Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wabunge Waeleza Jinsi Walivyo na Hofu Kwa Sasa Kuihoji Serikali

0
0
Baadhi  ya wabunge wameeleza kuingiwa woga wa kuhoji na kudadisi masuala mbalimbali kutokana na kutishiwa kutopatiwa fedha za miradi ya maendeleo majimboni kwao.

Kauli hiyo waliitoa wakati wakichangia semina ya wabunge juu ya jukumu la Bunge katika kufuatilia kikamilifu matumizi ya Serikali yaliyofanyika kwa kamati saba za Bunge.

Kamati hizo ni Kamati ya Bajeti, Kilimo, Mifugo na Maji, Viwanda, Biashara na Mazingira, Huduma za Jamii, Utawala na Serikali za Mitaa na Hesabu za Serikali za Mitaa.

Akizungumza katika semina hiyo, Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alisema wabunge wamekuwa waoga kusemea tofauti na Bunge la 10 na kwamba hoja zinajengwa kisiasa na wengine wanapohoji wanaambiwa hawatapelekewa fedha majimboni.

Alisema jambo linalowafanya wabunge kutosema yale wanayoyataka wananchi ni siasa kuingia bungeni tofauti na mabunge yaliyotangulia ambapo wabunge walikuwa wakiacha siasa lango kuu la kuingilia bungeni.

“Jambo hili linaweza kuwa linasababishwa na viongozi wa bunge ama serikali ambapo hoja zenye manufaa zinaweza kupelekwa bungeni, lakini wakaamua kuziua,”alisema Selasini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mpendae (CCM) Salim Hassan Turky, alisema mambo yote waliyoelezwa wanayajua, lakini kuna kitu kinachomoza bungeni na kinaondoa uhai wa bunge.

“Hasa unapohoji na kudadisi basi na wewe unaitwa na kuhojiwa na kudadisiwa," alisema Turky, "kwa hiyo wabunge wote wanakuwa waoga wa kuuliza maswali".

"Sasa sijui kama utaratibu huu utafanya haki itendeke?”

Aliomba viongozi wa Bunge wakaliangalie hilo na kwamba endapo wakisimamia serikali vizuri wataweza kutekeleza majukumu yao.

Naye Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara alisema kuwa tatizo lililopo ni Bunge kutofanya kazi inavyotakiwa.

“Inafikia Bunge mtu akisema hapana, waliosema hapana wasipewe fedha za maendeleo kwenye majimbo yao wakati hayo mambo hayakuwapo,” alisema Mbunge huyo.

Alisema wabunge sasa wanaogopa kuisema au kuikosoa serikali licha ya kuwa Bunge limeundwa ili kusema kero za wananchi.

“Bunge limebaki kuwa la muhuri na sio Bunge, na sisi hapa tunakuja kwa ajili ya posho na mishahara tu tuliyoambiwa,” alisema Mbunge huyo.

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) alisema nguvu ya Bunge ya kuisimamia serikali ni ndogo kutokana na ukosefu wa fedha.

“Ili tuweze kuwa na mchango madhubuti lazima tujengewe uwezo wa kushughulikia taarifa mbalimbali, Bunge lihakikishe linatujengea uwezo kwenye nyanja mbalimbali wabunge ili kuisimamia serikali ipasavyo kwenye masuala mbalimbali ikiwamo bajeti,” alisema.

Mbunge wa Ileje (CCM), Janet Mbene ambaye alikuwa mwenyekiti wa semina hiyo, alisema kwa umoja wao wabunge wakisimama kwa pamoja serikali itawasikiliza na hawatafanya kazi kwa woga.


Mwalimu Mkuu Amcharaza Viboko Mwalimu Mwenzake

0
0

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Migango wilayani hapa amemchapa viboko mwalimu mwenzake mbele ya wanafunzi akimtuhumu kwa wizi wa sahani tano pamoja na nusu kilo ya sukari iliyotolewa kwa ajili ya mahafali ya wahitimu wa darasa la saba.

Katika taarifa yake ya kulaani kitendo hicho, kaimu katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Biharamulo, Joseph Lugumba alisema mwalimu mkuu, Mateso Musaku alimpiga viboko mwalimu wake Hosea Masatu mbele ya wanafunzi tukio ambalo linalaaniwa na wazazi, uongozi wa CWT na jamii ya Kata ya Runazi wanakoishi walimu wa shule hiyo.

Lugumba alisema baada ya kupata taarifa za mwalimu huyo kuchapwa viboko Ijumaa iliyopita, uongozi wa CWT ulifika Runazi kujiridhisha ambako wanafunzi na wazazi walithibitisha tukio hilo ikidaiwa kwamba mwalimu huyo alifungwa kamba kwenye mti.

Alisema mwalimu Masatu alidaiwa kuiba vitu hivyo siku moja baada ya kumalizika mahafali ya darasa la saba na kwamba alipoulizwa alikiri.

Alisema mbali ya kuonywa, alipelekwa na kufungwa kamba chini ya mti na kuchapwa mbele ya wanafunzi kitendo alichokiita cha udhalilishaji na kinyume cha haki za mtumishi na binadamu.

