Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli: Watanzania Wameteseka Vya Kutosha......Fanyeni kazi usiku na mchana kukamilisha hii barabara

$
0
0
Rais Magufuli ameitaka kampuni ya Nyanza inayoshughulikia ujenzi wa barabara ya mkoani Kigoma kuanza kufanya kazi usiku na mchana kwa kuwa wapo baadhi ya wananchi hawajahi kuona lami maisha yao yote mpaka wanakufa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia wakazi wa Kakonko mkoani Kigoma katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo mpaka Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami.

"Wananchi hawa wanahitaji barabara ya lami wameteseka tangu dunia iumbwe, wako watu hawajui rangi ya lami, wapo watu hapa wamezaliwa, wamezeeka hawajui rangi ya lami ikoje. Kwa sababu hawajawahi kuona barabara ya lami katika maisha yao, kwa hiyo nataka hii lami ianze na mjipange kweli mfanye kazi usiku na mchana", amesema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amewaagiza makandarasi kufanya kazi ipasavyo na wasipofanya hivyo watachukuliwa adhabu kali zidi yao.

"Kwa bahati nzuri mimi kufukuza makandarasi ni kama kunywa chai, sasa asije akanirudisha kule nilipokuwa kwa sababu sasa ni Baba wa wote lakini nilipokuwa Waziri nilikuwa nafukuza tu, kwa kupitia bodi ya makandarasi nilikuwa nafuta wakandarasi na mimi nikuombe Prof. Mbalawa usiwe mpole. Makandarasi watakao kuwa wanafanya kazi hovyo hovyo, pole pole chukua 'action' ili kusudi kama kashindwa kufanya kazi ya ukandarasi akafanye nyingine hata ya kuvua samaki", amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewataka wananchi kibondo na kasuru wa mkoa wa Kigoma na watanzania wote kwa ujumla kudumisha ulinzi na usalama katika maeneo yao wanayoishi ili kupunguza au kumaliza kabisa matatizo ya kihalifu yanayotokea.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Kutana na Wauzaji Maarufu wa Mbao za Jumla Jumla.......Wanapatikana Mafinga Iringa

$
0
0
Tunapenda kuwajulisha wateja wa ununuzi wa mbao Tanzania bara na Visiwani kuwa tunauza mbao kwa ajili ya shughuri za Ujenzi, biashara na shughuli nyinginezo.

Aina ya mbao tulizonazo ni PINES zenye size zifuatazo: 

MBAO FUPI FT: 12
1 X 6 X 12 1 X 8 X 12 1 X 10 X 12 2 X 2 X 12 2 X 3 X 12 2 X 4 X 12 2 X 6 X 12 

MBAO NDEFU FT: 15 - 18:
1 X 8 x 18 1 X 10 X 18 2 X 2 X 18 2 X 3 X 18 2 X 4 X 18 2 X 6 X 18 

Unaweza kufika mjini MAFINGA au ukafanya malipo kupitia BANK na baada ya makubaliano na malipo
kukamilika mzigo utasafirishwa mpaka mahali unapotakiwa kufika. 

Karibu unufaike na huduma zetu bora kabisa kwani tuna uzoefu kwa zaid ya miaka 10 sasa, tunapatikana
mjini Mafinga – Iringa. 
Wasiliana na Mr. ESTHO SANGA
WhatsApp : 0628 165693
Mobile : 0753 935889
Email : estho2007@gmail.com

Polisi waenda kumpekua Tundu Lissu nyumbani kwake

$
0
0
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa Kituo cha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.

Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 22

Katibu wa habari Ikulu ajiuzulu kupinga uamuzi wa Rais Trump

$
0
0
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Shawn Spicer, amejiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kupinga mabadiliko ya Timu ya Mawasiliano ya Ikulu hiyo.

Bw. Spicer ameachia wadhifa huo, kwa sababu hakufurahishwa na uamuzi wa kumteua, Anthony Scaramucci kuwa Mkrugenzi mpya wa Mawasiliano wa Ikulu,

Mabadiliko hayo yanafanyika wakati White House ikikabiliwa na uchunguzi kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka jana.

