Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Zitto Kabwe Aitupia Lawama Serikali Baada ya Acacia Kusema Hawana hizo Dola Milioni 300 za Kuilipa Tanzania

$
0
0
Baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kudai kwamba haina pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa juzi  na kampuni ya Barrick Gold Mining,  Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.

Akifanya mahojiano maalalumu jana mchana, Mh. Kabwe alisema kwamba alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwa Kampuuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (ameiita kishika uchumba) kwani hata 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi waliahidi hivyo.

Mh. Zitto amesema kwamba tangu juzi  alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba "Tumefanikiwa" kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.

"Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo".

Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.

‪Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi Mhashamu Castory Msemwa, kilichotokea  tarehe 19 Oktoba, 2017 nchini Oman.

Mhashamu Askofu Castory Msemwa amefariki dunia Mjini Muscat akiwa safarini kuelekea nchini India kwa Matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Baba Askofu Msemwa, kilichotokea huko Oman, Baba Askofu Msemwa ametoa mchango mkubwa sio tu katika kutimiza majukumu yake ya huduma za kiroho bali pia katika kuisaidia jamii kupata huduma mbalimbali anazostahili binadamu na amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa taasisi nyingine zikiwemo za Serikali katika kudumisha amani, upendo, umoja na kuwahudumia wananchi, mchango wake utakumbukwa daima" Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amemuomba Rais wa TEC Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kumfikishia pole nyingi kwa Maaskofu wote wa TEC, Mapadre, Makatekista na waumini wote wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi kwa msiba huu mkubwa uliotokea na amesema anaungana nao katika kipindi cha majonzi na maombi kwa Marehemu.

"Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie, Marehemu Askofu Castory Msemwa apumzike kwa amani, Amina" Amemalizia Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mufti Sheikh Aboubakar Zubeir kufutia kifo cha Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Je,una Upungufu Wa Nguvu Zakiume,kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa,kufika Kileleni Mapema Na Kushindwa Kurudia ????

$
0
0
Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa na mambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA nk.

Upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa, mahusiano mengi kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,
1 KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA 
2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA 
3 KUWAHI KUFIKA KILELENI 
4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI 
5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO LA NDOA KABISA.

TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.

PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK 

WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO 

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha vidonda vya tumbo,korodani kuvimba,na anatoa dagu za utajiri kwa wanaohitaji bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM,NAUTALETEWA POPOTE ULIPO.

 SIMU; NO 0767145357/0629034550.

Daktari wa Kanumba Atoa Ushahidi Wake Mahakamani Jinsi Alivyofariki

$
0
0
DAKTARI wa familia ya msanii maarufu wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, Dkt, Paplas Kagaia, ameileza mahakama Kuu ya Tanzania kanda Dar es Salaam Kanumba alifariki toka nyumbani baada ya kumpima na kukuta mapigo yake ya moyo hayakuwepo.

Dk, Paplas amedai hayo jana  Oktoba 20, 2017 huu wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Sam Rumanyika.
 
Amedai kuwa, baada ya mdogo wa marehemu kumfuata hospitali kwake na kumwambia kuwa Kanumba amefariki, alichukua kipimo cha sukari na shindikizo la Damu(pressure) na kwenda moja kwa  moja nyumbani kwake Sinza ambako baada ya kufika nyumbani kwake alimpima sukari na kukuta iko kawaida lakini alipompima pressure haikuwepo kabisa.

Daktari Huyo mwenye elimu ya stashada ya juu (Advanced diploma) aliyejipatia Elimu yake chuo cha uuguzi cha jeshi cha Lugalo amedai kuwa, alikuwa daktari wa familia ya Kanumba kwa zaidi ya miaka mitano na anamiliki Hospitali yake binafsi ya St. Anna iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam alikuwa akimtibu Kanumba magonjwa ya kawaida na hakuwahi kugundua tatizo lake lolote.

==>Mahojiano kati ya Dr Paplas na Wakili wa serikali Batlida Mushi yalikuwa kama ifuatavyo;

Wakili: Ulipata wapi taarifa  ya kuugua kwa Kanumba?
Shahidi: Nikiwa naudumia wagonjwa kama kawaida nilipigiwa simu na Seth akiniomba niende kumuona Kanumba amedondoka, nikamwambia muda ule ulikuwa ni usiku sana aende kumchukua.

