Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ufafanuzi Kuhusu Lulu Kusamehewa na Rais Magufuli

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema katika msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya uhuru Desemba 9, 2017 haukumuhusu msaani wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Jenerali Malewa amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumuhusisha Elizabeth Michael kutokana na yeye kuingia gerezani wakati tayari mchakato wa kuangalia wafungwa wa kusamehewa na kupunguziwa vifungo ulikuwa umeshaisha

"Msamaha huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi hili lilikuwa limekamilika, kwahiyo labda misamaha ijayo kama itakuwepo lakini katika hii haikumuhusu",amesema Kamishna Malewa.

Kamishna Malewa pia ameeleza  kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza  kumfanya mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa kama endapo mfungwa atafata taratibu na kuonekana amerekebishika anaweza kupata msamaha na mengine mengi.

Desemba 9 mwaka huu siku ya uhuru kwa mujibu ya ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa  wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na wengine kupunguziwa vifungo vyao.

Takukuru Singida yamtia mbaroni Gulamali ( Aliyeshinda kura za Maoni CCM Jimbo la Nyalandu )

$
0
0
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Singida inamshikilia mshindi wa kwanza kura za maoni CCM jimbo la Singida kaskazini, Haider Hussein Ghulamali (46), kwa tuhuma ya kutoa rushwa ya shilingi milioni mbili taslimu kwa afisa usalama wa taifa (jina tunalo).

Lengo la Ghulamali  mfanyabiashara na mmiliki wa kiwanda cha magodoro  mjini Dodoma,ni kwamba afisa usalama huyo amtolee taarifa nzuri Kwenye vikao vya  ngazi za juu, ili aweze kuthibitishwa na vikao hivyo, kuwa mgombea ubunge jimbo la Singida kaskazini.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Joshua Msuya, alisema Ghulamali amekamatwa Desemba 12 mwaka huu saa 8.30 mchana, maeneo ya Rafiki resort wakati akikabidhi rushwa hiyo iliyokuwa imehifadhiwa kwenye bahasha.

 Msuya alisema desemba 11 mwaka huu,ofisi yake ilipata taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa mmoja wa wana CCM anayewania ubunge jimbo la Singida, ambaye ni Ghulamali.

“Baada ya kupokea taarifa hiyo uchunguzi ulianza ikiwa ni pamoja na kuchunguza vitendo rushwa alivyofanya  mtuhumiwa huyo, kabla na baada ya kura za maoni kupigwa desemba 10 mwaka huu huko kijiji cha Ilongero.Kura hizo zilimpitisha Ghulamali aliyepata kura 606 kati ya kura 1009 zilizopigwa,” alisema.

 Mkuu huyo, alisema baada ya zoezi hilo kupita la kura za maoni,mtuhumiwa kwa juhudi zake aliweza kupata namba za simu za afisa wa usalama wa taifa ambaye walikuwa hawafahamiani.

“Baada kupata namba ya simu ya afisa usalama taifa, Ghulamali aliweza kumpigia na akatoa maombi yake ya kusafishiwa taarifa kwenye vikao vya juu.Baada ya maombi hayo,aliweza  kutoa rushwa ya shilingi milioni mbili,na kumkabidhi afisa huyo. Ndipo alipokamatwa na TAKUKURU waliokuwa wameweka mtengo,” alisema Msuya.

Alisema uchunguzi zaidi bado unaendelea kuhusiana na mtuhumiwa Ghulamali  kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wa kura za maoni.

Mkuu huyo wa TAKUKURU,ametoa rai kwa wanachama wa vyama vyote vya siasa,wagombea na wananchi kwa ujumla, kuzingatia sheria za uchaguzi ndani ya vyama vyao.Pia kujiepusha na vitendo vya rushwa nyakati za uchaguzi ndani vyama.

“TAKUKURU itamkamata mgombea,mpambe na mwanachama yeyote atakayejihusisha na vitendo ya kuomba na kupokea rushwa,na ikipata ushahidi wa kutosha,itamfikisha mhusika mahakamani,” alisema Msuya.

Uamuzi wa dhamana ya Wanawake waliovishana pete Kutolewa Ijumaa

$
0
0
Hatima ya dhamana ya washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya kujihusisha na vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa ya mtandao itajulikana Ijumaa Desemba 15,2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza itakapotoa uamuzi.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma anayesikiliza shauri hilo aliliahirisha baada ya kusikiliza hoja kuhusu hati ya kiapo iliyowasilishwa na Jamhuri kuzuia dhamana.

Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza, mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote kuwa wanawake.

Wengine ni Aneth Mkuki anayedaiwa kufanikisha sherehe ya wawili hao kuvishana pete na Richard Fabian, anayeshtakiwa kwa kosa la mtandao kwa kusambaza video za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii.

Akiwasilisha hati iliyosainiwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa (RCO) wa Mwanza, John Ndibalema, Wakili wa Serikali Emmanuel Luvinga aliiomba Mahakama kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa sababu wakiwa nje wanaweza kuingilia upelelezi wa kesi ambao haujakamilika.

Luvinga alidai jana  kitendo walichokifanya washtakiwa ni kinyume cha maadili, jambo linaloweza kusababisha wadhuriwe na jamii iliyoangalia video ya wao kuvishana pete kupitia mitandao ya kijamii.

“Ni rai ya upande wa Jamhuri kuwa washtakiwa waendelee kushikiliwa mahabusu kwa usalama wao,” alisema wakili Luvinga.

Mawakili wa utetezi Mashaka Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole waliwasilisha hati kinzani kupinga hoja hizo wakisema licha ya dhamana kuwa haki ya washtakiwa na shauri linalowakabili kuwa na dhamana, msingi wa hoja za zuio ni hisia.

Upande wa utetezi ulisema jukumu la upelelezi na ulinzi wa washtakiwa ni la upande wa Jamhuri, hivyo hoja hiyo isitumike kuwanyima haki washtakiwa.

“Hoja zilizomo kwenye hati ya kiapo kuzuia dhamana ya washtakiwa zimejengwa kihisia kwa sababu haionyeshi namna gani washtakiwa watadhurika wala idadi ya walioona video wanaodaiwa kuchukizwa,” alisema wakili Tuguta.

Majonzi na Vilio Vyatawala Wakati wa Kuaga Miili ya askari 14 wa JWTZ

$
0
0
Serikali imetaka Umoja wa Mataifa (UN) kufanya uchunguzi wa kina na kwa haraka kubaini waliohusika katika shambulizi kwa askari wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari 14 waliofariki katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka baada ya uchunguzi huo hatua zichukuliwe ili kutenda haki.

Miili ya askari hao imeagwa leo Alhamisi, Desemba 14,2017 katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya Tanzania inataka Umoja wa Mataifa ufanye uchunguzi wa kina, ulio wazi na wa ukweli kwa damu hizi za Watanzania zilizomwagika ili tujue na haki iweze kutendeka. Ni matumaini yetu kuwa Umoja wa Mataifa watafanya hivyo kwa haraka,” amesema.

Majaliwa ameishukuru Serikali ya DRC na UN kwa ushirikiano baada ya kutokea shambulizi hilo. Amewataka Watanzania waungane kuwaombea mashujaa hao na kuenzi mchango wao kwa Taifa.

Amesema Tanzania imekuwa ikishiriki ulinzi wa amani sehemu nyingi kama vile Lebanon, Darfur na DRC na maeneo yote wanapokuwepo askari wa Tanzania wanasifiwa kwa ufanisi wa kazi.

“Msiba huu ni wa Taifa lote na watu wote wenye kupenda amani, daima tutawakumbuka mashujaa wetu na kuendelea kuenzi na kujivunia kazi zao na mchango wao mkubwa kwa nchi yetu na duniani kwa jumla,” amesema.

Waziri Mkuu Majaliwa ameliambia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwamba, yaliyotokea DRC yasiwakatishe tamaa katika kutimiza wajibu wao nchini humo na kwingineko ambako wanatekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani.

Awali, akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo alisema askari hao waliuawa kwenye mapigano yaliyodumu kwa saa 13.

Amesema majeruhi wa shambulio hilo linalodaiwa kufanya na waasi wa ADF wanaendelea vizuri na wanapatiwa matibabu katika hospitali zilizopo Goma, Kinshasa na wengine wamepelekwa Uganda.

Shughuli ya kuaga miili ya mashujaa hao imehudhuriwa na viongozi kadhaa wakiwemo, Rais mstaafu Jakaya Kikwete na mkewe Salma; wakuu wa majeshi wastaafu Robert Mboma, Mirisho Sarakikya na Davis Mwamunyange; Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda; mawaziri, wabunge na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa.

