Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Dereva Aliyegonga Treni Morogoro Afikishwa Mahakamani

$
0
0
Dereva wa daladala aliyesababisha ajali iliyoua wanafunzi watatu na abiria wengine 27 kujeruhiwa mkoani Morogoro amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka 30, likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kugonga treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Charles Petro ambaye alipata majeraha kwenye ajali hiyo amesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Joyce Mkoi.

Wakili wa Serikali, Caristus Kapinga amedai Agosti 24 asubuhi, kwenye makutano ya reli na barabara eneo la Tanesco, Manispaa ya Morogoro mshtakiwa alitenda makosa hayo.

Kapinga amedai kwa makusudi, huku akijua kufanya hivyo ni kosa mshtakiwa aliendesha gari aina ya Nissan kwa uzembe na kugonga treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Kutokana na ajali hiyo, wanafunzi watatu walifariki dunia na abiria 30 walijeruhiwa wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizoko Kihonda na Msamvu katika Manispaa ya Morogoro.

 Mshtakiwa amekana mashtaka yote na  hakimu ameahirisha kesi Hadi Septemba 13 itakapotajwa.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi haujakamilika. Mshtakiwa amepelekwa  rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya  Sh10 milioni na mwingine kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika.

Urusi yatia mguu mgogoro wa Korea Kaskazini, yaitahadharisha Marekani

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amemwambia waziri wa Ulinzi wa Marekani, Rex Tillerson kuwa kuiwekea vikwazo vingi Korea Kaskazini hakutasaidia chochote kutatua mgogoro uliopo kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi imesema kuwa viongozi hao wamezungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio yanayofanywa na Korea Kaskazini.

Lavrov amesema kuwa diplomasia ndio njia pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.

Hata hivyo, Waziri wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini ili iweze kuachana na mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia huku Rais Trump akisema mazungumzo sio suluhisho

Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu

$
0
0
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.

Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.

Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.

Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.

Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Rugemalira wa Escrow agonga mwamba Mahakama ya Mafisadi

$
0
0
 Mshtakiwa wa kesi ya uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, James Rugemalira amegonga ukuta katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi) baada ya kunyimwa dhamana.

Rugemalira ambaye anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yenye mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana, alikimbilia mahakamani hapo kuomba afutiwe mashtaka ya utakatishaji fedha kisha aachiwe huru kwa dhamana kwa madai hati ya mashtaka yanayowakabili ina kasoro za kisheria.

Jana, Jaji Mfawidhi Firmin Matogolo alitupilia mbali maombi hayo akisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa nafuu alizokuwa akiziomba.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, jopo la mawakili wa Rugemalira waliieleza Mahakama kuwa hati ya mashtaka haina maelezo yanayoonyesha kosa la utakatishaji fedha.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Dk Zainabu Mango alipinga hoja hizo, akidai mashtaka yanayomkabili mshtakiwa hayana dhamana.

Akijibu hoja ya kasoro za hati ya mashtaka, Wakili Mango alidai maombi hayo yamepelekwa kwenye jukwaa ambalo si sahihi.

Alisema kesi hiyo haijafikia hatua ya kusikilizwa katika mahakamani hiyo na kwamba inaweza kuangalia uhalali wa mashtaka hayo, shauri hilo litakapohamishiwa mahakamani hapo kwa usikilizwaji.

Hata hivyo, Jaji alikubaliana na hoja za Wakili Mango kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza uhalali wa hati ya mashtaka kwa kuwa suala hilo limefikishwa wakati ambao si muafaka.

Pia, Jaji Matogolo alisema kwamba Mahakama hiyo huwa na mamlaka ya kuchunguza uhalali wa mashtaka endapo maombi yangewasilishwa kwa njia ya mapitio na si dhamana.

Rugemalira na mshirika wake wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Sethi wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama Yagoma Kupokea Bangi Iliyokutwa Nyumbani kwa Wema Sepetu

$
0
0
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu imegoma kupokea bangi inayodaiwa kukutwa nyumbani kwa Mlimbwende Wema Sepetu, kama kielelezo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametoa uamuzi huo leo Agosti 31, kutokana na hoja za kupinga kupokelewa zilizowasilishwa na Wakili wa Wema, Tundu Lissu.

Awali Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima akiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula aliomba kutoa bangi kama kielelezo katika kesi hiyo mahakamani ambayo alidai kupima msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi.

