumba Chama hicho baada ya Mbunge huyo kuvuliwa nyadhifa zake  ndani ya chama hicho. 

Skendo ya kujiuza yamfanya baby madaha apigwe chini na Record label yake ya Candy and Candy ya huko Kenya na kupokonywa gari....Akiri uchawi upo

$
0
0
Mwanamuziki na muigizaji baby Joseph madaha amefunguka na kusema kuwa kweli ameamini uchawi na kupigana juju vipo kwenye gemu kwani mambo yaliyomtokea hivi karibuni haelewi hata imekauje.   Chanzo nini? Hapo siku za nyuma baby Madaha alipatikana na dhahama ya kukumbwa na kashfa nzito sana ya kujiuza kwa dau la milioni kumi kwa jamaa mmoja hivi mitaa ya Dar es Salaam Jambo

Waliotangaza nia CCM kabla ya wakati watiwa kikaangoni

$
0
0
Baadhi ya makada wa CCM ambao wataitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho, wanakabiliwa na shtaka la kutoa rushwa kwa lengo la kushawishi kukubaliwa kwao, Mwananchi limebaini.   Makada hao ni wale wanaodaiwa kuwa katika harakati za kuwania urais wa 2015, hatua ambayo imekigawa chama hicho katika makundi yasiyo rasmi ya yanayowaunga mkono wagombea hao.  

Mume amenitelekeza na watoto wanne..... Ndiye aliyesababisha nikomee darasa la sita

$
0
0
Nkasi, Rukwa MATUKIO ya utelekezaji wa mke na watoto nchini Tanzania bado ni changamoto kubwa katika jamii. Licha ya matukio haya kutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine bado yanachochewa na kulegalega kwa sheria za nchi ikiwemo sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kwa baadhi ya vipengele. Waathirika wakubwa wa matukio haya ni mama pamoja na watoto ambao ndio hutelekezwa huku baba

Muuaji wa Tarime afa kwa ugonjwa.......

$
0
0
Mtuhumiwa wa mauaji na unyang’anyi wilayani Tarime mkoani Mara, aliyekuwa akitumia majina matatu ya Charles  Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msongo (38) aliyekuwa akihojiwa na Polisi, amefariki katika Hospitali ya wilaya wakati akipatiwa matibabu. Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime/ Rorya, Justus Kamugisha, alisema mtuhumiwa huyo alifariki usiku wa kuamkia jana wakati

Moja kati ya yaliyotokea kwenye uchaguzi wa madiwani...... mbunge ajeruhiwa, na mabomu kurindima

$
0
0
    Chaguzi  za udiwani katika kata 27 uliofanyika jana katika maeneo tofauti ulitawaliwa na matukio mabaya yakiwamo ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi, huku mbunge mmoja akicharangwa mapanga na kukimbizwa hospitalini kupatiwa huduma. Katika kata ya Sombetini, jijini Arusha, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walirusha mabomu ya machozi kutuliza vurugu za watu

Vigogo wa TBA wahukumiwa miaka 9 Jela….Ni wale walioruhusu Ujenzi wa Jengo Linalochungulia IKULU.

$
0
0
 Vigogo wa TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar! (Picha na Maktaba). ** Watu  wawili wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 15 au kwenda jela miaka miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ya ujenzi wa jengo la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu lililopo mtaa wa Chimala Kitalu cha 45 na

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida afikishwa Mahakamani Kisutu kwa kosa la kutengeneza Dawa bandia za kurefusha maisha kwa waathirika wa UKIMWI ( ARV feki)

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam pia ni Mkurugenzi Mkuu Kiwanda cha Kutengeza Dawa (TPI Ltd) Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka matano ya usambazaji wa Dawa bandia za kurefusha maisha kwa waathirika wa UKIMWI na kuisababishia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) hasara ya

CCM yatoa shukrani kwa wananchi kwa kuimwaga CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana

$
0
0
   CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23. Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni

Maeneo ya Ikulu yageuzwa uwanja wa ngono na ukabaji

$
0
0
Wananchi wa mtaa wa Pwani katika Manispaa ya Bukoba, wamelalamikia vitendo vya ngono vinavyofanyika katika maeneo ya Ikulu ndogo na kutaka vidhibitiwe kwani  vinaidhalilisha serikali ya mkoa Kagera. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliotishwa na Mwenyekiti wa mtaa huo kuzungumzia hali ya ulinzi na usalama katika mtaa wao, wananchi hao walidai kuna watu wamekuwa wakiegesha magari

Wafanyabiashara waendelea kugoma kila kona kupinga matumizi ya mashine za EFD

$
0
0
Sakata la matumizi ya Mashine za Elektroniki za Kutolea Risiti (EFD), limechukua sura mpya baada ya wafanyabiashara mikoa mbalimbali kuja juu wakisema matumizi yake yanalenga kuwaangamiza katika biashara.    Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao wameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufikiria upya mfumo wa kuzitumia, vinginenyo watajikuta wanaingia kwenye mgogoro

Vigogo sita CCM ambao wanatajwa kuwania Urais 2015 waitwa Kamati ya Maadili....Yumo Lowassa, Wassira, Sumaye na Makamba

$
0
0
Vigogo sita ambao wanatajwa kuwa wanajiwinda kwa ajili ya kuwania urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu ujao, wameitwa mbele ya Kamati ya Ndogo ya Maadili ya chama hicho, kwa ajili ya kuhojiwa kwa tuhuma za kukiuka maadili.    Habari ambazo zililifikia gazeti la Mwananchi  jana zinawataja vigogo hao kuwa ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano

Rais Kikwete aongoza kikao cha kamati kuu ya CCM Ikulu jijini Dar leo

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)<!-- adsense -->

CUF kutosimamisha mgombea katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga....CHADEMA kumtangaza mgombea wake wakati wowote

$
0
0
   Mbio za kuwania ubunge katika Jimbo la Kalenga unabaki kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kuthibitisha kutosimamisha mgombea. Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Abdul Kambaya, amesema chama chake hakina mpango wa kusimamisha mgombea katika jimbo hilo na kwamba hivi sasa wanaandaa mikutano ya

Linex akanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na Agnes Masogange, ..."Sina haraka ya kuwa na mpenzi"

$
0
0
Linex Sunday Mjeda, ambaye hivi karibuni ameonekana kwenye picha kadhaa akipoz na video Queen maarufu Tanzania, Agnes Gerald (Masogange), amekanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na mrembo huyo.   Kupitia akaunti yake ya Facebook, mkali huyo wa ‘Kimugina’ ameonesha kusikitishwa na habari iliyoandikwa na tovuti moja kuwa yeye na Agnes wako kwenye mapenzi mazito.   “Ni kweli

Magazeti ya ufaransa yadai Obama ana uhusiano wa kimapenzi na Beyonce, waandishi wa Marekani wakanusha

$
0
0
Kuna mgongano wa habari kati ya baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa na vile vya Marekani kuhusu uhusiano uliopo kati ya Beyonce Knowles na rais wa Marekani, Barack Obama.   Gazeti la Ufaransa la Le Figaro liliripoti kuwa kuna uhusiano wa siri wa kimapenzi kati ya rais wa Marekani, Barack Obama na mwimbaji ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya Obama, Beyonce Knowles.   Habari
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images