Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Magari ya polisi yaliyokuwa yamekwama bandarini yachukuliwa

$
0
0
Hatimaye magari 50 ya Jeshi la Polisi yalikuwa yamekwama Bandari ya Dar es Salaam tangu mwaka 2015 yamechukuliwa wiki iliyopita.

Novemba 26 mwaka huu, Rais John Magufuli alitembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukuta magari ya polisi yakiwa yamekaa bandarini kwa muda mrefu wakati yalitakiwa kukaa hapo kwa siku 21.

Rais Magufuli alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro kuyachukua ili yakafanye kazi iliyokusudiwa.

Leo Jumanne, Msemaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Janeth Ruzagi amesema magari hayo yameshachukuliwa na polisi.

Alisema mamlaka hiyo na polisi wamefikia makubaliano na kuyachukua magari hayo na sasa yameshaondolewa bandarini.

Akizungumzia magari ya polisi, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa amesema ni kweli wameyachukua magari hayo.

Amesema walitii agizo la Rais na kufanya mazungumzo na bandari na sasa wameshayachukua kwa ajili ya kazi mbalimbali za polisi.

Mwalimu Aliyemtandika Ngumi ya Jicho Mwalimu Mkuu Afikishwa Mahakamani

$
0
0
Mwalimu Yaredi Amosi (27), wa Shule ya Msingi Kitarungu amepandishwa kizimbani leo Jumanne kwa kosa la kumshambulia kwa ngumi na kumsababishia majeraha mwalimu mkuu wa shue hiyo, Thomas Marwa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Serengeti, Ismael Ngaile mshtakiwa amedaiwa kutenda kosa hilo Desemba 6 mwaka huu, alipomvamia mwalimu Marwa ofisini kwake na kumshambulia kwa ngumi hadi kumsababisha jeraha katika jicho lake la kushoto.

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi hiyo namba 272/2017, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Renatus Zakeo amesema kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha 16 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Mshitakiwa alikana shitaka hilo na kupelekwa mahabusu hadi Desemba 27 shauri hilo litakapotajwa tena baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho na mmoja akiwa ni mtumishi wa Serikali.

Mbunge Wa CHADEMA Amkumbuka Kikwete.....Ni Baada ya Askofu Kanisa Katoliki Aliyetaka Katiba Mpya Kuhojiwa

$
0
0
Baada ya kuwepo kwa taarifa za kuhojiwa kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61) na Idara ya Uhamiaji kuhusu uraia wake, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesema utawala wa Rais Kikwete,makanisa yalisimama na kukosoa.

Heche amesema kwamba utawala wa Kikwete Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa  ya serikali na wala hakuwahi kushuhudia viongozi wa dini wakihojiwa na kususitiza kwamba watu wasimame imara kupinga kuporwa kwa uhuru

"Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati wa utawala wa Kikwete, sikuona kiongozi anahojiwa uraia wake naamini ingekuwa kipindi hiki kanisa lingefutwa wangesema sio kanisa la Kitanzania, tusimame imara kupinga uhuru wetu kuporwa, hakuna alie salama" Heche.

Taarifa zinadai kwamba Askofu Niwemugizi alihojiwa mara 2 na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na Uraia wake kati ya mwezi Novemba na Disemba 
 “Mara ya kwanza niliitwa na kufika ofisi za uhamiaji Ngara, Novemba 28 na mara ya pili niliitwa Desemba 4.

“Niliombwa kibali kinachoniruhusu kuwa nchini, nikashangaa, nikasema mimi ni Mtanzania, nikaambiwa nilete document (nyaraka).

“Nilipeleka hati ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura na cheti cha kuzaliwa, wakasema wataniita tena.

“Baada ya kuitwa mara ya pili, nilipewa fomu ya kujaza ambayo bado naendelea kuijaza hadi sasa.

“Waliniita tena wakasema bado wanataka kujiridhisha ndio maana wanataka nijaze fomu, ninaendelea kuifanyia kazi mpaka nitakapokuwa nimeikamilisha yote,” anasema Askofu Niwemugizi ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC).

Mwishoni mwa mwezi Septemba , Askofu Niwemugizi alisema kuwa  imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri ambayo pia italetwa na Katiba Mpya .

Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, amekiri askofu huyo kuhojiwa na kusema;

“Ni kweli anahojiwa na ofisi yetu ya Wilaya ya Ngara, ni suala tu la tuhuma si kwamba ni kweli au la, hivyo itakapothibitika basi itajulikana,” alisema Mtanda.

Pesa Haiendi Bure Ni Dawa Asilia Ya Kuongeza Ukubwa Wa Maumbile Ya Kiume.

$
0
0
Wanaume  wengi  wanakosa  raha  ya  kuwa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  kwa sababu  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Ndoa  nyingi  zimevunjia, mahusiano mengi  yameharibika, huku  chanzo  kikuu  kikiwa  ni  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume.

Uzoefu  wangu katika  tiba  asilia, umeniwezesha  kugundua kuwa,  wanawake  wengi  hulazimika  kutoka  nje  ya  mahusiano  au  kwenda  nje  ya  ndoa , pale  wanapo gundua  kuwa  wameangukia  kwenye  mikono  ya  mwanaume  mwenye  maumbile  madogo  ya  kiume.

Kitu  kikubwa  kinacho weza  kumfanya  mwanamke , kuendelea  kukaa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  na  mwanaume  mwenye  tatizo  la  maumbile  madogo  ya  kiume, ni  pesa. 

Hapa  mwanamke  husika, hulazimika  kuendelea  kuwa  katika  mahusiano  au  ndoa  na  mwanaume  huyo  kwa  sababu  mwanaume  huyo  ana  pesa, lakini  hulazimika  kutoka  nje  ya  ndoa  pindi  anapo hitaji kufurahia  mapenzi.

Ama  kwa  upande  wa  wanaume  wenye  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume. Hofu  na  mashaka  hutawala  katika  maisha  yao yote  ya  kimahusiano.

Huwa  hawajiamini  kama  mwanamke  anaweza  kuwapenda  kwa  jinsi  walivyo.

 Wivu  na  gubu  hutawala  katika  maisha  yao yote  kimahusiano. 

 Karibu  kila  kosa  linalo   fanywa  na  wenzi  wao hulihusisha  na  udogo  wa  maumbile  yao.

Kwa  mfano :  Wamekwaruzana kidogo, mke  kamnunia  au  labda  kamsonya, wao  hufikiri  wamenuniwa  au  kusonywa  kwa  sababu ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Amempigia  simu  mpenzi  wake  au  mke  wake, halafu  bahati  mbaya  simu  haijapokelewa zaidi ya  mara  tatu, basi  moja  kwa  moja  huhisi  mke au  mpenzi  anamsaliti kwa  sababu  ya  udogo  wa  maumbile  yake  ya  kiume .  Wakati  ukweli  unaweza  kuwa  tu  labda  simu  ilikuwa  silence  kwenye  pochi.

Wakiwa  wanafanya  tendo  la  ndoa, halafu  baada  ya  kumaliza  mshindo  mmoja,  halafu  baada  ya  dakika  kadhaa, mwanamke  akawa  anataka  waendelee tena, basi  mwanaume  huhisi  kama  vile  mwanamke  huyo  anamkejeli  kwa  sababu  ana  maumbile  madogo na  yasiyo  na  nguvu  za  kutosha.

Vile vile, wakifanya  tendo moja  tu  halafu  mwanamke  akasema  amechoka, basi  jamaa  atachukulia  hiyo  kama  amedharauliwa  na  mwanamke  huyo, kwamba  mwanamke  hafurahii tendo la ndoa  kwa  sababu  ya  maumbile  yake  madogo.

Maumbile  huwa  madogo  na  husinyaa  zaidi  mara  baada  ya  kumaliza  tendo la  ndoa. Hali  hii humfanya  mwanaume huyo  kutokujiamini zaidi  na  kuvaa  taulo  ama  kaptula  haraka, ili  mwanamke  wake  asimuone  katika  hali  hiyo.

Wanapokuwa  faragha  na  wanawake  wao  huwa  hawapendi  kushikwa  maumbile  yao, hasa  yanapokuwa  bado  hayajasimama.

Kwa  ufupi  wanaume  wenye  maumbile  madogo  ya kiume, wanaishi  maisha  ya  tabu  sana  katika  mahusiano  yao.

NINI  TIBA  YA  TATIZO   LA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME ?