Mulima aliomba kuitoa bahasha iliyofungwa, yenye muhuri, saini ya shahidi huyo na namba ya maabara 291 ya 2017 mahakamani hapo kwa utambuzi.

Wakili Lissu alipinga kisipokelewe kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.

“Mheshimiwa hakimu vipisi viwili vyenye majani  ukiviangalia kwa makini ni vishungi vya sigara ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua, kwetu vinaitwa twagooso, kitu kinachoitwa msokoto wa bangi hakijulikani  kimefungwa fungwa  tu karatasi, kuna kibiriti, karatasi nyekundu, haiwezekani vitu vilivyotolewa kwenye bahasha kuwa ndiyo vitu shahidi alivielezea, mahakama isikubali kuvipokea kama kielelezo,” alidai Lissu.

Baada ya mahakama kugoma kupokea kielelezo hicho imepanga kuendelea kusikiliza ushahidi wa Jamhuri Septemba 12 na 13 mwaka huu. Wema na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kulevya.

Harbinder Sethi wa Escrow kawekewa Maputo tumboni

$
0
0
Wakili wa mshtakiwa Harbinder Sethi, Joseph Makandege ameulalamikia upande wa Jamhuri kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Hospitali ya Taifa Muhimbili kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilivyoamuru.

Amedai hali hiyo inahatarisha afya ya mteja wake kwani akikosa kupata matibabu sahihi anaweza kupoteza maisha kutokana upasuaji aliofanyiwa uliosababisha kuwekewa maputo tumboni.

“Mara mbili mahakama ilitoa amri ikielekeza utawala wa Magereza kumpeleka mshtakiwa wa kwanza Muhimbili , amri ilitolewa baada ya mahakama kukubaliana na hoja za upande wa utetezi, lakini badala ya kumpeleka Muhimbili, Magereza walimpeleka mshtakiwa Hospitali ya Amana.

“Kwa taarifa za kitabibu ni kwamba hali ya mshtakiwa wa kwanza isipohudumiwa ipaswavyo inaweza kusababisha kifo kwani maputo yanaweza kupasuka tumboni , mahakama iliekeza mshtakiwa apelekwe moja kwa moja Muhimbili ambayo ni hospitali ya juu kabisa ya Serikali, ndio nategemea inaweza kuwa na wataalamu na vifaa thabiti kwa ajili ya matatizo yanayomkabili mshtakiwa wa kwanza,” amedai.

Makandege alidai amri zote zilizotolewa na mahakama hazijatekelezwa , aliomba mahakama itoe amri nyingine ya kuutaka upande wa Jamhuri kuamuru amri iliyotolewa itekelezwe.

Akijibu Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter amedai Jamhuri haijakaidi amri ya mahakama na kwamba Magereza wana utaratibu wao ambapo wanahojiana na mgonjwa wakiona tatizo lake hawana utaalamu nalo wanampa rufaa kwenda Muhimbili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 14 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo mshtakiwa Seth na James Rugemarila, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwa na mashitaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha hivyo kuwafanya wakose dhamana.

Mahakama Yadai Agness Masogange Ana Kesi ya Kujibu

$
0
0
Msanii  Agnes Gerald maarufu Masogange,  anayetuhumiwa kutumia dawa za kulevya amekutwa na kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 31, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Constatine Kakula, kufunga ushahidi wao kwa mashahidi watatu.

Mashahidi wa upande wa Jamhuri waliotoa ushahidi kwenye kesi hiyo ni Mkemia Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye alipima sampuli ya mkojo na maofisa wawili wa polisi ambao walimpeleka Masogange kwa mkemia.

Baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, Masogange ambaye anatetewa na Wakili Reuben Simwanza, alidai atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu, kwa ajili ya utetezi na kusema dhamana ya mshitakiwa inaendelea.

Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo  yasiyofahamika Dar es Salaam, alitumia dawa  aina ya heroin na Oxazepam.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 1

Mahakama Ya Juu Yafuta MATOKEO Ya Uchaguzi Uliompa Ushindi Uhuru Kenyatta

$
0
0
Mahakama ya Juu imefuta matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta kuwa madarakani kwa muhula wa pili.

Mgombea wa Muungano wa Nasa, Raila Odinga alifungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Agosti 8, akisema ulitawaliwa na udanganyifu ikiwemo kuchezewa mitambo ya kujumlishia matokeo.

