Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

BOT yatolea ufafanuzi taarifa ya kufungwa kwa benki ya Amana


Serikali Ya Burundi Yanuia Kuwarejesha Wananchi Wake Waliokimbilia Tanzania

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Burundi imesema ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi waliopo nchini Tanzania wanarejea nchini Burundi kwa haraka ili wakaijenge nchi yao.

Haya yamezungumza na Waziri wa mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Pascal Barandagiye, alipozuru katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli kutoa ujumbe wa kuwaasa kurejea wakimbizi nchini kwao Burundi.

Tangu zoezi la urejeaji wa wakimbizi lilipoanza mwezi septemba 2017 kwa awamu ya kwanza jumla ya wakimbizi 8347 wameshasaidiwa kurejea nchini kwao Burundi sawa na asilimia 100.3 ya lengo ya urejeshwaji kwa awamu ya kwanza.

Aidha, mwanzoni mwa mwezi Novemba wakimbizi wapatao 33,948 walijiandikisha kurejea nchini kwao Burundi lakini kutokana na kasi ndogo na taratibu ndefu zinazofanywa na Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR wakimbizi waliojiandikisha wameanza kusitisha nia yao ya kurejea kwani hawaoni jitihada zinazofanywa kuwarudisha, ambapo jumla ya wakimbizi 735 kati ya 33948 wamesitisha nia yao ya kureja kwa hiari.

Hali hii inatajwa na viongozi wa Burundi kuwa inachelewesha zoezi kwani wakimbizi wanaorejeshwa kwa mujibu wa mpango wa urejeaji ni ndogo. Mhe. Pascal Barandagiye amesema serikali ya yake ipo tayari kutoa magari kwaajili ya kuwasafirishwa wakimbizi kurudi nchi mwao, pamoja na kuwapa huduma muhimu za kibinadamu.

 “zoezi la urejeshaji wa Wakimbizi kwa hiari linaenda polepole mno tofauti na matarajio, shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linaenda kwa kasi ndogo tofauti na ilivyotarajiwa, hivyo kutokana na zoezi hilonkuenda taratibu Serikali ya Burundi ipo tayari kutoa magari, fedha na huduma nyingine za kibinadamu ili kusaidia kuweza kuharakisha zoezi la kurejesha wakimbizi waliojiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi” alisisitiza Barandagiye.

Akiongea katika nyakati tofauti tofuti katika kambi za nyarugusu, nduta na mtendeli, amewahakikishia wananchi wa  kuwa Amani nchini mwao ipo ya kutosha hakuna vurugu na serikali ya Burundi inawahitaji ili warejee kuenga taifa lao hakuna haja ya kuendelea kubaki makambini.

Wakimbizi wakiongea kwa nyakati tofauti wamemhakikishia kuwa bado wanapenda nchi yao Burundi, na wanatamani kurejea Burundi, lakini changamoto inayowakabili hadi kukata tamaa ya kurudi ni taratibu ndefu zinazowachelewesha kurejeshwa mara tu baada ya kujiandikisha

 Akiongea kwa niaba ya Wakimbizi walioko kambi ya Nduta Bw. Suleima Hamisi (65) ambaye amekuwa Mkimbizi mara Sita kwa nyakati tofauti tangu mwaka 1972 alisema “ Sisi tulishajiandikisha Zaidi ya miezi mine sasa ili tuweze kurejeshwa cha kushangaza hadi sasa badotupo makambi”  ameiomba serikali ya Burundi na Tanzania na Shirika la kuhudumia wakimbizi wakae na kuzungumza kwa pamoja juu ya mustakabali wa kuwarejesha haraka wenye nia ya kurudi Burundi.

Akitoa taarifa kwa Waziri wa mambo ya ndani na mafunzo ya uzalendo wa Burundi na Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania, Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu ikiyopo Wilayani Kasulu alisema kumekuwa na mwitikio Mkubwa wa wakimbizi wanao jiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi lakini changamoto imekuwa taratibu ndefu zinazochelewesha kurejea kwao zinawafanya baadhi yao kuahirisha kurejea kutokana na kusubiri kwa muda murefu.

