Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Taarifa Rasmi ya Jeshi la Polisi Kuhusu Wahalifu 13 Waliouawa Kibiti

$
0
0

Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu  usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.  

 Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake. 

Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam. 
 

Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha  kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:
1.  Hassani Ali Njame
2.  Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3.  Saidi Abdallah Kilindo
4.  Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5.  Issa Mohamed Mseketu @Mtawa
6.  Rajabu Thomas @Roja
7.  Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
 
Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.   
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
2.   
Anti Riot Gun 38mm = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
3.   
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam
4.   
MAGAZINI = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
5.   
Risasi za SMG 158
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
6.   
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea
7.   
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
VIELELEZO VINGINE
8.   
Pikipiki  = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali
9.   
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
10.       
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe

Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki  inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1.  Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3.  Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4.  Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la  Kibwibwi – Wilaya ya  Kibiti
5.  Kuua Afisa Mtendaji,  Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
 
Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
 
a.  Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi  wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.
 
b.  Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
 
c.  Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.
 
Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.

Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.
 
Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili  waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.
 
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii.  Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v.  Rashid Mtutula
 
Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.
 


Imetolewa na;
Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya August 11

Nitapenda Kuolewa Na Mwanaume Anaye Jiweza Kitandani

$
0
0
Mwanadada  Linda  Ikeji  ( 36 ) ambae  ni  blogger  mwenye  mafanikio  makubwa  huko  nchini  Nigeria, amewaacha  watu  midomo  wazi, mara  baada ya  kujibu swali  kuhusu  aina  ya  mwanaume  atakae  penda  kuolewa  nae.

Akijibu  swali  la  mwandishi  wa   Vanguard, jarida  maarufu  la  habari  za  masupastaa nchini  Nigeria, kwamba   utakapo  fika  wakati  wake  wa  kuolewa, atapenda  kuolewa  na  mwanaume  wa  aina  gani  au  mwenye  sifa  zipi,  Linda  alijibu  “

“   Nitapenda  kuolewa  na  mwanaume  mwenye  sifa  kuu  mbili, sifa  ya  kwanza, awe  amaefanikiwa  kwenye  field  yake  ili  niweze kupata  kitu  cha  kujifunza  na  kujivunia  kutoka  kwake, lakini  sifa  ya  pili, lazima  awe  anajiweza  kitandani.  Siwezi  kabisa  kuolewa  na  mwanaume  ambae  hawezi kuniridisha  kitandani  “

Kusoma  mahojiano  ya  mwanadada  huyu, tafadhali  <<BOFYA HAPA>>

Maneno  ya  Linda  Ikeji  yanaonekana  kushabihiana  na matokeo  ya  uchunguzi  wetu. Uchunguzi  wetu  umetuwezesha  kugundua  kuwa, kutokuwa  na  uwezo  wa  kuwaridhisha  wapenzi  wao  kitandani, ni moja  kati  ya  sababu  kubwa  zinazo  wafanya  wanawake  wengi  kutoka  nje  ya  mahusiano  yao au kuyavunja kabisa !
Kutokuwa  na  uwezo  wa  kumridhisha  mwanamke  kimapenzi  kuna sababishwa  kwa  kiasi  kikubwa  na  tatizo  la  ukoseefu  na  ama  upungufu  wa nguvu za  kiume  ambalo  linazidi kushamiri  katika  jamii  yetu.

Kufahamu  jinsi  tatizo  la  ukosefu  na  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, linavyo  tokea  na  jinsi  unavyo  weza  kulidhibiti,  << BOFYA  HAPA>>

TANESCO yakanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi Agosti 8.

Waziri Mwijage Acharuka.......Avifunga Viwanda 10 kwa Kushndwa Kuendelezwa

$
0
0
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amesema serikali imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya kutwaa viwanda walivyopewa wawekezaji na kushindwa kuviendeleza huku viwanda vingine vikiwa chini ya uangalizi wa muda

Waziri Mwijage amesema hayo jana Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao kilichojumuisha wawakilishi wa Wizara za Fedha, Tamisemi na Wizara ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu.

Amevitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha korosho Lindi, Mgodi wa Pugu Kaolin, Mkata Saw Mills Ltd, Manawa Ginnery Co Ltd, Kiwanda cha Chai Dabaga, Tembo Chipboard Ltd, Kiwanda cha Nguo cha Kilimanjaro, Mang’ula Mechanical and Machine Tools co. Ltd na Polysacks cha Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Mwijage amesema serikali ambayo awali ilibinafsisha mashirika 341 ya umma ambayo yalijumuisha viwanda, mashamba, makampuni ya biashara, mahoteli na makampuni ya usafirishaji lakini kati ya  hayo, viwanda vilivyobinafsishwa vilikuwa 156 huku viwanda vinavyofanya kazi vizuri ni 62, huku viwanda vinavyosuasua vikiwa 28, wakati viwanda visivyofanya kazi vikiwa 56 na viwanda kumi vikibinafsishwa kwa kuuza mali moja moja.

==>Msikilize hapo chini

Mbunge wa CCM Singida Atiwa Mbaroni

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia Mbunge Manyoni(CCM), Daniel Mtuka (51) kwa tuhuma ya kumgonga kwa gari mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Sukamahela, Salome Paschal (10) na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, debora Magilingimba alisema tukio hilo limetokea jana katika Kijiji cha Sukamahela tarafa ya Kilimatinde Wilaya ya Manyoni.

Alisema siku ya tukio mbunge huyo akitokea Dodoma mjini akiwa njiani kurundi jimboni kwake akiendekesha gari lake aina ya Toyota Prado alimgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa  akijaribu kuvuka kutoka upande wa kulia kwenda kushoto mwa barabara.

Kamanda huyo alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva Mtuka, kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

“Mtuhumiwa mbunge Mtuka  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na baada ya mahojiano, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kwa uchunguzi wa daktari na baada ya hapo, utakabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi,”alisema.

Katika hatua nyingine, Kamanda Debora alisema watu wawili akiwemo Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ngara mkoani Kigoma, Alfred Kafuku  wamefariki dunia  papo hapo, baada gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori aina ya DAF kwa nyuma.

Amewataja waliofariki kuwa ni  dereva wa gari raia wa Congo ambaye jina lake halikuweza kupatikana na wala kitambulisho chake. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya August 12

Rais Magufuli amteua msemaji mkuu wa serikali

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Hassan Abbas umeanza tarehe 09 Agosti, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002.

Dkt. Hassan Abbas ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, ambapo nafasi hiyo imebadilishwa kutoka Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya uteuzi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


DPP Aifuta Kesi ya Ugaidi ya Lwakatare

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameaondoa maombi yake dhidi ya Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kuhusiana na shtaka la ugaidi dhidi yake.

DPP alikuwa amefungua maombi Mahakama ya Rufani akiomba kibali cha kufungua maombi ya mapitio kuhusiana na uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi.

Maombi hayo ya DPP yalitarajiwa kusikilizwa leo Ijumaa, Agosti 11 na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mussa Kipenka, lakini DPP akaamua kuyaondoa kabla ya usikilizwaji.

Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka ameieleza mahakama kuwa DPP hana nia ya kuendelea na maombi hayo.

Kutokana na nia hiyo ya DPP, wakili wa mjibu maombi, Richard Rweyongeza amesema kuwa hana pingamizi dhidi ya nia ya DPP kuyaondoa maombi hayo na Jaji Kipenka akatoa amri ya kuyaondoa mahakamani maombi hayo.

Kwa uamuzi huo sasa Lwakatare anabaki na shtaka la kula njama ili kutenda kosa, katika kesi ya msingi inayosikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali, Lwakatare na mwenzake walikuwa Ludovick Rwezaura walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka manne likiwemo la kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi kwa lengo la kumdhuru kwa sumu aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.

Mashtaka mengine yalikuwa ni ya ugaidi, wakidaiwa kuandaa mikutano ya kupanga makosa ya kigaidi na kufadhili vitendo vya kigaidi.

Hata hivyo, Lwakatare kupitia kwa mawakili wake walifungua maombi Mahakama Kuu wakipinga mashtaka hayo yaliyokuwa yakiangukia katika Sheria ya Ugaidi.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Lawrence Kaduri ilikubaliana nayo na akamfutia Lwakatare mashtaka hayo ya ugaidi na hivyo kubakiwa na shtaka moja tu la kula njama ambalo haliangukii katika sheria hiyo ya ugaidi.