Katika uamuzi wake, Mahakama imesema uchaguzi huo ulikuwa na dosari nyingi, hivyo kukiuka misingi ya uchaguzi huru na wa haki kama ilivyoelekezwa katika Katiba ya nchi hiyo.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Taifa hilo kwa Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi na inaweka rekodi mpya katika historia ya uchaguzi barani Afrika ndani ya mfumo wa vyama vingi.

Katika uchaguzi uliopita, Odinga alienda mahakamani kupinga matokeo lakini Mahakama hiyo ilitupilia mbali hoja zake na kuridhia matokeo yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.

Katika uchaguzi wa Agosti 8, Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku mpinzani wake Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.

Kwa uamuzi uliotolewa na mahakama, uchaguzi mwingine unapaswa kufanyika katika kipindi cha siku 60. Iwapo ushindi wa Kenyatta ungeidhinishwa angepaswa kuapishwa Septemba 12.

Kumekuwa na shamrashamra katika mitaa mbalimbali ya Nairobi na Mombasa kushangilia uamuzi huo, huku Odinga akiwa na wanasiasa wenzake wamepongeza wakisema watatoa taarifa zaidi baadaye.

Makongoro Mahanga nusura atupwe Jela

$
0
0
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana katika Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga jana alinusurika kutupwa jela kutokana na kushindwa kutekeleza amri ya mahakama kulipa deni kila mwezi.

Mahanga ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Ukonga na Segerea kupitia CCM, aliamriwa kumlipa mwanasheria Kainerugaba Msemakweli kiasi cha Sh14 milioni zikiwa ni gharama za kesi alizozitumia katika kesi ya madai aliyofunguliwa na Mahanga.

Hata hivyo, Mahanga ameshindwa kumaliza deni hilo, baada ya kulipa kiasi cha Sh6 milioni tu mpaka sasa na hivyo kudaiwa Sh8 milioni.

Kutokana na kushindwa kulipa fedha hizo na kutokufika mahakamani bila taarifa, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Juni 16, ilitoa amri kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala kumkamata na kumfikisha mahakamani hapo.

Hata hivyo, hakuweza kutekeleza amri hiyo licha ya kukumbushwa mara kadhaa hadi mahakama hiyo ilipomtaka kamanda huyo mwenyewe afike mahakamani kujieleza ni kwa nini hajatekeleza amri hiyo.

Mahanga aliamriwa awe analipa Sh2 milioni kwenye akaunti ya Msemakweli kila mwezi na kuwasilisha risiti mahakamani hadi deni hilo litakapokwisha, lakini alipofika mahakamani jana baada ya kukamatwa, aliwasilisha risiti ya malipo ya Sh500,000 badala ya Sh2 milioni.

Mahakama ilikataa kuipokea risiti hiyo kwa kuwa kiasi hicho ni kinyume cha makubaliano na pia alikuwa nje ya muda wa makubaliano.

Kutokana na hali hiyo, Mahanga alikuwa anakabiliwa na hatari ya kutupwa jela kwa kuwa Msemakweli tayari alishalipa mahakamani Sh300,000 kwa ajili ya kumhudumia gerezani kama mfungwa wa madai kwa kushindwa kulipa deni hilo.

Hatahivyo, alinusurika baada ya kujitetea huku akieleza kuwa anakabiliwa na matatizo ndipo mahakama ikamwonea huruma na kuamua kumwachia kwa dhamana huku ikimtaka kulipa deni hilo lote lililobakia ifikapo Septemba 7.

Mdhamini wake, Dickson Biseko alisaini bondi ya dhamana ya Sh2 milioni, ili kwamba kama Mahanga hatafika mahakamani siku hiyo pamoja na kiasi hicho, basi yeye ndiye atakayekamatwa. 

Uhuru Kenyatta: Sikubaliani na uamuzi wa Mahakama lakini Ntauheshimu

$
0
0
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa hakubaliani na uamuzi wa Mahakama ya Juu nchini humo ya kubatilisha uchaguzi wa urais uliopita na kuagiza kufanyika upya kwa uchaguzi lakini anaheshimu uamuzi huo wa mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  kuhusu uamuzi huo wa Mahakama, Rais Kenyatta amesema kuwa Jubilee iko tayari kurejea kwenye uchaguzi kama Mahakama ilivyoamuru huku akiwataka Wakenya kudumisha amani.