Miili ya askari hao ilirejeshwa nchini kwa ndege ya Umoja wa Mataifa Desemba 11,2017.

Jumapili Desemba 10, 2017 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema askari hao walivamiwa kambini na waasi wa ADF na mapigano yalidumu kwa takriban saa 13. Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44 walijeruhiwa na wengine wawili  hawajulikani walipo.

Taarifa iliyotolewa baadaye na jeshi ilisema askari mmoja amepatikana.

Mwakibolwa alisema tukio hilo lililotokea Desemba 7,2017 katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu nchini DRC.

==>Tazama Live hapo chini

Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Kutembelewa na Mwenyekiti Mpya wa BAVICHA

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki ambaye sasa Kenya akiendelea na matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017 amefunguka juu ya viongozi ambao wanasaliti CHADEMA na kusema jambo hilo lisiwatishe bali wao waendelee na kazi yao.

Tundu Lissu aliyasema hayo jana alipoonana Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Patrick Ole Sosopi ambaye alimtembelea Mhe Lissu hospitali jijini Nairobi jana kumjulia hali

"Ndugu zangu Mhe Lissu ameweza kunieleza mambo mengi sana na binafsi naamini ameniagiza kwa niaba ya Baraza la Vijana na tutayetekeleza kwa maslahi mapana ya nchi na chama chetu, hajasita kuniambia kwamba hali ya siasa yetu ndani ya nchi yetu kwa biashara inayoendelea kununua Viongozi uchwara na wenye tamaa wa chama chetu, amesema tusipate hofu CHADEMA hatujaanza kusalitiwa leo na hao wanaondoka, sio ajabu hata kidogo kwani mbona Yesu aliwahi kusalitiwa tena na mwanafunzi wake na hakuacha kazi yake" aliandika Ole Sosopi

Aidha Sosopi aliendelea kusema kuwa Tundu Lissu amemweleza kuwa hata watu ambao waliwahi kuisaliti CHADEMA kipindi cha nyuma hawajapata mafanikio yoyote katika maisha yao

"Wanaotusaliti hawajawahi kuwa na mafanikio katika maisha yao, tusikate tamaa mapambano yaendelee. Mwisho kabisa Mhe. Lissu ametuma salamu nyingi kwa Watanzania wote wanaoendelea Kumchangia na Kumuombea, ameendelea kuwasihi waendelee kumchangia na kumuombea, maana Bunge na serikali wamekataa kabisa kumtibia ili hali kwa mujibu wa sheria ni haki yake" alisema Ole Sosopi

Kauli ya Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro baada ya Mbunge Mwingine wa CHADEMA Kujiuzulu na Kuhamia CCM

$
0
0
Barua na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza mbunge wa Siha (Chadema) mkoani Kilimanjaro, Dk Godwin Mollel amejiuzulu ubunge imezua mjadala.

Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema leo Alhamisi Desemba 14,2017 amesema naye ameona video na barua kwenye mitandao ya kijamii lakini hawana uthibitisho wowote.

"Mheshimiwa Mollel hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kuwa yuko kwenye hilo wimbi na mimi nimeona hiyo barua na video kwenye mitandao. Bado kwangu nachukulia kama uvumi mpaka tutakapothibitisha," amesema.

Lema amesema kwa utaratibu alipaswa kumuandikia barua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe au viongozi wa Chadema.

Amesema akiwa katibu wa mkoa wa chama hicho hajapokea barua yoyote kutoka kwa Dk Mollel.

"Ukiangalia hata barua inayosambaa haijasainiwa na video inaonyesha ni mtu tu kajirekodi akarusha. Katika mazingira hayo hatuwezi kukurupuka kuzungumzia hilo jambo," amesema.

Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ambayo haina saini inaonyesha kuandikwa na Dk Mollel akieleza ameamua kujivua uanachama wa Chadema kuanzia leo Alhamisi Desemba 14,2017.

Pia, ametangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge na kwamba huo ni uamuzi wake alioufanya akiwa na akili timamu na hajashinikizwa na mtu yeyote.