Serikali ya Burundi pia imedai Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR linatakiwa kubadilisha utaratibu wa kuwapatia au kuwagawia vyakula na pesa wakimbizi wanapokuwa wanarejea wameomba zoezi hilo lifanyike wakati tayari wakimbizi wakishapatiwa nyumba na maeneo yao ya makazi kuepusha kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo vya kuwapokelea.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali ya Tanzania itahakikisha wakimbizi waliopo nchi wanahifadhiwa kwa mujibu wa makubaliano ya taratibu za kimataifa na wale wanaopenda kurejea kwa hiari itashirikiana na UNHCR,  nchi ya Burundi ili kufanikisha zoezi hilo. Hatua ya kuwarejesha wakimbizi katika nchi yao ya asili ni moja kati ya suluhisho la kudumu la ukimbizi kwa mujibu wa sharia ya kimataifa ya wakimbizi ya mwaka 1951 na Sheria ya Wakimbizi ya Tanzania yam waka 1998 kifungu Na. 3

Zoezi la kurejea kwa wakimbizi nchini mwao waliopo Tanzania lilianza kuratibiwa mara tu baada ya tamko la viongozi rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza walipo kutana Mwezi Julai 20, 2017 na kutamka kuwa wakimbizi waliopo Katika Makambi nchi Tanzania warejee nchini kwao kwani Burundi kuna amani ya kutosha.

Hadi sasa idadi ya wakimbizi walioko katika Mkoa wa Kigoma ni 210,005 na waomba hifadhi 26,410, kati ya hao 95,243 wapo kambi ya Nduta, 48147 kambi ya Mtendeli na 66615 Nyarugusu, aidha waombahifadhi wote wapo katika kambi ya nduta.

Kuondolewa VAT Kwenye Vifaa Vya Ujenzi Kutapunguza Mapato ya Serikali

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Serikali imesema kuondolewa kwa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifaa vya ujenzi kwa lengo la kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za makazi kutawanufaisha wafanyabiashara wachache kuliko wananchi wa kawaida na kupunguza  mapato ya Serikali.

Hayo yamesemwa Bungeni jana Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.  Godbless Lema juu ya Serikali kuondoa VAT kwenye vifaa vya ujenzi.

“Matumizi ya vifaa vya ujenzi ni mtambuka, ni vigumu kutambua kama mnunuzi atatumia kwa ujenzi wa makazi binafsi, biashara au miundombinu kama barabara” alisema Dkt. Kijaji.

Aidha, Dkt. Kijaji aliongeza kuwa lengo la kutoza kodi ni kuiwezesha Serikali kuwa na mapato ya kutosha ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa huduma muhimu za kijamii kwa Wananchi wake.

“Uhai wa Taifa lolote ni kodi hakuna maendeleo yanayopatikana katika Taifa lolote bila kodi hivyo makusanyo ya kodi ndio yanasababisha Serikali kuweza kutoa huduma nyingi  bure kwa wananchi wake”.  Alifafanua Dkt. Kijaji.

Hata hivyo Dkt. Kijaji alisema kuwa nyumba zinazojengwa na kuuzwa na Shirika la Nyumba la Taifa ni mradi wa kibiashara na si huduma, pia wauzaji wa nyumba hapa nchini ni wengi  hivyo kuondoa kodi ya VAT kwenye nyumba zinazouzwa na Shirika la Nyumba la Taifa peke yake utakua ni ubaguzi kwa wauzaji wengine wa nyumba ikiwa na kuikosesha Serikali mapato kwa manufaa ya Taifa

Taarifa Ya Spika Wakati Wa Kuahirisha Bunge

Serikali Yatoa Mafunzo Kwa Vijana Zaidi Ya 11,000

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweza kutoa mafunzo kwa vijana 11,492 katika fani mbalimbali kupitia vyuo vya umma, binafsi na makampuni ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi.

Amesema programu hiyo ambayo ilianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2016/17, inalenga kuweka maeneo mahususi ya kuwezesha vijana wawe na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri katika soko la ajira la ndani na la nje ya nchi.

Ametoa kauli hiyo jana mchana (Ijumaa, Novemba 17, 2017) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Januari 30, mwakani.

