Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Alichokisema Mama Kanumba Baada Ya Lulu Michael Kuhukumiwa Miaka Miwili

$
0
0
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipozikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.

Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.

“Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano“

“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani”
  Mama Kanumba

Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.

Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Maneno ya Diamond kwa Lulu Michael Baada ya Kuhumiwa Miaka Miwili

$
0
0
Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema hukumu ya miaka miwili aliyopewa mwigizaji Elizabeth  Michael maarufu Lulu siyo adhabu bali ni mtihani ambao unalenga kumfanya kuwa imara zaidi.

Amesema mwigizaji huyo ambaye leo Jumatatu Mahakama Kuu imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela, amechaguliwa na Mungu kwa kuwa anaamini anao uwezo wa kuhimili mikikimikiki.

Katika mtandao wa Instagram, Diamond anayetamba na wimbo Halleluyah, ameandika:  "Mwenyezi Mungu ameamua kukupa mtihani huu wewe kwa sababu anaamini wewe ni shujaa na imara...pia anaamini wewe ndio msichana pekee unayeweza kuuhimili mtihani huu... hivyo usisononeke, Make him Proud.”

Mbali na Diamond, wasanii wengine wametuma salamu za pole kwa Lulu akiwamo Wema Sepetu, Mboni Masimba, Snura, Dj Choka, Dk Cheni na wengine wengi.

Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na Lulu kwa muda mrefu amesema huu ni wakati wa kumuombea Lulu kwa kuwa hakuna anayejua kesho atapata mkasa gani.

Katika mtandao wa Instagram aliweka picha ya Lulu na kuandika: "Tumuombee mtoto huyu kwa kuwa hakuna anayeijua kesho yake,".

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Serikali Yamuonya Zitto Kabwe.....Yatishia Kuifuta Manispaa ya Mji wa Kigoma Ujiji Inayoongozwa na Chama Chake

$
0
0
Serikali imeionya Manispaa ya Mji wa Kigoma Ujiji kuacha kuendelea kuwasiliana na Mpango wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) na kama ikiendelea itachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kuvunja Baraza la Madiwani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kujiondoa katika mpango huo mapema mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema bungeni leo Jumatatu wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe ambaye chama chake kinaongoza manispaa hiyo.

Zitto katika swali lake la nyongeza amesema kuwa nchi za Hungary na Urusi ambazo Serikali inasema nazo  zimejitoa katika mpango wa OGP ni miongoni mwa nchi zinazoendeshwa kidikteta kwa kutofuata utawala bora.

"Nchi za Hungary na Urusi zinaendeshwa bila kufuata demokrasia zinaendeshwa kidikteta ni aibu sana kwa Serikali kusema inaiga nchi ambazo zinaenda kinyume na demokrasia," amesema.

Amesema majukwaa hayo ya kimataifa yanatengeneza mahusiano na kwamba Canada ni mwenyekiti wa mpango huo.

Hata hivyo, amesema juzi ameona Rais John Magufuli amemwandikia Waziri Mkuu wa Canada kuhusu suala la Bombardier.

"Serikali haioni kwamba ingeendelea kuwa mwanachama wa OGP na mwenyekiti ni Canada hili ombi lingeshughulikiwa kwa uzito zaidi," amehoji Zitto.

Zitto amesema Manispaa ya Kigoma Ujiji ni miongoni mwa miji 15 duniani ambayo ipo katika mpango huo na kwamba Serikali inatoa kauli gani juu ya ushiriki wa mji huo  katika OGP ambayo imekuwa ikifaidika na mpango huo na miji mingine inayotaka kuingia katika mpango huo.

Akijibu hayo Mkuchika amesema Tanzania imejitia katika mpango kwa hiari yake  yenyewe na kwamba hawajaiga nchi yoyote.

"Sisi ni Taifa huru linalojitawala linalofanya matumizi yake yenyewe, bila kushurutishwa na Taifa lolote liwe dogo ama kubwa duniani," amesema.

Amesema Canada na Tanzania ni wanachama wa Jumuiya ya Madola na pia Tanzania ina ubalozi wake na hivyo kuwa mwanachama wa OGP na kutokuwa mawasiliano na nchi hiyo haiwezi kuwa tatizo.

Amesema andiko la mpango huo linasema nchi ikijiondoa uanachama na washirika wake wote shughuli na uanachama unakoma.

Hata hivyo, amesema kuwa Serikali ina taarifa kuwa Manispaa ya Kigoma Ujiji bado inaendelea na mpango huo na OGP walimwandikia waziri wa mambo ya nje kuwa bado wana nia ya kuendelea na halmashauri hiyo.

"Sasa nataka kupitia Bunge lako tukufu kuionya Manispaa ya Ujiji kutoendelea. Nchi inayozingatia utawala bora haiwezi Serikali kuu ikafanya maamuzi lakini baraza la madiwani likasema haliwezi kutekeleza. 