Gazeti la New York Times linaarifu kwamba, Bw. Spicer alipinga vikali uteuzi wa Bw. Scaramucci kama Mkurugenzi wa Mawasiliano akidai ni kosa kubwa.

Bw. Scaramucci, ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Mike Dubke kujiuzulu Mei mwaka huu.

NHC yaagizwa kujenga nyuma katika maeneo yote mapya ya utawala

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la nyumba Nchini kwenda kujenga nyumba bora za makazi katika maeneo yote mapya ya utawala ikiwemo mikoa na wilaya ili kusaidia kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi.

Pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe zinazojengwa katika kijiji cha Tindingoma, unaojengwa na Shirika la Nyumba Nchini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana  (Ijumaa, Julai 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Naming’ongo wilaya ya Momba akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.

“Nalipongeza Shirika la Nyumba kwa mikakati waliyonayo ndani ya shirika hilo na kwamba waendelee na utekelezaji wa mipango hiyo ya ujenzi wa nyumba ili maeneo yote mapya ya utawala yaweze kuwa na makazi bora ya kuishi watumishi.”

Pia aliwataka wakazi wa kata ya Chitete yaliko makao makuu ya wilaya ya Momba kuhakikisha wanachangamkia fursa ya uwepo wa makao makuu wa wilaya kwenye kata yao kwa kujenga nyumba za kisasa kwa ajili ya kupangisha watumishi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu amesema mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 2.2 ulianza kujengwa Machi 2016 na unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.

Amesema mradi huo ulibuniwa baada kupokea maombi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Momba na kwamba unatekelezwa kwa awamu mbili ya kwanza ni ujenzi nyumba nane na tayari zimekamilika.

Ameongeza kwamba ujenzi wa awamu ya pili unajumuisha nyumba tisa ambapo gharama ya ujenzi wa nyumba itatumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya ofisi za Halmashauri hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHC , Bi. Blandina Nyoni amesema shirika hilo lilianzisha mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwawezesha wananchi kuwa na makazi bora.

Amesema katika miradi 54 ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na shirika hilo katika maeneo mbalimbali nchini kati yake miradi 24 imekamilika ikiwemo 14 ya nyumba za gharama nafuu.

Pia Mbunge wa jimbo la Momba (CHADEMA), David Silinde amesema anashukuru Serikali kwa ujenzi wa nyumba hizo na kumueleza Waziri Mkuu kwamba wananchi wa Momba wanaridhishwa na utendaji wa Serikali na kwamba maendeleo hayana chama.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 21, 2017

TLS yalaani Polisi kumkamata wa Tundu Lissu


Unasumbuliwa na Kiharusi,Ngiri au Kifafa?......Unatatizo la Nguvu za Kiume, Kuachika au Tatizo la Uzazi? . Kutana na Mtalaamu Huyu Akusaidie

$
0
0
SASA YUPO DAR; Anauwezo wa kutabiri nyota yako na kukuletea mafanikio makubwa katia biashara yako, kazini na malengo yako ya maisha.Pia anatoa pete ya bahati yenye uwezo wa kukuletea mafanikio makubwa na kutimiza ndoto zako.

Je, Umedhurumiwa? unamdai na hakulipi?...Njoo upatiwe dawa ulipwe haraka. Anadawa ya kumvuta mpenzi wako popote alipo kwa masaa 6 tu na kumtuliza asitoke kwako

Je, unaugomvi usioisha na mpenzi wako na unaachwa mara kwa mara? Njoo upate dawa ufurahie penzi tulivu la umpendae.

Anadawa za nguvu za kiume, kuimarisha mishipa iliyolegea, kuongeza homoni na kukufanya udumu katika tendo hadi dakika 45 na unaweza kurudia tendo hata mara 4 bila kuchoka.