Rais Magufuli atishia kuifuta Benki ya Walimu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mwelekeo wa benki ya Walimu hauridhishi na inawezekana ikafutwa na kufilisika kabisa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)  na kuongeza kuwa kati ya benki 58 zilizopo nchini, benki ya wlimu ni miongoni mwa ambazo zina muelekeo wa kufutwa.

“Nilialikwa kwenda kufungua benki ya walimu sijaenda kufungua. Nilitamani kwenda kuifungua lakini nilipopewa ripoti na BoT nilisikitika. Tuna benki sasa hivi katika nchi hii benki 58, lakini benki ambazo zina mwelekeo wa kufutwa na kufilisika na ninyi mmeweka mtaji wenu mojawapo ni benki ya walimu,” amesema Rais Magufuli.

Rais aliwataka walimu kuhoji namna ambavyo fedha walizoziwekeza zinavyotumika katika kuendeleza benki hiyo na maslahi ya walimu.

“Sitaki kuwaficha walimu wenzangu. Ni lazima muulize hiyo mitaji mliyoiweka pale imeenda wapi. Mliowaweka pale wana maslahi ya walimu?,” amehoji Rais Magufuli.

Aidha rais magufuli amewahakikishia walimu wote wanaodai madeni yao kwa serikali kuwa watalipwa mara baada ya uhakiki kukamilika endapo tu madeni yote ni halali.

“Nataka kuwaahidi kwamba haya madeni ya walimu, hata kama yangekuwa bilioni ngapi, Kama ni madeni halali nawahakikishia kuwa nitayalipa yote. Nataka niwaahidi walimu wenzangu, mara baada ya kazi hii ya uhakiki kumalizika, wale wote wanaodai madeni halali watalipwa,” alisema Rais Magufuli.

Bofya Hapa Kuyatazama Majina ya askari 14 wa JWTZ waliouawa DRC

$
0
0
 Haya ni majina ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani.

Wanajeshi hayo ni;  
  1. Hamad Haji Bakari, 
  2. Chazil Khatibu Nandonde, 
  3. Idd Abdallah Ally, 
  4. Juma Mossi Ally,  
  5. Ally  Haji Ussi, 
  6. Pascal Singo, 
  7. Samwel Chenga, 
  8. Deogratius Kamili, 
  9. Mwichumu Vuai Mohamed, 
  10. Hassan Makame, 
  11. Issa Mussa Juma, 
  12. Hamad Mzee Kamna, 
  13. Salehe Mahembano na 
  14. Nazoro Haji Bakari.
Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.

Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.

Rais Wa Msumbiji Filipe Nyusi Awasili Mkoani Dodoma Na Kupokewa Na Mwenyeji Wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakipita kwenye gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za utamaduni mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakati vikundi vya ngoma vilipokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi katika Ikulu ya Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao.

PICHA NA IKULU

Mbunge mwingine wa CHADEMA atangaza kujivua ubunge na kuhamia CCM

Video: Msikilize Mbunge wa CHADEMA aliyejiuzuli Ubunge akieleza sababu za Kujiuzulu

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Siha, Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Godwin Oloyce Mollel, aliyetangaza kujivua uanachama wa chama chake na kujiuzulu ubunge amewashukuru wananchi wake wa Siha kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati akiwa madarakani.

Godwin Mollel amejiuzulu nafasi yake ya Ubunge pamoja na kujivua uanachama wa CHADEMA huku akiomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kumpokea na kusema kuwa sababu kubwa iliyomfanya ahame ni kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli katika kupigania rasilimali za nchi.

==>Bofya hapa kutazama video ya Godwin Mollel akieleza sababu zaidi

Mwanamke adaiwa kumuua mke mwenza na kumzika shambani

$
0
0
Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara anatuhumiwa kumuua mke mwenza na kumzika shambani.

Kifo hicho kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi kimetokea katika Kata ya Kibimba mkoani Kagera ambako aliyeuawa alizikwa kwenye shamba la viazi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayenzi, Philipo Rutumbanya amesema Edina Joseph (28) anatuhumiwa kumuua Noelina Joseph (24).

Wawili hao ni wake wa Joseph Laurean (33), mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara.

Rutumbanya amesema mauaji hayo yalifanyika jana Jumatano Desemba 13,2017 saa 7:30 mchana na kwamba mtuhumiwa amefikishwa polisi.