“Wenzangu, amani… amani… amani. Mshike jirani yako mkono umwambie hii ni vita ya wale, sisi ni kitu kimoja. Sisi ni jamii ambayo inaitwa ‘Wakenya’ na hivyo ndivyo itakavyokuwa,” amesema Kenyatta.

“Na mimi namshukuru ndugu yangu hapa [Ruto] amesema yuko tayari kurudi uwanjani,” ameongeza.

Kenyatta amewataka Wakenya kujiandaa na uchaguzi mwingine na kwamba Jubilee wataingia tena barabarani ‘kupiga debe’ ili wachaguliwe tena.

Leo, Mahakama ya Juu iliamua kubatilisha uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 8 mwaka huu ambao kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo, Kenyatta alishinda kwa zaidi ya asilimia 54 dhidi ya Raila Odinga (NASA) aliyepata asilimia 44.7.

Mahakama imeeleza kuwa kulikuwa na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na katiba ya nchi hiyo uliopelekea uchaguzi huo kutofaa kuwa halali. Imeamuru uchaguzi huo kufanyika baada ya siku 60 (Novemba Mosi).

Alichokisema Raila Odinga Baada ya Mahakama ya Juu Kufuta Matokeo yaa Uchaguzi Kenya

$
0
0
Mgombea urais wa Kenya kupitia Muungano wa Nasa, Raila Odinga amesema Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ni lazima ifanyiwe mabadiliko ili kurudia  uchaguzi.

Mahakama ya Juu ya Kenya leo Septemba Mosi imefuta matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta kuwa madarakani kwa muhula wa pili.

Kwa uamuzi uliotolewa na mahakama, uchaguzi mwingine unapaswa kufanyika katika kipindi cha siku 60. Iwapo ushindi wa Kenyatta ungeidhinishwa angeapishwa Septemba 12.

Odinga amesema ni lazima waliosababisha dosari kwenye uchaguzi wa Agosti 8 waondolewe.

“Tume ya uchaguzi ni lazima isafishwe ili turejee kwenye uchaguzi mwingine na nina uhakika tutashinda,” amesema Odinga katika mkutano na waandishi wa habari ambao pia uliwashirikisha viongozi wengine wakuu wa Nasa.

Amesema ni lazima viongozi waliohusika wawajibishwe akisisitiza mitambo ya Tume ya Uchaguzi ni lazima iwe wazi kwa ukaguzi.

Odinga amesema hawana imani na IEBC inayoongozwa na Wafula Chebukati kwa kuwa haikuwatendea haki kwenye uchaguzi huo.

“Leo tunasherehekea sikukuu ya Eid lakini tuna sherehe nyingine ambayo Mahakama imetupatia tunaisherehekea,” amesema.

Amesema uamuzi wa Mahakama umeipa heshima Kenya katika ujenzi wa demokrasia. Ameipongeza kwa umakini uliozingatia uamuzi wa Wakenya wa kutaka uchaguzi huru na wa haki.

 “Uamuzi wa Mahakama umetoa sura mpya na umetuma ujumbe kwa Afrika namna demokrasia yetu ilivyokomaa. Kulikuwa hakuna haja ya kurudia uchaguzi kama tume ingeonyesha matokeo katika mitambo yake,” amesema.

Odinga amesema majaji wameonyesha Mahakama zinaweza kuwa na uhuru na kusimama dhidi ya nguvu za marais Afrika.

“Mahakama imeashiria mwanzo wa Kenya mpya na daima ni kwamba, ukweli ndiyo msingi wa yote na jina na Jaji Maranga litaendelea kukumbukwa katika historia ya Kenya,” amesema. David Maranga ndiye Jaji Mkuu wa Kenya.

Shehena ya Almasi Yakamatwa Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro

Mwakyembe apinga vikali uzushi juu ya ubovu wa ndege za Bombardier

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Watanzania kupuuza maneno ya upotoshaji yanayosemwa na watu wachache hususani wanasiasa kuhusu ubovu wa ndege za Serikali aina ya Bombardier.

Amesisitiza kuupuza habari hizo kwani anaamini kuwa wazushaji hao hawana utaalamu wowote wa kutambua jambo hilo.