Alisema katika kutekeleza programu hiyo, Serikali imejikita katika maeneo ya kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi (apprenticeship); kutoa mafunzo ya ujuzi na uzoefu kazini (internship) kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo hususan wale wa vyuo vikuu; kutoa mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo; na kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini.

Waziri Mkuu alisema katika kujenga ujuzi wa vijana kushiriki kwenye shughuli za kilimo, Serikali imeandaa mafunzo maalum ambayo yataanza rasmi Desemba, 2017 katika Halmashauri zote zilizowasilisha maombi.

“Tumeshirikisha Wakuu wa Mikoa yote na kuwaelekeza waandae maeneo ya kujifunzia vijana hao kwenye Halmashauri zote za mikoa yao,” alisema.

Alisema ofisi yake imepokea maombi ya kushiriki kutekeleza programu ya kukuza ujuzi katika eneo la kilimo kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House) kutoka mikoa mitano ya Kagera, Manyara, Ruvuma, Kilimanjaro na Shinyanga. “Ofisi yangu imefika katika Halmashauri zote za mikoa hii ili kujiridhisha kuwa imetenga maeneo kwa ajili ya kujenga vitalu vyumba vya kufundishia,” ameongeza.

Alisema katika mwaka huu wa fedha (2017/18), Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imetoa fursa za mafunzo mbalimbali ya vitendo kupitia Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kukubaliana kuwa ifikapo Desemba, 2017 vijana wote wawe wamepatiwa fursa za mafunzo katika maeneo ya kazi.

Waziri Mkuu alitoa wito kwa viwanda na taasisi mbalimbali zishirikiane na Serikali kuwapa nafasi kwa vijana ili wajifunze kwa vitendo katika maeneo ya kazi  na kupata uzoefu  na ujuzi stahiki.

“Tuna vijana wengi waliomaliza vyuo vikuu walioomba kushiriki mafunzo ya vitendo na kupata uzoefu wa kazi. Natoa wito kwa waajiri watoe nafasi kwa vijana wetu hawa kujifunza kwa vitendo. Serikali itaendelea kugharamia mahitaji ya msingi ya vijana hawa wakati wa mafunzo hayo,” alisisitiza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Serikali Yakarabati Vyuo 10 Kwa Sh. Bilioni 12

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 11.9 kufanya ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na mabweni katika vyuo 10 vya ualimu nchini.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Morogoro, Mpwapwa, Butimba, Kasulu, Songea, Tukuyu, Marangu, Kleruu, Korogwe na Tabora. 

“Ukarabati huu umewezesha wanachuo 5,920 waliokuwa wanasoma Stashahada maalum ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuhamishiwa katika vyuo hivyo,” aliongeza.

Ametoa kauli hiyo jana mchana (Ijumaa, Novemba 17, 2017) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Januari 30, mwakani.

Alisema ili kuongeza fursa za wanafunzi kusomea ualimu, Serikali imepanga kujenga na kukarabati vyuo vya ualimu vya Kitangali, Ndala, Mpuguso na Shinyanga kwa thamani ya sh. bilioni 36.47.

Alisema mradi huo ambao utatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2016/2017 – 2018/2019, unalenga kuongeza fursa kwa wanafunzi wenye sifa kupata nafasi ya kujiunga na elimu ya ualimu.

“Ujenzi na ukarabati huu utasaidia kuongeza udahili katika vyuo vya ualimu vya Serikali kutoka wanachuo 20,535 katika mwaka 2017 hadi kufikia wanachuo 23,835 katika mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la wanachuo 3,300,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanza maandalizi ya awamu ya pili ya ukarabati wa vyuo saba vya ualimu vya Serikali. Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Tandala, Nachingwea, Tarime, Kinampanda, Mandaka, Patandi na Ilonga.

Alisema vyuo vya ualimu vya Murutunguru, Kabanga na Mhonda vitalazimika kujengwa upya baada ya wahandisi kubaini kuwa vyuo hivyo havifai kukarabatiwa kutokana na uchakavu mkubwa wa majengo yake.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema ili kukabiliana na upungufu wa wahadhiri kwenye vyuo vya elimu ya juu, katika mwaka 2017/18, Serikali imepanga kusomesha wahadhiri 100 katika ngazi za shahada za umahiri na uzamivu.

