Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Spika Ndugai aigomea Serikali jina la Shirika la Wakala wa Meli wa Taifa

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai jana Alhamisi amegomea Serikali na kulazimika kuahirisha Bunge kwa muda wa saa moja ili warudi na kukubaliana kubadili jina la Shirika la Wakala wa Meli wa Taifa (NASAC)

Spika Ndugai alitoa agizo la kuahirisha Bunge baada ya mvutano wa Serikali na Kamati ya Bunge ya Miundombinu ambao walipendekeza kubadilishwa kwa jina hilo.

Mapema wakati Serikali ikijibu maoni ya wabunge kuhusu muswada huo, Spika alionyesha dhahiri kutokukubaliana na wazo la Serikali na badala yake akasimama katika mawazo ya kamati na wabunge wengine kuwa jina hilo halifai.

Mara baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kumaliza yake, Spika alihoji ni kwa nini asikubaliane na mapendekezo ya wabunge katika kubadili jina la muswada lakini mwanasheria huyo akatupia mpira kwa waziri kuwa angekwenda na majibu.

Hata hivyo, katika majumuisho ya michango ya wabunge, Waziri Profesa Makame Mbarawa alitoa sababu za kutobadilisha jina akisema halikuwa na maana yoyote na wala lililopendekezwa halikuwa na madhara kwani waliosema kuwa jina hilo ndilo lililofilisi hawakujua kuwa kulikuwa na usaliti.

“Mheshimiwa Spika, jina halina shida yoyote kwani hata lile la awali siyo kwamba lilipeleka madhara bali kilichotokea ni namna ambavyo baadhi ya watu waliokuwa ndani ya chombo hicho walikuwa ni wasaliti,” alisema Mbarawa

Baada ya hoja za waziri huyo Bunge lilikaa kama kamati na kuanza kuangalia vifungu hivyo ndipo Spika akampa nafasi mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Norman Sigala ambaye akasema Serikali ilikuwa imewadanganya.

“Nakushukuru mheshimiwa Spika, Serikali hapa ni kama imetudanganya maana kusema itaangalia huko mbeleni ni sawa na kutudanganya sisi, tulichokubaliana kwenye kamati sicho kilichowasilishwa bungeni,” alisema Profesa Sigala.

Spika alimpa nafasi Waziri ambaye aliendelea kuweka msimamo kuwa jina hilo liendelee kama lilivyowasilishwa na Serikali ili kama kutakuwa na marekebisho mbeleni Serikali itafanya hivyo.

Kauli ya waziri ilimuinua Spika ambaye alisema jina hilo linapeleka picha mbaya kwani haiwezekani Serikali kuunda chombo kipya kizuri lakini ikatumia jina ambalo lina maudhui mabovu.

“Hapa ndipo tunatunga sheria yenyewe, sasa kama mnaona kubadili jina kunaweza kuathiri kisheria niambie lakini kama hakuna, sioni kwa nini tuendelee kuvutana sana, naahirisha shughuli za Bunge kwa saa moja nendeni katika ukumbi wangu hapo mkutane na mjadiliane ili mkirudi hapa mniletee jina,” alisema Spika na kuahirisha Bunge

Wabunge walilipuka kwa makofi na makelele ya kumshangilia Spika huku wanasheria wakikutana kwa haraka ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi waliwaongoza wajumbe wa kamati na serikali haraka kuingia ukumbini kwa ajili ya kutafuta jina hilo.

Rais Mugabe azungumza na wajumbe wa SADC

$
0
0
Serikali ya Afrika Kusini imesema Rais Robert Mugabe amekutana na wajumbe kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( Sadc) katika juhudi za kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Alisafiri hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na jeshi.

Wanajeshi waliingilia kati na kutangaza kudhibiti serikali Jumatano katika kinachoonekana kuwa juhudi za kumzuia mke wa Mugabe, Grace, asitwae madaraka.

Duru zinadokeza kwamba Bw Mugabe anataka kusalia madarakani hadi wakati wa kufanyika kwa uchaguzi mwaka ujao.

Lakini mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya taifa.

Makamu wake wa zamani Joice Mujuru pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Mzozo wa Zimbabwe pia unajadiliwa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, nchini Botswana.

Mhasibu Mkuu wa TAKUKURU afikishwa Mahakamani

$
0
0
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Godfrey Gugai, amefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, na kusomewa mashtaka 44.

Baadhi ya mashtaka aliyosomewa Godfrey gugai, ni pamoja na kutakatisha fedha, kughushi fedha na kudanganya mali anazomiliki.

Siku mbili zilizopita Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Generali, John Julius Mbungo, alitangaza dau nono la shilingi 10 milioni kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Godfrey Gugai, ambaye hakuwa anajulikana alipo, lakini Novemba 15, alijisalimisha mwenyewe na kuhojiwa na taasisi hiyo.

TAKUKURU imemfikisha mahakamani, Gugai kwa tuhuma za kumiliki mali nyingi ambazo haziendani na kipato chake jambo ambalo ni kunyume cha sheria ya Utumishi wa Umma.

Mali zilizotajwa kumilikiwa na Gugai ni pamoja na viwanja zaidi ya 30, magari matano, nyumba 5 na piki piki moja ambavyo vitu hivyo viko maeneo mbalimbali hapa nchini.

Spika Ndugai awataka mawaziri kuacha Kupiga stori bungeni

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewaonya mawaziri kuacha kupiga stori wanapokuwa bungeni, badala yake wawe makini kusikiliza mijadala na maswali kutoka kwa wabunge.

Ndugai alitoa onyo hilo jana katika kipindi cha maswali na majibu baada ya kuwataja baadhi ya manaibu ili wajibu maswali lakini walishindwa kusimama kwa kuonyesha hawakusikiliza kilichokuwa kimeulizwa na wabunge.

“Waheshimiwa mawaziri acheni kupiga stori ndani ya Bunge, ndiyo maana mnashindwa kusikiliza kinachoendelea humu, hebu punguzeni na mjikite katika kusikiliza,” alisema Ndugai.

Kiongozi huyo alianza na naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ambaye alimtaka ajibu swali la nyongeza la Mwantumu Dau Haji (viti maalum - CCM) ambalo lililenga katika suala zima la upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Kabla ya swali hilo, tayari mbunge huyo alishauliza swali la msingi ambalo lilielekezwa ofisi ya Makamu wa Rais na lilijibiwa na naibu waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola likihusu masuala la mabadiliko ya tabia nchi.

Aweso alisimama asijue nini cha kujibu huku akiendelea kutazamana na Spika Ndugai kwa sekunde kadhaa ndipo akaamuliwa kuketi kwa kuwa alikuwa hajui swali gani liliulizwa.

“Tatizo lenu mawaziri hamsikilizi kinachoendelea ndani ya Bunge, mnapiga stori tu. Haya naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais okoa jahazi hilo,” alisema Ndugai.

