Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli ataja siri ya CCM kuongoza uchaguzi wa madiwan

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dkt john pombe Magufuli, amesema kuwa ushindi wa kishindo uliopatikana katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba 26 mwaka huu umetokana na uimara na ukomavu wa chama hicho.

Rai Magufuli amesema hayo leo katika Mkutanmo Mkuu Maalum wa Taifa wa CCM unaoendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Mjini Dodoma na kuongeza sababu nyingine zilizopelekea kishindo hicho.

Rais Magufuli ameeleza kuwa ushindi huo unaashiria Matokeo ya kukubalika kwa Chama cha Mapinduzi pamoja na uimara na ukomavu wa chama hicho.

Ameongeza kuwa Utekelezaji kwa vitendo mambo waliyoyaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi na Ilani ya uchaguzi ni moja ya sababu zilizopelekea wao kushinda.

Vilevile Rais Magufuli ametaja kuwa Umoja na mshikamano mkubwa kati ya wana CCM umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ushindi huo uliopatikana.

Katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika Novemba 26 mwaka huu, Chama cha Mapinduzi kilipata ushindi wa kata 42 kati ya kata 43 zilizofanya uchaguzi huku upinzani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ukipata kata moja peke yake.

Aidha Rais magufuli ameelza kuwa lengo la CCM ni kushinda kwa kishindo zaidi ambapo wamejipanga kupata ushindi mkubwa zadidi na ikiwezekana wapinzani wasipate nafasi hata moja.

“Tunataka ikifika uchaguzi mwingine washindani wetu ambao wanatusikiliza humo wasiambulie chochote,” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana, yeye ameeleza kuw sababu nyingine zinazopelekea CCM kushinda katika uchaguzi kuwa pamoja na uwepo wa demokrasia na uhuru wa kujieleza kwa wanachama wote.

“Watu wengi wanajiuliza kwanini Chama chetu kinashinda uchaguzi. Sababu kubwa ya ushindi ni Demokrasia ndani ya Chama. Sababu nyingine kubwa zaidi ni uhuru wa kujieleza ndani ya chama chetu kila mtu anauwezo wa kusema” amesema A. Kinana.

Gdbless Lema atoa kauli Takukuru kutupa ushahidi wa Flashi ya Nassari

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kutupwa ushahidi wao na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ni kupoteza sifa na imani kwa wananchi.

Amesema uamuzi huo unatoa sura ya matabaka kwamba kuna watu ambao wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na wengine hawastahili.

Takukuru kupitia msemaji wake, Musa Misalaba jana Jumapili Desemba 17,2017 alisema taasisi hiyo imeshindwa kuendelea na uchunguzi wa tuhuma za rushwa zilizowasilishwa na Lema pamoja na mwenzake Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki.

Imesema uamuzi huo unatokana na wabunge hao kuingilia uchunguzi na kuuvuruga licha ya kutahadharishwa kuhusu suala hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 18,2017 mjini Arusha, Lema amesema uamuzi wa Takukuru umepoteza imani kwa wananchi ambao walikuwa na imani na chombo hicho.

Amesema kitendo cha mamlaka ya uteuzi kumteua waliyemtuhumu, Alexander Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kinatoa ujumbe kwa Takukuru.

Akizungumzia hilo, katibu wa Chadema kanda ya kaskazini, Aman Gorugwa amesema Takukuru ilipaswa kutafuta ushahidi.

Takukuru yamwachia Mukoba

$
0
0
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini imemuachia aliyekuwa Rais wa Chama cha walimu (CWT)  Gratius Mukoba bila kumfikisha mahakamani.

Kamanda wa Takukuru mkoa wa Dodoma Emma Kuhanga  amesema Mukoba hakupelekwa mahakamani kama ilivyotakiwa.

"Hapana hatujampeleka mahakamani, tulishamuachia,....ni hivyo kwamba mahakamani hakupelekwa," amesema Kuhanga

Mwishoni mwa wiki Takukuru ikimkamata Mukoba kwa madai ya kujihusisha na ugawaji wa rushwa kwa wajumbe na alitarajia kufikishwa mahakamani leo.

Alipoulizwa iwapo Rais huyo wa zamani wa CWT ataitwa tena ama taasisi yake imeona hana hatia, Kamanda Kuhangwa amesema "wewe elewa kuwa hatujampeleka mahakamani lakini tumemwachia,"

Magufuli: Wapinzani Mtaisoma Namba

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri wa Muungano Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kutangaza kuuvuruga upinzani Tanzania kwa kupokea Mbunge mmoja kutoka chama cha upinzani na madiwani wengine saba.

Magufuli amesema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao umefanyika leo Disemba 18, 2017 mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwepo marais wastaafu.

"Nimepokea majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao wanataka kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia yupo Mbunge mmoja anataka kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na madiwani saba kwenye jimbo lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma namba kweli kweli" alisisitiza Rais Magufuli

Aidha Magufuli amewataka viongozi wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha wanafanya kazi ya kuongeza wanachama wapya katika chama hicho na kuongeza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa wataendelea kupokea na kuwatangaza watu ambao wanahamia kwenye chama hicho, na kusema kuwa lazima kwanza wajiridhishe ili wasije kupokea na watu wengine ambao hawana mpango mzuri kwa CCM.

Rais Magufuli awatoa wasiwasi Watanzania Kuhusu Ukomo wa Uongozi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. John Pombe Magufuli amewatoa wasiwasi wananchi kwa kusema wazi kwamba anatamani siku moja ifike naye aitwe mzee mstaafu wa taifa hilo kama alivyo Kikwete na wengine.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua uchaguzi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama NEC Taifa, mkoani Dodoma akiwakaribisha na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakiwemo Marais wastaafu.

''Natamani siku moja na mimi nistaafu, niitwe mzee mstaafu kama mzee Kikwete niwaachie wengine,'' amesema.

Vipindi vya ukomo kwa sheria iliyopo kwa nafasi ya Rais ni miaka 10 , sheria inaruhusu kila baada ya miaka mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu ili kuwapa demokrasia wananchi kuweza kuchagua kiongozi anayefaa.

Mwezi Julai, 2017 kuliibuka mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii kujadili kauli ya Rais mstaafu ya awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, aliyoitoa katika Baraza la  sikukuu ya Iddi aliyosema  kama isingekuwa matakwa ya kikatiba angetegemea kuona Rais aliyepo madarakani John Pombe Magufuli akipewa nafasi ya kutawala bila kikomo.

Mkutano huo wa leo utakipatia viongozi wapya wa ngazi ya juu chama hicho ikiwemo Mwenyekiti taifa na Mwenyekiti baraza la mapinduzi Zanzibar. 

Tayari Rais magufuli amethibitisha kuwa katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana ataendelea na nafasi yake.

TAKUKURU yafunguka kuhusu Nehemia Mchechu wa NHC

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imekanusha taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa wanamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Nehemia Mchechu.

Afisa habari wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema wanashangaa taarifa hizo zimetoka wapi na wao kama taasisi hawamshikilii Mkurugenzi huyo aliyesimamishwa na Waziri Lukuvi wiki iliyopita.

“Hizo taarifa sijui zimetoka wapi, lakini sisi hatuna huyo mtu, hatujamkamata saa tunashindwa kuelewa watu wanazusha kwa lengo gani”, amesema Misalaba.

Aidha msemaji huyo ameongeza kuwa wao kama taasisi hawajapokea agizo lolote la kumkamata na kumfanyia uchunguzi ndugu Nehemia Mchechu hivyo hawana sababu ya kumkamata.

Nehemia alisimamishwa kazi na Waziiri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi siku ya Jumamosi wiki iliyopita. Jana jioni kwenye mitandao zilisambaa taarifa za kukamatwa kwake ambavyo leo TAKUKURU imekanusha.

Rais Magufuli Kamteua Abdulrahman Kinana Aendelee Kuwa Katibu Mkuu CCM

$
0
0
Katibu mkuu wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo ameteuliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli  kuendelea kuwa katika nafasi yake kwa kipindi kingine.

Akiongea katika mkutano wa 9 wa Chama hicho unaoendelea mkoani Dodoma amemshukuru kwa kazi yake nzuri  kwa muda wote ambao amekuwa  katika nafasi hiyo huku akiweka wazi kuwa ni lazima aendelee kufanya nay kazi kwasababu ameridhishwa na utendaji wake wa kazi.

''Namshukuru ndugu Kinana kwa msaada wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho nafikiri  anafaa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi kingine,'' amesema Magufuli. 

Kauli ya Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana ameandika barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa kuwa haridhishwi na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.

Baada ya kupata nafasi  hiyo Abdulrahman Kinana amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini pamoja na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kukijenga chama hicho pamoja na nchi  kwa ujumla.

Kinana aliwahi kuwa mtumishi wa Jeshi la Tanzania kwa miaka 20 pamoja na kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi 2006, amechaguliwa kuwa Katibu mkuu wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu 2012.

Rose Muhando Atangaza Kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM

$
0
0
Msanii wa nyimbo za Injili aliyetamba kwa vibao vyake murua na vyenye kuburudisha Rose Muhando, ametangaza kujunga rasmi na Chama cha Mapinduzi.

Msanii huyo ambaye aliomba kujiunga na chama hicho amekabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi leo yeye pamoja na kikundi chake, katika Mkutano Mkuu Maalum wa Tisa wa CCM Taifa, unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, mjini Dodoma.