"Nataka nionye Halmashauri ya Kigoma Ujiji iache mara moja. Yale ni maamuzi ya Serikali na wakiendelea kufanya mawasiliano kama wanavyofanya sasa Serikali itachukua  hatua kali za kisheria na nyinyi mnajua kwenye baraza la madiwani hatua kali za kisheria ni kulivunja baraza na kuunda Tume ya Manispaa," amesema.

Mkuchika ameomba madiwani na Zitto kutoifikisha Serikali huko.

Katika swali lake la msingi Zitto amehoji kwanini Serikali imeamua kujiondoa kwenye mpango huo.

Akijibu Mkuchika amesema Serikali imejiunga na mipango ya kikanda na kimataifa mbalimbali hivyo ni maoni yake kuwa shughuli zinazotekelezwa kupitia mipango hiyo mingine kupitia vyombo mbalimbali inatosha kwa nchi kujijengea misingi imara ya uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi kuongeza uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa.

Mkuchika amesema kujitoa katika mpango huo hakuna madhara yoyote.

Kigwangala amshambulia Nyalandu, amkabidhisha kwa Takukuru

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala amemlipua waziri wa zamani wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka na kumlalamikia kupoteza mabilioni ya fedha za Serikali.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018, Bungeni Jijini Dodoma, Dk Kigwangalla ameiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.

Dk Kigwangala amesema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

Mbali na tuhuma hiyo, pia alimtuhumu kutumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni, kipindi cha kampeni zake za kugombea urais 2015, wakati kampuni ya raia huyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.

Hata hivyo wakati Kigwangala akitoa tuhuma hizo tayari Nyalandu alishasema kuwa tuhuma ambazo zimeanza kuibuliwa mitandao dhidi yake si za kweli bali zinalenga tu kumchafua.

Taarifa hiyo imekuja kipindi ambacho Lazaro Nyalandu amejiondoa CCM na kujiunga CHADEMA.

Serikali kupiga mnada ng’ombe 10,000 wa Rwanda, Uganda

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametangaza kupiga mnada ng'ombe zaidi ya 10,000 wa nchi za Uganda na Rwanda waliokamatwa katika operesheni inayoendelea nchini.

Mpina alitangaza hayo leo Jumatatu bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019.

Waziri huyo ambaye alikuwa akijibu hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wabunge amesema ng'ombe hao watapigwa mnada wakati wowote kama ilivyofanya kwa ng'ombe 1,325 wa Kenya.

Amesema uhusiano wa Tanzania nchi nyingine washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mzuri na akisisitiza hakuna ushirikano wa kihalifu.

Mpina amesema walioingiza ng'ombe hao ni wahalifu na wamevunja sheria za nchi na kutahadharisha wafugaji wa nchi jirani kufuata sheria wanapotaka kuingiza mifugo nchini.

Mbowe Amvaa Profesa Lipumba

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amedai kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa chama alichokijenga.

Akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Mtwara, Mh. Mbowe amesema kwamba hana ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu.

Mh. Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha.

"Sina ugomvi na Prof Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni Profesa wa ajabu kweli kweli. Mimi simuogopi mtu nitazungumza straight. Amesema Mbowe

Pamoja na hayo Mbowe amedai kwamba Spika wa Bunge pamoja na Msajili wa vyama vya siasa wanatumika katika kuibomoa CUF na kuongeza kwamba hataacha kusema ukweli kwani hakuna mtu yoyote anayemuogopa isipokuwa Mungu pekee.

Ameongeza kwamba kasi inayotumika kuibomoa CUF inatumika pia kuibomoa CHADEMA na kuweka wazi kwamaba siku chama cha Chadema kikiuliwa labda awe amefariki lakini siyo wakati huu ambao bado anapumzi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 14


Vyama vya siasa vyatakiwa kufanya kampeni kwa kuzingatia taratibu za uchaguzi

$
0
0
Hussein Makame-NEC
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistolces Kaijage amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya Uchaguzi.

Jaji Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa NEC na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam jana Novemba 13 kuelekea Uchaguzi mdogo wa madiwani.

Alisema iwapo ukiukwaji au uvunjaji wa Maadili hayo utatokea, Chama au Mgombea awasilishe malalamiko hayo mbele ya Kamati husika ili ishughulikiwe kisheria.

Aliwakumbusha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume inayo mamlaka ya kuruhusu kuwepo kwa Kampeni za Uchaguzi katika maeneo ya Uchaguzi na siyo Mikutano ya Vyama vya Siasa.