Anatibu Busha bila kupasua,uzazi, mshipa wa ngiri,kiharusi,kifafa,kuondoa majini machafu nakadhalika.

Mpigie kwa simu: 0755505099

Waziri Lukuvi Aonya Maafisa Ardhi Wasio Waadilifu

$
0
0
Na Hassan Mabuye Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini.

Waziri  Lukuvi  aliyasema  hayo  jana  katika ukumbi wa shule  ya sekondari  Lugalo mjini  Iringa  wakati  wa  Uzinduzi wa Master  Plan ya  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa.

Alisema mchezo huo wa ufisadi ambao umekuwa ukitumiwa  miaka  yote na maofisa ardhi nchini ameubaini na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutokubaliana na ramani za maeneo mapya zinazoletwa na wataalam  hao bila ya wao kufika maeneo husika na kuoneshwa maeneo hayo ili kujiridhisha.

Waziri Lukuvi alifichua kuwa ufisadi unaofanywa na maafisa ardhi nchini kwa kupima viwanja  hewa kwa  ajili ya maslahi yao na kusema kuwa mbinu ambayo  wamekuwa  wakiitumia  kuiibia  serikali amekwisha  ibaini na  hata kubali  kuona mbinu  hiyo inapewa nafasi katika serikali  hii ya awamu ya  tano chini ya  Rais Dkt John Pombe Magufuli .

Maafisa ardhi wakishirikiana na maafisa mipango miji pamoja na wapimaji wamekuwa  wakitajirika  sana kwenye idara  zao na  wanatakata kwa  ujanjaujanja  na  ufisadi   wanaoufanya kwa kutengeneza ramani zinazoonesha maeneo mazuri na muhimu katika miji kwamba hayafai kutumika, kumbe wameyauza maeneo hayo kwa mlango wa nyuma na kwa bei za juu.

Unakuta kwenye ramani  inayonyesha  kuna bonde  kubwa  lisilofaa kujengwa  kumbe ukifuatilia  eneo hilo  ni  zuri  kuliko  yote na hapo  wametenga  viwanja  vya kuuza. Unakuta  ukipima  kuna  viwanja vingi na vizuri ambavyo ni vyao  wao   wanachofanya baada ya  kuuza  viwanja  halali za Halmashauri hurudi  kupima maeneo hayo walioonyesha ni mabonde na kugawana  wao kwa ajili ya kuuza kwa  faida  yao.

Lukuvi  alisema  kuwa wathamini  nao pi wamekuwa  wakiwapunja  wananchi  wasio elewa kwa  kuwafanyia  tathimini   kubwa  zaidi  ya uhalisia wake na  pindi pesa  inapotoka utakuta nyumba inathamani ya milioni 7 wakati wao wanasema inathamani ya milioni 20 ili cha juu wapate wao.

“wakati nilipokuwa Mkuu wa  Mkoa wa Dar es salaam niliweza  kubaini  ujanja wa wathamini baada ya  eneo ambalo nyumba  zake zina thamani kati ya  milioni 20 hadi 50  kwa maana  nyumba hizo ni za udongo  ila maofisa  hao  walimtafuta  mtu  na kutafuta nyumba  nzuri zaidi na kumshikisha  kibao  kisha kumpiga  picha na  kuandika kuwa  nyumba  hiyo inathamani ya  zaidi ya  milioni 200.

"Niliamua kufanya uchunguzi wangu na kumtafuta mtu aliyekwenye picha na kumbana ndipo aliniambia ukweli kuwa mthamini huyo ni ndugu yake  hivyo walikubaliana pesa ikitoka atalipwa  milioni 70 na milioni 130 ni za afisa huyo”

Hata hivyo alisema kuwa ujenzi holela katika miji na halmashauri imesababishwa na ukilitimba wa utoaji wa vibali kwa wakati na ndio  sababu ya  wananchi  kuvamia maeneo yasiyo pimwa japo kuanzia sasa  wote  waliopo katika maeneo yasiyo pimwa  watapewa leseni ya makazi ya  miaka  mitano na watalipa  kodi ya ardhi na baada ya miaka mitano wahakikishe  wamepimiwa  ili  kupewa hati.

