Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yalifungia Gazeti la Mwanahalisi miaka miwili

0
0
Serikali imelifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili. Imesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abassi ametangaza uamuzi huo leo Jumanne mbele ya waandishi wa habari.

Dk Abassi amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017.

Amesema kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.

Amezitaja baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo ni ile iliyotolewa Januari 5 iliyobebwa na kichwa cha habari "Ufisadi ndani ya Ofisi ya JPM".

Dk Abassi amesema, "Habari hii ilisheheni nia ovu dhidi ya Rais wakati suala husika lilihusu Shirika la Elimu Kibaha, wahariri walikiri udhaifu wakaomba radhi na kupewa onyo kali."

Amesema Gazeti la Mwanahalisi toleo la  jana lilichapisha makala yenye matusi, dhihaka na maneno yasiyofaa dhidi ya Rais John Magufuli.

"Tulipowaita wakajitetea kwa kutumia neno mubashara yaani walichukua maneno yanayotolewa mitandaoni. Serikali imeona utetezi huo ni dhaifu kwa kuwa habari lazima izingatie maadili," amesema.

==>Taarifa kamili ipo hapo chini

Majaji wapewa angalizo Kuhusu Matumizi ya mitandao ya kijamii

0
0
Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, ametoa angalizo kwa Majaji wafawidhi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika mahusiano pamoja na kutoa michango kwenye mitandao hiyo juu ya jumbe zisizofaa.

Jaji Mkuu ametoa  angalizo hilo wakati akifunga mkutano wa Majaji wafawidhi wa kanda nchini, uliofanyika Jijini Arusha

"Katika suala la matumizi ya mitandao, kuweni makini. Msi- like picha ambazo hazina maadili au kuchangia kwa kutoa maoni katika mitandao ya kijamii," alisema.

Aidha, amewataka kuwa makini na ndugu au jamaa wanaowatembelea, akisema baadhi yao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali ya kijinai.

Aliwataka majaji hao kujenga tabia ya kupenda kujisomea na kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge kwa kurekebisha sheria ili kuweza kugundua makosa mbalimbali yanayofanywa na Mahakama za chini na wafundishane namna ya kuboresha hukumu zinazotolewa ili kupunguza mrundikano wa mashauri.

"Ni vizuri kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge wakati wa kurekebisha sheria, kazi na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kufungua mashauri," alisema.

Kuhusu migongano kati yao na vyombo vingine vya serikali, aliwataka kutambua mipaka ya vyombo hivyo na wao watambue mipaka yao huku akisisitiza kwamba kila chombo kikitambua mipaka yake wataheshimiana na hakutakuwa na mgongano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkutano huo wa majaji wafawidhi ulikuwa mahususi kutathmini na kuweka mikakati ya kumaliza mrundikano wa mashauri 2,198 yaliyopo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, kati yao mengine yamekaa zaidi ya miaka 10.

Zari Amruka Diamond Sakata la Kuzaa na Hamisa Mobeto..... ataka asimchezee

0
0
Sakata la Diamond na mwanamitindo Hamisa Mobetto limechukua sura mpya baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe.

Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo tena.

Wakati Diamond akiendelea na mahojiano katika kituo cha Clouds FM, Zari aliandika katika mtandao huo akisema: “Hahahaha unajidanganya, unasema uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno yako.”

 Aliendelea kuandika: “Inawezekana mimi ni mama wa watoto wako ndio maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda ugoogle kuhusu ‘defamation of character law suit’, usinijaribu.”

Diamond alipoulizwa kuhusu kauli hizo amesema anamwelewa kwa kuwa kuna baadhi ya mambo hakumweleza na kwa mara ya kwanza huenda ameyasikia wakati huo.

Joseph Musukuma na Madiwani Geita Wafikishwa Mahakamani

0
0
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, madiwani na baadhi ya wananchi leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita 

Kwa nyakati tofauti kuanzia Septemba 14 hadi 17 walikamatwa na polisi wakituhumiwa kuhusika kufunga barabara za kuingia kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).

Septemba 14 madiwani wa halmashauri mbili za Wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia GGM wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za Marekani zinazotokana na ushuru wa huduma.

Ongeza Hips, Makalio Na Mapaja, Kuwa Mweupe Na Softi...... Ongeza Maumbile Ya Kiume, Nguvu Na Hamu Ya Tendo

0
0
Natural beauty product Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya. 
 