Hivyo, kampeni hizo zifanyike kwenye Kata husika na inategemewa kuwa Mikutano ya Kampeni italenga kuwashawishi, kwa namna ya kistaarabu, wananchi wa Kata husika ili wamchague Mgombea anayefanyiwa kampeni.

”Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1. (c) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 tunategemea kila Chama cha Siasa kiendelee kufanya Kampeni kwa mujibu wa ratiba. Kampeni zote zinatakiwa kuanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni,” alisema Jaji Kaijage.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Tume imekwisha kutoa ushauri kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya ili katika kipindi hiki cha Uchaguzi wahakikishe wanazingatia wajibu wao na ukomo wa madaraka yao katika shughuli za Uchaguzi kuanzia kipindi cha Kampeni hadi kutangazwa kwa Matokeo.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kailima Ramadhani aliaviomba Vyama vya Siasa kuwahimiza wanachama na wapenzi wao walioandikishwa kuwa Wapiga Kura wajitokeze Siku ya Uchaguzi kwenda Kupiga Kura zao bila hofu yoyote kuhusu usalama wao.

“Ni imani ya Tume kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa mtakuwa chachu ya kuwaongoza na kuwaelekeza wanachama, wafuasi na mashabiki wenu katika kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu,” alisema Kailima.

Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017 ambapo wapiga kura 333,309 wanategemewa kupiga kura siku ya uchaguzi huo.


VIDEO: Waziri Mpina Akiongelea kuhusu uchomaji wa vifaranga kutoka Kenya

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema serikali ilichoma vifaranga 6,400 kutoka Kenya ili kuzuia magonjwa ya ndege lakini pia mmiliki hakuwa na vibali na vifaranga havikukaguliwa.

==>Msikilize hapo chini

Lazaro Nyalandu amjibu Waziri wa Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amemjibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kuhusu tuhuma ambazo amezitoa juu yake wakati akizungumza bungeni  jana Novemba 13, 2017.

Nyalandu andika katika mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa anasikitishwa na namna Dkt. Kigwangalla anavyotumia muda mwingi kumchafua mara baada ya yeye kutangaza kujivua uanachama wa CCM na kauli anazotoa dhidi yake ni za uongo.

Nyalandu ameandika;

INASIKITISHA sana kuona WAZIRI Kigwangalla akitumia MUDA wake ndani ya BUNGE leo kunichafua, kunidhihaki, na kusema UONGO na UZUSHI dhidi yangu, ikiwa ni NJAMA za makusudi zilizopangwa kunichafua mara baada ya mimi kukihama Chama Cha Mapinduzi -CCM. Aidha, hatua hiyo imepangwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama kudiriki tena kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM katika Serikali hii ya awali ya tano. AIDHA, Waziri Kigwangalla anatumika VIBAYA, kwa kauli za UONGO na UZUSHI aliuanza DHIDI yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza kutoa kauli za kejeli dhidi ya UTUMISHI wangu uliotukuka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wenye REKODI thabiti.

NIANZE na UZUSHI alioutoa Waziri Kigwangalla mapema leo BUNGENI, huku moyoni mwake akiwa anajua fika kuwa ametumwa kusema UONGO dhidi ya Waziri Nyalandu kwa lengo la kuandaa MAZINGIRA ya kumkamata na kubwa zaidi, kudhalilisha azma ya WATANZANIA ambao WAKO tayari kwa mabadiliko ya UONGOZI wa nchi kupitia UPINZANI. AIDHA, propaganda za Kigwangalla ameamua zimuhusu Waziri moja tu wa Maliasili, tangu TAIFA kupata Uhuru. Waziri huyu ni Nyalandu, jambo linalothibitisha NJAMA na Progaganda za kuzimisha MOTO na nguvu ya umma kupitia UPINZANI, hasa baada ya kitendo changu Cha kukihama CCM.

1) WAZIRI Kigwangalla amekejeli kuwa Waziri Nyalandu alitumia Fedha za Serikali kusafiri USA na mwanadada Aunt Ezekiel. -HABARI hii ilikuwa ya KUZUSHA na ilichunguzwa na vyombo vya dola 2014 na kuthibitika ilitungwa na ilikuwa ya UONGO. Katika Mkutano huo wa Washington, DC, Waziri Nyalandu alialikwa na Balozi wa Tanzania, Marekani, na alipewa RUHUSA ya maandishi na Serikali kuhutubia Mkutano huo kwa siku Moja. Wasanii wote
 
Walioalikwa, akiwepo Mwanadada Aunt Ezekiel, hawakuwa na mwaliko wa Wizara ama Serikali, bali waandaji wa Kongamano. Na Serikali haikulipa gharama zozote kwao.(Mthibiti Na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza kuthibitisha)

2) Waziri Kigwangalla amedanganya BUNGE kuwa Waziri Nyalandu alitumia helikopta kugombea URAIS 2015.
-Habari hii ni ya uzushi na UONGO, na Waziri atakuwa aidha hana BUSARA ambayo angepaswa kujiridhisha na Taarifa kabla ya kuisoma Bungeni, ama waliomtuma wamemwambia ASOME TU hivyo hivyo. UKWELI ni kuwa, Waziri Nyalandu, alipokuwa CCM, aligombea katika kinyang’anyiro cha URAIS kuomba kuteuliwa ndani ya CCM, na alitumia aidha usafiri wa MAGARI au NDEGE za kawaida kwa kulipa nauli (fixed wings pale ilipobidi), hadi mchakato ulipoisha kama uilivyoisha.
 