Hivyo  Lukuvi  aliwataka  maafisa ardhi na wathamini wa ardhi manispaa ya Iringa kutofanya kama maeneo mengine kwa kufuata mpango maeneo  yote ambayo yameelekezwa  kwenye Masta Plan hiyo na kwenda  kutenda haki.

Katika hatua  nyingine  waziri  Lukuvi  alitoa  agizo kwa  wale wote  waliopewa ardhi kwa ajili ya  ujenzi wa hoteli na  viwanda na wale waliouziwa viwanda  vya serikali, hotel na mashamba ya  serikali  kuviendeleza haraka kabla ya  ardhi hiyo haijapokonywa  .

Nae Mkuu  wa  Mkoa  wa Iringa Bibi  Amina Masenza  akimkaribisha  waziri Lukuvi  alsema kuwa mkoa  wa Iringa  umeendelea  kuhamasisha  wananchi  kuzingatia  sheria  na taratibu za ujenzi na kuachana na ujenzi  holela na ndio  sababu ya  kuja na Masta Plan hiyo ambayo  imeanzishwa na aliyekuwa mstahiki meya wa halmashauri hiyo Amani Mwamwindi.

Akitoa taarifa ya uandaaji wa Masta Plan hiyo kwa ajili ya mwaka 2015-2035 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dkt William Mafwere, alisema kuwa dhumuni la mpango huo ni kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Manispaa na kuwa dhana kuu ya mpango huo ni dhana unganishi ikijumuisha dhana nyingine.

Alisema jumla ya miradi 31 itatekelezwa katika awamu ya kwanza 2015-2020 kuwa baadhi ya miradi hiyo ni kituo cha mabasi Igumbilo, kituo hicho kimeanza ujenzi na hatua ya utekelezaji imefikia asilimia 30.
 
Nae Mbunge wa jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema  kuwa kazi inayofanywa na  Waziri  Lukuvi ni tofauti na mawaziri  wengine kwani amekuwa ni waziri wa mfano katika  kuchapa kazi.

“Kwa  mnaonifahamu  vizuri  mimi sio mbunge wa kusifia  sifia ni mbunge  mwenye msimamo ila nampongeza  sana Waziri Lukuvi ni  waziri  mchapakazi na kazi zake zinaonekana na ndio maana  hata  bungeni ni waziri pekee ambaye bajeti yake ilipitishwa kwa kishindo  hata na  sisi  wabunge wa kambi ya upinzani”

Mpango Kabambe ni chombo cha kuchochea utumiaji wa fursa zilizopo katika mji,  kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali  za kiuchumi na kijamii na kupunguza na kumaliza migogoro ya ardhi. kudhibiti ujenzi holela mijini na hutumika pia kuongoza, kusimamia na kudhibiti ukuaji na uendelezaji wa mji na kutoa uhakika kwa wawekezaji katika Halmashauri za Manispaa ya husika.

Rais Magufuli Atishia Kuifunga Migodi ya Madini Endapo Barrick Watachelewa Katika Mazungumzo

$
0
0
Wakati Kampuni ya Acacia ikisema imepoteza mapato ya Sh385 bilioni katika kipindi cha miezi sita kutokana na kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini nje, Rais John Magufuli ametishia kufunga migodi ya wawekezaji iwapo hawatajitokeza mapema katika mazungumzo.

Rais Magufuli amesema hayo takriban wiki moja baada ya kudokeza kuwa Serikali ingeanza mazungumzo “na waliokuwa wanatuibia” mapema wiki hii.

Jana, Rais Magufuli alisema Serikali haitasita kufunga migodi yote ya madini ambayo wamiliki walitakiwa kufanya mazungumzo na Serikali kuhusu ulipaji kodi.

