Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Makamu wa Rais Samia awataka polisi wa Kike kupambana na ugaid, uchochezi na wizi wa mitandao

$
0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka polisi wanawake kupambana na vitendo vya kiuhalifu ikiwemo uchochezi, wizi wa mitandao, ujangili ugaidi na utakatishaji wa fedha haramu.

Hayo ameyasema jana  Novemba 9  akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao wa polisi wanawake yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha taaluma ya Polisi Kurasini.

Makamu wa Rais alisema suala la  kuwepo kwa ulinzi  ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.

Alisema  kwamba  kuwepo kwa polisi wanawake kumeleta mtazamo tofauti katika jamii, watu wamekuwa wakiona polisi ni rafiki wa umma.

Aliwataka polisi kufuata sheria katika matukio yote ya unyanyasaji wa kijinsia badala ya kuwaacha kwenda kuyatatua kifamilia.

" Unakuta mtu kanyanyaswa kijinsia anapofika kituoni polisi wanasema hiyo ni aibu mkayamalize kifamilia amesema  Samia "

Katika vita ya unyanyasaji wa kijinsia aliwataka polisi kushirikiana kutoa elimu bila kujali jinsia kwani vita hiyo sio ya wanawake tu.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni aliwapongeza polisi kwa mshikamano pamoja na ujasiri waliouonyesha.

Masauni aliwahakikishia polisi kuwa kila kitakachopatikana Serikalini atahakikisha kinagawanywa kwa usawa ili kuhakikisha polisi wanafanya kazi kwa ufanisi.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mstaafu na mlezi wa mtandao huo  Saidi Mwema alisema alipokuwa mkuu wa jeshi hilo alipanga kubadilisha muundo wa jeshi hilo.

Alisema "nilipofanya ziara Afrika ya kusini na kuona muundo wao nilivutiwa nao sana na niliporudi  nchini  nilianzisha mfumo huo"

Naye mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Alvaro alisema katika jeshi la Umoja wa Mataifa wapo pia polisi wanawake na wengine kutoka Tanzania.

Hivyo nawapongeza kwa ujasiri na umoja wenu kwa kudhubutu ili kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.

Katika maadhimisho yalipambwa na vikosi mbalimbali vikiongozwa na polisi wanawake ikiwemo gwaride, kuendesha pikipiki na farasi, kikosi vya makomandoo pamoja na vyakutuliza ghasia.


Jafo Azindua Kampeni Ya Mkoa Wetu Viwanda Vyetu

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini, jana Mjini Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Jafo alisema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda.

“Historia ya Viwanda siyo ngeni katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961 Serikali imekuwa ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo tokea wakati huo viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa na kusimamiwa huku sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na Serikali” alieleza Mhe. Jafo.

Aidha alisema kuwa ili azma hiyo iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini.

“TAMISEMI kupitia Mikoa na Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa uanishe Viwanda vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za Viwanda zinazopatikana kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya soko” alifafanua Mhe. Jafo.

Hata hivyo, Mhe. Jafo aliwataka Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na Halmashauri kuwatumia ipasavyo Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ugani ili kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya alisema kuwa Wizara yake itaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga majengo maalumu kwa ajili ya uendelezaji viwanda katika Ofisi zote za SIDO Mikoani.

Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa Kauli Mbiu ya Mkoa wetu viwanda vyetu itapunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini.

Dr Slaa Aajiriwa Kwenye Duka la SuperMarket Canada

$
0
0
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika.

Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2105.

Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket.

Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya Sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.

Akizungumza na Gazeti la Mtanzania jana kwa simu , Dk. Slaa alisema kuwa kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake  kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.

“Niko, ninafuatilia matukio Mutukula (ziara ya Rais Dk. John Magufuli jana). Siku zote nimesema ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu. Canada ili uishi vizuri, unahitaji kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne. Hayo nimeweka wazi, sijui jambo jipya kama mtu alikuwa hafuatilii.

“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi ina members (wanachama) 10,000.  Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.

Mbali na hilo, alisema kuwa pia anafanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na ushauri (Consultancy).

Alisema kila mara amekuwa akiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mtandao wala propaganda.

“Canada ni kazi, Profesa wa Chuo Kikuu anafanya kazi ya Uber. Sijui kama Uber inafahamika Tanzania, ni dereva Taxi kwa kutumia gari lake binafsi. Ofisa wa Serikali usiku anaosha vyombo hotelini.

“Ndiyo maana familia ina magari mawili au zaidi, TV, nyumba ya kisasa, chakula cha kisasa. Wanatekeleza sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa matendo. Nadhani nimekupa taarifa za kutosha ikiwa ni pamoja na kujibu propaganda kuwa nilihongwa mabilioni.

“Niwahakikishie tena, wakati wa kusoma nilikuwa na scholarship, tangu nianze kazi ninaishi kwa jasho la mikono yangu. Mke wangu yeye ameingia Chuo Kikuu cha York baada ya Diploma yake na bado anapata scholarship.

“Ndiyo maana tuna uwezo wa kuwa na magari mawili aina ya Jeep na Dodge, ukifanya kazi utaishi vizuri. Hii ni pamoja na kugharamiwa bima ya afya (Health Insurance), watoto kusomeshwa na Serikali ya Canada,” alisema Dk. Slaa.

Mei mwaka huu, Dk. Slaa, alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.

Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

“Sina tabia ya kuyumbishwaa, sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,” alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie, ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Credit: Mtanzania

Polisi: Mnunuzi wa nyumba za Lugumi alitumwa na Lugumi Mwenyewe

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa Dk. Louis Shika ambaye alishinda mnada wa ununuzi wa nyumba za Said Lugumi na baadae kuzua kizaa-zaa, alitumwa na Lugumi mwenyewe.

Dk. Louis ambaye alifunga mnada wa nyumba hizo kwa kuahidi kulipia shilingi milioni 900, alishindwa hata kutoa robo ya kiasi hicho kwa mujibu wa masharti ya mnada hali iliyopelekea kufikishwa katika kituo cha polisi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linahisi kuwa alitumwa na Lugumi kutokana na mazingira ya tukio husika.

“Aliwekwa na Lugumi ili kukwamisha mnada,” Mambosasa anakaririwa na Mwananchi ingawa aliweka angalizo kuwa hana vielelezo kuhusu hilo.

“Ingawa sina facts (vielelezo) kuthibitisha hilo, lakini alichokuwa anafanya kinatufanya tuamini hivyo. Kwasababu alikuwa anapandisha bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” aliongeza.

Alisema kuwa hata muonekano wa mnunuzi huyo ulikuwa unatia shaka na kwamba Jeshi hilo linaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi.

Elimu ya msingi Tanzania kuwa miaka 6

$
0
0
Serikali inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa elimu hapa nchini ambao elimu ya msingi itakuwa inatolewa kwa miaka 6, tofauti na ilivyo sasa ambapo hutolewa kwa miaka 7.

Akijibu swali linalohusu watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Joseph Kakunda ametolea ufafanuzi suala hilo na kusema kwamba mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima.

“Napenda kutoa majibu sahihi waliopata mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu huko tunakoelekea inabadilisha mfumo wa sasa wa elimu ambao utahitaji mtoto aanze chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari miaka minne na itakuwa ni lazima”, amesema Mheshimiwa Kakunda.

Mheshimiwa Kakunda ameendelea kwa kueleza kwamba kutokana na mfumo huo mpya ambao utaruhusu mwanafunzi kusoma kwa muda mfupi, na baada ya kuhitimu ndio utakuwa kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na ndipo ataruhusiwa kuolewa.

Hivi karibuni Waziri kakunda alitoa taarifa ikisema kwamba ili mtoto wa kike aweze kuolewa atahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu sekondari, suala ambalo liliibua mjadala kwa wananchi.

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu,vidonda Vya Tumbo,busha,nguvu Za Kiume

$
0
0
MTALAAM NA BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU NAYALIYOSHINDIKANA KAMA VILE PUMU,VIDONDA VYA TUMBO,BUSHA,NGUVU ZA KIUME,KISUKARI,MIVUTO YOTE,KUSAFISHA NYOTA,KURUDISHA MALI,NK.
 
Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani
 
Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI,KIUNO KUUMA,MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA,KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO,NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni SUPER SAYI 3,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu 

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

SUPER SAYI 4 Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI,PRESHA,UZAZI,NGIRI,PUMU,MALARIA SUGU,VIDONDA VYA TUMBO,CHANGO AINA ZOTE,BP,BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR UPENDO ANAPATIKA KADA YA ZIWA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM HUDUMA HIZI UTAZIPATA MAGOMENI 

SIMU NO 0753 15 30 26, 0715 26 85 10 

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 11

Wabunge Cuf Washinda Maombi Ya Zuio Dhidi Ya Lipumba Na Wenzake Katika Kesi Ya Kuwavua Uanachama

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
IJUMAA TAREHE 10 NOVEMBA, 2017 Mbele ya MHESHIMIWA JAJI LUGANO MWANDAMBO , MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM imetoa maamuzi (Ruling) juu ya Maombi ya Zuio (Temporary Injunction) dhidi ya Lipumba na wenzake 14 katika Shauri dogo la madai [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017] USHINDI ULIOUPATA CUF NA WABUNGE WAKE 8 NA MADIWANI 2 kutoka Mahakama Kuu ni kama ifuatavyo;

1. Mahakama Kuu IMETENGUA KUFUKUZWA KWAO UANACHAMA NA IMESITISHA UTEKELEZWAJI WA KUFUTWA KWAO UANACHAMA mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

2. Mahakama imemzuia Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF [Bodi FEKI iliyosajiliwa na RITA] na au Wakala wao yeyote KUJADILI juu ya uanchama wa Wabunge 8 na Madiwani 2 mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

3. Mahakama Kuu imekubaliana na HOJA ZA Wabunge 8 wa CUF [WAPELEKA MAOMBI -APPLICANTS] KWAMBA; imeona kuwa Zipo HOJA ZA MSINGI ZA MADAI YAO ZINAZOPASWA KUANGALIWA JUU YA UHALALI WA MASUALA YOTE HAYO YALIYOWASILISHWA MBELE YAKE.

4. Mahakama Kuu imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliwekwa na Lipumba na Wenzake katika shauri hili.

Haya ndio maamuzi ya msingi yaliyotolewa  na  MAHAKAMA KUU. Maamuzi haya tafsiri yake ni kwamba kile alichokifanya SPIKA WA BUNGE Job Ndugai ni BATILI, NA WABUNGE 8 NA DIWANI 1 WA MANISPAA YA TEMEKE WALIOAPISHWA NI BATILI KWA KUWA WAHUSIKA WOTE BADO NI WANACHAMA HALALI WA THE CIVIC UNITED FRONT[CUF-CHAMA CHA WANANCHI]. NI KWA MSINGI NI HUO Hatua na taratibu za kisheria zitachukuliwa kuhakikisha kuwa HAKI INAREJESHWA KWA WENYE KUSTAHIKI NAYO NA WABUNGE WA LIPUMBA WATATOKA BUNGENI.

Aidha, Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za Mwanasheria wa Manispaa wa Ubungo na Temeke juu ya utaratibu uliotumika Manispaa zao kufikishwa Mahakamani hapo kuwa haukufuata taratibu za kisheria na kwamba Mahakama haina Mamlaka kwa mujibu wa Sheria kuchunguza Maamuzi yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] kwa Mujibu wa Katiba na Sheria.

MAHAKAMA KUU IMEFUNGUA MLANGO WA KUSHUGHULIKIA Shauri la msingi (CIVIL CASE NO. 143/2017) Lililopangwa kusikilizwa/kutajwa Tarehe 13/2/2017 kati ya Wabunge wetu 8 ambao ndio WADAI [APPLICANTS]

1. MIZA BAKARI HAJI
2. SAVERINA SILVANUS MWIJAGE [MBUNGE]
3. SALMA MOHAMED MWASA [MBUNGE]
4. RAISA ABDALLAH MUSSA [MBUNGE]
5. RIZIKI SHAHRI NG'WARI [MBUNGE]
6. HADIJA SALUM ALLY AL QASSIM [MBUNGE]
7. HALIMA ALI MOHAMED [MBUNGE]
8. SAUMU HERI SAKALA [MBUNGE]
9. ELIZABETH ALATANGA MAGWAJA- DIWANI VITI MAALUMU MANISPAA YA TEMEKE.
10. LAYLA HUSSEIN MADIBI- DIWANI VITI MAALUM-MANISPAA YA UBUNGO.

DHIDI YA WADAIWA [RESPONDENTS]

1) BODI YA WADHAMINI -CUF,
2) MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA,
3) KAIMU KATIBU MKUU-CUF,
4) MKURUGENZI TUME-NEC,
5) KATIBU WA BUNGE,
6) MKURUGENZI MANISPAA- TEMEKE
7) MKURUGENZI MANISPAA -UBUNGO
8) RUKIA AHMED KASSIM,
9) SHAMALA AZIZ MTAMBA,
10) KIZA HUSSEIN MAYEYE,
11) ZAINAB MNDOLWA AMIR,
12) HINDU HAMIS MWENDA,
13) SONIA JUMAA MAGOGO,
14) ALFREDINA APOLINARY KAHIGI,
15) NURU AWADH BAFADHILI

HOJA ZA WABUNGE WETU :

1. Wabunge na Madiwani Wetu walikuwa wanadai HAKI YA UANACHAMA WAO ambayo tayari leo imerejeshwa kwao.

2. Wanahoji jinsi mchakato uliotumika kufikia maamuzi ya kuwavua uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi yanayoendelea mahakamani yanayohoji uhalali wa Uongozi juu ya ‘Mgogoro uliopandikizwa na Vyombo vya dola kwa kumtumia Msajili wa Vyama vya siasa nchinji unaoendelea.

3. Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za nidhamu dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa rasmi za tuhuma zao kwa maandishi, siku na tarehe ya kikao hicho, kupata nafasi ya kujitetea, huku ikizingatia kuwa si wote wanaoishi Dar es Salaam, kulikofanyika kikao cha maamuzi.

4. Uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila kujiridhisha vyakutosha.

5. Kutokupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CUF na vikao kuendeshwa kwa speed ya mwendokasi-‘DART'

6. Maamuzi hayakuzingatia haki za kikatiba za mwanachama ikiwemo haki ya kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5) ya katiba ya CUF, Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani ya Chama.

7. Je Vyombo vilivyowachukulia hatua za kinidhamu vina uhalali wa Kikatiba ndani ya CUF? Hayana mengine mengi ndiyo yanayohojiwa Mahakamani katika shauri hili la msingi.

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Mawakili wetu Wasomi Peter Kibatara na Omary Msemo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kulisimamia suala hili kwa weledi mkubwa. Tunawapongeza Viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali za Chama, Wanachama, Madiwani na Wabunge wote waliokuwa pamoja na CHAMA NA AMBAO HAWAKUKUBALI KUYUMBA WALA KUYUMBISHWA kwa kufanikisha na kusimamia mapambano haya ya kisheria. Tunaamini na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwamba HAKI NA USHINDI VIPO KARIBU KUPATIKANA.

JAJI NDYASOBERA ATOA AMRI YA KUITWA WAJUMBE BODI YA RITA:

Katika hatua nyingine ya mapambano ya kisheria Jumatatu Tarehe 13/11/2017 Mbele ya Mheshimiwa Jaji Ndyansobera, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini FEKI' ya Lipumba wameitwa Mahakama Kuu kwenda kujieleza MMOJA MMOJA juu ya uhalali wao.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 10/11/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

Rais Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na watanzania waishio Uganda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Watanzania waishio nchini Uganda katika Mji wa Masaka na kuwahakikishia kuwa hatua zilizoanza kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mabadiliko zimeanza kuzaa matunda.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Mawaziri na viongozi wakuu wa taasisi za Serikali ametaja baadhi ya matokeo hayo kuwa ni kusimamia vizuri uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia 7, kudhibiti mfumuko wa bei hadi asilimia 5.1, kuokoa Shilingi Bilioni 238 walizokuwa wanalipwa watumishi hewa kwa mwaka na kuondoa watumishi wenye vyeti feki waliokuwa wakilipwa Shilingi Bilioni 142 kwa mwaka.

