Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mange Kimambi Aibua Mapya Wema Kurudi CCM

0
0
Mwanadada Mange Kimambi ameibukia sakata la Wema Sepetu kurudi CCM,ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu atabiri mpango wa Wema Kurudi CCM.

Akizungumza kupitia  ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Kimambi amesema Wema  hajawaangusha watanzania  pekee bali  amejiangusha yeye  mwenyewe kwa kutokua na msimamo.

“Hujawaangusha waTZ tu, umejiangusha mwenyewe pia, your fans and everyone who cared for you. Hivi kizazi hiki kina Winnie Mandela hakuna kabisa eehe? Nakuonea huruma mnoooo sababu umepoteza credibly yooooote kwenye jamii”Ameandikia Mange Kimambi.

Hivi karibuni Mange alisema kuwa anazo taarifa za uhakika kuwa Wema Sepetu pamoja na Mama yake watarudi chama cha Mapinduzi akidai kuwa mama yake amekubali kurudi isipokuwa anasuburiwa yeye.

Mange alisema mpango wa kurudi CCM unafuatia Wema na Mama yake kubanwa katika mambo  mbalimbali kutokana na kuwa upande wa upinzani.

Wakati akitangaza kurudi CCM jana Wema alisema..

“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani” . Wema Sepetu.

Wema alijiunga chama cha Chadema mwezi februari mwaka huu akitokea chama cha Mapinduzi.

Patrick Ole Sosopi Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Kuziba Nafasi ya Patrobasi Katambi

0
0
Kamati ya Utendaji ya Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limemchagua  Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo kuchukua nafasi ya Patrobasi Katambi aliyehamia Chama cha Mapinduzi.

Kamati hiyo pia leo Desemba 2  imetangaza kuziba nafasi ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumteua John Pambalu, nafasi iliyoachwa wazi na   Sosopi. Viongozi hao wameteuliwa kuongoza baraza hilo kwa muda wa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita amesema uamuzi huo ulifanyika jana kufuatia kikao cha dharura cha kamati hiyo ya utendaji.

Amesema  baraza hilo ni mojawapo ya taasisi imara na  itaendeleza mapambano."Tunawahimiza vijana wa Chadema na vijana wote wa Tanzania wasimame kidete kwenye kazi ya kuijengea na kuipigania demokrasia ya nchi yetu katika misingi ya utawala bora na haki za binadamu,"

Kwa upande wake Ole Sosopi amesema katika uongozi wake atahakikisha baraza hilo linarudi kwenye misingi imara na kuongoza mapambano ya kudai demokrasia.

Amesema akiwa mwenyekiti hatavumilia kuendelea kuona uonevu wanaofanyiwa wanachama wa Chadema.

"Bavicha inaenda kuwa taasisi bora na imara zaidi baada ya kuondoka Katambi. Tunakwenda kupambania Demokrasia a, tutawashawishi vijana kuwa wamoja kulitetea taifa bila kujali maslahi ya vyama," amesema Ole Sosopi

Wolper: Ntamsifia Mwanaume Mwenye Pesa na Sio Mwenye Mashine Kubwa

0
0

Muigizaji wa filamu bongo ambaye sasa anajihusisha zaidi na ujasiriamali, Jackline Wolper, amesema anapenda wanaume wenye maumbile madogo kwani yeye mwenyewe maumbile yake ni madogo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV Jackline Wolper amesema hana sababu ya kupenda au kusifia wanaume wenye maumbile makubwa wakati yeye maumbile yake ni madogo.

"Actualy siwezi kusema nachukuliaje wanaume wenye maumbile madogo, na ndio nawapenda pia, kwa sababu mimi mwenyewe mdogo, nitapendaje vitu vikubwa ambavyo siwezi kuvihimili? 

"Unajua mwanamke anayesema mwanaume mashine namshangaa, mwanaume pesa bwana, mwanamke ambaye anajua maisha,  hawezi kusema mwanaume mashine, mimi mwenyewe siwezi kusifia mashine", amesema Wolper.

Pamoja na hayo Jackline Wolpler amesema kwa sasa hataki kujihusisha sana na masuala ya mahusiano, kwani amezipa kipaumbele kazi zake tu.

Mama Wema: Mwanangu Amenidhalilisha,Amenitoa Utu na Ninajisikia Vibaya yeye Kurudi CCM

0
0

Mama mzazi wa msanii Wema Sepetu ambaye hapo jana ametangaza kurudi CCM, Bi, Mariam Sepetu, amesema kitendo cha Wema kurudi CCM bila kumuomba ushauri ni kitu ambacho kimemdhalilisha kama mzazi.

