Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais wa zamani wa Brazil ahukumiwa kwenda jela miaka tisa na nusu

$
0
0
Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa na nusu jela kutokana  na kupatikana na makossa ya rushwa yaliyokuwa yakimkabili.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano, alijizolea umaarufu kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha nchini Brazil.

Lakini sasa mambo yamegeuka na amekutwa na hatia ya kupokea rushwa ya zaidi  ya Sh2 bilioni za malipo ya  ukarabati wa ghorofa  lake la mapumziko kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, ya OAS.

Hukumu hii inakuja wakati Lula ameshatoa msimamo mkali kwamba, ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea urais mwakani.

Kufuatia hukumu hiyo, Rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wakiahidi kukata rufaa.

Wakati huohuo, kamati ya Bunge la Congress ya Brazil inajadili iwapo iiruhusu mahakama kuu kusikiliza kesi ya rushwa inayomhusisha Rais mwingine wa Brazil Michel Temer.

Temer kwa upande wake, alishtakiwa mwezi uliopita kwa tuhuma za kupokea hongo kutoka kampuni kubwa ya usindikaji nyama.

Kamati hiyo inatarajiwa kupiga kura kesho.

Waziri Mpango Awatuliza Machinga Nchini

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amewahakikishia wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga kwamba Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo baada ya kukagua zoezi la usajili wa wafanyabiashara hao linaloendelea katika katika Ofisi za TRA wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo ameshuhudia idadi kubwa ya wafanyabiashara hao wakiwemo waendesha bodaboda, mamalishe na wauza bidhaa mbalimbali wakiendelea kujisajili ili wapate vitambulisho.

“Ndio maana tumeona tuweke utaratibu wa kuwaandikisha na tuwapatie vitambulisho hatimaye tuweke mpango maalumu wa kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyiabiashara zenu badala ya kila siku kuwatumia askari mgambo kuwafukuza wakati mnatafuta riziki,” alisema Dkt. Mpango.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwawekea wafanyabiashara hao wadogo utaratibu mzuri ii waendelee kufanya kazi zao za kujenga familia na Taifa kwa ujumla bila bughudha kwa kuwa Serikali inathamini mchango wao katika uchumi na maendeleo ya nchi.

“Ni lazima ifike mahali kila mtanzania achoke na umasikini, na sisi Serikali yenu tufanyekazi ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi badala ya kuwakandamiza,” aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango amesema nchi ya Sweden imeweka utaratibu mzuri wa masoko maalumu kwa ajili ya wamachinga wao kila siku za Jumamosi na Jumapili ambapo watu wengi hufika maeneo hayo kununua bidhaa hali inayoashiria kuwa suala la uwepo wa wafanyabiashara wadogo wadogo ni la nchi nyingi duniani.

“Nawasihi mkawaeleze Watanzania wengine na wafanyabiashara ndogo ndogo wenzenu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili wasajiliwe na kupewa vitambulisho vitakavyowasaidia kujulikana,” alisisitiza Dkt. Mpango

Amerejea kauli yake ya kuwapongeza Watanzania wote kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kujitokeza kwa wingi kulipa kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo kwa kuwa kodi hizo zinaipa Serikali nguvu na uwezo wa kuwahudumia ipasavyo.

Mkiona barabara zinajengwa, tunaboresha huduma za afya kwa nunua dawa za kutosha, mjue kuwa kodi yenu hiyo kidogo kidogo mnayotoa ndiyo inayotumika kuwezesha mambo hayo kufanyika (makofi)” Alisisitiza Waziri huyo wa Fedha na Mipango

Dkt. Mpango ameahidi kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi na vitendeakazi katika kituo hicho cha uandikishaji ama usajili wa wafanyabishara wadogo wadogo kilichoko katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ilala Jijini Dar es Salaam ili kufanikisha kazi hiyo.

Kwa upande wao, wafanyabiashara wadogo wadogo hao wameipongeza Serikali kwa hatua waliyoichukua ya kuwatambua rasmi na kuwaingiza katika mfumo wa ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi.

Wamemwomba Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango awafikishie salamu zao za dhati kwa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, kwamba wanamuunga mkono katika jitihada zake za kuwaletea wananchi maendelo na kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na kujenga nidhamu ya watumishi wa umma na matunda yake yameanza kuonekana katika uwajibikaji.


Lowassa Aripoti Polisi.....Atakiwa Kurudi Tena Alhamisi Ijayo

$
0
0
Baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuwasili katika ofisi ya mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, kama alivyotakiwa kufanya Juni 29, ameruhusiwa kuondoka na kutakiwa kurudi tena Alhamisi ijayo.