“Tunashauri mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kwa kutumia mamlaka zilizomteua mwalimu mkuu huyo kuongoza shule hiyo amuwajibishe kwenye ngazi za kinidhamu kwa maana amekiuka kanuni za uteuzi katika kuongoza walio chini yake,” alisema Lugunda.

Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Novemba Mosi baada ya mwalimu Masatu kukamatwa saa nane mchana na mkuu wa shule na kufungwa katika mti uliopo mbele ya shule hiyo na kuchapwa viboko saba huku wanafunzi wakishuhudia.

Mwalimu Musaku alithibitisha kumchapa mwenzake kwa madai kwamba alipata ridhaa kutoka kwa mwalimu aliyetuhumiwa kwa wizi na hakufikiria kama suala hilo lingeweza kuleta matokeo hasi katika jamii.

Alisema kwamba katika madaraka aliyopewa hakuna kipengele kinachomruhusu kutoa adhabu kama hiyo ya kipigo na kwamba ilitumika baada ya mwalimu huyo kukiri kosa na kutaka apewe adhabu ya viboko saba.

Hata hivyo, mwalimu Masatu alisema kitendo cha kupigwa na mkuu wake wa kazi kwa tuhuma za wizi wa mali ya shule ni udhalilishaji.

Alisema baada ya tukio la kupigwa alipelekwa kituo kidogo cha Polisi Runazi ambako alikaa rumande kwa siku tatu kwa madai ya kulewa saa za kazi na aliachiwa Novemba 3.

Hata hivyo, Polisi wilayani Biharamulo hawakutaka kuzungumzia suala hilo.

Kutokana na tukio hilo, Mwalimu Masatu alisema hana amani katika kata ya Runazi na Wilaya ya Biharamulo kutokana na taarifa za tukio hilo la kudhalilishwa kwake kusambaa.

Alisema hana imani kama ataingia darasani na kufundisha ipasavyo kwani ameathirika kisaikolojia. 

Aidha, alikana madai ya kuiba sukari na sahani tano na kwamba ametuma malalamiko kwa mratibu elimu kata na mwenyekiti wa kamati ya shule ili wachukue hatua dhidi ya mkuu wake kumdhalilisha kiutumishi na kijamii.

Walimu katika Shule ya Msingi Migango, Francisco Leonard na Faustine Mathias walioshuhudia tukio hilo walisema kitendo alichofanyiwa mwenzao ni udhalilishaji na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuanzia kamati ya shule hiyo mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya zifuatilie na kujiridhisha juu ya ushahidi utakaotolewa ili kuhakikisha mwalimu aliyedhalilishwa anatendewa haki kwani kila anakopita ananyooshewa vidole na kukosa amani kuanzia kwenye familia yake.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wende Ng’ahala alisema japokuwa hajapewa taarifa anajipanga kulishughulikia.

Zitto Kabwe aripoti polisi, apigwa kalenda Hadi Ijumaa Ijayo

0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe, leo ameripoti kituo cha Polisi Chang’ombe kama alivyotakiwa baada kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana Oktoba 31, 2017. Baada ya kuripoti Polisi wamemueleza kuwa anapaswa kuripoti tena kituoni hapo Ijumaa ijayo, Novemba 17 mwaka huu.

Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ameeleza kuwa Kadhia hii inahusisha baadhi ya maneno katika hotuba yake ya Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke. Maneno hayo ni yafuatayo:

1.Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.

2.Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

Mh. Ndugu Zitto aliongozana na timu ya mawakili wa chama pamoja na mke wake kituoni Chang’ombe.

Hatime Viongozi wa ACT- Wazalendo waitikia wito wa polisi

0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Doroth Semu amefika katika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Semu amefuatana na Katibu wa Kamati ya Ulinzi ya chama hicho, Mohamed Babu.

Viongozi hao pamoja na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Yeremia Maganja wanatakiwa kufika katika kitengo hicho wakiwakilisha wajumbe wote wa Kamati Kuu ambao walitakiwa kuripoti leo.

Novemba 2, 2017, Chama  hicho kilidai kimepokea wito toka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) wa kuwataka Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo wafike Kituo cha Makosa ya Fedha (Financial Crime Unit) kilichopo Maeneo ya Kamata, Kariakoo Jijini Dar es salaaam kwa ajili ya mahojiano siku ya leo Jumatatu, Novemba 6, 2017. 

Awali, chama hicho kiligoma kuitikia wito huo kwa madai kwamba Jeshi la Polisi halina madaraka ya kushughulikia wala kuingilia maamuzi halali ya vyombo (organs) katika vyama vya siasa na  kikasema kuwa  kitaendelea na kampeni  za uchaguzi mdogo wa madiwani kama kawaida huku kikiwataka  Polisi watafute namna na wakati sahihi wa kufanya mahojiano na viongozi wa chama hicho. 


Hatima ya Zitto Kabwe na Kubenea Kutimuliwa Bungeni Au Kutotimuliwa Kujulikana Kuanzia Kesho

0
0
Mkutano  wa tisa wa Bunge la 11 utaanza vikao vyake kesho mjini Dodoma  huku kukiwa na hofu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya chombo hicho cha kutunga sheria kwa wabunge wawili Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) na Saed Kubenea (Chadema).