DPP hakukubaliana na uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ndipo akafungua maombi ya kibali kufungua maombi nje ya muda, ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia mashtaka hayo ya ugaidi.

Unasumbuliwa na Kiharusi,Ngiri au Kifafa?......Unatatizo la Nguvu za Kiume, Kuachika au Tatizo la Uzazi? . Kutana na Mtalaamu Huyu Akusaidie

$
0
0
SASA YUPO DAR; Anauwezo wa kutabiri nyota yako na kukuletea mafanikio makubwa katia biashara yako, kazini na malengo yako ya maisha.Pia anatoa pete ya bahati yenye uwezo wa kukuletea mafanikio makubwa na kutimiza ndoto zako.

Je, Umedhurumiwa? unamdai na hakulipi?...Njoo upatiwe dawa ulipwe haraka. Anadawa ya kumvuta mpenzi wako popote alipo kwa masaa 6 tu na kumtuliza asitoke kwako

Je, unaugomvi usioisha na mpenzi wako na unaachwa mara kwa mara? Njoo upate dawa ufurahie penzi tulivu la umpendae.

Anadawa za nguvu za kiume, kuimarisha mishipa iliyolegea, kuongeza homoni na kukufanya udumu katika tendo hadi dakika 45 na unaweza kurudia tendo hata mara 4 bila kuchoka.

Anatibu Busha bila kupasua,uzazi, mshipa wa ngiri,kiharusi,kifafa,kuondoa majini machafu nakadhalika.

Mpigie kwa simu: 0755505099

Uhuru Kenyatta atangazwa mshindi wa Urais Kenya

$
0
0
Tume huru ya uchaguzi Kenya (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.

Kenyatta amepata kura 8,203,290 na angalau asilimia 25 ya kura katika vituo 35.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amekabidhi cheti cha ushindi kwa Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.

Akihutubia jana mara baada yakutangazwa kuwa mshindi, Rais Kenyatta amewashukuru wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali yake.

“Nawaahidi tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Kenya. Kadhalika, naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya,” alisema.

“Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine.”

Kwa upinzani alisema: “Sisi si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila shindano, kutakuwa na washindi na wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa Wakenya. Nawapa moyo wa ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya wanataka sisi tufaulu.”

“Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana, tutakua pamoja na kuendeleza nchi pamoja.”

“Kwa Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani yako bado ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya fujo, sisi wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki.”

Serikali Yataifisha Magari Yaliyokutwa na Magufuli

$
0
0
Serikali imetaifaisha magari matatu ya kifahari kati ya saba yaliyokutwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini na kubainika hayakuwa na Nyaraka stahiki.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga amesema kuwa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeamuru washtakiwa wa magari hayo Sulatani Ibrahimu rai wa Uganda na Ramadhani Ukwaju wa Tanzania kulipa faini.

Kati ya Makosa wanaoyoshatikiwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na udanganyifu kwa maafisa forodha kuhusu vitu walivyokuwa wameviingiza nchini ambapo nyaraka zao walionyesha walikuwa wameingiza viatu na nguo za mitmba lakini kwenye makontena kulikua na magari hayo ya kifahari.

Aidha Kosa lingine wanaoshatikiwa watuhumiwa hao ni pamoja na kusabiashia serikali hasaara zaidi ya milioni tisini kutokana ukwepaji wa kodi kutoka na uingizaji huo wa magari ya thamani kwa kulipa ushuru kidogo wa nguo na viatu.

Marekani Kupitia Shirika Lake La Misaada La USAID Yaipatia Tanzania Dola Milioni 225 Kwa Ajili Ya Miradi Mbalimbali Ya Maendeleo

$
0
0
Siku moja baada ya Marekani kutangaza kutoa fedha za nyongeza katika mwaka ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, nchi hiyo imetiliana saini na Wizara ya Fedha na Mipango makubaliano ya kutoa Dola Milioni 225. 
 
Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na Utawala bora.
 
Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini Bw. Andy Karas.

Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Bw. Doto James ameishukuru Marekani kwa kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na Tanzania na amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Nae Bw. Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani wanafurahishwa na kuendelea kwa ushirikiano mwema kati yao na Serikali ya Tanzania katika maendeleo na ameahidi kuwa ushirikiano huo utadumishwa.
 
Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.

Pata Tiba ya Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM .HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Miss Tanzania 1996 Shose Sinare Awalalamikia Wapelelezi Kwa Kuchelewesha Kesi Yake

$
0
0
Aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996  Shose  Sinare ameuomba upande wa mashitaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, pamoja na wenzake wawili, walete  mawasiliano yanayofanyika kati ya Tanzania na Uingereza juu ya upelelezi dhidi ya kesi yao.

Shose amedai hivyo jana katika  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha.
 
Mbali na Sinare, washitakiwa wengine ni   katika kesi hiyo ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Msamire Kitilya, na Sioi Solomon.

Sinare alidai  kuwa mpaka sasa wamekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka na nusu hivyo upande wa mashitaka uwasilishe mawasiliano hayo.

Mapema, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika kwani bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi huo.

Kufuatia hayo, Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25 mwaka huu ili upande wa mashitaka ueleze muendelezo wa kile kilichowasilishwa kortini. 

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550  kwa  serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Agosti 2, 2012 Sinare kwenye  Makao Makuu ya benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni kwa  nia ya kudanganya aliandaa nyaraka  ya pendekezo akijaribu kuonyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stanbic  ya Tanzania  watatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni  550 kwa serikali  ya Tanzania  kwa ada ya uwezeshaji ya asilimia 2.4 ya kiasi cha mkopo huo wakati akijua kuwa sio kweli.

Inadaiwa kuwa  Agosti 2, 2012 ,Sinare alitoa nyaraka za uongo za mapendekezo ya kuonyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania,  watatoa mkopo wa dola za kimarekani  milioni 550 na kuziwasilisha katika ofisi za Wizara ya fedha  wakati akijua kuwa sio kweli.

Aliendelea kudaiwa kuwa  Septemba 20, 2012 katika  Makao Makuu ya Benki ya Stanbic nchini yaliyopo Kinondoni, alitenda kosa la kughushi barua.

Sinare anadaiwa kughushi barua ya mapendekezo ikionyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania  watatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 550 kwa Serikali  ya Tanzania  kama ada ya uwezeshaji wa asilimia 2.4 ya kiasi cha mkopo huo wakati akijua kuwa sio kweli.

 Agosti 21,2012,  Sinare anadaiwa kuwa kwa lengo la kulaghai aliwasilisha nyaraka hizo za uongo kuiwezesha Serikali ya Tanzania kupata mkopo huo wa kiasi hicho cha ada ya uwezeshaji, katika ofisi za Wizara ya Fedha.

Washtakiwa hao kwa pamoja  wanadaiwa kughushi nyaraka za makubaliano  kwamba  Novemba 5 ,2012 katika benki ya Stanbic makao makuu Kinondoni  Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya walighushi waraka wa makubaliano wa Novemba 5, 2012.

 Inadaiwa kuwa waraka huo ulikusudia kuonesha kuwa Stanbic Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano  na kampuni ya Enterpirise Growth Market Advisors  (Egma) Limited kuwezesha upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550  kwa ajili Serikali ya Tanzania .

Wanadaiwa kuwa  Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd. Washtakiwa  hao wanadaiwa  kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani milioni sita  katika akaunti tofauti tofauti  za benki.

Kati ya  Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa  kuwa waliweka pesa hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa pesa hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.

Waziri Mkuu: Wananchi Waliopewa Uraia Muheshimu Sheria Za Nchi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu.

Ametoa onyo hilo  jana mchana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora.

Amesema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa huo.

"Taarifa nilizonazo zinaonyesha katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na matukio ya mauaji 35, ujambazi matukio 12, umiliki wa silaha nao unatisha. Yamekamatwa magobole 11, bunduki aina ya SMG saba na Mark Four mbili."

"Tulikamata pia risasi 714 za SMG zikiwa kwenye ndoo za mafuta na juu yake wamepaka mafuta ya mawese. Pia risasi mbili za Mark Four zilikamatwa," amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amewataka wakazi hao ambao baadhi yao wamepewa uraia na wengine bado ni wakimbizi waonyane wanapokutana kwenye vikao vyao kwa sababu matendo yao yanaikwaza Serikali ambayo iliamua kuwapa hifadhi. "Ni vema mkikutana kwenye vikao vyenu muelezane na kuonyana," amesema Waziri Mkuu.

