Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yasema Bado Inamtambua Maalim Seif Kama Katibu Mkuu wa CUF

$
0
0
Na Margareth Chambiri, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha Wananchi (CUF) kumaliza mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho kwani unaweza kusababisha kupoteza nafasi za Udiwani katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika wakato wowote kuanzia sasa.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani katika mahojiano maalum Ofisini kwake kuhusu tuhuma  mbalimbali zilizoelekezwa Tume hiyo ikiwemo suala la Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum kupitia CUF.

Bw. Kailima amesema mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) hauna tija, hivyo ameshauri pande mbili zinazovutana kukutana na kumaliza tofauti zao kwani hali hiyo itawanyima nafasi ya kutoa wagombea kwenye uchaguzi huo mdogo.

“Mimi niwashauri, CUF wana mgogoro wao wamalize mgogoro wao. Ni vizuri wakutane wamalize mgogoro wao kwani hii inaweza kuwaletea matatizo wagombea wakati wa Uchaguzi.’ alisesema Kailima na kusisitiza kuwa mgogoro ndani ya chama hicho hauna tija na badala yake unakidhoofisha.

Amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, inakitaka Chama cha Siasa kumsimamisha Mgombea mmoja kwa nafasi moja, lakini pia mgombea wa nafasi ya Rais na Mbunge  lazima fomu yake isainiwe na Viongozi wa ngazi ya Taifa wanaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

"Lakini ukisoma Maelekezo ya Vyama vya Siasa na Wagombea yanasema iwapo chama cha Siasa kina mgogoro ni lazima fomu zake zisainiwa na kiongozi wa juu wa ngazi ya Mkoa, sasa kwa hali hii iwapo CUF wasipokutana watapoteza nafasi." Amesema Mkurugenzi huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Bwana Kailima amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatambua taarifa za Vyama vya Siasa iliyowasilishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa Chama cha CUF viongozi wanaotambuliwa na Tume hadi hivi sasa ni Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu ni Maalim Seif Sharif Hamad.

"Tume inatambua kuwa Mwenyekiti wa CUF ni Prof. Ibrahim Lipumba, Inatambua Katibu Mkuu wa CUF ni Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Mkuu upande wa Bara ni Magdalena Sakaya" amesema.

Amesema Tume haijazuiliwa na Mahakama wala na Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba isifanye mawasiliano na Viongozi hawa, na kubainisha kuwa Tume itaendelea kufanya mawasiliano na Viongozi mpaka hapo itakavyoelekezwa vinginevyo na Msajili wa Vyama au Mahakama.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amesema Tume inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na kwamba mawasiliano ya Tume na Chama cha Siasa ni kwa mujibu wa maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye anayesajili Vyama vya Siasa nchini.

Aidha katika hatua nyingine Bwana Kailima ameelezwa kusikitishwa na taarifa za upotoshaji zinazoihusisha Tume kwenye kikao cha Wanasheria kwa lengo la kumshauri Spika wa Bunge kuhusu Chama cha Wananchi CUF na kubainisha kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Akielezea hatua zinazoweza kuchukuliwa na Tume dhidi ya upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya Wanasiasa na Vyombo vya Habari kuhusu utendaji kazi wa Tume Kailima amesema Tume itatumia Mamlaka zinazohusika na usajili ingawa hata hivyo amesisitiza kuwa ni vyema Vyama vya Siasa vitumie Wanasheria wao kusoma Sheria na taratibu za Uchaguzi ili kupata habari sahihi.

"Hatua ya kwanza tunayochukua ni hii ya kuelimisha Chama pengine ni bahati mbaya lakini hatua ya pili ni ya kuzitaarifu mamlaka Kwa upande wa Vyama ni Msajili wa Vyama kwa upande wa Vyombo vya Habari vya Magazeti tunamtaarifu Msajili wa Magazeti ili ashughulike nao’ lakini kubwa tunawashauri jamani someni au ulizeni Tume," amesema Kailima.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya August 1

Je, Una Tatizo La Nguvu Za Kiume, Kukosa Hamu Ya Tendo, Kushindwa Kurudia Tendo Au Maumbile Madogo Ya Uume? Soma Hapa

$
0
0
JE, UNA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME? SOMA HAPA 👇👇👇👇

Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, sio Tanzania tu bali duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo sio ugonjwa ila ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili.

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME HUSABABISHA MAMBO KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
      @natural beauty pro. Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye kisukari kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @220,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 7.5 @140,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @140,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kurudia tendo hata mara 3 bila kuchoka @130,000/=
5.DISCREET.Ni dawa ya kuondoa mvi milele na zisiludi tena @130,000/=
 
    KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
       @natural2162
       @natural2162
       @natural2162
   Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa no (+255)
0759029968 na 0659618585
 
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. 
 
      Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na hazina kemikali wala madhara kwa mtumiaji. Zimethibitishwa kiafya.

                          < WELCOME ALL>

Tanzania na Uganda kushirikiana kupeleka umeme vijiji vya mpakani

$
0
0
Na Veronica Simba, Kagera
 Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano ya Awali (MoU) wa kupeleka umeme kwenye Vijiji vya Mpakani mwa nchi hizo.

Hati ya Makubaliano hayo ilisainiwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akiwakilisha Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Dk. Simon D’Ujanga, wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa nchi hizo kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya mpakani, uliofanyika mjini Bukoba, wilayani Kagera.

Makubaliano ya msingi katika Hati iliyosainiwa ni utekelezaji wa Mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vya Nangoma, katika eneo lililopo mpakani mwa Tanzania na Uganda na vijiji vingine vya maeneo hayo kwa kutokea upande wa Tanzania.