             NB. Matokeo ni uhakika na garantii na risiti
🍉🌿🍅🍍🍒🍉🍓🍅🍒
          BIDHAA ZETU:-
  
1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @170,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta  @130,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka (Inaongeza inch 6-7) @150,000/=
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
(C)HANDSOME UP ORIGINAL- kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo @250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @130,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @130,000/=
(b)Mkanda wa kawaida @120,000/=
(c)Micro-computer belt wa umeme @200,000/=
9.Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @130,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kurudisha usichana  (bikra) @120,000/=
        Wasiliana nasi :- (+255)
             0759029968 au.       
                0659618585
 
  TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
     Follow us on instagram  @natural2162
@natural2162
            
                              [ WELCOME ALL]

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 20

Marekani: Tutaisambaratisha Korea Kaskazini tukilazimishwa

0
0
Rais wa Marekani, Donald Trump amezionya nchi za Korea ya Kaskazini na Iran kufuatia vitisho vinavyotolewa na nchi hizo vya kufanya majaribio mbalimbali ya silaha za nyuklia, huku akisema kuwa atazigeuza mavumbi kama ikibidi.

Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa katika mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa unaoendelea Jijini New York, ambapo amesema kuwa silaha za nyuklia ni tishio kwa usalama wa dunia.

Aidha, Katika hotuba yake hiyo ya kwanza katika mkutano wa Baraza la Umoja huo unaofanyika Jijini New York, Trump ameonya kuwa Marekani itaiangamiza Korea kaskazini iwapo italazimika kujitetea ama kuwalinda washirika wake.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Trump amesema kuwa Iran ni nchi ya kifisadi inayoongozwa kidikteta, hivyo ameitaka kuacha mara moja kusaidia makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakihatarisha amani ya mashariki ya kati.

Jaji Mkuu Kenya azungumzia vitisho vinavyomkabili kwa kufuta uchaguzi

0
0
Jaji Mkuu wa Kenya, David Maranga amesema tangu kutolewa kwa uamuzi wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, mhimili huo umekuwa ukitishiwa.

Kupitia tamko lake kwa umma, Jaji Maranga ameeleza kuwa kumekuwa na vitendo vya kuitishia mahakama kwa kufanya maandamano yanayoambatana na vitendo viovu.

“Maandamano yamejikita katika vitendo viovu na vurugu, vinaonesha wazi kuwa vinalenga kuitishia Mahakama,” alieleza.

Tamko hilo limekuja kufuatia maandamano makubwa yanayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini humo kupinga uamuzi huo wa Mahakama uliobatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta uliokuwa umetangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya IEBC.

Katika uamuzi wake, Mahakama ilieleza kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi na kwamba haukuwa wa haki.

Kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama uliozingatia Katiba ya nchi hiyo, uchaguzi wa marudio unapaswa kufanywa Oktoba 17 mwaka huu ukisimamiwa na IEBC.

Hata hivyo, upande wa NASA ukiongozwa na Raila Odinga, ambao umeshinda kesi hiyo umeendelea kupinga IEBC kuandaa tena uchaguzi huo wakidai ni wahalifu ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na sio kupewa kazi nyingine.

Kikwete asikitishwa na uzushi unaozagaa mitandaoni

0
0
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na taarifa za uzushi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za kumhusu yeye akionekana kujibu moja ya kauli ya Rais wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli kitu ambacho si kweli.

Kikwete ametumia mtandao wake wa twitter kuonyesha masikitiko yake hayo kwa watu wanaofanya jambo hilo huku akionyesha kusikitishwa zaidi na mapokeo ya watu ambao wengi wao wameamini hiyo kauli wakidhani huenda ni kweli imetoka kwake kitu ambacho si cha kweli

“Nasikitishwa sana na uvumi huu unaosambazwa juu yangu. Inasikitisha sana. Inasikitisha zaidi kuwa wako watu timamu wanaoamini uzushi huu,”ameandika rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye ukurasa wake wa twitter

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo mstaafu kuzushiwa uzushi na watu kupitia katika mitandao ya kijamii ambapo mara kwa mara amekuwa akiwasihi wanaofanya hivyo kuacha mara moja

Faida Nyingine Za Mti Mvunge Mbali Na Kurefusha, Kunenepesha Uume Na Kuongeza Ukubwa Wa Makalio.

0
0
 Watu  wengi  wanaufahamu  mti  wa  mvunge  kama  mti unaotumika  katika  tiba  ya  kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  ya  kiume  pamoja  na kuongeza  ukubwa  wa  makalio  kwa  wanawake.