 Mwanasheria wa Lowassa, Peter Kibatala amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa Lowassa ametakiwa kurudi Alhamisi bila sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo kuwekwa wazi.

“Hatujaambiwa kwa nini ila tumeambiwa tuje alhamisi ijayo kwa ajili ya maelekezo na kuwasikiliza zaidi,” alisema

Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kwenda katika ofisi za DCI ambako anahojiwa kwa tuhuma za uchochezi.

 Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alihojiwa Juni 28 na Juni 29 na Wakili Kibatala alizungumza na wanahabari mara baada ya mahojiano hayo.

Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya kichochezi Juni 23, mwaka huu katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 10, 184 Kuziba Mapengo ya Waliogushi Vyeti

$
0
0
Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, imefahamika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Utumishi, Florence Temba, ilieleza kuwa agizo hilo linazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala wa Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma.

Ilimnukuu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam jana.

“Mgawanyo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, vipaumbele vya Taifa kwa sasa na upatikanaji wa watumishi kutoka katika soko la ajira,” alisema Kairuki.

Kairuki aliongeza kuwa taratibu za kukamilisha mgawo wa nafasi za ajira 4,816 zilizosalia unaendelea ili kuwezesha wizara na taasisi nyingine zilizokamilisha uhakiki wa watumishi wa umma hivi karibuni kuajiri watumishi wapya kuziba nafasi wazi zilizojitokeza.

Alieleza kuwa serikali imetoa kibali kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti baada ya zoezi la uhakiki.

“Watumishi wa umma watakaoajiriwa kuziba nafasi hizo wanatarajiwa kuripoti kazini kuanzia mwezi Agosti, 2017,” alieleza Waziri Kairuki, na kuongeza kuwa utaratibu wa ajira mpya za serikali upo palepale na amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi wowote wa ajira hizo.

“Napenda kusisitiza kuwa vibali tulivyovitoa leo ni vile vilivyoziba pengo la walioghushi vyeti, naomba wananchi watambue kuwa suala la ajira mpya bado liko pale pale kama serikali ilivyojipanga,” alisema Kairuki.

Aprili mwaka huu, Rais John Magufuli alipokea ripoti yenye orodha ya watumishi wa umma ambao kati yao wanadaiwa kuwa na vyeti pungufu, vyenye utata na vya kughushi kutokea kwa Waziri Kairuki.

Waliokuwa na vyeti vya kughushi walikuwa 9,932, na Rais aliapa kwamba hawatarudi kazini. Rais Magufuli aliagiza kufutwa kazi kwa wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo na kuzuia mishahara yao ya mwezi huo, lakini hata hivyo bado mlango uliwekwa wazi kwa wenye pingamizi na wapo waliokataa rufaa huku wengine wakienda kwenye mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Wiki iliyopita akiwa Dodoma, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alitangaza kuwa wiki hii serikali itatoa vibali 3,000 vya ajira katika sekta ya afya vikiwemo vya madaktari na wauguzi pamoja na maofisa hesabu 535 kwa ajili ya vituo vya afya vya kata ili washughulike na ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya afya na zahanati.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Yalaani Matamshi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imesema imesikitishwa na matamshi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema imesikitishwa na kauli ya rais wa awamu ya tatu akirudia maneno ya kejeli ya watanzania wenye maoni tofauti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Mkapa alisema akiwa Chato, Geita kuwa Takwimu zilizotolewa na Waziri wa Afya siku hiyo( Julai 10, 2017)  ya makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na Mkapa Foundaton  Zitawasaida kupunguza Upumbavu Wale aliowaita hivyo Wakati wa Kampeni  2015.

Taarifa hiyo imesema kuwa matamshi ya Mkapa hayapendezi kusikika yakitoka kwa kiongozi wa kitaifa, na ni matamshi yasiyoheshimu maoni tofauti.

==>Isome taarifa hiyo hapo chini

TUCTA Yawatoa Hofu Watumishi Wenye Vyeti FEKI

$
0
0
Shirikisho  la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limewatoa hofu watumishi wa Serikali waliokutwa na vyeti feki na kuwataka kupuuza taarifa kuwa hawatolipwa malimbikizo ya madai yao.

Limewahakikishia watumishi hao, wanaoidai Serikali malimbikizo mbalimbali kuwa mchakato wa ulipaji wa malimbikizo yao ya mishahara na madai mengine utaanza hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makubaliano waliyoafikiana na Serikali.