Amesema Edina alihisiwa kuhusika na mauaji baada ya mumewe kumkuta akiwa na damu mwilini shambani.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema Laurean  alipomhoji mkewe hakujibu lolote na alipofuatilia shambani aliona nguo za mkewe mdogo lakini yeye hakuwepo.

Amesema Laurian alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ndipo mtuhumiwa Edina alipohojiwa na alieleza alikuwa na chuki na mke mwenzake aliyeolewa miezi miwili iliyopita.

Mwenyekiti huyo amesema walimweka Edina chini ya ulinzi na aliwapeleka kwenye shamba la mume wake ambalo ni mali ya binamu yake John Shimimana alikoonyesha alikomzika mwenzake kwenye tuta la viazi.

Akizungumzia tukio hilo, mume wa wake hao, Laurian amesema ameishi na Edina kwa miaka 12 na wamejaliwa watoto watano; wa kike mmoja na wa kiume wanne. Pia ni mjamzito.

Laurian amesema mkewe mdogo alimpangia nyumba katika Kijiji cha Kanazi umbali wa kilomita sita kutoka Kijiji cha Mayenzi na alimpatia shamba ambalo alipewa na binamu yake Shimimana, ambaye ni diwani wa Kata ya Kibimba.

Amesema alipotoka matembezi kijijini alifika nyumbani kwa Edina alikokuwa amelala Jumanne Desemba 12,2017 lakini  hakumkuta.

Laurian amesema alikwenda kumuona mkewe mdogo Noelina aliyekuwa shambani ambako alimkuta Edina akiwa na jembe na mwili ukiwa na damu.

Amesema alipomhoji kuhusu damu alitetemeka na alipofuatilia alikuta nguo za Noelina lakini yeye hakuonekana.

"Tangu nioe mke wa pili kumekuwa na malumbano na malalamiko lakini niliona kawaida sikutarajia kama angechukua uamuzi wa kumuua mwenzake," amesema Laurian.

Polisi wilayani Ngara imefika eneo la tukio ambako Edina amekamatwa na baada ya kupata kibali cha Mahakama ya Wilaya ya Ngara mwili wa Noelina umefukuliwa.

Akizungumza wakati wa kufukua mwili ofisa upelelezi wa Polisi wilayani Ngara, Edward Masunga amewataka wananchi wakiwemo wanandoa kufuata utaratibu wa kufikisha malalamiko kwa viongozi wa vijiji badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Maaskari wakifukua mwili wa Noelina aliyeuliwa na mke mwenza

Rais Magufuli: Wanaosema Vyuma Vimekaza Waweke Grisi la Sivyo Vitavunjika

$
0
0
Rais John Magufuli amesema vyuma vikikaza vinatakiwa kuwekwa grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa.

Amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Rais Magufuli amesema waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali ndiyo wanaosema vyuma vimekaza.

“Vyuma vimekaza na bado vitavunjika kabisa nawashauri muweke grisi,” amesema.

Msemo wa vyuma vimekaza umekuwa maarufu katika siku za karibuni ukiwa na maana maisha yamekuwa magumu.

Rais Magufuli amesema alipoingia madarakani alikuta changamoto nyingi zikiwemo za wafanyakazi hewa, vyeti feki na ufisadi. 

Amesema baada ya kudhibiti, watumishi wa umma 12,000 wamepatikana na vyeti feki wakiwemo walimu 3,655 tangu walipoanza kuhakiki.

Amesema uhakiki huo ulibaini watumishi hewa 20,000 na kwamba, Serikali ilikuwa inapoteza fedha nyingi kuwalipa mishahara.

“Kila kitu kilikuwa hewa hata mapenzi inawezekana yalikuwa hewa,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kutokana na udhibiti wa fedha za Serikali ni lazima watu waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali watalalamika kuwa vyuma vimekaza.

Kuhusu madai ya walimu, amesema Sh25 bilioni wanazoidai Serikali zitalipwa baada ya uhakiki kumalizika

==>Msikilize hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 15

Serikali yamkamata Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)

$
0
0
Na Joel Maduka, Geita
Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .

Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .

Akiwa katika katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Geita,Mhe.Kangi Lugola ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria huyo baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi ya wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na bila kutarajiwa.Mwanasheria huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo ili usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka, alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo usibebeshwe mzigo huo.

Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.

