Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wananchi Iyumbu Wampongeza Rais Magufuli Kwa Kuwarejeshea Maeneo Yao.

$
0
0
WANANCHI wa kata ya Iyumbu katika jimbo la Dodoma mjini wamempongeza na kumshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuwarejeshea ekari 129 ambazo zilitengwa kwa ajili ya makaburi ya Viongozi wa Kitaifa.

 Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kupokea maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde wakati wa ufunguzi wa nyumba 300 za Shirika la Nyumba Taifa (NHC) katika eneo la Iyumbu.

 Wakizungumza kuhusu hatua hiyo, wananchi hao wamesema wamepokea kwa furaha kubwa sana na kwamba dhamira ya Rais ya kuwajali wanyonge imetimia.

 Mmoja wa wananchi hao, George Makapi amesema urejeshaji huo utawawezesha kuendeleza maeneo yao ambayo yalichukuliwa tangu mwaka 2006 kwa lengo la kutumiwa kuzikia viongozi hao.

 Katika maombi yake, Mavunde alimuomba Rais Magufuli kulirejesha kwa wananchi eneo hilo lililotengwa kwa ajili ya makaburi ya Viongozi wa Kitaifa kwa kuwa ni zaidi ya miaka 7 imepita bila wananchi kulipwa fidia yoyote na kushindwa kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kilimo na ufugaji kama walivyokuwa wanafanya awali.

 Kufuatia ombi hilo, Rais Magufuli ameagiza ekari zote 129 zirejeshwe kwa wananchi kwa kuwa serikali haina mpango wa kulitumia eneo hilo kwa sasa.

 Aidha Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kuwa na Mbunge mchapakazi na anayewajali wananchi wake na ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi yao.

Rais Magufuli Aahidi Kulipa Madeni Yote ya Walimu

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kulipa madeni ya walimu takribani shilingi Bil. 25 mara baada ya  viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuthibitisha uhalali wa madeni hayo.

Rais Dkt. Magufuli ametoa tamko hilo jana Mjini Dodoma ,alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa CWT ambao umehusisha wawakilishi kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara   .

“Ninawaahidi walimu wenzangu, mara baada ya zoezi la uhakiki kuisha wale walimu ambao wanadai malipo halali watalipwa,” alifafanua Rais Dkt. Magufuli.

Aliendelea kusema kuwa kabla hajawa Rais alikuwa mwalimu hivyo anazifahamu vizuri shida za walimu hivyo walimu wajisikie wana muwakilishi mzuri.

Aidha, Rais Magufuli amewataka viongozi wa CWT wa wilaya na mikoa kuhakiki madeni ya walimu ya maeneo yao na kuyawasilisha kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya kulipwa.

Rais Dkt. Magufuli amesema Serikali ya awamu ya Tano imeendelea kufanya jitihada za kuboresha maslahi ya walimu ambapo tangu imeingia madarakani jumla ya shilingi bilioni  56.92 zimetolewa kwa ajili ya kulipa madeni ya walimu ambapo kati ya fedha hizop, shilingi bilioni 14.23 ni madeni ya mishahara na shilingi  bilioni 42.69  ni madeni yasiyo ya mishahara.

Vile vile Rais Magufuli amewasihi walimu wenzake kupokea kile kidogo ambacho Serikali inakitoa wakati huu ambapo Serikali inawekeza katika kutekeleza miradi mbalimbali kama vile miradi ya afya, umeme, maji, barabara na reli. Miradi ambayo inawagusa pia walimu katika maisha yao ya kila siku nawanapotimiza majukumu yao.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewaahidi walimu hao kufanyia kazi maombi mbalimbali ambayo wamewasilisha ikiwemo kurudisha posho ya kufundishia pamoja na  Serikali kutoa mikopo isiyo na riba ili kuwasaidia kujenga nyumba za kuishi.

Hata hivyo, amewata viongozi husika kushughulikia uwiano sahihi wa walimu wa shule za msingi na sekondari walioko mijini na vijijini kutokana na walimu wengi kupangiwa mijini.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais CWT Leah Ulaya alisema kuwa wanaimani na Rais Magufuli na juhudi zake zinaonekana wazi katika  kupambana na ufisadi, uzembe, rushwa, uhujumu uchumi na vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Polisi wakerwa wizi wa mafuta ya treni Tazara

$
0
0
KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Tazara, Patrick Byatao amesema wafanyakazi wasio waaminifu wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) wanalisababishia hasara shirika hilo kutokana wizi wa mafuta katika treni.

