Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

JWTZ yapewa jukumu jipya nchini Kongo la kuwasambaratisha waasi wengine wa ADF-Nalu

0
0
VIKOSI vya Tanzania vinavyolinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa (Monusco), vimepewa jukumu jipya la kuwasambaratisha waasi wa kundi la Allied Democratic Forces-NALU (ADF-Nalu). Hatua hiyo inakuja baada ya vikosi vya Tanzania vilivyopo nchini humo, kufanikiwa kuwasambaratisha waasi wa kundi la M23 mwishoni mwa mwaka jana. Waasi wa

Sad News: Basi la Zuberi lapinduka na kuua wanne papo hapo...Chanzo cha ajali ni bibi kizee aliyekuwa akikatisha barabarani

0
0
  Hii  ni  picha  ya  maktaba ( si ya tukio la leo ) ** BASI la Zuberi lenye namba T119 AA2 limepata ajali mbaya katika kijiji cha Nkuhi wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na watu wanne wameripotiwa kufa papo hapo kwa kukatwa vichwa huku majeruhi wengi wakiwa wameumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili.   Akizungumza kutoka eneo la tukio leo mchana huu, mwandishi wa habari, Nathanieli

Ajira: Utaratibu wa kujiunga na jeshi la polisi kwa wahitimu watarajiwa wa kidato cha sita 2014

0
0
  Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013. Ili kutekeleza azma hii tumeweka fomu kwenye tovuti ambayo wahitimu watarajiwa wa kidato cha sita wa mwaka 2014 watajaza kabla ya kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita.  Baada ya kujazwa kikamilifu wakabidhi fomu kwa wakuu wa shule ambao

Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba azungumza na TRA na kutoa msimamo wa serikali kuhusu matumiza ya mashine za EFD

0
0
  Na Habari Kwanza Blog — Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba hii leo asubuhi (Tar. 05/02/2014) amekutana na Watendaji/Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hazina Ndogo na Wahakiki Mali za Serikali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kufahamiana nao, pia kuzungumza nao kuhusu uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato nchini, msimamo wa Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD kwenye

Taarifa ya Wizara ya fedha kukanusha malipo ya milioni 160 kwa wabunge wanapostaafu

0
0
TANGAZO KWA UMMA Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti yamekuwa yakitoa taarifa za upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa Waheshimiwa Wabunge. Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha amethibitisha ongezeko hili. Taarifa hizo ziliendelea kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi 160 milioni kila mmoja.

Taarifa ya kukatika kwa mawasiliano ya mtandao wa Vodacom- Tanzania

0
0
Dar es Salaam, 5 Februari, 2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari  5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na  nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.   Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha

Mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Ernest Mangu afanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi nchini...Bofya hapa ujionee

0
0
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi. Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na: 1. Aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi

Mbunge wa CHADEMA, Diwani wake na wanachama 14 wafikishwa mahakamani kwa kufanya vurugu wakati wa kampeni za udiwani

0
0
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.    Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Zitto Kabwe aibuka na DVD

0
0
WAKATI Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akijipanga kuanza ziara katika mikoa kadhaa nchini kujibu mapigo ya tuhuma dhidi yake zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ziara ya Operesheni M4C Pamoja Daima, mbunge huyo ameibuka na DVD inayowananga viongozi wa CHADEMA.   Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa DVD hizo zitasambazwa

Polisi 8 watuhumiwa kumtesa mahabusu mwanamke kwa kumvua nguo na kumwingizia chupa ya bia katika sehemu za siri.

0
0
ASKARI Polisi saba wa kiume na mmoja wa kike, wanakabiliwa na tuhuma za kumtesa mahabusu mwanamke kwa kumvua nguo na kumwingizia chupa ya bia katika sehemu za siri.   Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi wa mjini Sumbawanga, Rosalia Mugissa, mshitakiwa katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Clara God (32), alidai kufanyiwa unyama huo na askari wa kiume mbele ya askari mwanamke.  