“Kumekuwapo na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa watumishi waliokutwa na vyeti feki hawatolipwa madai yao,  jambo hilo si kweli, nawahakikishia watumishi hawa TUCTA tumekutana na waziri mwenye dhamana na katibu mkuu wake ambao nao wamesema taarifa hizi hazina ukweli.

“Tumeambiwa uhakiki utakapokamilika, ndipo watatangaza uamuzi wa madai yao,” alisema.

Kuhusu malimbikizo ya mishahara na madai mengine ya watumishi wa Serikali, wakiwamo walimu, Nyamhokya alisema wamehakikishiwa wataanza kulipwa hivi karibuni.

“Ingawa hatukupewa muda kamili yataanza kulipwa lini, niwatoe hofu watumishi kuwa madai yao yote yataanza kulipwa hivi karibuni… kauli ambayo imetoka kwa waziri mwenyewe, baada ya kukutana naye ana kwa ana ofisini kwake hivi karibuni,” alisema.

Licha ya kupongeza juhudi za Rais Dk. John Magufuli katika kuisafisha Serikali, Nyamhokya aliiomba Serikali kutekeleza ahadi za rais  alizozitoa wakati akihutubia sherehe za Mei Mosi, mwaka huu.

“Aliahidi kurejesha madaraja kwa wafanyakazi katika mwaka huu wa fedha, kuongeza mishahara pamoja na kulipa madeni ya watumishi wote,” alisema.

Hadi kufikia Novemba, mwaka jana, Serikali imelipa Sh bilioni 29 kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwamo walimu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa hotuba aliyotolewa bungeni Aprili 18, mwaka huu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angellah Kairuki, ni madai 18,823 ya malimbikizo ya watumishi yenye thamani ya Sh bilioni 32.8 ambayo yamehakikiwa na kuingizwa kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi na mshahara kwa malipo.

Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya

$
0
0
IGP Sirro, amefanya mabadiliko katika jeshi la polisi ili kuboresha utendaji wa jeshi hilo kwa kumuhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga na kuwa Kamanda wa polisi wa mkoa Mbeya

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema kuwa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya upelelezi.

Kufuatia mabadiliko hayo nafasi aliyokuwa nayo Mohamed Mpinga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.

Kwa mujibu wa Barnabas Mwakalukwa (ACP) ambaye ni msemaji wa jeshi la polisi, Makao Makuu ya Jeshi hilo amesema uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

IGP Saimon Sirro alishauriwa na Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko katika jeshi hilo ili kuleta ufanisi na kuboresha utendaji wa jeshi la polisi nchini, jambo ambalo tayari inaonyesha ameanza kulifanyia kazi kwa kufanya mabadiliko kama haya.

Tiagi Masamaki wa TRA na Wenzake watano Waachiwa HURU na Mahakama ya Kisutu

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.

Washtakiwa hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA)  kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

"Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.

Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.

Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo  iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  TRA, Habib Mponezya  (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton  Mponezya (51).

Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi  Mrema (31),  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.

Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano tu ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na Ashraf Khan.

Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.

Ofisi za kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki vituo vya Star TV na Radio Free Africa (RFA) leo zimefungwa na TRA

$
0
0
Ofisi za Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki kituo cha televisheni cha Star na cha redio cha Radio Free Africa (RFA) zimefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa deni la Sh4.5 bilioni.

Ofisi hizo zimefungwa leo Alhamisi (Julai 13) na wakala wa TRA, Kampuni ya Sukah Auction Mart and Court Brokers ya jijini Mwanza.

Meneja utumishi na utawala wa Sahara Media Group, Raphael Shilatu amesema ni kweli wana malimbikizo ya madeni yanayotokana na kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.

Balozi Mwapachu ajitoa katika Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Acacia

$
0
0
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji ya Acacia, Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa vipindi viwili.

Mwapachu amechukua uamuzi huo leo, Julai 13 baada ya muhula wake wa pili wa miaka mitatu mitatu wa ujumbe wa bodi hiyo, kumalizika.

Taarifa iliyotumwa leo na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Acacia imeeleza kuwa inamshukuru Balozi Mwapachu kwa utendaji wake na ushirikiano wake wote  alipokuwa mjumbe.

“Tunamtakia maisha mema,” imesema taarifa hiyo.

Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi ya Acacia itabaki na wajumbe saba, wakiwamo wanne wakurugenzi na wasio wakurugenzi.