Akizungumza katika hafla ya kuwapa zawadi wafanyakazi bora 10 wa mwaka 2017, Dar es Salaam jana, Kamanda Byatao aliyataja maeneo korofi ambayo wizi huo hufanyika kuwa ni pamoja na stesheni ya Mlimba (Kilombero), Makambako (Njombe), Kongaga (Mbarali), Mpemba (Songwe) na Tunduma.

Alisema watumishi hao hususani madereva wamekuwa wakishirikiana na wananchi kuiba mafuta na ndiyo maana shirika hilo haliendelei. Kamanda Byatao alisema kuwa Oktoba 7, mwaka huu, walifanikiwa kumkamata dereva wa treni, Kagwa Ruoga na Mathew Mkula ambao walikuwa wakiendesha treni lililobeba shaba kutoka Zambia kwenda Dar es Salaam na kwamba huku treni hilo likiwa linatembea waliingiza watu watano na kuanza kuchukua mafuta ya dizeli.

Aliwataka wananchi kutoshiriki katika matukio hayo ya uhalifu na kwamba watumishi hao watachukuliwa hatua za kisheria kwa kuhujumu uchumi. 

Aidha, aliwataka askari hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa wadadisi ili kugundua matukio mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha.

Mmoja wa askari waliopata zawadi, Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Tazara, Insepkta Halid Kingazi alisema kuwa wataendelea kupambana na uhalifu ili kuhakikisha wizi unaofanywa unaisha na shirika kubaki salama.

Kingazi alisema kuwa waendesha mashitaka wanapaswa kuwapa ushirikiano kwa kuhakikisha kesi wanazozipeleka mahakamani zinakwisha kwa wakati. 

Kikosi hicho kimetoa zawadi kwa askari wake walipo makao makuu Tazara, Kituo cha Mlimba Kilombero na Iyunga Mbeya ambapo treni hiyo inapita.

Polepole Kawavaa Tena Wapinzani...."Muulizeni Mwenyekiti Wenu Alikopeleka Pesa"

$
0
0
Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Humphrey Polepole amevipiga kijembe vyama vya upinzani akimtaka mwenyekiti wa moja ya vyama hivyo kusema hela ziko wapi.

Kupitia ukurasa wake wa “Twitter” Polepole amendika maneno hayo bila kufafanua ni mwenyekiti wa chama gani na hela za nini japo wafuasi wake wengi katika mtandao huo wamechangia mawazo wakitaja huenda ni hela za ruzuku.

Mbali na hilo Polepole pia amesema kuwa kile alichowahi kukitabiri kuwa upinzani hawataweza kushindana na chama chake siku za baadaye kimeanza kutimia.

Hii inatafsiriwa kama majibu kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freman Mbowe ambaye hivi karibuni alitangaza chama chake hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge endapo Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) haitazifanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwezi Novemba mwaka huu.

“Nalipata kuwaambia wataweka mpira kwapani, wakasubiri siku kadhaa na hatimaye imekuwa. Kwa lugha ya shule ya msingi miaka ile ningesema "wameogopa kuputa", wangeputa waone namna ambavyo kwetu siasa za masuala zinalipa. Ushauri wangu: "Mwenyekiti" lazima aseme hela ziko wapi”, ameandika Polepole.

Godbless Lema Afichua Wanachohongwa Wabunge wa CHADEMA Ili Wahamie CCM

$
0
0

Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amefunguka na kusema ahadi ambazo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakipewa jambo linalopelekea kujiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lema amesema hayo jana Disemba 14, 2017 mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na uanachama wa CHADEMA kuanzia jana  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Nitakupa mshahara wako wote kwa miaka iliyobaki, pia nitakulipia madeni yako yote, nitakupa kiinua mgongo chako chote nitakupa na mlinzi kwa kipindi hiki na ukitaka tena kugombea nitakupa kipaumbele wewe au kazi nyingine utakayotaka? Je, utakuwa tayari? Si utakuwa tiyari wajameni?" aliandika Lema kwenye mtandao wake wa Twitter

Baadhi ya vyama vya upinzani nchini vimekuwa vikikumbana na changamoto ya baadhi ya viongozi wao au wananchama kujivua uanachama na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai wanaunga mkono juhudi na utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli.