Katika mkutano uliopita wa chombo hicho cha kutunga sheria, Spika Job Ndugai aliagiza wawili wakamatwe na polisi na kufikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akiwatuhumu kwa utovu wa nidhamu.

Zitto, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, alifika mbele ya kamati hiyo na kujitetea, lakini kamati hiyo haikufanikiwa kumhoji Kubenea baada ya Mbunge wa Ubungo huyo kufika mbele yake akiwa anasukumwa kwenye kiti cha wagonjwa.

Kubenea anadaiwa kulitumia Kanisa la Ufufuo na Uzima kumtuhumu Spika kusema uongo bungeni kuhusu idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).

Kwa upande wa Zitto, anadaiwa kumtuhumu Spika kukosea utaratibu alioutumia katika kushughulikia ripoti mbili za uchunguzi wa almasi na tanzanite akidai ripoti zake zilipaswa kujadiliwa bungeni.

Kutokana na tuhuma hizo, kamati hiyo ya bunge inatarajiwa kutoa taarifa yake kuhusu kuhojiwa kwa wabunge hao na hatima yao katika mkutano wa chombo hicho utakaoanza kesho.

Masuala mengine yanayotarajiwa kuwamo katika shughuli za vikao vya mkutano huo ni pamoja na wabunge kujadili na kuishauri serikali kuhusu mapendekezo ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali katika mwaka wa fedha unaofuata.

Kwa mujibu wa kifungu cha 94(1) cha Kanuni za Bunge, chombo hicho katika mkutano wake wa Oktoba - Novemba kwa kila mwaka, kwa siku zisizopungua tano, kinapaswa kukaa kama kamati ya mipango ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 63(3)(C) cha Katiba kwa kujadili na kuishauri serikali kuhusu mapendekezo hayo.

Katika mkutano huo, Bunge pia linatarajiwa kupokea, kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali.

Kifungu cha 94(2)(b) cha Kanuni za Bunge kinabainisha kuwa Bunge katika mkutano huo litapokea, kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu vyanzo vya mapato vya serikali na pia litapokea, kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu mapendekezo ya utekelezaji wa mpango wa serikali na vipaumbele kuhusu mpango huo.

Wabunge watapokea taarifa za utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa nusu mwaka kuanzia Julai hadi Novemba.

Katika mkutano huo, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha miswada mbalimbali ukiwamo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 wa mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano (TTCL) wa mwaka 2017 na Muswada wa Uwakala wa Meli Tanzania.

Bunge pia linatarajiwa kuutumia mkutano huo kutapokea taarifa za utekelezaji wa kamati zake katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18.

Hakimu Atoa Onyo.....Atishia Kuifuta Kesi ya Vigogo wa NIDA

0
0
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Respicious Mwijage ameuambia upande wa mashtaka kuwa siku akipandwa na mashetani ataifuta kesi ya vigogo wa Mamlaka ya Vitambulisho vyaTaifa (NIDA) endapo kama upelelezi hautakamilika.

Hakimu Mwijage alitoa angalizo hilo baada ya Wakili wa Serikali, Peter Vitalis kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na baada ya kusema hayo, Hakimu Mwijage alisema kesi hiyo ina takribani siku 365 na upelelezi haujakamilika jambo ambalo linatoa taswira mbaya.

“Kamilisheni upelelezi ili kama hawa wamekula fedha za umma wafungwe au kama hawajala waachiwe huru, siku mashetani yangu yakipanda nitafuta hii kesi.”

Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi December 6,2017 huku akiutaka upande wa mashtaka kufika na taarifa kuhusu upelelezi.

Kesi hiyo inamkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake saba, ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 1.16.

Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege,  Xavery Kayombo, Meneja Biashara wa mamlaka hiyo, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani.

Washtakiwa pamoja na mashtaka mengine yakiwemo kuisababishia Serikali hasara wanadaiwa tarehe tofauti kati ya January 15 hadi 19,  mwaka 2010 katika Makao Makuu ya NIDA wilayani Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kwa nafasi walizokuwa nazo walitumia madaraka  vibaya kwa kuidhinisha malipo bila kufuata viwango vya kubadilishia fedha.

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu,vidonda Vya Tumbo,busha,nguvu Za Kiume

0
0
MTALAAM NA BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU NAYALIYOSHINDIKANA KAMA VILE PUMU,VIDONDA VYA TUMBO,BUSHA,NGUVU ZA KIUME,KISUKARI,MIVUTO YOTE,KUSAFISHA NYOTA,KURUDISHA MALI,NK.
 
Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani
 
Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI,KIUNO KUUMA,MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA,KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO,NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni SUPER SAYI 3,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu 

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

SUPER SAYI 4 Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI,PRESHA,UZAZI,NGIRI,PUMU,MALARIA SUGU,VIDONDA VYA TUMBO,CHANGO AINA ZOTE,BP,BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR UPENDO ANAPATIKA KADA YA ZIWA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM HUDUMA HIZI UTAZIPATA MAGOMENI 

SIMU NO 0753 15 30 26, 0715 26 85 10 

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

Tiba ya Asili ya Pumu, Vidonda vya Tumbo, Busha na Nguvu za Kiume

0
0
Tatizo La Upungufu Wangu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Ile Tiba Sahihi Ya Matatizo Haya 

CHAZO CHAKE NA VISABABISHO VYAKE:
DALILI:-Mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata Choo vizuri hata ukipata Choo kinakuwa kigumu Kama cha mbuzi ,Misuri  kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. Miguu kuuma na kuwaka au kufa ganzi

TIBA YAKE:
RADI-90-POWER---Ni dawa ya vidonge asilia iliyo tengenezwa kutokana na miti shamba yenye uwezo mkubwa kabisa ktk kutibu matatizo (4) Kwa wakati ==>(1)Huongeza nguvu za kiume maradufu (2)kati ya umri (15-90)(3)hurefusha na kunenepesha uume mdogo kadrii upendavyo inch (6-8)kwa dakika (15)tu.(4)kuchelewa kufika kileleni (5)kuimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa. 

Nini huchangia kuwa na matatizo Kama haha? Kisukari,Presha,Ngiri,Zinaa,Kiuno kuuma, Tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kutopata Choo vizuri, Mgongo kuuma. 

RADI-90-POWER:-Hutibu na kumaliza matatizo haya kwa mda mfupi tu na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika(45)kwa tendo(1) na utarudia Mara (5)na zaidi bila kuchoka huanza kazi baada ya dakika( 30)tu.Pia huongeza Hamu ya kufanya tendo la ndoa maradufu(2),Kumbuka tatizo hili si geni, kigeni ni tiba sahihi ya kutibu matatizo haya na pia ina guarantee ya miaka(65)na zaidi. 

Tunatibu :---Kisukari, Presha, uzazi, Ngiri, Pumu, maralia sugu, vidonda vya tumbo, chango aina zote, kifua kikuu na busha bila upasuaji. 

ITUJA NO2:--Nidawa ya mvuto wa biashara, kazi, kupandishwa cheo, kupendwa na mwajiri, kumvuta mme/mke,mpenzi, hawara, mchumba unaye muhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zake kwa dhati utampata kwa lisaa limoja (1)tu na atatulia daima na kumfunga asitoke nje ya ndoa.

BOMBA2:--Ni dawa ya kupunguza matiti makubwa, unene turbo, kitambi,mafuta mwilini,uzito,toa fangasi makovu, chunusi, nyama zembe, michirizi, kwa siku tatu (3)tu.NO7:--Inaongeza makalio, Hips, miguu kwa saizi uipendayo kwa siku (2)tu.

HUDUMA HIZI Na zingine nyingi UTAZIPATA popote TANZANIA Name NJE YA NCHI:--MUONE DR SHARIF AU PIGA SIMU NO:-0659347707, 0763483813 ,0688991509,0659347707.  DR SHARIF

Mwigulu awataka wananchi kutofanya hasira kwenye kuchagua Madiwani.......Awataka Waichague CCM

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mwigulu Nchemba amewataka wananchi ambao wanafanya uchaguzi mdogo wa udiwani nchini wasitumie hasira kwenye upigaji kura bali wachague wagombea wa CCM ili kutimiza nguzo tatu za uongozi.

Mh. Nchemba ameyasema hayo wakati akimnadi Mgombea udiwani wa kata ya Nangwa wilaya ya Hanang  ambapo amewaambia wananchi watambue kwamba serikali iliyopo madarakani inaongozwa na CCM hivyo wachague wagombea hao 

Aidha Mh. Nchemba ameongeza kwamba uchaguzi mdogo ni uchaguzi rahisi sana kama watu wataamua kutafakari kwasababu ilani inayotekelezwa ni ya CCM na la pili ni huu ni uchaguzi wakujaza nafasi

"Kwasasa ilani inayofanya kazi ni ya CCM hivyo msifanye hasira katika kuchagua kwani huwezi kuwasha tochi kwa kuweka mabetri mawili ya CCM alafu la tatu liwe bunzi, Tochi haiwezi kuwaka," Mh. Nchemba

Pamoja na hayo Nchema amewataka wananchi hao waweze kumpitisha mgombea huyo mwanamke kwa kudai kwamba anafaa kuongoza na kwamba wa kina mama ni waaminifu zaidi kwani Diwani aliyepita alikuwa mwanaume lakini alihukumiwa mahakamani kwa kosa la ubadhilifu wa mali za umma

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Rais Magufuli Kufanya Ziara ya iku 3 Nchni Uganda

0
0
Rais John Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini Uganda ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo tangu aingie madarakani.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema Rais Magufuli atawasili nchini humo Novemba 9,2017 na atapokewa na mwenyeji wake, Rais Yoweri Museveni.

Akiwa nchini humo pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli atashuhudia utiaji saini wa makubaliano mbalimbali.

Pia, atatembelea eneo litakalokuwa kituo cha pamoja cha huduma kati ya Tanzania na Uganda.

