Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CHADEMA Wamjibu Lawrence Masha

$
0
0

Baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama wao Lawrence Masha kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu za kujivua kwake.

Kwenye kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari.

“Lawrence Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu na ngumu ,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni uamuzi wa aibu . Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Godbless Lema.

Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake.

“Tunaojua sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni danganya toto, tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa CHADEMA imejipanga kuingia ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani na wabunge nchini kuanzia 1995 hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena si mrefu”, ameandika Joshua Nasari.

Pia Katibu Mkuu wa chama hiko Vicent Mashinji aesema Masha kuondoka CHADEMA ni haki yake kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za yeye kuondoka.

“Mheshimiwa Masha ana haki kisheria, namtakia heri, lakini lazima auambie umma nini hasa kilichotokea”, ameandika Mashinji.

Lawrence Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema chama hiko hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya upinzani huwa.


Mbowe azungumzia watakachofanya sheria mpya vyama vya siasa Ikipita.....

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema iwapo Sheria Namba Tano ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 itawasilishwa bungeni wa ajili ya kupitishwa watakuwa tayari kufa kuliko kukubali ipitishwe.

Akizungumza jana Jumanne jioni wakati wa kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Ibhigi, iliyopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Emmanuel Simba, Mbowe amesema kama kuna wakati wanaume wanatakiwa kusimama wahesabiwe ni wakati huo.

Alisema kupitisha sheria hiyo maana yake ni kuingiza ubatili walioufanya ili uwe sheria kamili, kwamba hakuna mikutano ya vyama vya siasa, hakuna majadiliano ya mustakabali wa nchi.

"Wanaanda mkakati wa kubadilisha sheria ya vyama  vya siasa taarifa tunayo,  wanataka kuiingiza sheria hiyo kwa nguvu, Sugu(Joseph Mbilinyi) tunaanzia bungeni, wakati huo ukifika wakituua watuue, wakitunyonga watunyonge hatutakubali tutaandamana mahali popote," alisema Mbowe.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai alisema watalikataa hilo ili watoto watakaokuja kesho na keshokutwa wajue baba na mama zao walipambana kulipigania Taifa lao.

Alisema Watanzania kwa umoja wao wasilikubali hilo kwa sababu litawanyima haki  kukutana na kujadili wanataka nini kifanyike na watakuwa wamekubali kurudi nyuma miaka mitano.

Kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyokutana juu na wawakilishi wa vyama vya siasa , ambapo ilitoa tamko kuwa katika  kampeni za uchaguzi wa marudio ya udiwani, wasijadili masuala ya siasa nje ya kata, jambo ambalo ni la kipuuzi.

Alisema "tusipokuwa makini na haya matamko ipo siku tutaambiwa wake zetu walale upande huu na sisi upande huu”

"Wanataka mimi mwenyekiti wa chama Taifa nije kujadili masuala ya kata, halafu masuala ya Taifa atajadili nani," alihoji Mbowe.
 
Alisema wamezuiliwa kuzungumza na wananchi kwa miaka miwili sasa ndiyo nafasi pekee waliyopata kuzungumza nao, "Haya ni makatazo ya kipuuzi," alisema.

Mbowe pia alizungumzia kashfa zinazodaiwa kufanywa na  aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema kama wana uhakika na tuhuma hizo wampeleke mahakamani.

"Ilianza kwa Edward Lowassa alipohamia Chadema, ikaja kwa Fredrick Sumaye na sasa Nyalandu, kila anayehamia upinzani anaitwa fisadi, sisi hatuogopi Mahakama kwa sababu tunajiamini, wawachunguze na wawapeleke mahakamani.

" Nimezungumza na Nyalandu asubuhi ya leo, nikamuuliza kuhusu tuhuma hizo atachomoa, akasema hilo ni jambo dogo atadili nalo na halimpi shida," alisema Mbowe.