Kama  una  tatizo  la  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume, liwe  limetokana  na  kusinyaa  kwa  sababu  ya  kujichua  kwa  muda  mrefu, kuugua  chango  la  kiume  au  kurithi  kwa  wazazi  wako, tumia  tiba  ya  asili  iitwayo   PESA  HAIENDI BURE.

Ni  tiba  ya  asili  ambayo  imekuwa  ikitumika  toka  enzi  za  mababu  na  mababu  wa  mababu. 

Itasaidia  kuimarisha, kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  yako  ya  kiume  na  kukufanya  kufurahia   tendo la  ndoa.

Tiba  hii  haitakufanya  kufurahia  tendo la  ndoa  tu, bali  hata  mke  wako au  mpenzi  wako, itamfanya  pia  afurahie  tendo la ndoa  na  kuongeza  upendo  na  uaminifu  kwako.

Unapokuwa  na  uwezo  wa  kufurahia  tendo  la  ndoa  pamoja  na  kumfanya  mke  au  mpenzi  wako  kufurahia  tendo  la  ndoa, unakuwa  pia  unajiepusha  na  uwezekano  wa  kupatwa  na  maradhi  ya  kuambukizwa  kwa  njia  ya  kujamiiana  kama  vile  Kaswende, Kisonono  na  hata  V.V.U  .

JINSI  YA  KUPATA  TIBA  HII: Kupata  tiba  hii, wasiliana  na  DOKTA.  MUNGWA  KABILI  KWA  SIMU  NAMBA  :   

0744  000  473.     www.mungwakabili.blogspot.com

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano yya Disemba 13

CCM yafuta mchakato wa kumpata mrithi wa Lazaro Nyalandu

Taarifa ya Serikali kuhusu kufanyika kwa mnada wa madini ya Tanzanite

Mbunge Chadema apingana vikali na Mbowe

$
0
0
Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.

Ukawa wamesema kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haitaahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani ili kuruhusu majadiliano, hawatashiriki uchaguzi huo. Lakini Komu amesema kufanya hivyo ni kosa kubwa linaloweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.

Viongozi wa Ukawa unaoundwa na Chadema, Chauma, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF waliitaka Nec kuahirisha uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido, Songea Mjini na ule wa kata sita ili wadau wapate nafasi ya kujadili kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo kwenye kata 43 vinginevyo hawatashiriki.

Viongozi wa Ukawa; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa Baraza Kuu la CUF, Julius Mtatiro; Kaimu Katibu wa Chauma, Eugene Kabendera na Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Danda Juju walitoa msimamo huo juzi lakini jana Komu akizungumza kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.

“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.

“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji.

Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... 

“Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”

Juzi, Mbowe alisema kulikuwa na kasoro nyingi kwenye uchaguzi wa kata 43 ambazo zinahitaji kurekebishwa, lakini mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima katika taarifa yake aliyoitoa jana alisema chama cha siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe.

“Ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,” alisema Kailima.

Zitto Kabwe na Bashe waungana Kupinga kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu wa Jimbo la Katoliki, Severine Niwemugizi.

$
0
0
Mbunge Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wameungana kwa pamoja kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu wa Jimbo la Katoliki, Rulenge Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti wameeleza hisia zao juu ya jambo hilo na kudai  watu wanaofanya jambo hili ni wazi hawana hofu ya Mungu lakini pia ni njia ya kuwatisha watu hususani wale ambao wanakuwa wanaikosoa serikali.

"Najuai inavyokuwa unapoambiwa ama kuanza kujazishwa fomu na kuhojiwa juu ya Uraia Wako ni kama kujazishwa fomu kuambiwa huyu sio Mama yako or Baba yako. Pole Askofu Severine Niwemugizi wanaofanya haya hawana hata hofu ya Mungu" aliandika Hussein Bashe 
Hata hivyo Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe naye amechangia na kusema kuwa suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya watu ambao wanaonekana kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali ambayo serikali inakuwa inafanya.

"Baba askofu pole sana. Kuna watu wakubwa tu kwenye Taasisi nyeti wanaamini kwa ushahidi kuwa aliyeagiza uhojiwe mwenyewe sio raia wa Tanzania. Suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya wakosoaji wa Serikali. Ni ushamba" alisisitiza Zitto Kabwe 
Askofu Severine Niwemugizi amesema kuwa amehojiwa kuhusu uraia wake mara mbili. Mara ya kwanza aliitwa kwenye ofisi za uhamiaji Ngara Novemba 28, 2017 na mara ya pili Disemba 4, 2017.