Waziri Mkuu alisema kati ya mwaka 2016/17 na 2017/18, Serikali imeratibu upatikanaji wa wanafunzi wa Kitanzania wanaofadhiliwa kusoma nchi za nje ambapo China wapo wanafunzi 86, Uingereza (17), Misri (4), Korea (3), Urusi (13) na Thailand (2) huku baadhi ya wanufaika wakiwa ni wahadhiri wa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu nchini.

Vilevile, kupitia kuimarika kwa mahusiano yetu ya kidiplomasia, Waziri Mkuu amesema, Septemba, mwaka huu, Serikali ilitia saini makubaliano na nchi ya Hungary ambapo itakuwa inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanza mwaka 2018/2019.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.

Majaliwa:Mwenendo Wa Ukuaji Uchumi Wa Taifa Unaridhisha

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Taifa unaridhisha, ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 5.7.

Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Novemba 17, 2017) wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Bunge, mjini Dodoma.

“Mwenendo wa uchumi wetu ni wa kuridhisha, mfano, ukuaji wa uchumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 5.7, robo ya pili ilikuwa asilimia 7.8 na nusu ya kwanza ya mwaka huu ilikuwa ni asilimia 6.8.”

Alisema hali hiyo inafuatia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi na usimamizi thabiti wa matumizi ya Serikali, ambapo nakisi ya bajeti ya Serikali imeshuka na kufikia asilimia 1.9 kwa mwaka 2016/2017

Pia alisema akiba ya fedha za kigeni inatosheleza kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa zaidi ya kipindi cha miezi mitano, ikiwa ni zaidi ya lengo la miezi minne.

Akizungumzia kuhusu kasi ya upandaji bei, Waziri Mkuu alisema takwimu zinaonyesha kwamba katika nusu ya mwaka 2017, mfumuko wa bei uliendelea kubaki katika kiwango cha tarakimu moja.

“Takwimu zinaonyesha kwamba mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Oktoba 2017 ulikuwa ni asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilima 5.3 mwezi Septemba, 2017.”

Alisema kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa bei wa bidhaa za vyakula, ambavyo vimepungua kutoka wastani wa asilimia 9.3 mwezi Septemba, 2017 hadi asilimia 8.8 mwezi Oktoba, 2017.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii ianzishe Mamlaka ya Fukwe za Bahari na Maziwa ili kutangaza na kuendeleza fukwe ambazo hazina shughuli.

Alisema fukwe za bahari ni eneo mojawapo ambalo likiendelezwa vizuri, linaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi, hivyo ni lazima zipewe kipaumbele.

Pia ametoa wito kwa wizara hiyo iongeze kasi ya kuleta mabadiliko katika sekta nzima ya maliasili ili iweze kuchangia zaidi kwenye uchumi.

Ametolea mfano Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 60.1 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi bilioni 102 mwaka 2016/2017.

Waziri Mkuu amesema ongezeko hilo la mapato limekuja baada ya Serikali kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kielektroniki.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Canada Aijibu Serikali ya Tanzania Sakata la Bombardier Kuzuiliwa Nchini Humo

$
0
0
Wakati katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akiwa nchini Canada kushughulikia suala la ndege ya Bombardier, waziri mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau amesema hawezi kuingilia uhuru wa mahakama ambayo anaamini itatenda haki.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alisema amemwandikia barua waziri huyo mkuu wa Canada ili kujua hatima ya ndege hiyo.

Hata hivyo naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alisema jana kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu waziri mkuu yupo na wao hawajapata taarifa rasmi.

“Lakini kingine naomba utambue kuwa katibu mkuu bado yupo Canada, kwa hiyo mambo mengi mimi sijayapata hadi atakaporudi aje kutu-breaf kilichojiri huko,” alisema Nditiye.

Akizindua uwanja wa ndege mjini Bukoba, Novemba 6, Rais Magufuli alisema amemwandikia barua waziri mkuu wa Canada kumuomba kuachiwa kwa ndege hiyo na amemtuma mwanasheria mkuu wa Serikali, George Masaju kwenda nchini humo kushughulikia suala hilo.