Baada ya maswali kadhaa kupita aliwataka naibu mawaziri ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda na Joseph Kandege kujibu swali la nyongeza kuhusu umaliziaji wa majengo ambayo yanaanzishwa na wananchi.

“Haya naibu mawaziri Tamisemi, Josephat Kandege naomba ujibu swali hilo. Kama hujajipanga naomba mwenzako Joseph Kakunda ajibu, jamani ndiyo haya niliyosema wapo hapa tu lakini wanapiga stori na hawasikilizi kinachoendelea,” alisema spika.

Ndugai aliwaonya pia wabunge kutozungumza na waziri mkuu na kumtaka kiongozi huyo wa shughuli za Serikali kuzungusha macho ili kuona namna ambavyo wabunge walikuwa wamesimama na kutaka kuuliza maswali kuhusu maji.

“Mheshimiwa waziri mkuu, naomba hao wanaozungumza na wewe wakuache kwanza, hebu geuka nyuma na uangalie pande zote uone namna ambavyo wabunge wamesimama kutaka kuuliza maswali kuhusu maji majimboni kwao, Serikali iangalie jambo hili,” alisema.

Wakati huo spika aliitaka Serikali kutafakari namna ambavyo imekuwa ikitoa maagizo na amri kila wakati kupitia mabaraza ya madiwani akisema siyo afya na haijengi.

Alikuwa akitolea majibu mwongozo ulioulizwa na mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul kuhusu mpango wa Serikali kuagiza wananchi kuendelea kumalizia majengo ya zahanati, maabara na madarasa waliyoyaanzisha.

“Ndugu zangu Serikali, anachokisema mbunge ni sahihi maana sasa imekuwa ni kero kubwa, hebu angalieni jambo hilo kwani kila mahali ni maagizo maagizo na hata tukienda kwenye baraza la madiwani utasikia kuna ajenda ya kudumu ambayo ni maagizo, hii inakera jamani,” alisisiza Ndugai.

Pia, aliwataka viongozi kuangalia namna bora ya kufanya ili kufikisha ujumbe kuliko kuagiza kila mara ambako kunaondoa imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Hata hivyo, alisema kumekuwapo na tabia ya baadhi ya viongozi kujiona kama miungu watu na wanaamini kuagiza kila wakati kwa kutumia amri ndiyo itakuwa maendeleo wakati si kweli.

Tume ya uchaguzi yapokea taarifa kutoka kwa Spika Ndugai Kuhusu Jimbo la Lazaro Nyalandu na Lile la Onesmo Ole Nangole

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia, Lazaro Samwel Nyalandu kujivua Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.

Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo, Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.
 
Wakati huo huo Waziri wa Tamisemi kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
 
Hata hivyo, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.
 
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo
 
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
NA.MKOAHALMASHAURIJIMBO
1.SingidaHalmashauri ya Wilaya ya SingidaSingida Kaskazini
2.ArushaHalmashauri ya Wilaya ya LongidoLongido

Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
NA.MKOANA. HALMASHAURI NA. KATA
1.Kagera  1.Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.1Keza
2.Arusha   2Halmashauri ya Jiji la Arusha2Kimandolu
3.Pwani  3. Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.3Kurui
4.Tabora 4.Halmashauri ya Wilaya ya Tabora







Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne

$
0
0
Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne
 
Kutana Maajabu ya Mtabibu MAALIM MOHAMEDI MASUDI Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..
MAALIM MOHAMEDI MASUDI ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
 
Je unasumbulia na Mapenzi..?
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na MAALIM MOHAMEDI MASUDI Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
Wasiliana na MAALIM MOHAMEDI MASUDI Kwa Majibu ya Maswali yako..

Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA.

Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.
Wasiliana nae kwa namba
0655516982
0688856265
0621898709(Whatsapp)

Tanzania Kuwa Mnunuzi Mkuu Wa Dawa Na Vifaa Tiba Ukanda Wa SADC

$
0
0
Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC) kwa kauli moja wamepitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (Pooled Procurement Services (SPPS).

Uteuzi huo wa nchi ya Tanzania umepita bila kipingamizi mwishoni mwa wiki kwenye Mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC uliowakutanisha Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaohusika  na masuala ya UKIMWI uliofanyika mjini Polokwane, Limpopo – Afrika Kusini.

Hatua ya uteuzi wa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara umetokana na juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa MSD ambapo sasa inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa .

Aidha,umahiri na uzoefu wa Bohari ya Dawa (MSD) katika masuala ya ununuzi, utunzaji na usambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara (yaani mnyororo wa ugavi) unaeleweka na kuaminika vizuri hata na nchi nyingine zilizowahi kututembelea kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Kwa hatua hiyo MSD itakuwa na dhamana na majukumu yafuatayo:
  1.   Kununua Dawa na Vifaa Tiba kwa ajili ya nchi za SADC
  2.   Usimamizi wa taarifa na takwimu za Dawa na Vifaa Tiba vitakavyohitajika
  3.   Usimamizi wa kanzidata (Database) ya dawa za nchi wananchama wa SADC na usimamizi wa bei elekezi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara
  4.  Kusimamia manunuzi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Ukanda wa SADC na kusimamia mnyororo wa ugavi
  5.   Kutoa huduma za kitaalamu na kupanga bei elekezi na
  6.   Kutoa huduma za ushauri wa kitaalam katika masuala ya dawa na vifaa tiba.
Hatua hii itapunguza kwa kiasi kikubwa bei ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya nchi wananchama wa SADC. Jambo ambalo limeipatia heshima na sifa kubwa Tanzania, kwani imeaminiwa kufanya ununuzi wa dawa kwa niaba ya nchi nyingine kumi na tano (15) ambazo ni wanachama wa SADC.

Tanzania kupewa jukumu hilo ni jambo la kujivunia sana tena inaonyesha dhahiri tumetambulika tuko vizuri kwenye masuala mazima ya mnyororo wa ugavi kwa nchi wanachama wa SADC.

Faida zitakazopatikana kwa Tanzania kuwa Mwenyeji wa huduma hii ni kama zifuatazo:
  1. Heshima kwa nchi yetu kwa kuaminiwa na nchi wanachama wa SADC baada ya kukidhi vigezo vya kitaalam
  2.  Viwanda vyetu vya ndani vitaweza kuuza dawa zao kwa nchi za SADC, kwani wajumbe wa mkutano tumekubaliana kuwa na kituo kimoja kitakachoshughulikia udhibiti ubora na ukaguzi
  3.  Bei ya dawa itapungua zaidi maana sasa tutaweza kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji sio kama nchi (Tanzania), lakini kama Ukanda unaoshughulikia nchi 15
  4. Itaongeza ajira na kuijengea uwezo Bohari ya dawa(MSD)
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya

Kama Ulishiriki Kusambaza Ujumbe Huu Basi Imekula Kwako!