Wakili: kwani nini Seth akupigie wewe simu?
Shahidi: Nilikiwa daktari wa familia yao kwa miaka kama mitano hadi sita.

Wakili: Baada ya kukupigia simu, ulifanya nini?
Shahidi: Nilichukua vifaa vya mashine ya sukari na BP, niliingia chumbani kwake nikifuatana na Seth nilipofika nilikuta Kanumba amelala chini chali, nikampima sukari ilikuwa normal nikampima pressure mapigo ya moyo hayakuwepo kabisa.
 
Wakili:Baada ya kujua mapigo ya moyo hayapo ulichukua hatua gani?
Shahidi: Nilimwambia Sethi  umvalishe nguo wafanye utaratibu wa kumpeleka hospitali kubwa ya Muhimbili akafanyiwe Vipimo.

Wakili: Baada ya hapo ulifanya nini?
Shahidi: Baada ya kumvalisha nguo kwa kusaidiana na kijana mmoja wa jirani na mama mwenye nyumba tulimpeleka Muhimbili kitengo cha emergency.
Wakili: Mlipofika Muhimbili kitengo cha Emergency ulifanya nini?
Shahidi: Nilimuomba Dk tuliyemkuta pale ampime Kanumba na alipompima alisema kuwa ameshafariki.

Wakili: Wakati huo anapimwa mlikuwa mahali gani?
Shahidi: Alimpima pale pale nje hata ndani hatukuingia, alitushauri tufuate taratibu za polisi, alituambia twende Kituo cha polisi cha Slender Bridge tukachukue PF3.

Wakili: Mlipokuwa Polisi nini kiliendelea?
Shahidi: Tulipewa askari ili watusaidie kupeleka maiti Mochuari kisha tukaambiwa twende Kituo Osterbay Polisi tukatoe Maelezo.

Wakili: Unamfahamu Lulu?
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Unamfahamuje?
Shahidi: Nimemfahamu kwa kupitia Kanumba.

Wakili: Unamfahamu kama nani?
Shahidi: Alikuwa mpenzi wake Marehemu Kanumba.
Wakili: Je Aprili 7 mwaka 2012 baada ya wewe kwenda Polisi Osterbay ulimuona?
Shahidi: Hapana sikumuona.

Wakili: ulimuonea wapi?
Shahidi: Nilimuona usiku kwenye saa 11 alikuwa Sinza sehemu moja inaitwa Bamaga, baada ya yeye kunipigia simu.

==>Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake kwa upande wa mashtaka wakili wa utetezi, Peter Kibatala naye alipata nafasi ya kumuhoji shahidi huyo ambapo mahojiano yao yalikuwa hivi;
 
Wakili Kibatara: Kwa nini ulipofika eneo la tukio ulimpima Sukari?
Shahidi: mtu akianguka ghafla Mara nyingi sukari inaweza kuwa imeshuka
Wakili Kibatala; kabla ya Octoba 7 uliwahi kumfanyia uchunguzi marehemu kuhusu sukari.
Shahidi: Hapana
 
Wakili: Uliwahi kumfanyia vipimo kama anauvimbe kichwani
Shahidi: hapana.
Wakili: je ulimkuta na jeraha lolote?
Shahidi; hapana.
Wakili Kibatara: Ni sahihi kuwa mshtakiwa alikuwa anakupigia simu Mara kwa Mara?
Shahidi: Ni sahihi kweli alikuwa akinipigia hata kabla hajaenda hospitali.

Wakili Kibatara:Ni sahihi kwamba mshtakiwa alikuwa anakupigia simu Mara kwa Mara akifikiria kuwa marehemu alikuwa amezimia tu?
Shahidi; Ndiyo ila alikuwa na hofu kama marehemu amekufa.

Wakili Kibatara: Ni sahihi kuwa mshtakiwa alikuwa anaogopa kuonana na wewe kwa sababu alidhani uko na marehemu na ulikuwa ni mtego tu wa kumkamata ili andeleze tabia yake ya wivu uliopindukia?
Shahidi: hapana.
 