Rose Muhando kabla ya kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM alitumbuiza kwa kibao maalumu alichokiandaa kwa ajili ya Rais John Pombe Magufuli ambacho amekipa jina la “Magufuli Tubebe”.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey polepole alitangaza kuwa Rose Muhando pamoja na Kundi lake wameomba kupewa nafasi ya kutumbuiza kwa wimbo huo maalumu pamoja na kukabidhiwa kadi za CCM.

“Kundi la Ndugu Rose Muhando na yeye mwenyewe niwakaribishe Jukwani kwa wimbo ambao wameutunga maalumu kwa Ndugu Magufuli. Kundi hili walipokuwa wanakuja walikuwa na maombi mawili, ombi la kwanza ni kupewa nafasi ya kuimba wimbo huu maalumu na pili kujiunga rasmi na CCM,” amesema katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole.

Hata hivyo Polepole amesema kuwa Rose Muhando na kundi lake watakabidhiwa kwa makatibu wa mikoa husika kwa ajili ya michakato ya kuwaandikisha kama wanachama wapya wa CCM.

Kinana Asema Yupo tayari kuitumikia CCM....Atoboa Siri ya Ushindi wa Kishindo

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema yuko tayari kuendelea kukitumikia chama hicho.

“Neno la mwenyekiti kwangu ni amri kama umeona bado unahitaji niendelee kukusaidia niko tayari kufanya hivyo,” amesema Kinana leo Jumatatu Desemba 18,2017 katika mkutano mkuu wa CCM unaoendelea mjini Dodoma.

Kinana ametoa kauli hiyo wakati kukiwa na minong’ono kuwa ameandika barua akiomba kuachia nafasi yake ya ukatibu mkuu.

Awali, Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aliweka wazi kuwa Kinana amekuwa msaada mkubwa katika kukiongoza chama hicho.

“Mzee Kinana amenisaidia sana. Amenisaidia mno kwenye kufanya mabadiliko ndani ya chama na ni mategemeo yangu ataendelea kunisaidia,” amesema.

Katika hatua nyingine, Kinana ametoa siri ya ushindi wa kishindo wa chama hicho katika uchaguzi kuwa ni kutokana na ilani bora, demokrasia  na kusikilia maoni ya wanachama.

Kinana amesema demokrasia imekuwa msingi wa chama hicho ndiyo sababu kinaimarika.

“CCM tunazingatia demokrasia, wanachama wapo huru kutoa maoni ndani ya chama. Hili linafanyika kwa kuwa usipowapa uhuru wa kusema ndani watasema nje,” amesema.

Katibu Mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda Amwangukia Rais Rais Magufuli

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amepiga goti na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweze kukisaidia chama chake cha Ada Tadea milioni 60 ili waweze kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotegemewa kufanyika mapema 2018

Shibuda ameomba hilo leo Disemba 18, 2017 akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema endapo Rais akiwasaidia milioni 20 kwa kila jimbo hivyo wataweza kushiriki uchaguzi wa marudio wa Ubunge katika majimbo matatu ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018.

"Nakuomba utombee kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atutazame tupate ruzuku vyama visivyo pata ruzuku ili tuwe sawa na wale unaowapa ruzuku lakini hawapendi kushiriki katika masuala ya uzalendo na utaifa, lakini chonde chonde nakuomba utuombee" alisema Shibuda

Baada ya maombi yake hayo Rais Magufuli alimuuliza kama yeye na chama chake atashiriki katika uchaguzi wa marudio wa wabunge ndipo hapo aliporudi na kuomba apewe milioni 20 kwa kila jimbo.

"Naomba nisaidie milioni 20 kwa kila jimbo ili niwezeshe kwenda kugombea kwa hiyo kwa majimbo matatu tusaidie chama milioni 60 kwa sababu unaowapatika ruzuku hawatakwenda kushiriki" alisisitiza Shibuda.

Baadhi ya Vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania kikiwepo CHADEMA, CUF, TLP, CHAUMMA pamoja na ACT Wazalendo vimejitoa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio wa nafasi ya Ubunge ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018 kwa kile walichodai kuwa uchaguzi wa madiwani uliofanyika karibuni haukuwa wa haki na ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na kanuni za uchaguzi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 19

Nassari Aishangaa TAKUKURU Kutupa Ushahidi Wake

$
0
0
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshangazwa na Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa kushindwa kuona uhalisia au uongo kwenye ushahidi waliouwasilisha dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti na badala yake,wameona siasa.

Nassari amesema hayo ikiwa ni siku moja kupita baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi wao kwa kudai kwamba uliharibiwa kwa kuingiza siasa.

Nassari amesema kwamba “Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka. Cha ajabu hawajaona uhalisia au uongo uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi," Nassari.

Nassari amefafanua kwamba katika kuwasilisha ushahidi wa kununuliwa kwa madiwani aliwakabidhi moja ya kifaa alichotumia kurekodia baadhi ya matukio.

"Niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo".  Ameongeza Nassari

ANC yapata mwenyekiti mpya, Mama Zuma ‘apigwa mtama’

$
0
0
Chama cha African National Congress (ANC), Afrika Kusini kimemchagua Cyril Ramaphosa, kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho akimrithi Jacob Zuma.

Ramaphosa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC leo baada ya kufanyika uchaguzi.

Makamu huyo wa  rais aliyeibuka mshindi alikuwa na upinzani mkali na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa  Zuma.

Kulikuwa na  mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura.

Uwaniaji madaraka umeleta mvutano  wa kisiasa nchini humo  hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019.

Ramaphosa ameibuka mshindi kwa kupata kura  2,440 huku mpinzani wake  Dlamini-Zuma akipata kura 2,261

Mvutano Mkali Waibuka Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala)

$
0
0
Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) ambao ulikua ufanyike jana umesogezwa  hadi leo kupisha mashauriano yatakayofanywa na baraza la mawaziri  wanachama wanaohusika moja kwa moja na Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) baada ya mbunge kutoka Uganda, Freddy Mbidde kupinga Tanzania kuwa na mgombea.

Chanzo cha mgogoro huo kinadaiwa ni Tanzania kuwa na mgombea wa nafasi ya Uspika, Adam Kimbisa wakati nafasi hiyo huwa ni kupokezana na Spika wa kwanza wa Eala, Abdulrahman Kinana alitoka Tanzania akifuatiwa na Kenya kisha Uganda.

Mbidde ametoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge kutokana na akidi kutotimia wakati wa kufanya uchaguzi licha ya wabunge kutoka nchi zote sita kula kiapo cha utii mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Madete.

Baadaye ilibainika wabunge wengi wa Tanzania na Burundi hawakuwemo kwenye ukumbi wa bunge na Mbidde kuomba kutoa muda wa mashauriano zaidi ili kuruhusu nchi zinazostahili kuwa na wagombea kufanya hivyo ambazo ni Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Hata hivyo hadi jana wagombea wa nafasi hiyo walikua watatu ambao ni Adam Kimbisa, Leontine Nzeyimana ambaye ni Waziri wa zamani Afrika Mashariki wa Burundi na Mwendesha mashtaka Mkuu mstaafu wa Rwanda, Dk Martin Ngoga huku Sudani Kusini ambaye ni mwanachama mpya katika jumuiya hiyo haikutoa mgombea.

Katibu wa Bunge, Kenneth Madete aliahirisha bunge hadi leo saa 8:30 mchana kwaajili ya kumchagua Spika na baadaye makamishna na kuunda kamati mbalimbali zitakazosaidia kutekeleza majukumu ya bunge hilo la nne.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dk Suzane Kolimba amekiri kuwa baraza la mawaziri watakutana kushauriana ni njia ipi itumike kabla ya uchaguzi wa kumpata Spika wa nne.

"Kumetokea kutokuelewana na sisi baraza la mawaziri tutakutana kushaurina namna ya kusonga mbele katika hali hii na uchaguzi utafanyika kama mnavyojua suala la akidi ni muhimu katika vikao vya wabunge," alisema Kolimba

Awali wabunge tisa kutoka nchi sita wanachama wa EAC ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini waliapa kuwa wabunge katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa bunge la Tanzania, Azzan Musa Zungu amemwakilisha Spika wa Bunge, Job Ndugai  pia walikuwepo Spika wa bunge la Senate la Kenya, Ken Lusaka .Spika wabunge la Senate ya Rwanda, Banard Mukuza, Spika wa bunge la Sudani Kusini, Anthony Makana.

Daktari FEKI Anaswa Hospitali ya Mkoa Mwanza

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la kujifanya daktari, katika hospitali ya mkoa Sekou Toure.

Joseph Mbagata 25,mkazi wa mtaa wa Mabatini jijini humo amekamatwa leo Desemba 18  na jeshi hilo baada ya kubainika kwamba sio mwanataaluma na alikuwa akiwatapeli wagonjwa kwa kuwaomba hongo, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Taarifa kutoka kwa jeshi hilo zimesema kwamba mtuhumiwa alikuwa akiwaomba hongo, huku akiahidi kuleta dawa muhimu na pia kufanya mipango ili mgonjwa apate huduma kwa haraka.

Awali zilipatikana taarifa kuwa siku chache zilizopita alionekana mtu aliyevalia mavazi ya udaktari na kujifanya daktari, kisha anapita wodini kuwaona wagonjwa. Pia ilisemekana kuwa mtu huyo tayari amechukua Sh30,000  kwa mgonjwa ili aweze kumpatia matibabu.