Hii  ni  kwa  sababu, mti  wa  mvunge  umekuwa  ukitumika  katika  tiba  ya  kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  ya  kiume  pamoja  na  kuongeza  ukubwa  wa  makalio  tangu  enzi   za  mabibi  na  mababu.
 
Vile  vile, mti wa  mvunge  tayari umethibitishwa  kitaalamu  kuwa  na  uwezo  wa  kitabibu  katika  kurefusha  na  kunenepesha   maumbile  ya  kiume  pamoja  na  kuongeza  ukubwa  wa  makalio.
 
Taarifa  ya  kuthibitishwa  kwa  mti  wa mvunge, imeripotiwa  katika  gazeti  la  Mwananchi  la  tarehe  26, Januari  2013.
 

Hata  hivyo, mbali  na  kuwa na  uwezo wa  kurefusha  na  kunenepesha maumbile  ya  kiume  pamoja na kunenepesha makalio, mmea  wa  Mvunge unazo faida  nyingine  lukuki  kwa afya  ya  mwanadamu.
 
Baadhi  ya  faida hizo  ni kama  ifuatavyo ;

FAIDA   NYINGINEZO   ZA   KITABIBU ZA   MTI  WA  MVUNGE

1.    Mti  wa  mvunge  una  uwezo wa  kutibu majeraha ya vidonda
2.   Mti wa  mvunge  hutibu  vidonda  visivyo pona ‘ Vidonda  Ndugu ‘
3.   Mti  wa  mvunge  hutumika  kutibu  vidonda  vya  tumbo
4.   Majani  ya  mti  wa  mvunge  hutumika  kutibu  magonjwa mbalimbali ya  zinaa  kama  vile  kaswende  na  kisonono.
5.   Unga  wa  tunda  la  mvunge hutumika  katika  tiba  dhidi ya magonjwa  mbalimbali  ya  ngozi.
6.   Unga wa  tunda  la  mvunge  hutumika  kutibu chunusi za  usoni  na  mwilini
7.   Mti wa  mvunge  hutumika katika  kutibu bacteria  na  maambukizi  ya  bacteria
8.   Mti  wa  mvunge  hutumika kuongeza  ukubwa wa  matiti na kuyasimamisha
9.   Mti  wa  mvunge  unatumika  kutibu  ukurutu
10.   Mti  wa  mvunge  ni  tiba  nzuri  sana  dhidi ya majipu au  upele  wenye  kutoa  usaha.
11.  Mti  wa  mvunge  unatumika  kutibu maumivu ya  chini  ya  mgongo
12.   Mti  wa  mvunge  hutibu  maradhi  ya  maumivu  kwenye  magoti
13.  Mti wa  mvunge  ni  tiba  nzuri  sana  ya  tatizo la  baridi yabisi.
14.  Mti  wa mvunge  unasaidia  kutibu  maumivu ya  tumbo
15.  Mti  wa  mvunge  husaidia kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo la maumivu  ya  kwenye  meno.
16.  Mti  wa  mvunge  hutumika  katika  tiba  dhidi ya  Homa  ya  mapafu
17.  Mti  wa  mvunge  husaidia  kutibu  tatizo  la  kukosa  choo
18.  Mti  wa  mvunge  husaidia kuupa  mwili  nguvu na  joto
19.  Mti  wa  Mvunge  hutumika  kutibu  bawaziri
20.  Mti  wa  Mvunge  hutumika  kuondosha  minyoo  wa  tumboni
21.  Mvunge  unapochemshwa  kitaalamu  kwa  pamoja  na  asali  mbichi  ya  nyuki wadogo, husaidia  sana  kuondoa  lehemu( Cholestrol ) isiyo  hitajika  mwilini.
22.  Mti  wa  Mvunge  husaidia  kuongeza  maziwa  kwa  mama  anaye nyonyesha

Tunachukua   fursa hii kuonya kuwa wasomaji wasijiamini sana katika kutengeneza dawa na kuzitumia mara baada ya kusoma makala haya. 

Unashauriwa upate ushauri wa kutosha kutoka  kwetu  au kwa  wataalam waliobobea katika tiba asili
zinazohusu mti  huu  wa  mvunge.

Na  kwa  mahitaji  ya  bidhaa  mbalimbali  zitokanazo  na  mti   wa  Mvunge  kwa  ajili  ya  matumizi  mbalimbali  ya  kitabibu, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  Salaam, tunawatumia bidhaa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabus  mbalimbali.