Mtoto wa Chacha Wangwe Ahukumiwa

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu
Mtoto wa Marehemu Chacha Wangwe ambae alikua Mbunge wa Tarime, Bob Chacha Wangwe kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela au kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 baada ya kupatikana na hatia kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa Facebook.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6 na vielelezo 5 dhidi ya Bob ambae pia ni Mwanaharakati.

Alisema kuwa Mei 7, 2016 polisi walipata taarifa ya chapisho la Bob ambapo walianza kumfatilia na kumkamata kisha walichukua simu na kuipeleka maabara ya Polisi ili kuikagua.

“Kimsingi Bob hukupinga kuandika maneno hayo lakini umedai kuwa hukuyachapisha katika jamii bali yalikuwa ni siri kwenye akaunti yako“.

Hakimu Shaidi alisema kuwa wakati wa ushahidi simu yake ilipokaguliwa ilionekana ilitumika kuchapisha ujumbe huo kwa jamii na watu walimjibu, ikiashiria ujumbe uliwafikia.

“Hivyo ni dhahiri ulikuwa na nia ya kuchapisha taarifa hiyo, kueleza kile ambacho ulikiona sahihi kama ingekuwa ni ujumbe wako binafsi basi Polisi wasingeweza kukutafuta na watu wasingekujibu“

Hakimu Shahidi amesema kutokana na hatua hiyo Bob amekutwa na hatia chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 ambapo katika utetezi wake, Bob aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni Mwanafunzi wa masomo ya Sheria na pia ni kijana mdogo na ni kosa lake la kwanza kulitenda.

Hakimu Shaidi alisema anakubaliana na hoja za Bob kwani Mahakama inamuona bado ni mdogo na anapaswa kufanya mambo mengi mazuri katika jamii ambapo pia amesema kama yeye ni mwanafunzi wa masomo ya sheria anapaswa kufanya mambo mema katika jamii vitu ambavyo wengine watamuiga.

“Hivyo Mahakama inakuhukumu kulipa faini ya Sh.milioni 5 ama uende jela mwaka mmoja na nusu na pia milango ya dhamana ipo wazi“

Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wange anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook March 15,2016 ambapo aliandika maneno yafuatayo hapa chini.

“….Tanzania ni ambayo inajaza chuki wananchi.… matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwasababu za kijinga.”

Jeshi la Zimbabwe Lawatia Mbaroni Mawaziri Watatu wa Mugabe

$
0
0
Mawaziri kadhaa katika serikali ya Rais Robert Mugabe wamekamatwa baada ya Jeshi la Ulinzi kuonyesha uwezo wake na kushikilia majengo yakiwemo ya shirika la utangazaji (ZBC).

Milipuko mikubwa ilisikika na ikafuatiwa na ya bunduki katika maeneo yanayokaliwa na watu maarufu ya Borrowdale usiku kucha hali iliyozidisha hofu kwamba jeshi lilikuwa kazini.

Shirika la TimesLIVE limeripoti kwamba waliokamatwa ni watu maarufu kutoka kundi la G40 ndani ya chama cha Zanu PF lililokuwa likiongozwa na memsapu wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.

Baadhi ya watu waliokamatwa ni Waziri wa Elimu Jonathan Moyo‚ Serikali za Mitaa Saviour Kasukuwere na Waziri wa Fedha Ignatius Chombo.

Jeshi limesema katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake moja kwa moja kupitia ZBC kwamba Rais Mugabe yuko “salama na mwenye afya njema”. Taarifa hii imekuja baada ya askari wakiwa na silaha jana Jumanne kwenda katikati ya mji wakiwa kwenye magari ya kijeshi.

Shirika la Utangazaji la Zimbabwe ambalo majengo yake yako eneo la Pocket Hills jijini Harare lilitekwa saa 10:00 alfajiri.