Mama Wema ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia kitendo cha Mawanaye kurudi CCM, huku lawama nyingi zikiwa zinamuelekea yeye kama mzazi kwa kutomshauri vema binti yake.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo, mama Wema amesema watu wanaomshauri Wema kama wazazi wake si watu wazuri akimtaja Steve Nyerere, huku akisema hawana mapenzi ya kweli na Wema kwani alipopata matatizo walimkimbia, na badala yake CHADEMA ndio waliokuwa wakihangaika naye.

"Nasema haya kuhusiana na Steve, Wema alipopata matatizo hakuweza kutokea central kumuona Wema, leo anashangilia Wema kurudi CCM, lakini akumbuke mimi nitabaki kuwa mzazi, CHADEMA walipoona nataabika nahangaika, waliweza kuja mpaka nyumbani kwangu, kuja kutoa pole, wamemsaidia Wema, napenda kusema CHADEMA ni familia moja, na nilijua kwamba kama kunalolote Wema angerudi kutaka ushauri kwangu, hiki sio kitu chepesi, ni kitu ambacho kimenidhalilisha, kimenitoa utu na najisikia vibaya", amesema mama Wema.

Pamoja na hayo mama Wema amesema Wema atabaki kuwa mtoto wake na hawezi kumchukia kwa sababu ya kuhama chama, ingawa kitendo hiko kimemuumiza.

CCM, CHADEMA Kuchuana tena Jaruary 13 Jimboni kwa Nyalandu

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid amesema tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika ya kwamba nafasi ziko wazi.

Jimbo la Singida Kaskazini liko kutokana na kujivua  uanachama wa CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu, Songea Mjini baada ya kifo cha Leonidas Gama na Longido baada ya Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Onesmo Ole Nangole.

Akizungumzia uchaguzi wa kata sita amesema waziri mwenye na serikali za mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata hizo Tanzania Bara

Alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu(Arusha), Kihesa (Iringa), Bukumbi (Uyui), Kurui (Kisarawe), Keza (Ngara) na Kwagunda (Korogwe).

Amesema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya Desemba 12 hadi 18, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya Desemba 14 hadi 20 mwaka huu.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza Desemba 19 na kumalizika Januari 12.

Katika jimbo la Songea Mjini, amesema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2017.

Jaji Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata sita.

Breaking News: Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia ajiuzulu Ubunge VUF na Kuhamia CCM

0
0
Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Maulid Mtulia (CUF) leo ametangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa Chama cha Wananchi CUF na kuhamia CCM.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Mtulia amesema kuwa ameamua kufanya uamuzi huo leo Disemba 2, kwa utashi wake bila shinikizo la mtu yeyote.

Mtulia ameelezea sababu za kujiuzulu nafasi yake hiyo ya ubunge na kuhama chama kuwa imetokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya ubunge, na kusema “nimebaini kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza” alisema.

Aidha Mbunge huyo amesema kuwa nia yake ni kuwatumikia wananchi, na haoni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake anaona ni vema aungane na juhudi za Serikali, kwa kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali.

Mtulia amesema anawashukuru wananchi wa Jimbo la Kinondoni, kwa kumpa dhamana ya ubunge, katika uchaguzi mkuu uliopita na amewaahidi kuwa yupo tayari kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo, akiwa katika uwanja mwingine wa siasa ambao ni Chama Cha Mapinduzi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 3

Serikali kuajiri waalimu wa shule za msingi na sekondari

0
0
Serikali imepanga kuajiri walimu 11,000 wa shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha wa 2017/18.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo alisema katika mpango huo, walimu 7, 000 watakuwa wa shule za msingi na 4,000 wa sekondari.

“Hadi kufikia Desemba 31, walimu 2,700 watakuwa wameshaajiriwa,” alisema Jaffo

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma wakati wa kurekodi kipindi cha Tujadiliane kinachoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kurushwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari, Jafo alisema ajira hizo zitapunguza upungufu wa walimu unaotokana na ongezeko la wanafunzi tangu Sera ya Elimu Bure ya Msingi ianze kutekelezwa.