Kwenye barua yake ya majibu ambayo yameripotiwa na gazeti la National Post la nchini humo, waziri mkuu wa Canada Trudeau amesema hana cha kufanya kwa kuwa shauri hilo lipo mahakamani.

“Ni bahati mbaya kwamba suala hili limechelewesha kuwasili kwa ndege hii. Serikali ya Canada haina uwezo wa kuingilia, ila tuna imani mahakama itaamua kwa weledi na haki,” amekaririwa akisema Trudeau katika gazeti hilo.

Ndege hiyo, Bombardier Q400-8 inashikiliwa kwa amri ya mahakama nchini humo kutokana na shauri lililopo kati ya Serikali na kampuni ya Stirling Civil Engineering.

Kampuni hiyo ilikuwa na mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo ambao ulivunjika kabla haujakamilika, hivyo ikaamua kukimbilia kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ambako ilishinda kesi. Baada ya kushinda kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada.

Kwa miezi mitatu sasa, mahakama nchini Canada inaendelea kuishikilia ndege hiyo iliyonunuliwa kwa Dola 32 milioni za Marekani (zaidi ya Sh70.4 bilioni) kwa niaba ya kampuni ya Stirling inayoidai Serikali Dola 28 milioni (zaidi ya Sh61.6 bilioni) ambazo ni thamani ya mkataba uliovunjwa pamoja na riba.

Ndege hiyo ni miongoni mwa zile ambazo Rais Magufuli aliahidi kununua ikiwa ni mikakati ya kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Awali, ndege hiyo litarajiwa kuwasili nchini mwezi Julai, lakini hilo halikufanyika na Agosti 18, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema ndege hiyo imekamatwa nchini Canada na inaweza kupigwa mnada kutokana na deni ambalo Serikali inadaiwa na kampuni hiyo yenye makao yake Montreal, Canada.

Agosti 19, Serikali ilifanya mkutano na wanahabari kukanusha taarifa hizo, lakini ilikiri kuwapo mgogoro na kampuni hiyo.

Aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Zamaradi Kawawa alisema mgogoro kuhusu ndege hiyo upo na kimsingi umetengenezwa na Watanzania ambao kwa bahati mbaya wameweka masilahi ya kisiasa na ya binafsi mbele zaidi ya masilahi ya Taifa.

Alisema Serikali ilikuwa imeanza majadiliano ya kidiplomasia kwa ajili ya kulimaliza suala hilo. Kwa sasa, ATCL inamiliki ndege mbili mpya aina ya bombardier zilizoingia nchini Septemba 2016, na imeagiza ndege nyingine tatu za aina hiyo na Boeing Dreamliner moja.

Akizungumzia mafanikio ya miaka miwili ya Rais John Magufuli hivi karibuni msemaji mkuu wa Serikali, Hassan Abbasi alisema mpaka Juni mwakani ndege zote zitakuwa zimewasili nchini.

Mbowe Awataka Viongozi wa Dini Wasione Aibu Kuikosoa Serikali

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa dini kupaza sauti kukemea maovu ili kuiokoa nchi katika kilio.

Mbowe  alisema hayo jana wakati wa ibada ya kumuaga marehemu mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Hai, Looka Mushi iliyofanyika katika Usharika wa Nkwarungo.

“Dunia yetu imejaa uovu, sisi ambao tuko kwenye siasa tunatambua nguvu ya viongozi wa kiroho, kauli yao moja kukemea uovu inatingisha nchi nzima,” alisema Mbowe. “Semeni tunatambua tangu enzi mmekuwa mkikemea maovu na ‘kui-shape’ nchi, msione aibu kuwakemea viongozi waovu.

“Viongozi wa dini msiingize roho ya uoga, mtaiponya nchi, mkikaa kimya nchi itakufa, nchi inateketea, nchi inaangamia viongozi msikae kimya watu wanauawa.

“Itafika kipindi kwa kiburi cha madaraka wataamrisha baba askofu alale rumande kwa mfano, Mungu akunusuru sana Baba Askofu Dk Frederick Shoo atakapoambiwa alale ndani ndiyo utakuwa ukombozi wa Taifa letu Bwana Yesu asifiwe,” alisema Mbowe.

