Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wananchi Jijini Mwanza Wafurika Ofisi Ya TRA Kulipia Kodi Ya Majengo

$
0
0
Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa wamepanga  foleni nje ya Jengo la Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Kanda ya Mwanza, kusubiri muda wao wa kwenda kulipia Kodi ya Majengo   ambayo leo Juni 30 ndio mwisho wa kulipia kwa wale ambao bado. 


Wahalifu Wanne Wauwawa Katika Mapambano Na Polisi Kibiti

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.

“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.

Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.

Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.

Utendaji wa Rais Magufuli waivutia serikali ya Norway

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Norway itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania hususani kuboresha huduma za kijamii na uwekezaji katika miradi mikubwa ya maendeleo.

Mhe. Borge Brende aliyeongozana na Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne-Marie Kaarstad amesema hayo leo tarehe 30 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Borge Brende amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kupambana na rushwa, kukabiliana na matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusimamia vizuri uchumi na shughuli za maendeleo na kwamba Norway inavutiwa na juhudi hizo na ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha zaidi juhudi hizo.

“Uhusiano wa Tanzania na Norway umedumu kwa miaka 55 na tumeshirikiana katika mambo mengi yakiwemo kuendeleza elimu na miundombinu mbalimbali na sasa tunatarajia kushirikiana zaidi na Tanzania kwa kuwekeza katika miradi mikubwa kama vile uzalishaji wa umeme, kuchakata gesi na kuzalisha mbolea” amesema Mhe. Borge Brende.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya Norway kwa mchango wake mkubwa ilioutoa kwa Tanzania tangu uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi uanze na amesema Serikali ya Awamu ya Tano inakaribisha ushirikiano zaidi na Norway hasa uwekezaji utakaokuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

“Hivi sasa tumedhamiria kujenga mradi wa kuzalishaji umeme kwa kutumia maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), lakini pia nchi yetu ina vyanzo vingine vya kuzalisha umeme kama vile maporomoko ya maji katika mito mingine, gesi ambayo mpaka sasa tumegundua futi za ujazo zaidi ya Trilioni 57, tuna makaa ya mawe, jua na upepo mwingi kwa ajili ya kuzalisha umeme, kwa hiyo tunawakaribisha wawekezaji kutoka Norway tushirikiane kuwekeza kwenye maeneo hayo” Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 1

TCRA yapiga marufuku matangazo kwenye miito ya simu

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku matangazo ya biashara yanayowekwa mtumiaji anapopiga simu ili kutoa fursa kwa watumiaji kupata mawasiliano bila usumbufu.

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema jana (Ijumaa) kuwa mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa simu wakilalamikia matangazo hayo yanayotolewa na kampuni za simu.

Amesema tayari TCRA imeshaziandikia barua kampuni zote za simu kusitisha matangazo hayo na itakutana nazo kwa majadiliano ya kina Julai 6.

Amesema mamlaka haitambui utaratibu huo na inauchukulia kama kero kwa watumiaji wa simu ambao hutegemea kutumia njia hiyo ya mawasiliano kurahisisha mambo.

“Tuna imani mtu anapopiga simu ana shida ya haraka na anahitaji afanye mawasiliano, unapomuwekea matangazo kwa dakika tatu au nne ni usumbufu,” amesema.

Katika siku za karibuni imekuwa ni kawaida kwa mtu anayepiga simu kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara na baadaye kuambiwa namba anayopiga haipatikani.

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?
 
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
 
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

Whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Ndugai Akerwa Kuitwa DHAIFU......."Mimi ndio Spika, nasema mwaka mtu hakanyagi hapa. Tutaona Dhaifu ni Nani"

$
0
0
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka kuwa wabunge wanaodai kuwa bunge ni dhaifu basi ni wazi watakuwa na mambo yanawasumbua ndio maana wanatoa kauli za kudhihaki chombo hicho.

Mhe. Ndugai amesema hayo jana mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge wanaotoa kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya bunge bila kufikiria kwamba wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa wapiga kura wao pamoja na kwa serikali kwa ujumla.

"Yupo mwenzetu alisimama hapa na kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa maoni yangu hizi ni lugha za kuudhi kwa sababu wenzako wengi namna hii waliochaguliwa na watu wakaletwa hapa halafu wewe unawaona kwa wingi wao ni dhaifu haipendezi. 

"Unajua sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa nafasi  mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako," alisema Ndungai

Pamoja na hayo, Ndugai ameendelea kwa kusema "Katika bunge letu kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia na lugha, tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale kwenye ulazima tutachukua hatua.

"...Unapomwita kiongozi ni dhaifu, maana yake unamlazimisha awe mkali, achukue hatua. 