Tangu mwaka jana, Serikali inatekeleza sera hiyo inayoligharimu Taifa zaidi ya Sh20 bilioni kila mwezi, huku idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa katika shule za msingi na wale wanaojiunga na za sekondari ikiongezeka kwa zaidi ya wanafunzi milioni moja.

Kuhusu miundombinu shuleni alisema kwamba Serikali imetenga zaidi ya Sh37 bilioni za ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari za umma 148.

Akifafanua, Jafo alisema zaidi ya Sh21 bilioni zimetumika kujenga mabweni 85 katika awamu ya kwanza ya mpango huo, huku awamu ya pili ya kujenga mabweni 65 iliyoanza kutekelezwa Agosti ikitarajiwa kugharimu Sh16 bilioni.

Kuhusu matundu ya vyoo na vyumba vya madarasa, Waziri Jafo alisema Serikali imetenga zaidi ya Sh246 bilioni kukabiliana na upungufu wa matundu ya vyoo na vyumba vya madarasa katika shule za umma.

“Theluthi moja ya fedha hizo, sawa na Sh82 bilioni zitatumika kukamilisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi,” alisema.

Waziri Jafo alisema kuwa Serikali imepanga kujenga vituo vya afya 172 kwa fedha kutoka Benki ya Dunia (WB), Serikali ya Canada na wadau wengine kupitia mfuko wa pamoja wa kuendeleza Sekta ya Afya (Basket Fund).

“Lengo ni kutekeleza sera ya zahanati kila kijiji na kituo cha afya katika kila kata ili kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma za afya,” alisema Jafo.

Alifafanua kuwa hivi sasa ni kata 530 pekee kati ya 3,900 zilizopo nchini ndizo zenye vituo vya afya.

Kuhusu upatikanaji wa dawa na vifaatiba, alisema Serikali imeongeza bajeti hadi kufikia Sh269 bilioni kwa ajili hiyo.

“Tunazo pia zaidi ya Sh127 bilioni za Basket Fund zitakazoelekezwa kwenye utatuzi wa changamoto ya upungufu wa dawa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali za umma,” alisema.

Akizungumzia upungufu wa watumishi katika sekta ya afya iliyochangiwa na uhakiki wa vyeti feki, Waziri Jafo alisema tayari Serikali imeajiri watumishi 2,058 huku wengine zaidi wakitarajiwa kuajiriwa.

Suala la uhakiki wa vyeti lililoendeshwa na Serikali mwaka jana liliwanasa zaidi ya watumishi 19, 000 ambao ajira zao zilisitishwa, huku sekta ya afya na elimu zikiathirika zaidi.

Waziri Kigwangala afanya ziara ya kushtukiza bandarini

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam ambapo alibaini uwepo wa makontena yenye magogo ambayo ni mazao ya misitu yaliyokaa bandarini hapo kwa zaidi ya miaka 10.

Waziri Kigwangalla ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo hayo 938  na kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikali.

Aidha Dkt. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka nchini Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia na yalivunwa wapi na kwa vibali gani vya nchi hiyo pamoja na kufuatilia nyaraka za kuingiza ndani ya Tanzania.

Ameagiza kitengo cha kuzuia ujangili kifuatilie kubaini uhalisia na uhalali wa taarifa hizo vinginevyo yatakuwa mali ya Serikali.

Dkt. Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika, pia uwepo wa taarifa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaotoa vibali na kugonga nembo kinyume cha taratibu za kisheria, hali inayotishia usalama wa raslimali adimu ya misitu yetu ya asili.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Anthony Diallo Adai Kukerwa Kupekuliwa na Maofisa wa TAKUKURU

0
0
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Anthony Diallo amedai kukerwa na kitendo cha maofisa wa Takukuru kusimamisha gari lake na kulipekua, wakati alipokuwa kwenye harakati za kampeni wilayani Ukerewe.

Mfanyabiashara huyo maarufu Kanda ya Ziwa anatetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika jana.

Hali hiyo, imekuja wakati uchaguzi wa viongozi wa CCM ukiwa umefikia ngazi ya mkoa huku katika baadhi ya mikoa kukiwa na malalamiko mengi ya rushwa.

Akizungumza wakati akiomba kura jana, Diallo alisema amesikitishwa na kutofurahishwa na kitendo cha maofisa hao.

“Kitendo hiki (cha gari kupekuliwa), hakikuwa cha kiungwana,” alisema Diallo ambaye anamiliki kampuni ya Sahara Media inayomiliki kituo cha televisheni na redio.