Kwa upande wake, Askofu Shoo alisema viongozi wa dini waache unafiki na waige mwenendo wa Mchungaji Mushi.

“Watumishi wengi ni wanafiki, hivyo waache unafiki na kuwa na rangi mbilimbili muige mwenendo wa mchungaji Mushi,” alisema Dk Shoo.

Askofu mstaafu Erasto Kweka alisema matendo mema yaliyotangauliza neno la Mungu ndiyo silaha ya kweli ya kila binadamu.

Alisema jambo muhimu ni kuishi kwa kuangalia waliofanikiwa katika imani walifanya nini.

“Leo tunamuaga mpendwa wetu, anayesifiwa na kila mmoja kutokana na kutukuka kwa matendo yake mema, tutafakari na kutenda kwa kumpendeza Mungu kama alivyofanya Mchungaji Mushi,” alisema Kweka.

Muhubiri katika ibada hiyo, Mchungaji Lewis Hiza alisema watu wanashangaa kwa nini alikuwa na urafiki na Mchungaji Mushi.

“Jibu ni kuwa wazee wanaozeeka vizuri, huwa na urafiki na vijana ili kuwaachia yaliyo mema na neno alilokuwa akiniambia kila siku nishike neno kwa sababu litaniweka pazuri na litakuwa majibu ya kila swali,” alisema Hiza.

Akisoma wasifu wa marehemu, katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Arthur Shoo alisema Mchungaji Mushi alipata tatizo la mapafu mwaka 2008 na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali.

Alisema mwaka 2014 aliugua na kufanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe tumboni katika Hospitali ya Manipal Bangalore nchini India.

“Pia mwaka huohuo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume. Mwaka 2015 alirudi tena India kwa uchunguzi, alionekana anaendelea vizuri japokuwa aliendelea kusumbuliwa na tatizo la mapafu ambalo mzizi wa tatizo ulianza kwenye ugonjwa wa pafu mpaka alipofariki Ijumaa iliyopita,”alisema Shoo.

Story Ya Sorry Madam Sasa Inarudi Hewani Kupitia Ubuyu Blog

$
0
0
Nipende kutanguliza samahani kwa wafwatiliaji wa hadithi zangu kupitia hapa mpekuzi pamoja na blog ya Ubuyu. Kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu, hadithi ya SORRY MADAM D.F.E ilisimama. Baada ya kutatua tatizo sasa hadithi hiyo itaendelea kama kawaida wiki hii.

Pia nina wakaribisha wasomaji wangu kuniunga mkono kwa kununua vitabu katika mtandao(online) kwa kupitia whatsapp namba zangu 0657072588 au 0768516188 au email eddazariaM@gmail.com. Vitabu ambavyo vipo kwenye mauzo leo ni SEX DEALERS na HARD DAY vyote utavipata kwa sh 5000 TU(Vyote kwa pamoja)  Pia muendelezo wa SORRY MADAM season THREE(President Wife) utaipa kwa sh 8000 tu. 
 
Huduma zetu ni za haraka na uaminifu sana. Kwani siku zote huwa nina amini kwamba mimi sio kitu mbele ya SHABIKI. Nipo kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wangu na pale kwenye maoni na ushauri ninaomba muweze kunishauri hata kwa kunipigia kwa simu yangu ya mkononi 0657072588 au 0768516188 Utazungumza nami moja kwa moja.

Tumefungua group la hadithi WHATSAPP, ambalo wasomaji wangu wote mutakuwa muna jisomea episode zaidi ya 48 kwa MWEZI na ada yatu ni sh 3000 tu, Wahi sasa kwani nafasi zikijaa hatuto pokea watu wengine zaidi. 
 
Utaweza kutupata kupitia Facebook kwa jina la @StoryZaEddy-tz Instergram @StoryZaEddy-tz na Twitter @Eddy_Msu
Ukisoma tangazo hili nina kuomba uweze kumjulisha na mwengine.