WASILIANA NASI KWA  SIMU  NAMBA  0766  53 83 84.

Na  kwa taarifa  zaidi kuhusu huduma zetu, tutembelee kupitia :

Rais Magufuli ziarani Arusha Leo

0
0
Rais  John Magufuli leo Jumatano  anatarajiwa kutua Arusha kwa ziara maalumu ambapo mapema asubuhi atafungua barabara ya Kami  kutoka  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi Mererani wilayani Simanjiro.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kupokewa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro saa mbili asubuhi.

Gambo amesema  baada ya kupokelewa atakwenda Mererani Mkoa wa Manyara kuzindua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu  wa kilomita 26.

Amesema baada ya uzinduzi huo atazungumza na wananchi na baadaye kurejea Arusha. Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kutoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi.

"Napenda kutumia fursa kuwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Septemba 23 kuanzia saa 12:30 asubuhi,"amesema.

Polisi Dar yakamata ‘Wasiojulikana’ watano

0
0
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza kuwakamata watu watano ambao wamekiri kufanya uhalifu na kuvunja katika ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys iliyopo katika jengo la Prime house, Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi limeweza kuwakamata watu hao ambao mwanzo baadhi ya wananchi walikuwa wakisema watu wasiojulikana ambao walifanya uhalifu huo na kudai wamekiri kuhusika na uvunjaji wa ofisi hiyo na kuiba.

"Kutokana na msako mkali jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kuhusiana na kesi ya uvunjaji wa ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys mnamo Septemba 12, 2017 jeshi la polisi lilipokea taarifa ya kuvunjwa kwa ofisi ya mawakili hao ambapo wahalifu hao walifanikiwa kuvunja na kuiba kasiki iliyokuwa na pesa milioni tatu laki saba, waliiba kompyuta mpakato mbili pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi hiyo na wateja" alisema Lazaro Mambosasa

Aidha Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kuwa kutokana na msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi uliweza kuwakamata watu watano ambao waliwataja kuwa ni pamoja na "Said Idrisa Salehe (47), Mustapha Ibrahim Said (35), Somvi M Somvi (52), Imani Bago Mhina (36) na mshtakiwa na watano ni Husein Hajib Suleman (45) baada ya mahojiano na watuhumiwa hao wote wamekiri kuhusika na tukio hilo na kuonyesha Kasiki la fedha pamoja na mitungi mitatu ya gas iliyotumika kuvunja ofisi hiyo" alisema Mambosasa

Aidha Mambosasa amewataka Watanzania pamoja na viongozi mbalimbali kuwa wavumilivu pundu tukio linapotokea na kutoa nafasi kwa jeshi la polisi kuweza kufanya uchunguzi na upelelezi wake wa kina kuwapata wahalifu wanaokuwa wamehusika kwenye matukio hayo.

"Kwa hiyo masihara mengine yanayofanywa na Watanzania yanalenga kupotosha ukweli lakini pia wanajaribu kuingilia upelelezi wa polisi ili ukweli usijulikane sote sasa tunashuhuda tulianza kwa kutowafahamu mashuhuda lakini upelelezi wa kina umefanyika na tumewapata kwa majina na wao wenyewe wamekiri kufanya matukio hayo, sasa nimualike aliyekuwa akipotisha Watanzania kwa nguvu kuwa aliyetenda kosa hilo hajulikani aje sasa atueleze kuwa na yeye ni miongoni mwa waliotenda makosa hayo kwa sababu tayari hawa wapo na wamekiri kufanya makosa hayo" alisisitiza Mambosasa 

==>Msikilize hapo chini

PICHA: Rais Magufuli Alivyo Agana na RC Wa Dar Paul Makonda na Kuelekea Arusha

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya Kikazi. PICHA NA IKULU

Waziri Mkuu atua mkoani Pwani, aacha maagizo mawili Tanzania ya viwanda

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutembelea Mkoa wa Pwani kisha akatoa maagizo mawili kwa uongozi na wananchi kuhusiana na mpango wa Serikali wa kujenga Tanzania ya viwanda.

Katika agizo la kwanza, Majaliwa amewataka viongozi kuboresha miundombinu ya maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ili waweze kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani.

Alisema kuwa ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa viwanda mkoani humo na kuagiza wahakikishe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yanakuwa na maji, umeme na barabara.

Kisha, Waziri Mkuu aliwageukia wananchi waliopata ajira katika viwanda viwili alivyovitembelea akiwataka wawe mabalozi wazuri wa Taifa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kuwathibitishia wawekezaji kwamba wana uwezo mkubwa wa kazi na hakuna haja ya kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Keds kilichopo Kibaha na kile cha vigae cha Twyford kilichopo Chalinze.