-AIDHA, miaka yote nikiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, nimekuwa nikifanya kampeni za kumalizia kwa njia ya helikopta. Inawezekana Waziri Kigwangalla haelewi hili, lakini naomba nimjulishe TU kuwa matumizi ya helicopta ilipobidi yalisaidia kufika baadhi ya maeneo Jimboni kwangu wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2000, 2005, 2010, na 2015.
-AIDHA, Mwaka 2015 nilitumia Helicopter kwa SIKU TATU za kumalizia Kampeni, na nilikodi helikopta hiyo kwa Sh milioni tano kwa siku (Jumla, milioni 15)
 
-Pia ingependeza kama hamaki za Kigwangalla zingemkumbusha kuwa Waziri Nyalandu akiwa Wizarani ALIPATIA Serikali Helikopta mpya Moja, alileta ndege kwa matumizi ya kupambana na Ujangili, Alishawishi Benki ya dunia, Ujerumani na USA kuleta mamilioni ya dola za kmarekani kusaidia mapambano hayo, na kwamba alifanikiwa Sana kutokmeza ujangili nchini. RAIS KIKWETE alikiri hili wakati wa kuzindua Tangazo la Tanzania (Tanzania, the soul of Africa). 3) Kigwangalla amezusha kuwa Waziri Nyalandu alitumia vibaya madaraka yake. Amezungumzia suala la Waziri Nyalandu kutotia sahihi TOZO mpya zilizopendekezwa na TANAPA. Jambo ambalo Waziri Kigwangalla angepaswa kulijua kabla ya kutoa kauli isiyo sahihi Bungeni ni kuwa SAKATA la TOZO za Tanapa lilijadiliwa BUNGENI mbele ya Spika Mama Anne Makinda, likiwa limeletwa na Kamati ya Lembeli, na kwa kupitia Wizara, Waziri Nyalandu alilitolea ufafanuzi na likamalizika na GN ilitolewa.
 
-SAKATA la kupandishwa ghafla kwa TOZO za mahotelini zinazojulikana kama (Fixed Rates) lilianza kabla sijawa Waziri. Aidha, kulikuwa na kesi Mahakama Kuu, ambako hadi kufikia mwaka 2012, uamuzi wa Mahakama uliyotolewa. Bado Nyalandu hakuwa Waziri. Aidha, nilipoteuliwa kama Waziri, Nikatazama SAKATA hilo ambalo lilishachukua muda mrefu sana hadi kufikia 2014, mimi nilipokuwa Waziri. Sheria inasema ”Concession Fees shall be 10% of half Board”, na kulikuwa Na GN ya Serikali kuhusu TOZO hizo, takribani kuanzia mwaka 2002. Hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu ilielekeza kuwa TOZO zozote mpya ni sharti zipate GN mpya, na sheria ya msingi ilitaka TOZO ziwe kwa asilimia (percentage), na sio TOZO za kukisia, (fixed rate) ambazo ndio msingi mkubwa wa kupendeleana na rushwa katika kupanga nani alipe kiwango gani Cha kodi. Baada ya kuitolea maelezo Bungeni (na hansardi Zipo), Bunge na Wizara tulikubaliana namna ya kulimaliza na ndivyo ilivyofanyika na GN ilitolewa. Uamuzi wangu kama Waziri ulizingatia matakwa ya sheria na Kanuni. Waziri Kigwangalla hajasema ukweli na amezusha kuhusu suala hili kwa sababu anazozijua mwenyewe.

4) Sakata la VITALU: Inasikitisha SANA na inatia AIBU kwamba Waziri atalihadaa BUNGE kwamba Waziri Nyalandu amehusika na kuuza VITALU au kugawa VITALU, na baya Zaidi kwa NJIA ya RUSHWA. -Sheria ya Wanyamapori inatamka wazi kuwa VITALU vitagawiwa kwa wawindaji kwa kila baada ya miaka MITANO. -Mara ya mwisho VITALU vimegawiwa Januari, 2017. Nyalandu hakuwa WAZIRI. (Waziri alikuwa Mh. Prof Maghembe)
-Kabla ya hapo, VITALU viligawiwa mwaka 2013. Nyalandu hakuwa Waziri. (Waziri alikuwa Mh Maige)
Hii ni AIBU sana na natumaini kwa Waziri Kigwangalla na wanaomtuma wangetamani sana miaka ibadilike ili isomeke Waziri Nyalandu.