Wakili Kibatala: umesema, mlikutana na mshtakiwa Bamaga, kwa nini mshtakiwa alikubali kuonana na wewe Bamaga?, Ni ushawishi gani ulimwambia hadi akakubali kuja?
 
Shahidi: alikubali tukutane Bamaga alikuwa hajui kwamba Kanumba ameshafariki, yeye ndio alinipigia simu akasema si umesema Kanumba hajafa nikamwambia ndio akasema tukutane Sinza nikasema tukutane Bamaga.

Naye shahidi wa tatu, mrakibu msaidizi wa Polisi PF 16519 ASP Ester Zefania akitoa ushahidi wake huku akiongozwa na wakili wa Serikali,  Ayoub Abood amedai, Oktoba 7, 2012 akiwa kituoni Osterbay alipewa maelekezo na Mkuu wa upelelezi Wa mkoa Wa Kinondoni Camilius wambura kwenda Sinza kwa Kanumba kufuatilia taarifa alizopata za kifo cha Kanumba.

Amedai aliondoka na askari watatu pamoja na msanii Ray ambaye aliwaongoza hadi  Sinza kwa marehemu ambako alikuta watu wengi wengine wakilia kuashiria hali ya msiba 

==>Mahojiani yake na Wakili Abood yalikuwa hivi;

Wakili: Baada ya kufika hapo nyumbani ulifanya nini?
 
Shahidi : Nilijitambulisha wa watu waliokuwepo pale kuwa Mimi ni askari kutoka kituo cha polisi cha Osterbay, nikaitiwa mdogo wake Kanumba Seth, ambapo nilipomuuliza nini kilitokea alinielezea kwa kifupi.
 
Baada ya hapo mimi pamoja na askari 2 pamoja na Ray tuliiingia chumbani kwa marehemu kwa ajali ya uchunguzi.

Wakili : Baada ya kuingia humo chumbani ulikuta hali gani? na  mliweza kuona kitu gani katika chumba hicho?
 
Shahidi:Kitanda kilikuwa kimevurugwa, pembeni yake kulikuwa na stuli juu yake ilikuwa na chupa ya soda aina ya Sprite, glass iliyokuwa na kinywaji nusu na chupa ya whisky ya Jackie Daniel, pia pembeni chini ya tendegu za kitanda kulikuwa na panga na pembeni yake kulionekana michirizi ya mburuzo wenye rangi kama nyeusi isiyokolea.

Wakili: Baada ya hapo nini kilitokea?
Shahidi: Nilimpigia simu kamanda Wambura na kumpatia taarifa ambaye aliniambia angetuma timu ya wapelelezi wa matukio kutoka mkoani na eneo la tukio libaki vilevile.

Wakili: Baada ya kufika wakuu wa upelelezi ulifanya nini?
Shahidi: Nilindoka nikarudi kituoni.

Wakili: Baada ya kufika kituoni ulimkuta nani?
Shahidi; Nilimkuta kamanda Wambura ambaye alinipa (task) jukumu la kumtafuta Lulu apelekwe kituoni hapo kwani kwa taarifa alizokuwa nazo atakuwa anafahamu nini kilimpata Kanumba.

Wakili: Alikupa Huyo Daktari kwa ajili gani?
Shahidi; Alinipa Daktari Paplas ili tusaidiane nae kumpata Lulu kwani ndio alikuwa akiongea naye  Mara nyingi ambapo alimpigia simu na kukubaliana kukutana nae bamaga ndipo waliweza kumkamata.
 
==>Wakili Kibatala nae alimhoji mrakibu msaidizi wa Polisi PF 16519 ASP Ester Zefania mahojiano yao yalikuwa hivi;

Wakili Kibatala: Mlipomkamata Lulu mlimpeleka hospitali?
Shahidi; Ndio 

Wakili Kibatala: Mlimpeleka Lulu hospitali kutibiwa nini?
Shahidi: sifahamu, sikuingia kwenye chumba cha daktari.

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba sababu ya kupelekwa Lulu kwa daktari kuwa alipigwa na ubapa wa panga mapajani na alikuwa na maumivu

Shahidi; Sifahamu.