 Akizungumza katika ziara yake mkoani Kigoma ambako alizindua Barabara ya Kibondo-Nyakanazi, Rais Magufuli alisema Taifa linapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa madini.

“Ni matrilioni ya fedha ambayo yanapotea, na sasa hivi tumewaita tufanye mazungumzo lakini wakichelewachelewa nitafunga migodi yote,” alisema.

Alisema ni bora migodi hiyo ikakabidhiwa kwa Watanzania kuliko wawekezaji ambao hawalipi kodi.

Rais Magafuli alipiga marufuku usafirishaji wa mchanga huo nje ya nchi, na baadaye kuunda kamati mbili; moja ya kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa katika makontena 277 yaliyozuiwa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine kuangalia athari za kiuchumi na kisheria tangu mchanga huo uanze kusafirishwa mwaka 1998.

Ripoti ya kamati ya kwanza ilisema kuwa Acacia, inayoendesha migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, haikusema ukweli kuhusu kiwango cha dhahabu, ikidai kuwa imebaini mchanga huo una madini hayo mara kumi ya kiwango kilichotangazwa na wawekezaji hao.

Ripoti ya kamati ya pili ilionyesha kuwa katika kipindi cha miaka 20, Serikali ilipoteza zaidi ya Sh108 trilioni na kwamba Acacia haijasajiliwa nchini na hivyo inafanya kazi kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Acacia haijakubaliana na matokeo ya ripoti hizo, ikisema inataka uchunguzi wa kamati huru na kwamba kama matokeo hayo ni ya kweli, Tanzania ingekuwa moja ya nchi tatu zinazozalisha dhahabu kwa wingi duniani.

Jana, Acacia ilisema imepoteza Sh385 bilioni katika kipindi cha miezi sita. Acacia pia imesema endapo hali itaendelea kuwa hivyo, italazimika kuufunga mgodi wake wa Bulyanhulu na kusitisha mikataba ya ajira kwa wafanyakazi.

Hata hivyo, katika taarifa yake ya jana inayozungumzia kipindi cha Januari mpaka Juni, Acacia imesema  imepata changamoto kubwa katika utendaji wake nchini.

 “Nusu (ya kwanza), imetupa changamoto kubwa katika shughuli zetu Tanzania baada ya kuwekewa zuio la usafirishaji wa makinikia kuanzia Machi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Brad Gordon. “Mapato yetu yameshuka mpaka dola 175 milioni za Kimarekani kutoka dola 318 milioni tulizotarajia.”

Licha ya kushindwa kuingiza Dola 175 milioni za Marekani (zaidi ya Sh385 bilioni) zilizotarajiwa, Acacia inasema imelipa dola51 milioni za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambazo ni zaidi ya Sh112.2 bilioni.

Ili kulinda masilahi ya wanahisa wake, Acacia imewasilisha notisi kwa msuluhishi kwa ajili ya migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ambayo ndiyo inayozalisha mchanga wa madini kwa sasa.

Buzwagi imekuwa ikisafirisha mchanga huo kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuyeyusha ili kupata mabaki ya dhahabu, shaba na fedha kutokana na teknolojia hiyo kutokuwapo mgodini.

Hatua ya kwanza ya kuchenjua dhahabu hufanyika mgodini na mchanga unaosalia ndio unaosafirishwa nje. Acacia imekuwa ikieleza kuwa mchanga huo una asilimia 0.02 ya dhahabu wakati shaba ni asilimia 10.

Acacia pia imekanusha taarifa ya kuwapo amri ya kutakiwa kuondoka nchini kwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kigeni.