Akifafanua zaidi kuhusu makubaliano husika, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, ambaye pia alishiriki Mkutano huo mkubwa, alisema kuwa Wakala wa Nishati Vijijini kwa upande wa Tanzania (REA-Tanzania) utahusika katika kugharamia ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 kufikisha umeme katika eneo la mpakani, umbali wa kilomita 0.8 kwa gharama ya Dola za Marekani 36,923.05.

Aidha, aliongeza kuwa, kwa upande wa Uganda, Wakala wa Nishati Vijijini wa nchi hiyo (REA-Uganda) utahusika kugharamia ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 umbali wa kilomita 7.5 kutoka eneo la mpakani hadi katika vijiji vya Bukwali Gamuli, Bushungulu, Nangoma, Omurushenye, Mizinda na Lukunyu kwa gharama ya Dola za Marekani 724,239.06.

Alieleza kuwa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), litakuwa na jukumu la kuuza umeme kulingana na Mkataba wa kusambaza umeme utakaosainiwa kati yake na Shirika la Umeme la Uganda.

Vilevile, alisema kuwa, REA-Tanzania itashiriki katika kusaidia upatikanaji wa Mkandarasi atakayehusika na ujenzi wa Mradi kwa upande wa Uganda.

Katika Mkutano huo pia, masuala mengine ya ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, katika sekta ya nishati yalijadiliwa ambapo ilielezwa kuwa, mwaka 2014, Serikali hizo mbili zilisaini makubaliano (Bilateral Agreement) kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kuzalisha umeme wa Murongo-Kikagati wa Megawati 14 kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Mradi mwingine wa ushirikiano katika sekta ya nishati, uliojadiliwa katika Mkutano huo ni wa kuzalisha umeme wa Nsongezi wa Megawati 35, ambapo ilielezwa kuwa, Serikali za Tanzania na Uganda zina nia ya kutekeleza Mradi huo kwa kutumia chanzo cha maji ya Mto Kagera ambao upo mpakani mwa nchi hizo.

Wataalam wamependekeza kuwa, hatua muhimu za utekelezaji wa miradi kama vile kufanya Upembuzi yakinifu wa Mradi, upatikanaji wa Mshauri Mwelekezi na Mwendelezaji wa Mradi, zifanyike kwa Ubia, chini ya uongozi wa Serikali ya Tanzania na Uganda.

Masuala mengine ya ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Uganda katika maeneo ya Mpakani, yaliyojadiliwa katika Mkutano huo wa Mawaziri ambao uliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Tanzania) ni kilimo na uvuvi, maji, ardhi pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.

Mkutano wa Mawaziri wa Tanzania na Uganda ulitanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kutoka nchi hizo mbili wanaoshughulika na masuala ya ushirikiano katika maeneo ya Mpaka, uliofanyika Julai 28, mwaka huu mjini Bukoba.


Uhuru Kenyatta: Nipo Tayari Kukabidhi Madaraka Iwapo Nitashindwa

$
0
0
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amesema ikiwa atashindwa kwa haki, Uchaguzi Mkuu wa tarehe nane mwezi Agosti, atakubali matokeo na kukabidhi madaraka kwa amani.

Rais Kenyatta ametoa hakikisho hilo wakati akijibu maswali mbalimbali kupitia runinga na kumtaka mpinzani wake Raila Odinga, naye kuwa tayari kufanya hivyo ikiwa atashindwa katika Uchaguzi huo.

Kenyatta amesisitiza kwamba, yeye ni mtu anayeheshimu uamuzi wa wananchi, na kuwaomba wapinzani wake nao wafanye hivyo.

Aidha, amesema serikali yake imelenga Uchaguzi huo uwe wa amani ndiyo maana maafisa wa usalama wamejihami na wako tayari kukabiliana na wale watakaotaka kuzua fujo.

Naye Bw. Odinga, anayepeperusha bendera ya muungano wa upinzani NASA, amekuwa akisema kuwa atakubali matokeo hayo ikiwa Uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

Hata hivyo, hivi karibuni ametoa madai mazito kuwa Rais Kenyatta anatumia jeshi kumsaidia kuiba kura, madai ambayo serikali imekanusha.

Taarifa ya serikali kuhusu madai ya raia 16 wa Somalia, Pakistan na Lebanon kukamatwa uwanja wa ndege Dar.

$
0
0

Tarehe 31/07/2017 chombo kimoja cha habari kilitoa taarifa za upotoshaji kwamba wageni 16 wenye uraia wa Lebanon, Pakistani na Somalia walinaswa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) baada ya kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP).

Taarifa sahihi za suala hili ni kwamba Tarehe 30107/2017 abiria wanne (4) Raia wa Taifa la Pakistan waliwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa eha Julius Nyerere (JNlA) na kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP Lounge) ambapo nyaraka zao za safari zilikaguliwa na Maafisa wa Uhamiaji na baadae kuruhusiwa kuingia nchini baada ya kujiridhisha kuwa ni halali. 

Abiria hao walikuwa na kibali kinachowaruhusu kutumia ukumbi wa watu mashuhuri (VIP) kilichotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Utaratibu uliopo katika matumizi ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP Lounge) JNIA ni kwamba wageni wote toka nje ya nehi wanaohitaji kutumia ukumbi huo wanalazirnika kuomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Wizara husika inapojiridhisha na vigezo vya waombaji,hutoa vibali hivyo.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inatoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuandika habari kwa weledi na kuhusisha pande zote zinazohusishwa katika taarifa zao mbalimbali, ili kuepuka mkanganyiko na upotoshaji kwa jamii kwa jambo husika.