Matokeo mengine ni kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Shilingi Bilioni 850 hadi wastani wa Shilingi Trilioni 1.2 kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA), kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma umbali wa kilometa 726 ambapo Shilingi Trilioni 7 zitatumika, kununua ndege 6 za Serikali kwa ajili ya kuinua utalii na kuimarisha usafiri wa anga, kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Bilioni 31 hadi 269.

Mhe. Rais Magufuli pia amesema Serikali imechukua hatua madhubuti za kuwavutia wawekezaji na sasa wengi wapo katika hatua mbalimbali za uwekezaji ikiwemo ujenzi wa viwanda na ametoa wito kwa Watanzania hao kuendelea kuwashawishi wawekezaji wengine kwenda kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa fursa zipo nyingi.

Katika mkutano huo Watanzania waishio Uganda wamemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi mbalimbali anazozifanya na wameomba Serikali iwajengee mazingira bora pale wanapowapeleka wawekezaji nchini Tanzania.

Pamoja na Mhe. Rais Magufuli kuahidi kufanyia kazi maoni ya Watanzania hao, Mawaziri waliokuwa wakijibu hoja mbalimbali zilizotolewa wamewataka kutosita kuwasiliana nao pale wanapokuwa na jambo linalohitaji majibu ya Serikali.

Huu ni mkutano wa kwanza wa Mhe. Rais Magufuli kukutana na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora), na Uganda kuna Watanzania 45,000 waishio nchini hapa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Masaka, Uganda

10 Novemba, 2017

Walichoongea Rais Magufuli na Rais Museveni nchini Uganda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wamewaagiza Mawaziri wa nchi hizi mbili kujadiliana juu ya namna ya kuongeza biashara kati ya nchi hizi ili kupata manufaa makubwa zaidi ya uhusiano na ushirikiano wa kidugu uliopo.

Viongozi hao wametoa kauli hiyo jana tarehe 10 Novemba, 2017 baada ya kufanya mazungumzo rasmi na kisha kuzungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda ambako Mhe. Rais Magufuli ameendelea na ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku 3.

Akisisitiza juu ya agizo hilo Mhe. Rais Magufuli amesema kwa muda mrefu biashara kati ya Tanzania na Uganda imekuwa ni takribani shilingi Bilioni 200 kwa mwaka kiasi ambacho ni kidogo mno ikilinganishwa na fursa zilizopo, uhusiano na ushirikiano wa kidugu uliojengwa tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

“Tumewaagiza Mawaziri na wataalamu wakae na waangalie vikwazo vyote vinavyosababisha tufanye biashara kwa kiasi kidogo, wakishajadili watatuambia tufanye nini, tunataka kuona biashara ya Tanzania na Uganda inakua, hivi sasa Uganda imewekeza Dola za Marekani Milioni 47 tu nchini Tanzania na kuzalisha ajira 146,000, kiasi hiki ni kidogo sana, ni lazima tuongeze” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kuhusu hatua ambazo Tanzania imeanza kuchukua Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma umbali wa kilometa 726, Serikali imekarabati reli iliyopo, pamoja na kivuko cha mabehewa ya treni cha Umoja katika ziwa Victoria ili kuwezesha mizigo ya kutoka bandari ya Dar es Salaam kufika Kampala kwa gharama nafuu na pia inaendelea kujenga na kuimarisha barabara za mpakani.

“Napenda pia kukushukuru Mhe. Rais Museveni kwamba Serikali yako sasa itajenga kipande cha kilometa 11 za reli kutoka Portbell hadi Kampala, na sisi tumeamua kuweka bandari kavu pale Mwanza ili wafanyabiashara wa Uganda wasisumbuke kwenda hadi Dar es Salaam, mizigo yao wataipata Mwanza, hii ni njia ya uhakika na nafuu ya kusafirisha mizigo” ameongeza Mhe. Rais Magufuli.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari Mhe. Rais Magufuli ameeleza kuwa Tanzania imejipanga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Uganda kwa kuhakikisha miradi mbalimbali inakwenda vizuri ikiwemo kituo cha pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post – OSBP) na mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Museveni amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya kupambana na rushwa na kuimarisha uchumi, na amemuagiza Waziri wake wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Monica Azuba Ntege kuharakisha mchakato wa ujenzi wa kipande cha reli cha kilometa 11 kutoka bandari ya Portbell hadi Kampala ili usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli kutoka bandari Dar es Salaam uanze mara moja.

Mhe. Rais Museveni amesisitiza kukuzwa kwa biashara katika ya Tanzania na Uganda hasa wakati huu ambapo Uganda inahitaji kununua gesi ya Tanzania kwa ajili ya viwanda vyake vya mbolea na chuma na pia kurudisha historia ambapo Uganda ilikuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa za Tanzania.

Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Marais wote wawili wameshuhudua utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Utangazaji wa Uganda (UBC) na makubaliano kati ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Jeshi la Polisi la Uganda.

Mhe. Rais Magufuli atamaliza ziara yake rasmi ya siku 3 kesho na kurejea nchini Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Masaka, Uganda

Video: Mbunge Nape Nnauye akosoa miradi ya serikali

$
0
0
Mbunge wa Mtama kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amekosoa utekelezaji wa miradi mikubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli akidai kuwa inapelekea serikali kukopa fedha nyingi kutoka kwa wadau wa maendeleo na hivyo deni la taifa kuzidi kukua hali inayoweza kusababisha taifa kutokopesheka.

Nape ameyasema hayo jana bungeni katika kikao cha pili cha mkutano wa 9 wa bunge la 11 unaoendelea mjini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019.

Nape amesema kuwa hadi sasa kiwango cha serikali kukopa kimefikia asilimia 32 huku deni la taifa likiwa ni dola bilioni 26 na kusema kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa huenda ikapelekea serikali kukopa dola 21 bilioni na hivyo kufanya deni la taifa kuwa dola 47 bilioni wakati ukomo wa kukopa ni dola bilioni 45.

Miongoni mwa miradi ambayo Nape ameikosoa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (SGR), mradi wa kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) pamoja na mradi wa kufua umeme wa Stieglers Gorge katika maporomoko ya Mto Rufiji mkoani Pwani.

Nape ameeleza kuwa endapo serikali itaendelea kukopa ili kufadhili miradi hiyo, italazimika kutumia fedha kutoka sekta nyingine kulipia madeni hayo, jambo ambalo litakuwa likiumiza sekta hizo.

Aidha, mbunge huyo alisema, kutokana na miradi inayotekelezwa sasa na serikali ya awamu ya tano kuwa ya muda mrefu, serikali italazimika kuanza kulipa madeni iliyokopa kutekeleza miradi hiyo kabla ya miradi yenyewe kuanza kuwanufaisha wananchi, jambo ambalo litaifanya serikali kuchukua fedha kidogo ambazo zinatokana na kodi za wananchi kulipa madeni.

Katika hatua nyingine, Nape ameishauri serikali kuachana na utaratibu wa kutaka kufanya kila kitu yenyewe, badala yake itengeneze mazingira mazuri kwa ajili ya sekta binafsi kukua, ili kuepusha serikali kutumia fedha zote inazokusanya katika miradi ya ujenzi wa miundombinu, kuzalisha umeme, shughuli ambazo zingeweza kufanywa na sekta binafsi.

==>Msikilize Mbunge Nape Nnauye akizungumza hapa chini;

Lowassa, Mbowe kuongoza kampeni za udiwani Chadema

$
0
0
Viongozi wa juu wa Chadema , Freeman Mbowe na Edward Lowassa wataongoza kampeni za uchaguzi  mdogo wa  nafasi za udiwani kwenye kata 43.

Chama hicho kimeunda Kamati za Kitaifa 10, zitakazoongeza nguvu, hamasa na mikakati ya kampeni za uchaguzi wa marudio kwenye nafasi hizo  kuanzia kesho hadi siku ya uchaguzi.