==>Isome taarifa ya Acacia hapo chini

DCI Ajitosa Sakata la Mchele wa Plastiki....Atoa ONYO Kwa Aliyesambaza Video

$
0
0
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wenye tabia hiyo.

Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki nchini.

Boaz amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka kwa udi na uvumba mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.

Na amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha madhara makubwa katika jamii.

”Kabla ya kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika wa vyanzo vyako, wahsuika wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa ya msingi”. amesema Boaz.

Aidha waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy Mwalimu ametaarifiwa na  Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.

Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya July 14

Fahamu Uhusiano Uliopo Kati Ya Unene & Uzito Kupita Kiasi ( Overweight & Obesity ) Na Tatizo La Ukosefu & Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.

$
0
0
Unene  na  uzito  uliozidi  ( Obesity )  ni  miongoni  mwa  vyanzo  na  visababishi  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Kwa   mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitabibu, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wenye   unene  na  uzito  uliozidi, wanakabiliwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

KWANINI  WANAUME  WENYE  UNENE  NA  UZITO  ULIOZIDI  WANAKABILIWA  NA  HATARI  KUBWA  YA  KUPATWA  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Wanaume  wenye  uzito na  unene  uliozidi  wapo  katika  hatari  kuu  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuna  uhusiano mkubwa  kati  ya  unene/uzito  uliozidi  pamoja  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

Kama  tulivyo elezea  katika  makala  zetu  za  nyuma,  SUALA  LA NGUVU  ZA  KIUME NI  SUALA  LA  KIMFUMO.  Mfumo  wa  nguvu  za  kiume  unahusisha  ogani  mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu.

Ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, ni  lazima  ogani  zote  zinahusika  katika  mfumo, ziwe  imara  na  zenye  afya  njema, na  pia  ni  lazima  ziwe  na  ushirikiano  imara.

Kudhoofishwa  kwa  ogani  moja  wapo  kati  ya  ogani  hizo  kutasababisha  mhusika  apatwe  na  tatizo  la  ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Kwa  kukumbushia  tu,  mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa   nguvu  za  kiume  yapo  matano  ambayo  ni

1. Ubongo  imara  na  wenye  afya  njema

2. Mishipa  imara  ya  kusafirishia  damu  mwilini

3. Mfumo  imara  na  wenye  afya  wa usafirishaji  damu  mwilini.M .3

4.Mishipa  na  misuli  ya  uume  iliyo  imara na  yenye  afya  njema

5.Pamoja  na  uhusiano  imara  na  wenye afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyo katika  ubongo  ( nerves),mishipa  ya kwenye  uti  wa  mgongo  ( spinal  cords ) pamoja  na  mishipa  & misuli  ya  kwenye uume.

Sasa  basi, hitilafu  yoyote  katika  mojawapo  kati  ya  mambo  matano  tajwa  hapo  juu, itamfanya  mhusika  apatwe  na  tatizo  la  ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

UNENE  NA  UZITO  ULIOZIDI   UNA  SABABISHA  VIPI  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA/AMA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kwa lugha nyepesi  na  yenye  kueleweka  kwa  kila  mtu,  mtu mwenye  unene  na  uzito  uliopitliza, maana  yake  ni  kwamba  ana  mafuta  , sukari  na  kolestrol  nyingi  katika  damu  yake.

Kwa  maana  nyingine, ni kwamba  kama  wewe  una  unene  uliopitiliza, maana  yake ni  kwamba, ogani  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinaogelea  katika  mafuta  yaliyomo  ndani  ya  mwili wako.

1.  Kolestrol   nyingi   katika  damu, huathiri  mfumo  usafirishaji  damu  katika  mishipa  ya  inayo  tumika  kusafirisha  damu  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili  ikiwamo  katika  mishipa  ya  kwenye  uume. Matokeo  yake  basi  , kolestrol  hiyo  husababisha  kuziba  kwa  ateri  ambayo  ndio  njia  itumikayo  kupeleka  damu  katika  mishipa  na  misuli  ya  kwenye  uume, na  kama  damu  haitaweza  kusafirishwa  hadi  kwenye  mishipa  ya  kwenye  uume, maana  yake  ni  kwamba, mwanaume  huyo  hatokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake  kwa  sababu, damu  ndio  inayo  ufanya   uume  uweze  kusimama.