“Hata mimi najua rushwa ni adui wa haki na nimeahidi kupambana na rushwa kwa ahadi na imani ya mwana CCM.”

Mbali na kupekua gari la waziri huyo wa zamani, Takukuru iliwahoji baadhi ya wagombea na wanachama mkoani Simiyu kwa tuhuma za rushwa.

Wakati mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza, Ernest Makale akithibitisha kupekuliwa kwa gari la Diallo, mwenzake wa Simiyu, Adili Elinipenda amesema taasisi yake inawashikilia viongozi na wanachama kadhaa kwa mahojiano.

Kuhusu gari la Diallo kupekuliwa, Makale alisema tukio hilo lilitokea wilayani Ukerewe baada ya maofisa wa Takukuru kupata taarifa kuwa kiongozi huyo aliyekuwa wilayani humo kufanya kampeni alikuwa akijihusisha na vitendo vya rushwa.

“Hata hivyo, baada ya kulisimamisha gari yake na kufanya upekuzi, hatukukuta ushahidi wowote na kumuachia kuendelea na kampeni zake,” alisema Makale.

Diallo aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, ni miongoni mwa wagombea waliopitishwa na Halmashauri Kuu kutetea nafasi yake.

Katika tukio la Simiyu, Elinipenda alisema Takukuru inaendelea kuwahoji baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM lakini hakuwa tayari kuwataja.

“Nitatoa taarifa na kutaja majina ya tunaowahoji baada ya zoezi la kuwahoji kukamilika,” alisema Elinipenda.

Polisi, TCRA wazungumzia akaunti ya Mange Kimambi

0
0
Jeshi la Polisi limetaka liachwe liendelee kufanya kazi yake kwa weledi katika kushughulikia suala la Mtanzania aishiye ughaibuni, Mange Kimambi, ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwatusi mitandaoni watu mbalimbali wakiwamo viongozi.

 Akizungumza na Nipashe  kuhusiana na uwezekano wa wao kuifunga akaunti ya Kimambi ikiwa sehemu ya hatua wanazochukua kwa sasa, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, alisema ni kweli jeshi lao linalifanyia kazi suala hilo.

Hata hivyo Mwakalukwa hakutaka kukubali au kukataa juu ya kile kilichodaiwa kutokea kwenye akaunti ya Kikambi na badala yake kutaka apewe muda wa kulifanyia kazi ndipo alitolee maelezo ya kina.

“Hili jambo lina mambo mengi sana. Watu wengi wanahusika na taasisi nyingi (pia) zitahusika kulishughulikia, Hivyo tunaendelea kupokea mawazo ya watu mbalimbali kuhusu namna ya kwenda nalo… mawazo wanayotupa tunayafanyia kazi lakini naomba mtuache kwanza tunaendelea kulishughulikia,” alisema Mwakalukwa.

Aidha wakati Msemaji wa Polisi akisema hayo, TCRA ilisema kuwa haiwezi kufunga wala kuingilia akaunti ya Kimambi kwa sababu huo siyo wajibu wake kisheria.

Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala, aliiambia Nipashe kuwa mamlaka yao haina nguvu za kisheria kufanya kazi hiyo bali wenye wajibu wa kufanya hivyo ni kitengo cha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni cha Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi, msemaji huyo alisema makosa yote yanayohusu mitandao, yakiwamo ya watu kutishiwa maisha, kutukanwa, kuibiwa kwa njia ya mtandao au kunyanyaswa kwa namna yoyote mtandaoni, wanaohusika ni polisi na siyo TCRA.

“Masuala ya akaunti za watu kwenye mitandao kama hiyo unayosema (ya Kimambi)… mwenye mamlaka ya kuingia na kuzifunga ni Jeshi la Polisi. Bunge liliipa mamlaka ya kisheria polisi kuchunguza na kukamata wahalifu kama hao… waulizeni wao,” alisema Mwakyanjala.

Hata hivyo zipo taarifa mitandaoni  zilimkariri Mtanzania huyo aishiye Marekani kuwa kilichotokea ni matokeo ya kazi ya wadukuzi wa mitandaoni, maarufu kama ‘hackers’ kupoteza akaunti yake yenye wafuasi takribani milioni 1.5.

Pamoja na hayo upo ujumbe wa lugha ya kigeni uliokuwa ukisambaa kwenye mtandao wa instagram ukionyesha kuwa akaunti inayofahamika kuwa ni ya Kimambi, imefungwa na waendeshaji wa mtandao wa Instagram kwa sababu ya kuwapo kwa malalamiko dhidi ya machapisho ya akaunti hiyo.