"Naona wengine wanahaingaika sijui kufungua kesi....Lakini nasisitiza, Mimi ndio Spika, nasema mwaka mtu hakanyagi hapa"

==>Mtazame hapa Ndugai akifunguka zaidi.

Tundu Lissu Ahofia TLS Kufutwa......Aitisha Mkutano wa Dharula wa Wanasheria

$
0
0
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharula wa wanasheria nchi nzima kwa ajili ya kujadili mapendekezo na kutoa msimamo wao dhidi ya Serikali ya kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mawakili.

Akizumza jana  kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao za sheria.

Alisema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri itakavyoona inafaa.

"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa .

"Huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo  linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya" alisema Mh. Tundu Lissu.
 
Mbali na hayo Lissu aliwaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana ya  kuwepo kwa chama hicho.


UVCCM Wawabeza CCM.......Wadai Mzee Mwinyi Hakukosea Kutoa Maoni ya Rais Magufuli Kuongoza Milele

$
0
0
Ndugu Waandishi wa Habari
Kwa heshima kubwa tunawashukuru kwa dhati na kwa uungwana wenu wa kuitikia wito wetu wa kuwaomba  kuhudhuria mkutano wetu huu  ili kuzumgumza nanyi kama ilivyo ada na kawaida na hatimaye muweze kufikisha ujumbe wetu kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Ndugu Wandishi wa Habari
Itakumbukwa  kuwa hivi karibuni katika moja ya  Baraza la Idd El Fitri lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijijini Dar es Salam, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Mzee Ali Hassan Mwinyi, alitoa maoni yake binafsi  baada ya kuutazama, kuudurusu na kuridhika  na utendaji wa Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli.

Ni ukweli usiofichika  wala kupingika kuwa  maoni ya Mzee Mwinyi bila shaka yoyote yatakuwa yamepata mshawasha baada ya kuvutiwa mno na uchapakazi wa Rais Magufuli, pia maoni hayo hayakuwa ni uamuzi wala shuruti kama ambavyo baadhi ya watu walivyokishilia bango na kulishupalia suala hilo kwa mtazamo hasi.

Maoni ya Mzee Mwinyi yalikuwa bayana au kwa lugha nyingine  ni maoni mubashara yanayoweza kumlazimisha kila binadamu mwenye akili timamu afahamu kwa yakini alichotamka  katika matamshi yake. Alichosema au kushauri ni  jambo lenye  mantiki kulingana na mtazamo wake  ambao kwa hakika ulijiegemeza chini ya uhalisia wa mazingira ya nyakati na utendaji wa Rais Dk John Pombe Joseph  Magufuli  kwa kadri unavyoonekana.

Kwa bahati mbaya sana, eti wanaojiita ni wazee wa CHADEMA bila kufanya tafakuri, uchambuzi wa maana katika dhana kamili yenye uyakinifu wa jambo hilo, jana wakajikuta wakikurupuka, na kumuandama Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi bila ya kuwa na sababu za msingi kwa kumtolea maneno yasiyo na kichwa wala miguu.

Tokea Rais Dk  John Pombe Magufuli aingie madarakani baada  kuchaguliwa kidemokrasia na wananchi mwaka 2015, sasa yapata miaka miwili, utendaji wa Serikali yake ya awamu ya tano licha ya kumvutia kila mtanzania, umeitikisa na kuamsha mjadala nchini, Afrika Mashariki, Afrika na Dunia nzima .

Mjadala ni kuhusu kipimo cha utendaji wake unaochukua nafasi pana katika vichwa vya  Magazeti ya nje na ndani, kwenye vipindi vya runinga na mitandao ya kijamii,  Kitaifa na Kimataifa yote ikiwa ni katika kuutazama uadilifu wake, uwazi na  uwajibikaji wa Serikali yake chini ya misingi  ya uzalendo.

Watu mbalimbali wamekuwa wakijadili kutokana na kushawishika kwao Rais Magufuli kuhusu umakini alionao, uchungu kwa nchi yake na watu anaowaongoza akiwa na azma ya kupigania na kutetea maslahi ya umma huku akitaka rasilimali za nchi kuinufaisha nchi na watu.

Hakuna mtu au kiongozi  wa ndani au nje ya  chama tawala na nje ya nchi waliotumwa wajadili wanavyojadili iwe kwa kumpongeza na kumsifu kunakofanywa na watu hao.

*Ndugu Waandishi wa Habari*
Waswahili wa kale na wahenga wana semi mashuhuri isemayo“Kizuri hujiuuza na kibaya Hujitembeza”. Yaonekana ndivyo inavyotokea kwa walimwengu wanavyoutazama na kuufuatilia uongozi wa Awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli na Serikali yake katika mtazamo chanya wenye  mafanikio.