5) Waziri Kigwangalla amedai kuwa Waziri Nyalandu alikuwa anafanyia Kazi katika Chumba maalumu katika hoteli ya Serena. Naomba Waziri Kigwangalla, athibitishe ni Chumba namba ngapi, na wahusika wa hoteli pia wathibitishe. Kama Waziri, nilifanya Kazi katika ofisi yangu iliyopo Wizaranya Maliasili na Utalii. Kigwangalla pia akumbuke mimi nilikuwa MTEULE wa Rais ambaye alikuwa na vyombo vya kumsaidia kusimamia Mawaziri.

6) MADAI kuwa Waziri Nyalandu ALIUZA Twiga mwaka 2011/12 ni ya AIBU, UZUSHI na UONGO kuzidi shetani mwenyewe. Mwaka 2011/12 Nyalandu alikuwa NAIBU WAZIRI wa VIWANDA na BIASHARA! Uongo huu ni wa aibu na ni kazi ya Shetani Lusifa mwenyewe, na MUNGU wa mbinguni awakemee wote wanaohusika.
 
7) Mbwembwe hizi na kusingiziwa kunakofanywa kwa makusudi baada ya mimi Nyalandu kukihama CCM ni aibu kwa TAIFA na ni matumizi mabaya sana ya MADARAKA. Aidha, ifahamike kuwa Vitisho na njama dhidi yangu na familia yangu kunakofanywa na wote wanaohusika hakutazimisha azma ya watanzania kutaka mabadiliko ya kweli nchini. Imeandikwa, WAONGO wote, sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto kwa kiberiki. Haki huinua Taifa, na uonevu na dhuluma ni dhambi itakayowatafuna wahusika siku zote za Maisha yao. 

— —— ——
Lazaro S. Nyalandu

Serikali Yatoa Majibu Bungeni Kuhusu Kujenga Uwanja wa Ndege Chato

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani Chato utakapokamilika utatumika kusafirisha madini, watu na vifaa.

==>Msikilize hapo chini akitoa majibu bungeni

Kauli ya Mbowe yaikera Serikali......Waziri Amtaka Aache Kuingilia Madaraka ya Rais

$
0
0
Serikali imemjia juu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kutokana na kauli yake kuwa Rais John Magufuli amekuwa akipendelea baadhi ya kanda katika uteuzi wake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama jana Jumatatu jioni alisema Mbowe anapotosha na kumtaka aache kuingilia madaraka ya Rais.

Wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019, Ijumaa iliyopita Mbowe alienda mbali na kudai anaweza kuleta uthibitisho kama Bunge litamkata kufanya hivyo.

“Mumwambie bwana mkubwa unapoamua mambo mengine tenda haki pande zote. Lakini unapokuwa haki hiyo unaipeleka mahali fulani na unakandamiza upande mmoja unawanyima haki”

Mbowe alitolea mfano wa teuzi mbalimbali alizozifanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani mwaka 2015, akisema hazikugawanywa kwa usawa wa mikoa kama utamaduni uliokuwepo awamu zilizopita.

Hata hivyo, jana Jumatatu jioni Jenister amesema Ibara ya 36 (1) (2)(3)(4) imempa Rais madaraka ya kuanzisha na kufuta ya nafasi za mbalimbali kwa utumishi na haijasema atazingatiwa usawa wa kanda.

“Ibara hiyo haisemi kuwa Rais wakati atakapokuwa anafanya uteuzi eti aangalie ukanda. Haisemi hivyo Ibara hiyo haisemi anavyoandaa uteuzi aaangalie makabila mbalimbali,”alisema Mhagama.

“Unasimamaje ndani ya Bunge kuhoji madaraka ambayo Rais amepewa kwa mujibu wa Katiba? Alihoji Mhagama na kutoa mifano ya teuzi tatu zilizofanywa na Rais kutoka mikoa ya Kaskazini.

“Ameteuliwa Aggrey Mwandry kutoka Siha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na anafanya kazi vizuri sana. Ameteuliwa Alexander Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara,”alisema na kuongeza

“Ameteuliwa Anna Kilango kutoka Same. Nina orodha ndefu lakini uteuzi huo unafuata madaraka ya kikatiba. Niwaombe sana wabunge tusiingile madaraka ya Rais aliyopewa kwa mujibu wa Katiba.”

Alisema Rais amekuwa akifanya teuzi mbalimbali kwa utashi wa hali ya juu na anateua watu wa kubeba dhamana ya kumsaidia kuongoza kwa niaba yake pasipo upendeleo.