Taarifa hiyo imesema Rais Magufuli na mwenyeji wake watazungumza na waandishi wa habari Novemba 10,2017.

Ziara ya Rais Magufuli inafanyika katika wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili ukitajwa kuimarika zaidi ikiwemo kuzinduliwa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta.

Bomba hilo la mafuta ambalo litagharimu Dola 3.5 bilioni za Marekani litapita katika mikoa minane nchini.

Mara ya mwisho Rais Magufuli kutembelea Uganda ilikuwa Mei 2016 alipokwenda kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Museveni.

Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amezitembelea nchi za Kenya, Rwanda na Uganda.

Zitto Kabwe Kufungua Kesi Mahakamani Kupinga Kuwa Na Mamlaka Moja tu ya Kutoa Takwimu za Taifa

0
0
Kiongozi wa  ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema watafungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vilivyomo katika Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kitengo cha upelelezi wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam, Zitto amesema haiwezekani kukawa na mamlaka moja ya kutoa takwimu.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema tangu kutungwa kwa sheria hiyo imekuwa ikipigiwa kelele kutokana na kuminya uhuru wa wananchi kuchambua takwimu.

"Tunataka kufungua kesi mahakamani kupinga sheria ya takwimu kuzuia watu kuchambua, huko ndiko ukweli utajulikana na wananchi watajua sheria hii ilivyo. Hii itakuwa kesi ya kwanza kwa sheria hii kupelekwa mahakamani," amesema Zitto.

Amesema, "Tuna taarifa ambazo hatukuzitoa, tukifika mahakamani tutazitoa na NBS- (Ofisi ya Taifa ya Takwimu) haiwezi kusema una hatia au la kwa kuwa wao si Mahakama. Sisi tulitumia takwimu zao kuchambua na tumewaeleza polisi kwamba tutawaeleza zaidi tukifika mahakamani."

Zitto ametoa kauli hiyo siku moja baada ya jana Jumapili Novemba 5,2017 Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa kusema mtu mwenye mamlaka ya kutoa takwimu ni ofisi hiyo pekee.

Dk Chuwa katika kipindi maalumu kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Azam kuhusu miaka miwili ya utawala wa Rais John Magufuli aliyeingia Ikulu Novemba 5,2015 alisema takwimu za Taifa ni lazima ziheshimiwe na si kila mtu anastahili kuzitoa.

Zitto akizungumzia tuhuma za uchochezi zinazomkabili amesema, “Nimeripoti leo kama nilivyotakiwa lakini nimeelezwa nirudi tena Ijumaa Novemba 17,2017 wanadai wanasubiri chaji kutoka kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na baada ya hapo wataona kama watanipeleka mahakamani au la.''

"Lakini kesho, mimi nitakuja hapa (kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha) saa tatu au saa nne kama nilivyotakiwa. Mtakumbuka natuhumiwa kwa kesi mbili ya sheria ya takwimu na makosa ya mitandao," amesema.

Zitto pia amezungumzia uamuzi wa Jeshi la Polisi la kuiita kamati kuu ya ACT- Wazalendo akisema haina uwezo huo na wao kama walivyoeleza jana katika mkutano na waandishi wa habari watawakilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Yeremia Maganja na Katibu Mkuu Doroth Semu.

"Polisi hawana uwezo wa kuihoji kamati kuu, ndiyo maana mwenyekiti na katibu mkuu wapo hapa wanaendelea na mahojiano... huwezi kuwaita wajumbe wote wa kamati kuu kwa kuwa mtendaji wa chama ni katibu mkuu na msemaji ni mwenyekiti na ndicho tumekifanya," amesema.

Taarifa Muhimu Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Novemba, 2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mkoa wa Kagera.

Akiwa njiani Kutoka Chato Mkoani Geita alikokuwa mapumzikoni kuelekea Bukoba Mjini Mhe. Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Muleba na Kemondo, Bukoba Vijijini na kuwahakikishia kuwa Serikali itasaini mkataba na kampuni ya kutoka Jamhuri ya Korea kati ya mwezi Desemba mwaka huu na Januari mwakani kwa ajili ya kuanza kuunda meli mpya katika ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba idadi kubwa ya abiria na mzigo mkubwa zaidi ikilinganishwa na meli zilizopo

“Tunaunda meli ya kisasa itakayobeba abiria wengi na mizigo mingi, na pia tutakarabati meli zilizopo za MV Victoria na MV Butiama, tunataka pamoja na kujenga barabara, tuhakikishe kuna meli za uhakika ili muweze kusafiri na kusafirisha mazao yenu kwenda kwenye masoko” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu ufugaji Mhe. Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha mifugo yote inawekwa alama kwa mujibu wa sheria, ili kurahisisha utambuzi wa mifugo inayoingizwa nchini kutoka nchi jirani na pia kudhibiti ruzuku inayotolewa na Serikali kwa dawa za mifugo ya hapa nchini.

“Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani, ndio maana tumeamua kukamata mifugo na kuchukua hatua kwa mujibu wa kisheria, na hata huko kwenye nchi jirani wakishika mifugo ya kutoka Tanzania wachukue hatua za kisheria za nchi hizo” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Hata hivyo amewataka wananchi wa Kagera kuacha kuvamia maeneo ya hifadhi ikiwemo hifadhi ya Burigi na ameagiza viongozi wa Wilaya ya Muleba kufuatilia madai ya wananchi juu ya kuuzwa kwa ardhi ya kijiji kulikosababisha wananchi kukosa maeneo ya kulima na kulisha mifugo yao.

“Na kuna watu waliouziwa ranchi na Serikali, watu hao hawajaziendeleza ranchi hizo na badala yake wanawakodisha wananchi, wafuatilieni na mkiona hawajaziendeleza nyang’anyeni muwape wananchi wazitumie kwa ufugaji, lakini pia hakikisheni wananchi hawavamii maeneo ya hifadhi yaliyotengwa” ameongeza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Mkoa na Wilaya za Mkoa wa Kagera kuwachukulia hatua maafisa wote wa halmashauri ambao bado wanawatoza ushuru wakulima wanaosafirisha mazao yaliyo chini ya tani moja kwa kuwa tayari Serikali imeshaamua kuondoa adha hiyo na kuwawezesha wakulima wadogo kunufaika na kilimo chao.

Mchana wa leo (06 Novemba, 2017) Mhe. Rais Magufuli atafungua mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Bukoba
06 Novemba, 2017

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Waziri Mkuu Avuna Wanachama Wapya 37 Toka CHADEMA na CUF

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama 35 kati ya hao wametoka CUF na wawili wametoka CHADEMA.

Wanachama hao walipokelewa jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Bw. Essau alisema wanachama hao wote wametoka kata za Mbekenyela na Matambalale. Walikabidhiwa kadi mpya za CCM, na kula kiapo cha uaminifu.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake wapya, Bw. Mohammed Issa Ndogoro ambaye amehamia kutoka CHADEMA, alisema wamejiunga na CCM baada ya kuridhishwa na mwelekeo wake. Alisema wameguswa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli inavyofanya kazi ya kutatua kero za wananchi.

Alisema amekaa upinzani kwa miaka 23 lakini anaikubali CCM sababu ya uwazi wake na ameshangaa kuona akipewa kadi na stakabadhi ya walipo yenye jina lake, jambo ambalo hajawahi kuliona katika vyama vingine vya upinzani.

“Sote sisi tumehamia CCM, uhai wa chama ni michango. Nani aseme hapa kama aliwahi kupewa stakabadhi katika chama chake, na kama yupo nampa sh. 5,000/- sasa hivi,” alisema Bw. Ndogoro na kuamsha kicheko kwenye mkutano huo.

Waziri Mkuu: Watakaokwamisha Malipo Ya Korosho Kukiona

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote watakaokwamisha malipo ya wakulima wa zao la korosho.

“Hatutamuacha mtu yeyote atakayesababisha wakulima kuchelewa kulipwa fedha zao. Tutawakamata wote na kuwachukulia hatua stahiki.”

Ametoa kauli hiyo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu alisema wakulima hao ni lazima walipwe fedha zao kwa wakati na asitokee mtu wa kuzitamani fedha hizo.

“Mkulima amelima mikorosho mwenyewe, ameokotoa na kukodoa mwenyewe wao wamepewa dhamana ya kuziuza, hivyo wahakikishe wanawapelekea fedha zao na wala wasizitamani.”

Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika vya Msingi wahakikishe mkulima hakosi sh. 3,500 katika kilo moja ya korosho atakayoiuza baada ya kukatwa michango.

Alisema bei ya juu ya korosho katika minada ya mkoa wa Lindi sh. ni 3,970 na ya chini sh. 3,800. “Vyovyote itakavyokuwa mkulima hawezi kukosa sh. 3,500, viongozi wa AMCOS mnisikie.”

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa bei ya zao la korosho pamoja na kupungua kwa makato ya mkulima ambapo kwa sasa hayazidi sh. 300 katika kilo moja ya korosho.

Rais Magufuli Ameirudisha Nchi Kwa Wananchi

0
0
Na Judith Mhina – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha nchi kwa wananchi na kwamba hayo ni mapinduzi ya ajabu ambayo hayajawahi kutokea katika nchi zetu hususan Afrika.

Maneno hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba alipofanya mahojiano na redio Uhuru mwishoni mwa wiki iliyopita katika ofisi zao zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar-es-salaam.

Dkt.Rioba amesema Mhe. Rais ameirudisha nchi kwa wananchi kwa kuwa anatekeleza “kile anachoambiwa na wananchi, na ahadi alizowaahidi wakati akiwaomba kura” anaeleza Dkt. Rioba na kuongeza kuwa yeye binafsi anamshukuru Mhe. Rais kwa “kuirudishia heshima Tanzania“.

Katika mahojiano hayo, Dkt. Rioba alieleza kuwa tangu kushika madaraka miaka miwili sasa  Rais Magufuli amekuwa ‘busy’ kuhakikisha nchi inakaa sawa kimfumo ndio maana hajashughulika sana na safari za kwenda nje ya nchi.