'Expansion joint' Ya Mabweni ya Chuo ya UDSM Yazibwa

$
0
0
Wakala wa Majengo nchini (TBA) umefanya ukarabati wa majengo ya mabweni ya chuo kikuu cha Dar es salaam ambayo hivi karibuni yalionekana kuweka nyufa.

Vyombo vya habari vilivyofika kwenye eneo hilo vilikuta tayari mafundi wameshaweka plasta ili kuziba nyufa hizo, ambazo Mkurugenzi Mkuu wa TBA Elius Mwakalinga alisema zimesababishwa na 'expansion joint' ambayo ni kitu cha kawaida kwenye ujenzi.

Hivi karibuni kulisambaa picha za majengo zikionyesha kuwa na nyufa, huku yakiwa hayajamaliza mwaka tangu yakabidhiwe na kuanza kutumika na wanafunzi, kitendo kilichosababisha mpiga picha hizo ashikiliwe na polisi.
Picha zinazoonyesha nyufa hizo zikiwa zimezibwa

Baada ya kuhojiwa uraia, Askofu Niwemugizi azungumza na Rais Magufuli

$
0
0
Baada ya kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wa uraia wake Askofu wa Jimbo la Ngara - Rulenge, Severine Niwemugizi ameeleza kwamba amezungumza na Rais John Magufuli.

Jana, askofu huyo alikaririwa akisema amehojiwa mara mbili na Uhamiaji katika kile kinachoelezwa ni utata wa uraia wake huku akieleza kuwa amezaliwa wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Alipoulizwa kama mazungumzo hayo  na Rais Magufuli ni baada ya taarifa za kuhojiwa na Uhamiaji, Askofu Niwemugizi alijibu huku akianza kwa kucheka, “Hahahahaha!! Ni kweli Rais kataka kujua hasa kuna nini, yeye amesema atalifuatilia na kukiwa na... nitamfahamisha.”

Askofu huyo ambaye Septemba mwaka huu aliibua mjadala wa Katiba Mpya na kusema kuwa yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi alisema kuhojiwa huko hakutamrudisha nyuma katika misimamo yake, “Siwezi kurudi nyuma, nimetumwa na Kristo, Nabii anaweza kupendwa au kuchukiwa na mimi siwezi kunyamaza.”

Askofu Niwemugizi aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) alisema,“Mimi nazungumza lakini kuna Watanzania wengine wanazungumza sana. Lakini mimi kuhojiwa mara mbili hakutaninyamazisha.”

Ujumbe aliouweka Facebook, unasema, “Nasali Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, uniokoe na mtu wa hila asiye haki. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?

Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea? ...Nafsi yangu, kwa nini kuinama, na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu na Mungu wangu” (Zab 43:1-2,5). Asante Rais wangu JPM kwa faraja uliyonipa.”

Rais Magufuli aagiza kufungiwa kwa benki na kampuni za simu.....Aaagiza Milioni 100 Alizopewa Kama Zawadi Zikatumike Kujenga Wodi ya Wagonjwa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza mamlaka husika kuzichukulia hatua ikiwamo kuzifungia kampuni za simu na benki ambazo zitashindwa kuanza kutumia mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki ifikapo mwisho wa mwaka huu 2017.

“Kwa kampuni za simu au benki zitakazoshindwa kutekeleza agizo hili, taratibu husika zifanyike. Ikiwezekana makampuni hayo au benki hizo zifungiwe kufanya kazi nchini” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma katika hafla ya ufunguzi wa tawi la benki ya CRDB lililopo katika jengo la LAPF-Dodoma.

Rais amezitaka benki zote pamoja na makampuni ya simu ambayo yanataka kuendelea kufanya biashara hapa nchini kuhakikisha kuwa wanajiunga na mfumo huu wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki kabla ya kufika mwisho wa mwaka huu wa 2017.

“Kwa taarifa nilizo nazo ni benki chache tu ambazo tayari zimejiunga na mfumo huu wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki. Benki na kampuni nyingi za simu bado hazijajiunga na mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki.  Benki na Kampuni zote za simu zinazotaka kufanya biashara Tanzania zihakikihshe zinajiunga na mfumo huu kabla ya mwaka huu (2017) kuisha,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameagiza fedha kiasi cha shilingi 100 milioni alichopewa kama zawadi na Benki ya CRDB zitumike kujenga wodi ya wagonjwa katika hospitali ya Dodoma na kutaka wodi hiyo iitwe ‘wodi ya CRDB’ kama ishara ya heshima kwa benki hiyo.