Mbunge Mwingine CHADEMA Huenda akatangaza Maamuzi Magumu Leo

$
0
0
Mbunge wa Chadema, Upendo Peneza amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya mbunge huyo kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kueleza atakachozungumza na wengi wameanza kutabiri huenda na yeye akatangaza maamuzi magumu ya kukihama chama hicho.

Peneza mbunge kutoka Mkoa wa Geita ameitisha mkutano huo kipindi ambacho kumekuwa na vuguvugu la wabunge kukikimbia chama hicho na kujiunga na CCM.

Mkutano huo umeitisha ikiwa ni siku moja kupita tangu mbunge wa Siha wa Chadema, Dk Godwin Mollel alipotangaza kuhamia CCM akiunga jitihada za Rais John Magufuli.

Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kumtandika Risasi ya Kichwa Askari Mwenzake

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa Jeshi la Magereza, Faustine Masanja, kwa tuhuma za kumwua kwa kumpiga risasi askari mwenzake, wakiwa kazini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea jana  asubuhi katika eneo la Magereza, Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Mkumbo alimtaja marehemu kuwa  ni Ombeni Mwakiyani.

Alisema  siku ya tukio wakiwa kazini, Faustine alidaiwa kumjeruhi askari mwenzake ambaye alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

“Tukio limetokea   asubuhi…Faustine alimjeruhi mwenzake wakiwa kazini na baada ya kumjeruhi alipelekwa hospitalini kupata tiba ila alifariki dunia.

“Tunachunguza   kubaini nini hasa chanzo cha kumjeruhi mwenzake na kumsababishia kifo,” alisema Kamanda.

Mmoja wa askari magereza aliyeshuhudia tukio hilo, alidai  Masanja na Mwakiyani wameoa katika familia moja na inadaiwa kulikuwa na ugomvi wa familia kati yao.

Chanzo hicho kilidai   asubuhi wakiwa kazini, Faustine alimpiga mwenzake risasi ya nyuma ya kichwa ambayo ilitokea usoni.

“Wameoa familia moja na wote wanakaa kambini na Faustine aligombana na mke wake ambaye ameondoka nyumbani hivyo akawa anamtuhumu marehemu kupitia mke wake kuwa walimjaza mkewe maneno na kusababisha aondoke nyumbani.

“Baada ya kumpiga mwenzake risasi alitupa silaha yake chini na kusema akamatwe wala hakimbii kwa sababu  anajua ameua. Ila ugomvi wenyewe hatujajua ulikuwa ni nini hasa,” kilisema chanzo

Breaking News : Mbunge Mwingine wa CHADEMA anazungumza na waandishi wa habari Muda huu ... kulikoni?

$
0
0
Mbunge wa Chadema, Upendo Peneza yupo kuongea na waandishi wa habari muda huu. kulikoni? Msikilize hapo chini

Makamu wa Rais ahamia Dodoma rasmi

$
0
0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu leo Ijumaa Desemba 15 amehamia rasmi makao makuu ya nchi  ikiwa ni mwendelezo wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo

"Nilikuwa hapa kwa muda mrefu kidogo lakini nilipangiwa kuhamia rasmi leo Desemba 15 na nimefurahi kwamba nitafanya kazi mahala pangu pa kazi pa kudumu," amesema Samia.

Amesema kauli mbiu yake kwa wakazi wa Dodoma ni kuufanya mji huo kuwa wa kijani hivyo Desemba 21 ataendesha mpango wa kupanda miti katika wilaya zote.

"Kwa kuwa nasimamia pia masuala ya mazingira nitaendesha zoezi hilo ili kurudisha hali ya Dodoma," ameongeza.