 TAA ipo tayari kutoa ushirikiano kwa chombo chochote cha  habari kinachowasiliana nacho kutaka ufafanuzi wajambo fulani, iii waweze kuandika kwa umakini na ufasaha zaidi.

 IMETOLEW ANA:

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VY A NDEGE TANZANIA  (TAA)

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Serikali Yajibu Mapigo ya CHADEMA

$
0
0
Wakati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imejipambanua kuongeza vitega uchumi kama vile ununuzi wa ndege mpya aina ya bombardier, Chadema wameibuka na uchambuzi wa hali ya uchumi na kudai hali sasa ni tete ukilinganisha na awamu iliyopita.

Jana, Chadema ilitoa tamko la tathmini ya hali ya uchumi nchini baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kukutana kwa dharura kwa siku mbili mfululizo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema tamko hilo limejikita katika ripoti ya hali ya uchumi inayotolewa kila mwezi na Benki Kuu Tanzania (BoT) kama ilivyotolewa Julai 14, 2017.

Alisema Julai 14, BoT ilitoa ripoti ya Juni inayohusu tathmini ya Mei. 

Kwa kuzingatia umuhimu wake, alisema Chadema imefanya uchambuzi wa ripoti hiyo kwa kuangalia hali ya uchumi mpaka kufikia Mei 2017 ikilinganishwa na hali ya uchumi iliyokuwapo Mei 2015 ikiwa ndio mwaka wa mwisho wa Awamu ya Nne ili kuona mwelekeo wa hali ya uchumi na athari zake chanya au hasi kwa mustakabali wa Taifa.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu madai ya Chadema kuhusu kuporomoka kwa uchumi wa Tanzania, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kwamba yuko kijijini na hajui kinachoendelea.

“Mimi nataka nikiongelea kitu niwe ninakifahamu vizuri, hilo suala sijalisikia kwa hiyo siwezi kusema chochote kupitia mtu wa tatu,” alisema Profesa Ndulu akisisitiza kwamba kwa sasa hayupo ofisini.

Lakini, Mbowe ambaye aliambatana na viongozi waandamizi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa alisema uchumi hupimwa kwa vigezo vingi na umuhimu wa vigezo husika huwa na maana kutegemeana na namna vinavyoathiri maisha ya wananchi. Katika uchambuzi wao, waliangalia vigezo vichache ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja kwenye maisha ya wananchi.

Mbowe alisema kwa kipindi cha Mei, 2015 kiasi cha akiba ya chakula kwenye Ghala la Taifa (NFRA) kilifikia tani 406,846 ukilinganisha na akiba ya tani 74,826 ilipofika Mei 2017, sawa na asilimia 18.3 tu ya kiasi cha chakula katika kipindi kama hicho mwaka 2015.

“Bei za jumla kwa vyakula muhimu kama mahindi, Mei 2015 ilikuwa Sh47,163 kwa gunia wakati mwaka huu mwezi kama huo ilifikia Sh90,149.9 sawa na ongezeko la bei kwa asilimia 92 wakati mchele gunia mwaka 2015 ilikuwa Sh162,701 na mwaka huu mwezi kama huo ilifika Sh176,330,” alisema Mbowe.

Mwanasiasa huyo aliongeza kuwa mazao mengine yote ya chakula ikiwamo maharage, viazi na sukari nayo yamepanda bei kwa wastani wa asilimia kati ya 40 na 60 kutegemea na msimu.

Mbowe alisema kuwa sekta hiyo imekua kwa asilimia 1.7 pekee mwaka 2016/17, kiwango ambacho ni cha chini kupata kutokea kwa zaidi ya miongo mitatu.

“Wakati mataifa yote duniani yanasaidia wakulima kuongeza tija katika kilimo kwa kuwasaidia ruzuku ya mbolea, Tanzania ambayo asilimia 75 wanategemea kilimo mwaka 2015 ilikuwa Sh78 bilioni wakati mwaka 2016/17 ruzuku hii ilikuwa Sh10 bilioni tu,” alisisitiza Mbowe.

Alisema kwa upande wa tume ya maji iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria 2015 kwa lengo la kuhakikisha wanaongeza kilimo cha umwagiliaji katika bajeti ya mwaka 2016/17, ilipata Sh 0 (sifuri) katika bajeti yake ya maendeleo.

Mwenyeiti huyo ambaye aliwahi kugombea urais kwa tiketi ya chama chake na kushindwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema wakati bei zikiwa juu sasa kuliko mwaka 2015 kabla ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, hali ya ujazo wa fedha imekua kinyume chake na hivyo kuathiri biashara, uzalishaji, thamani ya mali kama ardhi huku ujazo wa fedha katika dhana pana kwa mwaka kwenye uchumi uliongezeka kwa asilimia 15 Mei 2015 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 5.2 Mei mwaka huu.

Alisema kwa upande wa mzunguko wa fedha kwa maana ya kiasi cha fedha katika matumizi kwa mwaka, inaonyesha Mei 2015 kiliongezeka kwa asilimia 15.2 wakati 2017 kilikuwa na ongezeko hasi kwa asilimia tatu.

“Hiki ni kielelezo cha usimamizi hafifu wa uchumi na ndio msingi wa ukata unaoendelea nchini.”

Alisema athari za kushuka kwa ujazo wa fedha na mzunguko wa fedha kwenye uchumi katika vipindi hivyo tofauti wakati kiasi cha mfumuko wa bei kikiwa na tofauti ndogo, kwa maana kutoka asilimia tano mwaka 2015 mpaka asilimia sita 2017 ni pamoja na fedha kuwa vigumu kupatikana japo inashuka thamani.