Alisema mbali na viwanda hivyo kutoa ajira nyingi kwa Watanzania, pia vitakapoanza uzalishaji vitawawezesha wananchi kupata bidhaa mbalimbali kama vigae kwa bei nafuu kwa kuwa vitakuwa vinazalishwa nchini.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda hivyo, Jack Feng alisema ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 90 na sasa wako katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na ufungaji mitambo na vinatarajiwa kuanza uzalishaji Oktoba.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alimuomba waziri mkuu asaidie upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.

Bulembo Abadili Msimamo.....Agoma Kugombea CCM

0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Alhaji Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa madai kuwa anaamini kati ya wagombea 48 waliojitokeza wanatosha.

Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi CCM amesema hatogombea tena nafasi hiyo na amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo na kueleza kuwa awali alichukua fomu kutokana na shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa jumuiya hiyo.

"Leo nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa Katibu Mkuu wa chama ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo

Bulembo amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Novemba 20 hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni mapema huyo atakuwa ameshajiondoa mwenyewe. 

Kuhusu hoja ya kuchukua fomu amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za chama zinaruhusu na upo uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.

"Kumekuwa na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea nafasi nyingine,  hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010, 2012 na 2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea lakini kamati kuu ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa lakini kwa upande wangu sitagombea" amesema.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lapinga serikali kulifungia gazeti la MwanaHalisi

Waziri Mkuu Ataka Ulinzi Uimarishwe Kwenye Maeneo ya Viwanda na Uwekezaji Dhidi ya " Watu Wasiojulikana "

0
0
WAZIRI mkuu,Kassim Majaliwa amezitaka serikali za vijiji na ngazi nyingine mkoani Pwani,kujikita kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kulinda mali na usalama wa wawekezaji na watanzania kijumla.

Amesema haijajulikana hadi sasa nia na dhamira ya watu wasiojulikana wanaojihusisha kupoteza maisha ya watu ,na ni hatari endapo watajiingiza katika maeneo ya uwekezaji kwani hakuna mwenye uhakika wa azma yao.

Aidha Majaliwa ,ametoa wiki mbili kwa waziri wa maji kutathmini matokeo ya mwenendo wa mradi wa maji wa WAMI ,ili kutoa utaratibu na kama sheria inaruhusu kuvunja mkataba ikiwa mkandarasi ameshafikia kiwango cha asimilia 50 ya utekelezaji.

Waziri huyo ,pia ameziagiza halmashauri nchini kuona umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya kununua magari ya zimamoto yatakayosaidia kudhibiti majanga ya moto yanapotokea hususan kwenye maeneo ya uzalishaji na viwanda.

Katika hatua nyingine amelitaka shirika la umeme Tanesco,Dawasco kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya umeme na maji katika maeneo yenye uwekezaji ili kuvutia wawekezaji.

Alitoa rai hiyo,wakati wa ziara yake ya siku moja ,aliyoifanya mkoani Pwani kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KEDS kilichopo Kibaha,na cha kutengeneza vigae Twyford Ceramics Ltd/Pingo,Chalinze ,Bagamoyo.

Majaliwa ,alieleza kuwa ni lazima raia mmoja mmoja na jukumu la kila mmoja kusimamia kulinda nchi kuanzia maeneo wanayoishi .

Alisema serikali imejipanga kuendelea kusimamia amani na utulivu,ambapo amewataka wananchi waiunge mkono serikali kupambana na wahalifu wasio na nia njema na serikali.

“Hatuna uhakika kwa watu hawa wanaofanya vitendo vya ovyo,watanzan ia waungane na serikali,kupambana ili wasije kuingia kwa wawekezaji na kupoteza ndoto za serikali za kupata wawekezaji “alisema Majaliwa.

Akizungumzia tatizo la uhaba wa maji ,alisema mradi wa WAMI ulikuwa ukamilike tangu mwezi July mwaka huu.

Alisema alitembelea mradi huo mwezi juni mwaka huu ukiwa chini ya asilimia 38 na kusema mkandarasi akiendelea kusuasua watamfukuza na kutoa agizo ikifika mwezi huu wafikie asimilia 80.