$
0
0
Hatimaye, uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umekanusha juu ya taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa zikiwahusu vigogo wa shirikisho hilo wakiongozwa na rais wao, Wallace Karia kujilipa posho ya kiwango cha juu.
 
Hivi karibuni kulisambaa taarifa mitandaoni juu ya vigogo hao wa TFF kujilipa fedha nyingi.

Kumbuka viongozi wa kuchaguliwa TFF hawapati mishahara, badala yake wanalipwa posho, sasa ilielezwa kwamba Karia analipwa Sh milioni sita, makamu wake Sh milioni tano huku wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakilipwa milioni moja kwa kila mwezi.
 
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema suala hilo halina ukweli na kudai kuwa Karia alikataa kulipwa na kusisitiza posho yake ipelekwe katika masuala mingine ya kimpira kwa kuwa yeye ni muajiriwa serikalini na analipwa mshahara huko.
 
“Hizo taarifa hazina ukweli wowote kwa sababu viongozi wa hapa hakuna ambaye anachukua kiasi hicho cha fedha.
“Hata kwenye suala la wajumbe, nao hakuna ambaye anapokea shilingi milioni moja kwa mwezi kama inavyosemekana badala yake tunatoa shilingi milioni moja na nusu kwa miezi mitatu tena kwa yule ambaye anachakarika na tunaona juhudi zake kwa kupitia ripoti ambazo anawasilisha kwenye vikao.
 
“Lakini kwa sababu jambo hilo limechafua sura ya taasisi yetu tuna mpango wa kuwafungulia kesi ya makosa ya kimtandao wale wote ambao wamehusika kwenye suala hilo na tayari tuna majina 10 ya watu ambao tutaanza nao,” alisema Kidau.

Pamoja na TFF kuamua kulitolea ufafanuzi suala hilo, bado inaonekana haukuwa mjadala mpana hasa nje ya mitandao na huenda waliamua kuwahi mapema ili kumaliza mjadala.
 
WARAKA WA TUHUMA UNAZOSAMBAZWA NI HUU;

“KAMATI TENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) KUTUMIA MILIONI 438 KWA MWAKA  KUJILIPA POSHO.
Tarehe 28/10/2017 Kamati ya Utendaji ya TFF, ilifanya Kikao katika Hoteli ya SEA SCAPE Kunduchi Beach jijiji Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine ilipitisha azimio la Wajumbe wa Kamati hiyo kuanza kulipwa posho  ya kila mwezi kwa mchanganuo ufuatao: 
 
1. Rais wa  TFF  Tsh.Mil.6 kwa mwezi  sawa na Mil.72 kwa Mwaka.
2. Makamu wa Rais wa TFF, Tsh. mil. 5  kwa mwezi sawa na Mil.60 kwa mwaka.
3. Wajumbe 20 wa Kamati ya Utendaji kila mmoja Tsh. Mil. 1 kwa mwezi sawa na mil.12 kwa mwaka ,  kwa wajumbe 20 ni Tsh.  Mil. 240 kwa mwaka.
 
NB: Posho hizi ni mpya na hazijawahi kuwepo katika shirikisho hilo katika uongozi uliopita.  
 
Aidha Posho za kila kikao zimepanda kutoka Tsh. 300, 000/=  uongozi uliopita hadi laki tano (500,000/) uongozi wa sasa kwa kila mjumbe,  kwa mwaka kuna vikao vya kawaida visivyopungua sita,  kwa Wajumbe wote 22 kwa mwaka itakuwa mil.66. 
 
Kwa  mchanganuo huo, Gharama za Posho tu kwa mwaka kwa Wajumbe wa  Kamati ya Utendaji tu ni milioni mia nne thelathini na nane (mil.438). Bado posho za vikao vya dharura, posho za watumishi wengine n.k
 
Moja ya changamoto za maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania ni Ukosefu wa fedha.  Timu zetu za taifa zinashindwa kukaa kambini,  Waamuzi wanakosa Mafunzo, viwanja vya michezo vinashindwa kuboreshwa, vilabu vya michezo havisaidiwi na mambo mengine chungu nzima hayafanyiki sababu ya ukosefu wa fedha, leo hii EXCOM  inakwenda kujifungia Sea ESCAPE na kuidhinisha  mil. 438 kwa ajili kujilipa posho!  

Kwa mwendo huu tusitegemee maendeleo katika soka Tanzania. Rais wa TFF,  WALES KARIA na Makamu wake, MICHAEL WAMBURA wanapaswa kujitathmini upya,”.

Ushuhuda: Nilivyowatumia Bundi Kubatilisha Ndoa ya Mtoto wa Shangazi Yangu

$
0
0
Bwana Yesu  Asifiwe , jina langu  ninaitwa  Winnie, mkaazi  wa wilaya  ya  Kisarawe mkoani  Pwani.

Kwa  sasa  nimeokoka na  kumpokea  Yesu  kama Bwana   na  Mwokozi  wa  maisha yangu  lakini  kabla  sijaokoka nilikuwa  mtumwa wa shetani kupitia uchawi.

Nimeamua kuandika  waraka  wangu  huu  baada ya kuguswa .
Ninaona  nina  wajibu  mkubwa  wa  kuelezea  siri  hizi  za  wachawi  ili  niweze   kuwekwa  huru  lakini pia niweze  kuwasaidia  watu  wengine  waweze  kuwa  huru, kwani  maandiko  matakatifu yanasema nanyi mtaijua kweli nayo  itawaweka  huru.

Nimeona  si  vyema  endapo  nitakufa  nikiwa  na  siri yangu  hii. Mambo  niliyo  yapitia  yamefunza  mambo mengi  sana  maovu  yanayo  tendeka katika  ulimwengu  huu ambayo  nilikuwa  siyafahamu hapo awali.

 Ninataka  ulimwengu  mzima  uyafahamu  na  hivyo  kuwa  huru.

Nisiwachoshe  kwa maneno mengi  ila kwa ufupi tu ni  hivi mwaka 2014  rafiki  yangu  mmoja  alinipeleka  kwa  mganga  wa  kienyeji  ili anisaidie  niweze  kupata  mume  wa  kuniona.

Nilifikia  uamuzi  huu  baada ya  mwanaume alie kuwa  anataka kunioa  kufariki ghafla  kwa ajali ya  gari  huku akiniacha  na  kichanga cha  minane  tumboni.

Tukio  hilo  lilini huzunisha  sana  kwa  sababu mwaka  huo wa 2014  nilikuwa  nimetimiza umri wa  miaka  40  nikiwa  bado  naishi  nyumbani  kwa wazazi  wangu  huku  nikiwa  na  watoto  wawili  huku  kila  mmoja  akiwa  na  baba ake.