Timu hizo ambazo zitafanya kazi kwa kushirikiana na kamati zingine za hamasa katika ngazi za kanda, mikoa, majimbo, kata na matawi katika maeneo yenye uchaguzi huo, zitaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene imeeleza kuwa Mbowe  ataanza kuzindua kampeni kesho katika Kata ya Saranga, jijini Dar es Salaam.

Makene ametaja watakaoongoza timu hizo zilizopangwa kwa makundi A hadi G, kuwa ni  Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara), Profesa  Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Zanzibar) Said Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama  Dk. Vincent Mashinji.

Amewataja wengine watakaoongoza timu hizo kuwa ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Bara),  John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar), Salum Mwalimu.

Amesema timu hizo zitasaidiwa kwa ukaribu na timu zingine tatu chini ya uratibu na mikakati ya mabaraza ya chama, ikiwamo  Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) na Baraza la Wazee wa Chadema.

Timu hizo zitazunguka katika maeneo yote ya uchaguzi wa kata hizo 43, lengo ni kuwafikia wananchi wote kuelekea uchaguzi huo.

“Chadema  tutaweza kuwafikia na kuzungumza na wananchi katika majimbo 37, halmashauri 36, mikoa 19 nchi nzima.

“Chama kimedhamiria kuweka ushindani mkubwa na kushinda kata hizo 43 ambazo chama kimeweka wagombea, tunaamini ushindi upo na ndiyo maana tunakutana na wananchi kuwahamasisha na kuwasikiliza wanataka nini ” amesema Makene.

VIDEO MPYA: Rosa Ree - Dow (Official Video)

$
0
0
Rapper wa kike kutoka Tanzania Aitwaye Rosa Ree usiku wa Jana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ndio mkali wa Kurap kwa upande wa wadada Afrika baada ya kuachia Video kali ya wimbo wake unaitwa Dow...

Itazame Hapa Chini .

Mahakama upande wa Watoto yatupilia mbali shtaka la Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond kuhusu malezi ya mtoto wao

$
0
0
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
 
Uamuzi huo umetolewa jana Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
 
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.  Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
 
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
 
Mobeto  anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
 
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto  anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
 
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto  akidai  gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni  kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Kagasheki amvaa Kigwangalla kumhusisha na rushwa

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu.

Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea,"

Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao

"Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu sana. Tuongee kindugu nje ya hapa! Kuweka sawa ni kwamba 'sikukutaja!" Kigwangalla.

Hivi karibuni Waziri Kigwangalla aliweka wazi kwamba amewaondoa Askari wote wa kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji huyo ambaye ana uhusiano wa Karibu na Prof. Songorwa (aliyemsimamisha kazi siku chache zilizopita) na alikuwa na uhusiano ya karibu na Prof. Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na Utalii wa zamani.

Balozi Kagasheki aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika uongozi wa serikali ya awamu ya nne ambapo aliongoza wizara hiyo Mwaka  (2012-2013)

Siri Ya Bundi Kupendwa Na Wachawi

$
0
0
Wakati  watu wengine  wakimuona  bundi  kama  ishara  ya  uchuro, nuksi  na  mikosi, wachawi wao  humuona  bundi  kama    kiumbe  mwenye hekima  na  busara.

Haya  si  maneno yangu  bali  ni  maneno  ya Mganga wa  Jadi kutoka  nchini  Tanzania  ajulikane  kama  MUNGWA  KABILI.
 
Dokta. MUNGWA  KABILI aliyasema  maneno  hayo  hivi  karibuni, alipokuwa  akifanya  mahojiano  ya  moja  kwa moja  kwenye  kituo  kimoja  cha  redio  kilichopo  jijini  Mombasa  nchini  Kenya.
 
Maneno ya  Dokta Mungwa  yalikuja mara  baada  ya  mwanamama  mmoja  kutoka  Malindi  Kenya  kupiga  simu  akielezea  alivyo  jawa  na  hofu  kubwa  kwa  sababu  usiku  wa  kuamkia  siku  hiyo,  bundi  walitua kwenye  mti  ulio kuwa  kwenye  nyumba  iliyo  jirani  yake  na  kutoa vilio  vya  uchuro  kwa  masaa  mawili.
 
Dokta  Mungwa  Kabili  alikuwa  na  haya  ya  kusema :
Pole  sana  dada  angu  kwa  masaibu  yaliyo  kukuta, lakini  hata  hivyo  usiwe  na  hofu  kwa  sababu, si kila  mlio  wa  bundi  una  maanisha  uchuro.  Wakati  mwingine  bundi  hutoa  sauti  kumaanisha  kitu  tofauti  kabisa  lakini  kwa  sbabu  watu wengi  tumeshajiaminisha  kuwa  kila  bundi  aliapo ni  uchuro  basi  tunapotokea  na  hali  hiyo  hujawa  na  hofu  kama  ilivyo  kutokea  wewe.
 
Kitu  kimoja  cha  hakika  ninacho penda  kukujulisha  ni  kwamba,  siku  yoyote  utakayo  pata  kusikia  sauti  ya  bundi,  basi  jua  kuwa  umesikia  sauti  hiyo  kwa  sababu  bundi  wenyewe  ndio  wametaka  wewe  usikie  sauti  yao. Hii  maana  yake  nini  ? Maana  yake  ni  kwamba, kuna  ujumbe  ama  ishara  fulani  ambayo  bundi  wanataka  uipate.
 
Katika  ndege  wote  walio umbwa  na  Mwenyezi  Mungu, bundi  ndio  ndege  pekee  mwenye  uwezo  wa  kuruka,kupaa  na  kutua  bila  kupiga  kelele wala  kutoa  sauti  yoyote  ile. Mungu  ameya  dizaini  mabawa ya bundi katika namna  ya  kipekee, namna  inayo  mfanya  bundi  aweze  kupaa  bila  kupiga  kelele  pamoja  na  kwamba, kwa kufanya  hivyo  huku’nguta  mbawa  zake.
 
Bundi  anaweza  kutua  kwenye  paa la nyumba  yako, akakaa  hadi alfajiri  na  kuondoka pasi na  wewe  kujua.
Ukiona  umesikia  sauti  ya  bundi, basi  tambua  ni  bundi  mwenyewe  ndio  amekusudia  usikie  sauti  yake  kwa sababu  kuna  ujumbe  maalumu  anataka  kukupa.
 
Wachawi  wanamfahamu  vizuri  sana  bundi  ndio  maana  wanampenda  sana  wala  hawashitushwi  na  mlio  wake.
Wachawi  wanampenda  sana  bundi  kiasi  cha  kuiga  karibu  tabia  zote  za ndege  huyu  wa usiku.

Baadhi  ya  tabia  za  bundi  ambazo  wachawi  wameziiga  ni  pamoja  na:

1. Bundi ndio ndege  pekee  ambae  huwa  hapigi  kelele  anapokuwa  anapaa  na  kutua. Ndege  wengine  wote  huwa  wanapiga  makelele  pindi  wanapokuwa  wanapaa  kwa  sababu  ya  kupiga  mabawa  hali  ambayo  ni  tofauti  kwa  bundi. Bundi  hupaa kimya  kimya  na  hutua  kimya  bila  mawindo  yake  kujua.  Hii  inatokana  na  jinsi  Mungu alivyo  ya  dizaini  mabawa  na  manyoya  yake  ili  viweze  kumsaidia  kupata  ridhiki yake  ya  kila  siku. Wachawi  wanapokuwa  wanafanya  mipango  yao  ya  kichawi  hufanya  kimya  kimya  bila  watu  wengine  kujua. Na  huwa  hawataki  kabisa  kujulikana.

2. Bundi  hutaka  sauti  yake  isikike  pale  tu  anapo  amua  isikike.  Unaposikia  sauti  ya  bundi  jua  umeisikia  kwa  sababu  ametaka  uisikie  na  wala  si  vinginevyo . Vivyo hivyo  wachawi  pia  hutaka  nguvu  zao au  mambo  yao   yajulikane  pale  tu  wanapotaka  vijulikane  na  si  vinginevyo.

3. Bundi  huanza  kuruka  usiku giza  linapo  ingia. Vivyo  hivyo  wachawi  huanza  shughuli  zao usiku  pindi  giza  linapo  ingia.