“Hatuna taarifa za kutolewa kwa amri hiyo kwa mfanyakazi wetu yeyote wa kigeni aliyepo Tanzania. Tunashirikiana vizuri na Serikali kwenye mazungumzo yanayoendelea na hakuna aliyekamatwa habari hiyo si sahihi,” inasema taarifa hiyo.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Rais Magufuli: Tukikaza Mkanda Kidogo, Lazima Tutakusanya Kodi ya Trilioni 2 kwa Mwezi

$
0
0
Wakati takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zikionyesha makusanyo ya kodi kwa mwezi ni wastani wa Sh trilioni moja hadi 1.3, Rais Dk. John Magufuli, amesema kibano cha kodi kikiongezwa kidogo, mapato yatafika hadi Sh trilioni mbili kwa mwezi.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana asubuhi, wakati akihutubua wananchi wa Wilaya Kibonda, kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Kibondo-Nyakanzi.

“Fedha zinazofanya miradi ni zenu, Serikali haina shamba, haina chochote, inategemea kodi za wananchi, ndiyo maana mimi nawachukia sana wanaokwepa kulipa kodi,” alisema.

Pia alisema wanaokwepa kulipa kodi si wananchi wa kawaida, bali ni watu wakubwa kwa sababu wananchi wanalipa hata wanapotoa nauli za basi.

“Mkipanda kwenye basi, lililipiwa kodi lilivyonunuliwa na mafuta yakiwekwa mnalipa mkodi, ni jukumu tu la waliokusanya kodi kwenye vituo vya mafuta wazirudishe Serikalini, lakini wapo wanaobaki nazo. Hao ndio nataka kulala nao mbele, nimeshatoa siku 14 na sasa hivi zimekabaki 12 au 13,” alisema na kuongeza:

“Serikali ikikusanya kodi, baadaye inazirudishe kwenye maendeleo ya wananchi, tulipoingia madarakani kwa awamu ya tano, kodi zilizokuwa zinakusanywa kwa mwezi ilikuwa kati ya shilingi bilioni 800 hadi 850, tulipobana tu kidogo, tunakusanya shilingi trilioni 1.2 hadi shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi.

“Nina uhakika tukibana zaidi tutapata shilingi trilioni mbili ama shilingi trilioni mbili na kitu, tulipokusanya hizo shilingi trilioni 1.2 hadi shilingi trilioni 1.3, ndugu zangu wa Kakonko na Watanzania kwa ujumla, tulianza kuzitumia fedha hizo, tulianza kwa kutoa elimu bure kwa watoto wetu kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari wanasoma bure, hakuna kulipa ada.

“Walikuwa wanasoma group (kundi) la watu fulani tu wakubwa, watoto wa masikini hawaendi shule, nikasema haiwezekani.

“Kwenye kampeni niliwaambia nitasomesha Watanzania bure, wakasema haiwezekani, nikawaambia nimekuwa waziri kwa miaka 20 najua zinapovuja nitaenda kuziba hukohuko.”

Alisema fedha nyingi zimekuwa zikivuja serikalini kutokana na matumizi mabaya ndani ya Serikali.

“Watu wanazunguka wanatembea kila mahali, semina za ajabu ajabu, mikutano ya ajabu ajabu, posho za ajabu ajabu, hizo ndiyo zimekuwa ni fedha za wananchi  wanyonge. Na mimi nimesema semina hamna, maposho ya ajabu ajabu hamna, kusafiri hadi nikupe kibali, ili fedha zinazobaki zirudi kwa wananchi,” alisema.

Alisema kwa matokeo ya kubana fedha hizo, kwa mwaka huu bajeti ya dawa imepanda kutoka Sh bilioni 30 hadi Sh bilioni 250 na vitanda vya Sh bilioni 33 vimenunuliwa kwa ajili ya hospitali.

Wawili wafariki baada ya daladala kugonga treni Dar

$
0
0
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 36 wamejeruhiwa baada ya gari la abiria (daladala) kugonga kichwa cha treni katika eneo la Yombo, Temeke jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Temeke, Gilles Moroto (pichani) waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea mapema leo asubuhi ni mwanamke mmoja aliyekuwa abiria wa gari hilo aina ya coaster na mwanaume mmoja ambaye ni kondakta.