“ Ndio maana pamoja na mwaka 2017 fedha kuwa ngumu kuliko mwaka 2015 kwa mujibu wa takwimu hizi za BoT, lakini thamani ya bei ya chakula kama mahindi na maharage vimepanda karibu mara mbili kwa ulinganisho wa miaka hiyo miwili,” alisisitiza.

Mwenyekiti huyo alisema pia kuwa gharama ya uzalishaji kwa sehemu kubwa inabaki kuwa juu kwa sababu bidhaa za mtaji na mashine sehemu kubwa zinanunuliwa nje na hivyo bei yake haiamuliwi na hali ya ndani kwa sababu wateja kipato kimeshuka, soko la bidhaa zinazozalishwa hushuka na kusababisha mdororo wa biashara.

Alisema kwa sababu ya mdororo wa biashara, wafanyabiashara wanashindwa kulipa mikopo na hivyo kuongeza presha kwenye kasi ya mikopo isiyolipika (non performing loans -NPL).

Alisema mpaka sasa kwa mujibu wa ripoti mbalimbali mikopo isiyolipika imeongezeka kutoka chini ya asilimia tano mwaka 2015 mpaka asilimia zaidi ya nane mwaka 2017 jambo alilodai kuwa linapunguza imani ya benki za biashara kukopesha sekta binafsi.

Alisema ukata huo unasababisha kushuka kwa thamani ya mali kama ardhi, nyumba au mashine na mitambo iliyowekwa dhamana benki kwa ajili ya kupata mikopo kwa sababu uwezo wa watu kununua umeshuka.

“Ndiyo sababu viwanja ambavyo viliuzwa Sh100 milioni sasa ukitangaza bei ya Sh50 milioni hupati mteja, gari au mashine ambayo mwaka 2015 ungeuza kwa Sh50 milioni leo huwezi kupata nusu yake kwa sababu ya ukata.”

Alisema pia uwezo wa Serikali na watu kujitegemea unapungua kwa sababu wigo wa makusanyo unapungua kutokana na biashara nyingi na ajira kupotea.

“Kwa sababu hiyo, maamuzi ya kisera na kisheria ya kushinikiza kampuni za simu zilizoorodheshwa soko la mitaji (DSE) yamekuwa na mafanikio hafifu hata kuhitajika kubadilisha sheria kwa sababu sera mbovu za kiuchumi zimepunguza uwezo wa Watanzania kutumia fursa hizo kuwekeza. Ndio sababu majuzi kampuni ya Vodacom imejaribu kuongeza muda kuwa ipo pamoja na sasa kuruhusu wasio wazawa kununua hisa hizo,” alisema mbunge huyo wa Jimbo la Hai.

Serikali Yajibu Mapigo
Akizungumzia tuhuma za Chadema kuhusu hali ya uchumi, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alihoji tuhuma hizo kwamba haziendani na hali halisi ipi wakati wanafunzi wanasoma bure hadi kidato cha nne?

Dk Abbas aliwashangaa Chadema kwa kusema;“hawaoni miradi mikubwa ya ujenzi inayoendelea kama vile barabara, mradi wa umeme wa Kinyerezi II Dar es Salaam, flyover ya Tazara na ununuzi wa ndege.

“Serikali inaajiri wafanyakazi wapya; inalipa mishahara kwa wakati; miradi ya maji inaendelea nchi nzima ikiwemo mikubwa ya kutoa maji Ziwa Victoria,” alifafanua Dk Abbas.

Alisema Serikali imeongeza makusanyo ya mapato na imeongeza bajeti katika huduma za jamii, kama vile afya hasa kwenye ununuzi wa dawa. Na kwamba hata wabunge wa Chadema wakiwa bungeni wanalipwa posho zao kama kawaida.

“Wanataka uhalisia upi zaidi ya ushahidi huu kuwa uchumi wa nchi unafaidisha wananchi kupitia huduma hizo?" alihoji Dk Abbas .

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole yeye alisema chama chake hakina muda wa kulumbana na kwamba sasa wana kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.

“Sisi tuna mkataba na wananchi wa Tanzania kuhakikisha tunawaletea maendeleo, kwa sasa tupo ‘busy’ kufanya kazi hiyo, kiukweli hatuna muda wa kufanya malumbano yasiyo na tija, tunachojua ni kazi kubwa iliyopo mbele yetu ambayo tumesaini mkataba mpaka mwaka 2020.”

“Hatuna muda wa kuhangaika na watu wasio na dhamira njema, tunaendelea na kazi na matunda yake yatawanufaisha wananchi wa kawaida kabisa ambao ni wakulima, wafanyabiashara na wafanyakazi. Sisi hatuna muda wa kupoteza,”alisisitiza Polepole

Serikali yawaonya waajiri kuhusu wafanyakazi wanaonyonyesha

$
0
0
Serikali imeonya waajiri wanaoweka vikwazo kwa wafanyakazi wao wanaonyonyesha watoto walio chini ya miezi sita.

Onyo hilo limetolewa leo Jumanne na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati anafungua maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.

"Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora, imeweka kanuni inayompa nafasi ya saa mbili mama mwenye mtoto wa chini ya miezi sita kumnyonyesha mwanaye," amesema Waziri Mwalimu.

Amesema kutokana na kanuni hiyo, waajiri wanapaswa kuwapa ushirikiano mzuri akina mama hao, kwa kuwa maziwa ya mama ndiyo msingi wa afya bora ya mtoto.

Waziri Mwalimu amebainisha kuwa ili mtoto aweze kuwa na afya bora, anapaswa kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita mfululizo bila kinywaji au chakula kingine chochote.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Chakula na Lishe, Dk Joycline Kaganda, amesema maadhimisho haya hufanywa kila mwaka kuanzia Agosti 1 hadi 7.