Yaliyojiri Wakati Wa Mkutano Wa Msemaji Mkuu Wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Na Waandishi Wa Habari Dodoma Leo

$
0
0
*YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI NA WAANDISHI WA HABARI DODOMA LEO*

Nawashukuru wanahabari wote kwa kushiriki vyema katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru;

Napenda kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma.Idara imeshahamia Dodoma na huduma zote zinatolewa hapa;

Nawakumbusha press card zinamalizika muda wake Disemba 2017 hivyo wanahabari wanapaswa kuanzia Januari kuwahi kupata vitambulisho vipya kwa haraka kwani baada ya muda hakuna mwandishi ataruhusiwa kushiriki matukio makubwa bila press card.

Nizungumzie pia taarifa ya IMF ambayo wataalamu wake wamekamilisha kazi hapa nchini juzi kama ambavyo pia wamekamilisha tathmini kama hizo Afrika na kwingineko;

Ripoti yao ni nzuri na imebainisha mambo mazuri ambayo nchi imepiga hatua na changamoto ambazo tunaendelea kuzifanyiakazi;

Lakini kama kawaida kuna wanasiasa "vyuma vimekaza"-hawana ajenda bali kutafuta matukio na mwanya wa pa kusemea ili kuropokaropoka;

Sasa ngoja niwape mambo ya hakika kuhusu walichosema wataalamu hao. Ripoti yao imeonesha uchumi wa Tanzania upo imara, unakuwa kwa asilimia 6.8 kwa maana ya kuelekea nusu ya mwaka huu na mfumuko wa bei upo chini ya asilimia 5 tofauti na nchi nyingine zilizofanyiwa tathmini.

Katika nchi ambazo zimefanyiwa tathimini kuanzia Novemba hadi Desemba mwaka huu Tanzania ipo juu kwa maana ya ukuaji kuna nchi moja ya Afrika wataalam hao wameeleza uchumi wake unakua kwa asiliamia 1.1 na huenda mwakani ukawa -1.

Taarifa ya IMF imeonesha nchi yetu imepata daraja ya juu kwamba imetekeleza vyema ushauri wa kitaalam iloyopewa maana mradi huu haukuwa wa fedha bali ushauri wa kitaalam;

Sisi kama nchi tumeridhishwa na maoni ya wataalam wa IMF na kwenye changamoto tutaendelea kuzifanyia kazi.

Niwapongeze wakulima kwani taarifa inaonesha mavuno mazuri ya mazao katika mwanzo wa mwaka huu yamesaidia sana upatikanaji wa chakula cha kutosha na hivyo kushusha bei za chakula.Tuendelee na kazi kubww mashambani na viwandani;

Taarifa za IFM zinaonesha mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 Novemba mwaka huu ikiwa ni chini ya lengo ambalo IFM ilidhani mfumuko ungekuwa asilimia 5 na zaidi.

Benki nyingi za Tanzania bado zina mitaji ya kutosha wameeleza wataalam hao na masuala ya changamoto za kushuka mikopo yanashughulikiwa lakini watanzania ni vyema wakajifunza kukopa na kulipa;

#Zoezi la kuhuisha takwimu za kiuchumi (Debasing) ni la kawaida chini ya mifumo ya upimaji uchumi duniani kwa lengo la kuongeza shughuli mpya za kiuchumi tofauti na anavyopotosha mwanasiasa mmoja ambaye ni dhahiri "vyuma vimekaza" hana tena ajenda anarukiarukia matukio na kuokoteza vitakwimu;

Zoezi hili la kuhuisha takwimu linaendelea katila nchi zote za EAC na Tanzaniq hii ni marq ya 5 kufanyika na matokeo yatatangazwa mwishoni mwa Disemba hii ili kuingiza mchango wa shughuli mpya za kiuchumi kama gesi, viwanda vipya n.k;

IMF wamesifu pia makusanyo yetu kutokana na utekelezaji wa sera.Ndio maana makusanyo ya Serikali yameongezeka kutoka tril. 9.9 mwaka 2015 hadi Tril 14 mwaka 2017 kwa wastani wa mwaka;

Wametusifu pia kuwa Serikali yetu inajitahidi kulipa madeni na kama mlivyosikia juzi Rais amesema katika miaka miwili hii ameshalipa madeni ya zaidi ya TZS bilioni 900 na nyingine uhakiki unaendelea na atalipa fedha hizo zipo hakuna shida;