4. Sio kwamba  bundi  hawawezi  kuruka  mchana . Wakati mwingine  bundi  huruka  mchana  kutafuta  mawindo  yao  na  hufanya  hivyo  pindi  kunapo kuwa  na  sababu  ya  msingi kama vile  kutafuta  chakula  hasahasa  katika  kipindi  ambacho wanakuwa na   upungufu  wa  chakula  au  hawakupata  mawindo  ya kutosha  wakati  wa  usiku.

Vivyo  hivyo  wakati  mwingine  wachawi  hulazimika  kufanya  baadhi  ya shughuli  zao  nyakati  za  mchana  ingawa  uchawi  unao  fanyika  usiku  huwa  na  nguvu  kubwa  zaidi  kuliko  unao  fanyika  mchana.

5. Bundi  hupenda  kufanya  shughuli  zao  usiku  wakati  mawindo  yao  yamelala, vivyo  hivyo  wachawi  hupenda  kufanya  shughuli  zao  usiku  wakati  wahanga  wao  wamelala.

6. Bundi  huwa  hawajengi  vichali  vyao  wenyewe  na  badala  yake  hutumia  vichali  vya  ndege  wawindao  mchana  kama  vile  mwewe,  fundi chuma  na  kunguru.    Vivyo  hivyo  wachawi  huwa  hawaishi kwenye  nyumba  walizo jenga kwa  jasho  lao  wenyewe. Huishi  kwenye  nyumba  zilizo  jengwa  na  watu  wengine, na  wao  huzimiliki  kwa  kutumia  nguvu  ya  uchawi.

Kama  hiyo  haitoshi ,wachawi   huwa  hawahifadhi  majini  wabaya  kwenye  miili  yao  wenyewe. Hutumia  miili  ya  watu  wengine  kuhifadhi  majini  na  mapepo  wachafu. Wakati mwingine  unaweza  kuwa  na  mapepo  wachafu  sio  kwa  sababu  kuna  watu  wamekutumia  ili  upate  madhara  ila  kwa  sababu  wachawi  wanatumia  mwili  wako kama  kibanda  cha  kufugia  na  kutunzia  majini  yao.

7.  Wakati mwingine   bundi  hulana  wao kwa  wao.  Bundi  wakubwa  wenye  pembe  kubwa  huwala  bundi  wa  saizi ya  kati  na  bundi  mbilikimo  vivyo  hivyo  bundi  wa  saizi  ya  kati  hula  bundi  mbilikimo isipokuwa  bundi  mbilikimo ndio  hawana  uwezo  wa  kuwala  bundi wengine.  Vivyo  hivyo  wachawi  hutoa  sadaka  zap  watoto  wao , waume,wake , wazazi  na  ndugu  zao.

8.  Kwa kawaida  bundi  huishi  hadi  miaka  kumi . Bundi  hutaga  mayai  matatu  hadi  manne na huatamia  mayai  kwa  wiki tatu  hadi  nne.  Wanapototoa  watoto, bundi  mbilikimo  huwalisha  makinda  yao  kwa  siku  27  wakati  bundi  wa  saizi  ya  kati  na  wale bundi wakubwa wenye mapembe  makubwa  huyalisha  makinda  yao kwa  muda  wa  siku 70. Wanapokuwa  wanayalisha  makinda  yao, huyalisha  kwanza  makinda  yenye  afya  na  nguvu  kisha  hufuata  makinda  dhaifu. Hii  maana  yake ni  kwamba, kama  hakuna  chakula  cha  kutosha, basi  makinda  yaliyo  dhaifu  yatakufa   kwa  njaa.  Vivyo hivyo  wachawi katika  kafara  zao  huwa  wanatoa  kafara  zilizo  nona  kwanza  kisha  hufuata kafara  dhaifu.

9. Bundi  hawaoni  vitu  vya  karibu, huona  vitu  vya  mbali tena  mbali  sana. Vivyo hivyo   Wachawi  kwa  kutumia  rada  zao  za  kichawi  wanaweza  wasijue  kesho  utapatwa  na  nini  lakini  wanaweza  kujua  utakuja  kuwa  nani  baada  ya  miaka  ishirini ijayo.  Ndio  maana  huweza  kuiba  nyota  za  watu wakingali  wachanga.

10. Ukiachilia  mbali  nyani  na  sokwe, bundi  ndio  kiumbe  mwenye  sura  inayo  fanana  sana  na  sura  ya  mwanadamu.   Hii  ni  kwa  sababu  macho   ya  bundi  yamekaa  kama ya  mwanadamu. Macho  ya  bundi  yamekaa   kwa  mbele  na  yanaona  kitu  kimoja  kwa  wakati  mmoja   ilihali  ndege  wengine  macho  yao  yamekaa  pembeni  kulia  na  kushoto   na yanaona  vitu  viwili  kwa  wakati  mmoja, yani  jicho  la  kulia  linaona  kitu  kingine  na  jicho  la  kushoto  linaona  kitu  kingine  kwa  wakati  mmoja.

Kwa  sababu  hii  Mungu  amempa  bundi  shingo  yenye  uwezo  wa  kuzunguka  mbele  nyuma . Unapopita  kwenye  mti  ambao  bundi  ametua  atakutazama, ukimpita  katika  usawa  wake  wa  machoi  atageuza  macho  yake  na  kukutazama  hadi  mwisho  wako. Wachawi  pia  hufanya  vivyo  hivyo.  Unapowapita  katika  vijiwe  vyao,watakutazama  hadi  utakapo  malizikia.

11. Bundi  hufumba  macho  kama  mwanadamu  yaani  kutoka  juu  kwenda  chini  tofauti  na  ndege  wengine  wote  ambao  wao hufumba  macho  kutoka  chini  kwenda  juu.

 Na Sio kweli  kwamba  bundi  hawaoni mchana, bundi  wanaona  mchana  vizuri  sana  tu, ila  kwa  sababu  macho  yao  ni  makubwa na  makali  sana  yenye  uwezo  wa  kuona mara  saba  zaidi  ya  mwanadamu, usiku kwao  huwa  kama  mchana  kwetu  ndio  maana  hupendelea zaidi kuwinda  usiku.  Wachawi  hutoka usiku  kuwanga  sio  kwa  sababu  hawaoni  mchana. Hufanya  hivyo  kwa  kumuiga  bundi.

12.Bundi  anapokutana  na  hatari  hutuna  na  kuwa  mkubwa  mara  mbili  ya  ukubwa wake  wa  asili. Mchawi  anapokutana  na  changamoto   yoyote katika  shughuli  zake  za  kichawi   huenda  kutafuta  msaada  kwa  wachawi  wenye uwezo  mkubwa  mara mbili zaidi  yake.

13.Bundi  huwa  na  mkia  mfupi  sana  kiasi  kama  huwajui  bundi  ukimuona  kwa  ukaribu  zaidi  kwa  mara  ya  kwanza  unaweza  kudhani  mkia  umekatwa. Wachawi  huwa  na  mawazo  mafupi sana. Mfano Wachawi  hutumia  mkia  wa  bundi  kufanya  shughuli  mbalimbali  za  kichawi  kama vile  kufupisha  maisha  ya  maadui zao, au  kufunga  maumbile  ya  kiume  yawe  mafupi, kufunga  mahusiano yawe  mafupi nakadhalika.

14. Pamoja  na  kwamba  bundi  wana  tofautiana  ukubwa  wa  maumbile, yaani  wakubwa, saizi ya  kati  na  wadogo  ama  bundi  mbilikimo, lakini  bundi  wote wana  sifa  zinazo  fanana,  mfano  bundi  wote  huwa  na  vichwa  vikubwa  kuliko  maumbile  yao, wote wana  manyoya  laini, wote  huwa na   mikia  mifupi  sana, wote  huwa  na  rangi  ima  ya  kahawia  au  ya  kijivu , huwa  na  milio  inayo  fanana, huruka  na  kupaa  kimya kimya, huwa  na  manyoya kwenye  miguu. Vivyo  hivyo  wachawi  pamoja  na  kwamba, wanaweza  kuwa  na  nguvu  na  madaraja  tofauti  katika  uchawi,lakini  wote  huwa  na  tabia  zinazo  fanana  kama  vile  chuki, husda, unafiki , roho ya  mbaya,mawazo mafupi  nakadhalika.