Nilimfuata  dada  mmoja  jirani  yangu  ambae  alikuwaga  ananisaidia   hela  na  chakula  kila  nilipokuwa naenda  kumuomba

Nilipo  mfuata  kuomba  ushauri  nifanye nini, nilimuelezea  historia yangu  yote  kuanzia  mume alietaka  kuniona  wakati  bado  nipo  msichana  kisha akaingia  mitini  kabla  ndoa  haijafungwa, mwanaume  nilie zaa  nae  mtoto wa  kwanza, wapili  hadi  huyu  ambae  amefariki na  kuniacha  na kichanga  cha miezi  minane.

Dada  huyu  akaniambia  atasaidia  kunihudumia  hadi  nitakapo  nijifungua na  nikisha jifungua  atanipeleka  kwa  mganga  ambae  atanisaidia.

Kweli  alifanya  kama alivyo  niahidi. Bahati  mbaya  mtoto  hakuwa riziki. Alizaliwa akiwa amefariki  tayari.

                       NAPELEKWA KWA  MGANGA

Tulipofika  kwa  mganga akanitazama  na  kuniambia kuwa  nimefungwa  kichawi.

 Mganga  akaniambia kuwa nyota  yangu iliibwa  kichawi  muda  mrefu   kwa ajili ya   kwenda  kutumikishwa  kichawi.

Mganga  akaniambia  hakuna haja  yoyote  ile ya kuirudisha nyota hiyo  kwa  sababu  imeshakufa  huko  ilipo na  haiwezi  kunisaidia  kitu  chochote  hata kama  itarudishwa kwa  sababu  imetumikishwa .

Akaniambia ilikuwa  niolewe tangu nikiwa na  miaka 20,lakini  “ndoa” yangu  ilibatilishwa  kichawi  kwa  kutumia  bundi  na  bahati  yangu  ya  kuolewa  akapewa mwanamke mwingine.

Na kweli  kwa mujibu  wa kumbukumbu  zangu, nikiwa  nina  umri huo  kuna  mwanaume  mmoja  alitaka kunioa lakini  badae ndoa  ikapeperuka  hata  sijui  kitu  gani  kilitokea.

Mganga  akaniambia  kwa  kuwa  bahati  yangu  ya  ndoa  iliibwa  kwa  kutumia  bundi  basi  na  mimi  itabidi  niibe  bahati  ya  mtu  mwingine  kwa  kutumia  bundi.

Sikuwa na  jinsi  Zaidi  ya  kukubaliana  na  mganga  pamoja  na  kwamba  sikujua  lingewezekanaje  hilo..

NAAMBIWA  NIKACHUME  MTI  WA  PILIPILI  NIKIWA KWENYE  SIKU ZANGU.

Mganga  akaniambia  nirudi  nyumbani, halafu  siku  nitakapo  ziona  siku  zangu  basi  niende  kwenye  mti wa  pilipili  nichume  pilipili  halafu  niutazame  vizuri  huo  mti  kisha  nimjulishe  nimeona nini.

NACHUMA   MTI   WA   PILIPILI  NIKIWA  KWENYE  SIKU  ZANGU

Siku nilipoziona  siku  zangu  nikaenda  kuchuma  pilipili. Niliona  kitu cha  ajabu  sana. Kitu  ambacho  sikuwahi  kukiona  tangu  nizaliwe.Ule  mti wa  pilipili ulikauka  ghafla. Niliogopa  sana  nikampigia  mganga. Mganga  akaniambia niuchume  huo  mti  halafu  kesho niende nikamuone.

NAPELEKA  KWA  MGANGA  MTI  WA PILIPILI  ULIO KAUSHWA NA  HEDHI

Kesho  yake  nikadamkia  kwa  mganga  na  mti  wa  pilipili  ulio  kauka. Mganga  akauchukua  huo  mti  na kuusaga  pamoja  na  dawa zake  nyingine anazo  zijua  yeye  mwenyewe. Baadae  akanichanja  akanipaka mafuta  ambayo  sikujua  ni  mafuta  ya  nini. Akanipa  dawa  za  kuoga, na  kunywa  pamoja  na  hirizi.

Halafu  akanipa  dawa  ya  kuchoma  usiku.

MGANGA   ANANIELEKEZA   NAMNA   YA  KUWAITA  BUNDI NA   KUWASILIANA  NA  BUNDI KWA  ISHARA.

Mganga  akaniambia  haya  mafusho  ninayo  kupa ni  uchawi mkubwa sana.

Zingatia  masharti  yote nitakayo kupa vinginevyo  utapata  madhara makubwa  sana.

Akaniambia  hilo  ni  fusho  maalumu  la kuwaita bundi. Kwa  kutumia fusho  hilo utakuwa unawaita bundi  na  kwa  kuwatumia bundi hao  utaweza  kujua ni  katika  nyumba  gani kuna mwanamke mwenye  bahati ya kuolewa.

Kupitia  bundi  utaweza  kujifunza  vitu  vingi sana ambavyo  ulikuwa  hauvijui.

Mbali  na  kujua  mwanamke  gani  ana  bahati  ya  kuolewa, unaweza kujua  kwenye nyumba  gani  kuna  watu  wana nyota nzuri  nakadhalika.

Mganga  akaniambia nitakufundisha  namna  ya  kutafsiri  ishara  mbalimbali  za  milio  ya bundi.

i.                 Bundi  akilia  mara  moja, anatoa  ishara  kuwa  katika  nyumba  hiyo  kutatokea  msiba  hivi  karibuni. Na hapo  itategemea  amelia  saa ngapi. Kama  akilia  kati  ya  saa  sita  na  saa  saba  usiku basi  anakuwa anatoa  ishara  ya  kutokea  kwa  msiba  na  kama  kama  atalia  kati  ya  saa  4 na  saa  5  usiku  anakuwa anatoa  ishara  na  kuwaonya  wenye  mji  juu  ya  ujio  wa  wachawi  katika  mji  huo usiku  huo.