Rais anataka kutengeneza “mfumo wa kimkataba au kibiashara na hawa mabwana wakubwa (wawekezaji toka nje) utakaowezesha kugawana nusu kwa nusu katika kile kinachopatikana katika uendelezaji wa rasilimali zetu badala ya mifumo ya zamani ya kukubali kila mfumo unaoletwa na nchi zilizoendelea” alisema Dkt. Rioba.

Mkurugezi Mkuu huyo alikieleza kituo hicho cha redio kuwa yeye binafsi anadhani kilichosababisha Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Barrick kumsikiliza Mhe Rais ni umakini wa kiongozi huyo kwa “hanunuliki, hahongwi hongwi maana Afrika ina viongozi wengi ambao wananunuliwa na kuhongwa” lakini sasa wanajua huyu ni tofauti.

Dkt. Rioba anamuona Rais Magufuli kuwa kiongozi anayesimamia mambo yanayo wanufaisha wananchi wake na “hakimbii kimbii kwenda huku na kule kuomba” na kuifananisha nchi yetu na zile zinazotoa misaada katika nchi nyingine. Kwa kuwa fedha wanazozipata zinatokana na  rasilimali zetu na kueendeleza nchi zao.

Mhe Magufuli alisema; “Nchi yetu ilitakiwa kuwa Donor Country, yaani nchi inayotoa misaada kwa nchi nyingine”.

Ninachoweza kuwaambia Watanzania wenzangu miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano madarakani, hakika viongozi wetu wameonesha nia nzuri na wanatakiwa kuunga mkono kwa hili analolifanya Rais Magufuli wakati huu wa mpito.

Nchi yoyote inapopita katika mpito ni lazima kuna mambo yalikuwa hayaendi sawa   na mengine yamekwenda sawa. Mpito ukitokea kuna mabadiliko yatakayojitokeza. Mfano Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipendekeza mfumo wa vyama vingi japo wananchi wengi, bado waliutaka mfumo wa chama kimoja.  Aidha kutokana na kubadilishana uongozi hapa Tanzania, mabadiliko mengi yalijitokeza ambayo yalikuwa mazuri na mengine sio mazuri kwa kuwa ni kipindi cha mpito.

Dkt. Rioba amesema ujio wa Rais Magufuli ulikuwa ujio muhimu sana kwa wakati huu, kwa ajili ya kurekebisha yale yote yaliyojitokeza ambayo hayakuwa sawa. Akitoa mfano wa mwana falsafa mmoja anayeitwa Fans Fanon wakati wa vita vya ukombozi nchini Algeria alisema:

“Kila kizazi kinakutana na majukumu yake ya msingi ya kutekeleza au kuyatelekeza na kusubiri matokeo yake”

Mkurugezi Mkuu huyo wa TBC alieleza kuwa kwa maoni yake Rais Magufuli amekuwa kiongozi sahihi aliyekuja kwa wakati sahihi, ili kurekebisha mambo kwa namna moja au nyingine ambapo hapa na pale tulijikwaa kwa sababu tulitoka nje  ya  misingi iliyojengwa na Taifa letu.

Kuhusu suala la kuwa na uchumi mzuri katika nchi Rioba amesema tafiti zinafanyika kwa mrengo wa kimagharibi zaidi ambapo, wanahalalisha mifumo ya uchumi wanayoitaka wao. Wachumi walio wengi wanasema ili uchumi uwe mzuri na nchi kuendelea ni lazima kuwa na Ardhi, tekinolojia, rasilimali ziwe nyingi nk , lakini sio kweli.

Mfano nchi ya Singapore hawana rasilimali zaidi ya bahari na samaki lakini uchumi wao ni mzuri sababu moja kubwa ni uongozi bora ambao unasimamia matumizi sahihi ya rasilimali kwa manufaa ya wananchi wa nchi husika. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi ya 4 duniani kwa wingi wa madini lakini haijaendelea, mpaka leo kuna watu wanaomiliki madini katika nchi hiyo wako nje hivyo faida yote inayopatikana kutokana na madini hayo inazinufaisha nchi za nje.

Jambo la msingi Rais Magufuli anataka rasilimali zilizopo, hata kama kidogo kitumike kwa manufaa ya wananchi wanyonge wa Tanzania.  Tanzania ya Rais Magufuli amesema hapana haya madini yanayopatikana hapa Tanzania ni lazima tugawane nusu kwa nusu.

Dkt. Rioba anasema Rais ameonesha mfano kwa nchi nyingine za Afrika zenye rasilimali kama zetu, kuwa hili la kugawana faida nusu kwa nusu, hata kama hatuna tekinolojia na mitaji linawezekana.

Zipo nchi nyingi za Afrika ambazo zilitumia rasilimali zao vibaya mfano, Siera Leoni, Liberia wakawa wanachimba almasi kwa ajili ya kuendesha vita na kununua silaha kutoka nchi zilizoendelea.  Afrika ifike mahali ioneshe ukomavu na kuacha mambo ya kipumbavu kama hayo ioneshe kuwa Afrika ina watu wanaweza kufikiri na kuweza kugawana rasilimali kama alivyofanya Rais Magufuli.