Diwani wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea kuwa wananchi wamekuwa wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia na kwamba kutokana na wao kuwa ndani ya bikoni kumesababisha kutokupatiwa huduma mbali mbali za kijamii hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu kuwasaidia wananchi hao.

Bw Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza Naibu waziri kwamba wamekuwa wakiishi maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo hayo ya mgodini na kwamba mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya shilingi elfu ishirini jambo ambalo limeonekana kuwa ni udhalilishaji kwani pesa hiyo ni ndogo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu suala la fidia hadi sasa kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza walilipa kiasi cha sh,Bilion Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia wananchi

Pesa Haiendi Bure Ni Dawa Asilia Ya Kuongeza Ukubwa Wa Maumbile Ya Kiume.

$
0
0
Wanaume  wengi  wanakosa  raha  ya  kuwa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  kwa sababu  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Ndoa  nyingi  zimevunjia, mahusiano mengi  yameharibika, huku  chanzo  kikuu  kikiwa  ni  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume.

Uzoefu  wangu katika  tiba  asilia, umeniwezesha  kugundua kuwa,  wanawake  wengi  hulazimika  kutoka  nje  ya  mahusiano  au  kwenda  nje  ya  ndoa , pale  wanapo gundua  kuwa  wameangukia  kwenye  mikono  ya  mwanaume  mwenye  maumbile  madogo  ya  kiume.

Kitu  kikubwa  kinacho weza  kumfanya  mwanamke , kuendelea  kukaa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  na  mwanaume  mwenye  tatizo  la  maumbile  madogo  ya  kiume, ni  pesa. 

Hapa  mwanamke  husika, hulazimika  kuendelea  kuwa  katika  mahusiano  au  ndoa  na  mwanaume  huyo  kwa  sababu  mwanaume  huyo  ana  pesa, lakini  hulazimika  kutoka  nje  ya  ndoa  pindi  anapo hitaji kufurahia  mapenzi.

Ama  kwa  upande  wa  wanaume  wenye  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume. Hofu  na  mashaka  hutawala  katika  maisha  yao yote  ya  kimahusiano.

Huwa  hawajiamini  kama  mwanamke  anaweza  kuwapenda  kwa  jinsi  walivyo.

 Wivu  na  gubu  hutawala  katika  maisha  yao yote  kimahusiano. 

 Karibu  kila  kosa  linalo   fanywa  na  wenzi  wao hulihusisha  na  udogo  wa  maumbile  yao.

Kwa  mfano :  Wamekwaruzana kidogo, mke  kamnunia  au  labda  kamsonya, wao  hufikiri  wamenuniwa  au  kusonywa  kwa  sababu ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Amempigia  simu  mpenzi  wake  au  mke  wake, halafu  bahati  mbaya  simu  haijapokelewa zaidi ya  mara  tatu, basi  moja  kwa  moja  huhisi  mke au  mpenzi  anamsaliti kwa  sababu  ya  udogo  wa  maumbile  yake  ya  kiume .  Wakati  ukweli  unaweza  kuwa  tu  labda  simu  ilikuwa  silence  kwenye  pochi.

Wakiwa  wanafanya  tendo  la  ndoa, halafu  baada  ya  kumaliza  mshindo  mmoja,  halafu  baada  ya  dakika  kadhaa, mwanamke  akawa  anataka  waendelee tena, basi  mwanaume  huhisi  kama  vile  mwanamke  huyo  anamkejeli  kwa  sababu  ana  maumbile  madogo na  yasiyo  na  nguvu  za  kutosha.

Vile vile, wakifanya  tendo moja  tu  halafu  mwanamke  akasema  amechoka, basi  jamaa  atachukulia  hiyo  kama  amedharauliwa  na  mwanamke  huyo, kwamba  mwanamke  hafurahii tendo la ndoa  kwa  sababu  ya  maumbile  yake  madogo.

Maumbile  huwa  madogo  na  husinyaa  zaidi  mara  baada  ya  kumaliza  tendo la  ndoa. Hali  hii humfanya  mwanaume huyo  kutokujiamini zaidi  na  kuvaa  taulo  ama  kaptula  haraka, ili  mwanamke  wake  asimuone  katika  hali  hiyo.

Wanapokuwa  faragha  na  wanawake  wao  huwa  hawapendi  kushikwa  maumbile  yao, hasa  yanapokuwa  bado  hayajasimama.