Akiikabidhi hundi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rais Magufuli ameonya wahusika wote kutumia vizuri fedha hizo ili kuhakikisha ujenzi wa wodi hiyo unakamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachofaa.

Marekani Yasema Ipo Tayari Kufanya Mazungumzo na Korea Kaskazini Bila Masharti Yoyote

$
0
0
Marekani iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema.

Taaarifa yake ilionekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabala ya mazungummzo yoyote kufanyika

Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wake Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika.

Hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia imesababisha Marekani kuongoza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo.

Kando na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Korea Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la nchi za Atlantic siku ya Jumanne, Bw Tillerson alisema kuwa Marekani haiwezi kukubali Korea Kaskazini kujihami kwa silaha za nyuklia.

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

$
0
0
🎁OFFER YA X-MASS.🎁
    PENDEZA SASA KWA PUNGUZO KUBWA LA BEI. 
       KATIKA KUSHEREHEKEA MSIMU WA SIKUKUU  @natural2162 TUNA  PUNGUZO LA 20% KWA BIDHAA ZETU ZOTE, IKIWA NI SHUKRANI KWA KUTUUNGA MKONO.
 
BIDHAA ZETU ZOTE ZIMETENGENEZWA KWA MIMEA NA MATUNDA HAZINA KEMIKALI WALA MADHARA.
    KWA WANAUME TUNATIBU👇👇
☆Kukosa hamu ya tendo.
☆Kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo.
☆Maumbile madogo ya uume.
☆Kuchoka sana wakati wa tendo na uume kusinyaa  nk.
      @natural2162 tumeandaa tiba bora kabisa kama ifuatavyo:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @220,000/=
2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @130,000/=
3VigRX  CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @170,000/=
4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @140,000/=
5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @220,000/=
6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @140,000/= 
 
     PIA KWA WANAWAKE WANAOPENDA KUWA NA MUONEKANO MZURI ZIPO ZA👇👇👇
1.Kuongeza hips, makalio na mapaja @180,000/=
2.Kushepu mguu (CHUPA YA BIA) @130,000/=
3.Kuwa mweupe bila sugu kwa:-
(a)mafuta @130,000/=
(b) Vidonge @150,000
4.Kurefusha nywele na kutokukatika ovyo @130,000/=
5.Kuongeza hips, makalio na mapaja kwa vidonge (YODI PILLS ORIGINAL) @200,000/=
6Kupunguza au kuongeza maziwa kuyasimamisha @130,000/=
7.Kubana uke na kuondoa uchafu ukeni @120,000/=
8.Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
        NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri na garantii ili kukuhakikishia ubora na usalama wa bidhaa za NATURAL BEAUTY CO

    Wasiliana nasi Popote
  ulipo duniani kwa (+255)
           0659618585 na
           0759029968
 
        UTAPATA HUDUMA.
👉🏻OUR WEBSITE:- www.naturalworldbeauty.og
👉🏻INSTAGRAM PAGE:-
@natural2162
@natural2162
@natural2162

         < WELCOME ALL>

Mabilioni ya Fedha za Kigezi yakamatwa yakiingizwa Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema zaidi ya dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

Akiwa jukwaani mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, Rais Magufuli ameweka wazi kuwa amepata taarifa zaidi ya kiasi cha dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kinyume na sheria kupitia uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

“Ninapozungumza tu sasa hivi nimepata taarifa zaidi ya bilioni moja dola zimeshikwa Airport zilikuwa zinaingizwa Tanzania kwasababu Tanzania kimeshaonekana ni kichaka cha fedha za kigeni” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine Rais amezitaka mahakama za biashara nchini kuharakisha kesi zinazohusiana na kesi za mikopo ili kuwezesha Benki kuendelea kutoa mikopo. Pia ameongeza kuwa baadhi ya wakopaji hutumia fedha hizo hizo za mikopo kuchelewesha kesi, hivyo mahakama zinatakiwa kutoa hukumu kwa wakati.