Alichokisema Mzee Mwinyi si kuwataka au kuwashawishi wananchi kufanya mabadiliko ya Katiba hatimaye kumpa nafasi ya vipindi vingine vya utawala Rais John Magufuli abaki madarakani kinyume na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Matamshi ya Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi aliyaweka bayana akiyatanguliza  utangulizi wa maneno adhimu na dibaji yaliosema nanukuulaiti nchi yetu isingelikuwa si yenye kufuata  utawala wa kikatiba, Rais Dk John Magufuli alitosha na kufaa  kuongoza nchi yetu kwa siku na miaka mingine.

Umoja wa Vijana ya CCM (UVCCM) hatuoni kama hilo ni kosa au baa, ama iwe mwao au uonekane  uchuro kutokana na maneno hayo. Mzee Ali Hassan Mwinyi ni mweledi, mlinzi mzuri wa Demokrasia na mtu anaheshimu Katiba, Katu hakusema na kutaka Katiba ibadilishwe ili Rais abaki madarakani kama inavyopotoshwa kauli yake.

Ndugu Waandishi wa Habari
Hata hivyo inaonyesha wanaojiita Wazee wa CHADEMA hawana kumbukumbu ya kutosha. Wamesahau   Rais wa Awamu ya Kwanza Baba wa Taifa marehemu  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitawala kwa kipindi cha miaka 23 tokea mwaka 1961 hadi mwaka 1985.

Mwalimu Nyerere hakutawala miaka 23 kwa lazima yake, nguvu za udikteta au kutumia misuli ya ubabe, alitawala  kwa matakwa, ridhaa, utashi na maamuzi ya wana nchi wenyewe  ndiyo waliomshinikiza na kumuomba kila wakati abaki madarakani kila alipopania kujiuzulu na kumpisha mtu mwingine.

Ifahakime kuwa Nchi yoyote na mahali popote, dunia inahitaji ipate mtawala na utawala wenye tija, manufaa na maendeleo yanayoonekana, kuwaridhisha au kuwapendezesha na kuwanufaisha wananchi.

Kushawishika na kuhamasika kwa wananchi na watu mbali mbali juu ya kazi nzuri inayofanywa na Dkt. Magufuli nadhani imewakumba mpaka Viongozi wenye nyadhifa mbali mbali katika Vyama Vya Siasa na makundi mengine. Mfano siku za karibuni  kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi na wanachama wa Chadema wakiwemo madiwani sita kwa hiari na ridhaa yao wameamua kuachia ngazi na kukikimbia Chadema wakirejea CCM kwa kuridhika, kutosheka na utendaji wa Serikali ya Rais Dk John Magufuli.

Wanaojiita Wazee wa Chadema ingelipendeza sana kama wangekuwa na mapenzi na chama hicho wangalikaa chini kutafakari na kutathmini sababu ipi inayowafanya wanachama, viongozi waandamizi  na madiwani hasa katika Mkoa wa Arusha wakikimbie chama hicho na kurejea CCM badala ya wazee hao kucheza ngoma isiowahusu.

Ndugu Waandishi wa habari
Wote hapa tunaelewa Katiba ya nchi si Quran wala Bibilia. Katiba imetungwa kutokana na maoni, weledi na utashi wa watu. Na watu hao hao kwa kujali  kwao mahitaji na matakwa yao,  wanaweza kugeuza chochote ndani ya katiba kwa kujali maslahi yao na wala  isiwe baa au muujiza.

Umoja wa Vijana wa CCM unaamini ukishafikia hatua ya uzee wakati mwingine unapoteza kumbukumbu muhimu, tunawakumbusha wanaojiita wazee wa CHADEMA hakuna ushahidi  unaoonyesha  Mzee Mwinyi aliwahi kuwa na mpango wa kutaka kujiongezea muda ili abaki madarakani kama ilivyodaiwa na genge la Wazee hao. Kama mjuavyo kule Chadema kuna maprofesa wa kuzua hili nalo Mzee Mwinyi wamemzulia na kumpakazia.

Ingalikuwa Mzee Mwinyi alitamani kujiongezea muda ili aendelee kubaki madarakani kwa wakati ule, angeweza kwa sababu uongozi wake uliwakuna na kuwapendezesha mno wananchi mijini na vijijini na wala isingelikuwa ni kazi kubwa ya kukubalika na kuungwa mkono .

Zipo semi na hadithi nyingi zinazodai Mwalimu Nyerere katika Kitabu chake cha Tanzania na Hatma ya Uongozi alikiandika kwa lengo la kuwalenga viongozi  aliowakusudia kuwapasha na kutaka wajisahihishe, kujisuta, kujiuzulu au kujirejebisha.