Soma: Jeshi lasema Mugabe, familia wako salama

Msemaji wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alitangaza kwamba jeshi lilikuwa linadhibiti kwa lengo la kuhakikisha linawashughulikia “wahalifu” wanaomzunguka Mugabe.

“Sisi tunawalenga wahalifu wanaomzunguka yeye (Mugabe) wanaofanya uhalifu ambao unawasababishia watu mateso katika Nyanja za kijamii na kiuchumi hapa nchini na kisha tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria‚” alisema Moyo.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Jeshi Lamuweka Kizuizini Rais Mugabe

$
0
0
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewekwa kizuizini na Jeshi la Ulinzi usiku wa kuamkia jana katika mji mkuu wa Harare, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amethibitisha.

Zuma alisema jana kwamba alipigiwa simu na Mugabe mwenyewe. Taarifa kutoka ofisi ya Zuma ilisema: "Rais Zuma alizungumza na Rais Robert Mugabe mapema leo na amedokeza kwamba anazuiliwa nyumbani kwake lakini alisema yuko salama."

Kuanzia Jumanne wanajeshi walionekana wakivinjari na kupiga doria katikati ya Harare, baada ya kuteka kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Zimbabwe (ZBC) kwa kile kilichoelezwa wanawalenga “wahalifu”.

Hatua hiyo ya jeshi inaweza kuwa ni mpango wa kumwondoa Mugabe na kumweka katika nafasi hiyo makamu wake aliyefukuzwa kazi wiki iliyopita Emmerson Mnangagwa, shirika la BBC limeripoti.

Ofisa mmoja wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alionekana kwenye televisheni baada ya kukiteka kituo hicho akisema Mugabe na familia yake wako “salama na afya njema na ulinzi wao ni wa uhakika ".

Meja Jenerali Moyo alisema, “Sisi tunawatafuta wahalifu waliomzunguka yeye (Mugabe) ambao wanafanya uhalifu na kusababisha machungu ya kijamii na kiuchumi nchini.”

"Mara tutakapokuwa tumekamilisha operesheni hii, tunatarajia kwamba hali itarudi kuwa ya kawaida."

Kufukuzwa kazi kwa Mnangagwa wiki iliyopita kutengeneza njia kwa mke wa Rais Mugabe, Grace kuteuliwa katika nafasi hiyo hivyo kuwa na matumaini ya kuteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha mumewe.

Milio mizito ya bunduki ilisikika kaskazini mwa mji wa Harare hadi jana alfajiri.

Mhasibu wa Takukuru aamua kwenda kujisalimisha mwenyewe

$
0
0
Aliyekuwa Mhasibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey John Gugai amejisalimisha katika taasisi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema Gugai amejisalimisha na hatua za kisheria zinaendelea.

"Ni kweli amejisalimisha na yupo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama na hatua zaidi za kisheria zitafuata" amesema Kamishna Mlowola

Mtumishi huyo anatuhumiwa kujipatia mali kinyume cha Sheria za Utumishi wa umma huku Takukuru wakidai kwamba kama atadhibitisha uhalali wa umiliki wake ataachiwa na akishindwa atachukuliwa hatua.

Gugai amejisalimisha ikiwa ni siku moja imepita tangu Takukuru ilipotangaza zawadi ya Sh 10 milioni kwa mwananchi yoyote ambaye angefanikisha kumtia nguvuni mtumishi  huyo.

Hata hivyo, Kamishna Molowa ameshindwa kufafanua kama amejisalimisha mwenyewe au kuna mtu katoa taarifa.

Rais Magufuli aagiza Makao Makuu ya TANESCO kubomolewa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Novemba 2017, amerejea jijini Dar es salaam akitokea kijijini kwake Chato, mkoani Geita.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dare es salaam, Mhe. Rais amepokelewa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wa mkoa.