2. Kama  ilivyo  kwa  kolestrol, sukari  na  mafuta  mengi  katika  damu  huathiriki  utiririkaji  wa  damu   mwilini  na  hivyo  kufanya  vigumu  damu  kutiririka  kuelekea  kwenye  mishipa na misuli   ya  uume  ambayo  ndio  inahusika  na  kuufanya  uume   usimame.

3. Unene  na  uzito  uliopitiliza  una  uhusiano  mkubwa  sana  na  ugonjwa  wa  kisukari. Na  ugonjwa  wa  kisukari nao  una  uhusiano  mkubwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, kwa  sababu  unaathiri  mfumo  mzima  wa  nguvu  za  kiume  kama  ifuatavyo : Kwanza;unashambulia  na  kudhoofisha  mishipa  ya  ubongo  na  kuifanya  ishindwe   kuwa  na  uhusiano  mzuri  na  mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo, pamoja  na  mishipa  na  misuli  ya  kwenye  uuume. Pili unashambulia na  kudhoofisha  mishipa  ya  usafirishaji  damu  mwilini na  tatu  unasababisha  kudhoofika  kwa  ogani  muhimu  katika  mwili  wa  mwanadamu  kama  vile  figo.

Hivyo  basi, mwanaume  mwenye  unene  na  uzito  ulio zidi, yupo  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, kuliko  inavyo weza  kufikiriwa.

4. Unene  na  uzito  uliopitiliza  una  uhusiano  mkubwa  na  tatizo  la  shinikizo  la  damu. Kwa  lugha  nyingine  ni  kwamba, watu  wanene  wapo  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kupatwa  na  tatizo  la  shinikizo  la  damu,. na  tatizo  la  shinikizo  la  damu  nalo  lina  uhusiano  mkubwa  sana  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Shinikizo  la  Damu husababisha  mishipa  ya  ateri  ambayo  hutiririsha  damu  iingiayo  kwenye  uume  kuziba  na  kushindwa kutanuka  kwa  kiwango  inachotakiwa  kutanuka.

Pia  huifanya  mishipa  laini  katika  uume   kushindwa  ku-relax  na  hivyo  kushindwa  kuizuia  mishipa  ya  vena  ya  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  maeneo  mengineyo  ya  mwilini.

Matokeo  yake  kunakuwa hakuna  kiasi  cha  kutosha  cha  damu  iingiayo  kwenye  uume  na  hivyo  kufanya  uume  ushindwe  kusimama.

Vile  vile  hata  kiasi  kidogo  cha  damu  kinacho  ingia  kwenye  uume, kinashindwa  kuendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  uume  wakati uume  ukiwa  umesimama, na  matokeo yake  ni  uume  kusinyaa  ndani  ya  kipindi kifupi  sana  tangu  usimame.

Kama  hiyo  haitoshi, tatizo  la  unene  na  uzito  kupita  kiasi  lina  weza  kupelekea  mhusika  kupatwa  na  magonjwa  ya  presha  na   moyo  ambayo  nayo  yanachangia  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  kiasi  kikubwa  sana.

SULUHISHO  LA  TATIZO  NI  NINI?
Kama  wewe  ni  mwanaume  mwenye  tatizo  la  unene  na  uzito  ulio zidi, unapaswa  kufanya  mambo  yafuatayo:

i.  Kupunguza  kolestrol   mwilini: Unaweza  kupunguza  kolestrol  na  mafuta  mengi   mwilini  kwa  kufanya  mazoezi  na  diet  ama  kwa   kutumia   dawa  mbalimbali    za  asili  ama  vyote  kwa  pamoja.

ii.  Unapaswa  kupunguza  unene  na  uzito  : Unaweza  kupunguza  unene  na  uzito  kwa  kutumia  mazoezi na  diet  ama  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  MKATAA  KITAMBI  ambayo  inasaidia  sana  kupunguza  mafuta  mwilini, kupunguza  unene  na  uzito.

TIBA  ASILIA  YA  NGUVU  ZA  KIUME  KWA  WANAUME  WENYE  UNENE & UZITO  ULIOZIDI.
Kwa  mwanaume  mwenye  unene &  uzito  uliozidi  ambaye  pia  ana  sumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, anashauriwa  kutumia  dawa  zifuatazo kwa  pamoja

1.  Dawa  ya  kuondoa  kolestrol  na  mafuta  mengi  kwenye  damu.

2.  Dawa  ya  kupunguza  unene  na  uzito  pamoja  na

3. Dawa  asilia  ya  nguvu  za  kiume  iitwayo JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  ukosefu na/ama upungufu  wa  nguvu  za  kiume  ndani  ya  siku  thelathini  tu.