Ukweli ulivyo  si hivyo, Mwalimu kama Mwalimu kitaaluma  aliandikia Kitabu chake kwa msukumo wa maono yake ili kuiasa nchi yetu, viongozi wa sasa na wajao pia kuitazama hatma ya nchi yetu kiutawala, kidemokrasia na kiutendaji bila kumlenga au kumdhamiria yeyote kama inavyodaiwa na makuhani wa kuzua.

Ndugu zangu Waandishi wa habari.
Mtu mwerevu siku zote  anapotaka kumuasa mwenzake atoe kibanzi katika jicho lake, kwanza huanza kutoa yeye boriti katika jicho lake. Kama tujuavyo Katiba za baadhi za vyama vya Siasa vikiwemo vile vya Ukawa. Katiba zao zinalalamikiwa kwa madai ya kuwa na udikteta.

Tumeshuhudia mivutano ikirindima  ndani ya vyama hivyo huku viongozi wa Vyama hivyo wakigombana kwa sababu ya kulinda matakwa ya Katiba zao na baadhi yao wamekuwa ni zaidi ya wafalme na masultani waliojenga  himaya ndani ya Vyama vyao huku wakiwa hawana ndoto wala  fikara ya kuachia madaraka.

Wapo wanachama wengine wamefukuzwa na hata kuvuliwa uanachama ndani ya vyama vya upinzani kwasababu  ya kutaka kuwania nyadhifa za juu ambazo wakubwa hawataki ziguswe kwakuwa kushika nafasi hizo  ni kunagusa maslahi yao.

Wengine wanadaiwa kupoteza maisha katika mazingira ya kutatatanishi kwa kujaribu kwao kuchukua fomu za kuwania nafasi za juu huku wagombea urais wengine waliohama toka vyama vingine walipojiunga na vyama hivyo nyakati za asubuhi, jioni yake wakapitishwa kwa mbwembwe  kuwa wagombea urais kinyume na matakwa ya Katiba zao .

Ndugu Waandishi wa Habari
Mwisho Umoja wa Vijana wa CCM  tunawataka wazee maslahi wa Chadema waache kulishwa maneno na kuwa wazushi na waongo, waache papara ya kujibu kila wanachokisikia kwa kuchochewa na ushabiki baada ya kuoayiwa milungula na bahashish na kukimbilia  kuwadhalilisha viongozi waliolitumikia Taifa hili kwa uadilifu na bidii na juhudi huku wakiongoza nchi kwa  hekima, busara   kubwa zilizosaidia kuleta mageuzi kadhaa  ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yalioacha alama ya utumishi wao uliotukuka kwa watanzania.

Tunaendelea kuwaaminisha watanzania Chama Cha Mpainduzi ni chama kikubwa ndani Afrika na duniani kwa ujumla hivyo siku zote hakifanyi makosa katika kuwaletea viongozi makini, wenye upeo na uweledi wa hali ya juu.

Ahsanteni

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

Mafuta yashuka bei. Hizi ndizo bei zilizoanza kutumia leo Julai 1, 2017

$
0
0
Licha ya Serikali kuongeza kodi ya Sh 40 kwa kila lita ya mafuta, bei nchini imeshuka ikilinganishwa na zile za Juni 7 mwaka huu, ambapo kwa sasa bei ya petroli kwa lita imepungua kwa Sh 37, dizeli kwa Sh 14 na mafuta ya taa kwa Sh 19 kwa lita.

Akitangaza bei mpya ya mafuta Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Godwin Samwel, alisema kuwa katika mwaka uliopita wa fedha, kodi ya serikali kwenye mafuta ya petroli kwa lita ilikuwa Sh 339, mafuta ya dizeli Sh 215 na mafuta ya taa Sh 425.

Kaguo alisema kwa sasa kodi ya mafuta ya petrol, itakuwa ni Sh 379, mafuta ya dizeli Sh 255 na mafuta ya taa Sh 465 kwa lita. 

Hata hivyo, Kaguo alioa onyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta ambao walihodhi kwa ajili ya kupandisha bei mafuta hayo kuanzia leo, kwamba lengo lao halijatimia, kwa kuwa bei zilizotangazwa ndizo zinazotakiwa kuanza kutumika.

==>Tazama beo zote kwa kila mkoa hapo chini

Mradi Wa Umeme Stiegler’s Gorge Hautaathiri Mazingira Ya Pori La Selous

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Katavi
Wizara ya Maliasili na utalii imewataka wadau wa uhifadhi kote nchini kuunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji kwenye pori la akiba la Selous ambao ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,100.

Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi amesema utekelezaji wa mradi huo wa umeme ni wa muhimu kwa taifa kwani  utasaidia kuharakisha maendeleo ya taifa kuelekea azima yake ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.
 
Akiongea wakati akifunga mafunzo ya askari wa wanyamapaori kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania -TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu mkuu Meja Jenerali Gudance Milanzi amesema mradi huo wa umeme pamoja na mradi wa bwawa la maji la Kidunda utachukua eneo dogo tu la pori la akiba la Selou lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba elfu 50.
 