"Maadhimisho haya yanalenga kusisitiza umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama," amesema

Katika maadhimisho hayo, programu ya huduma ya taarifa za lishe kupitia simu za mkononi (M-Nutrition) imezinduliwa. Progrtamu hiyo inakusudia kuleta mabadiliko ya tabia kuhusu afya na lishe ya watoto, wanawake wajawazito  na wanyonyeshao.

TFF yafanya mabadiliko ya kanuni za ligi kuwabana wachezaji wa kigeni

$
0
0
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana Jumapili Julai 30, 2017 katika Ukumbi wa Hosteli za TFF, zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam yaliko Makao Makuu ya shirikisho.

Kikao hicho, kimepitisha mambo mbalimbali ambako miongoni mwake ni mabadiliko ya Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Miongoni mwa kanuni ziliguswa ni ya kuhusiana na kujali afya za wachezaji pamoja na mikataba wanayoingia na klabu.

Hivyo, TFF imeagiza msimu wa 2017/18 mchezaji atayesajiliwa hatapewa leseni ya kumruhusu kucheza mashindano husika kama vile Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL), Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kama hatakamilisha masharti makuu matatu kwa mujibu wa kanuni.

Masharti hayo ni kukatiwa Bima ya Matibabu, Kuidhinishwa afya yake ambayo mara baada ya fomu yake kupitishwa na Kamati ya Tiba ya TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 18 (1) ya Ligi Kuu na Mkataba wake wa maandishi ‘hardcopy’ kuwasilisha TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 69 (8) ya Ligi Kuu.

Kama kuna timu haitakidhi japo sharti moja kati ya hayo, basi mchezaji wake hatapewa leseni ya kucheza kwa msimu husika. Kaimu Rais wa TFF, Wallace Karia, akifunga hoja hiyo, alisisitiza akisema: “Wakati huu hatutaki siasa. Tusimamie kanuni hizi, hatutaki kuleta mchezo msimu huu.”

Hayo yamekuja baada ya klabu kutakiwa kuwawekea Bima ya Matibabu kwa mujibu wa kanuni ya 18 (1) inayosema: “Kila Klabu ina wajibu wa kuwawekea wachezaji wake bima ya matibabu na fidia kutokana na ajali michezoni. Klabu itakayokiuka kanuni hii itakuwa imepoteza sifa ya kuwa klabu ya Ligi Kuu, na usajili wa wachezaji wa timu yake hautathibitishwa na haitashirikishwa katika Ligi Kuu.

Kuhusu Mikataba kwa mujibu wa Kanuni ya 69 (8), Kamati ya Utendaji imekubaliana kwamba: “Mikataba yote ya wachezaji ambao haujasajiliwa na kuthibitishwa na TFF, hautatambuliwa.”

Kadhalika, kuhusu wachezaji wa Kigeni kwa mujibu wa Kanuni ya 57 (5), kitasomeka kama ifuatavyo: “Mchezaji ye yote wa kigeni anayesajiliwa katika Ligi Kuu atalipiwa ada maalumu ya Sh milioni mbili (Sh 2,000,000) kwa msimu kwa mchezaji mmoja ili usajili wake uweze kuthibitishwa na kuruhusiwa kucheza.

Gharama za awali zilikuwa ni dola 2,000 za Marekani (sawa na Sh. 4.5 milioni.) kwa mchezaji mmoja.

Kadhalika, sasa kwa mujibu wa kanuni ya 13 (6) Klabu Mwenyeji itakuwa na nafasi ya kuweka mpaka mabango 10 ya Mdhamini/Wadhamini wake. Ukubwa wa bango moja lile lenye vipimo vya 6m x 1m.

Kama timu ni mgeni katika mchezo husika, ana uwezo kufanya makubaliano na mwenyeji wake akampa nafasi katika hayo 10 ambayo yameruhusiwa kikanuni.

Aidha, Kanuni ya 14 imeongezwa kipengele kimoja. Kanuni ya 14 (48) Klabu ina wajibu wa kushirikiana na mdhamini wa matangazo ya televisheni ikiwemo kupata picha za wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao.

Na Kanuni 14 (49), inasema: TFF/TPLB itachukua hatua kwa ukiukwaji wo wote wa taratibu za mchezo kama zilivyoanishwa kwenye Kanuni ya 14 kwa kutoa onyo kali au karipio au kutoza faini kuanzia Sh. 200,000 (lakini mbili) mpaka Sh. 300,000 (laki tatu), na/au kufungia mchezo isiyozidi mitatu (3) au kipindi kisichozidi miezi mitatu (3) kwa mchezaji, kiongozi au timu.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji imeridhishwa na maandalizi ya Mkutano Mkuu ujao wa TFF ambako pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya Uchaguzi Mkuu wa shirikisho unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Mjumbe wa FIFA, Solomon Mudege alikuwa nchini kwa siku ya Jumamosi ambako alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe; Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yussuph Singo pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF wakiongozwa na Kaimu Rais Wallace Karia.

Mara baada ya kupata maelezo ya kuridhisha kutoka kwa wanafamilia hao wa mpira wa miguu ambao baadhi yao alikutaa nao mmoja baada ya mwingine, alibariki mchakato wa uchaguzi uendelee na Kamati ya Utendaji imetangaza kuwa utafanyika Ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma.

Mudege alikuwa nchini kuangalia hali maendeleo ya mpira wa miguu nchini hasa katika utawala, lakini kwa kuwa uongozi uliokaimu madaraka umefuata taratibu, kanuni na sheria tangu mwanzo, mjumbe huyo aliridhia mchakato wa uchaguzi na shughuli nyingine ziendelee kama zilivyopangwa.