Mwakyembe alizungumza hayo pindi akifanya mahojiano na maalumu na waandishi wa habari akiwa katika chumba cha abiria kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe akijiandaa kusafiri kwenda Dar es salaam.

Dk Mwakyembe amesema wapo watu wamekuwa wakipiga kelele za uzushi kwamba serikali imenunua ndege mbovu, jambo ambalo siyo la kweli kwani mchakato wa upatikanaji wa ndege hizo ulianza muda mrefu ukiwashirikisha wataalamu mbalimbali kwa kuzingatia mazingira ya nchi pamoja na viwanja vilivyopo.

“Kuna watu wanasema ndege hizi ni mbovu sasa watuletee za kwao ambazo siyo mbovu. Kwanza hawana hata utaalamu wa kujua ndege nzima au mbovu pia wanachoangalia ni kutumia pangaboyi tofauti na zingine lakini ubora ni uleule,”.

Habari Zilizopo Katika Magazet ya Leo Jumamosi ya Septemba 2

Unasumbuliwa na Kiharusi,Ngiri au Kifafa?......Unatatizo la Nguvu za Kiume, Kuachika au Tatizo la Uzazi? . Kutana na Mtalaamu Huyu Akusaidie

$
0
0
SASA YUPO DAR;Anadawa ya kumvuta mpenzi wako popote alipo kwa masaa 6 tu na kumtuliza asitoke kwako

Je, unaugomvi usioisha na mpenzi wako na unaachwa mara kwa mara? Njoo upate dawa ufurahie penzi tulivu la umpendae.

Anadawa za nguvu za kiume, kuimarisha mishipa iliyolegea, kuongeza homoni na kukufanya udumu katika tendo hadi dakika 45 na unaweza kurudia tendo hata mara 4 bila kuchoka.

Anatibu Busha bila kupasua,uzazi, mshipa wa ngiri,kiharusi,kifafa,kuondoa majini machafu nakadhalika.

Mpigie kwa simu: 0755505099

JWTZ lawarudia wananchi......Hii ni Hotuba ya Mkuu wa Majeshi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo

$
0
0
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo (jana) limetimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake ambapo akiongeza na waandishi wa habari Jenerali mabeyo aliwaambia waandishi kuwa yuko na Jenerali Sarakikya (rtd) Mkuu wetu wa Majeshi ya Ulinzi wa Kwanza Mzalendo, Jenerali Mwamunyange (rtd) Mkuu wa Majeshi wa Saba, ambaye nimepokea kijiti hiki toka kwake mwezi Februari, 2017.

Wapo pia, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Isamuhyo, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi (Machifu) wa Makao Makuu ya Jeshi na Sajini Meja wa Jeshi letu.

Nimeona nijumuike nao wote hawa ili kwa pamoja kupitia kwenu Waandishi wa Habari mtuwasilishie salamu zetu za Maadhimisho ya Miaka 53 ya JWTZ, kwa Watanzania wote. Maadhimisho haya yalianza tarehe 25 Agosti, 2017 kwa Wanajeshi wote kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Michezo, kufanya Usafi kwenye maeneo ya kijamii na Tiba. Leo hii tunahitimisha Madhimisho hayo.

Siku hii ya leo JWTZ linasherehekea kutimiza miaka 53 tangu kuundwa kwake Septemba Mosi, 1964.  Hii ni siku muhimu sana kwetu na kwa wananchi wa Tanzania kwa ujumla, kwa sababu, JWTZ ni Jeshi letu sote na limeundwa kutokana na Wananchi wa Tanzania.  Awali ya yote kwa heshima na taadhima ninapenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Pili kwa niaba ya JWTZ na kwa niaba yangu mwenyewe napenda kumshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT, pamoja na Wizara anayoiongoza kwa mwongozo anaotupatia na ushirikiano mkubwa anaoutoa kwa Jeshi.

Aidha, Wakati tunatimiza Miaka 53 napenda pia kuwashukuru Baraza la Mawaziri pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali kwa Maelekezo mbalimbali wanayoyatoa kwa Jeshi letu. Ushauri wao umekuwa mhimili mkubwa kwa utendaji wa Jeshi letu. Ninawashukuru pia Wakuu wa Majeshi Wastaafu, wengine ninao hapa leo mnawaona kwa namna walivyolilea Jeshi letu katika nyakati mbalimbali hadi hii leo tunatimiza miaka 53 likiwa Jeshi kubwa kabisa, lenye nidhamu kubwa, weledi na uhodari mkubwa.