Amesema pori hilo ndilo kubwa miongoni mwa mapori ya aina hiyo ulimwenguni na ukubwa wake ni zaidi ya nchi za Rwanda na Burundi zikiunganishwa kwa pamoja.
 
Katibu Mkuu amesema ujenzi wa miradi hiyo hauna tafsiri kwamba Tanzania haithamini masuala ya uhifadhi bali unazingatia uhifadhi wenye manufaa kwa jamii na maendeleo ya taifa na hasa dhamira ya serikali ya rais Dk John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda ambayo inahitaji nishati ya umeme itakayoyotosheleza mahitaji ya taifa.
 
Amesema Tanzania inatambua umuhimu wa uhifadhi ndiyo maana imetenga eneo la zaidi ya asilimia 28 ya eneo lote la nchi kavu Tanzania bara kwaajili ya uhifadhi wa aina mbalimbali ukiwemo wa wanayamapori na misitu ya vyanzo vya maji ambayo ni muhimu kwa shughuli za kijamii na kiuchumi, “ ni nchi chache sana duniani zenye eneo kubwa la uhifadhi kama Tanzania” alisisitiza katibu mkuu.
 
Katibu mkuu amewataka wafanyakazi wa wizara na watanzania kwa ujumla kutokuwa kikwazo kwa utekelezaji wa mradi huo na kwamba wadau wanaotaka kuisaidia Tanzania wasaidie kuhakikisha inatumia maliasili zake kupiga hatua ya kimaendeleo ikiwemo misaada ya teknolojia za kisasa na rafiki wa mazingira kusaidia kufikia malengo yake kimaendeleo.
 
“Mtakumbuka mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli hivi karibuni alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani amezungumzia kwa kirefu sana umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo wa bwawa la Kidunda na wa umeme wa Stieglars Gorge, sasa sisi kama wahifadhi na kama watumishi lazima tumuunge mkono na tusiwe kikwazo katika dhamira hii njema” alisema Jenerali Milanzi’’.
 
Ametoa mfano wa nchi ya Qatar ambayo amesema ilikuwa na eneo la uhifadhi lililokuwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia kutokana na uwepo wa baadhi ya viumbe adimu lakini walipogundua mafuta, waliamua kujitoa kwenye urithi wa dunia ili wachimbe mafuta na kuinufaisha nchi hiyo na maendeleo ya wananchi wake.
 
Akizungumzia kuhusu tatizo la mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, Katibu mkuu amewataka wahifadhi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo na kusimamia sheria zilizotungwa na Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zinakataza mifugo kuingia hifadhini kinyume cha sheria.
 
Amesema ndiyo maana serikali inatumia fedha nyingi kugharamia mafunzo ya askari wa wanyamapori na wahifadhi ili kuwaongezea ujuzi na weledi wa kulinda maliasili za taifa kwa kuzingatia sheria zilizopo.
 
Katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudance Milanzi amezungumzia pia umuhimu wa kuhakikisha mapori ya uhifadhi yanatumiwa kwa uhifadhi badala ya kutumika kwa mambo mengine ikiwemo kilimo cha bangi na maficho ya majambazi na majangili na amewataka wahifadhi na askari kushirikiana na vyombo vingene vya ulinzi na usalama kuwafichua wahalifu wanaojificha kwenye mapori hayo na kufanya ujangili na uhalifu mwingine.
 
Mapema katika taarifa yake kwa katibu mkuu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania -TAWA Martin Loibooki alieleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuimarisha uhifadhi kwenye mapori mbalimbali ya akiba nchini na maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori.
 
Aliwashukuru wadau mbalimbali wa uhifadhi wa ndani na nje ya nchi wanaofadhili mafunzo hayo na vitendea kazi juhudi ambazo amesema zimeanza kuzaa matunda ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya tembo na wanyamapori wengine kwenye mapori mengi nchini.
 
Mfunzo hayo yaliyowashirikisha askari wa wanyamapori wapatao 98 kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Maliasili na utalii kwa askari wa wanyamapori na watumishi wengine wa wizara hiyo katika hatua za kuelekea mfumo wa jeshi usu.

Rais Magufuli Awapongeza Watanzania Kwa Kujitokeza kwa Wingi Kulipa Kodi ya Majengo

$
0
0
Rais John Magufuli amewapongeza Watanzania kwa mwamko waliounyesha wakati wa ulipaji wa kodi ya majengo.

Akizungumza leo (Julai 1) wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Rais amesema  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilipochukua jukumu la kukusanya kodi hiyo imewezesha wananchi kulipa kodi kwa amani.