MATOKEO YA MWISHO USAILI TAFCA, KAMPENI ZAANZA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametangaza orodha ya majina sita ya mwisho ya wagombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Kwa mujibu Mambosasa, wagombea hao kwa sasa hawana budi kuendelea na kampeni hadi Agosti 9, mwaka huu ambako uchaguzi huo umepangwa kufanyika kufanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.

Waliopitishwa katika orodha ya mwisho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi – ngazi ya taifa ni pamoja na Kidao Wilfred, Lister Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Maka Mwalwasi na Mohammed Tajdin.

Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

jAJI wARIOBA: Viongozi Tumsaidie Rais Kutatua Kero

$
0
0
Na Judith Mhina – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, anahitaji kupata usaidizi wa kutosha kutoka kwa viongozi na hasa wasaidizi  kuanzia ngazi ya nyumba kumi hadi taifa.

Maneno hayo yametamkwa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba alipofanya mahojiano na Idara ya Habari – MAELEZO - ofisini kwake Oysterbay Jijini Dar-es-Salaam.

Jaji Warioba ameona kuna udhaifu mkubwa wa kiutendaji ambapo wananchi hawatoi changamoto zinazowakabili mpaka wamuone Rais amefika katika eneo lao, au wanaeleza changamoto zinazowakabili kwa viongozi husika ila, viongozi hawazifanyii kazi, ambapo wananchi wanaamua kuziwasilisha kwa Rais mara wanapomuona.

 “Rais hawezi kufanya kazi peke yake naomba tuimarishe utendaji wetu wa kazi, kama utendaji ungekuwa mzuri suala la makontena kufika hadi bandarini lisingekuwepo, na hata kugundulika kwake kusingefanywa na Rais,” amesema Jaji Warioba.

“Nampongeza sana Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na  Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa, kwa utendaji wao wa kazi. Viongozi hawa ni wasikivu na wanatekeleza kazi zao bila mihemko kwa kutoa maagizo na maelekezo kwa wahusika ili wayatekeleze”, aliongeza  Mhe. Warioba.

Wema Sepetu ashindwa kupokea kadi CHADEMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi rasmi kadi ya chama hicho aliyekuwa mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.

Tukio hilo lilipangwa kuhitimisha tangazo la wema miezi kadhaa iliyopita kujiondoa Chama cha Mapinduzi(CCM) na akijiunga na Chadema.

Akizungumza na waandishi leo wakati akitangaza kuahirisha mkutano huo, Sumaye, ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu katika awamu ya Tatu, alisema tukio hilo limeahirishwa kwa sababu Wema ameshindwa kufika kutokana na kubanwa na ratiba za Mahakama.

"Hadi sasa Wema yuko ndani ya ukumbi wa mahakama  akisubiri kesi yake inayomkabili, mawakili walitueleza kesi ingemalizika asubuhi na saa 6:00 mchana tungefanya moutano huu,” alifafanua Sumaye.

Wema anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo.

Sumaye aliyekuwa amengozana na Mwenyekiti  wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee na Makongoro Mahanga, alisema Wema angekabidhiwa kadi na kuzungumza sababu za kujiunga Chadema.

Waandishi wa habari walifika ofisi za kanda hiyo kuanzia saa 5:00 asubuhi lakini ilipofika saa 6:00 mchana waandaji wa mkutano huo waliomba kusogeza mbele muda.

Rais Magufuli amuapisha Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mhe. Benedict Martin Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi

Mhe Benedict Martin Mashiba amechukua nafasi ya Mhe. Victoria Richard Mwakasege ambaye amestaafu nafasi hiyo, mbali na hilo Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho wa Mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mbali na hilo Rais Magufuli amewapongeza mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na kuwaomba mabalozi hao kutilia mkazo diplomasia ya Uchumi kwa kuongeza juhudi za kuhamasisha wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na Tanzania katika biashara na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ujenzi wa viwanda, Kilimo na huduma za jamii.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni
1.Mhe. Nguyen Kim Doahn – Balozi wa Vietnam hapa nchini.

2.Mhe. Prof. Ratlan Pardede – Balozi wa Indonesia hapa nchini.

3.Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski–Balozi wa Vatican hapa nchini.

4.Mhe. Dkt. Detlef Wachter – Balozi wa Ujerumani hapa nchini.

5.Mhe. Richard Tumisiime Kabonero – Balozi wa Uganda hapa nchini.

Unasumbuliwa na Kiharusi,Ngiri au Kifafa?......Unatatizo la Nguvu za Kiume, Kuachika au Tatizo la Uzazi? . Kutana na Mtalaamu Huyu Akusaidie

$
0
0
SASA YUPO DAR; Anauwezo wa kutabiri nyota yako na kukuletea mafanikio makubwa katia biashara yako, kazini na malengo yako ya maisha.Pia anatoa pete ya bahati yenye uwezo wa kukuletea mafanikio makubwa na kutimiza ndoto zako.

Je, Umedhurumiwa? unamdai na hakulipi?...Njoo upatiwe dawa ulipwe haraka. Anadawa ya kumvuta mpenzi wako popote alipo kwa masaa 6 tu na kumtuliza asitoke kwako

Je, unaugomvi usioisha na mpenzi wako na unaachwa mara kwa mara? Njoo upate dawa ufurahie penzi tulivu la umpendae.

Anadawa za nguvu za kiume, kuimarisha mishipa iliyolegea, kuongeza homoni na kukufanya udumu katika tendo hadi dakika 45 na unaweza kurudia tendo hata mara 4 bila kuchoka.

Anatibu Busha bila kupasua,uzazi, mshipa wa ngiri,kiharusi,kifafa,kuondoa majini machafu nakadhalika.