Dawa  ya  JIKO  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI.

Dawa  ya JIKO  pamoja  na  dawa  za  kuondoa  kolestrol   & mafuta  mwilini, kupunguza  unene  na  uzito  zinapatikana  katika  duka  la  kuuza  dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  karibu  na  Shule  ya  Sekondari ya  Mt. ANNUARITE.

AU 

Ubungo  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  wateja  waliopo  jijini  DAR  ES  SALAAM, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu,  watapelekewa  dawa  mahali  walipo  ( DELIVERY )

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  watatumiwa  dawa  kwa   njia  ya  boti.

Kwa  wateja  wa mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya   MABASI na

Kwa  wateja  wa  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya   POSTA  au DHL.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu   tiba  asilia  ya  magonjwa  mbalimbali, tembelea  kila  siku :www.neemaherbalist.blogspot.com

Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani

$
0
0
Watu wasiojulikana wameichoma moto ofisi ya Chama cha Mapinduzi tawi la Mshonzini iliyopo wilayani Mafia mkoani Pwani na kuteketeza mali mbalimbali za chama hicho.

Akithibitisha tukio hilo, Katibu wa CCM wilayani Mafia Mohammed Dhikiri amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana  Alhamisi Julai 13.

Dhikiri amesema moto huo umeteketeza kabisa ofisi hiyo pamoja na samani za ndani.

Amesema bado haijajulikana sababu za ofisi hiyo kuchomwa moto kwa kuwa wakati tukio linatokea hakukuwepo na viashiria vyovyote vya vurugu miongoni mwa wanachama.

Amesema bado halijafahamika ni nani aliyehusika na tukio hilo na kueleza kuwa wameliachia Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi zaidi dhidi ya tukio hilo.

Naye  Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau amesema vipo viashiria vinavyoonyesha kuwa alifika mtu asiyejulikana karibu na ofisi hiyo kisha kuwasha na kurusha kijinga cha moto kwenye paa la makuti la ofisi hiyo.

Dau amesema mtu huyo baada ya kutekeleza kitendo hicho aliondoka kuelekea kichakani kama ambavyo alama za nyayo za miguu yake zilivyoonyesha.

Amesema hilo ni tukio la kwanza kutokea wilayani humo kwa kuwa hadi linatokea hapakuwa na viashiria vyovyote vile vya kutokuwepo kwa Amani kati ya wanachama au viongozi.

Jaji Mutungi Atishia Kuchukua Hatua Kali za Kisheria Dhidi ya CHADEMA na CUF

$
0
0
Siku chache baada ya vyama vya upinzani vya Chadema na CUF (Upande wa Profesa Ibrahim Lipumba) kutishiana kuharibiana kupitia oparesheni zao mpya, msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevionya vyama hivyo.

Chadema walikuwa wa kwanza kutangaza kuingilia mgogoro ndani ya CUF wakitangaza kuanzisha ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’ wakilenga kumuondoa mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba.

CUF inayomuunga mkono Profesa Lipumba pia ilijibu mapigo kwa kudai kuwa itakuja na ‘Oparesheni Futa Chadema’, wakilaani kitendo cha Chadema kuingilia mgogoro huo.

Kufuatia kauli hizo, Jaji Mutungi amevionya vyama hivyo kuwa vitakabiliwa na mkono wa sheria endapo vitajihusisha na vurugu ya aina yoyote.

Msajili aliongeza kuwa ingawa amesikia kupitia vyombo vya habari vitisho hivyo, hajapokea barua yoyote ya malalamiko ofisini kwake kutoka kwa vyama hivyo.

“Natoa onyo kwa chama chochote cha siasa ambacho kitaonesha ubabe na kutumia wafuasi wake waweze kufanya vurugu. Tutakichukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria,” Jaji Mutungi anakaririwa na Mtanzania.

“Kama kungekuwa na tatizo wangeleta barua ofisini kwangu ya malalamiko, lakini mpaka sasa sijapata barua yoyote inayohusiana na madai yao zaidi ya kusoma kwenye vyombo vya habari,” aliongeza.

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alifanya mkutano na vyombo vya habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa wamebaini Profesa Lipumba anatumika kuidhoofisha CUF hali itakayodhoofisha pia muungano wa Ukawa, hivyo wameamua kumuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. 

Kubenea alitangaza rasmi ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’ akidai kuwa tayari ilishaanza wakiwa Bungeni mjini Dodoma kwa kuwatenga wote wanaoshirikiana na Profesa Lipumba.

