Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 17


TAKUKURU Wamtia Mbaroni Rais mstaafu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) Gracian Mkoba

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU inamshikilia Rais mstaafu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) Gracian Mkoba kwa tuhuma za rushwa.

Hilo limethibitishwa na Afisa Uhusiano wa TAKUKURU Makao Makuu, Mussa Misalaba, ambaye amesema wanamshikilia Mkoba kwa tuhuma za kugawa fedha kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho ili kuwashawishi wamchague mgombea anayemtaka.

"Mukoba ameshastaafu, lakini kuna mgombea mmoja alikuwa anataka achaguliwe, tumemkamata leo asubuhi akigawa rushwa kuwashawishi wapiga kura kwenye ukumbi wa Chimwaga wamchague huyo mgombea wake," amesema Misalaba.

Misalaba ameongeza kuwa TAKUKURU inaendelea kufanya uchunguzi zaidi dhidi ya Mukoba kabla ya kumfikisha mahakamani.

Mukoba anakuwa mtu wa tatu kukamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa kwenye uchaguzi ndani ya wiki moja, wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis na mfanyabiashara Haider Gulamali.

Zitto Awaumbua Msando, Kitila na Mghwira......Kadai Kilichowaondoa ni madaraka na ahadi walizopewa

$
0
0
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema wanachama wa Chama hicho waliohamia Chama cha Mapinduzi (CCM) sio kweli wanaunga mkono juhudi za Rais bali ni kwaajili ya madaraka na ahadi walizopewa.

Hayo ameyasema jana kwenye hotuba yake kwa Kamati Kuu Juu ya chama hicho juu ya Hali ya Siasa Nchini Tanzania. 

Mh. Zitto alieleza kuwa hoja inayotolewa na wanachama wanaohama ACT Wazalendo ya kuunga mkono jitihada za Rais haina mashiko kwani walikuwa na nafasi ya kuunga mkono wakiwa ndani ya chama hicho.

"Takribani watu wote wanaoondoka kutoka vyama vya upinzani kwenda chama tawala wanasema wanaunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Tawala katika uendeshaji wa nchi yetu. Hii sababu haitoshi kueleza maamuzi yao, hususani kwa wale wanaotoka chama chetu cha ACT Wazalendo", alisema Zitto.

Kiongozi huyo wa Chama aliongeza kuwa Halmashauri Kuu ya Chama iliyooketi katika ukumbi wa Jeshi la Wokovu, Aprili, 2016 iliazimia masuala ambayo chama hicho kinaweza kuunga mkono ikiwemo mapamabno dhidi ya Ufisadi.

"Ni dhahiri kuwa wenzetu wana sababu zaidi ya kumuunga mkono Rais, kuna ambao sababu ni vyeo walivyopewa, na wengine ahadi za vyeo watakavyopewa", alisema Zitto.

Chama Cha ACT Wazalendo hivi karibuni kimeondokewa na wanachama wake waandamizi ambao ni Profesa Kitila Mkumbo, Anna Mghwira, Albert Msando, Samson Mwigamba na Edna Sunga. Wote wamejiunga na CCM.

Serikali Yazungumzia Hali ya Uchumi wa Nchi

$
0
0
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) inaonyesha uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.

Dkt. Abbasi aliyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.

“Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8, takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya,” alisema Dkt. Abbas.

Aidha, kutokana na usambazaji mzuri wa chakula mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 ikiwa ni chini ya lengo ambalo IMF ilitabiri mfumuko ungekuwa asilimia 5.

Aidha alisema, Serikali imeendelea kulipa madeni ya ndani ambapo mpaka sasa Shilingi bilioni 900 zimeshalipwa na shilingi bilioni 37 zimelipa madeni ya watumishi wa Serikali.

Timu hiyo ya wataalamu kutoka IMF iliongozwa na Bw. Mauricio Villafuerte ambapo walifanya ziara juu ya tathimini ya uchumi katika nchi Saba Afrika ikiwemo Tanzania pamoja na Msumbiji, Rwanda, Nigeria, Uganda, Senegari na Cape Verde.

==>Msikilize hapo chini

Ramsey Nouah alivyofanya ibada kwenye kaburi la Kanumba Huku mama Kanumba Akilia kwa Uchungu

$
0
0
Muigizaji kutoka nchini, Nigeria Ramsey Nouh ambaye alifanya movie moja itwayo ‘King Of Devil’ na marehemu Steven Kanumba, ametua nchini Tanzania wiki hii kwaajili ya kukutana na wasanii wa Bongo Movies ambapo jana alipata nafasi na kunywa chai na Mama Kanumba na baadaye kwenda makaburini kwaajili na ibada.

Wakiwa makaburini hapo, Ramsey na Mama Kanumba walitumia muda mwingi kukumbatiana na kulia kwa huzuni jambo lililoteka na kuvuta hisia za watu wengi. 

Mbali na tukio hilo, Ramsey alizidisha machungu kwa mama huyo baada ya kuanza kutamka maneno kama anazungumza na marehemu Kanumba ambapo alimueleza mambo yenye kuumiza.

“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,” alisema Ramsey katika mazungumzo yale na Kanumba aliyoyatoa kwa hisia kali hali iliyomsababishia Mama Kanumba maumivu makali. 

Maombolezo ya askari 14 wa JWTZ waliouawa pembeni ya Daraja la semuliki huko Beni Kivu kaskazini

$
0
0
Maombolezo ya askari 14 wa JWTZ  waliouawa pembeni ya Daraja la semuliki huko Beni Kivu kaskazini

==>Tazama hapo chini

Rais Magufuli atoa wito kwa viongozi wa dini kuliombea taifa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli leo tarehe 17 Desemba, 2017 wameungana na waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma kusali ibada ya Jumapili.