Hii ni kwa sababu  bundi  anaweza  kuona  mambo  ya sirini, mambo aliyo fichwa  mwanadamu  na  mambo  yatakayo  tokea  siku  za  mbeleni.

ii.             Bundi  akilia  mara  mbili  maana yake ni  kwamba wewe  ulie  isikia sauti  hii utapata  mafanikio   makubwa  sana  katika  kitu unacho taka  kukianzisha  hivi  karibuni, na  ili ufanikiwe  katika  kitu  au jambo  hilo ni lazima  ukifanye  haraka iwezekanavyo.

iii.         Bundi  akilia  mara  tatu  basi anatoa  ishara  kwamba  katika  nyumba  iliyopo  karibu  na  mti  ambao  bundi  huyo alitua  wakati  analia, kuna  mwanamke ataolewa  na ndoa yake  itadumu kwa muda mrefu.

iv.          Bundi  akilia  mara  nne anakuwa  anatoa  ishara  kwamba     wakaazi wa nyumba au  mtaa  huo  watapata  usumbufu  mkubwa  katika siku  za  karibuni.

v.   Bundi  akilia  mara  tano  anatoa  ishara  kwamba wewe  ulie  sikia  sauti  hiyo  utapata  safari  nzuri  hivi  karibuni.

vi.    Bundi  akilia  mara  sita  anatoa  ishara  kwamba, kuna wageni  wapo njiani  wanakuja  kuwatembelea.

vii.      Bundi  akilia  mara  saba anatoa  ishara  kwamba kuna  mtu  au  watu  katika  nyumba  hiyo  watapatwa  na  matatizo  ya  msongo wa  mawazo.

viii.  Bundi  akilia  mara  nane, anakuwa  anatoa  ishara  kwamba  katika nyumba  hiyo  utatokea  msiba  wa  ghafla.

ix.          Bundi  akilia  mara  tisa  anatoa  ishara  ya  bahati  njema  katika  nyumba  hiyo.


Sasa  basi, wachawi  huwa wanakuwa  makini sana  kusikia  sauti za  bundi pindi  wanapolia.   .

Baada ya  hapo mganga   akaniambia  natakiwa  kwenda  kumwaga   mafusho  hayo  kidogo  kwenye  mti  wowote  mkubwa ulio   jirani  na  nyumba ambayo nimeikusudia  na  kuchukua  jani  la huo  mti kwenda  nalo  hadi  chumbani  kwangu   kisha  kulichoma  kwenye  chetezo  pamoja na hayo mafusho  huku  nikitamka maneno  maalumu  ya  kuwaita  bundi  waje  kwenye  huo  mti  ili waweze  kujua  ni mwanamke  gani  anakaribia  kuolewa ndani  ya  nyumba  hiyo.

Usiku  wa  siku  hiyo  nikafanya  kama  nilivyo  elekezwa. Nikaenda  kuchuma  jani  la  huo  mti na kuwamga  fusho  kidogo  kwenye  mti kisha  ilipofika  saa  tatu  za  usiku  nikaanza  kuchoma  ilo  fusho  pamoja  na  jani  la  huo  mti.

Ilipofika  saa  sita  usiku kweli  bundi wakaja  na muda si mrefu  wakaanza  kulia. Nikasikia  kwa makini  sana.

Bundi  akalia  mara tatu .  Alilia kutoka  kwenye  mti uleule  ulio  jirani  na nyumba  ya shangazi  yangu. Nilichagua  mti  ulio  jirani  na  nyumba ya  shangazi  yangu  kwa  sababu shangazi  yangu  alikuwa  na  watoto  wengi  wa  kike  na  nyumba  yake  ilikuwa  na  wageni  na  wapangaji  wengi  wanawake.

Mganga   aliniambia  bundi wakisha  nyamaza  tu  nimjulishe haraka  sana.

Kama alivyo  nielekeza  mganga  nikamjulisha.

 Nilipo mjulisha akaniambia sawa, nilale halafu kesho  asubuhi  nihakikishe  naenda  kwa  shangazi  yangu  au  naongea  na  mtu yoyote  anaeishi  nyumbani  kwa  shangazi  yangu.

 Nitakapo  kuwa  hapo kwa shangazi yangu  nisikie  kama watazungumza  chochote  kuhusu  bundi na kama wasipo  zungumza  basi  nijifanye  kuanzisha  mazungumzo  kuhusu  bundi, nijifanye  na  mimi  jana  bundi walitua  nyumbani  kwetu  na  kwamba  ninaogopa  sana.

 Na  watakacho nijibu  basi  nimjulishe  mganga.

Kweli  nikaenda  hadi  kwa  shangazi  na  bahati  nzuri nikamkuta  binamu  yangu  ambae  ndio  nilibatilisha  ndoa yake  kichawi.

Binamu  hakuwa  na  dalili  zozote  za  kupiga  story  kuhusu  bundi  hivyo  nikaanzisha  story  za  bundi kwamba  jana  bundi  walilia  sana  batini  kwangu na  kwamba   nilishindwa  kulala.

Binamu  akaniambia  hata  kwao  ilikuwa  hivyo  hivyo  na  sio  kulia  tu  bali  kuna  wakati  bundi  waliingia  hadi  ndani  wakatua  na  kuondoka.

Tukaongea  kwa muda  kidogo  kisha  baada  ya  hapo  nikampigia  mganga  na  kumueleza  kila kitu.

Mganga  akaniambia  vizuri  sana, mambo  yako  yatakuwa mazuri  sana.

Niseme kitu  kimoja, wachawi  kwa  kumtumia  bundi, wakishajua  kwenye  nyumba  Fulani  kuna  mtu  ana nyota  ya  kuolewa  hivi karibuni  au  kuna  watu  wenye  nyota  kali  wamelala kwenye  nyumba  hiyo  huwa  wanawatuma bundi kwenda  kuiba  nyota  hizo.

Hivyo  basi  siku  ukisikia  bundi   wamelia  mara  tatu  karibu na  nyumba  yenu  halafu  baadae  wakaingia  ndani  basi  jua  bahati  ya  kuolewa  ya  mtu  imeibiwa  na  kama  kuna  watu  wenye nyota  kali  walikuwa  ndani  ya  nyumba  hiyo  basi  na nyota  zao zinakuwa  zimechukuliwa  pia.

Hivyo  ndivyo  alivyo  niambia  Dokta  na  akaniambia  ikitokea  nimeenda  kwenye  mji  wa  ugenini  halafu  jambo  hilo  likatokea, basi  nihakikishe  huyo  bundi  atakae  ingia  ndani  anauliwa  au  anakamatwa kabla  hajapaa,jambo  ambalo  hata  hivyo   ni  gumu sana   kwa  sababu  bundi  wanapo ingia  ndani  huwezi  kuwasikia  kwani  huwa  wanapaa bila  kupiga kelele  wala  kutoa sauti.

Dokta  akaniambia   huu  ni  uchawi  unao tumika sana na  hautumiki  kwenye  masuala  ya  mapenzi  tu  bali  biashara  pia.

Akaniambia wafanya  biashara  wengi wametajirika  na  wanaendelea  kutajirika  kwa  kutumia  uchawi huu  wa  kuiba  nyota  za  watu  kwa  kuwatumia  bundi.

Na  hii  ndio  sababu  bundi  anatukuzwa  sana  miongoni  mwa  wafanya  biashara.

Mganga  akaniambia  ili nyota  isichukuliwe na  bundi  kwa  staili hiyo  natakiwa  niwe  na  kinga  maalumu  ya  kuwazuia  bundi  kuchukua  nyota.