Saa chache baadae, Naibu Katibu Mkuu CUF upande wa Bara, Magdalena Sakaya ambaye anatambuliwa na Ofisi ya Msajili na anayemuunga mkono Profesa Lipumba alijibu mapigo kwa kueleza kuwa kambi yake itakuja na ‘Oparesheni Futa Chadema’.

Everton Yairarua Timu ya Gor Mahia

$
0
0
Timu ya Soka ya Uingereza, Everton imewafunga mabingwa wa kombe la SportPesa 2017, Gor Mahia ya Kenya 2-1 katika mchezo ulioshuhudiwa na maelfu katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.

Everton walikuwa wa kwanza kushindilia goli la kwanza nyavuni kupitia mchezaji wake mpya Wayne Rooney katika dakika ya 34 akipiga shuti kali umbali wa takribani hatua 30.

Hata hivyo, Gor Mahia walifanya purukushani zenye mahesabu mazuri na kurudisha kipigo hicho ndani ya dakika nne, hali iliyowaweka Everton mguu sawa. Magoli hayo yalidumu hadi wakati wa mapumziko huku timu hiyo ya Uingereza ikionekana kumiliki zaidi mpira.

Piga ni kupige iliyoambatana na makosa ya hapa na pale yaliyokuwa yanafanywa na Gor Mahia ilipelekea Everton kupata goli la pili lililowekwa nyavuni na Kieran Dowell aliyewatoka walinzi na kupiga shuti kali, hivyo kufanya matokeo kuwa 2-1 yakidumu hadi kiliposikika kipyenga cha mwisho.

Tofauti na wengi walivyotegemea, Gor Mahia walijitahidi kuwapa wakati mgumu Everton hali iliyosababisha kocha Dylan Kerr kutoa maelekezo ya mara kwa mara kwa wachezaji wake.

Rooney pia alikutana na kisiki cha kukamiwa na wachezaji wa Gor Mahia wakitimiza ahadi yao ya kumdhibiti ingawa nahodha huyo wa zamani wa Manchester Utd hadhibitiki kirahisi, hali iliyopelekea kuwapa madhara ya goli moja.

Rufaa Vyeti Feki: 600 Wagonga Mwamba, 450 Warudishwa Kazini

$
0
0
Watumishi wa umma 450 walioondolewa kazini kutokana na kudaiwa kutumia vyeti vya kughushi wamerudishwa kazini baada ya kushinda rufaa zao.

Baada ya kutangazwa kwa Orodha ya watumishi wenye vyeti feki, 1050 walikata Rufaa huku  8800 wakiridhika na matokeo hayo.

Mbali na hilo, Serikali imesitisha mishahara kwa watumishi wa umma ambao walitakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk.Laurean Ndumbalo alisema watumishi hao wameshinda rufaa zao hivyo wataandikiwa barua za kurudishwa katika utumishi wa umma.

Alisema katika rufaa hizo, wengi walikuwa wanawake walioolewa na kubadili majina yao kwa kutumia ya waume zao.

“Kuna baadhi walitumia majina mawili alipokuwa kidato cha nne baadaye alilazimika kutumia matatu na kusababisha mkanganyiko hivyo tumejiridhisha na wanarudishwa katika utumishi wa umma,” alisema Dk. Ndumbalo.

Alisema Serikali pia imesitisha mishahara kwa watumishi wa umma ambao walitakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

“Serikali imesitisha mishahara ya watumishi wote ambao muundo wa utumishi wao uliwataka kuwa na sifa ya kufaulu kidato cha nne wakati wanaajiriwa lakini hawakuwasilisha vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani.

“Tunasitisha mishahara yao kuanzia mwezi Julai hadi hapo watakapowasilisha vyeti vyao kuhakikiwa,” alisema Dk. Ndumbalo.

Dk. Ndumbalo aliongeza kuwa kwa watumishi walioajiriwa wakiwa darasa la saba kabla ya waraka wa Utumishi wa Umma namba moja wa mwaka 2004 uliowataka waajiriwa kuwa na sifa ya kidato cha nne, wataendelea na kazi mpaka watakapostaafu.

Alisema sera ya Menejimenti na Ajira katika utumishi wa umma toleo la mwaka 1998 lilianza kutekelezwa Mei 20, 2004 hivyo kwa walioajiriwa kabla ya hapo warudishwe kazini kama waliondolewa kimakosa.