Akizungumza baada ya Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli amewashukuru viongozi wote wa dini na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa kuendelea kuliombea Taifa ili lidumishe amani na upendo.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali anayoiongoza inatambua juhudi zinazofanywa na viongozi wa Dini katika kudumisha amani na upendo na ameahidi kuwa itaendelea kushirikiana nao katika kujenga Tanzania bora.

“Nawaomba viongozi wa madhehebu yote ya dini tuendelee kuliombea Taifa letu liwe na amani na upendo, na Serikali itashirikiana nanyi muda wote” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Padre wa kanisa hilo Fr. Sergio Madinda amemshukuru Mhe. Rais kwa ushirikiano wake na kanisa na pia amemshukuru kwa uamuzi wake wa kuhamishia Serikali Dodoma.

Katika Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli ametoa Shilingi Milioni 3 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kigango cha Michese na kwaya ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma

17 Desemba, 2017

Rais Dkt. Magufuli ateuliwa kugombea CCM


ACT-Wazalendo yaungana na UKAWA kususia chaguzi za Januari 13, yatoa sababu tatu

$
0
0
ACT Wazalendo Kutoshiriki Uchaguzi wa Marudio wa Tarehe 13 Januari 2017

Jana, Disemba 16, 2017, Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo ilifanya kikao chake cha dharura jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kujadili hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama, Hali ya Uchumi wa Nchi, kupokea taarifa juu ya mwenendo wa Chaguzi ndogo katika Kata 43 nchini uliofanyika Novemba 26, 2017, pamoja na kutoa uamuzi juu ya ushiriki wa Chama katika chaguzi ndogo zilizotangazwa karibuni na tume ya uchaguzi nchini (NEC) na kutarajiwa kufanyika Januari 13, 2018.

A: Hali ya Nchi (Kisiasa na Kiuchumi)

Kamati Kuu ilijadili mwenendo wa matukio tangu ilipotoa taarifa yake juu ya kuisnyaa kwa uchumi wa nchi pamoja na taarifa za takwimu za Serikali. Tangu kukamatwa kwa Kiongozi wa Chama, kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, kuhojiwa kwa Katibu Mkuu wa Chama, Kuzuiwa kwa simu ya Kiongozi wa Chama, pamoja na Kompyuta za Chama pamoja na wito wa kutaka kuihoji Kamati Kuu nzima ya Chama kwa sababu ya taarifa yake juu ya takwimu za Serikali. Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo inapinga unyanyasaji unaofanyika dhidi yetu kwa sababu tu ya chama chetu kuzungumzia masuala ya Uchumi wa nchi unaosinyaa.

Juzi, Disemba 13, 2017 Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeitaka Serikali itazame upya vyanzo vyake vya takwimu za uchumi ili kupata picha halisi ya Hali ya uchumi wa Taifa letu. IMF wamethibitisha kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania unashuka (unasinyaa) kutoka 7.2% mpaka 6.8%, na kwamba Takwimu za Serikali ni lazima zitazamwe upya. Jambo ambalo sisi ACT Wazalendo tulilisema kabla.

Jeshi letu la Polisi halijavamia Ofisi za IMF na kumuweka ndani Mkurugenzi wake mkazi hapa nchini, inasikitisha kwamba Serikali inawasikiliza na kuheshimu zaidi maoni ya kiuchumi ya IMF kuliko yanayotolewa na Watanzania. Maoni kama ya IMF yalipotolewa na ACT Wazalendo yalisababisha unyanyasaji mkubwa kwa Viongozi wetu. Tunatarajia kuwa Jeshi la Polisi litarudisha vifaa vyote vya chama lilivyo navyo, na kutuacha kuendelea na uchambuzi wa shughuli za Serikali kwa uhuru.

Jambo moja muhimu ambalo watu wa IMF wameiambia Serikali ni suala la kuheshimu Bajeti. Mtakumbuka tulieleza katika kikao kilichopita kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza tabia ya kutumia fedha za Mashirika ya Umma bila kufuata taratibu za sheria. Kwa mfano mapema katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali ilipata gawio la shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kutokana na faida ya benki hiyo mwaka 2015/16. Taarifa juu ya gawio hilo inapatikana katika wavuti ya BOT.

Kinyume na utaratibu, Serikali haikutoa taarifa juu ya gawio hili popote kwenye taarifa zake za kiFedha. Mapato haya hayakupelekwa Bungeni kugawiwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa ni kuwa Serikali iliamua kutumia fedha hizi kulipia Mkandarasi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato, pamoja na madeni ya ndege za Bombardier na Boeing bila kufuata taratibu za sheria za fedha na bila Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG kuidhinisha kwa mujibu wa Katiba. Utaratibu unataka fedha kuingia kwenye Mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kisha kuidhinishwa na CAG, na ndipo Serikali kuanza kutumia.

Shilingi bilioni 300 kutumika na Serikali bila kushirikisha Bunge na kufuata sheria za nchi ni kusigina Katiba na kudharau Taasisi za Uwajibikaji za nchi. Kamati Kuu inamtaka CAG afanye ukaguzi maalumu wa fedha hizi na kutoa taarifa kwa Bunge, ili Bunge lichukue hatua za kuiwajibisha na kuisimamia Serikali ipasavyo.

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya hali ya usalama nchini, hasa juu ya mwenendo wa watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Tukio la karibuni likiwa ni kupotea kwa Mwandishi wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications, ndugu Azory, mwandishi wa habari za uchunguzi, hasa wa eneo la Kibiti. Tunaungana na Familia yake, waandishi wenzake, wa ndani na Nje ya Nchi, pamoja na Watanzania wote, kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha Azory anapatikana akiwa hai.