Tufike hatua kama watanzania katika kujenga nchi yetu kwenye kufikia Tanzania tunayoitaka, tujue sio kila kitu ni siasa kuna mambo ni uchumi wa nchi na kuna mambo ni maendeleo hayapaswi kufanyiwa tashtiti;

Katika tathmini hizi ambazo pia zimefanyika nchi mbalimbali ipo nchi moja kubwa tu ya Ulaya imeelezwa kuwa na changamoto nyingi za kiuchumi katika tathmini ya uoande wa nchi zilizokopeshwa fedha.

Sisi tupo vizuri na tunafanyiakazi changamoto zilizoainishwa kama vile mikopo chechefu na kuendelea kukusanya kodi na kuboresha sekta binafsi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*

Silinde Akanusha Tetesi za Kuhamia CCM

$
0
0
Mbunge wa Momba kwa tiketi ya CHADEMA , Silinde Ernest David amefunguka juu ya tetesi kuwa kesho na yeye ataongea na waandishi wa habari na kutangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema huo ni uzushi na hawezi kufanya hivyo.

Silinde ametumia mtandao wake wa Facebook kukanusha taarifa hiyo na kusema kuwa hawezi kufanya usaliti huo kwani anatambua kuwa Ubunge wake huo aliupigania kwa gharama kubwa kwani wapo watu walipoteza maisha, wengine walifungwa huku wengine ndoa zao zikivunjika ili yeye aweze kushinda nafasi ya Ubunge.

Aidha Silinde ametoa ahadi kuwa endapo likitokea jambo hilo basi wananchi waende kuchoma moto nyumba yake na mali zake zote ambazo wanazifahamu kama kuonyesha msisitiza kuwa hawezi kufanya jambo hilo.

"Uzushi unaosambazwa juu yangu katika mtandao wa jamiiforums kuwa nitafanya press kesho ni uongo uliopindukia. Nasema hili likitokea njoo mchome moto nyumba yangu na mali zangu zote mnazozifahamu. Nafasi ya ubunge wa Momba niliutafuta kwa gharama kubwa sana na kuna watu walikufa, wengine walifilisika, wengine wako jela mpaka leo kwa ajili yangu, ndoa zilivunjika n.k siwezi kusaliti kwa maslahi yangu binafsi ya ahadi ya cheo, pesa ama kitu kingine" alisema Silinde

Mbali na hilo Silinde amedai kuwa thamani ya Ubunge haiwezi kushushwa kama vocha ya simu kuwa ikiisha unaweza kukwangua nyingine na kuweka tena

Spika wa Bunge Aahidi Kwenda Nairobi Kumtembelea Tundu Lissu

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe.  Job Ndugai amefunguka na kusema atakwenda jijini Nairobi nchini Kenya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anafanyiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017.

Job Ndugai amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma nyumbani kwake na kusema kuwa watakwenda kumuona Tundu Lissu kwani ni mbunge wao na wao wanampenda sana na kudai kuwa kipindi cha nyuma alishindwa kwenda Kenya kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa kwenye uchaguzi na haikuwa na utulivu wa kisiasa ila kwa kuwa saizi imetulia anatarajia kwenda baada ya Christmas kumjulia hali.

"Mimi kama Spika siwezi kwenda na kutoka navyotaka Kenya bali napokwenda kule lazima kuwe na taarifa rasmi za kiserikali na kibunge na ninapokelewa hivyo na ninapopelekwa huko hospitali au wapi napelekwa kwa utaratibu huo ndiyo utaratibu wa nchi kwa nchi. Haiwezekani wao wana mechi kama zile (Uchaguzi) halafu spika nazunguka zunguka Nairobi wanaweza kusema ajenda aliyokuja nayo huyu siyo hii, katika pande hizi mbili Watanzania wamemtuma huyu ana ajenda nyingine kwa hiyo unapokuwa kiongozi lazima ujiongeze" alisema Spika Ndugai

Ndugai aliendelea kueleza kuwa "Haukuwa wakati mzuri kwenda Nairobi, ila kwa kuwa haya mambo yamepita na serikali saizi imekaa sawa sawa basi tusubiri Christmas ipite baada ya hapo mtamuona Spika muda si mrefu akienda kumuona Mbunge wake Nairobi au mahali pengine popote pale, yule ni Mbunge wetu na tunampenda sana na tusingependa asikitike kwa lolote lile" alimalizia Ndugai

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo huko anaendelea na matibabu.