Kesi hiyo itaendelea Oktoba 23, 2017( Jumatatu) na shahidi wa nne atatoa ushahidi wake.

Serikali Yamwaga Ajira 400 TRA

$
0
0
Benny Mwaipaja, Shinyanga
Serikali inatarajia kuajiri wafanyakazi 400 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi kifupi kijacho ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watumishi katika Mamlaka hayo, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na makusanyo ya kodi.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Shinyanga na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji wa Mamlaka hayo mkoani humo.

Dkt. Kijaji amesema kuwa taratibu zote zimekamilika na wakati wowote nafasi za ajira zitatangazwa na kwamba nafasi hizo zimelenga kuiwezesha TRA kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi.

“Tunatambua changamoto ya uchache wa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ndio maana tumeamua kuajiri wafanyakazi hao 400 ambao ni wengi kuliko kada nyingine ili tuweze kuimarisha utendajikazi wa Mamlaka na hivyo kuongeza makusanyo ya kodi zinazotakiwa kwa shughuli za maendeleo nchini” alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa pamoja na uhaba wa watumishi, anaamini kuwa lengo la mwaka huu la kukusanya shilingi trilioni 17 ambazo Mamlaka hayo imepangiwa yatafikiwa na ikiwezekana kuzidi kwa kutumia wafanyakazi waliopo.

Dkt. Kijaji alitoa rai kwa wafanyakazi wa TRA kuwa waadilifu na kwamba atakayebainika kukiuka maadili yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria.

Awali Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Shinyanga Bw. Jumbe Samson, alieleza kuwa mkoa wake umepangiwa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 18 na kwamba wanauhakika wa kufikia lengo hilo kutokana na mikakati mbalimbali waliyojipangia ikiwemo kusimamia ukusanyaji kodi kikamilifu katika sekta ya madini.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Bw. Beatus Nchota alisema kuwa Mamlaka yake imejiwekea mipango ya kufungua ofisi zake kila wilaya hapa nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili lengo walilopewa la kukusanya shilingi trilioni 17 liweze kufikiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Josephine Matiro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, alisema kuwa Serikali mkoani humo itahakikisha kuwa TRA inatimiza malengo yake ya kukusanya kodi na kumhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwamba watasimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Shahidi Aieleza Mahakama Jinsi Scorpion Alivyomtoboa Mtu Macho

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Ilala Oktoba 31,2017 itatoa uamuzi iwapo mshtakiwa Salum Njwete maarufu Scorpion ana kesi ya kujibu au la.

Uamuzi utatolewa baada ya jana  Ijumaa Oktoba 20,2017 upande wa Jamhuri kufunga ushahidi katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho, Said Mrisho inayomkabili Njwete (34).

Katika hati ya mashtaka, Njwete anayewakilishwa na wakili Juma Nassoro anadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 6,2016 saa nne usiku eneo la Buguruni wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka, Salum Masoud mkazi wa Buguruni ambaye ni mfanyabiashara wa kuuza chenji katika kituo cha daladala amedai siku ya tukio alikuwa katika biashara zake.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule alidai akiwa katika shughuli zake alishuhudia mabishano kati ya mshtakiwa na mteja aliyekuwa akinunua bidhaa eneo hilo.

Amedai alimuona mshtakiwa akigonga meza akimlazimisha mteja huyo kumfuata.

Shahidi huyo alidai mteja huyo alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu hivyo alikataa kwenda.

Masoud alidai alimuona mshtakiwa akimfuata mteja huyo, kumvuta, kumwangusha chini na kuanza kumpiga maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Amedai alimwona mshtakiwa akichomoa kisu na kumtoboa mteja huyo na alisikia sauti ya kilio chake cha kuomba msaada, huku akitokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Shahidi huyo alidai mshtakiwa alichukua mkufu aliokuwa amevaa mteja huyo shingoni na uliokuwa mkononi. Pia, alidai alichukua pochi iliyokuwa mfukoni na alimsukuma kwenye Barabara ya Mandela ambako alianguka.

Baada ya mshtakiwa kuondoka, Masoud anadai walimnyanyua mteja huyo na kumweka eneo la wazi linalotenganisha barabara.