Akasema kinga  hii  ni  tofauti  na  kinga  zingine  zote  na kwamba  hata kama  una  kinga  nyingine  yoyote  ile  lazima kinga  hii  uwe  nayo pia.

Akaniambia  kwa  kuwa  nimeingia  kwenye  mtandao  huu  inabidi  hiyo kinga  niwe  nayo.

Siku  ya  kutengeneza kinga  hii,mganga  alichukua paka mweusi, akauliwa  kisha akatobolewa  macho  halafu  kwenye  macho  yake zikawekwa mbegu  za  mti  wa  mnyonyo  kila  jicho.

Paka  huyo  akafungwa  kwenye kitambaa  cheupe  mfano  wa maiti akawekwa  kwenye  mfuko  nikapewa  kwenda  nae  na  kumzika   vichakani  kwenye  eneo  ambalo  nitaliweka  alama…  Nikawa namwagilizia maji  kila  siku  hadi  mti  ulipo  chipuka na  kukua.. Mti  ulipo  kua  mganga  akaniambia  nitoe mbegu, nikafanya kama  alivyo  nielekeza . Mganga  akaniambia nichukue mbegu saba  kisha  nimpelekee.

Nilipo mpelekea mbegu  hizo  mganga,  akazichukua akachanganya  na  dawa zake  anazo  zijua  mwenyewe  akachukua popo,akamkata  kucha  akiwa  hai  na  kumuacha, akaziasaga  na  muzichoma  kisha  kunichanja  na  kunipaka.

BAADA  YA  BUNDI  KULIA  NA  KUTUA  KWENYE  NYUMBA  YA  SHANGAZI  YANGU

Sikuwa  najua  kama  binamu yangu mtoto wa  shangazi  yangu  alikuwa  na  mpango  wa kuolewa kwa  sababu  ni  jambo lililofanywa  siri.

Lakini siku  chache  baada  ya  bundi  kutua  kwenye nyumba  ya shangazi  yangu  nikaanza kusikia  habari  za  kuharibika kwa  mipango  ya  ndoa  ya  binamu  yangu.

Binamu  yangu  alitaka kujaribu  kujiua  baada ya  mume   mtarajiwa  kugombana  nae  na  kuingia  mitini  na kisha  kuhamishia  uchumba  kwa mwanamke  mwingine.

Wakati  huo huo,mimi  nikapata  mwanaume mwenye pesa  ambae  alinichumbia na  kunioa  tena  kwa  harusi  kubwa.

Ni  hivi  bahati  ya  ndoa ya  mtu  inayo  ibwa  kwa kutumia  bundi, sio  lazima  wewe uolewe  na  aliekuwa  anataka  kumuoa  mwanamke  uliye  iba bahati  yake.HAPANA. Ni hivi inaweza  kutokea  mwanaume  huyo  labda  akafukuzwa  kazi  ghafla au  akafilisika  na  mipango  yake  kuvurugika.

Nyota  ya  mwanaume  huyo  inaibwa  anapewa  mwanaume  mwingine  ambae  atakuja  kukuoa  wewe.

NAAMUA   KUACHANA  NA   USHIRIKINA  NA  KUMRUDIA  MUNGU.

Niliishi  na  mwanaume  huyo  toka  2014 hadi  2016 katikati.. Siku moja nilipokea  taarifa  za  msiba  wa rafiki  yangu  ambae ndio  aliniunganisha  na  huyo  mganga.

Huyu  dada alikuwa anaishi  maisha  ya  kidini lakini  kumbe  alikuwa anafanya  ushirikina sana.

Kuhusu  kifo chake, sijui kama  kilitokana  na  ushirikina ama  ni mipango  ya   mungu  lakini nilipo ona  mwili  wake niliogopa sana.

Niliwaza  nakuwazua, nilitafakari  nakutafakari.  Nikajiuliza  moyoni kumbe na mimi  pamoja  na  mali na  pesa hizi  nilizo  zipata kwa  njia  ya  ushirikina  ipo  siku  nitakuwa  kama huyu ?

Kumbe  mimi  sio  kitu  kabisa katika dunia hii ? Kumbe  binadamu  ni  mchanga.

Kumbe  binadamu  ananuka  na  kutoa  harufu ?  Kumbe ipo  siku  ndugu  zangu  wataogopa kulala  na  mimi ?

Nilitakafakari  sana .. Nilikumbuka  mambo  mengi ya utotoni. Jinsi nilivyo  lelewa  na wazazi  wangu.

Nililelewa  kufuata  maadili  ya  Mungu  na  kuwa  mvumilivu  na  mstahimilivu  kwa  namna  yoyote   ile.

MAHUBIRI  YA  MCHUNGAJI  WAKATI  WA MAZISHI  YANILIZA

Nikiwa  katika  hali  ya  majuto  na uchungu  mkubwa  Mchungaji  alianza  kuhubiri neno la Mungu.

Alihubiri  mambo  mengi  sana lakini  kikubwa  aliwasisitizia  waombolezaji  kumkumbuka  Mungu  wakati  wa  uhai  wao na  kwamba hapa  duniani  tunapita  tu.

Mchungaji  waliwaasa  waumini  wasiwe  na  tamaa  na  mali  za  duniani  hapa  kwani  tutaziacha hapahapa duniani.

Mchungaji  akawakumbusha  waumini kwa  kuwasomea  neno  la Mungu  kutoka  katika kitabu  cha   MATHAYO  16 : 26  ambalo  linasema

“Kwa maana mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini aipoteze nafsi yake?au mtu atatoa nini ili aipate nafsi yake?”

Hapa  Mchungaji  akawa  kama  ananiongelea mimi kabisa.

Baadae akasema najua  kuna  watu wanakata  tamaa  ya  kufanikiwa  katika  maisha  kwa  sababu wamehangaika  muda  mrefu  bila mafanikio.

Shetani anazitumikisha  nafsi   zao  kwa  faida  yake  na  watu  wake.  Wametupiwa  nuksi na  mikosi na wachawi.

Mungu  anasema  katika  kitabu  cha  YOELI 2  Sura ya  25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu…

Baadae  Mchungaji  akasema  kama  kuna  watu  wapo  tayari  kuokoka basi  na wanyooshe  mikono yao  nami  nitawaongoza sara  ya  toba.

Nilidhani  ni  mimi  tu  nitakae  nyoosha  mkono  wangu  lakini  nilishangaa  kuona  na  watu  wengine  wengi  tu  wakinyoosha  mikono  yao.

Hata  yule  binamu  yangu  ambae  niliiba nyota  yake  kichawi  nae  alinyoosha  mkono wake.   Wote  tuliombewa  na  baadae  tukaanza  mafundisho  kanisani  na  hadi  muda  huu  ninaondika  waraka  huu  bado  tunaendelea  kumtumikia  Mungu.