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Dar aachiwa kwa dhamana

$
0
0
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefanikiwa kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ni baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

Katika mashtaka hayo mawili ni ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaominika, kila mdhamini akisaini bondi ya Sh 12 milioni.

Pia washtakiwa hao watoe fedha taslimu Sh 12 milioni ama mali isiyo hamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Wanawake waliovishana pete waachiwa kwa dhamana

$
0
0
Washtakiwa wanne katika shauri la kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa la kimtandao wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma leo Desemba 15, baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi, Mashaka Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka ni dhaifu mbele ya macho ya sheria.

Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote kuwa wanawake.

Wengine ni Aneth Mkuki anadaiwa kufanikisha sherehe wawili hao kuvishana pete na Richard Fabian anayeshtakiwa kwa kosa la mtandao kwa kusambaza video za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii.

Katika uamuzi wake, Hakimu Chuma amesema Mahakama haiwezi kufanyia kazi maelezo na vitu vya mashaka na uvumi kuwa washtakiwa wanaweza kudhuriwa na jamii iliyochukizwa na kitendo wanachoshtakiwa nacho.

“Ni uamuzi wa Mahakama kuwa dhamana ni haki ya washtakiwa na upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha hoja za msingi kwa nini wanyimwe dhamana zaidi ya kutoa hoja za hisia kuwa wakiachiwa watadhuriwa na jamii bila kueleza watadhurikaje na nani haswa atawadhuru,” amesema Hakimu Chuma katika uamuzi wake

Washtakiwa wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho na barua ya utambulisho kutoka mamlaka inayotambulika kisheria pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh6 milioni. Shauri limeahirishwa hadi Januari 8, mwakani.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 16


Taarifa ya Bunge kuhusu kujiuzulu kwa wabunge wawili

Kamati kuu ya CCM yatangaza majina ya wagombea ubunge wa majimbo yaliyo wazi

Hoja ya Miaka 7 ya Urais Yaibukia Zanzibar......Balozi Seif Idd asema ni Hoja Nzuri

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema ushauri wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka kuongezwa muda wa urais kutoka miaka mitano mpaka miaka saba ni suala zuri na linazungumzika bila matatizo.

Balozi Idd aliyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa nane wa Baraza la Tisa la Wawakilishi lililochukua muda wa wiki moja mjini hapa.

Awali baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 1984 na kuweka sheria ya mwaka 2017, walisema kuwa ili Zanzibar iepukane na matumizi hasa kipindi cha uchaguzi hakuna budi kuongezwa kwa muda wa utumishi wa urais.

Mmoja wa wawakilishi hao wa Jimbo la Shaurimoyo, Hamza Hassan Juma amesema kuwa ili kumpa Rais wakati mzuri wa kutumikia wananchi ipasavyo hakuna budi muda wake kuongezwa zaidi ili lengo la kufikisha maendeleo kwa wananchi liweze kufanikiwa.

Alisema kwa kuwa muda wa miaka mitano ya uongozi wa rais madarakani linaonekana kupoteza fedha nyingi za wananchi kwa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, ni vyema uongozi ukaliona hilo na kulifanyia kazi.

Alisema kwa mujibu wa tathmini yake ya uchaguzi mkuu mara nyingi hutumia fedha nyingi za walipakodi kiwango ambacho kinaweza hata kujenga zaidi ya shule kubwa 20 ambazo zingeisaidia jamii kuondokana na uhaba wa shule.

Alisema kuwa pamoja na katiba zote mbili ya Tanzania Bara na Zanzibar kuweka muda huo wa miaka mitano, bado kuna nafasi kubwa kwa Zanzibar kufanya marekebisho ya katiba yao ili kuongeza muda, akidai kuwa ni jambo ambalo haliwezi kuathiri hata kidogo Katiba ya Tanzania.