Kamanda Moroto amesema kuwa kati ya majeruhi 36 wa ajali hiyo, majeruhi wanne wako katika hali mahututi na kwamba wote wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Temeke kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Majeruhi wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Temeke. Miongoni mwa majeruhi hao, wanne wapo katika hali mbaya,” amesema Kamanda Moroto.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamepongeza juhudi za wananchi kwa ushirikiano wao katika kusaidia kuwaokoa majeruhi wa ajali hiyo kwa kuwatoa ndani ya gari.

Tundu Lissu Agoma Kupima Mkojo....Polisi Waondoka na CD 6

$
0
0
Baada ya jeshi la polisi kumkamata Tundu Lissu siku ya Alhamsi uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. Jana jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.

Siku ya jana Ijumaa ya tarehe 21/07/2017  jeshi la polisi walimchukua Tundu Lissu na kwenda naye mpaka kwa Mkemia Mkuu wakiwa na lengo la kutaka kumpima mkojo kabla ya kuelekea nyumbani kwake kufanya ukaguzi. Lakini kiongozi huyo aligoma kufanya kipimo hicho kwa madai kuwa tuhuma anazotuhiwa haziendani na vipimo hivyo.

Kwa mujibu wa Tumaini Makene ambaye ni Afisa habari wa (CHADEMA) anasema kuwa jana polisi baada ya kufanya ukaguzi nyumbani kwa Tundu Lissu waliweza kuchukua CD 6 na kuondoka nazo. 

"Jeshi la Polisi bado linamshikilia, Mhe. Tundu Lissu, Kwenye upekuzi jana nyumbani kwake walichukua CD 6 za 1996 zinazohusu masuala ya mgodi wa Bulyag'hulu, Shinyanga" ilisema taarifa ya CHADEMA

Leo ni siku ya pili toka kiongozi huyo anashikiliwa na jeshi la polisi Dar es Salaam lakini Wakili Peter Kibatala pamoja na Wakili Fatma Karume wa IMMA Advocates kwa upande wao wanasema wanaendelea na juhudi za kisheria kuhakikisha kiongozi huyo anapatiwa dhamana au kufikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo. 


CCM Kutoa Mikopo Kwa Wanafunzi Vyuo Vikuu

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wake, Humphrey Polepole kimetangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambao wamekosa mikopo ya kuendelea na masomo na wanafunzi ambao ni yatima.

Taarifa iliyotolewa na Polepole inasema kuwa wanafunzi hao wanapswa kufika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kusaidiwa shida zao hizo za mikopo, jambo ambalo limepokewa tofauti na baadhi ya watu wakidai kuwa suala la kutoa mikopo kwa wanafunzi ni jukumu la bodi ya mikopo. 
Kutokana na mitazamo ya watu kuwa tofauti katika jambo hili, Humphery Polepole aliibuka na kusema kuwa upinzani wa Tanzania ni mtihani mkubwa kwani wanapojaribu kutatua matatizo ya watu wanakujua juu na wasipotatua matatizo pia wanakuja juu.

"Tukikaa kimya kwa shida za watu inakuwa tatizo, tukishughulika na shida za watu inakuwa tatizo kubwa. Huu upinzani mtihani" alisema Polepole 



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 23

Waziri Mkuu amtumbua DED wa mbozi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma

$
0
0
Katika kuhakikisha kunakuwepo na matumizi mazuri ya fedha za umma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa  tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.

Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa hao mapema hii leo wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara yake ya kikazi.

Amesema kuwa Maofisa hao wamekiuka sheria za matengenezo ya magari ya Serikali kwa kwenda kutengeneza katika gereji ambazo hazikusajiliwa na wala hazifanyi shughuli hiyo, jambo ambalo halikubaliki.

“Halmashauri inanuka rushwa tunataka iwe safi. Hatuwezi kukubali kuona Halmashauri hii na zingine nchini zikigeuzwa kuwa magenge. Kwa Serikali hii no, hatuhitaji rushwa wala harufu ya ufisadi.”amesema Majaliwa

Aidha, amesema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona watumishi waliopewa dhamana wakijinufaisha kwa fedha za umma na kuwaacha wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za maji, afya na elimu, hivyo itaendelea kuwachukulia hatua.