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Tiba ya Asili ya Pumu, Vidonda vya Tumbo, Busha na Nguvu za Kiume

$
0
0
Tatizo La Upungufu Wangu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Ile Tiba Sahihi Ya Matatizo Haya 

CHAZO CHAKE NA VISABABISHO VYAKE:
DALILI:-Mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata Choo vizuri hata ukipata Choo kinakuwa kigumu Kama cha mbuzi ,Misuri  kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. Miguu kuuma na kuwaka au kufa ganzi

TIBA YAKE:
RADI-90-POWER---Ni dawa ya vidonge asilia iliyo tengenezwa kutokana na miti shamba yenye uwezo mkubwa kabisa ktk kutibu matatizo (4) Kwa wakati ==>(1)Huongeza nguvu za kiume maradufu (2)kati ya umri (15-90)(3)hurefusha na kunenepesha uume mdogo kadrii upendavyo inch (6-8)kwa dakika (15)tu.(4)kuchelewa kufika kileleni (5)kuimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa. 

Nini huchangia kuwa na matatizo Kama haha? Kisukari,Presha,Ngiri,Zinaa,Kiuno kuuma, Tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kutopata Choo vizuri, Mgongo kuuma. 

RADI-90-POWER:-Hutibu na kumaliza matatizo haya kwa mda mfupi tu na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika(45)kwa tendo(1) na utarudia Mara (5)na zaidi bila kuchoka huanza kazi baada ya dakika( 30)tu.Pia huongeza Hamu ya kufanya tendo la ndoa maradufu(2),Kumbuka tatizo hili si geni, kigeni ni tiba sahihi ya kutibu matatizo haya na pia ina guarantee ya miaka(65)na zaidi. 

Tunatibu :---Kisukari, Presha, uzazi, Ngiri, Pumu, maralia sugu, vidonda vya tumbo, chango aina zote, kifua kikuu na busha bila upasuaji. 

ITUJA NO2:--Nidawa ya mvuto wa biashara, kazi, kupandishwa cheo, kupendwa na mwajiri, kumvuta mme/mke,mpenzi, hawara, mchumba unaye muhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zake kwa dhati utampata kwa lisaa limoja (1)tu na atatulia daima na kumfunga asitoke nje ya ndoa.

BOMBA2:--Ni dawa ya kupunguza matiti makubwa, unene turbo, kitambi,mafuta mwilini,uzito,toa fangasi makovu, chunusi, nyama zembe, michirizi, kwa siku tatu (3)tu.NO7:--Inaongeza makalio, Hips, miguu kwa saizi uipendayo kwa siku (2)tu.

HUDUMA HIZI Na zingine nyingi UTAZIPATA popote TANZANIA Name NJE YA NCHI:--MUONE DR SHARIF AU PIGA SIMU NO:-0659347707, 0763483813 ,0688991509,0659347707.  DR SHARIF

Jeshi Latishia Kuingilia Kati Mgogoro wa Kuwania Madaraka Zimbabwe

$
0
0
Jeshi la Zimbabwe limeonya kuingilia kati mgogoro unaoendelea kati ya viongozi wa chama tawala cha ZANU-PF, baada ya Rais Robert Mugabe kumfukuza kazi aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga amefanya mkutano na vyombo vya habari akiwa na viongozi wengine waandamizi 90 wa jeshi hilo na kutoa onyo hilo.

Amesema endapo wapigania uhuru wataendelea kugombana kuhusu madaraka, jeshi hilo halitasita kuchukua hatua.

“Kung’olewa madarakani kunakoendelea sasa, ambako kwa uwazi kunalenga wajumbe wa chama ambao walipigania uhuru, lazima kusitishwe,” alisema Jenerali Chiwenga.

“Tunawakumbusha wanaofanya hivi kuwa katika masuala ya kulinda mapinduzi yetu, jeshi halitasita kuingilia kati,” aliongeza.

Rais Mugabe alimfukuza kazi Makamu wake wa Rais akieleza kuwa amekuwa akiendesha kampeni ya chinichini ya kutaka kumrithi bila kufuata utaratibu wa chama.

Pia, alidai kuwa Mnangagwa alienda kwa watabiri na waganga akitaka kujua ni lini Mugabe atafariki dunia.

Inaaminika kuwa baada ya Mnangagwa kuondolewa, mke wa Rais Mugabe, Mama Grace ndiye anapewa nafasi zaidi ya kurithi kiti cha urais kwa tiketi ya ZANU-PF.