“Nawahimiza wananchi kulipa madeni yao kwa wakati, dawa ya deni kulipa, na niziombe Mahakama za biashara kuharakisha kesi zinazohusu mikopo, mtu anapopelekwa amekopa na anatakiwa kuuziwa jengo lake au kufirisiwa, unachelewesha nini toa amri watu wakauze ilikusudi Benki ziendelee kukopesha wengine”, amesema Magufuli.

Rais Magufuli atoa onyo la Mwisho Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Baada ya Hapo Wasimlaumu

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewapa onyo la mwisho Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuwataka wawe wasimamizi wazuri wa fedha za nchi na kusema kama hawatajirekebisha basi wasijekumlaumu siku za usoni.

Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akizindua tawi moja la Benki mjini Dodoma na kuzitaka benki zote pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuangalia suala la matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi kwani jambo hilo linazidi kuuwa uchumi wa nchi.

"Haiwezekani nchi ikawa na 'curency' mbili,  tatu au zaidi zinazotumika zinaharibu uchumi, haiwezekani mtu ukiwa na dollar unakwenda kununua bidhaa dukani, ukiwa na pounds unakwenda kununua chochote nchini huu si utaratibu wa uchumi. Na hili nikuombe Waziri,  BoT na mabenki yote mlisimamie hili kikamilifu, na baya zaidi haya yamekuwa yakifanywa na BoT. Gavana upo hapa mnapotangaza tenda zenu hata za wafagiaji mnawalipa kwa Dollar .

"Sasa haiwezekani nyinyi BoT ambao mnasimamia fedha nyinyi hao hao mnakuwa wabaya wa kudhibiti fedha za nchi hili lazima muende nalo na mbadilishe haraka. 

"Msije kuwa chanzo cha kuharibu uchumi wa nchi yetu. Najua mnanielewa nililizungumza jambo hili mara ya kwanza nimelirudia leo mara ya mwisho litakalotokea msije kunilaumu" alisisitiza Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli amehitaji kuwe na uangalizi mzuri kwenye 'Bureau de Change' na kuwa na utaratibu ambao unaeleweka.

Dhamana kwa wanawake waliovishana pete yapingwa

$
0
0
Upande wa Jamhuri umewasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana ya washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya kujihusisha na vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa ya kimtandano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Hati hiyo imewasilishwa mahakamani leo Jumatano Desemba 13,2017 na Wakili wa Serikali, Emmanuel Luvinga.

Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Sonza, mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza, wanadaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote wawili kuwa wanawake.

Wengine ni Aneth Mukuki anayeshtakiwa kwa kufanikisha sherehe za wawili hao kuvishana pete na Richard Fabian anayekabiliwa na shtaka la kusambaza picha za tukio hilo mitandaoni.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma anayesikiliza shauri hilo, mawakili wa utetezi wameomba muda wa kuipitia na kuijibu hati hiyo kwa hati kinzani kwa sababu hawakuwa wameipata kabla ya kuwasilishwa mahakamani.

Ombi hilo lilikubaliwa na Mahakama ambayo imeahirisha shauri hilo kwa muda.

Mawakili wa utetezi ni Ogastin Kulwa, Mashaka Tuguta na Jebra Kimbole.

CUF Lipumba Yagonga Mwamba Tena Mahakamani

$
0
0
Maombi ya kumtaka Jaji  Wilfred Ndyansobera ajitoe katika kusikiliza mashauri ya Chama cha Wananchi (CUF) yanayoendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, yamekataliwa na kutupiliwa mbali.

Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na watu 10 wanaodaiwa kuwa ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, ambapo barua ya maombi hayo ilikuwa na malalamiko sita ikiwemo wadaiwa kutokuwa na imani na jaji.

Akisoma maamuzi ya kutokujitoa kusikiliza mashauri hayo leo Novemba 13, 2017, mbele ya mahakama, Jaji Ndyansobera, amedai kuwa baada ya kuchunguza malalamiko hayo, na kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili, amegundua kuwa hakuna kitu kinachoonyesha kama anapendelea upande mmoja, pia malalamiko hayo yalikuwa si sahihi kisheria kutokana kwamba watu 10 waliowasilisha maombi hayo, ni watu binafsi na si bodi halali ya wadhamini ya CUF.

“Bodi ya CUF ina taratibu zake za kutekeleza majukumu yake, mtu hawezi kusema anatumwa na bodi, bali bodi hufanya kazi zake. Jaji kujiondoa sio kitu chepesi ni kitu kizito,” amesema Ndyannsobera.