“Walipochukua TRA, sasa waliwathaminishia kodi ambayo wananchi wanaweza kuilipa, ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi. Haijapata kutokea wananchi wakataka kulipa kodi kwa kiasi kile, ni kwa sababu ilikuwa nafuu kwao,” amesema

Pia, Rais amewataka TRA kuendelea kukusanya kodi kwa njia ambazo ni rafiki kwa kuwa wananchi hawapendi kodi inayowaumiza bali kodi ambayo ni sahihi kwao.

“Wananchi wanapenda kulipa kodi  lakini iwe na manufaa kwako,” amesema

Rais Magufuli amuweka njia panda Chiza

$
0
0
Rais John Magufuli  ameshangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara nchini Christopher Chiza kuwa na mipango ya kujenga majengo mapya kwa ajili ya wafanyabiashara badala ya viwanda vitakasaidia nchi.

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, Rais Magufuli amesema kwamba ameshangazwa sana na mipangio ya kujenga mahoteli pamoja na kufanyia ukarabati wa majengo kwani hajui mahali pesa hizo zitakapopatikana.

"Mh. Chiza amezungumza kubadilisha majengo na kujenga mapya, mawazo mazuri lakini najiuliza hizo hela zimetoka wapi , haingii akilini wao ndio wanatusisitizia mambo ya biashara na viwanda na 'theme' ya mwaka huu inazungumzia kukuza biashara na maendeleo ya viwanda sasa wao badala ya kuzungumza juu ya maendeleo ya viwanda wanataka wajenge Hotel hapa, watengeneze majengo mapya sasa. Sijaelewa, sasa kama hizo hela zipo basi mzipeleke mkajenge kiwanda cha mfano

Aidha Rais magufuli amesisitiza kwamba  "Haya majengo yaliyopo ambayo mnayaona yamechakaa hawa wanaokuja kuonesha bidhaa zao wapeni bure wajenge ili kila mwaka wawe wanaonesha, hiyo Hoteli kwani mkijenga lazima walale hapa hapa? Mnaweza kujenga hoteli hapa bado wakaenda mjini.  Mimi nilifikiri badala ya  kujenga jenga majengo fikirieni zaidi katika kujenga viwanda kwa ajili ya mfano wa kuonesha Wizara kweli iko mbele kwa ujenzi wa viwanda.

Katika kuonyesha nia ya kufikia Tanzania ya viwanda inafikiwa Rais ameitaka wizara pamoja na bodi hiyo kutofikiria ujenzi wa majengo.

"Mwenyekiti nimekuteua juzi umeshaanza kufikiria majengo hapa pamoja na Bodi yako mnanifanya nifikirie zaidi. Haya majumba yanaweza yakawa siyo mazuri sana lakini ni mazuri kwa watu wa Tanzania ambao wanataka kuona bidhaa. Yanayowaleta hapa siyo majumba Watanzania wanakuja hapa kuangalia Teknolojia na vifaa vilivyomo.Inawezekana mimi nipo tofauti mnisamahee lakini katika muelekeo wangu ninaona hizo hela mnataka kuzitumia vibaya" Rais alisisitiza.

Pamoja na hayo Mh. Rais amewaomba waandaji wa maonyesho hayo pamoja na Waziri wa viwanda na biashara Mh. Charles Mwijage  kuongeza siku zaidi katika maonesho ili watanzania waweze kupata muda mzuri wa kununua na wafanyabiasha kuuza ambapo ombi lake lilikubaliwa hapo hapo na kuongezwa siku tano mbele.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 2

Polisi Watangaza Majina Ya Watuhumiwa 16 Wa Mauaji Yanayoendelea Kibiti, Mkuranga Na Ikwiriri

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Yussuf Masauni ametangaza kuwa, Jeshi la Polisi linawasaka watuhumiwa 16 wa mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea kufanyika katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani kwa muda mrefu sasa.

Masauni amesema jeshi jilo litatumia nguvu zote inazoweza kuweza kukomesha mauaji hayo ili wakazi wa eneo hilo waweze kuishi kwa amani na kurudi kwenye maisha yao ya kila siku.

Akitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa hao wanaotafutwa alisema ni pamoja na Hassan Haruna Kyakalewa Shujaa, kutoka Ikwiriri mwenye umri kati ya miaka 25-35. Mwingine ni Omari Abdallah Matimbwa.

Wengine  wanaosakwa na jeshi hilo ni, Anafi Rashid Kapera kutoka Kibiti mwenye miaka kati ya 25-30 mrefu wa wastani, mwenye uso wa mviringo na wa mwisho ni, Faraji Ismail Nangalava kutoka Kibiti mwenye kati ya miaka 25-35.

Masauni aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Jeshi la Polisi lina picha za watuhumiwa wote wanaotafutwa.

Aidha Jeshi la Polisi lilisema kuwa, zawadi nono itatolewa kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.