Aidha baada ya tuhuma hizo kufika katika uongozi wa hospitali waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa, akiwa amevalia mavazi ya udaktari huku akiwa amesimama nje ya wodi ya upasuaji.

“Tumekuwa tukilalamikiwa kwamba kuna baadhi ya madaktari hapa hawana ujuzi wala hawajitambui, kumbe ni dhahiri kwamba hao watu wapo na kuanzia sasa lazima tufanye ukaguzi wa hali ya juu ili hali hiyo isije ikajitokeza tena maana ni sehemu ya kuhatarisha maisha,” amesema  mmoja wa madakatri katika hospitali hiyo ambaye hakutaka kutajwa majina.

Baada ya daktari huyo feki kukamatwa, uongozi wa hospitali ulitoa taarifa polisi, ambapo askari walifika eneo la tukio na kumuweka mtuhumiwa chini ya ulinzi kisha kumfanyia upekuzi kwenye begi alilobeba na kukuta mavazi yanayotumiwa na madaktari katika vyumba vya upasuaji.

Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa wananchi hususani wagonjwa waliopo hospitalini akiwaomba kuwa makini na watu ambao ni matapeli wa aina kama hiyo wenye nia ovu dhidi yao.

Aidha pia aliwaomba viongozi wa hospitali zote kuendelea kutoa taarifa kwa polisi kuhusiana na watu wanao watilia shaka hospitalini, ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Majina ya walioshinda kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)

$
0
0
Mkutano wa tisa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umefanyika mjini Dodoma jana ambapo miongoni mwa viongozi wengi waliochaguliwa ni pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) ambapo jumla ya wajumbe 15 kutoka Tanzania wamchaguliwa.

Miongoni mwa wajumbe hao waliopigiwa kura jana, Stephen Wasira ameongoza kwa ushindi baada ya kujikusanyia kura 1505 kati ya kura halali 1779.

Wajumbe 15 waliochaguliwa ni,

1. Steven Wassira
2. Jerry Silaa
3. Dr Fenera Mukangara
4. Angel Akilimali
5. Jackson Msome
6. Dr Ibrahim Msengi
7. Theresia Mtewele
8. Mwantumu Zodo
9. Ernest Sungura
10. Deougratius Ruta
11. Eng Burton Kihaka
12. William Sarakikya
13. Richard Charles
14. Anna Msuya
15. Charles Shanda

Magufuli Agoma Kubadilisha Sekretarieti ya CCM.......Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa CCM Kwa Kura ZOTE

$
0
0
Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana mpango wa kubadilisha Sekretarieti ya chama hicho na itaendelea kama ilivyo chini ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.

Mwenyekiti huyo mpya alichaguliwa kwenye mkutano wa tisa wa chama hicho uliomalizika jana jioni mjini Dodoma kwa kupata kura zote 1821 za wajumbe wa mkutano mkuu. 

Rais Magufuli atahudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano kuanzia jana hadi mwaka 2022 utakapofanyika uchaguzi mwingine.

Katika hotuba yake baada ya kuchaguliwa Dkt. Magufuli alisema kwasasa hana mpango wa kubadilisha Sekretarieti na itaendelea kama ilivyo chini ya katibu mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana.

Matokeo ya Uchaguzi huo yalitangazwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ambaye aliwataja washindi wote katika nafasi za Mwenyekiti Taifa, Mwenyekiti Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Taifa.

Mbali na Mwenyekiti wa Taifa lakini pia Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura zote 1821 wakati Ndugu Philip Mangula akishinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Taifa kwa kura zote 1821.

Hotuba Ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa, Akiwasilisha Taarifa Ya Serikali Kuhusu Utekelezaji Wa Ilani Ya Uchaguzi Ya Chama Cha Mapinduzi Ya Mwaka 2015 – 2020

$
0
0

1.0.      UTANGULIZI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali ya Awamu ya Tano inatimiza miaka miwili toka iingie madarakani mwezi Novemba, 2015.

Katika kipindi hiki, Serikali imeendelea kutekeleza changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuweka sera madhubuti zinazosaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa mwelekeo wake wakati akifungua Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 hapa Dodoma.

Baada ya maelekezo haya, hatua kadhaa zimechukuliwa na mafanikio dhahiri tumeanza kuyaona.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Mafanikio dhahiri yameanza kuonekana katika kipindi hiki kifupi. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuimarika kwa nidhamu kwa Watumishi wa Umma; mabadiliko ya hali ya uchumi; kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo; kuongezeka kwa mapato ya ndani; kupungua kwa rushwa, kuimarika kwa Muungano wetu na kushughulikiwa kwa migogoro ya ardhi.

Suala la Nidhamu, Rushwa na Dawa za Kulevya.
Serikali iliweka dhamira ya kuwahudumia wananchi wote hususan maskini kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo na huduma muhimu za jamii. Ili kufikia azma hii ilibidi tuanze kujenga nidhamu ya Watumishi wa Umma kwa kubaini wazembe, wabadhilifu, wezi wa mali na fedha za umma, wala rushwa mahali pa kazi na wasio tayari kuwatumikia wananchi na hasa wanyonge; na kusimamia mwenendo wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji mali na kukusanya mapato.

Tulianzisha mapambano ya wazi dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya. Yote haya ilikuwa ni mkakati wa kuwezesha kutekeleza Ilani yetu kwa vitendo na kwa mafanikio. Yote haya tumeyaeleza kwa kirefu kwenye vitabu tulivyowapa.

2.0.      HALI YA UCHUMI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Mwenendo wa viashiria vya ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu kwa mwaka 2016 na 2017 vinaonesha kuwa uchumi wetu unakua na kuimarika. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ukuaji halisi wa Pato la Taifa kwa mwaka 2015 na 2016 ulikuwa asilimia saba na hivyo kuifanya Nchi yetu kushika nafasi ya tatu kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika. Tafiti na uzoefu kutoka nchi zilizoendelea unaonyesha kwamba, mwenendo huu wa ukuaji wa uchumi utaiwezesha Tanzania kufikia kundi la Nchi zenye Uchumi wa Kati lenye wastani kipato cha Dola za Marekani 1,043 sawa na wastani wa Shilingi Milioni 2.4 kwa mwaka. Wastani wa Pato la Mtanzania umeongezeka kutoka Shilingi Milioni 1.9 kwa mwaka 2015 hadi kufikia Shilingi Milioni 2.1 mwaka 2016, sawa na ongezeko la asilimia 11.

Aidha, Serikali imeweka juhudi kubwa katika ukusanyaji wa mapato. Kutokana na juhudi hizo, makusanyo ya ndani kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaliongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 850 kwa Mwezi mwaka 2015 hadi Shilingi Trilioni 1.3 kwa Mwezi mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 34.6.

Kupitia makusanyo hayo sasa serikali inaendelea kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika kila Halmashauri, Idara za Serikali, Wizara kwa kiasi cha Shilingi bilioni 428.5 kila mwezi.

(Sekta ya Uchumi na Fedha imeelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 4 hadi  wa 8 wa vitabu mlivyogawiwa).

3.0.      SEKTA ZA UZALISHAJI

3.1.     KILIMO

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeielekeza Serikali kutilia mkazo kuendeleza sekta ya kilimo ili kukifanya kilimo kuwa cha kisasa, chenye tija na cha kibiashara ambacho mazao yake yaongezwe thamani. Serikali imeimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo, kuimarisha huduma za ugani, kuimarisha huduma za umwagiliaji, kuwezesha upatikanaji wa masoko na kuhamasisha Sekta binafsi, vyama vya ushirika na kanzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Serikali iliingia makubaliano na kampuni za kuzalisha na kuuza mbegu kwa bei ambayo ni rahisi kwa mkulima. Serikali pia imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea ambapo kwa sasa ununuzi wa mbolea hufanywa kwa pamoja. Mfumo huu unaongeza upatikanaji wa mbolea na unapunguza bei kwa asilimia 30 kwa mkulima, mfuko wa mbolea sasa unauzwa kati ya Shilingi 50,000/= hadi 60,000/= na mfumo huo umeanza msimu huu wa kilimo ambapo hadi Septemba 2017 jumla ya tani 55,000 zimeingizwa nchini. Tayari manufaa yake tumeanza kuyaona.

Serikali inaendelea kuhimiza Bodi za mazao ya pamba, korosho, kahawa, ufuta, tumbaku na mazao mengine kuandaa mbegu na madawa ya kuulia wadudu kwa haraka na bei nafuu.

Kwa upande wa zana za kilimo, Serikali imejenga uwezo wa sekta binafsi katika kuwezesha upatikanaji wa zana za kilimo ambapo katika kipindi cha Novemba 2016 na Septemba 2017 jumla ya matrekta makubwa 2,500 na matrekta ya mkono 336 yaliingizwa nchini na sekta binafsi. Kupitia mpango wa kuendeleza viwanda, Tanzania imeanza kuunganisha matrekta ya kilimo kupitia kampuni ya Ursus ambayo tayari imetengeneza matrekta 1894 ya ukubwa tofauti. Pia, Serikali imenunua mashine za kisasa 14 za kusindika mpunga zenye uwezo wa kukoboa kati ya tani 5 hadi 30 kwa siku kwenye skimu 13 za umwagiliaji nchini.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imeongeza Maafisa Ugani kutoka 9,558 mwaka 2015 hadi 13,532 mwaka 2017. Kati ya hao, 8,232 ni Maafisa Ugani wa sekta ya kilimo, 4,283 mifugo, 493 uvuvi na 524 ni Maafisa Ushirika. Vituo vya mafunzo ya kilimo na mifugo vya kata vimeongezeka kutoka 147 mwaka 2015 hadi 322 kufikia Juni, 2017, sawa na ongezeko la asilimia 54.3 kwa sekta zote.