KUHUSU MUME  WANGU :  Mume  wangu  alinikimbia  baada  ya kuona  nimeokoka jambo ambalo nililishukuru  pia  kwa  sababu  hakuwa  haki  wala staili yangu.

MAISHA  YETU  YA  MAHUSIANO  KWA  SASA.

Kwa  sasa  mimi  nina  mchumba  na  yule  binamu yangu  ameshaolewa  tayari.

KUHUSU  MGANGA  ALIYE  NIINGIZA KWENYE  SUALA  LA  KUIBA  NYOTA  ZA  WATU KWA  KUMTUMIA  BUNDI.

Mganga  huyu  anajulikana  Zaidi kama  mungu  wa  kabili  na  namba  zake  za simu  ni  0744  -000  473.

NIMEWEKA  JINA  LAKE  NA  NAMBA  ZAKE  ZA  SIMU  ILI WATU  WAJUE  KWAMBA  HUYU  NI  MCHAWI  NA WAKALA  WA WACHAWI  NASHETANI  NA  WAEPUKANE  NAE  KWA  SABABU  ATAWAINGIZA  KWENYE  MAMBO YA  UTUMWA WA  ULOZI  NA  UCHAWI  KAMA  ALIVYO  FANYA  KWANGU.

Kikao Cha Kamati Kuu (CC) Na Halmashauri Kuu Ya Taifa (NEC) Ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kuanza Novemba 19 Na 23

Kamati Ya Bunge Ya Maadili Yamhoji Mhe. Kubenea Mjini Dodoma

$
0
0
Kamati ya  Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji  Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.

Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman  Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa  Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati  hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho   ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)   ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika  leo (jana) baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe.

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa  baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.

Mtoto wa Chacha Wangwe Ahukumiwa

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu
Mtoto wa Marehemu Chacha Wangwe ambae alikua Mbunge wa Tarime, Bob Chacha Wangwe kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela au kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 baada ya kupatikana na hatia kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa Facebook.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6 na vielelezo 5 dhidi ya Bob ambae pia ni Mwanaharakati.

Alisema kuwa Mei 7, 2016 polisi walipata taarifa ya chapisho la Bob ambapo walianza kumfatilia na kumkamata kisha walichukua simu na kuipeleka maabara ya Polisi ili kuikagua.

“Kimsingi Bob hukupinga kuandika maneno hayo lakini umedai kuwa hukuyachapisha katika jamii bali yalikuwa ni siri kwenye akaunti yako“.

Hakimu Shaidi alisema kuwa wakati wa ushahidi simu yake ilipokaguliwa ilionekana ilitumika kuchapisha ujumbe huo kwa jamii na watu walimjibu, ikiashiria ujumbe uliwafikia.

“Hivyo ni dhahiri ulikuwa na nia ya kuchapisha taarifa hiyo, kueleza kile ambacho ulikiona sahihi kama ingekuwa ni ujumbe wako binafsi basi Polisi wasingeweza kukutafuta na watu wasingekujibu“

Hakimu Shahidi amesema kutokana na hatua hiyo Bob amekutwa na hatia chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 ambapo katika utetezi wake, Bob aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni Mwanafunzi wa masomo ya Sheria na pia ni kijana mdogo na ni kosa lake la kwanza kulitenda.

Hakimu Shaidi alisema anakubaliana na hoja za Bob kwani Mahakama inamuona bado ni mdogo na anapaswa kufanya mambo mengi mazuri katika jamii ambapo pia amesema kama yeye ni mwanafunzi wa masomo ya sheria anapaswa kufanya mambo mema katika jamii vitu ambavyo wengine watamuiga.

“Hivyo Mahakama inakuhukumu kulipa faini ya Sh.milioni 5 ama uende jela mwaka mmoja na nusu na pia milango ya dhamana ipo wazi“

Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wange anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook March 15,2016 ambapo aliandika maneno yafuatayo hapa chini.

“….Tanzania ni ambayo inajaza chuki wananchi.… matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwasababu za kijinga.”

Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza toka Jeshi liingie Ikulu

$
0
0
Rais Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi lilipomweka chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya leo kuhudhuria mahafali ya chuo kikuu.

Akiwa amevalia joho la kisomi lenye rangi za bluu na njano na kofia, Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alikaa kwenye kiti mbele kabisa kwenye ukumbi na alishangiliwa kwa mbinja na vigelegele alipotangaza kwamba mahafali yamefunguliwa.

Mkongwe huyo aliyetawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, kwanza akiwa waziri mkuu (1980 hadi 1987) na baadaye rais (1987 hadi sasa) aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwake kuanzia Jumanne ikiwa ni wiki moja baada ya kumfuta kazi aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa.

Hatua ya kumfukuza kazi Mnangagwa ilichukuliwa na wengi kwamba ulikuwa mpango wa kumpandisha mkewe, Grace katika nafasi hiyo ya makamu wa rais na hivyo kumtengenezea mazingira ya kurithi urais wa mumewe.

Zimbabwe ilibaki imeduwaa baada ya jeshi kuingilia kati katikati ya mzozo mkali wa kuwania uongozi wa nchi kati ya Grace na Mnangagwa, 75.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba jeshi linapinga Grace kupanda hadi kuwa kiongozi wakati Mnangagwa ndiye mwenye uhusiano mzuri na jeshi hilo.

Mugabe na wakuu wa jeshi wamekutana kwa mazungumzo na hatua yao ya kunyakua madaraka ni ishara kwamba mkongwe huyo anaondoka.
Mnangagwa, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa kiongozi mpya amerejea nchini baada ya kutoroka nchi akihofia usalama wake. Jeshi limesema kuwa lilikuwa katika mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo.

Utaratibu wa kulipa kodi za nyumba kwa miezi 6 au mwaka kupigwa Marufuku Tanzania

$
0
0
Serikali iko katika mchakato wa maandalizi ya muswada wa sheria ambayo itasimamia sekta ya nyumba, hivyo kuondoa changamoto ya wamiliki kudai kodi ya pango ya zaidi ya mwezi mmoja.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema hayo bungeni leo Ijumaa Novemba 17,2017 akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Halima Bulembo.

Halima katika swali lake amesema vijana ambao ni kati ya asilimia 56 na 60 nchini, wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na gharama kubwa ya kodi ambayo hutakiwa kulipa kwa kipindi cha mwaka mmoja au miezi sita.

"Serikali inasemaje kuhusu kuleta sheria itakayofuta tabia ya wenye nyumba kulazimisha kulipwa kodi ya mwaka?" amehoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Mabula amesema Serikali imeliona tatizo hilo na ipo katika mchakato wa kuandaa muswada wa sheria utakaosimamia sekta hiyo.