Wakati tunaandika Historia ndefu ya Miaka 53, Jeshi letu limefikia mafanikio mbalimbali, miongoni mwa mafanikio ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) ni kudumisha amani na utulivu uliopo nchini mwetu tangu Taifa letu lipate Uhuru wake. Aidha, JWTZ limeshiriki Vita vya ukombozi Kusini mwa Afrika, Vita vya Kagera na Visiwa vya Comoros. Jeshi letu pia limekuwa ni nguzo muhimu katika kudumisha amani sehemu mbalimbali duniani kwa kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani, katika nchi za Liberia, DRC, Sudan (Darfur), Lebanon, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati n.k. Ndani ya Nchi Jeshi letu limeshiriki kutoa usaidizi katika masuala mbalimbali ikiwemo majanga, uokoaji na huduma za kijamii. JWTZ bado limeendeleza mshikamano na kuonesha uzalendo wa hali ya juu na hivyo kubakia kuwa Jeshi la Wananchi.

Naomba niwatakie Maafisa na Askari wa JWTZ na Watanzania kwa ujumla “Happy Birthday”. Ninawapongeza sana kwa kufikia siku ya leo. Kwa vile leo ni siku ya Eid El Hajj nawatakia Eid Njema pia wao na familia zao.

Mwisho, ninawaomba watanzania wote waliunge mkono Jeshi lao na JWTZ daima liko imara na tayari kuilinda Nchi yetu. Tutailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa uaminifu Serikali yetu. Namuomba Mungu atusaidie.

JENERALI VENANCE SALVATORY MABEYO, ndc

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI

Serikali yaongeza muda wa uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo inajukumu la kusajili, kuratibu na kufuatilia uendeshaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeamua kuongeza muda wa siku 16 kwa Mashirika ambayo bado hayajahakiki  taarifa zake kwa Msajili wa Mashirikka yasiyo ya Kiserikali kukamilisha uhakiki huo.

Akizingumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma jana  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alisema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kuja kuandikisha taarifa za asasi zao katika vituo mbalimbali vya usajili vya kanda.

Bibi Sihaba aliongeza kuwa Serikali ina nia njema ya na siyo mbaya kama watu wanavyohisi katika utekelezaji wa zoezi hili la uhakiki linaloendelea nchi nzima katika vituo vya Kanda tano (5), na lengo ni la zoezi ni kutambua takwimu halisi ya Mashirika yanayofanya kazi ili kuweka utaratibu mzuri wa kutambua mchango wa kila asasi katika kuhudumia jamii katika nyanja mbalimbali.

“Niwaombee wadau wetu watumie muda huu tuliouongeza vizuri kwa kujitokeza kwa wingi kufanya uhakiki wa Mashirika yao na wale wenye changamoto tutawaelekeza namna bora ya kuzitatua,” alisema Bibi Sihaba.

Aidha Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw. Marcel Katemba aliwahikikishia wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kuwa hakuna tatizo katika zoezi la uhakiki wao na ni muhimu sana kujihakiki ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa uhuru na uwazi.

“ Niwahakikishie wadau wetu kuwa zoezi hili ni muhimu sana kwenu na kwetu pia katika namna ya kuboresha utendaji kazi wetu,” alisema Bw. Katemba.

Naye Katibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru Serikali kuwa kuandaa na kuratibu zoezi la uhakiki wa mashirika hayo na kuwaomba wamiliki wa mashirka yasiyo ya kiserikali nchini kujitokeza kuhakiki mashirika yao.

“Niwaombe wamiliki wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini tuendelee kujitokeza kwa wingi tuje tuhakiki mashirika yetu ili tuondokane na usumbufu mara baada ya kumalizika kwa kuda wa uhakiki ulioongezwa,” alisema Bw. Ismail.

Zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini lilizinduliwa na katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Agosti 21,2017 na uhakiki huo ulitekelezwa kwa muda wa wili mbili mpaka Septemba 04,2017.

Hata hivyo kutokana na sababu za kijiografia na mwitikio mkubwa wa mashirika kutaka kuhakikiwa ikaamuliwa kuongeza kwa muda wa siku 16 mpaka Septemba 20 mwaka huu, ambao ndio utakuwa mwisho wa uhakiki.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images