Aidha, Serikali imejenga masoko na maghala ya kimkakati katika mipaka ili kudhibiti wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi kuingia    moja kwa moja mashambani na kununua mazao ya wakulima kwa bei ndogo. Aidha, mfumo wa stakabadhi ghalani umeonyesha mafanikio makubwa na mabadiliko ya Uongozi kwenye Menejimenti ya Bodi umeonesha matokeo chanya katika   zao la korosho. Mfano, katika msimu wa 2015/2017 kiasi cha korosho kilo laki moja na hamsini na tano (155,244,645) ziliuzwa kwa bei ya Shilingi Bilioni mia tatu themanini na nane (388,474,530,906.40).  Mheshimiwa Rais baada ya kutoa pembejeo bure kwa wakulima, uzalishaji umeongezeka na mwaka huu 2017/2018 hadi kufikia sasa kilo laki mbili sitini na tano (265,651,031) zimeuzwa kwa thamani ya Shilingi Trilioni moja nukta moja. Ambapo inatazamiwa kuwa hadi mwisho wa msimu itafikia 300,000 tutapata sio chini ya trilioni 1.4. Wastani wa bei kwa kilo umepanda kutoka Shilingi 1,300 hadi Shilingi 4,000.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Kilimo yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 8 hadi wa 13 wa vitabu mlivyogawiwa).

3.2.      MIFUGO

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Kwa upande wa sekta ya mifugo Serikali inaongeza uzalishaji wa mitamba, kujenga miundombinu ya mifugo ikiwemo malambo na mabwawa, kuzalisha mashamba darasa ya malisho, kuendeleza na kutoa elimu ya teknolojia ya uhamilishaji, kutenga, kupima na kumilikisha wafugaji maeneo ya ufugaji.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika kutekeleza maelekezo haya ya Ilani, Serikali inatoa elimu kwa wafugaji kufuga mifugo itakayompa tija mfugaji. Tumeanza kutambua mifugo kwa kuweka alama, kujua idadi na mahali ilipo ili kuweka takwimu, tumeagiza Maafisa Mifugo kuhudumia mifugo, tumezuia mifugo kutoka nje ili kuondokana na migogoro ya wafugaji na wakulima, magonjwa, n.k. tumetenga maeneo ya mifugo kila wilaya na mikoa. Hadi sasa, tumetenga jumla ya hekta 519,918 za maeneo ya ufugaji kwenye vijiji 80 katika Wilaya 17 za Mikoa 11 ya Tanzania Bara na kufanya jumla ya eneo lililotengwa hadi sasa kufikia hekta milioni 2.535 katika vijiji 728. Aidha, jumla ya hati za kumiliki ardhi kimila 44 zimetolewa kwa wafugaji katika Wilaya za Monduli, Ngorongoro, Hanang, Simanjiro na Karatu. Pia, Serikali imeanzisha mashamba darasa ya uzalishaji malisho katika Halmashauri za Bunda, Busega, Kiteto na Igunga. Lengo ni kuanzisha mashamba darasa katika maeneo yote ya wafugaji nchini.

Tumetoa mafunzo ya uhamilishaji kwa wahamilishaji 264 yanayohusu mabadiliko ya teknolojia, tumetoa vitendea kazi, ukarabati wa miundombinu, mitambo ili huduma za uhamilishaji ziwe za uhakika.

Pia, tunahamasisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo ili kumpatia faida kubwa mfugaji.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Mifugo yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 14 hadi wa 18 wa vitabu mlivyogawiwa).

3.3         USHIRIKA

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali inaendelea kusimamia sekta ya ushirika ambayo ilikuwa imepoteza mwelekeo. Dhana ya ushirika ni nzuri na endapo itasimamiwa vizuri, itamnufaisha mkulima. Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali za kufufua ushirika nchini kwa kufanya uhakiki wa mali na kusimamia fedha za ushirika.

Mheshimiwa Rais ameunda Tume ya Ushirika, tunaunda ushirika kwenye mazao yanayoendesha ushirika, tunachukua hatua kwa viongozi wanaofuja mali na fedha za ushirika, tulianza na ushirika   wa korosho, tumbaku, chai. Uchunguzi unafanywa kwa ushirika wa Kahawa. Tutaendelea na hatua hizo kwa mazao yote yanayoendeshwa kwa ushirika. Serikali inataka kuona Maafisa Ushirika wanasimamia ushirika ili mkulima mnyonge anufaike na kilimo kupitia ushirika.

3.4        MALIASILI NA UTALII

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Utalii ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa na ajira kwa wananchi. Kwa kutambua umuhimu wa sekta hiyo Serikali inasimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza utalii nchini kwa kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka, kuongeza bajeti ya sekta ya utalii, kuimarisha mafunzo ya utalii, kujenga mazingira ya kuwezesha vijana kuanzisha makampuni ya kitalii na kuhifadhi malikale. Pia tunatatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na mapori yaliyohifadhiwa kwa lengo la utalii.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya utalii ikiwemo kukarabati kilometa 2,571 za barabara zilizopo ndani ya hifadhi, njia za miguu zenye urefu wa kilometa 143.5 na kuongeza matangazo ya utalii ndani na nje ya Nchi. Juhudi hizo zimewezesha idadi ya watalii kuongezeka kutoka 1,137,182 mwaka 2015 hadi 1,284,279 mwaka 2016, sawa na ongezeko la asilimia 12 na kuliingizia Taifa Dola za Marekani Bilioni 2. Aidha, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imeongeza bajeti ya utalii hadi kufikia Shilingi Bilioni 6.6 ikilinganishwa na Shilingi Bilioni 4.2 zilizotengwa mwaka 2016/2017. Tunaimarisha matangazo ya vivutio vya Kitalii ili kuongeza idadi ya Watalii.

Serikali imehakiki mipaka yote ya maeneo ya hifadhi ikiwemo Ngorongoro kwa kuweka alama za kudumu na mabango ya tahadhari. Hadi mwezi Mei, 2017 vigingi 14,755 vimesimikwa, sawa na aslimia 62.4 ya vigingi 23,638 vinavyohitajika. Serikali inaendelea kudhibiti ujangili na uharibifu wa Misitu ili kulinda maliasili zetu.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Maliasili na Utalii yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 19 hadi wa 23 wa vitabu mlivyogawiwa).

3.5        VIWANDA

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali inahakikisha kuwa uchumi wa Nchi yetu unakua kwa kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda. Katika kujenga uchumi wa viwanda, Serikali imehamasisha wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Viwanda vinavyopewa kipaumbele ni vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini, vinavyotoa ajira kwa watu wengi na vinavyozalisha bidhaa zenye soko hapa ndani na nje ya Nchi.

Tumeona mwitikio mkubwa wa sekta binafsi kuwekeza katika viwanda. Baadhi ya viwanda vilivyoanzishwa katika kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 ni pamoja na; kiwanda cha kusindika maziwa cha Milkcom Ltd kilichopo Kigamboni – Dar-es-Salaam ambacho uwekezaji wake ni Shilingi Bilioni 44 na kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 67.5 za maziwa kwa mwaka na kutoa ajira kwa watu 500; kiwanda cha nyama cha Meat King Ltd kilichopo eneo la Moshono – Mkoa wa Arusha kimewekeza Shilingi Bilioni 5.5 kwa ajili ya kusindika nyama ya ng’ombe, kuku na kondoo; kiwanda cha Lakairo Polybag kilichopo Mwanza ambacho uwekezaji wake ni Shilingi Bilioni 4 chenye uwezo wa kuzalisha magunia ya sandarusi milioni 10 kwa mwaka; kiwanda cha Global Packaging kilichopo Kibaha – Pwani  kimewekeza Shilingi Bilioni 8 chenye uwezo wa kuzalisha magunia ya sandarusi milioni 11.75 kwa mwaka na ajira ya watu 110. Kiwanda cha Nyama kilichopo hapa Dodoma kinachinja Ng’ombe 350 – 500 kwa siku.

Baadhi ya viwanda vikubwa vinavyoendelea kujengwa hapa nchini ni: Kilua Steel Group – kiwanda cha nondo kinazalisha tani 2000 kwa siku; kiwanda cha marumaru cha Goodwill kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani; kiwanda cha kusokota nyuzi za pamba cha NAMERA kilichopo Gongolamboto, Dar-es-Salaam; kiwanda cha kukausha mbogamboga cha Vegeta Padravka Ltd kilichopo Bagamoyo – Pwani ambacho uwekezaji wake unatarajiwa kuwa Shilingi Bilioni 9.9 na kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kinachojengwa Mvomero – Morogoro ambacho kitahitaji ng’ombe 50,000 na mbuzi 60,000 kwa mwaka.

Serikali inaweka mkazo wa ujenzi wa viwanda, kila Mkoa ili kuzalisha bidhaa pia kupunguza tatizo la ajira nchini.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Viwanda yameelezwa  kwa kina kuanzia ukurasa wa 24 hadi wa 26 wa vitabu mlivyogawiwa).