Norway Yaipatia Tanzania Msaada Wa Dola Milioni 10.5 Kuboresha Elimu

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Norway imeipatia Tanzania msaada wa Dola Milioni 10.5 za Marekani kupitia programu ya miaka mitatu ya maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, inayotarajiwa kuanza Mwaka Mpya wa Fedha- Julai Mosi mwaka huu.

Mpango huo pamoja na uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, umezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo kwa niaba ya Serikali zao.

Dkt. Mpango ameishukuru Serikali ya Norway kwa msaada huo mkubwa utakaochangia kuboresha utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuijengea uwezo zaidi wa kitaalamu, miundombinu na vitendeakazi vingine vitakavyo changia kuongeza uwezo wa Mamlaka hiyo wa kukusanya mapato ya Serikali.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo amesema kuwa hatua ya Serikali ya Norway kuendelea kufadhili programu ya pili ya Mpango wa kuendeleza Sekta ya Mafuta utaiwezesha Serikali kubobea katika masuala ya utaalamu wa masuala ya sheria na usimamizi wa sekta hiyo.

Nae Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende amesifu utendaji kazi mahili wa Mhe. Rais Dokta John Pombe Magufuli wa kupambana na ufisadi na vitendo vya rushwa pamoja na kuimarisha ukusanyaji kodi, hatua ambayo itaifanya nchi ipige hatua za maendeleo haraka.

Amesema kuwa hajawahi kuona nchi yoyote duniani ikiendelea bila kuweka nidhamu na uwajibikaji serikali pamoja na kutokusanya mapato yake ipasavyo na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano kufanikisha mipango yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.

LAPF Yaibuka Kidedea Katika Mifuko Ya Kijamii Kwenye Maonyesho Ya Sabasaba

$
0
0
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pension wa LAPF Bwana James Mlowe akipokea tuzo kutoka kwa Rais JP Magufuli baada ya LAPF kuwa mshindi wa Kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika kategori ya mifuko ya Hifadhi ya jamii, Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage Mapema  jana Jijini Dar es salaam.

Meneja masoko na mawasiliano wa Mfuko wa Pension wa LAPF Bwana James Mlowe Akipokea tuzo kutoka kwa Rais wa JP Magufuli baada ya LAPF kuwa mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba Mapema  jana  Jijini Dar es salaam.
 Tuzo ya Mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika viwanja vya Mwl JK Nyerere barabara ya Kilwa DSM. Tuzo hii ilikabidhiwa kwa Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Raisi Dr. John Pombe Magufuli Mapema  jana Jijini Dar es salaam.
 Rehema Mkamba afisa mwandamizi masoko na mawalisiliano Bi Rehema mkamba akoionyesha tuzo baada ya LAPF Kuibuka mshindi wa kwanza katika kategori ua mifuko ya hifadhi ya jamii na bima kwenye maonyesho ya 41 ya sabasaba 2017 Mapema  jana Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa LAPF nje ya banda lao wakifurahia tuzo yao ya kuwa mshindi wa kwanza kategori ya mifuko ya Pensheni na Bima katika maonyesho ya 41 ya sabasaba waliyokabidhiwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk John Pombe  Magufuli

Kamati ya utendaji ya TFF yakutana, yatoa maamuzi magumu kuhusu Malinzi

$
0
0
Kamati Kuu ya Utendaji ya TFF imekutana jana  na kutoa maamuzi ya kuwasimika viongozi wa muda ambao wataziba nafasi zilizoachwa wazi na Rais wa Shirikisho hilo, Jamali Malinzi na Katibu mkuu wake Selestine Mwesigwa.

Aidha, majina yaliyopitishwa ni pamoja na Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa Shirikisho hilo huku Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi akiteuliwa  kuwa Kaimu Katibu Mkuu.

Kamati hiyo imesema kuwa viongozi hao walioteuliwa watakaimu nafasi hizo mpaka pale mahakama itakapotoa maamuzi ya kesi inayowakabili Rais wa Shirikisho hilo, Jamali Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa.

Waziri Mkuu Atangaza Kiama Kwa "Mchwa" wa Ushirika

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhilifu wa mali za fedha za Ushirika nchini.

“Kwa Serikali hii ya awamu ya Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”.

 Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Julai Mosi, 2017), katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD), iliyoadhimishwa kitaifa mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Alisema miongoni mwa changamoto zinazoukabili Ushirika nchini ni pamoja na wizi na ubadhilifu wa rasilimali za Ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wasiokuwa waaminifu.

 Waziri Mkuu alisema changamoto nyingine ni baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika kutoheshimu miongozo ya vyama vyao na kujifanyia mambo kwa maslahi yao binafsi.