Jaji Ndyansobera amedai kuwa, katika kusikiliza mashauri ya CUF, alifuata sheria na katiba ya nchi, ambapo sheria inamtaka jaji kutekeleza majukumu yake katika kutoa haki, bila ya woga wala upendeleo au shinikizo kutoka upande wowote.

“Kuna mambo mawili ya msingi ya kuzingatia, jaji anatakiwa kujiondoa kwa kuzingatia mazingira ya kesi kama alikuwa anapendelea… pili kama kuna uhusiano wa karibu na mtu mmojawapo kwenye kesi au masilahi binafsi, jaji inatakiwa ujiondoe. Mahakama inatakiwa kuwa huru, jaji au Mahakama inaweza kuamua kesi kwa kuzingatia ushahidi ulioko mbele yake pasipo kupata mashinikizo kutoka nje na ubaguzi,” ameongeza.

Hali kadhalika ametaja sababu tano zilizopelekea kutokujitoa katika kusikiliza mashauri hayo, ikiwemo kuzuia ucheleweshwaji wa kesi, upotevu wa fedha, pia Jaji aliyekuwepo (Ndyansobera) ameshatoa maamuzi kwenye baadhi ya kesi hivyo inabidi aendelee kusikiliza mashauri kutokana kwamba anazijua kesi vizuri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti yya Leo Alhamisi ya Disemba 14

Rais Magufuli alionya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza bodi na menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kujirekebisha kwa kuondokana na matumizi mabaya ya fedha na kuwasilisha upya ombi lake la kutaka kibali cha kukopa fedha kwa ajili ya kumalizia miradi yake ya ujenzi iliyokwama kutokana na ukosefu wa fedha.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo  tarehe 13 Desemba, 2017 katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi wa Iyumbu Mjini Dodoma baada ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Neemia Mchechu kuomba Serikali itoe kibali kwa NHC kukopa Shilingi Bilioni 232 kwa ajili ya kumalizia miradi minne mikubwa ya ujenzi wa majengo iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na agizo hili Mhe. Rais Magufuli pia amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Bodi ya NHC kuchukua hatua dhidi ya migogoro iliyopo ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watendaji wanaoleta chokochoko.

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Neemia Mchechu na wafanyakazi wa NHC kwa kazi nzuri wanazofanya ikiwemo ujenzi wa nyumba katika maeneo mbalimbali nchini na kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Bilioni 34 hadi 154.

“Mambo mengi mnafanya vizuri, naifahamu NHC najua mmepiga hatua kubwa ya kujenga nyumba sehemu mbalimbali, lakini jirekebisheni kwenye matumizi ya fedha, nataka Waziri Lukuvi ukakae na bodi ya NHC na Mkurugenzi Mkuu mfanye tathmini na mniletee maelezo ya namna mtakavyozirudisha hizo Shilingi bilioni 232 mtakazokopa, nikipata maelezo vizuri nitatoa maelekezo Wizara ya Fedha na Mipango iwape kibali” alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mapema akitoa maelezo ya mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Neemia Mchechu amesema katika awamu ya kwanza mradi wa makazi wa Iyumbu unajenga nyumba 300, ambapo 150 zimekamilika na zimeshanunuliwa na nyingine 150 ujenzi wake umeanza.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa nyumba za makazi Dodoma hata kabla ya mradi wa Iyumbu na amebainisha kuwa ili kuwafikia Watanzania wengi ameshatoa maelekezo kwa NHC kuachana na ujenzi wa majengo marefu na badala yake kujielekeza katika ujenzi wa nyumba za kawaida zitakazouzwa kwa gharama nafuu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli ameufuta mpango wa kuwepo eneo la makaburi ya viongozi na kuagiza eneo lenye ukubwa wa ekari 129 katika kata ya Iyumbu lililochukuliwa na Serikali lirudishwe kwa wananchi na waruhusiwe kulitumia kwa shughuli zao.

Mhe. Rais Magufuli pia ametaka mchakato wa kubadili sheria ya makaburi ya viongozi wa kitaifa ufanye kwa kuwa amejiridhisha kuwa viongozi wote hawana nia ya kuzikwa katika eneo hilo.

Sherehe za uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa makazi wa Iyumbu Mjini Dodoma umehudhuriwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri na Naibu Mawaziri na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images