3.6        MADINI

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Ili kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia kikamilifu katika kukuza uchumi na ajira, Serikali inaimarisha ukaguzi wa uzalishaji na mauzo ya madini katika migodi mikubwa na midogo nchini ambapo katika kipindi cha Novemba, 2015 hadi Novemba, 2017 jumla ya sampuli 8,497 za mikuo ya dhahabu na makinikia ya shaba (copper concentrate) kutoka kwenye migodi mikubwa zilifanyiwa uchunguzi kwenye maabara ili kujua kiasi na thamani ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa nje. Kaguzi pia zilifanywa katika Migodi ya Tanzanite One na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka ambazo zimeiwezesha Serikali kukusanya mrabaha wa jumla ya Dola za Marekani Milioni 6.99. Aidha, Serikali imefanya ukaguzi katika uzalishaji na mauzo ya madini ya ujenzi na viwandani katika Mikoa mbalimbali chini na kuwezesha malipo ya mrabaha wa Shilingi   Bilioni 9.97. Mrabaha huo unatokana na uzalishaji na mauzo ya tani milioni 20.69 za madini ya ujenzi na viwandani yenye thamani ya Shilingi Bilioni 324. Kwa sasa tunaendelea na ujenzi wa ukuta wa eneo la Tanzanite ili kudhibiti utoroshaji.

Vilevile, ukaguzi wa shughuli za uzalishaji na mauzo ya dhahabu kutoka kwa wazalishaji wanaotumia teknolojia ya “vat leaching” kuchenjua marudio katika Mikoa ya Mbeya, Mwanza, Geita, Shinyanga na Tabora umefanyika. Jumla ya kilo 2,500 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi Bilioni 183 zilizalishwa na wamiliki halali wa leseni katika maeneo hayo. Ukaguzi huo umewezesha malipo ya mrabaha wa kiasi cha Shilingi Bilioni 7.3. Ukaguzi umefanyika pia kwa Wachimbaji Wadogo wa dhahabu katika Wilaya za Chunya, Geita na Mpanda ambapo jumla ya Kilogramu 48.68 za dhahabu na mifuko 100,287 ya mawe yenye madini ya dhahabu yenye thamani ya wastani wa Shilingi Bilioni 6 ilizalishwa na wachimbaji hao na fedha Shilingi Milioni 244 zilikusanywa kama mrabaha. Mapato haya ni sehemu tu ya fedha zinazopatikana, nyingi zinapotea kwa utoroshaji wa madini yetu.

Katika jitihada za kulinda rasilimali za Taifa ikiwemo Rasilimali za Madini, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM aliagiza kuundwa kwa Tume mbili maalum za uchunguzi wa makontena yaliyokuwa na mchanga wa makinikia yaliyokamatwa bandarini, Dar-es-Salaam, na maeneo mbalimbali nchini na kuagiza kupata taarifa za uchunguzi huo. Aidha, Mheshimiwa Rais alizuia usafirishaji wa makinikia nje ya Nchi baada ya kugundua wizi wa utoroshaji unaofanywa na baadhi ya makampuni makubwa. Serikali ilitoa waraka wa sheria Bungeni wa kutunga Sheria ya Kulinda Rasilimali za Nchi. Tulikamata makontena yapatayo 423 yenye makinikia yaliyokuwa yanatoroshwa kwenda nje ya Nchi.

Serikali imehamasisha wawekezaji wa Smelter na Refinery kujitokeza kwa ajili ya kujenga mitambo hiyo hapa nchini. Jumla ya kampuni 25 zimeonesha nia na Serikali inaendelea na utaratibu wa kutafuta kampuni zitakazofaa kwa ajili ya ujenzi wa mitambo hiyo. Vilevile, Serikali itaendelea kuisimamia na kuilinda sekta ya madini na itaendelea kujiridhisha kuwa Watanzania wananufaika vizuri.

Ndugu Mwenyekiti  na WanaCCM wenzangu;
Serikali katika kipindi cha Novemba, 2015 hadi Julai, 2017 imetoa jumla ya leseni 4,207 zenye ukubwa wa kilomita za mraba 74.1 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini kote nchini. Aidha, jumla ya maeneo 11 yenye ukubwa wa hekta takribani 38,951 yenye uwezo wa kutoa leseni za uchimbaji 3,895 yametengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika Mikoa ya Kagera, Singida, Katavi, Ruvuma, Lindi, Tabora na Geita. Pia, Serikali imetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo 2,000 kuhusu teknolojia mbadala za uchenjuaji dhahabu, usalama migodini, ujasiriamali, utunzaji kumbukumbu na utunzaji wa mazingira.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Madini yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 26 hadi wa 32 wa vitabu mlivyogawiwa).

4.0.SEKTA YA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA KIUCHUMI

4.1.  ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali inatekeleza mipango ya kuendeleza ardhi ikiwa ni pamoja na kujenga mfumo utakaorahisisha umilikishaji wa ardhi na uhifadhi wa kumbukumbu za ardhi kwa kukamilisha ujenzi wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi, kutekeleza Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi, kutatua migogoro, kero ya ardhi kote nchini na kuhakikisha kuwa kila mwenye ardhi anapimiwa na kupewa hati.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imeanza kufunga Mfumo unganishi katika Halmashauri za Manispaa za Kinondoni na Ubungo Jijini Dar-es-Salaam. Kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Juni, 2018 na baadaye Mfumo huo utafungwa katika Halmashauri zote nchini. Aidha, Serikali imeboresha Mfumo wa Ukusanyaji Kodi ya Pango la Ardhi kwa kuweka Mfumo maalumu uitwao Government e-payment Gateway System katika Halmashauri 31 na hivyo kukomesha vitendo vya Maafisa Ardhi kugawa viwanja mara mbili; na sasa ada na tozo zote kulipwa kwa njia ya kielektroniki pia simu za mkononi. Serikali imeunda Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi yenye jukumu la kufuatilia na kuratibu malipo yote ya fidia yatakayofanywa na Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala, Mikoa na Halmashauri. Mwongozo wa namna shughuli za Mfuko wa Fidia ya Ardhi zitakavyofanyika umeandaliwa na kusambaza kwa wadau.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imefanya uhakiki wa mashamba pori yasiyoendelezwa ambapo ukaguzi wa mashamba ya uwekezaji 121 yenye ukubwa wa ekari 552,139 katika Mikoa ya Tanga, Morogoro, Dar-es-Salaam, Lindi, Manyara, Arusha Pwani, Njombe na Kagera umefanyika ambapo mashamba 58 yalibainika kutoendelezwa. Mashamba hayo pamoja na mengine yenye ukubwa wa ekari 429,654 yaliyopo katika Mikoa ya Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa na    Dar-es-Salaam yamefutiwa umiliki na kurudishwa kwa halmashauri husika kwa ajili ya kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi na kuigawa kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi yaliyopo katika eneo husika. Tutaendelea kubaini mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyagawa kwa wananchi.

 Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imepima vijiji 11,000 kati ya vijiji 12,545 Nchi nzima hadi kufikia Agosti, 2017. Pia, jumla ya hatimilki za kimila 69,208 zimeandaliwa na kutolewa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa upande wa upimaji wa viwanja, jumla ya hatimiliki za viwanja 82,633 na nyaraka za kisheria 122,106 zimesajiliwa na kutolewa. Kazi ya kubainisha viwanja 50,200 vitakavyorasimishwa katika Halmashauri za Manispaa za Musoma, Kigoma Ujiji, Tabora, Singida, Sumbawanga na Lindi inaendelea.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Ardhí, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 32 hadi  wa 40 wa vitabu mlivyogawiwa).

4.2.     UJENZI NA UCHUKUZI

4.2.1.   Barabara

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;

Serikali inaendelea kujenga miradi ya barabara na madaraja kwa kuzingatia vipaumbele kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama chetu. Ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza miradi ya barabara mijini na vijijini, Serikali imeanzisha Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini -TARURA yenye jukumu la kusimamia kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za mijini na vijijini ambazo ziko chini ya TAMISEMI ambazo hazipo chini ya Wakala wa Barabara Kuu yaani TANROADS.

Aidha, Serikali imeendelea kukamilisha kujenga barabara Nchi nzima. Zipo zilizokamilimika kwa kuunganisha Mikoa na miradi mbalimbali inatekelezwa kwa kiwango cha lami. Hii ni kukamilisha ndoto ya Mheshimiwa Rais ya kuwa Watanzania watasafiri kwa gari aina ya Mark II kutoka Sirari wilayani Tarime mkoani Mara hadi Mbamba Bay – Ruvuma, kwa kupita juu ya barabara ya lami.

Mpaka sasa tumekamilisha na tunaendelea na ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,500 kwa zaidi ya Shilingi trilioni 1.8 zikiwemo Barabara za:

(i)  Dodoma – Kondoa – Babati Km. 232; Shilingi Bilioni 335.46

(ii)  Tunduma – Sumbawanga Km. 223; Shilingi Bilioni 350.2

(iii) Tunduru- Nakapanya- Mangaka – Mtambaswala Km 202.5; Shilingi Bilioni 175.2

Ujenzi unaoendelea
(i)  Kidahwe –Kasulu Km 50: Shilingi Bilioni 46

(ii)  Nyakanazi – Kakonko Km 50; Shilingi Bilioni 46

(iii)Mafinga –Igawa Km 137.9; Shilingi Bilioni 235.4

(iv)Njombe – Makete Km 107.4; Shilingi Bilioni 217.53

(v)Arusha (Sakina) – Tengeru na mchepuo wa Arusha (Arusha by pass) Km. 56.5; Shilingi Bilioni 145.1

(vi) Mtwara – Mnivata Km 50; Shilingi Bilioni 89.59. Aidha tunaendelea kutafuta fedha kutangaza zabuni ya kuunganisha Newala – Masasi.