Waliombeza Dk. Shika ( Bilionea wa Nyumba za Lugumi) kuumbuka, adai mabilioni yake kutua Tanzania Hivi Karibuni

$
0
0
Bilionea wa nyumba za Lugumi aliyeteka vichwa vya habari siku za hivi karibuni, Dk. Louis Shika, amekamilisha malipo ya bima kwa ajili ya kutumiwa fedha zake kutoka nchini Urusi..

Dk. Shika aliingia matatani baada ya kushinda mnada wa uuzwaji wa nyumba za Said Lugumi hali iliyosababisha kukamatwa na polisi, lakini binafsi alisisitiza kuwa fedha hizo anazo na sasa anaelekea kuthibitisha hilo kwa kufanya mchakato wa kutumiwa fedha.

Waandishi wa habari walimkuta Dk. Shika akiwa katika huduma za mtandao wa internet katika shirika la Posta Jijini Dar es Salaam, ambao walikuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye na kujikuta hata mwenyewe akimshangaa bilionea huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutuma taarifa za miamala hiyo, Dk. Shika amesema ametuma kiasi cha dola 100 ambapo anatarajia muda si mrefu ataweza kutumiwa fedha zake na kwenda kulipia asilimia 25 ya fedha zinazotakiwa katika nyumba hizo.
Alipoulizwa kama fedha hizo zikichelewa na kukuta mchakato huo wa malipo umepita, amesema kwa kujiamini, atanunua nyingine kwani Dar es Salaam kuna nyumba nyingi zinazouzwa siyo lazima hizo za Lugumi.

Kiasi hicho cha fedha, amekilipa kwa kwa Benki ya Equity kwenda Benki ya Bankok nchini Thailand, mchakato utakaomwezesha kutumiwa fedha zake na kuweza kununua nyumba hizo.

Katika hatua nyingine Dk. Shika alisifia huduma za shirika hilo na kueleza kwamba ndiyo hutuma huduma za internet katika kutuma nyaraka zake mbalimbali ndani na nje ya nchi.

CCM Yatangaza Mabadiliko Ya Tarehe Ya Kikao Cha Halmashauri Kuu Ya Taifa NEC

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya tarehe ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuwa itakuwa ni Novemba 21, 2017 badala ya Novemba 22 na 23, 2017.

TANESCO yafanya Zoezi la Kusafisha na Kuunga Bomba la Gesi-KINYEREZI 1

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa  Jumamosi Novemba 18 na leo Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni, kama tulivyowatangazia.

Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme.

Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo.

Picha: Waziri Nchemba atunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) UDSM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba jana Novemba 18, 2017 ameweka historia nyingine katika maisha yake baada ya kuhitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Waziri Nchemba amehitimu masomo yake ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika uchumi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nchemba ameweka picha zake na kuandika, anamshukuru Mungu kwamba amehitimu masomo yake ya PhD.

Katika kuandika tasnifu (thesis) yake, Waziri Nchemba aliandika kuhusu “Sterilization of Foreign Exchange Inflows in Tanzania: Extent and Effectiveness.

Katika kuandika tasnifu hiyo, Waziri Nchemba alisimamiwa na wakufunzi, Dr. Jehovaness Aikaeli na Dr. Eliab Luvanda.

Waziri Nchemba amehitimu masomo jana baada ya kutunikiwa shahada hiyo katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City ambapo leo ni kundi la kwanza.

Kundi la pili linatarajiwa kufanya mahafali yao katika ukumbi huo huo, Novemba 21 mwaka huu.

Ndugai aunda kamati mbili kushughulikia sekta uvuvi na gesi

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameunda kamati mbili zitakazoshughulikia sekta ya Uvuvi na Gesi ili kuweza kujua ni kwa nini hazichangii pato la taifa.

Ndugai ameunda kamati hizo baada ya zingine mbili za kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi. umiliki na usimamizi wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilisha taarifa kwa Rais Dkt, John Magufuli na kusababisha baadhi ya mawaziri kujiuzulu.

Akitangaza kamati hizo bungeni mjini Dodoma, Ndugai alimrejesha Dotto Biteko aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyochunguza madini ya Tanzanite kuwa mwenyekiti wa kamati itakayochunguza sekta ya gesi.