B: Nafasi ya Chama chetu juu ya Miswada inayokwenda Bungeni mwaka 2018

Moja ya ajenda kubwa ya Chama chetu ni Hifadhi ya jamii. Chama chetu kinataka haki ya hifadhi ya jamii kwa kila raia ili kuwa na Taifa ambalo raia wake wote wana bima ya afya na uhakika wa pensheni uzeeni. Katika ilani ya Uchaguzi ya Chama chetu tuliahidi mabadiliko makubwa ya mfumo wa hifadhi ya jamii ikiwemo kuunganisha mifuko iliyopo na kubakia na mifuko 3 tu. Mifuko miwili ya pensheni, na mfuko mmoja ni mfuko wa Taifa wa bima ya afya.

Serikali imeamua kutekeleza wazo letu hilo na tayari muswada wa sheria ya hifadhi ya jamii umewasilishwa bungeni kwa ajili ya kuanza kufanyiwa kazi na kuunda mifuko miwili tu. Tunapongeza hatua hii ya Serikali kuchukua mawazo yetu na kuyafanyia kazi, japo utekelezaji wake unafanyika vibaya, na hivyo utashindwa kuleta mafanikio tarajiwa. Kamati Kuu imeona hatua ya Serikali kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii kwa Wafanyakazi wa sekta rasmi, lakini imesikitishwa na hatua ya Serikali hiyo hiyo kutochukua nafasi hii kuweka mazingira wezeshi ya kisheria kwa Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na wote walio katika Sekta isiyo rasmi kuingia kwenye Hifadhi ya Jamii.

Kamati Kuu ya ACT Wazalendo pia imeona kuwa muswada huu unaopendekezwa bungeni una matatizo makubwa ambayo yanaweza kusababisha wazee wetu 120,000 kukosa kabisa pensheni, hasa watakaoanza kustaafu mwaka huu na waliokwishastaafu tangu mwaka 1999.

Jambo hili ni la kihistoria kidogo, tutaeleza. Serikali mwaka 1999 iliunda Mfuko wa PSPF kwa ajili ya watumishi wa umma. Kabla ya mwaka 1999 Watumishi wa Umma walikuwa hawachangii pensheni zao, bali walikuwa wanalipwa pensheni kutoka Hazina moja kwa moja kupitia bajeti za Serikali za kila mwaka. Hii ndio sababu wastaafu wetu nchini wanapokea pensheni ndogo sana ya shilingi 50,000 tu kwa mwezi na kabla ya hapo shilingi 20,000 tu.

Serikali ya Awamu ya 3 iliamua kuunda Mfuko wa Pensheni ili kuboresha pensheni za watumishi wa umma. Hata hivyo, Serikali ilitakiwa kulipa michango ya wafanyakazi wote walioajiriwa kabla ya mwaka 1999 (pre 1999). Serikali ya Rais Mkapa ilikubali deni lakini haikulipa. Serikali ya Rais Kikwete ilifanya uhakiki wa Deni na kukubali kulipa lakini haikulipa. Serikali ya Rais Magufuli imeamua kutolipa kabisa kisheria. Taarifa ni kuwa Serikali imeamua kuachana na madeni haya, na hivyo wastaafu 120,000 nchini wako hatarini kutolipwa pensheni kabisa, mara tu baada ya muswada huu mpya kupita na kuwa sheria.

Vile vile muswada wa sheria hii unabadilisha kanuni ya mafao, na hivyo kuathiri Wafanyakazi wa Umma hususan Walimu wetu wote nchi nzima ambapo pensheni zao zitakatwa kwa 50%. Jambo hilo litakuwa na athari kubwa mno kwa walimu nchini.

Muswada pia umeshindwa kuwaka bayana jawabu la kujitoa kwenye mafao kupitia kinachoitwa 'Fao la Kujitoa'. Muswada umeweka mamlaka ya fao jipya la kukosa ajira kwa Waziri badala ya kuweka masharti yake wazi kisheria na hivyo kuendeleza utata wa suala zima la wafanyakazi na michango yao. Muswada pia umeendelea na kiwango cha michango cha 20% licha ya tafiti zote kuonyesha kuwa ni kiwango kikubwa mno na kinaweza kupunguzwa mpaka 12% ambapo Waajiri wachangie 7% na waajiriwa 5% ya mishahara yao kwa mwezi kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii.

Muswada pia umeshindwa kuunganisha Michango kwenye mifuko na Fao la Matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Hali ya sasa ni kwamba wafanyakazi wanalipa mara mbili, wanalipia pensheni kwenye mifuko ya pensheni, na wanalipoa NHIF kwaajili ya Bima ya Afya. Wakati Fao la Afya ni kitu kinachopaswa kuwa sehemu ya faida za mafao ya kuingia kwenye Hifadhi ya Jamii.

Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti ya Chama kuanza kazi ya kuhamasisha makundi ya vyama vya Wafanyakazi nchini kuungana na kusimama pamoja kuboresha muswada wa Sheria hii. Lengo likiwa muswada huu usiende Bungeni ili uboreshwe na kulinda maslahi ya wazee wetu wastaafu na wastaafu wajao.

Kamati Kuu imeagiza Chama kuitisha kongamano la wazi kuvileta pamoja vyama vya wafanyakazi, wafanyakazi wenyewe na wadau wengine muhimu ili kujadili sheria mpya ya pensheni na kujiunga na vyama vya wafanyakazi kuboresha muswada ili kutunga sheria inayohakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na haki ya Hifadhi ya jamii.

Muswada mwengine ni muswada wa Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa nchini, miongoni mwa miswada mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini, muswada ambao ukiachwa kama ulivyo na ukawa sheria basi utafuta siasa za vyama vingi nchini.