Kwa  ufupi  wanaume  wenye  maumbile  madogo  ya kiume, wanaishi  maisha  ya  tabu  sana  katika  mahusiano  yao.

NINI  TIBA  YA  TATIZO   LA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME ?

Kama  una  tatizo  la  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume, liwe  limetokana  na  kusinyaa  kwa  sababu  ya  kujichua  kwa  muda  mrefu, kuugua  chango  la  kiume  au  kurithi  kwa  wazazi  wako, tumia  tiba  ya  asili  iitwayo   PESA  HAIENDI BURE.

Ni  tiba  ya  asili  ambayo  imekuwa  ikitumika  toka  enzi  za  mababu  na  mababu  wa  mababu. 

Itasaidia  kuimarisha, kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  yako  ya  kiume  na  kukufanya  kufurahia   tendo la  ndoa.

Tiba  hii  haitakufanya  kufurahia  tendo la  ndoa  tu, bali  hata  mke  wako au  mpenzi  wako, itamfanya  pia  afurahie  tendo la ndoa  na  kuongeza  upendo  na  uaminifu  kwako.

Unapokuwa  na  uwezo  wa  kufurahia  tendo  la  ndoa  pamoja  na  kumfanya  mke  au  mpenzi  wako  kufurahia  tendo  la  ndoa, unakuwa  pia  unajiepusha  na  uwezekano  wa  kupatwa  na  maradhi  ya  kuambukizwa  kwa  njia  ya  kujamiiana  kama  vile  Kaswende, Kisonono  na  hata  V.V.U  .

JINSI  YA  KUPATA  TIBA  HII: Kupata  tiba  hii, wasiliana  na  DOKTA.  MUNGWA  KABILI  KWA  SIMU  NAMBA  :   

0744  000  473.     www.mungwakabili.blogspot.com

Tanzania na Msumbiji kubadilihsana uzoefu wa gesi na mafuta

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Mjini Dodoma.

Mhe. Filipe Jacinto Nyusi amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Dodoma na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kisha viongozi hao wamefanya mazungumzo rasmi na kusalimu wananchi kupitia vyombo vya habari.

Mhe. Rais Nyusi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumpokea na kufanya nae mazungumzo na amesema ujio wake umelenga kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na kidugu kati ya nchi yake na Tanzania.

“Mhe. Rais Magufuli japo kuwa nimetoa taarifa ya muda mfupi kuwa nakuja kuonana nawe, umenikaribisha umenipokea na tumezungumza mambo yenye manufaa kwa nchi zetu, nakushukuru sana” amesema Mhe. Rais Nyusi.

Amebainisha kuwa yeye na Rais Magufuli wamezungumzia namna Tanzania na Msumbiji zitakavyobadilishana uzoefu kuhusu ugunduzi mkubwa wa gesi na mafuta uliofanikiwa katika nchi hizi, masuala ya ulinzi na usalama na uimarishaji wa miundombinu ya usafiri.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Nyusi kwa kuja Mjini Dodoma na kwa kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria uliojengwa na waasisi wa mataifa haya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Samora Machel wa Msumbiji.

Mhe. Rais Magufuli amesema katika mazungumzo hayo pia wamekubaliana Tume ya pamoja ya ushirikiano ya Tanzania na Msumbiji zikutane haraka ili kuimarisha maeneo yote ya ushirikiano kwa manufaa ya nchi hizo.

“Nafurahi kuwa Mhe. Rais Nyusi pia amesema Msumbiji itatoa kibali kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kufanya safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Msumbiji haraka iwezekanavyo, ili kurahisisha usafiri kati yetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Nyusi ameondoka nchini jana jioni  na kurejea nchini Msumbiji.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma

Kauli ya CHADEMA kufuatia kujiuzulu kwa Mbunge wa Siha Godwin Molel

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) tarehe 14 Disemba,2017 tumepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Siha Dr.Godwin Mollel amejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM .
 
Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa.

Sababu hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.

Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu.

Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya ‘hapa kazi tu’ na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.

CHADEMA tuko imara sana na tutaendelea na ajenda zetu bila kuyumbishwa na wimbi hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga kura wao kwa kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali kwa maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.