Mpigie kwa simu: 0755505099

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Habari Zilizopo Katika Mahazeti ya Leo Jumatano ya August 2

Waziri Mkuu Atembelea Mtambo Wa Kusafisha Dhahabu Chunya

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea na kujionea mtambo wa kisasa wa kusafisha dhahabu kwa asilimia 99 unaomilikiwa na kampuni ya Sunshine Group uliopo katika kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Ametembelea mtambo huo  jana (Jumanne, Agosti 1, 2017) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya na kusema kuwa mtambo huo ni wa kwanza kuweza kusafisha dhahabu kwa kiwango hicho hapa nchini.

Alisema kwa Tanzania kampuni ya Sunshine Group ndiyo yenye mtambo wa kuweza kusafisha dhahabu na kufikia asilimia 99 ukilinganisha na makampuni mengine yanayomiliki migodi.

Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza kusafirisha dhahabu halisi.

Naye Ofisa Madini Mkoa wa Mbeya, Mhadisi Said Makwama alisema dhahabu inayosafishwa katika mtambo huo ikipelekwa nje ya nchi inaingizwa sokoni moja kwa moja tofauti na migodi mingine.

Mhandisi huyo alisema Sheria mpya ya Madini imesaidia Serikali kupata kodi ya juu itokanayo na Mrabaha wa asilimia 6 na ‘clearance and inspection fee’ ya asilimia moja ya thamani ya madini yanayosafirishwa ukilinganisha na mrabaha wa awali wa asilimia nne.

“Uzalishaji uliofanyika kwa mwezi Julai tu Serikali imepata mrabaha wa sh. milioni 333 ukilinganisha na sheria ya zamani Serikali ingepata shilingi milioni 191. Sheria mpya imewezesha Serikali kupata mapato zaidi ya sh. milioni 142. Awali ilikuwa inapata sh. milioni 191 kwa gramu 52. 518 kwa mgodi mmoja wa Sunshine.”

Kwa upande wake mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Victor Mwambalaswa ameiomba Serikali kukubali maombi ya Kampuni ya Sunshine ya kujenga mtambo wa kuchenjulia mabaki ya mchanga wa dhahabu wilayani Chunya ili kuweza kuongeza fursa za ajira, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Bw Leo Le alisema kampuni ya Sunshine Group ni ni miongoni mwa makampuni makubwa kutoka nchini China yaliyowekeza Tanzania, ambapo thamani ya uwekezaji wao ni zaidi ya Dola za Marekani milioni 100.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 1, 2017

Watanzania Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mradi wa Bomba la Mafuta

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma katika mahojiano maalum kuhusu uzinduzi wa mradi wa wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu yaliyofanyika mapema Julai 31, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

*********

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amewataka wananchi wanaoishi katika mikoa itakayopitiwa na miundombinu ya bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

Dkt. Pallangyo aliyasema hayo Jumatatu  jijini Dar es Salaam kupitia kipindi maalum cha 360 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds wakati akielezea maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu.

Alisema kuwa wananchi katika maeneo husika wanatakiwa kujiandaa kwa ajira wakati wa maandalizi na utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za vyakula, usafiri na ufundi.

“Fursa zitakazokuwepo ni nyingi mno, vijana waliomaliza Vyuo vya Ufundi wataweza kufanya kazi za uchomeleaji wa vyuma, madereva wenye leseni kupata kazi, wakina mama lishe kuuza vyakula, wakulima kuuza mazao kwa walaji watakaoongezeka kutokana na uwepo wa mradi huo, alisema Dkt. Pallangyo.

Akielezea manufaa ya mradi huo, Dkt. Pallangyo alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaleta mabadiliko ya kiuchumi katika nchi za Uganda na Tanzania.Alisisitiza kuwa mradi utatoa takribani ajira 10,000 na kufungua fursa za biashara katika mikoa itakayopitiwa na mradi

“Mradi utapelekea kufunguka kwa Ukanda wa Biashara kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Rwanda, Burundi, Kongo, Sudan ambapo wanaweza kuunganishwa na miundombinu hiyo na kusafirisha mafuta kwa urahisi,” alisisitiza Dkt. Pallangyo.

Aliendelea kusema kuwa, kukamilika kwa mradi huo nchi za Tanzania na Uganda zitapata mapato na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wake.

Dkt. Pallangyo alieleza faida nyingine kuwa ni pamoja na gharama za mafuta kupungua kutokana na nchi za Afrika Mashariki kutumia mafuta yake yenyewe kwenye magari pamoja na ndege hivyo kuchochea kasi ya utalii katika nchi husika pamoja na ajira.

Awali akielezea mradi huo, Dkt. Pallangyo alisema kuwa mradi ulikuwa na ushindani mkubwa hata hivyo bado ilionekana Tanzania kuwa na vigezo vya bomba hilo kupita katika sehemu kubwa ya ardhi yake ambapo alieleza vigezo hivyo kuwa ni pamoja na hali ya tambarare katika ardhi ya Tanzania hivyo gharama za uwekezaji kuwa rahisi.

Aliongeza kuwa ardhi ya Tanzania ni rahisi pamoja na kuwepo kwa hifadhi ya barabara katika maeneo mengi hali inayopelekea gharama za fidia kuwa ndogo.

Dkt. Pallangyo alieleza vigezo vingine kuwa ni pamoja na Tanzania kuwa na uzoefu mkubwa katika usimamizi wa bomba la Mafuta la TAZAMA na la Gesi linalotoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam.

“Pia bandari ya Tanga imeonekana inafaa kwa kuwa itawezesha mafuta kusafirishwa kwa mwaka mzima bila tatizo lolote,” alisema Dkt. Pallangyo.