Maana ni muswada unaompa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini mamlaka ya Udhibiti na Uendeshaji wa Vyama na kupoka mamlaka hayo kwa Vyama vyenyewe kupitia wanachama. Hata zuio haramu la mikutano ya hadhara nchini limewekwa kisheria katika mswada huo.

Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti ya Chama kuanzisha mara moja mazungumzo na Vyama vingine vya upinzani ili kuunganisha nguvu kuupinga muswada huu unaokwenda kurudisha nchi kwenye mfumo wa Chama kimoja cha siasa.

C: Ushiriki wa Chama Kwenye Uchaguzi wa Marudio wa Januari 13, 2018

Kamati Kuu ilijadili na kutathmini kwa kina yaliyojitokeza kwenye uchaguzi wa Novemba 2017. Kwenye uchaguzi huo, ilikuwa dhahiri kuwa;

I. Chama Tawala na Serikali yake kiliongeza matumizi ya mabavu kupitia vyombo vya dola hasa jeshi la polisi ili kuweka mazingira ya kushinda uchaguzi

II. Chama Tawala kilihakikisha kinawatumia vyema watendaji wa halmashari wanaohusika na usimamizi wa uchaguzi ambao wengi waliteuliwa kwa misingi ya ukada kwa Chama hicho ili kujihakikishia ushindi.

III. Mazingira yalipoonekana dhahiri kuwaelemea, Chama Tawala walitumia njia za kimabavu Kama vile kuvamia viongozi, kuteka viongozi, au kuwaweka mahabusu viongozi na mawakala

IV. Kila mbinu ilipoonekana kugonga mwamba, kwenye maeneo kadhaa, Chama Tawala, kwa kutumia vyombo vya dola kiliamua kujitangazia ushindi kimabavu licha ya matokeo kuonesha kuwa wameshindwa

V. Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC ilionekana kutojali kabisa hitilafu zilizojitokeza na kuchukua hatua kurekebisha kabla ya kuitisha Uchaguzi Mpya.

Kutokana na vitendo hivyo, ni dhahiri kwamba uwanja wa demokrasia nchini umevurugwa sana na mchakato mzima wa uchaguzi huru na wa haki kuharibiwa kabisa. Hivyo basi, Kamati Kuu ya Chama chetu imeazimia kuwa Chama chetu KISISHIRIKI kwenye uchaguzi ujao wa marudio wa tarehe 13 Januari 2018.

Hata hivyo tunatambua kuwa kutoshiriki chaguzi tu haitoshi kwani haijibu swali la nini kinafuata baada ya kususia. Chama pia kinatambua kuwa Chama tawala kinafurahia kususiwa na kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kubinya Demokrasia ili Vyama vya upinzani viendelee kususia chaguzi zinazokuja.

Kamati Kuu imeuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, pamoja na kuweka shinikizo kubwa kwa Serikali kufanya mabadiliko muhimu ya kisheria, kiutendaji na kikatiba ili kuweka sawa uwanja wa mapambano ya Kidemokrasia.

Chama chetu kitavitembela na kuanzisha mazungumzo na Vyama vyote vya upinzani ili kuona njia bora zaidi ya kimapambano ya pamoja katika kukabiliana na vitendo vya sasa vya Chama Tawala cha kuvuruga uchaguzi huru na wa haki.

Chama pia kitautumia muda wa sasa na mwezi Januari Kama kipindi cha kushirikiana na Vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe kupambana dhidi ya Muswada wa Sheria ya Pensheni ambao utawakosesha pensheni malaki ya wafanyakazi wa sekta ya umma hasa walimu kama utapitishwa kama ulivyo. Hatua hizi pia zitahusisha makundi ya walio kwenye sekta isiyo rasmi, kama wakulima, wavuvi, wamachinga, wajasiriamali nk, ambao sheria hii inawaacha nje kabisa.

ACT Wazalendo
Disemba 17, 2017
Dar es Salaam

Tundu Lissu amjibu Job Ndugai

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amefunguka na kumjibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kauli yake ya kusema kuwa utaratibu uliotumika kumsafirisha Tundu Lissu kwenda Nairobi kuwa ulikwenda kinyume na mfumo wa serikali na kibunge.

Tundu Lissu anadai kuwa kauli hiyo haina ukweli hata kidogo kwani kitendo cha yeye kusafirishwa kwa ndege mnamo Septemba 7, 2017 majira ya usiku kuelekea kwa matibabu nchini Kenya ni wazi kuwa kibali kilitolewa na serikali pamoja na Bunge kwani bila hivyo yeye asingeweza kusafirishwa.

"Mimi sikuamua kuja Nairobi sikuwa najitambua, watu walioamua mimi kuja Nairobi ni pamoja na Spika Ndugai mwenyewe watu wameniambia kwenye hicho kikao cha nipelekwe wapi Ndugai alikuwepo, Naibu wake alikuwepo, Katibu wa Bunge wakati huo Kashilila alikuwepo, Mwenyekiti wa chama changu alikuwepo ile ndege iliondoka saa sita usiku sasa ingerukaje kama haikuruhusiwa na serikali ya Tanzania kuruka kuja Nairobi? Kwa hiyo hii habari ya kwamba amepelekwa wapi ni mambo ya kujishikiza shikiza tu ni Bunge kujaribu kukwepa wajibu wake wa kisheria" alisema Tundu Lissu

Aidhaa Tundu Lissu aliendelea kufafanua kuwa "Nimesema mimi siombi fadhila, hakuna mtu anaomba kufadhiliwa hapa mimi naomba haki ambayo anatendewa mtu aliye Mbunge anayeumwa ambaye amelazwa nje ya kituo chake cha kazi hicho tu.