Wakati huohuo tunayo miradi iliyo katika maandalizi ya ujenzi na imetengewa fedha mwaka 2017/2018 yenye urefu wa zaidi ya Km 1,800 kwa thamani ya Shilingi trilioni 2.99  ikiwemo;

(i) Masasi-Nachingwea – Nanganga Km 91; Shilingi Bilioni 3.5

(ii)   Mbinga – Mbambabay Km 67; Shilingi Bilioni 129.3

(iii)  Tunduma – Sumbawanga, kazi inaendelea hadi Mpanda – Uvinza (mkandarasi yupo kazini).

Vivuko Na Madaraja
(i) Tumekamilisha ujenzi wa Kivuko cha juu cha Furahisha – Mwanza kwa Shilingi Bilioni 7.076 na Daraja la Mto Kilombero kwa Shilingi Bilioni 56.8, 

(ii) Sasa tunajenga madaraja ya juu (Flyover) ya TAZARA kwa Shilingi Bilioni 94, Ubungo Shilingi Bilioni 177.4 na tunatarajia kujenga Kivuko cha Mwenge.

Tunaimarisha usafiri jijini Dar-es-Salaam Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na tutajenga awamu tatu nyingine ili kuimarisha usafiri katika Jili la  Dar-es-Salaam kutoka:

§    Katikati ya Jiji – Mbagala

§    Katikati ya Jiji – Gongolamboto

§    Morocco – Mwenge – Tegeta.

Tutajenga pia Bandari Dar-es-Salaam; Bagamoyo; Mtwara.

Serikali inakusudia kutekeleza miradi iliyopangwa kwenye bajeti zaidi ya km 1,300 na tumefanya upembuzi yakinifu kwa kilometa 1,371. Aidha, Serikali inaendelea na ukarabati wa barabara za kwenye Miji na Halmashauri nyingi nchini.

(Kazi za ujenzi wa barabara za lami nchini tumefafanua kwenye Ukurasa 38 – 55)

4.2.2. Usafiri wa Anga

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
 Serikali imeimarisha Shirika letu la Ndege ambapo katika mwaka 2016/2017, Serikali iliingia mkataba wa ununuzi wa ndege mpya sita ambapo ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q 400 ziliwasili nchini Septemba, 2016 na zinaendelea kutoa huduma. Ndege moja, aina ya Bombardier Dash 8 Q 400 imekamilika na itawasili nchini wakati wowote. Ndege mbili aina ya C – series na Boeing 787-8 Dreamliner 1 zitakuwa zimeingia nchini ifikapo Juni, 2018.

Serikali inaendelea na ujenzi wa viwanja vya ndege. Uwanja wa Kimataifa wa JNIA – ujenzi wa Jengo Jipya (Terminal III) umefikia asilimia 66 na kazi ya ujenzi inaendelea. Tumekamilisha maeneo ya kusimamia ndege katika uwanja wetu wa KIA. Tunakamilisha jengo la kupokelea abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe. Tumepanua Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa thamani ya Shilingi Bilioni 60 na tunatarajia kuongeza njia kwa kilometa moja zaidi ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutua. Tunakamilisha ujenzi wa eneo la kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Tabora.

Serikali imesaini mikataba ya ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Shinyanga na Sumbawanga. Fedha zimetengwa mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Iringa (Shilingi Bilioni 3.76); Musoma (Shilingi Bilioni 3.85); Songea (Shilingi Bilioni 3.66); na Mtwara (Shilingi Bilioni 3.55). Tutatenga fedha kwa ajili ya Viwanja vya Ndege vya Lindi na Nachingwea. Tunaboresha kwa kuweka taa za kuongozea ndege na mawasiliano katika Uwanja wa Ndege wa Tabora. Tunarefusha njia ya kurukia, jengo la kuongozea ndege na jengo la mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kukamilisha jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.

4.2.3. Miundombinu ya Reli

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imeanza ujenzi  wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge kutoka Dar-es-Salaam–Tabora–Kigoma/Mwanza, Tabora–Mpanda, kipande cha Km. 300 kutoka Dar-es-Salaam hadi Morogoro kitakachogharimu Shilingi Trilioni 2.74 umeanza na Mkataba wa kuanza ujenzi wa kipande cha Km. 412 kutoka Morogoro hadi Dodoma (Makutopora) wenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.328 umesainiwa.  Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa reli ya Uvinza – Musongati imekamilika.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi zinaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia mradi huo. Pia, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa reli ya Mtwara – Songea – Mbamba Bay kwa thamani ya Trilioni 3.99 na matawi ya kwenda Mchuchuma na   Liganga (Km. 1,000) kwa Standard Gauge ilikamilika Juni, 2016. Vilevile, kazi ya usanifu wa kina wa njia ya Reli ya Tanga – Arusha imekamilika Mei, 2015 na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli mpya ya kutoka Arusha hadi Musoma (km 600) na matawi ya Engaruka (km 53), Minjingu (km 35) na tawi kuelekea Dutwa (km 2.8) pamoja na reli ya Tabora – Mwanza (km 120) unaendelea.

Tunatarajia kuongeza urefu wa reli kutoka Mpanda hadi Bandari ya Kalemie ili kuhudumia Ziwa Tanganyika.

4.2.4   Usafiri wa Majini

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali itaimarisha usafiri wa majini kwa kuwa na miradi ya kipaumbele. Serikali imeanza kutekeleza ahadi ya kuboresha usafiri wa majini kwenye Ziwa Tanganyika, Nyasa na Victoria.

Ziwa Tanganyika, taratibu za ununuzi wa Meli mpya unaendelea na watalaam. Meli ya thamani ya Shilingi Bilioni 24 yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na mizigo tani 200 itapatikana.

Ziwa Victoria, mchakato wa kumpata Mkandari kutoka Korea Kusini umakamilika. Meli ya thamani ya Dola za Marekani Milioni 37 yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400 itapatikana.

Kuhusu Ziwa Nyasa, Serikali imeshapata Meli 2 za mizigo zenye uwezo wa tani 1,000 kila moja kwa thamani ya Shilingi Bilioni 11.252 na sasa tunakailisha ujenzi wa Meli yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo ya thamani ya Shilingi Bilioni 9.119.

(Mafanikio tuliyoyapata katika sekta nzima ya Ujenzi na Uchukuzi yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 41 hadi  wa 69 wa vitabu mlivyogawiwa)

4.3.          NISHATI

4.3.1. Uzalishaji wa Umeme

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
 Serikali inaongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza Miradi mikubwa ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I na II ambayo kwa pamoja inatarajiwa kuzalisha megawati 565 kwa kutumia gesi asilia kwa gharama ya Shilingi Trilioni 1.2 na maandalizi kwa ajili ya miradi ya Kinyerezi III na IV ambayo itazalisha takribani megawati 600 inaendelea. Vilevile, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa maji wa Staglier’s Gorge ambao utazalisha megawati 2,100. Pia, Serikali imekamilisha Mradi wa Backbone wa kV 400 unaounganisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga wenye urefu wa Km. 670. Serikali inashughulikia tatizo kubwa linalokabili Mikoa ya Lindi na Mtwara kukosa umeme wa uhakika. Tumeagiza mashine zitakazoziba pengo la mashine zilizoharibika. Pamoja na mashine hizo, Serikali itaunganisha kwenye gridi ya taifa mikoa hiyo kutoka Dar-es-Salaam.

Serikali pia inakamilisha ujenzi wa njia ya umeme kutoka Makambako, Njombe, Madaba, Songea, pia Madaba hadi Ludewa kupitia Liganga. Kazi inaendelea. Serikali inajenga vituo vya kuongeza nguvu ya umeme Njiro – Arusha, Mahumbika – Lindi na Madaba – Songea ili kuwezesha usambazaji umeme wa uhakika hadi vijijini. Aidha, Serikali imeendelea kuhamasisha uzalishaji wa umeme wa jua kwa kutumia gridi ndogo katika maeneo ambayo hayafikiwi na Gridi ya Taifa ambapo hadi sasa kuna takribani MW.10 zinazalishwa. Pia Mradi mkubwa wa Kishapu –Shinyanga MW. 150 unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na Mradi wa Chuo Kikuu cha Dodoma MW. 55 unatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Kwa sasa mgao umepungua na matarajio yetu ni kuwa tutauza umeme nje ya Nchi.

4.3.2.  Umeme Vijijini

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Kwa upande wa umeme vijijini, Serikali imekamilisha kwa asilimia 98 Mradi Kabambe wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA Turn-key Projects phase II), jumla ya wateja 172,000 kati ya wateja 250,000 wameunganishwa na kazi inaendelea. Wakala wa Kusambaza Nishati Vijijini (REA) imeongezewa fedha ambapo katika bajeti ya Mwaka 2017/2018, Wakala ilitengewa Shilingi Bilioni 667.48 ikilinganishwa na Shilingi Bilioni 587.61 zilizotengwa katika Mwaka wa fedha 2016/2017. Duru ya kwanza ya Awamu ya Tatu ya Mpango Kabambe wa Kusambaza Umeme ambayo imeanza itahusisha kupatiwa umeme kwa vijiji 3,559 na vijiji vitakavyosalia vinavyofikia 4,314 vitapatiwa umeme katika duru ya pili ya Awamu ya Tatu ikihusisha maeneo yaliyopo nje ya gridi. Pia, umeme utapelekwa katika maeneo ambayo hayakupitiwa katika awamu mbili za mwanzo hii ni pamoja na taasisi za elimu, afya na pampu za maji katika maeneo ya vijijini.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Nishati yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 70 hadi  wa 74 wa vitabu mlivyogawiwa).