"Ninawasihi matukio haya myadhibiti la sivyo mtaharibu nia njema iliyoleta uwepo wenu.  Bunduki na risasi zinakuja kufanya nini wakati nyie mko maeneo salama? Mauaji ya nini?  Kama kuna tatizo limekupata, muone mwenyekiti wa kijiji,  atakusaidia," alisisitiza.

Alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi yao ambao wamegeuka mawakala na wameanza kuwaleta ndugu zao bila kufuata utaratibu. 

"Hatuzuii mtu kutembelewa na ndugu yake, lakini ni lazima mfuate taratibu. Tunataka tudumishe amani iliyopo nchini lakini pia tudumishe urafiki wa nchi zetu mbili za Burundi na Tanzania," aliongeza.

Mapema, Mbunge wa jimbo la Ulyankulu, Bw. John Kadutu alimuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la upatikanaji wa maji kwenye tarafa hiyo, pia aliomba wasaidiwe ili kata tatu za Kanindo, Igombenkulu na Milambo ziwezeshwe kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

Maalim Seif Apata Pigo Mahakamani.....Akwama Kuzuia Ruzuku kwa Profesa Lipumba

$
0
0
Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kmepata pigo jingine kufuatia Mahakama Kuu nchini Tanzania kutupilia mbali pingamizi lao kutaka Profesa Ibrahim Lipumba asipewe ruzuku za chama hicho.

Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo  jana tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya msingi ya madai kuhusu wizi wa ruzuku na shauri dogo la kuweka zuio kutolewa kwa ruzuku ya chama kutokana na wizi wa shilingi milioni 369 ambazo zilidaiwa kuibwa na Lipumba na kundi lake kwa kushirikiana na Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Pingamizi hilo limedumu kwa miezi minne kutoka Machi mwaka huu mpaka Agosti ambapo jana Mahakama Kuu imetupilia mbali zuio hilo lililowekwa na CUF upande wa Katibu Mkuu, hali ambayo inapelekea Msajili wa Vyama vya Siasa kuendelea kutoa ruzuku ya Chama hicho kwa Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa. Ibrahi Lipumba na wananchama wake ambao wanamuunga mkono.

Toka mwezi wa Septemba 24, 2016 baada ya Profesa Lipumba kudaiwa kufanya uvamizi wa ofisi za chama cha CUF pale Buguruni kinyume na sheria na taratibu baada ya Kujiuzulu kwa hiari yake na kuiacha ofisi hiyo takribani kwa kipindi cha mwaka mzima ndipo ulipoanza mgogoro kati ya pande mbili, upande unaomuunga mkono Lipumba na upande unaomuunga mkono Maalim Seif jambo ambalo limesababisha madhara mengi ya moja kwa moja ndani ya chama hicho.

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Tutataifisha Mali Za Wanaofanya Biashara Ya Kusafirisha Wahamiaji Haramu Kuja Nchini.

$
0
0
KAMANDA wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna (Pichani Kulia), amesema kuanzia sasa watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji hao  kwani navyo vitataifishwa .

Akizungumzia hatua walizozichukua kwa wahamiaji haramu 72 waliokamatwa mapema wiki hii,kamanda Shanna alisema kushiriki kwenye biashara hiyo ni kosa la kubwa la kijinai.

Amesema wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji fedha na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.

Kamanda Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za wale watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.

Amesema sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini hivyo itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa adhabu zote na kufungwa .

Kamanda Shanna ,alisema taarifa ikifika makwao kuwa wanafungwa na kupewa adhabu kali ndipo wataacha kuingia nchini kwani watajua Tanzania sio mahala pa mchezo wala kukimbilia.

“Hii kuwakamata kuwapiga faini na kuwarudisha kwao ndio maana wanafanya mchezo mchezo kukimbilia huku,ukiwapiga faini wanakwenda wanarudi ni mchezo wa kuigiza”alisema .

Kamanda Shanna alielezea kwamba,Tanzania ina sheria zake endapo sheria zitawabana wahamiaji hao na kukoma kugeuza nchi kuwa lango lao la kupita kwenda nchi jirani ikiwemo Afrika ya kusini.