“Nilitaka kuja mwezi huu lakini nikaambiwa speed ni ndogo na bado hali hairidhishi,na mkandarasi hajamaliza”mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amekuwa akiuliza juu ya kukwama kwa mradi huo”  ;”Nimetoa wiki mbili kwa waziri aangalie dhamana ya kampuni kwenye ubalozi wao wa India na kuangalia sheria namna ya kufanya ama kukamilisha mradi kwa muda mfupi uliobaki”alifafanua.

Kuhusu nishati ya umeme Majaliwa,alisema serikali ipo mbioni kutekeleza mradi mkubwa wa umeme stiegler’s gorge katika chanzo cha mto Rufiji, utakaozalisha megawatts 2,100 zitakazoondoa kama si kumaliza upungufu wa umeme uliopo.

Aliitaka halmashauri ya Chalinze,ijipange kwa matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro na kuondoa usumbufu kwa wawekezaji.

Kuhusu suala la zimamoto ,Majaliwa alisema mkoa huo kwasasa una viwanda vikubwa hivyo wakati serikali ikipokea changamoto ya uhaba wa vifaa na magari ya zimamoto ,halmashauri ijipange kupitia bajeti zao.

“Viwanda hivi ni vikubwa vinajengwa ,kiwanda hiki cha KEDS kina jengo hilo hapo lenye urefu wa mita 30 juu,tuombe mungu moto usitokee ,unawezaje kuzima moto kwa maji ya kwenye ndoo ,ipo haja ya kuangalia namna ya kutatua changamoto hii”

“Dar es salaam ambako ni mji wa kibiashara serikali itasaidia katika kununua mitambo ya kusaidia kuzima moto kutegemea ukubwa wa majengo yaliyopo”aliongeza Majaliwa.

Kwa upande wa miundombinu ya barabara,alitoa rai kwa halmashauri ya Mji wa Kibaha kuboresha barabara zilizopita mitaani na kuhakikisha mitaa yote iwe na barabara bora kwa kufumua zisizofaa na kuchonga barabara zenye viwango.

Pamoja na hayo ,Majaliwa alibainisha uwekezaji kama huu unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda ambapo itaongeza pato la nchi na itazalisha ajira kwa wingi.

Mambo makubwa matano aliyofanya Rais Magufuli Tangu Aingie Madarakani

0
0
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Katika kuelekea ujenzi wa  Tanzania ya uchumi wa kati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, Kiongozi anayesifika kwa uchapakazi, mtu wa watu, mtu wa  wanyonge na Mzalendo kwa kusimamia rasilimali za Taifa ambaye  ameonyesha nuru kubwa kwa watanzania.

Katika hotuba zake mbalimbali amekuwa akisisitiza wananchi kufanya kazi na kuienzi kauli mbiu yake “HAPAKAZI TU” huku katika utendaji kazi wake Rais Magufuli ameonesha dira kubwa kwa kuanza na miradi mikubwa ambayo itaipeleka nchi katika uchumi wa kati na wenye viwanda na huduma nzuri kwa jamii, watanzania wanatakiwa kumuunga mkono ili  aweze kuifanya kazi yake kwa ufasa kwa kuanzisha, kuendeleza na kumalizia miradi ambayo ipo mikononi mwake.

Kama alivyoahidi wakati wa kampeni kwamba Serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi huku akiwa mstari wa mbele katika kuchapa kazi na alipewa jina la uchapakazi kama  Tinga Tinga yani mtu wa kazi, ni miradi mingi ambayo Serikali yake imefanya na inaendelea kufanya mambo makubwa Kama yalivyoainishwa na mwandishi wa makala hii.

  1.  Barabara za Juu (Fly Over).
Aprili 16 ya mwaka 2016 uzinduzi rasmi wa ujenzi  wa barabara za juu  ulifanyika Jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Tazara ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, barabara ambayo itaondoa msongamano wa magari katika Jiji hilo na kuweza kusaidia kuokoa upotevu wa mapato utokanaona watu kuchelewa kazini na kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Faida kubwa ya barabara hii itatupunguzia fedha zilizokuwa zikipotea, katika tafiti zilizofanywa mwaka 2013 tulipoteza billion 411.3 katika Jiji la Dar es Salaam pekee kwa sababu ya msongamano mkubwa”, alisema Rais Magufuli.