“Nasisitiza kuwa watumishi wote wa umma walioajiriwa kwa sifa ya elimu ya darasa la saba kabla ya Mei 20 hawahusiki na uhakiki wa vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne na wataendelea kuwa watumishi wa umma katika vyeo vyao mpaka watakapostaafu kazi,” alisema Dk.Ndumbalo.

Aidha alisema serikali inatangaza ajira mpya 10,184 katika sekta mbalimbali huku ikitoa ajira 3,172 kwa sekta ya afya.

Serikali kuiunganisha mikoa ya Rukwa na Songwe

$
0
0
Serikali imesema kuwa itaanza kujenga daraja la Mto Momba litakaloiunganisha Mikoa ya Rukwa na Songwe kwaajili ya kuondoa kero kwa wananchi ambayo imekuwa ikiwasumbua hasa wakati wa masika.

Hayo yamesemwa Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani mara baada ya ziara ya ukaguzi wa barabara Kasansa mpaka Kilyamatundu ambapo amesema kuwa tayari Serikali imeshampata mkandarasi atakayejenga daraja hilo.

“Serikali imeshatoa kiasi cha sh. Bilioni tatu  fedha hizo zimetusaidia kutangaza zabuni na kumpata mkandarasi, tayari Mkandarasi wa ujenzi huu ameshapatikana na mkataba wa makubaliano ya ujenzi umeshakamilika hivyo mkandarasi atausaini rasmi hivi karibuni,” amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng.Ngonyani amesema kuwa ujenzi na kukamilika kwa daraja hilo kutasaidia kukuza uchumi na wa wananchi wa mikoa hiyo, hivyo kuongeza pato la taifa wakati huu nchi inaelekea kwenye uchumi wa kati wa Viwanda

Vile Vile amemuagiza Meneja Wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Rukwa kuhakikisha anatoa ajira kwa wakazi waliopo kata ya Kipeta ambapo ujenzi wa daraja hilo utafanyika.

Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ignas Malocha ameishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa daraja hilo ambalo kukamilika kwake kutawaletea maendeleo wakazi hao kwa vile litaufungua Mkoa wa Rukwa na kuunganisha na Songwe na Katavi.

Naye meneja wa TANROADS Rukwa Eng. Msuka Mkina amewahakikishia wakazi kijiji cha  Kilyamatundu kuwa Wakala utasimamia ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati na viwango na kupitia mradi huo wananchi hao watapata ajira.

ACACIA Yakubali Kulipa mirabaha iliyowekwa katika sheria mpya ya madini

$
0
0
Kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Bunge katika sheria za usimamizi wa rasilimali nchini, ongezeko la mrabaha unaotarajiwa kulipwa serikali uliongezeka kutoka katika asilimia 4 iliyokuwa katika sheria za zamani.

Katika kuonyesha kukubaliana na mabadiliko hayo, Kampuni ya uchimbaji madini nchini ya Acacia imekubali kuilipa serikali mrabaha wa asilimia 6 unaoendana na sheria mpya zilizoanza kutumika mwezi huu mwanzoni baada ya kusainiwa na Rais Julai 5.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo inaeleza kuwa, ili kuepuka mkanganyiko au mvurugano zaidi kwenye kazi zao katika siku za usoni, watatimiza matakwa yanayohitajika katika ongezeko la mrabaha wa katika madini ya dhahabu, fedha na shaba la asilimia 6

==>Isome taarifa ya ACACIA hapo chini

Makamu wa Rais: Hatupo Tayari Kupokea Misaada ya Wafadhili Wenye Mashart ya Kudhalilisha Utu

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Taifa halipo tayari hata kidogo kupokea misaada kutoka kwa wafadhili wenye masharti ambayo hayaendani na mila na desturi za kitanzania.

Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Craca Machel pamoja na ujumbe walioambatana nao Ikulu- Jijini Dar es Salaam.

"Kuna baadhi ya wafadhili wanaisaidia serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na bajeti vizuri sana na bila masharti mabaya lakini kuna baadhi ya wafadhili wanaonyesha wazi kuwa wanataka serikali ikubali masharti yao ambayo yanaenda kinyume na maadili ya taifa kitu ambacho hakiwezekani" amesema Mhe. Samia.

Pamoja na hayo, Mhe Samia Suluhu amesema kuwa serikali imeongeza maradufu bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa viwango vinavyotakiwa nchini.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Graca Machel, Craca Machel wameipongeza serikali kwa jitihada inazozifanya katika uimarishaji wa sekta ya afya nchini na wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa ipasavyo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images