TBS latolea ufafanuzi taarifa zilizosambazwa mtandaoni kulihusu

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 4

CHADEMA Wakausha Mnyika kujivua uanachama

0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha habari inayoenea kuhusu Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kujivua uanachama kuwa hazina ukweli wowote na zinapaswa kupuuzwa.

Chadema wametua kanusho hilo kupitia mtandao wa Twittter kwenye ukurasa wa chama hicho na kusema kwamba wanaosambaza habari za Mnyika kujivua ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.

"Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. John Mnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA. Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania".

Mo Dewji ashinda zabuni ya uwekezaji ndani ya Club ya Simba SC

0
0
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji amepita katika mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Tsh bilioni 20.

Dewji ambaye amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau kubwa la Tsh bilioni 20 kupata hisa kwa asilimia 51 ndani ya klabu hiyo amekubaliwa kwa dau hilo kwa kupata hisa 49.

Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo wa mabadiliko, Jaji Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa jana.

“Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” amesema Jaji Mihayo.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) yachunguza picha zinazodaiwa za hosteli UDSM

0
0
Wakati picha za majengo yenye nyufa zikisambaa mitandaoni ikidaiwa ni ya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umekwenda kukagua ili kujiridhisha.

Majengo hayo yaliyojengwa na TBA kwa miezi minane yakielezwa kugharimu Sh10 bilioni yalizinduliwa Aprili 15,2017.

Ujenzi ulifanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kumaliza tatizo la malazi kwa wanafunzi wa UDSM.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, jana alisema hata yeye ameziona picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.

“Nimeziona na muda huu najiandaa kwenda huko kuangalia kama taarifa hizo ni za kweli,” al;isema Mwakalinga 

Picha hizo zilianza kusambaa jana jioni. Mwakalinga alisema huenda picha hizo ni za majengo mengine lakini zimehusishwa na hosteli hizo.

“Nitatoa taarifa baada ya kukagua majengo hayo kwa sasa siwezi kuzungumza hadi nitakapoona,” alisema.

Mchungaji Rwakatare aomba Rais Magufuli aungwe mkono

0
0
Askofu wa Kanisa la Assemblies of God maarufu Mlima wa Moto, Dk Getrude Rwakatare ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kusimamia rasilimali za Taifa.

Akihubiri katika kongamano la Shiloh lililotumika kuliombea Taifa amani jana Jumapili Desemba 3,2017, Mchungaji Rwakatare alisema katika miaka miwili aliyokaa madarakani, Rais Magufuli  amefanya mambo mengi katika kusimamia rasilimali za nchi, kupambana na rushwa, ubadhirifu na kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma.

“Ili kumuunga mkono Magufuli ni lazima kila Mtanzania atimize wajibu wake katika kujiletea maendeleo yake na ya Taifa kwa jumla,” alisema katika kanisa lake lililopo Mikocheni B wilayani Kinondoni.

Mchungaji Rwakatare alisema wananchi wanaolalamika kwamba hali ya maisha ni ngumu ni lazima wabadilike na kuacha kuishi maisha ya kuigiza.

“Tuvae viatu vinavyotutosha kwa kuishi maisha yanayolingana na kipato chetu, tusiishi maisha ya kuigiza mambo ambayo hatuna uwezo nayo,” alisema.

Mchungaji Rwakatare alisema wananchi wanatakiwa kubadilika kwa kuwa fedha za ujanjaujanja ni vigumu kuzipata kutokana na Serikali kuziba mianya ya ubadhirifu.

Kuhusu kongamano hilo, alisema hufanyika kila mwaka likilenga kumshukuru Mungu kwa mambo ambayo amewafanyia.

“Tunapomaliza mwaka ni lazima tumshukuru Mungu kwa mambo ambayo ametufanyia na kuliombea Taifa kwa ajili ya mwaka 2018,” alisema.

Kabla ya maombi, waumini wa kanisa hilo waliimba wimbo wa Taifa wakiwa wameshika bendera za Taifa.

Mchungaji wa kanisa hilo kutoka Arusha, Dk Dastan Maboya alisema ni muhimu kuwaombea viongozi ili wafanye uamuzi wenye masilahi kwa Taifa.