Baada ya kutoka Uwanja wa Ndege, Rais Magufuli akiwa ameongozana na Makamu wa Rais pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, amekagua Ujenzi wa Daraja la juu Tazara ( Tazara Fly-Over) na Ujenzi wa Daraja la ghorofa tatu la Ubungo ( Ubungo Interchange)

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Ubungo, Rais Magufuli amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Ndyamukama Julius kuvunja sehemu ya jengo la TANESCO na jengo la Wizara ya Maji yaliyopo katika eneo la hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya daraja hilo.

”Sheria ya hifadhi ya barabara katika eneo hilo ni mita tisini kila upande kutoka katikati ya barabara hivyo ni lazima sheria hiyo iheshimiwe ili kuharakisha ujenzi wa Daraja la ghorofa tatu katika eneo hilo la Ubungo uanafanyika bila vikwazo kwani sheria ni msumeno haina budi kuzingatiwa hata na Serikali yenyewe” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameiagiza TANROADS kutangaza tenda ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita kumi na sita (16) kutoka eneo linapoishia Daraja la ghorofa tatu katika eneo la Ubungo kuelekea Chalinze ili itanuliwe kwa lengo la kurahisha usafiri katika jiji la Dar es salaam.

Rais Magufuli amewataka Makandarasi wanaojenga Daraja la Tazara na Ubungo kuharakisha ujenzi wa madaraja hayo usiku na mchana ili yaweze kumalizika kwa wakati ama kabla ya muda huo katika kurahisisha maendeleo ya kibiashara katika jiji la Dar es salaam.

”Dar es salaam ni jiji la kibiashara hivyo hakuna budi miundombinu yake ya usafiri iweze kurahisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani ya jiji na nje ya jiji la Dar es salaam” amesema Rais Magufuli.

Mhandisi wa Masuala ya Usalama wa Ujenzi Mhandisi Richard Baruani amemueleza Rais Magufuli kuwa Ujenzi wa Daraja la Tazara umefikia asilimia 64 ambapo Daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2018.

Kwa upande wa Daraja la ghorofa tatu la Ubungo, Mhandisi Mshauri Reginald Kayanga amesema  ujenzi wake unatarajiwa kuanza rasmi Desemba 2017.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

15 Novemba, 2017

Serikali Yalifutia Usajili Shirika la TSSF Lililotangaza Kutoa Mikopo kwa Wanafunzi

Serikali yawatahadharisha wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadanganya walimu wastaafu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 16

Mabasi ya Kilimanjaro yafungiwa kusafirisha abiria baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.

$
0
0
Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha utoaji wa huduma za usafiri kwa kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express Limited baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kampuni hiyo kutokuzaa matunda.

Kayombo amesema biashara ya mmiliki huyo kwa kipindi cha hivi karibuni haikuwa nzuri kwani mabasi yake 26 yalipungua hadi kufikia 12 lakini si kigezo cha kutokulipwa kwa kodi ya Serikali.

“Ni kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni jambo ambalo lilitufanya sisi kusimamisha shughuli tangu Jumatatu (ya Novemba 13) hadi hapo atakapolipa kodi anayodaiwa,” amesema Kayombo

Kwa upande wake, mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya amesema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani Kilimanjaro huku akieleza kuwa ni kweli anadaiwa lakini amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.

Amesema hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35 milioni lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiasi chote kilichobaki cha Sh500 milioni huku akieleza kwamba mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia mwafaka na kurejea kutoa huduma

Kilimanjaro ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Moshi na Arusha kwa zaidi ya miaka 20 ni kampuni tanzu ya Kilimanjaro Cargo Truck.

Ndege Yaanguka na Kuua 11 Arusha

$
0
0
Shirika la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana  asubuhi limesema kuwa watu wote 11 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki dunia.

Coastal wameeleza kuwa, ndege yao, Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki katika eneo la Empakaai, Ngorongoro ikiwa na rubani mmoja na abiria 11 wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti.

Shirika hilo limesema kuwa majina ya waliofariki katika ajali hiyo bado hayajawekwa wazi wakisubiria kuwajulisha ndugu zao.