15. Pamoja  na  kwamba  bundi  wote  huanza  kutafuta  mawindo  yao pindi  giza  linapoingia, lakini  hutoka  kwa  nyakati  tofauti  tofauti.   Mara  nyingi  huanza  kutoka  bundi  mbilikimo. Hawa  bundi  mbilikimo  hasa  wale  wanaoishi  porini hutoka  kuanzia  saa  4 usiku, bundi  wa  saizi  ya  kati hutoka  kuanzia  saa  sita  usiku  na  bundi  wenye  pembe  kubwa  hutoka  kuanzia  saa  nane  za  usiku .  Wachawi  nao  wanapo  kuwa  wanaenda  kuwanga  na  kufanya  shughuli  zao  za  kichawi  nyakati  za  usiku  hupishana  nyakati. Ingawa  vikundi vingi  vya  kichawi  huanza  kutoka  kuanzia  saa  sita  usiku,  lakini  hupishana. Vingine  hutoka  saa saba , vingine  saa  nane. Tofauti  ni  kwamba  karibu  wachawi  wote  hurudi  majumbani mwao  nyakati  sawa.

Hata  hivyo, bundi  hutoka  kwa  nyakati  tofauti  kwa  sababu  maalumu.  . Bundi  karibu  wote  wakubwa  kwa  wadogo  hushea  vichali na huishi  katika  eneo moja.  Hutoka  kuwinda  nyakati  tofauti  tofauti kwa  ajili  ya  kupunguza  ushindani  wakati wa  mawindo..
 
16. Pamoja  na  kwamba  macho  ya  bundi  yana  nguvu  sana  lakini  wanapokuwa  katika  mawindo  hutumia  zaidi  masikio  yao  kuliko macho  yao.  Masikio  ya  bundi  yana  nguvu  sana  na  huweza  kusikia  hata  sauti  ya  kitu  kilicho  umbali  mrefu  sana. Hata hivyo  bundi  wanapokuwa  wanaenda  kuwinda  wakati  wa  mchana  hutumia  macho  zaidi  kuliko  masikio.  Vivyo  wachawi, huamini  zaidi  vitu  wanavyo visikia  kuliko  wananvyo  viona. Yaani  mchawi kila anacho  ambiwa  kuliko  kile  alicho  kiona. Kwa mfano   wewe  A  una  ujauzito hata  wa  miezi sita. Lakini kwenye  kilinge  cha  wachawi  alipoenda  kukuroga ,ukapewa  jina  kuwa  wewe  ni  MGUMBA. Basi  mchawi  ataendelea  kukuita  na  kukuchukulia  na kuamini  kuwa  wewe ni  mgumba. Ataendelea  kuamini  hivyo  hata  kama  utazaa watotyo  kumi.

17. Bundi  wanapokuwa  wanapaa  huutawala  upepo  na anga. Wana  mamlaka  juu  ya  anga , na upepo. Vivyo wachawi  wanapo  kuwa  wanapaa  huamini  kuwa  wana  mamlaka  juu  ya  anga  na  upepo  kama  alivyo  bundi.

18.  Bundi  huzungusha  kichwa  kupima  umbali  wa  anapotaka  kuruka  vile vile  wachawi  hupima nguvu  ya  kiroho  ya  mtu kabla  ya  kumtupia  uchawi.

19. Ukiachilia  mbali  bundi  wanao  kula  wadudu, bundi  wengi  huwa  hawana  tabia ya  kuhama  hama. Wanaweza  kukaa  katika  eneo  moja  kwa  zaidi  ya  mwaka  mmoja. Wachawi pia  huwa  hawami hami. Huweza  kukaa  katika  mtaa  mmoja  kwa  zaidi  ya  miaka  arobaini. Na  wanapokuwa  wanatengeneza  uchawi  wa  kuwatuliza  wanaume  kimapenzi  hutumia  vichali  vya  bundi walio  kaa  kwenye  kichali hicho  kwa  muda  wa  mwaka  mmoja  na  zaidi.

20. Wakati  mwingine  bundi  hupenda  kuwinda  wadudu  wanao  tembea  usiku  ili  kuwa  na  uhakika  wa  kupata  kitoweo.  Wadudu  hao  ni  popo.  Vivyo  hivyo  wachawi wakati mwingine  hufanya  ulozi  nyakati  za  usiku   katika  maeneo  au  mazingira  ambayo  walengwa  wao  wanakuwa  macho  ili  kuwa  na  uhakika  wa  kupata  mawindo  yao.  Mfano  ni kwenye  klabu  za  usiku zinazo  kesha,  kwenye  misiba  au  sherehe  zinazo  kesha  nakadhalika

21.   Tunafahamu  kuhusu  uwepo  wa  bundi  pindi wanapo  toa  milio  na  sio  pindi wanapokuwa  kimya.  Vivyo tunafahamu  kuhusu  uwepo wa  wachawi  katika  mazingira  tunayo  ishi  pindi  wanapo  tupa  uchawi  wao na  sio  wanapokuwa  hawajatupa  uchawi.

22.              Bundi  wakubwa  hutoa  sauti  kubwa  kuliko  bundi  wadogo. Vivyo  hivyo, wachawi  wadogo  hujulikana  zaidi  kuliko  wachawi  wakubwa.

KWANINI  WACHAWI WANAMPENDA  SANA  BUNDI
Wachawi  wanampenda  sana bundi  kwa  sababu   wana  amini  bundi  ni  kiumbe  mwenye  faida  nyingi  sana  kwao.    Baadhi  ya  mambo  ambayo  wachawi  huya  amini  kama  faida  zinazo letwa  na  bundi  ni  kama  ifuatavyo :

1.Bundi  huwasaidia   wachawi  kuchunga  misukule  yao  ; Katika ulimwengu  wa  wachawi  mtu  aliye  chukuliwa  msukule  mara  baada  ya  kukatwa  ulimwi  hatua  inayo  fuatwa  huwa  ni  kulishwa  vumbi  la  mifupa iliyo  temwa na  bundi.   Dawa hiyo  huufanya  msukule  huo  usahau  kila  kitu  ulichokuwa  unakijua  kabla  ya  kuchukuliwa  msukule.

Kwa  wasio  fahamu, bundi  huwa  wanakula  wadudu  na  wanyama  mbalimbali  kama  vile  nyoka, nge,panya, pimbi, panyabuku, ndezi,  popo  na hata  samaki.  Bundi  huwa  wanakula  vitu  vizima  vizima  na  kutema  mifupa  yao. Sasa  hii  mifupa  inayo temwa na  bundi  ndio  wanayo  itumia  wachawi  kuwalisha  misukule   wao  kwa  minajili  ya  kuwafanya  wasahau  kila  kitu  walichokuwa  wanakijua  kabla  hawaja  chukuliwa  msukule  pamoja  na  kuwapa uwezo  wa  kuona  mambo  yasiyo  onekana  na  kutokuonekana na  watu  wa  kawaida.
2. Bundi  huwasaidia  wachawi  kulinda  mashamba  yao  dhidi  ya  wadudu  waharibifu  wa  mazao

Moja kati  ya  shughuli  kuu  za  wachawi  ni  kilimo  kwa  kuwatumia  misukule. Kwenye  mashamba  huwa  kunakuwaga  na  panya  waharibifu  wa  mazao . Na  kama  nilivyo  sema  hapo  mwanzo  kuwa,  moja  kati  ya  yakula  vinavyopendwa  sana  na  bundi  ni  panya.  Kwa  wastani  bundi mmoja  anaweza  kula  hadi  panya  elfu  moja  kwa  mwaka.  Mchawi  akiwakaribisha  bundi  ishirini  kuwa  wanatembelea  kila  siku  shambani  kwake  maana  yake  ni kwamba  ndani  ya  mwaka  mmoja  watakuwa  wamemsaidia  kula  panya  elfu  ishirini  ambao  wanaweza  kuharibu  hadi  tani  31  za  mazao.