Mbali na hilo Tundu Lissu amesikitishwa na upelelezi unaofanywa na jeshi la polisi kuhusu shambulio lake la kutaka kuuawa na kusema anashangaa mpaka leo jeshi la polisi halijasema linamshuku nani kuhusika na shambulio hilo na mpaka leo jeshi la polisi halijaweza kumhoji japo aweze kutoa maelezo yake.

Tundu Lissu alishambuliwa na risasi mnamo Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi kupatiwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo huko kwa matibabu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 18

Utajuaje Kama Ugonjwa Wa Kisukari Ulio Nao Ni Halali Au Haramu ?

$
0
0
Katika  uganga  na  uchawi  magonjwa  yamegawanyika   katika  makundi  makuu  mawili .

Kundi la   kwanza  ni  magonjwa  halali  na  kundi la  pili  ni  magonjwa  haramu.

Magonjwa  halali  ni  magonjwa  yanayo tokana  na  sababu  za  kisayansi  na  magonjwa  haramu  ni  magonjwa  yanayo  tokana  na  kurogwa.

Wachawi  wana uwezo  wa  kutengeneza  magonjwa  mbalimbali  na   kuwatupia  watu  walio  wakusudia.

Mtu  alietupiwa   maradhi  ya  kichawi  huonyesha  dalili  zote za  mgonjwa  wa  kawaida  mwenye  ugonjwa  huo  lakini  akienda  hospitali  ugonjwa  unakuwa   hauonekani  na  akitumia  dawa  hapati  nafuu  yoyote.

Wachawi  wanaweza  kutengeneza  ugonjwa  wowote  ule  lakini  magonjwa  ambayo  wachawi  hupenda  kuyatengeneza  ni  pamoja  na  kifafa, kiharusi, ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ugumba  kwa  wanawake, maradhi  ya  akili  ( ukichaa ), vidonda  vya  tumbo  na  maradhi  ya  kisukari  kwa  kutaja  machache…

Wachawi  wanapenda  kutengeneza  maradhi  hayo  niliyo  yataja  hapo  juu  kwa  sababu  ya  umuhimu  wake  katika  kutekeleza  mipango  yao  ya  kichawi  pamoja  na  upatikanaji  wa  malighafi  ama  vitendea  kazi  vya  kutengeneza  maradhi  hayo.

Nimesema umuhimu  wa  maradhi  hayo  katika  kutimiza mipango  ya   kichawi  kwa  sababu  wachawi  wanapo  mtupia  mtu  maradhi  au  uchawi  wowote  ule  huwa  na  kitu  au  jambo  wanalo  taka  kulitimiza.

Kwa  mfano  lengo  la  wachawi  linaweza  kuwa ni kumfanya  mtu  achanganyikiwe   akili  lakini  badala  ya  kumtumia  jinni  la  kumtia  ukichaa  moja  kwa  moja  wanaweza  kumtumia  uchawi  wa  kumfilisi  mali  na  utajiri  mtu  huyo  na  otomatik  mtu  huyo ataishia  kuchanganyikiwa.

Zipo  njia  nyingi  wanazo  tumia  wachawi  kuwatia  watu  umasikini, moja  ya  njia  hizo  ni   hii  hapa;

Wanachukua  nywele  za  sokwe  au  nyani, kucha  ya  kidole  kidogo cha  mkono wa  kushoto  cha  maiti  ya  mtu mzima,  mti  ulio chukuliwa  kutoka  kwenye  kitanda  cha  sokwe  mtu,  mzizi  ulio  okotwa  kaburini  wakati  kaburi  linachimbwa , sanda  iliyo  tumiwa  na  marehemu  au  kitambaa  kilicho  tumika  kukafinia  maiti  pamoja  na  vitu  vingine  kumi  na  moja  ambavyo  nachelea  kuvitaja  kuwaepuka  watu  wenyen roho  za  kichawi  ambao  wanaweza  kuvitumia  kuwaumiza  wenzao.

Uchawi  huu  hupikwa  kichawi  na  kisha  huenda  kuzikwa  kichawi  kwenye  nyumba   anayo  ishi  mtu  aliekusudiwa.

Basi  unaambiwa, mtu  huyo  yeye na  familia  yake  hawataishi  katika  nyumba  hiyo  kwa zaidi  ya  siku 49  wala  hawawezi  kuendelea  kuwa  na  mali  walizo  nazo  ndani  ya  siku  hizo  nilizo  zitaja.  Watafilisika  ndani  ya  siku  hizo   na  baada  ya  siku  hizo  mwenye  mali  ataanza  kuingia  katika  mchakato  wa  kuwa  mwehu/kichaa.

Turudi  kwenye  maradhi  ya  kisukari.  Watu  wengi  wanasumbuliwa  na  kuteswa  na  maradhi  hatari  ya  kisukari.

Baadhi  yao  wamefikia  hadi  hatua  ya  kukatwa  miguu  yao  kwa  sababu  ya  maradhi  ya  kisukari.

Swali  la  kujiuliza  mtu  anae  sumbuliwa  na   maradhi  ya kisukari  ni  Je UTAJUAJE  KAMA  KISUKARI  ULICHO  NACHO  NI  HALALI  AU  HARAMU ?  Ama  kwa  lugha  nyepesi  JE  UTAJUAJE  KAMA MARADHI  YA  KISUKARI  ULIYO  NAYO  NI  YA  KAWAIDA  AU  YANATOKANA  NA    KUROGWA ?

Ni vyema  kujua jambo  hilo  ili  upate  kujua  njia  sahihi  ya  namna  ya  kutibu  tatizo  lako.

JINSI  YA  KUJUA  KAMA  KISUKARI  ULICHO  NACHO  NI  HALALI  AU  HARAMU.
Ili  kujua  kama  kisukari  ulicho  nacho  ni  halali  au  haramu, fuata  maelekezo  yafuatayo.