4.4.      MAWASILIANO

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu
Serikali inahakikisha kuwa Taasisi za Elimu, Ofisi za Wakuu wa Wilaya/Polisi, Hospitali zote za Wilaya, Vyuo Vikuu na Vituo vya Posta 65 ziunganishwe katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Kwa kushirikiana na Kampuni ya VIETTEL hadi kufikia mwezi Septemba, 2017 Serikali imefikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Ofisi za Halmashauri 117, Vituo vya Posta 71, Vituo vya Polisi 129, Hospitali za Wilaya  90, Mahakama 27 na huduma ya intaneti bure kwa miaka mitatu katika shule 425.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali inafikisha huduma za simu za viganjani kwa wananachi wote ambapo kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Kata 443 zenye uhitaji wa huduma za mawasiliano zimepata wazabuni wa kupeleka mawasiliano husika. Kati ya kata hizo 443, upelekaji wa mawasiliano umekamilika katika kata 391 na Kata 52 zilizobaki zinategemewa kufikishiwa huduma hiyo kabla ya mwisho wa mwaka 2019. Vilevile, kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Serikali imetoa zabuni ya kufikisha huduma ya mawasiliano katika kata 75 zenye vijiji 154 ambazo zinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2018.

Kampuni ya Viattel imepewa zabuni ya kufikisha mawasiliano kwenye vijiji 4,000 vilivyobaki katika mwaka huu wa fedha.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Mawasiliano yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 74 hadi wa 77 wa vitabu mlivyogawiwa).

5.0.      HUDUMA ZA JAMII

5.1.      AFYA

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali inaimarisha huduma za Afya ili ziwafikie wananchi wote hadi vijijini ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Katika kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 hadi Novemba 2017, Serikali imeongeza Vituo vya kutolea huduma za Afya kutoka Vituo 7,014 mwaka 2014/2015 hadi 7,284 mwaka 2016/2017, sawa na  ongezeko la Vituo 269. Serikali imekamilisha ujenzi wa Hospitali za Mlonganzila, Benjamin William Mkapa na Hospitali za Rufaa kwa ngazi za Mikoa. Wilaya sasa zimeanza kujenga hospitali na ujenzi umefikia hatua mbalimbali katika maeneo tofauti. Hivi sasa Halmashauri 15 zinaendelea na ujenzi wa hospitali za Wilaya, Halmashauri nyingine 15 zipo katika hatua ya kupandisha hadhi Vituo vya Afya kuwa hospitali za Wilaya na Halmashauri 13 zimetenga maeneo na kuanza maandalizi ya ujenzi. Hospitali za Mikoa zote sasa zinahamishiwa Wizara ya Afya.

Aidha, Serikali imehamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ambapo idadi ya watu waliojiunga imeongezeka kufikia asilimia 34 mwaka 2017 kutoka asilimia 19 ya mwaka 2015. Uhamasishaji kwa wananchi walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) unaendelea katika Mikoa mbalimbali nchini.

Vilevile, Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi Bilioni 260 mwaka 2017/2018. Hadi mwezi Juni, 2017, asilimia 83 ya dawa muhimu zaidi (essential medical items) zinapatikana katika Bohari ya Dawa na hali ya upatikanaji wa dawa kwenye Hospitali kufikia mwishoni mwa mwezi    Julai 2017 ni asilimia 86.3. Lengo la Serikali ni kuondoa tatizo la ukosefu wa dawa, Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Afya yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 77 hadi wa 89 wa vitabu mlivyogawiwa).

8.3.      ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali inaboresha Sekta ya Elimu kuwa ya mwelekeo wa Sayansi na Teknolijia ili kufanikisha ujenzi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea.

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali ya Awamu ya Tano  ilianza kutekeleza Mpango wa Elimu Bila Malipo kuanzia shule za msingi hadi sekondari ambapo tangu Januari, 2016 Serikali ilitenga Shilingi Bilioni 18.77 kila mwezi kwa ajili ya kugharamia Elimu Bila Malipo. Mwezi Julai 2016, kiasi hicho kiliongezwa hadi kufikia Shilingi Bilioni 23.868, na hivyo kufanya Serikali kutumia jumla ya Shilingi Bilioni 465.6 kugharamia elimu bila malipo hadi mwezi Agosti, 2017. Hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi walioandikishwa Darasa la I kutoka 1,568,378 mwaka 2015 hadi kufikia wanafunzi 2,120,667 mwaka 2016. Changamoto iliyojitokeza ni upungufu wa madawati na Walimu. Madawati yametolewa ya kutosha na ajira za Walimu zimeanza kutolewa.

Aidha, Serikali imeweka juhudi katika kujenga maabara ambapo kwa sasa shule za Serikali zenye maabara ni 2,141 kati ya 3,614 na zisizo za Serikali zenye maabara ni 1,075 kati ya 1,145. Aidha, Serikali imenunua na kusambaza vifaa vya maabara vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa Shule za Sekondari 1,696 kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa Masomo ya Sayansi kwa nadharia na vitendo.

Vilevile, Serikali imeongeza Bajeti ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka Shilingi Bilioni 365 mwka 2015 hadi Shilingi Bilioni 483 mwaka 2017 na kuwezesha idadi ya Wanafunzi wanaopata Mkopo wa    Elimu ya Juu kuongezeka kutoka 98,300 mwaka 2015 hadi wanafunzi 125,000 mwaka 2017.

(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Elimu yameelezwa wa kina kuanzia ukurasa wa 90 hadi wa 100 wa vitabu mlivyogawiwa).

9.4.      MAJI

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;

Serikali imeweka nia ya dhati ya kuwapatia wananchi huduma ya maji safi, salama na ya kutosha, Mheshimiwa Rais ameanzisha kampeni ya kumtua ndoo mama kichwani yenye lengo la kumhudumia mwananchi kupata maji kwa umbali mfupi. Serikali imeboresha huduma ya maji vijijini ambapo hadi Septemba 2017, jumla ya miradi 1,423 ya maji vijijini ilikuwa imekamilika na kufanya jumla ya vituo vya maji vilivyojengwa kwenye miradi kufikia 117,190. Vituo hivyo vina uwezo wa kuhudumia watu 29,297,500, sawa na asilimia 79. Vilevile, Serikali inaendelea kukamilisha miradi mikubwa ya maji ya; kutoa Maji Ziwa Victoria kwenda Miji ya Igunga, Nzega, Sikonge na Tabora kwa thamani ya Shilingi trilioni 1.5, Busega – Bariadi hadi Itirima, Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe; Mradi wa Maji wa Chalinze; Mradi wa Maji Kutoka Ziwa Victoria hadi Miji ya Kahama na Shinyanga wa Shilingi trilioni 1.1. Aidha, Serikali inaboresha huduma ya maji katika Miji 17 kwa thamani ya Shilingi trilioni 3.4. Serikali inajenga miradi ya Arusha Jiji – Bilioni 476 na Longido – Bilioni 16. Upanuzi wa mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, Ulazaji wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara na ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo cha Ardhi kwa Jiji la Dar-es-Salaam umekamilka Agosti, 2017. Miradi mingine mingi ipo katika hatua mbalimbali.

(Mafanikio tuliyoyapata katika sekta ya maji yameelezwa kwa kina kuanzia Ukurasa wa 101 hadi wa 111 wa vitabu mlivyogawiwa).

10. KUIMARISHA MUUNGANO

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;

Katika kipindi hiki vimefanyika vikao vya majadiliano katika ngazi ya Makatibu Wakuu, Mawaziri wa SMT na SMZ chini ya Uongozi wa Makamu wa Rais na kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ. Kupitia vikao hivyo baadhi ya changamoto zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. Changamoto hizo ni pamoja na: masuala ya fedha; masuala ya ajira katika taasisi za Muungano na hoja ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Serikali imefuatilia utekelezaji wa miradi na program za pamoja zinazotekelezwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


(i) Mpango wa MKURABITA: Mpango huu umeendelea na shughuli za kuandaa, kuongoza na kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Kitaifa wa Umiliki Rasilimali na Uendeshaji Biashara utakaoboresha sheria, kanuni na taratibu za kijamii.

(ii) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III): Programu hii imekuwa na mafanikio kwa wananchi wa pande mbili za Muungano ambapo ruzuku zinazotolewa kwa walengwa zimewasaidia kupata mahitaji ya msingi yakiwemo ya chakula, mahitaji ya shule kwa watoto na miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato.

(iii) Programu ya Kuendeleza Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani ya Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini – MIVARF; Programu hii imetekelezwa kwa mafanikio kwa wananchi wa pande mbili za Muungano kwa kujenga miundombinu muhimu ya masoko kuongezewa thamani ya mazao yao, kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na masoko na huduma za fedha vijijini.