Amedai mtu aliyekuwa eneo hilo alitoa taarifa polisi ambao walifika eneo hilo na kuwatawanya kabla ya kumchukua majeruhi na kumpeleka hospitali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Octoba 21


Kwa Nini Wanaume Wengi Wana Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Asilimia 85 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vema wake au wapenzi wao na kuwasababishia waweze kuwasaliti na kutoka nnje ya ndoa 

NI NINI CHAZO CHAKE ; upiga punyeto, ngiri, vidonda vya tumbo, magonjwa ya moyo, presha, kisukari, korodani moja kuvimba, utumiaji hovyo madawa ya kizungu, msongo wa mawazo, kufanyiwa tohara ukubwani nk 

DOKTA HAMISI SASA KAPATA TIBA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO :

MAPRO POWER  ndio dawa tosha kwa sasa. Hutibu na kuponesha kabisa tatizo la NGUVU za kiume, utarudisha heshima ya ndoa yako 

1 itakufanya uchelewe kufika kileleni 
2 itakupa hamu ya kurudia tendo 
3 Huhimalisha moduli iliyoregea na kusinyaa

 OKOA NDOA YAKO SASA : MANGUNGU MIX ni tiba kwa wanaume wenye uume mfupi kwa msemo wa Dada zetu wanaita vibamia. Dawa hiyo huboresha uume saizi upendayo ich 1-8 na unene cm 1-5.

Dawa zipo za kupaka na kunywa na ni tofauti na ulizowai kutumia na hazina madhara.

Pia tunato Pete, mkufu au saa kwa mfanya biashara,mkulima mchimba madini 

Pete ya mapenzi nayo IPO NATOA GARANTII YA MIEZI SITA kama umepata tiba na ukafanikiwa na tatizo kujirudi utakuja kupewa bure tiba yako OFISI IPO MBAGALA ZAKHEMU UKISHUKA TU SITENDI . Pia utaipata popote huduma kama hauna nafasi ya kuja ofisini 

Mawasiliano; 0686980006

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605   au  0767358654

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Serikali yasimamisha shughuli za Shirika la CHESA kwa tuhuma za kuchochea vitendo vya ndoa za jinsia moja.

Mwalimu Ajiua Kwa Kujichinja Koromeo

$
0
0

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
 
Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja nyumbani kwake muda wa  saa sita mchana leo Jumamosi.
 
Amesema kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa  5 asubuhi alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe  na baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake.
 
Amesema kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake  mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.

Amesema baada ya kumdodosa mdogo wa marehemu huyo alidai kuwa kaka yake  siku za nyuma alikua na mgogoro na mkewe lakini ulikwisha ila anahisi kitendo cha mkewe kuondoka nyumbani na kwenda mjini Namanyere huenda jambo hilo lilimkasirisha na kuchukua hatua hiyo ya kujichinja.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana lakini polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kilichomsibu mwalimu huyo kiasi cha kuchukua maamuzi ya kujiua kikatili namna hiyo.

Zitto Kabwe: ACT- Wazalendo Sio Kijiwe cha Kuisifia Serikali

$
0
0
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama chake siyo jukwaa sahihi la kuisifia Serikali kama wanachama wengine wanavyodhani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Zitto amesema wanachama wanaodhani kama chama hicho ni jukwaa la kuisifia Serikali wajitathimini au kuchukua hatua kama wenzao walivyofanya.

Zitto amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba na wenzake kumi kuhamia CCM.

“Tulimwita Mwigamba katika kikao cha chama aje kutueleza kama tunakikuka misingi ya chama lakini hakufika. Chama kinaheshimu mchango wa kila Mwana-ACT, lakini tunawashauri wanaondoka wasiwashawishi wanachama wengine kuondoka,”

“Chama kimejiridhisha kwamba bado tunaendelea kusimamia misingi ikiwamo uzalendo sanjari na kupigania haki za demokrasia,”amesema Zitto

Amesema wanafanya yote hayo wakiongozwa na utu na uadilifu.

“Chama chetu kina ahadi tano ambazo ni kupambana na rushwa na ufisadi na kamati ya uongozi imebaini kama haijatoka katika misingi yake kama wengine wanaoondoka wanavyodai,”amesema Zitto.