1.   Kunywa  maji  ya  kutosha
2.   Mkojo  ukikubana  nenda  kwenye  eneo  lenye  mchanga
3.   Ukifika  kwenye  eneo  lenye  mchanga  au  udongo, kojoa  mkojo  wako.
4.   Baada ya  kukojoa  mkojo katika  eneo  hilo  tafuta  sehemu  upumzike   kwa  dakika  30  hadi  40  au  kama  unaweza  kusubiri  hapo hapo  ni sawa  tu.
5.   Baada  ya  dakika  30  au  40  rudi  katika  eneo  ulilo  kojoa  mkojo  wako..  UKIKUTA  KUNA  SISIMIZI  KATIKA  ENEO  HILO ULILO  KOJOA  BASI  JUA  MARADHI  YA  KISUKARI  ULIYO  NAYO  YANATOKANA  NA  KUROGWA  LAKINI  UKIKUTA  HAKUNA  SISIMIZI  BASI  JUA  MARADHI  YA  KISUKARI  ULIYO  NAYO NI  YA  KAWAIDA…

JINSI  WACHAWI  WANAVYO  TENGENEZA  KISUKARI  CHA  KICHAWI
Siwezi  kuelezea   kwa  uwazi  jinsi  wachawi  wanavyo  tengeneza  kisukari  cha  kichawi  kwani  kwa  kufanya  hivyo  nitakuwa  ninawafundisha  watu  ulozi .

Kidogo  ninacho weza  kukueleza  ni  kuwa, malighafi  kuu  inayo  tumika  kutengeneza  maradhi  ya  kisukari  cha  kichawi  ni  CHURA  WENYE  KUTOA  UDENDA ..  Wadudu  hao  huchanganywa  na  madawa  mengine  ya  kichawi  na uchawi  ukisha  kamilika  mtu  alie  kusudiwa  hulishwa  uchawi  huo  kupitia  kinywani  kwake.

NINI  TIBA  YA  MARADHI  YA  KISUKARI  CHA  KICHAWI… Ipo tiba  asilia  inayo  tokana  na  mimea  ya  porini.  Tiba  hii huwaponyesha  kabisa  watu  wenye  kusumbuliwa  na  maradhi  ya  kisukari  cha  kurogwa.

Vile  vile  tiba  hii  huwasaidia  pia  watu  wenye  maradhi  ya  kisukari  cha  kawaida  kwa  kurekebisha  kiwango  cha sukari  kwenye  damu..

Kwa  tiba  hii, wasiliana  na  DOKTA  MUNGWA  KABILI  kwa  SIMU  NAMBA  0744 – 000  473

Dk. Kigwangalla Afunga Mafunzo Ya 15 Ya Jeshi USU Kwa Maafisa Wanyamapori Wa Tawa, Tanapa Na Ngorongoro Mkoani Katavi

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Ametoa agizo hilo  Disemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

“Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye eneo lako la kazi, taasisi za kijamii, mamlaka za mikoa na wilaya, wananchi, halmashauri husika mshirikiane nao ili kupunguza madhara ya operesheni zetu, na zoezi hili la uhifadhi liwe endelevu,” alisema Dk. Kigwangalla.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.

Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.

Alisema katika kuelekea mfumo huo, Jeshi hilo litakuwa moja bila kubagua taasisi yeyote ambayo ipo chini ya Wizara yake. “Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 inampa Waziri mamlaka ya kuunda Jeshi Usu, haikusema jeshi la TAWA, TFS, TANAPA au NGORONGORO na kwa vile hili jeshi ni langu nataka liwe moja, na tunakimbiza mchakato huu kwa haraka ukamilike kwa mujibu wa Sheria.

“Tunafarajika Mhe. Rais ameshaunga mkono na ameshatupa maelekezo, Mwenyekiti wa Kamati ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Ulinzi naye ameshasaini, ni sisi sasa tuendelee kujipanga vizuri ndani ya wizara, tuanze kuishi kwenye mfumo huo, kuanzia kwenye sare, uratibu wa mafunzo, uongozi na mfumo wa utawala,” alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema mfumo huo wa Jeshi Usu utakuwa na mnyororo mmoja wa mamlaka (chain of comand) na kwamba utahusisha taasisi zote za uhifadhi zilizopo chini ya wizara yake kwenye sekta ya wanyamapori, misitu na mali kale. “Sijawaona watu wa misitu hapa au mambo ya kale, wote hawa ni ni muhimu, rasilimali za mali kale nazo ni muhimu sana kulindwa kwani zikiharibika hazitengenezeki tena” alisema.

Katika hatua nyingine amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa mafunzo yote ya Jeshi Usu ambayo yanaendelea katika kituo cha Mlele, Mkoani Katavi yanaratibiwa moja kwa moja na Wizara tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo uratibu unafanywa na taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Akizungumzia mafanikio ya vita dhidi ya ujangili na matunda ya mafunzo hayo alisema, “Katika siku za hivi karibuni tumepiga hatua kubwa ya kupambana na ujangili hasa wa tembo, Kwa dhati napongeza jitihada zinazofanywa na zinazoendelea kufanywa na wahifadhi, maaskari watumishi wengine na wadau wetu wote kwa ujumla ambazo zimeimarisha hali ya uhifadhi wa maliasili zetu”.

Alisema kwa kiasi kikubwa matukio ya ujangili yamepungua na kwamba nyara nyingi zinazokamatwa katika kipindi hiki ni za zamani ambazo zilikuwa zimefichwa na majangili kwa ajili ya kuzitafutia masoko au kukimbia mikono ya sheria.