Mbunge wa Arusha Mjini Chadema, Godbless Lema akamatwa na jeshi la Polisi na kisha kuachiwa baada ya mahojiano ya masaa kadhaa

0
0
Mbunge wa Arusha Mjini Chadema, Godbless Lema amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Arusha na kisha  kuachiwa  baada  ya  mahojiano  ya  masaa  kadhaa.... Lema  alikamatwa  ili   kuhojiwa kuhusu malalamiko ya vurugu zilizotokea kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi wa kiti cha udiwani Kata ya Sombetini wiki iliyopita ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. <!-- adsense -->

Habari kamili kuhusu vurugu kubwa za wakulima zilizotokea eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro na kusababisha barabara kufungwa

0
0
MABOMU ya machozi yalitumika   leo  mchana  kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.   Wakulima hao walikuwa wakidai kuwa wenzao watano jana walivamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi

MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa afikishwa mahakani kwa kosa la kujeruhi

0
0
  Na Francis Godwin, Iringa MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48) leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa akituhumiwa kwa kosa la kujeruhi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alisema Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo

Rais Kikwete afungua mkutano wa baraza la vyama vya siasa jijini Dar leo

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa rasimu ya katiba kwa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014

Mtuhumiwa amuua askari polisi kwa kumpiga jiwe

0
0
Askari polisi F. 5264 PC Sabato (37) wa Kituo cha Polisi cha Longido, wilayani Monduli, ameuawa kwa kupigwa jiwe na mtuhumiwa aliyekuwa akimpeleka mahabusu katika Gereza la Kisongo.    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema mauaji hayo yamefanywa na mtuhumiwa aliyekuwa akipelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya kuvunja na kuiba.  

Kitale wa bongo movie amkata mapanga adui yake na kutenganisha kichwa na kiwiliwili...

0
0
Maigizo mengi sana nchini huwa yanalalamikiwa kukosa uhalisia wa tukio,hebu tumia dakika zako chache kuangalia namna picha hizi zilivyochanganywa ambazo zinamuonyesha Kitale kama kamkata kichwa huyo jamaa.   Kwa haraka haraka unaweza kudhani kweli lakini bado  jina la movie hii  halijajulikana  ingawa kwa kisehemu hiki kinaonyesha kama ni movie inayoongea na vitendo zaidi,lakini

Mwanamke adondoka ghafla jijini Mwanza akiwa njiani kuelekea kwa mganga wa jadi.... Afariki dunia masaa machache baada ya kupelekwa hospitali

0
0
  Baadhi ya  vitu  alivyokuwa  navyo  Sharon: Mwanamke  mmoja  aliyefahamika  kwa  jina  la  Sharon Justice Laiza, mkazi wa  Kilimahewa  jijini  Mwanza amefariki dunia  katika  mazingira  ya  kutatanisha   baada  ya  kudondoka  ghafla  akiwa  njiani  kueleakea  kwa  mgonga  wake  aishiye  Kiseke, Ilemela  Mwanza... Kwa  mujibu  wa    mashuhuda  wa  tukio  hilo  lililotokea  juzi  saa  kumi 

Baada ya Malawi kutangaza kuwa baadhi ya vijiji vya Tanzania ni mali ya Malawi, JWTZ yakerwa, yadai haitaogopa vitisho vyovyote

0
0
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema haliogopi vitisho vya aina yoyote vinavyotolewa na Serikali ya Malawi kutokana na mgogoro uliopo. Hatua hiyo imetokana na viongozi waandamizi wa Serikali ya Malawi, kutangaza baadhi ya vijiji vya Tanzania vilivyopo kilomita 10 kutoka mpakani mwa Ziwa Nyasa kuwa ni mali yao. Hatua ya JWTZ imekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete

Bunge la Katiba kuanza Februari 18, Rais Kikwete kutangaza majina leo

0
0
Rais Jakaya Kikwete jana alitangaza rasmi kuwa Bunge la Katiba litaanza  Februari 18, mwaka huu. Aidha, alisema kuwa atatangaza majina ya wajumbe wa Bunge hilo leo. Akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam jana, Rais Jakaya Kikwete alisema maandalizi kwa ajili ya Bunge hilo yanaendelea vizuri na kilichobaki ni marekebisho madogo madogo.

Mwanaume afumaniwa na mke wa mtu wakifanya uchafu ndani ya gari bovu

0
0
Arobaini (40) za mke wa mtu zimetimia baada ya kunaswa ndani ya gari akifanya uzinifu na kijana mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ aliyejitambulisha kwa jina la Athumani (26) maeneo ya Bamaga Mwenge, jijini Dar.  Tukio hilo lilitokea usiku wa manane Februari 4, baada ya mke  huyo aliyetambulika kwa  jina moja la Husna na sharobaro wake kujiingiza kwenye mtego na kunasa wazimawazima. Mara
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images