Hivyo  basi  kwa  wachawi  hapo  bundi  huwa  msaada  wao  mkubwa  wa  kiuchumi. Huwasaidia  kutunza  na  kulinda  mashamba  yao  dhidi  ya  wadudu  waharibifu. Huwasaidia  kuokoa  gharama  za  kununua  dawa  za  kuua  wadudu  waharibifu  ambazo  zingeweza  kuwagharimu  mamilioni ya shilingi.

3.Bundi  huwasaidia  wachawi  kuondokana  na  madhara  ya  wadudu  hatari  kama  nyoka na  nge

Bundi  ni  walaji  wazuri  sana  wa  wadudu  hatarishi  kwa  binadamu  kama  vile  nyoka na  nge. Hivyo  kwa  mchawi  kuwakaribisha  bundi  shambani kwake  au  nyumbani  kwake  anakuwa amejihakikishia  kuwa  hawezi  kupatwa  na madhara  ya  kuumwa  na  nyoka  au  nge  kwa  sababu  bundi  wanapoweka  makazi  yao katika  eneo  lolote  lile, nyoka  hawawezi  kukaa  mahali  wapo.
4. Bundi  huwasaidia  wachawi  katika  shughuli  mbalimbali  za  kichawi.

Kwa  kutumia  maarifa  ya  kichawi, wachawi  humtumia  bundi  katika  shughuli  mbalimbali  zap  kichawi  kama  vile :

i.           Kwenda  kuzimu  :  Bundi  ni  mesenja  wa  kuzimu  na  dunia. Huchukua  habari  za  kuzimu  na  kuzileta  duniani na   habari  za  duniani  huzipeleka  kuzimu .  Bundi  ni  daraja  linalo  unganisha  kuzimu  na  duniani. Ni daraja  linalo  unganisha  ulimwengu  usio onekana  na  ule  unao  onekana.   Kwa  wale  wasio  fahamu, umbali  kutoka  duniani  na  kuzimu ni  kilomita  sifuri. Moja  kati  ya  mawakala  wa  malango    makuu  yanayo  unganisha  dunia  na  kuzimu  ni  huyu ndege  aitwae  bundi.Ukaribu  na  urafiki  wa  wachawi  kwa  ndege  huyu  unawanufaisha  wachawi na  kuzimu

ii.         Kuiba  na  kuharibu  nyota  za  watu  hususani  watoto  wachanga :   Wanapokuwa  katika  mchakato  wa  kuiba  nyota  za  watu  hususani  watoto  wachanga,  wachawi  humtumia  bundi  kufanikisha  mchakato.

KWANINI  WANAMTUMIA  BUNDI : Bundi   ana  sifa  moja  kubwa  sana. Hana  uwezo  wa  kuona  vitu  vya  karibu lakini  ana  uwezo  wa  kuona  vitu  vya  mbali  sana.  Hiyo  ni sifa  yake katika  ulimwengu wa  nyamja  ambayo  ina  sadifu  sifa  na  uwezo  wake  katika  ulimwengu  wa  roho. Katika  ulimwengu  wa  roho  bundi  ana  uwezo  wa  kuona  na  kujua  mambo  yatakayo  mtokea  mtu  miaka  30  hadi  sitini  ijayo. 
 
Bundi  anaweza  kuona  kifo  cha  mtu  miaka  kumi  mbele, siku moja  mbele, siku mbili  mbele, wiki nakadhalika.
Hii ndio  sababu  inayo  mfanya  bundi  kutoa  taarifa  kwa  mhusika, ndugu, jamaa  na  marafiki  zake siku kadhaa  kabla  ya  kifo  cha  mtu  huyo.
 
Bundi  hufanya  hivyo  kwa  kutoa  mlio maalumu. Wachawi  kwa  sababu  wanafundishwa  namna  ya  kuwasiliana  na  bundi, bundi  anapotoa  mlio  wa  kuashirikia  kutokea  kwa  msiba,  mchawi na  yeye  hupiga  mluzi ima  kwa  mdogo ima  kwa  filimbi  ya  kichawi  kumjibu  bundi, na  bundi  asipo  jibu  mlio  huo, basi  mchawi  anakuwa  amejua  kuwa  siku  zake  zap  kuishi  hapa  duniani  zimefika  ukingoni.

Mtoto  anapozaliwa, wachawi  kwa  kutumia  uchawi  na nguvu  za  kiroho zap  bundi  hupeleka jina  la  mtoto  huyo  ili  kujua  atakuwa  nani  baadae, na  endapo  itajulikana  kwamba  mtoto  huyo  atakuwa  mtu  mkubwa  mwenye  mafanikio, basi  nyota  yake  itaibwa  mara  moja.
Nyota  hii inapochukuliwa  ima, huuzwa  kwa  mtu, hutumikishwa  msukule, ama  kuzikwa.
 
Nyota ya  mtoto  mchanga  inapo chukuliwa, hubadilishwa  na  nyota  chafu  na  matokeo  yake  mtoto  huyu  anaanza  kuishi  maisha  ambayo  si  yake.
Vile vile  kwa  kumtumia  bundi, wachawi  huweza  kurudisha  nyuma  jambo  baya  ambalo  lingemtokea  mtu  miaka  ya  mbeleni.
 
Kwa  mfano  ramani  yako  ya  maisha inaonyesha  kuwa  utafariki  kwa  maradhi ya  kisukari  ukiwa  na  miaka  75. Wachawi   kwa  kumtumia  bundi  wanaweza  kuyarejesha  nyuma  maradhi  hayo  na  kukufanya  uyapate  ukiwa  na  miaka thelathini.
 
Mambo  mengine  ya kichawi  ambayo  wachawi  huwatumia  bundi  kuyafanya  ni  pamoja  na :
1. Mavi  ya  bundi hutumika   kwenye  ungo wa  kusafiria  kichawi

2. Mavi  ya  bundi  huchanganywa  na  mavi  ya  chatu,  sokwe, nyani, maji ya maiti, mavi ya mtu  aliye  jisaidia akiwa  porini  pamoja  na  madawa mengine, katika kumtia  mtu  mikosi.

3. Matambiko  ya  biashara na  madini  migodini

4. Hutumika   kufungua  milango  ya  kuzimu  wakati wa  kuvuka  kutoka  duniani  kwenda  kuzima  kwa  njia  ya kupitia  baharini.

5. Kuwa  na  uwezo  wa  kuona  wachawi, kuona  mambo  yaliyo  jificha, mambo yatakayo  tokea  mbeleni, mambo  ya  siri.                                                                                       

6. Kuwakaribisha  watu   kwenye  malango   makuu  ya  kichawi,ya  miji, nchi  nakadhalika.

ANAPOKUWA  NCHINI  TANZANIA, DOKTA. MUNGWA  KABILI  ANAPATIKANA  KWA  SIMU  NAMBA
0744  000 473

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Novemba 12

Rais Magufuli Na Museveni Walaani Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) Kuanza Kuichunguza Burundi

$
0
0
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ametoa tamko la kulaani uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ambayo imemuagiza mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo kuanzisha uchunguzi dhidi ya mgogoro wa Burundi.

Rais Museveni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema ICC inaingilia mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kuwahusisha viongozi wa Jumuiya hiyo jambo ambalo sio sahihi na linarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani ya Burundi.

Rais Museven amezungumza hayo kabla ya kuagana na Rais Magufuli ambaye jana amemaliza ziara rasmi ya kiserikali ya siku 3 nchini Uganda na kurejea nchini Tanzania.

Akizungumzia uamuzi huo wa ICC Mh. Magufuli amesema hatua hiyo inarudisha nyuma hatua zilizochukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo iliunda Kamati ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi inayoongozwa na Mhe. Rais Museveni na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa.

Rais Magufuli aliagana na Rais Museveni katika Mji wa Masaka na baadaye kusindikizwa na Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Edward Kiwanuka Sekandi hadi Mutukula, mpakani mwa Tanzania na Uganda.

TAWA, Polisi wakamata jangili, meno ya Tembo

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maafisa wa Uhifadhi wa Wanyamapori wamefanikiwa kumkamata jangili akiwa na meno ya Tembo 5 yenye thamani ya MIL 100 na mshitakiwa yuko kituo cha Polisi morogoro.