Amesema bado wanaendelea kupambana na umasikini na hali ya maisha kwa Watanzania wote.

“Hatujawahi hata siku moja kwenda kinyume  na misingi ya chama hiki kama watu wanavyodai.”

Uteuzi wa Mugabe kuwa balozi wa ‘WHO’ waibua maswali

$
0
0
Shirika la afya duniani (WHO) limemteua rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kuwa balozi wa kuunganisha vita ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza barani Afrika.

Kuteuliwa kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 kumewashangaza wanachama wengi wa shirika hilo pamoja na wafadhili hasa kutokana na hali ya sekta ya afya nchini Zimbabwe.

Wanachama wengi na wafadhili wa shirika la afya duniani wamedai kuwa chini ya uongozi wa rais Mugabe sekta ya afya nchini Zimbabwe imezorota huku wafanya kazi wakiwa hawalipwi ipasavyo na dawa pia hazitoshi jambo ambalo linaonyesha kuwa Mugabe hakustahili kupewa wadhfa huo.

Upande wa upinzani chini Zimbabwe umeuita uteuzi huo kuwa vichekesho na matusi kwani kiongozi huyo ameshindwa kuhimarisha sekta ya afya nchini kwake wakati yeye na familia yake wakitibiwa nje ya nchi.

Hata hivyo kiongozi mpya wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus kutoka Ethiopia ambaye ni mwafrika wa kwanza kuongoza shirika hilo alipongeza juhudi za Zimbabwe kwa kujitoa kuboresha afya za wananchi.

Mganga wa Jadi Atiwa Mbaroni kwa Kubaka watoto 14

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji mkazi wa mtaa wa Minga, Daud Idd (74), kwa tuhuma ya kunajisi watoto 14 wenye umri kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri.

Mgonga huyo maarufu kama Babu Karatu ameelezwa kuwa alikuwa akishirikiana kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake aitwaye Abdallah Yahaya (31).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumamosi, kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Isaya Mbughi amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.

Amesema kuwa mwathirika mmoja mwenye umri wa miaka saba siku ya Oktoba 16 mwaka huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake alilalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri.

Amesema baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake mama huyo aliweza kumchunguza kwenye sehemu zake za siri na kubaini kuwa michubuko inayotokana na kuingiliwa kimwili.

“Mama huyo baada ya kuona michubuko hiyo kwenye sehemu za siri za binti yake alimhoji mtoto wake na mtoto huyo aliweza kumtaja mganga wa kienyeji Karatu. Mwaathirika huyo alienda mbele zaidi na kumweleza mama yake kuwa si yeye pekee hufanyiwa vitendo hivyo, bali wapo watoto wengi wamefanyiwa.”

Kaimu kamanda huyo amesema baada ya hapo mama huyo alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Minga na kisha yeye na mwenyekiti wa mtaa waliweza kuongozana hadi kituo cha kati cha polisi mjini hapa.

“Jeshi la polisi liliweza kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaishi katika nyumba moja, kwa tuhuma ya ubakaji. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto waliofanyiwa unyama huo wanasoma katika Shule za Msingi Singidani, Nyerere na Mughanga,” amesema.

Mbughi amesema mbinu iliyokuwa inatumika kuwanasa watoto hao wa ni kuwarubuni na kisha kuwaonyesha video/movie, kwenye kompyuta mpakato.

“Wakati watoto hao wa kike wakiendelea kuangalia video sebuleni, mtuhumiwa huyo alikuwa akichomoa mmoja na kuingia naye chumbani na kumwingilia kimwili. Wachache alikuwa akiwachezea sehemu zao za siri. Baada kuingiliwa kimwili watoto hao walikuwa wakipewa zawadi ya shilingi mia mbili au shilingi 2,000,” amesema.

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

$
0
0
        NATURAL BEAUTY PROD.
NDIYO KAMPUNI PEKEE INAYOTOA BIDHAA ORIGINAL GARANTII PAMOJA NA SISITI. 
Sasa ni wakati wako mpendwa wa kupendeza na bidhaa hizi bila kemiko wala madhara kwa mtumiaji yoyote.

Pata bidhaa hizi upate matokeo mazuri kwa haraka na uhakika zaidi. Bidhaa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda.