Juma alisema ikiamuliwa kufanyika hivyo ni wazi kuwa faida kubwa inaweza kupatikana ikiwamo Rais kupata muda mwingi wa kutumikia jamii badala ya muda wa sasa wa miaka mitatu tu ya kutumia jamii huku miaka miwili iliyosalia akishughulikia masuala ya uchaguzi.

Balozi Iddi akitolea ufafanuzi suala hilo alisema kwa kuwa jambo hilo linahusiana na pande mbili za Muungano ni vema kwa wakati huu suala hilo likaachiwa kwa viongozi husika kwa kulifanyia kazi na ikionekana linafaa ni wazi linaweza kupunguza gharama kubwa hasa kwa upande wa chaguzi za viongozi wakuu.

“Hili itakuwa si suala jipya kwetu kwani hata ndugu zetu wa Rwanda nao wameongeza muda wa uongozi, hivyo nasi tukibadili miaka badala ya mitano tukaweka saba tunaweza kufanikiwa kimaendeleo kwa hatua kubwa,” amesema Balozi Idd.

Alisema hali hiyo pia inaweza kuleta mafanikio makubwa katika chaguzi zijazo kufanyika kwa ufanisi mkubwa hasa baada ya marekebisho ya sheria ya uchaguzi yaliyofanyika.

Alisema Serikali ipo tayari na itaendelea kila mara kuwa hivyo kwa kupokea michango mbalimbali ya wawakilishi ambayo inaonekana inafaa kwa ajili ya kujenga maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Balozi Iddi akifunga mkutano huo alisema kuwa Serikali imedhamiria kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wake ili kuona nao wanaishi katika hali ya matumiani.

Alisema kuwa miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na Serikali tayari wameanza kununua meli moja ya mafuta, huku harakati za ununuzi wa meli kwa ajili ya abiria zikiendelea kutoa matumaini.

“Meli hizi kwa ufupi zinaweza kusaidia harakati za wananchi wetu hasa kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao utasaidia katika upatikanaji wa huduma mbalimbali,” alisema Balozi Idd.

Hatua nyingine zinazochukuliwa ni kuwa Serikali inaendelea katika ufanikishaji wa mradi wa maji safi na salama, mradi ambao unadhaminiwa na Benki ya Maendeleo Afrka kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar ambao unataraji kutumia dola za Marekani 25,673.

Msigwa Aomba Nyumba yake Ichomwe Moto Kama Atahamia CCM

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM.

Msigwa amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni kuuza hadi utu wa wapiga kura.

Msigwa ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.

"Nikihamia CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu  na magari yangu. Sikuingia bungeni kwa sababu nataka hela ila nimeingia kwa sabu kuna hoja kuna agenda na kozi kama chama tunapigania.  Mkome kabisa kunipigia simu mimi sina bei itakayonihamisha CHADEMA," amefunguka Msigwa

Akizungumzia kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani" I am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka wazi

Aidha Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni na kuongeza kwamba  alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na mbunge.

"Sikuingia Bungeni kwa ajili ya pesa, sipo tayari kurubuniwa kwa maneno matamu wala fedha au ushawishi kuuza utu ambao wananchi wa manispaa ya Iringa wamenipa. Ukiniangalia kwani nashindwa kuwa CEO, naweza kuwa Mkurugenzi wa kampuni yoyote. Mimi nilikuwa na maisha kabla ya kuingia hta bungeni.  Sisi bado tupo imara....wacha hivi vivulana viondoke sisi ambao tunajua nini tunakutaka bado tupo imara ndani ya chama" Msigwa.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Asimamishwa Kazi

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amemsimamisha  kazi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba  NHC Bw. Nehemia Mchechu kupisha uchunguzi.

Katika taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa wizara ya ardhi Doroth Mwanyika imebainisha kumsimamisha Mchechu  kwa mamlaka aliyopewa waziri Lukuvi kupitia kifungu f. 35 cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2009.

Waziri Lukuvi pia  ametoa agizo kwa bodi ya Shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa huduma za mikoa na Utawala Raymond Mndolwa ili kupisha uchunguizi wa tuhuma zinazowakabili watendaji hao.
 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images