Mkurugenzi Mkuu wa Coastal, Julian Edmunds amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana, na kwamba mara kadhaa amekuwa akisafiri na ndege za shirikia hilo na hivyo anaimani na marubani pamoja na ndege zao.

Aidha, ameeleza kuwa kwa niaba ya shirikia hilo na wafanyakazi wake, watafanya kila litakalowezekana ndani ya uwezo wao kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo kwani hakuna kitu cha umuhimu kwao zaidi ya usalama wa abiria.

Kwa sasa wameeleza kwamba wanafanya uchunguzi katika eneo la tukio na kuwa, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa kamili zitakapopatikana.

Lowassa Amjibu airi Mkuu Sakata la Katiba Mpya

$
0
0
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemtumia ‘salamu’ Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwamba gharama za kuandaa Katiba Mpya si kubwa ukilinganisha na mahitaji ya Watanzania.

Akihutubia mamia ya watu katika viwanja vya Soko Kuu la Kwa Mromboo jijini Arusha juzi, Lowassa alimsihi Rais John Magufuli kuruhusu mjadala wa Katiba Mpya kwa kuwa ndiyo kiu ya Watanzania kwa sasa.

“Wananchi wamesema Rais Magufuli aruhusu mjadala wa Katiba Mpya, lakini waziri mkuu wake amesema ni gharama sana mimi nasema gharama hizo ukilinganisha na idadi ya watu wanaohitaji jambo hili ni kubwa sana atukubalie tujadili Katiba Mpya,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

Baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo ni Godblesss Lema (Arusha Mjini), Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) na meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro.

Lowassa, awali aliwauliza wananchi: “Tunahitaji Katiba Mpya hatuhitaji?” na wananchi walijibu: “Tunahitaji.”

“Mimi pendekezo langu ni kwamba mheshimiwa Rais kwa heshima zote akubali mjadala wa Katiba Mpya,” alisisitiza Lowassa.

Hata hivyo, Lowassa aliwaambia watu waliohudhuria mkutano huo kuwa jambo jingine lililomfikisha mbele yao ni kuwashukuru kwa dhati baadhi ya Watanzania walivyompigia kura mwaka 2015, kwa sababu alizuiwa kuzunguka nchi nzima.

Awali, mgombea udiwani wa Chadema, Simon Mollel alitaja vipambele vyake kuwa ni kushughulikia kero za jamii hususan maji na kuwaomba wananchi wamchague.

Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne

$
0
0
Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne
 
Kutana Maajabu ya Mtabibu MAALIM MOHAMEDI MASUDI Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..
MAALIM MOHAMEDI MASUDI ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
 
Je unasumbulia na Mapenzi..?
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na MAALIM MOHAMEDI MASUDI Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
Wasiliana na MAALIM MOHAMEDI MASUDI Kwa Majibu ya Maswali yako..

Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA.

Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.
Wasiliana nae kwa namba
0655516982
0688856265
0621898709(Whatsapp)

Mbowe: Masha hakuwa na msaada wowote Chadema

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe

\Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.

Je,una Upungufu Wa Nguvu Zakiume,kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa,kufika Kileleni Mapema Na Kushindwa Kurudia ????

$
0
0
Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa na mambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA nk.

Upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa, mahusiano mengi kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,
1 KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA 
2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA 
3 KUWAHI KUFIKA KILELENI 
4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI 
5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO LA NDOA KABISA.

TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.

PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK 

WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO 

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha vidonda vya tumbo,korodani kuvimba,na anatoa dagu za utajiri kwa wanaohitaji bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM,NAUTALETEWA POPOTE ULIPO.

 SIMU; NO 0767145357/0629034550.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 17

Profesa Kitila Mkumbo ajiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)

$
0
0
Profesa Kitila Mkumbo amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), taarifa ya Prof. Mkumbo kujiunga CCM imetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images