Hata hivyo, Majaliwa amewataka Madiwani na Wakuu wa Idara katika Halmashauri zote nchini wabadilike na wahakikisha wanashirikiana na kufanya kazi kwa ushirikiano kwani wakigawanyika watashindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Rais Magufuli: Aliyemuita Kafulila tumbili yeye ndiye tumbili kwa IPTL

$
0
0
Rais wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kutokana na namna alivyojitoa katika kutetea maslahi ya Watanzania kwenye sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza ambapo alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya unafiki itakayompeleka motoni.

Akizungumza, Rais alisema anatambua kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini kwenye suala la IPTL, aliweka maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli hivyo anampongeza na pongezi hizo ni za dhati kwani zinatoka moyo. Rais alieleza umma uliokuwa umejitokeza mahali hapo kuwa, wizi uliokuwa unafanywa na IPTL ni mkubwa hivyo Kafulila alisimama kutetea umma wa watannzani.

Lakini pia Rais alieleza vikazwo ambavyo Kafuli alikutana navyo wakati akipambana kuhusu wizi huo uliokuwa ukiratibiwa na baadhi ya watumishi wa serikali kwa manufaa yao wenyewe.

“Wakamtisha wengine kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili, huyu (Kafulila) alifanya kazi ya Mungu ya kuwatumikia Watanzana,”  alisema Rais Magufuli huku wakazi wa eneo hilo wakilipuka kwa furaha.

Akiendelea kumwaga sifa hizo za dhati, Rais Magufuli alisema kwenye hili suala la wizi wa IPTL, atampongeza Kafulila kwa maisha yake yote.

Akizungumzia suala la uzalendo, Rais amesema nchi ilikosa uzalendo na kwamba kila aliyekuwa akichaguliwa alikazana kukusanya mali zake yeye mwenyewe bila kujua kuwa atakufa na atazikwa kwenye shimo moja, hivyo akawasihi watanzania wajenge uzalendo.

Alisema maendeleo hayana chama na kwamba, kiongozi mzuri ni yule anayewatumikia watu wake bila kujali chama, kwani mradi huo wa maji anaoufungua utanufaisha watu wote hata wasio na chama.  Alieleza kwamba, ushabikia wa vyama ndio unaochelewesha maendeleo ya watanzania.

Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji mkubwa katika kata ya Nguruka uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 ambao unatarajiwa kukamilika Disemba 30 mwaka huu ambao utafuta kero ya maji kwa wananchi wa kata ya Nguruka.

Rais Magufuli Ammwagia SIFA mbunge wa Kaliua, (CUF) Magdalena Sakaya

$
0
0
Rais John Magufuli amemmwagia sifa mbunge wa Kaliua, (CUF) Magdalena Sakaya na kusema kuwa mwili na tabia yake ni za CUF lakini roho na damu yake ni ya CCM.

Ameyasema hayo leo Jumapili, Julai 23 wakati wa ziara yake mkoani Tabora na kuwataka wabunge wa CCM kumpa ushirikiano anapofanya shughuli za maendeleo.

“Inawezakana hata siku zijazo akahamia CCM, damu yake na roho yake ni CCM ingawa mwili na maneno na tabia zake ni CUF,” amesema.

Amesema ni mara kumi uwe na CUF, Chadema au NCCR anayefanya mambo ya CCM kuliko uwe na CCM anayefanya mambo ya vyama vingine.

“Hasara yake ni kubwa mno, mnafikiri ni mwenzenu wakati siyo mwenzenu, nani hayajui haya hata wakati wa kampeni yalitokea unafikiri siyajui,” amesema.

Amewataka wabunge wa CCM kumpa ushirikiano Sakaya na kuwataka wasimbague kama asivyowabagua.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images