Alisema Wizara yake itaendelea kutumia mbinu za kisasa za kiitelijensia za kukabiliana na ujangili ikiwemo kutumia ndege zisizo na rubani kwa ajili ya doria na kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano ambayo haitaweza kuingiliwa na majangili au watu wengine wenye nia ovu na uhifadhi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Dk. Nebo Mwina akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo hayo ya Jeshi Usu, aliwataka kuishi kwenye viapo vyao kwa kudumu katika ukakamavu, uhifadhi, maadili mema na nidhamu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Dk. James Wakibara aliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyopewa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwa kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali, kujiepusha na rushwa na kudhibiti vitendo vya ujangili.

Mhifadhi Gloria Bidebeli kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA akisoma risala ya wahitimu hao alisema mafunzo hayo yatawawezesha kuboresha ufanisi wa shughuli za uhifadhi kwa kutii amri na kutekeleza maagizo kwa wakati.


Mafunzo hayo ya wiki nne ambayo yalianza Novemba, 20 mwaka huu yalihusisha Mameneja wa Mapori ya Akiba na Tengefu 20, Wakuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili wanane, Maafisa Wanyamapori 29 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Wahifadhi Wanyamapori watano kutoka TANAPA na Wahifadhi Wanyamapori 26 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Mafunzo hayo yalihusisha matumizi sahihi ya silaha, mbinu mbalimbali za kupambana na uhalifu, huduma ya kwanza, ukakamavu, sheria mbalimbali zinazosimamia maliasili, ukamataji na upekuzi wa wahalifu na jinsi ya kuwafungulia hati za mashtaka.

Tangu kuanzishwa kwa mafunzo hayo Septemba 2015 jumla wahifadhi 1468 wakiwemo Askari wa Wanyamapori na Viongozi mbalimbali kutoka TAWA, TANAPA na NGORONGORO wameshapatiwa mafunzo hayo katika kituo hicho cha Mlele. 

Mfungwa aliyesamehewa na Rais Magufuli atupwa jela miaka 15

$
0
0
Gerald Deus (30), mkazi wa Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita aliyetoka jela kwa msamaha wa Rais, amehukumiwa tena kifungo cha miaka 15 jela.

Deus aliyehukumiwa kifungo hicho juzi na Mahakama ya Mwanzo Bukombe baada ya kukiri kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu, ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliopewa msamaha Desemba 9 na Rais John Magufuli.

Msamaha huo wa Rais ulitolewa wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara).

Deus alihukumiwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Bukombe, Damas Gakwaya baada ya kukiri kosa la kupora Sh300,000 kutoka kwa Dina Mwende, mfanyabiashara wa soda za jumla wilayani Bukombe.

Tukio hilo kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Polisi, Mohamed Simai lilitokea katika Mtaa wa Malendeja, Kata ya Katente wilayani Bukombe saa sita mchana Desemba 14, ikiwa ni siku nne tu tangu mshtakiwa huyo atoke gerezani.

Simai aliiambia Mahakama kuwa kabla ya kupora kiasi hicho cha fedha, mshtakiwa alifika dukani akijifanya anataka kununua soda za jumla kwa ajili ya vibarua aliodai walikuwa wakilima shambani kwake.

“Wakati muuza soda akiendelea kupanga kreti dukani, ghafla mshtakiwa alimvamia na kumpora Sh300,000 na kuanza kutimua mbio kabla ya kukamatwa na raia wema waliojitokeza kutoa msaada baada ya kelele za aliyeporwa fedha,” Simai aliieleza Mahakama.

Mwendesha mashtaka alisema baada ya kumkamata, wananchi walianza kumshambulia lakini aliokolewa na polisi waliofika eneo la tukio. Baada ya kusomewa mashtaka, mshtakiwa Deus alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama imhurumie kwa kumpa adhabu ndogo kwa sababu ana siku tano tu tangu alipotoka gerezani kwa msamaha wa Rais Magufuli.

Akitoa hoja baada ya mshtakiwa kukiri kosa, mwendesha mashtaka aliiomba Mahakama kumpa Deus adhabu kali kwa sababu anaonekana ni mhalifu mzoefu na hajajifunza kwa kipindi cha miezi sita aliyokaa gerezani akitumikia kifungo cha mwaka mmoja alichohukumiwa kwa kosa la wizi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama, Juni Mosi, mwaka huu, Deus alihukumiwa kifungo cha miezi 12 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la wizi wa nguo mali ya Naomi Musa, mkazi wa Mtaa wa Kapela, Kata ya Igulwa katika mji mdogo wa Ushirombo wilayani Bukombe.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mujuni Mchunguzi wa Mahakama ya Mwanzo Bukombe katika shauri la jinai namba 188/2017.

Kabla ya kutoka kwa msamaha wa Rais Desemba 9, mshtakiwa alikuwa akitumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela katika Gereza la Kahama ambako ndiko alikorejeshwa juzi.

“Kwa sababu mshtakiwa amekiri kosa; na kwa kuzingatia ametenda kosa hilo siku chache tu baada ya kutoka Magereza kwa msamaha wa Rais; naiomba Mahakama kumpa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo,” aliomba Simai.

Akitoa hukumu, Hakimu Gakwaya aliyeonyesha mshangao kwa mshtakiwa kushindwa kutumia vizuri msamaha wa Rais Magufuli, alisema Mahakama inamhukumu kifungo cha miaka 15 jela badala ya miaka 30 aliyostahili kwa mujibu wa sheria kwa sababu hakuisumbua Mahakama kwa kukiri kosa.

“Kwa sababu hujaisumbua Mahakama kwa kukiri kosa; nakupa adhabu ya onyo ya miaka 15 na kazi ngumu gerezani ili iwe fundisho kwako na kwa wengine,” alisema hakimu Gakwaya.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 285 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 16 na marekebisho yake ya mwaka 2002.