“Amani iliyopo si kwa sababu imeshuka kutoka mbinguni bali ni misingi bora iliyofanywa na waasisi wa Taifa hili, tuwaombee viongozi waliopo waendelee kufuata nyayo zao,” alisema.

Bavicha wasema Wema hakuwa mwanachama Chadema bali Alikuwa ni Shabiki Tu

0
0
Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) umesema mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006,  Wema Abraham Sepetu hakuwahi kuwa mwanachama wala kukabidhiwa jukumu lolote katika operesheni za chama hicho kikuu cha upinzani kwani alikuwa shabiki.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Patrick Ole Sosopi amesema hayo juzi baada ya kutangazwa kurithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Patrobas Katambi ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi mwezi uliopita.

“Wema alikuwa shabiki wa Chadema na Chadema ina wafuasi wa namna mbalimbali. Wapo tunaowafahamu na tusiowafahamu. Wema hakuwa chochote ndani ya Chadema. Wema hakuwahi kufanya ‘movement’ yoyote. Msiwe mnasema amerudi, kwani anatoka wapi?"-  Ole Sosopi.

Aliongeza; “Wema hakuwahi kupewa kadi yoyote ya Chadema. Alikuja kwa matatizo yake na ameondoka kwa matatizo yake lakini hakuwa na sifa hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Wema ameondoka peke yake, wacha waondoke".

Ole Sosopi aliyeteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha kuwa kiongozi wake, alisema kwa sasa Chadema inapitia kipindi muhimu kitakachoiimarisha.
 
Hata hivyo Ole Sosopi aliongeza kwamba  CHADEMA wameweka mipango katika katiba kuhusiana na watu wanaohama wakitaka kurudi ndani ya chama hicho hawatakubaliwa mpaka wafanyiwe uchunguzi wa kutosha kama dhamira yao ni njema kwani wao si kama daladala ambalo unapanda, unashuka ili mradi uwe na nauli.

Waziri awataka wanafunzi kuitumia Vizuri Mikopo Wanayopewa

0
0

 Naibu Waziri wa Fedha  Dk  Ashatu Kijaji amewataka wanafunzi wanaochukua mikopo ya elimu ya juu kwa ajili ya kujiendeleza kuitumia ipasavyo  kwa kusoma zaidi  ili watimize ndoto zao za elimu na hatimaye waliwezeshe taifa kupata wataalamu wa kutosha.

Amesema hayo  jana Desemba 3  kwenye  mahafali ya 19 ya Chuo cha Uhasibu Arusha  kikishirikiana na chuo kikuu cha Coventry cha Uingereza.

Alisema kuwa ,serikali kwa sasa inapambana katika kuhakikisha kuwa vijana wanapata mikopo ya kujiendeleza elimu ya juu hivyo ni vyema wanafunzi wote walionufaika na fursa ya kupata mikopo hiyo kuitumia kwa kusoma kwa makini ili kuliwezesha taifa kupata wataalamu wa nyanja mbalimbali.

"Nawaombeni Sana  mtumie fursa hiyo ya mikopo kujiendeleza zaidi katika fani mbalimbali ili tupate wataalamu watakaowezesha kuziba mianya mbalimbali ya wataalamu wanaohitajika ambao wamejiendeleza zaidi na waliobobea katika gani mbalimbali  "alisema Kijaji.

Kwa  upande wa Mwenyekiti wa baraza la uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha, Rukia Adamu alisema kuwa, chuo hicho kimejikita katika kutoa mafunzo katika ngazi za Astashahada, shahada, stashahada na stashahada za uzamili  katika fani mbalimbali.

Alisema kuwa, chuo hicho pia kimeanza programu  maalum ya kujitolea kufundisha katika shule za sekondari zilizo Karibu na chuo kama mchango wao kwa taifa katika kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya hisabati, biashara  na teknolojia ya habari.

Rukia alisema kuwa, mojawapo ya mikakati ya chuo hicho ni kuanzisha kozi mbalimbali ambazo zinaendana na mahitaji ya soko kwa sasa ,huku chuo kikiendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kujua mahitaji ya watanzania ili kuweza kuanzisha kozi mbalimbali zinazokidhi mahitaji yao ili kuondoa adha wanayoipata watanzania kwenda kutafuta hizo kozi nje ya nchi kwa gharama kubwa.