      Zimethibitishwa kiafya
🍉🌿🍅🍍🍒🍉🍓🍅🍒
            🍋🍇🥝🥒
          BIDHAA ZETU:-
   
1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @150,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @170,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta  @150,000/=
(11)Vidonge @170,000/=

4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka @150,000/=
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @150,000/=

(C) VIG RX- Ni dawa mpya ya kuongeza maumbile hadi nchi 7.5 inapatikana kwa @200,000/=
(C)Handsome up original ni kifaa kinachoongeza maumbile kwa %99 size uipendayo  @250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=

7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @150,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=
(b)Mkanda wa kawaida @150,000/=
(c)Micro-computer belt wa umeme @200,000/=
9.Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @150,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @150,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @150,000/=
12.Kurudisha usichana  (bikra) @150,000/=
        

        Wasiliana nasi :- (+255)
             0759029968 au.       
                0659618585
  TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
     Follow us on instagram  @natural2162
@natural2162
@natural2162
 
                      [Welcome all]

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapilili ya Octoba 22

Rais Magufuli amteua Janeth Masaburi kuwa Mbunge

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bi. Janeth Masaburi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka ya kuteua wabunge 10 watakaokuwa miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bi. Janeth Masaburi ataapishwa kulingana na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Polisi na Wanajeshi 53 Wauawa Misri

$
0
0
Idadi ya wanajeshi na polisi waliouawa katika mapambano na wapiganaji wa Kiislamu katika eneo la Bahariya magharibi mwa jangwa imefikia 53, maofisa usalama na matabibu wamesema.

Wizara ya mambo ya ndani imesema vikosi vya usalama vilikuwa vinawasaka wapiganaji wa Kiislamu lakini waliviziwa katika chemchem ya maji ya Bahariya umbali wa kilomita 200 kusini mashariki mwa Cairo na kushambuliwa. Pia, imesema wapiganaji wa Kiislamu 15 wameuawa katika makabiliano hayo.

Vyanzo vilivyo karibu na maofisa usalama vinasema msafara huo ulishambuliwa kwa roketi na wapiganaji hao pia walitumia vilipuzi. Duru za usalama zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na ofisa wa jeshi aliyetoa amri ya kuvamia alishindwa kuagiza wanajeshi kuimarisha kikosi chake.

Hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika ingawa kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa juu ya wapiganaji wa kikundi kinachofahamika kama Hasm, kilichowahi kushambulia majeshi ya usalamasiku za nyuma. Hata hivyo, Twitter ya kikundi hicho inayotumiwa mara kwa mara kutoa taarifa haijafanya kazi tangu Oktoba 2.

Tangu jeshi lilipomwondoa madarakani Rais Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood, makundi ya kigaidi yameongeza sana mashambulizi yao dhidi ya wanajeshi na polisi.

Brotherhood, waliowahi kuwa kundi kubwa la upinzani nchini wamekanusha kuhusu katika machafuko.

Mohamed Morsi alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012, lakini jeshi lilimpindua mwaka mmoja baadaye baada ya kuibuka maandamano ya kupinga sheria ya Kiislamu zinaosababisha mgawanyiko.

Nape Awataka Watanzania Waache Ushamba

$
0
0
Mbunge wa Mtama, kwa tiketi ya (CCM) Nape Moses Nnauye amefunguka na kuwataka watu kuacha ushamba kwani kusifu au kukosoa juu ya jambo fulani ni kazi ambazo Mungu amewapa watu kuzifanya hivyo mtu baki hupaswi kukerwa na kuhangaika na hayo.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema mtu ambaye anachukizwa na watu ambao wana sifu juu ya jambo fulani au kukosoa basi huyo mtu ni mshamba.

"Mungu kagawanya kazi, wengine kusifu, wengine kukosoa, wengine yote pamoja! Kwanini unakerwa na kuhangaika na mgawanyo wa kazi? !Acha ushamba" alisistiza Nape Nnauye

Aidha kiongozi huyo amezidi kusisitiza kuwa watu wanapaswa kutimiza wajibu wao na kuacha kuhangaika na watu ambao wanasifia juu ya mambo au kukosoa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images