11.  UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;

Mapambano ya dhati ya vitendo vya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi kwa kuanzisha Mahakama Maalumu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Hadi Juni 2017, jumla ya mashauri 30 yalipokelewa ambapo mashauri nane yamesikilizwa kwenye masjala ya Dar-es-Salaam na Mashauri 22 yamesikilizwa katika masjala ndogo zilizopo kwenye kanda mbalimbali za Mahakama Kuu ya Tanzania. Aidha, Serikali imeimarisha mfumo wa utoaji haki kwa kujenga Mahakama za Wilaya na Mahakama ya Mwanzo. Pia, kufanya ufuatiliaji na tathmini ya Usimamizi na Ukaguzi wa shughuli za kimahakama katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Pwani, Singida, Tabora, Mwanza na Mara ikihusisha Mahakama za Mwanzo 26, Mahakama za Wilaya 18 na Mahakama za Hakimu Mkazi sita.

12. KUHAMIA MAKAO MAKUU DODOMA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu
;
Tarehe 23 Julai, 2016 ulitangaza uamuzi wa kuhamishia Shughuli za Serikali kutoka Dar-es-Salaam kwenda Dodoma. Awamu ya kwanza ilitekelezwa mwezi Septemba 2016 hadi Novemba 30, 2017 ambapo jumla ya watumishi 2,869 walihamia Dodoma wakiwemo Waziri Mkuu, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na watumishi wengine wa kada mbalimbali. Hivi sasa Serikali inaendelea kuhamisha watumishi Awamu ya Pili na Tatu ambapo watumishi wengine wapatao 5,136 watahamia katika mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais amehamia rasmi tarehe 15 Desemba 2017 na Mheshimiwa Rais atahamia wakati wowote hadi 2019.

Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo mapya ya Serikali Dodoma. Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) wameshahamishia Ofisi yao Dodoma.

13. UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI

Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;

Serikali imehamasisha wananchi kuanzisha na kuendeleza Vyama vya Ushirika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Hadi kufikia Juni 2017, Vyama vya Ushirika vimeongezeka kufikia 10,596 zikiwemo SACCOs 5,640. Vyama hivyo vina jumla ya wanachama Milioni 1.3  na vina hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 52.9.  Aidha, Serikali kupitia Mifuko mbalimbali imetoa mikopo ya jumla ya Shilingi Trilioni 1.4 kwa zaidi ya wananchi 750,500.

Pia, katika Mwaka 2016/2017, Halmashauri zilitenga Shilingi Bilioni 28.4 kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake ambapo hadi Juni, 2017 Shilingi Bilioni 8 zilikopeshwa kwenye vikundi 6,076 vya vijana vyenye wanachama 30,380. Tumeanzisha Mfuko wa Uwezeshaji ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo pia umeanza kuwezesha makundi ya ushirika vijijini wakiwemo walemavu.

Serikali imeipa SIDO Shilingi Bilioni 7 ili kukopesha wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo. Hata hivyo, Serikali imetoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa kuwaruhusu Machinga kufanya biashara kwa kuwapangia maeneo mazuri kufanya biashara zao bila bughudha.

14. UJUZI KWA VIJANA
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaelekeza kuweka maeneo mahususi ya kuwezesha vijana wawe na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri katika soko la ajira la ndani na la nje ya Nchi. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imefanya mambo yafuatayo:-

(i)  Kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi (Apprenticeship);

(ii)  Kutoa mafunzo ya ujuzi na uzoefu kazini (Internship).

(iii)  Kutoa mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo ambayo yanatambua watu wenye ujuzi uliopatikana katika mfumo wa mafunzo usio rasmi.

(iv) Kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini kwa lengo la kuijengea uwezo nguvukazi iliyopo kazini.

Tangu programu hii ianze kutekelezwa mwaka 2016/17, jumla ya vijana 11,492 wamepatiwa mafunzo katika fani mbalimbali kupitia Vyuo vya umma, binafsi na makampuni. Kati ya vijana hao, 3,000 wamepatiwa mafunzo ya kubuni na kutengeneza nguo kwa kutumia teknolojia za kisasa kupitia viwanda vya Tooku (Dar-es-Salaam) na Mazava (Morogoro). Aidha, zaidi ya vijana 2,600 kati ya waliopata mafunzo hayo wameajiriwa na viwanda hivyo.

15.  MWISHO


Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli chini ya Chama cha Mapinduzi bado iko imara.

Nyote mmeshuhudia mengi yaliyofanywa katika kipindi hiki kifupi. TUENDELEE KUMUOMBEA NA KUMUUNGA MKONI. CCM MPYA TANZANIA MPYA.

CCM OYEE!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
MAPINDUZI!x2

Ndugu Mwenyekiti naomba kuwasilisha.
Asanteni kwa Kunisikiliza.

Sadifa apata dhamana baada ya kukaa rumande siku saba

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis anayekabiliwa na makosa ya rushwa ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Sadifa amefikishwa mahakamani leo Jumanne Desemba 19,2017 baada ya kukosa dhamana Jumatatu Desemba 11,2017 kutokana na upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana kwa madai kuwa angevuruga upelelezi na kuingilia uchaguzi wa UVCCM uliofanyika Desemba 10 na 11,2017 mjini Dodoma.

Mahakama leo imetupilia mbali pingamizi hilo na kutoa masharti ya dhamana kwamba Sadifa awe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh1 milioni na wenye vitambulisho vinavyotambuliwa na mamlaka ya maeneo wanakoishi.

Sadifa pia ametakiwa kutotoka nje ya mipaka ya nchi bila kibali cha Mahakama. Amekidhi masharti hayo na amechiwa kwa dhamana na kesi itatajwa Januari 18,2018.

Alipofikishwa mahakamani awali, wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Biswalo Biswalo alidai Sadifa anashtakiwa kwa makosa mawili.

Katika shtaka la kwanza anadaiwa Desemba 9,2017 katika makazi yake kwenye Kata ya Mnada mjini Dodoma akiwa mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM aliwahonga wanachama ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.

Sadifa katika shtaka la pili anadaiwa katika eneo hilo na siku hiyohiyo, aliwaahidi kuwalipia usafiri wanachama wa umoja huo kuwasafirisha kutoka Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi huo.

Biswalo alisoma hati ya kiapo iliyotolewa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga kupinga maombi ya dhamana kwa sababu endapo atapewa dhamana atavuruga upelelezi na kuingilia uchaguzi wa vijana.

Wakili wa Utetezi, Godfrey Wasonga alipinga hoja hiyo akisema makosa aliyoshtakiwa nayo mteja wake yana dhamana na hawezi kuingilia uchaguzi kwa kuwa ulishafanyika na mshindi alishatangazwa.

Kutokana na mabishano hayo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Joseph Fovo aliahirisha kesi hadi leo Desemba 19,2017 kutoa nafasi ya mahakama kupitia kiapo kilicholetwa na upande wa mashtaka ili kutoa haki katika maombi ya dhamana ya mshtakiwa. Sadifa alipelekwa rumande.

CCM yapewa meno dhidi ya Serikali

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli ametoa onyo kwa viongozi wa Serikali na hasa anaowateua kuwaheshimu na kuzingatia maagizo yanayotolewa na viongozi wa chama hicho, vinginevyo atawachukulia hatua.

Dk Magufuli aliitoa kauli hiyo jana mara mbili alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa chama hicho asubuhi na akairudia tena alipokuwa anaufunga usiku.

Katika mkutano huo uliofanyika siku nzima na kuonyeshwa muda wote moja kwa moja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Magufuli alichaguliwa na wajumbe wa mkutano huo kuwa mwenyekiti wa CCM kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kupigiwa kura zote 1,828 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

“Viongozi wa Serikali wanapaswa kutambua kwamba viongozi wa CCM ndio hasa wanaostahili. Kiongozi wa Serikali wa cheo chochote anawajibika kwa viongozi wa CCM,” alisema Rais Magufuli na kuamsha shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.

“Viongozi wa Serikali katika ngazi yoyote watambue kuwa waajiri wetu wakuu ni CCM, mimi bila CCM nisingekuwa Rais, CCM ndiyo kimejadili jina langu. Tupo hapa kwa ajili ya kutekeleza ilani ya CCM na wenye ilani hiyo ni hawa hapa (wajumbe) nendeni mkawasikilize,” alisema.

Dk Magufuli alionya asijitokeze kiongozi yeyote wa Serikali wa kusema hayajui (mambo) ya CCM.

“Kama mimi Rais niliyewateua ninayajua ya CCM asitokee mtu yoyote akasema hayajui mambo ya chama changu,” alisema.

Hata hivyo, alisema kauli hiyo isiwavimbishe kichwa viongozi wa CCM na kufanya mambo kinyume wakitegemea uongozi wao ndani ya chama hicho tawala.

“Nataka viongozi wa CCM kuheshimu viongozi wa Serikali na viongozi wa Serikali kuheshimu sana sana sana viongozi wa chama,” alisisitiza.

Katika mkutano huo, Magufuli alichaguliwa kwa kupata kura zote 1,828, huku makamu mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akichaguliwa kwa kura 1,827. Makamu mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akichaguliwa kwa kura 1,819.

Viongozi hao watatu walichaguliwa kwa kupata asilimia 100 ya kura zilizopigwa.

Mkutano huo pia uliwachagua wajumbe 30 wa Halmashauri Kuu (NEC) kati yao 15 kutoka Tanzania Bara na 15 wa Zanzibar.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images