Naye Kaimu Mkuu wa chuo hicho cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi alisema elimu waliyopatiwa wahitimu hao utawawezesha kujiajiri wenyewe badala ya kuajiriwa katika nyanja mbalimbali walizosomea, huku ukizingatia uwezo wa serikali kuajiri wahitimu katika nyanja mbalimbali unapungua siku hadi siku.

Dk Kasidi amewataka wahitimu hao kutumia elimu yao kujitengenezea ajira, badala ya kuchagua kazi halali ambayo inawapatia kipato halali, hivyo akiwataka wote kuhakikisha wanaungana pamoja katika kuelekea nchi ya viwanda.

BomoaBomoa Ilivyoacha Kilio na Majonzi Dodoma

0
0
Vilio vimetawala katika  bomoabomoa kwa watu waliojenga katika eneo la hifadhi ya kampuni ya Miliki ya Raslimali za Reli (Rahco) ambapo jumla ya nyumba 128 na vibanda vidogo 487 vimebomolewa katika eneo hilo.

Watu hao waliwekewa alama za X  wakitakiwa kubomoa  kwa hiari yao Novemba 25 mwaka jana kwa mara ya mwisho wakitakiwa kupisha eneo la hifadhi ya reli walilovamia.

Akizungumza jana Desemba 3  mara baada ya kukamilisha zoezi hilo, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Catherine Moshi alisema bomoabomoa hiyo ilihusisha vibanda vya stendi ya daladala ya Jamatini, vibanda vya stendi ya mabasi ya kwenda mikoani, Ofisi za kampuni ya mabasi ya Shabiby na Abc, Mgahawa wa Cape Town na kituo kimoja cha mafuta kilichokuwa karibu na ofisi za Shabiby.

Kuhusu stendi ya mabasi, amesema wamekubaliana na uongozi wa mkoa na manispaa kuwapa muda wa kuondoa stendi mbili za mabasi yaendayo mkoani na ya daladala ya Jamatini.

“Wamesema kuondoa stendi sasa italeta shida kwa hiyo kuna makubaliano ambayo tumekubaliana na Mkuu wa Mkoa (Dk Binilith Mahenge) wa kutoa muda wa wao kuzihamisha,”alisema.

Hata hivyo, alisema makubaliano yao si kwamba stendi hizo zinabaki bila kubomolewa bali ni kwa muda na ukiisha wawe wamepata eneo la kupeleka huduma hizo ili eneo libaki tupu likabidhiwe kwa mkandarasi.

Alisema wamemaliza kazi hiyo kwa Dodoma mjini isipokuwa maeneo ya kanisa, misikiti, makaburi na ambayo mahakama imezuia ikiwemo kituo cha mafuta kilichomo mkabala na stendi ya daladala ya Jamatini.

Moshi  amesema  wamebomoa nyumba kamili 128 na  vibanda 487 ambazo waliziwekea alama lakini wapo wengine walioamua kujiondoa wenyewe.

Amesema kuwa walishasaini mkataba na mkandarasi Novemba 29 mwaka huu  na kwamba kabla ya kumkabidhi mkandarasi eneo hilo ni lazima wahakikishe kuwa njia ya reli ziwe safi.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, John Banda alisema kuwa makubaliano na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge yaliyofanyika Ijumaa hayakutekelezwa baada ya kufika katika eneo hilo Jumamosi akiwataka wafanyabiashara hao kuondoka.

Awali wafanyabiashara hao waliomba kupewa muda wa kuhama na kuonyesha eneo jingine la kufanyia biashara baada ya kuondolewa katika eneo hilo.

“Jumamosi Mkuu wa mkoa alifika katika eneo hilo kuwapelekea wafanyabiashara majibu aliyoyapata baada ya kukutana na kamati yake ya ulinzi na usalama. Aliwaambia watu wa Jamatini ni vyema kila mmoja aondoe kibanda chake yeye mwenyewe,” amesema.

Amesema kuwa amekwenda kule (kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa) amepata elimu. Amekuja kuwaletea majibu ya kamati ya ulinzi na usalama kuwa ni vizuri kubomoa wenyewe kabla ya kusubiri kuondolewa.

Amesema kuwa eneo walilopelekwa la Makole lilopo nyuma ya mahakama halina biashara kwa sababu wateja wao wakuu walikuwa wakiwategemea ni abiria wanaotumia stendi hizo.

“Eneo hilo (Makole) lina vumbi sawa lina miundombinu ya vyoo na nini. Lakini kikubwa kule hakuna biashara kwa sababu wateja wetu ni abiria,” amesema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images