Mradi huu mkubwa ambao utagharimu fedha za kitanzania shilingi billion 101.6 unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JAICA),  ambapo  Shirika hilo litatoa kiasi cha shilingi billion 93.44 na Tanzania ikitoa billion 8.36,Mradi huu ambao ni wa aina yake Tanzania unatarajia kumalizika ifikapo oktoba 2018, huku barabara nyingine ya aina hiyo iliyoko makutano ya Ubungo ikitarajiwa kamilika ifikapo 2020 na kuwezesha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufurahia maisha kwani sasa wataondokana na adha ya usafiri hivyo kuwahi kwenye maeneo yao ya kazi kuchapa kazi na kuijenga Tanzania ya viwanda.

2. Bomba la Mafuta Ghafi (Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanzania).

Ilikuwa ni siku ya pekee kwa wananchi wa chongoleani ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseveni walizindua mradi mkubwa ambao ni wa kipekee duniani.

Ni bomba ambalo lina urefu wa kilomita 1445 huku Tanzania likichukua sehemu kubwa yaani kilomita 1115 na kilomita 130 ni kwa upande wa Uganda, ni mradi ambao utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani billion 3.5 na utasimamiwa na kampuni tatu yaani SNOOC,TOTALE zote kutoka nchini Ufaransa pamoja na TUROL ya Uingereza na unatarijia kukamilika  mwaka 2020.

“Ni mradi wa kipekee duniani kwa kuwa mradi kama huu upo India ambao unasafirisha mafuta ghafi lakini una kilomita 600 tu, kwa hiyo bomba hili ni la kwanza duniani”, alisema Rais Magufuli.

Mradi huu utapita katika Mikoa nane kwa Tanzania bara Wilaya 24 huku Vijiji 184 vikifaidika na mradi huo mkubwa wa kipekee ambao utatoa ajira 10,000 wakati wa ujenzi na 1,000 kwa uendeshaji wake, Wahenga walisema “Kizuri kula na nduguyo” ndivyo ilivyo kwa Rais Museveni wa Uganda kukubali kushirikiana katika mradi huu mkubwa kwa kupata ushawishi mkubwa wa usalama kutoka kwa Rais mchapakazi Dkt.John Pombe Magufuli (Tinga Tinga).

 3.   Kufufua Shirika la Ndege (Air Tanzania).
Serikali ya Awamu ya Tano ilianzisha nia na matumaini katika kukuza na kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa kufufua shirika lake la ndege (ATCL) ambalo  mwaka 2016 lilianza rasmi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kununua ndege zake mpya ambazo zimekuwa zikisaidia Watanzania hususani wafanya biashara waendao mikoani mara kwa mara kwa kupunguza gharama kubwa za usafiri.

“Tumeleta bombardier Q 400 imepunguza gharama za safari kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza wanalipa 160,000 hadi 200,000 wakati nauli ilikuwa imeshafikia hadi  800,000 kwa safari za Dar es Salaam –Mwanza”, alisema Rais Magufuli.

Mnamo septemba 2016 serikali ya awamu ya tano ilileta ndege mbili aina ya Bombadier Q400 ambazo litengenezwa nchini Canada, katika matarajio yake inatarajia kuwa na ndege 7 ambapo kwa awamu ya kwanza zimekuja mbili , lakini pia ndege mbili aina ya  Jeti CS 300 zenye uwezo wa kubeba abiria 137-150 zitaletwa  nchini 2018 , bila kusahau ndege kubwa aina ya Boen 787-8 Dreamliner  yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo nayo italetwa waka 2018, itasaidia kwa safari za kimataifa kwani itakuwa na uwezo wa kutoka moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa kimataifa  wa Julius Nyerere hadi Marekani ama Ulaya bila kutua kokote.Huu ni mradi ambao utaleta fursa ya maendeleo hususani katika sekta ya utalii.

   4. Sekta ya Utalii.
Sekta ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ameendelea kuinua zaidi ni Sekta ya Utalii baada ya ununuzi wa ndege ambazo zitakuwa kimbilio katika kukuza na kuimarisha Utalii nchini.

“Huwezi kuendeleza nchi bila kuwa na Watalii sisi tunazungumza Watalii hawajaweza kufika hata milioni 2, lakini nchi kama Morocco inapokea Watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka kwa hiyo ni vyema kushirikana nao katika masuala ya Sekta ya Utalii”, alisema Rais Magufuli.

Sekta ya Utalii ni chachu kwa maendeleo ya Taifa kwani inalipatia pato kubwa na kuweza kuimarika kiuchumi kupitia fedha za kigeni, lakini kwa Tanzania kumekuwa na upungufu wa ndege kwa kuliona  hilo Serikali ya Awamu ya Tano imeweza  kununua ndege kubwa aina ya Boen 787-8 dreamliner ambayo itakuwa inatoka moja kwa moja kutoka Ulaya, Amerika na kwingineko duniani na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

“Tunataka Watalii wawe wanatoka Marekani wanakuja moja kwa moja Dar es Salaam, ile ndege inauwezo wa kutoka Marekani, Australia bila kutua popote”, alisema Rais Magufuli.

Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendeleza Utalii kwa kuingia makubaliano  na nchi mbalimbali ikiwemo Serikali Morocco kupitia ziara ya Mfalme Mohammed VI ,ya mwaka 2015 ambapo waliingia makubaliano ya mkataba kwa Sekta ya Utalii unaolenga kubadilishana Watalii kwani nchi ya Morocco ina idadi kubwa iliyofikia milioni 12 kwa mwaka 2015 na idadi hiyo inatarajia kuongezeka mpaka milioni 14 mwaka 2017 kwa hiyo ni vyema kuwa na ushirikaiano ili kukuza Sekta hii nchini.

5. Mradi mkubwa wa umeme (Kinyerezi I na II).
Juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano yenye malengo makubwa katika kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda imetambua kuwepo kwa viwanda kunaambatana na nishati ya uhakika ya umeme kwa hiyo Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameweza kuanzisha mradi mkubwa wa umeme ili kuendana na Sera yake ya Tanzania ya viwanda.

“Umeme ni maendeleo, umeme ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi kwa Taifa lolote duniani, bila ya kuwepo kwa umeme wa uhakika ndoto yetu ya kujenga uchumi wa viwanda haitaweza kutimia”, Rais Magufuli.

Katika mradi huu wa umeme ulianza na kinyerezi I ambayo itaweza kutoa megawati 150 lakini katika uzinduzi wa ujenzi wa kinyerezi II ambayo itatoa megawati 240 kwa watanzania, Mradi huu wa kinyerezi II ambao unafadhliwa na Serikali ya Japan iliyotoa dola za kimarekani milioni 292 ambayo ni asilimia 85 ya ujenzi huku Tanzania ikitoa dola milioni 120 ambayo ni sawa na asilimia 15 ya mradi, Uzinduzi huu uliambatana na ongezeko la megawati kinyerezi I ambapo megawati 180 zitakazogharimu dola milioni 20 jumla ya  megawati 330 zitapatikana katika Mradi huo na hii ni faida kubwa kwa Watanzania wote kwani wataweza kuanzisha viwanda vidovidogo na hatimaye kukuza uchumi.

“Tunataka tuwe kama nchi zingine duniani kwa matumizi ya umeme sisi bado tuko wati 30 kwa kila mtuamiaji wa nishati hii, lakini Kenya wati 40, China wati 490, Afrika ya Kusini wati 500 na Marekani wati 1,683 kwa kila mtu kwa hiyo sisi bado tuko nyuma”, Rais Magufuli

Katika mradi huu ambao utajengwa kwa awamu yaani kinyerezi I mpaka VI utasaidia kuondokana na adha ya umeme nchni.

Kwa uchache hayo ndio baadhi ya mafanikio ambayo JPM ameweza kuyafikia katika kipindi kifupi alichokaa madarakani, hii ni ishara kuwa hadi atakapomaliza muhula wake Tanzania itakuwa imepaa kiuchumi na kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali.

Nyalandu aomba kumsafirisha Tundu Lissu Marekani kwa Matibabu Zaidi

0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweka kambi nchini Kenya kuangalia uwezokano wa kupata ruhusa kutoka kwa madaktari ya kumsafirisha Mh Tundu Lissu kwenda Marekani kwaajili ya matibabu zaidi baada kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Nyalandu amedai ni siku ya tatu bado hajapata ripoti inayoonyesha maendeleo ya mgonjwa huyo ili waangalie kama wanaweza kwenda nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi.

==> Hii  ni Taarifa ya Mh Nyalandu 

Je,una Upungufu Wa Nguvu Zakiume,kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa,kufika Kileleni Mapema Na Kushindwa Kurudia ????

0
0

Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa na mambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA nk.

Upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa, mahusiano mengi kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,
1 KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA 
2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA 
3 KUWAHI KUFIKA KILELENI 
4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI 
5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO LA NDOA KABISA.

TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.

PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK 

WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO 

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha vidonda vya tumbo,korodani kuvimba,na anatoa dagu za utajiri kwa wanaohitaji bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM,NAUTALETEWA POPOTE ULIPO.

 SIMU; NO 0767145357/0629034550.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images