Ukiangalia nchi ya Nigeria asilimia 80 ya mafuta yanayosafirishwa kwenda nje ni asilimia 1 tu ya mafuta hayo ndio yanarudi Nigeria, lakini Tanzana ya Magufuli amesema hapana

Akitoa mfano Dkt Rioba alisema Baba wa Taifa mara baada ya Uhuru wa Tanganyika, wasomi walikuwa wachache sana wasingeweza kutosheleza katika masuala ya utaalam na kuleta maendeleo kupitia rasilimali tulizonazo.  leo hii nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika suala la taaluma na elimu ambapo hatukuwa na Chuo Kikuu hata kimoja. Leo Tanzania ina vyuo vikuu takriban 50, na wataalamu wako wengi, tunachokosa ni Wataalamu wanaoipenda nchi yao wazalendo wenye nia ya kusukuma gurudumu la maendeleo.

Dkt. Rioba anaeleza kuwa ni vizuri kuwa na waaalam vijana  wenye moyo wa kujituma na uzalendo na kuwa tayari kuwa watumishi wa wananchi  na kusaidia kutimiza ndoto ya Tanzania ya viwanda  na ndivyo anavyotaka Rais Magufuli.

Akizungumzia suala la kuondoa dhana ya kuwa na matabaka ya watu katika Taifa,  Rioba amesema kwa sababu Tanzania iko katika mpito, ambapo ilitoka katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea (Azimio la Arusha) na sasa ni kama kutengeneza Azimio la Arusha jipya lakini katika muktadha wa zama za sasa. Kwa wale watanzania ambao ni wazalendo kabisa kabisa, Dkt. Rioba anasema watakubaliana nae kuwa anayoyafanya Rais Magufuli ni lazima aungwe mkono kwa kuwa anaipeleka nchi panapostahili.

Dkt. Rioba katika mahojiano hayo amesema ni wakati sasa kwa kila Mtanzania kuona uchungu kwa kila aina ya wizi wa rasilimali za nchi na kwamba dhambi kubwa ambayo watanzania wanaweza kuifanya ni kudhani kuwa jukumu la kulinda rasilimali za nchi ni la Rais Magufuli pekee.

“Haijawahi tokea kiongozi yeyote barani Afirika kusema wananchi tumeibiwa mno na mbali zaidi, kutafuta suluhisho la kuibiwa huko. Hongera Rais Magufuli jitihada zako ni ukombozi kwa rasilimali zote Barani Afrika na mwisho wa Bara la Afrika kuwa Shamba la Bibi (akimaanisha kila mtu anakuja kujichukulia na kundoka)” Dkt. Rioba alimazilia mahojiano hayo.

Rais Magufuli azungumzia Ndege ya Bombadier Iliyozuiwa Canada

0
0
Rais John Magufuli amemwandikia barua waziri mkuu wa Canada kuulizia kuhusu ndege ya Bombadier, inayoshikiliwa nchini humo na kumtaka ashughulike suala hilo kwa haraka.

Akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege mjini Bukoba leo Jumatatu Novemba 6, Rais Magufuli amesema amemtuma pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenda Canada kushughulikia suala hilo kisheria.

"Nimemwandikia barua waziri wa Canada kuulizia kwanini ndege yetu inakaa zaidi ya miezi sita, tumechoka kusubiri. Nimemtuma pia mwanasheria mkuu ili akapambane nao kisheria," amesema.

Amesisitiza kwamba kama wameamua kupambana kisheria watapambana na amewataka wanasheria wa Tanzania kushikamana ili kuhakikisha kwamba ndege hiyo inakuja Tanzania.

Rais Magufuli amewaonya wananchi pia kuacha kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii. Alisema “ninawaomba watu wa vyama vyote waunge mkono juhudi hizi zinazofanywa na serikali.”

Magufuli ambaye ametimiza miaka miwili tangu achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania amesema ndege zote sita zilizonunuliwa na Serikali zitakuja.

Rais Magufuli Aamuru Watu Watatu Wachunguzwe Kwa Kutaka Kuiibia Serikali Mabilioni

0
0
Rais  Dk. John Magufuli, ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali, kwa tuhuma za kuandika madai yasiyo halali, kwa lengo la kuiibia serikali.

Rais Magufuli ametoa amri hiyo wakati akizindua Uwanja wa Ndege wa Bukoba wenye urefu wa kilomita 1.5 ambapo amewataja watumishi hao kuwa ni Jackson Kaswahili Robert, Mwachano Msingwa na Gidioni Zakayo.

Alifafanua kwamba, Jackson alijaza fomu zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.626 lakini madai hayo yalipochunguzwa, ilibainika kuwa hadai chochote.

Akaongeza kwamba Mwachano yeye alijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.754 wakati ukweli ni kwamba anaidai shilingi milioni 2 tu huku Gidioni Zakayo

Akijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi milioni 104 wakati si kweli.

“Hawa wote pamoja na maofisa wizarani walioidhinisha malipo haya, naagiza vyombo vya dola viwashughulikie. Tumekuwa na watu ambao hawana uchungu na wengine,” alisema Rais Magufuli.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images