Kitabala: Lulu Anaweza Kupata Dhamana Akisubiri Rufaa Kusikilizwa

$
0
0
Wakili wa Elizabeth Michael ‘Lulu’, Peter Kibatala, kufuatia hukumu ya miaka miwili dhidi ya Lulu jana, ametoa ufafanuzi kupitia akaunti yake ya Instagrame kuhusu kitakachofuata alipoulizwa maswali na watu wengi ambapo alitumia fursa hiyo kuwafafanulia sheria inavyosema kuhusu nini kinafuata.

Majibu yake kwa maswali hayo ni yafuatayo:
  1. Amesema kuwa hakuna hukumu tofauti inayoweza kutolewa kabla mhukukiwa hajatumikia theluthi ya kufungo chake ambacho kwa Lulu itakuwa ni kuanzia miezi  mitano.
  2.  Ndani ya hiyo miezi mitano dhamana inaweza kuombwa wakati wakisubiria rufaaa ianze kusikilizwa.  Kwa maana hiyo anaweza kutoka kwa dhamana muda wowote mahakama ikmpatia dhamana.
  3. Huwezi kuacha kijana wa miaka 22 mwenye maisha marefu mbele yake ahukumiwe kwa uhalifu kwa sababu ya suala la muda, kwani itaharibu maisha yake ya mbele. Kwa hiyo rufaa imelenga katika kuondoa tatizo hilo.
  4.  Kukata rufaaa na kuomba dhamana  na kufanya kazi za jamii vinaweza kufanyika kwa wakati mmoja wakati suala hili likisubiriwa kusikilizwa na mahakama ya rufaa.
==>Huu ndo Ujumbe wa Kitabala katika Instagram yake

Ujumbe Mzito wa Afande Sele Baada Ya Lulu Kuhukumiwa

$
0
0
Baada ya mrembo katika tasnia ya filamu, Elizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa miaka 2 jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu, Steven Kanumba, kuna mengi yanazungumzwa kupitia mitandao ya kijamii.

Afande ameandika ujumbe huu…
Nakumbuka vizuri saana mwaka 2006 yaani miaka miwili tu baada ya mimi kushinda taji la ufalme wa rhymes Tz na kukabidhiwa ile gari maridadi sana ya zawadi aina ya toyota sera yenye milango ya kubinuka kama mabawa ya ndege anaejiandaa kuruka….Jumamosi moja ktk mwaka ule nikiwa kwenye ubora wangu wa hali ya juu na ushawishi mkuu kuliko msanii yeyote Tz nilialikwa kutumbuiza Tabata kwenye ukumbi wa Dar West uliokua maarufu sana nyakati zile…

Lkn wakati nikiwa back stage kabla sijapanda jukwaani huku usiku ukiwa umetamalaki yaani ule usiku wa manani au usiku wa manane kama wengi tulivyozoea kusema ingawa tunakosea nikashangaa nashikwa begani na mtu aliyekua nyuma yangu ambapo kulikua na watu wengi tu😴…nilipogeuka niangalie ninani aliyenishika bega”Hammad”nikamuona Lulu michael aliyekua bado ni bint mdogo sana ingawa tayari alikua na umaarufu si haba labda kwa sababu ya hayo maigizo yao ambayo baadae wakayaita filamu au bongo movie lkn pia wkt flani Lulu alishawahi kuwa mtangazaji wa kipindi cha watoto ktk kituo cha ItV…

nilipomuona akaniamkia kwa bashasha namimi nikaitikia huku sura yangu nikiikunja na kuwa ya kuogofya kisha nikaamuuliza kwa ukali kidogo ni kwanini yupo pale ukumbini ktk muda ule ambao kwa umri wake hakupaswa kuwepo?..

lulu hakua na majibu ya maana na papo hapo nikamtoa nje ya ukumbi na kisha nikamtuma dereva wangu wkt ule alikua home boy wangu ephraim nguzo aka bad card amrudishe nyumbani kwao haraka na ahakikishe mama yake amempokea…

Bad alifanya hivyo kiroho safi akarejea ukumbini na akanimbia kuwa alitimiza yote niliyomuagiza ukizingatia na yeye badi tayari alikua na familia hivyo aliujua vyema uchungu wa mwana…

lkn miezi michache baadae nikaja kupigwa butwaa baada ya kusikia kuwa et kale kabint lulu kumbe tayari kalikua na ukaribu usio wa kawaida na baadhi ya hao wasanii mabazazi wa maigizo wasiokua na utu wala aibu😢…niliumia sana moyoni nikiwa kama mzazi wa mtoto wa kike ninaempenda sana na kutamani kumuona akitimiza ndoto zake muhimu kwenye maisha kama kupata elimu kwa wkt muafaka…

lkn niliumia zaid baada ya matatizo aliyoyapata lulu kupitia kanumba na kwa hakika sikua miongoni mwa waliohuzunika wala kushiriki kivyovyote ule msiba wa kanumba ingawa wkt wote wa pilika za msiba ule mimi nilikua dar tena palepale sinza msiba ulipokuwepo…sikutaka kuvaa joho la unafki kama ilivyo kwa waTz wengi…

kwangu hata sasa kanumba ni mtu mbaya na alifanya kitendo kibaya kabisa dhidi ya bint mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio.kumtumia kwa sababu ya umaarufu wake…

leo kanumba amepumzika au anapambana na Mola wake kwa kutofuata yale maandiko yasemayo kuwa’TAMAA Ikichukua Mimba Huzaa Dhambi na Dhambi Ikishakukomaa Huzaa MAUTI…