Taarifa kutoka kwa jeshi la Polisi morogoro mshtakiwa anategemea kufikishwa mahakamani. Aidha, Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA Bw. Twaha Twaibu ameeleza kuwa walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa jangili huyo wa meno na kutuma maafisa wanyamapori kutoka Makao Makuu ya TAWA wakishirikiana na jeshi la Polisi na kuweza kumkamata jangili huyo.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akiongelea tukio hilo, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliejulikana kwa jina la Nehemiah Nashon akiwa katika chumba namba 104 cha Hoteli ya BZ iliyopo maeneo ya Nane-nane Mjini Morogoro, na kwamba vipande hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 100.

Taarifa Ya Waziri Wa Afya,ummy Mwalimu Ya Mwezi Septemba Na Oktoba Kuhusu Mwenendo Wa Ugonjwa Wa Kipindupindu Nchini

$
0
0
Ndugu Wanahabari,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kutoa taarifa za ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeendelea kuwepo katika mikoa kadhaa hapa nchini ukiwa unaongezeka na kupungua kwa vipindi tofauti.

Ndugu Wanahabari,
Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 Septemba 2017 hadi 30 Septemba 2017, jumla ya wagonjwa walioripotiwa walikuwa ni 532 na vifo 8. Mikoa na wilaya zilizoripoti kipindupindu kwa mwezi Septemba ni Tanga-104 na vifo-2(Tanga Jiji-2, Korogwe Mjini-45, Korogwe Vijijini-23 na kifo-1, Handeni Vijijini-20, Handeni Mjini-8 na kifo-1, Muheza-6), Iringa-22 na kifo-1(Iringa Vijijini1), Njombe-10(Wanging’ombe-10), Katavi(Katavi Vijijini-6), Iringa-2(Mufindi-2), Songwe-82(Songwe Vijijini-82), Mbeya-254 na vifo-3(Mbeya Vijijini-16, Mbeya Mjini-11, Chunya-68, Mbarali-159 na vifo-3) na Kigoma-52 na vifo-2(Kigoma mjini-52 na vifo-2).

Vile vile katika kipindi cha kuanzia tarehe 1 hadi 31 Oktoba 2017 , jumla ya wagonjwa walioripotiwa walikuwa ni 570 na vifo 10. Mikoa na wilaya zilizoripoti kipindupindu kwa mwezi Oktoba ni Dodoma-14 na kifo-1(Kongwa-1, Chamwino-9, Bahi-4 na kifo-1), Iringa-58 na kifo-1(Iringa Vijijini-58 na kifo-1), Tanga-6 na kifo-1(Mkinga-6 na kifo-1), Morogoro-7(Kilosa-7), Mbeya-109 na vifo-3(Chunya-53 na kifo-1, Mbarali-25,  Mbeya Mjini-18, Mbeya Vijijini-13 na vifo-2) na Songwe-376 na vifo 4(Songwe-376 na vifo-4).

Ndugu Wanahabari,
Bado maambukizi mapya ni tishio kwani kuna ongezeko la idadi ya Mikoa na Halmashauri zinazotoa taarifa za wagonjwa.  Vile vile nchi yetu inaelekea katika majira ya mvua ambazo zinaweza kuongeza kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa, hivyo tunahitaji kuzidisha juhudi za kuzuia ugonjwa huu, kwa kusimamia kikamilifu maelekezo na miongozo stahiki inayotolewa.

Ufuatiliaji wa ugonjwa wa Kipindupindu umebaini kuwa wagonjwa wamekuwa wakiishi mbali na jamii linganifu na mahali pale kituo cha afya kilipo. Hii imechangia wagonjwa kutofika kituo cha kutolea huduma za afya kwa wakati na hivyo kupelekea kupoteza maisha. Hivyo, Wizara inaagiza kuwa vituo vya kutolea “Oral Rehydration Salt”, maarufu kama ORS, katika jamii (Community ORS points) vianzishwe na halmashauri kwa kushirikiana na jamii ili kuzuia vifo. Jamii zielekezwe namna ya kutumia ORS kwa usahihi. Endapo ORS haitapatikana, jamii ielekezwe kuchanganya chumvi na sukari kwa kutumia maji safi yaliyochemshwa kiasi cha lita moja na vijiko viwili vya sukari na nusu kijiko ya chumvi. Njia hii ya kutumia ORS au mchanganyiko wa chumvi na sukari ndio njia ya muhimu ya kuokoa maisha ya mgonjwa wa Kipindupindu kwani inasaidia kupunguza kasi ya kupungukiwa kwa maji mwilini inayosababisha kifo.

Ndugu Wanahabari,
Ni dhahiri kuwa ushirikishwaji wa sekta zote kwa ngazi zote hadi katika jamii ni muhimu sana katika kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu.  Wizara inasisitiza kuwa wadau wote wapewe nafasi katika mapambano haya kupitia vikao mbalimbali ili kujadili udhibiti wa ugonjwa wa Kipindupindu kwenye halmashauri na mikoa. Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala pia wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.

Wizara inaendelea kuwasihi wananchi kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa Kipindupindu.  Jamii izingatie kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na:
  1. Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo tunamoishi.
  2. Kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo, na baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia.
  3. Kunywa maji safi na salama yaliyotakaswa kwa dawa (kama vile water guard) au yaliyochemshwa na kupoa.
  4. Kuzingatia ushauri na elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu, ili jamii iondokane na imani potofu kuhusu Kipindupindu.
  5.  Kufikisha wagonjwa wa Kipindupindu mapema katika vituo vya kutolea huduma ili wawahi kupata matibabu.
Ndugu Wanahabari,
Changamoto moja wapo katika kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu ni upatikanaji wa maji safi na salama. Wizara inasisitiza yafuatayo yasimamiwe kwenye halmashauri na mikoa yote nchini.

 Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote mijini na vijijini hasa wakati wa mlipuko wa Kipindupindu. Hii ni pamoja na:
  1. Mamlaka za maji katika ngazi zote ziweke mkazo wa kuwepo kwa vyanzo mbadala vya maji.
  2.  Utakasaji wa maji ya bomba kwa njia ya kutumia klorini ufanyike kama miongozo inavyotaka na ufuatiliaji wa ubora wa maji ufanyike kulingana na miongozo.
  3. Utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, za ugonjwa wa Kipindupindu kwa kufuata miongozo iliyopo.
  4. Kuongeza uwajibikaji wa viongozi na watendaji (Leadership and accountability): Usimamizi wa utekelezaji wa miongozo katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa huu ni muhimu kwa viongozi na wanaowasimawa. Hii ni pamoja na;
  1. Usimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogondodo za usafi wa mazingira ili kuimarisha matumizi ya vyoo.
  2. Usafi wa mazingira pamoja na udhibiti wa biashara za chakula na pombe za kienyeji katika mitaa.
  3.  Kuzingatia agizo la Mheshimiwa Rais la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Ndugu Wanahabari,
Wizara yangu imekuwa karibu na mikoa na halmashauri katika kudhibiti ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:
  • Kutuma timu za wataalamu kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika kushirikiana na mikoa na Halmashauri katika kudhibiti ugonjwa huu
  •  Kupima vipimo vya maabara na kubaini aina ya vimelea vinavyosababisha ugonjwa pamoja na kupima usikivu wa dawa inayofaa kutibu wagonjwa katika mlipuko huu
  • Kupeleka Vifaa tiba na dawa katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Mabarali kupitia kanda ya bohari ya Dawa (MSD)
  • Kusambaza dawa ya kutibu maji majumbani katika mikoa ya Iringa, Kigoma, Katavi na Tanga

HITIMISHO
Wizara inaendelea kushukuru mchango wa wadau mbalimbali katika kudhibiti ugonjwa huu ikiwemo Sekta ya Maji kwa kuendelea kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji, bila kuwasahu wanahabari kwa kuendelea kusaidiana na Serikali katika kuwaelimisha wananchi juu ya ugonjwa huu. Wizara inaendelea kutoa wito kwa wadau wote katika ngazi zote kushirikiana kwa pamoja katika jitihada za kutokomeza ugonjwa huu.

Asanteni sana
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images