Ajali Yaua Watano na Kujeruhi 13 Mwanza

$
0
0
Watu watano wamefariki dunia na 13 wajeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Mwanza kwenda Shinyanga eneo la mtaa wa Buhongwa Nyamagana mkoa wa Mwanza baada ya gari yenye namba za usajili T.107 BKK Toyota coaster kugongana na Lori

Gari hiyo aina ya Coaster ilikuwa ikiiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Badru Habibu (33) mkazi wa Nyegezi na chanzo cha ajali hiyo kimefahamika kuwa ni mwendokasi wa dereva wa Coaster aliyekuwa akijaribu kuyapita magari ya mbele bila tahadhari na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 13.

Marehemu waliofariki katika ajali hiyo hadi sasa ametambulika jina moja tu ambaye ni 1. Abdul Mustafa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 42 hadi 45, huku marehemu wengine wa nne majina yao bado hayajafahamika. 

Aidha majeruhi wote kumi na tatu wapo hospitali ya rufaa ya Bugando wakipatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri, miili ya marehemu pia imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi, Ahmed Msangi anatoa wito kwa waendeshaji wa vyombo vya moto hususani madereva wa magari ya abiria akiwataka kuwa makini pindi wawapo barabarani huku wakijua wamebeba roho za watu, hivyo wazingatie sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepusha vifo na majeruhi ya aina kama hii yanavyoweza kuepukika.

Wasamaria Wema Wakitoa Msaada Kwa Mwendesha Bodaboda

$
0
0
Wasamaria wema wakimsaidia mwendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda yenye nambari MC307 BPG (jina halikupatikana) amabaye alidondoka chini baada  ya kugonga  kwa nyuma gari dogo aina ya Toyota RAV 4 nambari T924 BPG kwenye eneo la Kanisa Kuu Katoliki la Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Dodoma, Desemba 17, 2017. 

Wasamalilia Wema hao walimpeleka kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa matibabu. (Picha na Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls 0658316976
0755911233
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Rais Magufuli Awaonya Wamachama wa CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dk John Magufuli ameendelea kusimamia azma yake ya kumaliza rushwa ndani ya chama hicho.

Dk Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano amesema CCM haitasita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika.

Akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18,2017 Rais Magufuli amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa.

Amewataka wajumbe wa mkutano kuchagua watu waaminifu na wenye mapenzi ya dhati na CCM.

“Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema.

Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza Aprili, 2017.

“Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema.

Takukuru yatupa ushahidi wa Flashi ya Nassari, Lema

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema imeshindwa kuendelea na uchunguzi wa tuhuma za rushwa zilizowasilishwa na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) na Godbless Lema (Arusha Mjini).

Msemaji wa TAKUKURU, Musa Misalaba alieleza sababu ya kufikia uamuzi huo kuwa ni wabunge hao kuharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.

“Ni kweli flash tulikabidhiwa, lakini Nassari na mwenzake kwa sababu walivuruga uchunguzi hatuwezi kuendelea nalo. Unajua pale kilichofanyika ni kuendeleza kufanya siasa,” alisem Misalaba

Misalaba aliongeza kuwa wabunge hao waliligeuza jambo hilo kuwa la kisiasa na kufanya kuharibika kwa uchunguzi kwani hawakuwa wanawasilisha ushahidi wote kwa wakati.

“Ilionekana kama sanaa, hawakuwa na utayari wa kutuletea taarifa, walikuwa wanaleta kipande kidogo halafu kesho wanafanya kama mchezi wa Isidingo, kwa hiyo uchunguzi hauendi hivyo,” aliongeza Misalaba.

Takukuru imeeleza kuwa pamoja na kuwa na kiasi kidogo cha ushahidi, haiwezi kuendelea nao kwa sababu aliyepaswa kutoa ushahidi hakuwa tayari kushirikiana na taasisi hiyo huku akisema kuwa mmoja ya wabunge waliwasilisha ushahidi huo hakutokea pale alipotakiwa kuongeza taarifa zaidi za ushahidi.

“Ule haukuwa ushahidi, kuna mmojawapo tulimwambia aje kutoa ushahidi hakuonekana, matokeo yake wakawa wanaenda kwenye vyombo vya habari, kwa hiyo tunawaambia hatuwezi kufanya kazi kama hiyo. Sisi ni chombo huru kinachopaswa kufanya kazi bila kuingiliwa wala kushinikizwa na mtu,” alisisitiza .

Mbunge Joshua Nassari waliwasilisha ushahidi wa video ambao alidai kuwa unawaonyesha madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha waliohamia CCM wakati wa ziara ya Rais Magufuli mkoani humo kuwa walinunuliwa kwa rushwa.

Madiwani hao walieleza kuwa wamejiuzulu nafasi zao na kujivua uanachama kisha kuhamia CCM kutokana na kuvutiwa na utendaji kazi pamoja na kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mahakama Kuu yamuachia huru Sheikh Issa Ponda

$
0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchihi, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyokuwa imemuachia huru.

Mahakama chini ya Jaji, Johnson Mkasimongwa ambaye ameeleza kuwa anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro ya kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa lugha ya uchochezi.

Jaji Mkasimongwa amesema Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na yeye anakubaliana na uamuzi huo, hivyo amechukua uamuzi wa kumuachia huru.

Akitolea maelezo juu ya maamuzi hayo, Jaji Mkasimongwa amefafanua  kwa kusema kuwa upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.

Sheikh Ponda alishtakiwa kwa tuhuma za uchochezi ambapo mnamo August 10, 2013, August 10, 2013, alidaiwa kutoa kauli za kichochezi kwa waumini wa kiislam ambapo moja ya kauli zake alisema kwamba (Waislam) wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images