Tutaendelea kujenga Taifa letu na Chama chetu bila kujali njaa za baadhi yetu wala maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama. Ni dhahiri wale waliotanguliza ubinafsi hatutaweza kufika nao mwisho wa safari hii.

Imetolewa  Alhamis 14 Novemba, 2017 na ;
John Mrema,
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Serikali kufuta utitiri wa mifuko hifadhi ya jamii

$
0
0
Rais John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili.

Amesema mifuko itakayobaki ni kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma.

Rais Magufuli amesema Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) litabaki kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi wakati mifuko mingine yote itaunganishwa na kuwa mmoja.

Amesema hayo jana Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mjini Dodoma.

Mifuko mingine inayotoa huduma ya hifadhi ya jamii ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

Rais Magufuli alisema baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa haiwasaidii wafanyakazi badala yake imekuwa ikiwekeza kwenye ujenzi wa majengo makubwa.

“Mifuko hii haiwanufaishi wafanyakazi bali wapiga dili ambao huamua majengo yajengwe na wao kupata asilimia 10,” alisema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aagiza Benki Zisizokidhi Vigezo Zifutiwe Leseni

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania BOT kuzifutia leseni benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi zitakazoshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli za kibenki nchini.

 Ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT).

"Kwa taarifa niliyonayo hadi sasa baadhi ya benki hazijatimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha, hali ambayo haiwezi kuachwa iendelea hata kidogo, kwani haiimarishi sekta ya fedha na haiwasaidii wananchi kuendelea kiuchumi” alisema Waziri Kassim Majaliwa katika hotuba hiyo

 Alisema Benki Kuu ilitoa muda hadi mwishoni mwa Desemba 2017, benki za wananchi ziweze kuongeza mtaji na kwamba muda huo hautaongezwa na wala Serikali haitatoa mtaji kwa benki hizo.

 “Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania haitasita kuifungia benki yoyote na kufuta leseni yake ya biashara pindi itakapobaini inavunja sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi ambao unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja kama tulivyofanya kwa Mbinga Community Bank PLC kuanzia tarehe 12/5/2017” alisema Dkt. Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu.

 Maagizo hayo yamekuja siku moja baada ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango wakati akifungua tawi kuu la Benki ya CRDB mjini Dodoma, kuhakikisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, inazifuta benki zote zinazoshindwa kujiendesha kibiashara hata kama zinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.

 Alisema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha benki za wananchi zinaimarika zikiwemo kuruhusiwa kuanzisha mifumo ya ushirikiano katika Nyanja ya Mfumo wa Mawasiliano na Habari (ICT), Idara za Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit Services), kupunguza wingi wa idara na kuwa na idara tatu (3) tu muhimu, kuruhusiwa kuungana (Federation), ambazo zitapunguza gharama za uendeshaji wa benki za wananchi na kuleta ufanisi katika kutoa huduma.

 “Napenda kusisitiza kuwa sekta ya benki ni muhimu sana kwa uhai na ukuaji wa  uchumi kama ilivyo damu kwa mwili wa binadamu na kutokana na umuhimu wake huo, sekta hii ni kati ya sekta chache zinazosimamiwa  kwa karibu sana ili kulinda amana za wateja pamoja na kuhakikisha uhimilivu wa mfumo mzima wa sekta ya fedha na mwenendo wa uchumi wa Taifa” aliongeza Dkt. Mpango

 Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT) Bw. Rukwaro Senkoro, alisema hadi kufikia Juni, 2017, Benki za Wananchi nchini zilikuwa na wateja zaidi ya milioni 1.4, wateja wa vikundi zaidi ya 10,000, Matawi 12, Vituo 59, na wanahisa 66,492.

 “Benki hizo zina amana zenye thamani ya shs bilioni 74.2, zimetoa mikopo ya sh. bilioni 56.8, na jumla ya mali zenye thamani ya shs. bilioni 92.3” Alisema Bw. Senkoro

 Hata hivyo, kutokana na Utafiti wa Matumizi ya Huduma za Kifedha uliofanyika mwaka 2017 umebaini kuwa asilimia 28 ya wananchi bado hawapati huduma za kifedha hapa nchini hususan vijijini na kutaja changamoto ya ukosefu wa mitaji ya benki hizo kukwaza sekta hiyo. 

 Dhana kuu ya mkutano huo wa COBAT uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ni “Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania”, ambayo ni dhana mpya.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images