Afariki Kanisani Baada ya Kutoa Sadaka

$
0
0
Mkazi  wa Mtaa wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Beatrice Kangu (48) amekufa muda mfupi baada ya kutoa sadaka katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda kilichopo katika Mtaa wa Makanyagio B.

Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa kigango hicho, Charles Kanyanda alisema Kangu ambaye ni mwanakwaya, alikuwa muumini wa Kanisa Katoliki, na Jumapili alihudhuria ibada ya Misa Takatifu kwenye kigango hicho ambayo ilifanyika saa moja na nusu asubuhi.

Alisema Beatrice alihudhuria ibada ya misa hiyo ambapo kwa kuwa alikuwa mwanakwaya aliingia kwenye nyumba ya ibada na kujiunga na wanakwaya wenzake iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu wa Dini (Katekista) wa Kigango, Agustino Ntalwila.

“Ibada ya Misa Takatifu iliendelea kama kawaida na ndipo ilipofikia muda wa kutoa sadaka na Beatrice alikwenda kutoa sadaka kama kawaida kisha akarudi kwenye nafasi yake na kuendelea kuimba ghafla baadaye alianguka na kupoteza fahamu.

Taharuki iliibuka kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo ilipobainika kuwa alikuwa amekata roho,” alieleza Kanyanda na kuongeza kuwa wanakwaya wenzake walijitahidi kumpatia huduma ya kwanza bila ya mafanikio.

Kanyanda alisema maziko yake yalifanyika katika makaburi ya Mwanga jana ambayo yaliongozwa na Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Maria Imakulata, Monsinyori, Padri George Kisapa aliyemwelezea alikuwa mcha Mungu na ameacha pigo kubwa kwenye kwaya ya Kigango cha Makanyagio B.

Serikali Yazidi Kujibu Mapigo ya CHADEMA......Yasisitiza Uchumi wa Tanzania ni Imara na Tunaongoza Afrika Mashariki

$
0
0
By Bushiri Matenda-MAELEZO
Licha ya kuyumba kwa uchumi na kuongezeka kwa mfumuko wa bei duniani, Tanzania imeendelea kuongoza kwa ukuaji wa uchumi miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zimetaja uchumi wa Tanzania kuwa imara.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alibainisha hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya uchumi nchini.

“Uchumi wa Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo sasa bado uko katika ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji wa juu katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Rwanda inakua kwa asilimia 6, Uganda asilimia 5 na Kenya asilimia 6.4”, alisema Dkt. Abbasi.

Alieleza kuwa sambamba na ukuaji wa uchumi, Tanzania imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo taarifa ya hivi karibuni zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa mfumuko wa bei nchini umeshuka kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei hadi kufikia asilimia 5.4 mwezi Juni mwaka huu.

Aidha, Mkurugenzi Dkt. Abbasi alieleza kuwa katika eneo la mazingira bora ya uwekezaji, Tanzania imeendelea kufanya vizuri ambapo alitoa takwimu za taasisi ya Quantum Global Research Lab ya Uingereza kuhusu Farihisi ya Uwekezaji Afrika ambazo zilionesha Tanzania ikiongoza miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki na ya nane Barani Afrika, ikiwa imepanda kutoka nafasi ya 19 mwaka 2015.

“Mashirika ya Kimataifa kama IMF, Benki ya Dunia katika ripoti zao za hivi karibuni yamesisitiza kuwa uchumi wa Tanzania ni imara na wamesifu mageuzi makubwa yanayofanywa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli”, alieleza Dkt. Abbasi na kusema kuwa mashirika hayo yameitaka Serikali iendeleze mapambano zaidi dhidi rushwa na udhibiti wa mapato ya Serikali.

Alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kufanyia kazi maoni hayo ya IMF na Benki ya Dunia na kwamba mabadiliko makubwa yamefanyika katika kupambana na rushwa na kudhibiti mapato ya Serikali ambapo ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 925 kwa mwaka 2015 hadi shilingi trilioni 1.069 kwa mwaka 2016/17 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.

Dkt. Abassi ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, alieleza kuwa kutokana na uchumi wa Tanzania kuwa imara kumeiwezesha Serikali kufanya maboresho makubwa katika sekta mbalimali zikiwemo afya, elimu, miundombinu na nishati ambapo katika sekta ya afya Serikali imetenga shilingi trilioni 1.077 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kulinganisha na shilingi bilioni 796 zilizotengwa mwaka fedha 2016/17.

Alieleza kwa kwa upande dawa na vifaa tiba, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutekeleza ahadi yake kwa kuongeza fedha katika ununuzi wa dawa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu fedha za ununuzi wa dawa na vifaa tiba zimeongezea kutoaka shilingi bilioni 30 mwaka 2015/16 mpaka kufikia shilingi bilioni 261 katika bajeti ya mwaka 2017/18.

“Katika kuhakikisha Watanzania wengi wanaelimika, Serikali imeendelea kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ambapo takribani shilingi bilioni 18 hutumika kwa mwezi na zinawafikia walengwa na kwa wakati”, alieleza Dkt. Abbasi na kuongeza kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani kulikuwa na shilingi bilioni 341 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu lakini Rais John Pombe Magufuli akaongeza hadi kufikia shilingi bilioni 475 na kwa mwaka 2016/17 bajeti ya mikopo ya elimu juu iliongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 483.

Alieleza kuwa kutokana na uchumi imara, Tanzania imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo ikiwemo ile ya umeme, maji, reli ya kisasa, barabara na pia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mapka Tanga nchini Tanzania, ambapo mradi huu unatekelezwa kwa pamoja na nchi hizo mbili.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images