Mabula amesema baada ya kukamilika kwa sheria ambayo itaunda chombo cha kusimamia sekta hiyo, wapangaji hawatalipa kodi ya mwaka wala miezi sita tena bali watalipa kwa mwezi na kuweka amana ya miezi mitatu.

Katika swali la msingi, Halima amesema kumekuwa na upandaji holela wa gharama za pango kwa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

"Je Serikali haioni kuna haja ya kudhibiti upandaji holela ambao unaathiri wananchi wengi kutokana na kipato chao?" amehoji.

Akijibu, Mabula amesema utaratibu wa urekebishaji wa viwango vya kodi za shirika hilo husimamiwa na bodi ya wakurugenzi ambayo imepewa mamlaka ya kisheria ya kusimamia kodi ya pango na kuidhinisha viwango vya kodi vinavyotozwa kwa wapangaji wa nyumba za shirika.

"Kwa mara ya mwisho bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa iliidhinisha viwango vipya vya kutoza kodi kwenye nyumba za shirika mwaka 2011 ambavyo ndivyo vinavyotumika mpaka sasa," amesema.

Mgombea udiwani Mwanza na meneja wa kampeni wake Watupwa Gerezani.....Hakimu Kuamua Hatima yao Novemba 21

$
0
0
Mgombea udiwani kata ya  Mhandu (Chadema), Godfrey Misana na kampeni meneja wake, Charles Chinjibela, wamepandishwa kizimbani kujibu shtaka la kujeruhi.

Misana (46) na Chinjibela (37) wanadaiwa kumjeruhi meneja wa kampeni za CCM katika kata hiyo, Thomas Warioba.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, mbele ya hakimu Ainawe Moshi wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 14,2017.

Akisoma mashtaka katika shauri hilo namba 540/2017, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Elizaberth Barabara amedai leo Ijumaa Novemba 17,2017 kuwa washtakiwa walitumia visu na mawe kumjeruhi Warioba.

Kabla ya kuhamia CCM, Warioba alikuwa mwanachama wa Chadema.

Upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile ilichoeleza ni kwa usalama wao.

Ombi hilo la Jamhuri limepingwa na wakili wa utetezi, Gasper Mwanaliela.

Wakili Mwanaliela amesema dhamana ni haki ya wateja wake na kwamba, kuwanyima kutawazuia kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Moshi amesema Mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana Novemba 21,2017.

Washtakiwa wamepelekwa mahabusu hadi siku huyo.

Heche Amshukuru Spika Kwa Kumlinda Asikamatwe

$
0
0
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata.

Mh. Heche amweka hilo wazi jioni hii huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa.

"Nimepokea barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka gerezani mwezi wa 4" Amesema Heche na kuongeza;

"Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali"

Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema leo Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro.

"Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.

Patcho Mwamba Ampa Neno Mama Kanumba

$
0
0
Mwanamuziki na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba ya kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja ya kuendelea na 'beef' kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba hai.

Patcho ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba amesema kwamba Mama kanumba anapaswa  kuwa na moyo wa kusamehe kwa sababu binti huyo akimaliza kifungo atarudi mtaani na ataendelea na maisha yake hivyo kujengeana chuki siyo jambo jema.

"Sina la kusema juu ya jukumu ya Lulu, lakini Mahakama imeamua kama ilivyoamua, kwa upande mmoja kuna unafuu kwani kwa kesi ile kufungwa miaka miwili ni bahati, ukija upande wa pili inaumiza sana kwani jela siyo sehemu nzuri sana kwa mtu kuwepo kila mtu anajua hilo hasa ukizingatia   bado ni mdogo hivyo tumuombee Mungu ampe nguvu, uwezo naamsaidie aweze kustahimili hiyo hali" Patcho.

Aidha Patcho ameongeza "Nimemuona mama anasema anashukuru (Mama Kanumba) haki imetendeka, mimi sidhani kama kunahitajika kuwepo na ma Beef. Mwanaye, ambaye pia ni rafiki yetu ameondoka lakini tunaamini ni mipango ya Mungu. Hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba aishi. kusema naenda kumzika Kanumba upya sidhani kama kuna haja ya kuendeleza ma beef japo yapo. End of the day Lulu atatoka wataongea vizuri?. Sidhani yule mama yangu hivyo simshauri aendee kuwa na kinyongo".

Patcho amemalizia na kusema kwamba "Kusema kufungwa kwa Lulu kutampatia unafuu sidhani  ni uongo yeye aendelee kuwa mama maana ninachoamini Lulu hakumuua Kanumba bali alikuwa shahidi wakati Kanumba anakufa  ndichi ninachokiamini. Baadaye Lulu atatoka jela je  ukimuon utamgonga na gari? au Mama Lulu utaweza kuongea naye na wale ni Wahaya ni kabila moja. Sidhani kama Lulu alikuwa akikaa na kufikiria ipo siku atamuua Kanumba".

Rais Magufuli Atoa Msaada Kwa Msikiti Wa Noor Kijijini Mkange, Miono, Wilaya Ya Chalinze Mkoa Wa Pwani Leo

$
0
0
Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono,  Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani ,wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.

Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.

Mara baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.

Akiungumza mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombil lao la kupata zulia, na kwamba  kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.

Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea  kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchinikuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pwani
17 Novemba 2017.

Ufafanuzi Kuhusu Sheria Mpya Ya Ttcl Kwa Vyombo Vya Habari

$
0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyotolewa kwenye magazeti ya Mwananchi na Uhuru ya tarehe 15/11/2017. Gazeti la Mwananchi liliandika, “Serikali ‘yaiua’ rasmi TTCL na gazeti la Uhuru liliandika,“TTCL ‘bye’ ‘bye’. Vichwa hivi vya habari vimewachanganya wasomaji na kuleta taharuki kwa wateja na wafanyakazi wa TTCL, wadau wa Sekta ya Mawasiliano na wananchi kwa ujumla.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewasilisha Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania katika mkutano wa Tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 14 Novemba, 2017 mjini Dodoma. Bunge lilijadili na kupitisha Muswada na kutungwa kuwa Sheria itakayoanzisha Shirika la Mawasiliano Tanzania. Madhumuni ya Muswada yalikuwa ni kuanzisha Shirika la Umma la Mawasiliano nchini kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na kutoa huduma za mawasiliano kwa ubora unaotakiwa. Pia, kulipa Shirika la Mawasiliano jukumu la kusimamia miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano nchini.

Sheria mpya itaiwezesha TTCL kutekeleza majukumu yake kama Shirika la Mawasiliano nchini. Hizi ni jitihada za Serikali kuimarisha TTCL na sio kuiua. TTCL bado ipo na itaendelea kutekeleza majukumu yake kama Shirika la Mawailiano nchini. Shirika litaendelea kutoa huduma kwa wananchi kwa ubora na ufanisi zaidi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
17 Novemba, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 18

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images