Alisema kuwa hali ya kusuasua katika sekta hizo unahitaji kufanyiwa utafiti ili kuweza kuona ni namna gani zitaweza kuchangia pato la taifa.

Hata hivyo. Ndugai alimuagiza Katibu wa Bunge kuwawezesha wabunge hao ili waanze kazi mara moja na kamati hizo zimetakiwa kufanyakazi ndani ya siku 30 tangu zilipokabidhiwa majukumu.

Wazimbabwe waungana na wanajeshi kumtaka Mugabe aondoke madarakani

$
0
0
Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo la kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go.

Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.

Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.

Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka.

Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.

Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.

Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa uongozini hadi chama kitakapofanya mkutano wao mkuu mwezi ujao. 

Chadema wasema wako tayari kuuza figo kugharamia matibabu ya Tundu Lissu

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za  matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni  moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.

Akizungumza jana  Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema alisema utekelezaji wa  majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Alisema  pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa   kimedhihirika  kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" alisema Lema.

Alisema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.

Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa Lowassa

$
0
0
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi kumwezesha mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kupata nafasi ya kupita mjini Moshi.
 
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamefunga barabara.
 
Takriban mabomu manne ya kutoa machozi yalifyatuliwa saa 10:30 jana jioni ya  Jumamosi Novemba 18,2017  katika eneo la Soko la Manyema ambako Lowassa na msafara wake alikuwa apokewe ili kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani eneo la Pasua Relini.
 
Kabla ya Lowassa kufika, vijana madereva wa bodaboda walipita katika Barabara ya J.K. Nyerere.
 
Vijana hao walipopita mzunguko wa magari wa Coca Cola saa 10:15 jioni, gari la polisi aina ya Toyota Land Cruicer likiwa na polisi wenye mabomu ya machozi lilionekana likiwafuata.
 
Haikupita dakika 15, ndipo kulisikika milio ya mabomu katika eneo la Manyema ambalo ni njia panda ya kuelekea eneo la mkutano.
 
Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema ambaye yuko katika msafara wa Lowassa, alisema eneo la Manyema lilikuwa halipitiki kutokana umati wa watu.
 
Lema alisema ni kutokana na hali hiyo, ili kumwezesha Lowassa na msafara wake kupita, FFU walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mabomu hayo yamepigwa ili kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamefurika kwenye eneo hilo na kumuwezesha Lowassa kupita.
 
“Alikuwa hana njia ya kupita, watu walifurika kiasi kwamba hata Lowassa mwenyewe asingeweza kupita, tulifanya hivyo kuwapunguza na ameshapita ameenda zake kwenye mkutano,” alisema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Novemba 19

Mbowe kumnadi mgombea wa CHADEMA aliye mahabusu

$
0
0

Wakati Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe anatarajiwa kuwahutubia wakazi wa Kata ya Mhandu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani, mgombea wa chama hicho, Godfrey Misana yupo mahabusu kutokana na kukabiliwa na shtaka la kujeruhi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Boniphace Nkobe  amesema Mbowe ameambatana na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na aliyekuwa mbuge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na utafanyika saa kumi jioni.

Misana (46), mgombea udiwani wa Chadema katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017 na kampeni meneja wake, Charles Chinjibela (37) Ijumaa Novemba 17,2017 walipandishwa kizimbani wakidaiwa kumjeruhi meneja wa kampeni za CCM katika kata hiyo, Thomas Warioba.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, mbele ya hakimu Ainawe Moshi wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 14,2017.

Akisoma mashtaka katika shauri hilo namba 540/2017, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Elizaberth Barabara alidai washtakiwa walitumia visu na mawe kumjeruhi Warioba.

Upande wa Jamhuri uliomba Mahakama kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile ilichoeleza ni kwa usalama wao.

Ombi hilo la Jamhuri limepingwa na wakili wa utetezi, Gasper Mwanaliela.

Wakili Mwanaliela alisema dhamana ni haki ya wateja wake na kwamba, kuwanyima kutawazuia kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Moshi alisema Mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana Novemba 21,2017. Washtakiwa walipelekwa mahabusu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>