Kanumba amevuna alichopanda lkn Lulu unyonge wa kiumri na udhaifu wa kisichana vimebakia kuwa mateso ktk maisha yake…

MUNGU ni mwema atamuafu Lulu amalize kifungo chake salama kama alivyompa kanumba haki ya matendo yake mabaya kwa kumlaza mapema…

Mwisho wa siku wote wawili wabarikiwe kwa kutufundisha tuliobakia ili tuchague njia sahihi za kupita….DUNIA..GUNIA…

Ruge afunguka Mazito kuhusu ndoa ya Zamaradi

$
0
0
Hatimaye Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezungumzia suala la ndoa ya mama watoto wake, Zamaradi Mketema.

Ruge amezungumzia suala hilo ikiwa ni wiki kadhaa tangu isambae sauti iliyoaminika kuwa ni ya kwake, akisikika mtu anazungumza na Zamaradi kwenye simu huku akilia kwa sauti ya mateso akilalama kuachwa.

Amesema kuwa kama mwanaume muungwana, huwa hazungumzii masuala ya ndani ya mahusiano yake ya kimapenzi, akitumia msemo wa kiingereza kuwa ‘Gentlemen don’t kiss and tell’, kwa tafrisi isiyo rasmi ‘hatubusi na kusimilia’. Msemo huu una maana ya kuwa wanandani hawasimulii kuhusu yao ya ndani.

Ruge amesema kuwa alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinaendelea kuhusu ndoa ya Zamaradi na kwamba alikuwa amempa baraka zote tofauti na ilivyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameshtukizwa na kuumizwa.

“Kila kilichofanyika nilikuwa na taarifa na kilikuwa na baraka zangu. Ni sehemu ya maisha tunapitia. Kubwa kuliko yote, nina watoto wawili ambao nimezaa na Zamaradi. Nina mheshimu mno na hadi sasa naendelea kumheshimu mno,” Ruge amefunguka kupitia kipindi cha Clouds 360.

“Unajua kama kuna kitu nitakufundisha [mtangazaji] kama mdogo wangu , ‘When you are a gentleman, you don’t kiss and tell’ (Ukiwa mwanaume muungwana, haubusi na kusimulia). Vitu vingine vinabaki kuwa vyako binafsi vya ndani,” aliongeza.

Ruge ameeleza kuwa hata wikendi iliyopita alikuwa na watoto wake aliozaa na Zamaradi na kwamba anawapenda sana na hataacha kumheshimu mama yao.

Amesema amelazimika kulizungumzia hilo ili kuweka kumbukumbu sawa na sio vinginevyo.

Zamaradi alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alikifanya kipindi hicho kuwa maarufu huku akishiriki kuandaa filamu zilizoshika mitaa ikiwemo filamu ya ‘Kigodolo’.

Magufuli atuma salamu kwa Nape na Bashe

$
0
0
Rais John Magufuli amewataka wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye na Hussein Bashe, ambao michango yao bungeni imekosoa uendeshaji uchumi, wampelekee majina ya wawekezaji wanaokwamishwa ili awape kazi.

Wabunge hao wa Mtama na Nzega Mjini waliikosoa Serikali wakati wa kujadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye alishutumiwa na wabunge hao kumpotosha Rais, alisema wakati akihitimisha mjadala huo kuwa alipigiwa simu na mkuu wa nchi na kuelezwa hayo.

“Naomba ninong’one na Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala, alinipigia simu na aliniambia hivi,” alisema Waziri Mpango.

“Waziri, mwambie ndugu yako mheshimiwa Nape na mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway.

“Wawalete hata kesho niko tayari kuwapa reli ya kutoka Kaliua –Mpanda au Isaka-Mwanza au reli ya Mtwara-Mchuchuma hadi Liganga waijenge.

“Hayo ni maneno ya mheshimiwa Rais. Natumaini waheshimiwa husika will raise up to this challenge from his excellence the president (wataifanyia kazi changamoto ya mheshimiwa Rais.”

Akijibu hoja za wabunge hao na wengine, Dk Mpango alisema si kwamba Serikali imeiweka pembeni sekta binafsi bali bado haijakaa vizuri na wakati mwingine inakuja na masharti yasiyotekelezeka.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images