Hata hivyo ,kamanda huyo alisema wahamiaji waliokamatwa wameshawafikisha ofisi ya uhamiaji mkoani hapo na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Jeshi hilo,linaendelea kudhibiti wahamiaji haramu ili kupungua wimbi kubwa linaloingia kupitia njia za panya mkoani hapo hasa bandari bubu 18 zilizopo Bagamoyo .

Pamoja na hilo,Kamanda Shanna alisema wanafanya oparesheni kusaka wahalifu mbalimbali ,zoezi ambalo ni endelevu.

Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri,Mhe. Abdel Fattah Al Sisi anatarajia kufanya ziara ya Kitaifa wiki Ijayo.

$
0
0
Kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri atafanya Ziara ya Kitaifa nchini Tanzania wiki ijayo. Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi nchini Tanzania tangu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aingie madarakani.

Lengo la ziara hii ni kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili, ziara hii pia itatoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili, ya kikanda na kimataifa.

Mheshimiwa Rais Al Sisi atawasili nchini kupokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mheshimiwa Rais Al Sisi mchana atakuwa na mazungumzo (tete-a-tete) na mwenyeji wake kabla ya kushiriki mazungumzo rasmi (official talks) na baadae jioni Mheshimiwa Rais Al Sisi atahudhuria dhifa ya kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake.

Tanzania na Misri zina mahusiano mazuri ya kidiplomasia ya muda mrefu ambayo yamezidi kuimarika hasa katika miaka ya karibuni. Ushirikiano huu unatokana na misingi ya mahusiano na mashirikiano ya karibu sana kati ya Marehemu Baba wa Taifa na muasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi mashuhuri wa Misri na muasisi wa Jamhuri ya Taifa la Kiarabu ya Misri, Marehemu Gamal Abdel Nasser.

Uhusiano wa nchi hizi mbili umejengwa katika misingi ya ushirikiano na maelewano katika Nyanja za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na kiusalama pamoja na medani za siasa za ushirikiano kimataifa, kutetea haki za binadamu, kuimarisha umoja na maendeleo ya Afrika, ukombozi wa Bara la Afrika na kupinga ukoloni, dhuluma na aina zote za ukandamamizaji duniani. Uhusiano huu umejengwa katika Nyanja zote za uhusiano katika sekta za huduma za kijamii na kiuchumi zikiwemo elimu, afya, kilimo, mawasiliano, usafiri, ulinzi na usalama na ushirikiano wa kimataifa.

Misri ni nchi ya pili yenye uchumi mkubwa Barani Afrika. Takwimu za mwaka 2016, zinaonesha kwamba pato la taifa (GDP) la Misri lilikuwa Dola za Kimarekani Billioni 266.213. Sekta kubwa kabisa katika uchumi wa Misri ni sekta ya huduma ( huduma za benki, mawasiliano, usafirishaji na utalii) ambayo inachangia takribani asilimia 52.5 kwenye GDP. Viwanda (manufacturing) inachangia asilimia 36.3, na kilimo asilimia 11.2.

Tanzania na Misri zinashirikiana katika ngazi za taasisi za serikali ambazo ni Taasisi ya Udhibiti wa utawala ya Misri (Administration Control Authority of Egypt) ambayo inashirikiana na Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa ya Tanzania (TAKUKURU), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja zimesaini makubaliano ya Ushirikiano na Hospitali ya El Shatby ya Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kina mashirikiano ya kubadilishana wataalamu na usimamizi wa pamoja wa Shahada za juu za uzamili na uzamivu na Chuo Kikuu cha Azhar cha Misri, Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupitia SUMA JKT wamesaini Makubaliano ya Ushirikiano na Kampuni ya Polyserve ya Misri .

Aidha, kutokana na takwimu za kituo cha Uwekezaji (TIC) kimesajili jumla ya miradi nane kati ya mwaka 1990 hadi 2017, miradi hii ina jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani 887.02 na kutoa ajira zipatazo 953, uwekezaji huo ni katika maeneo ya Kilimo, viwanda(mbao, mbolea, madini, dhahabu na shaba) na sekta ya Huduma.

Hivyo ziara hii ina umuhimu mkubwa sana hasa katika wakati huu ambapo msisitizo wa Serikali ni katika kujenga uchumi wa viwanda.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
11 Agosti, 2017.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images