Alisema katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake na kuweka mazingira rafiki ya kustawisha Ushirika nchini ili kutoa fursa ya Ushirika kushamiri na kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi yao.

“Haikubaliki hata kidogo kuona sekta hii inayosadifu maisha ya Mwafrika hamnufaishi ipasavyo , hivyo naelekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ihakikishe kuwa vyama vya Ushirika vinaendeshwa kisayansi na kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Pia alizielekeza Kamati za Ushauri za Mikoa na Wilaya nchini, ziingize agenda ya Maendeleo ya Ushirika kama moja ya agenda muhimu inayopaswa kujadiliwa na kuwekewa maazimio ya utekelezaji. Pia wawe na takwimu za vyama vya Ushirika na Wanaushirika.

Hata hivyo Waziri Mkuu alizielekeza mamlaka zote zinazohusika na Ushirika nchini zijiwekee malengo yanayopimika ya namna ya kuboresha sekta ya Ushirika.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alielekeza kwamba masuala yote yanayohusu Ushirika wa kilimo nchini lazima yaratibiwe na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Aidha, Waziri Mkuu alizielekeza Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zifanye mapitio kubaini elimu na ujuzi katika ngazi zote za Ushirika kwa ajili ya kuwaandalia kozi za muda mfupi za kuongeza ujuzi au kubainisha aina ya watumishi wanaohitajika kwenye sekta hiyo.

Pia aliwaagiza Maofisa Ushirika nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri uchanguzi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kuwaondoa wagombea wote waliowahi kuwa viongozi, ambao waliondolewa madarakani kutokana na ubadhilifu wa mali na fedha za Ushirika.

Awali, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alisema wizara itaendelea kusima na kuchukua hatua kwa viongozi wote wa vyama vya Ushirika watakaobainika kufuja mali na fedha za Ushirika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.

Serikali Yawataka Wataalam wa Mikataba Kuwa Wazalendo

$
0
0
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO
Wataalamu wa majadiliano ya mikataba wametakiwa kuweka maslahi ya Taifa mbele wanapoandaa mikataba ya kimataifa ili kulinda na kusimamia raslimali za nchi.

Wito huo umetolewa jana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerson Mdemu wakati akifunga mafunzo ya maafisa waandamizi wa serikali za nchi tisa za kiafrika kuhusu majadaliano ya mikataba ya kibiashara ya kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mdemu aliwasititiza washiriki wa mafunzo hayo kutumia ujuzi walioupata kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika kwa majuma mawili kwa ajili ya maslahi ya nchi zao ili kulinda raslimali  za nchi husika ili zitumike kwa manufaa ya umma.

“Tangulizeni maslahi ya nchi na si ya kwenu binafsi katika mikataba ya kimataifa na kuondokana na vitendo vya rushwa”, alisema Mdemu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mafunzo wa Uongozi Institute, Kadari Singo amesema mafunzo hayo yameandaliwa kutokana na nchi za kiafrika kuwa nyuma katika majadaliano ya mikataba ya kimataifa.

“Tumeamua kufanya mafunzo haya kuwafundisha maafisa waandamizi toka nchi za kiafrika ili kuwapa ujuzi na utaalamu wa kufanya majadiliano ya mikataba ili iweze kuwa na manufaa kwa nchi husika”, alisema Singo.

Kwa mujibu wa Bwana Singo, mafunzo ya aina hiyo yatakuwa endelevu kwa watumishi wa Serikali ii kuiwajengea uwezo katika eneo hilo na yatakuwa yakifanyika kujumuisha wataalam wa sekta husika kama vile, sekta madini, misitu, wanyamapori na sheria.

Aidha, Singo alisema mafunzo haya yatahakikisha yanapinga vikali vitendo vya rushwa kwenye mikataba ili kuzinusuru nchi za kiafrika kutumbukia katika mikataba isiyowanufaisha wananchi.

Mafunzo haya yameandaliwa na Uongozi Institute na yamewajumuisha watumishi wa serikali waandamizi kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Kenya, Ghana, Nigeria, Uganda, Namibia na wenyeji Tanzania.

Hivi karibuni, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wakati akipokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa madini alimtaka Spika wa Bunge kutumia Bunge lake kupitia sheria za madini ili kuhakikisha sheria hizo zinaleta manufaa kwa wananchi.

Mikataba ya madini na mali za asli nyingine imekuwa ikipigiwa kelele kuwa haina lengo la kuinufaisha nchi bali watu wa nchi nyingine. Hivyo Miswada ya Maliasili za nchi imepelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharula ili kutoa nafasi ya kutunga sheria mapema iwezekanavyo za kuleta manufaa na tija kwa nchi hasa kupitia madini na maliasili nyingine zikiwemo mbuga za wanyama na hifadhi nyingine za Taifa.

Kwa kuzingatia unyeti na umuhimu wa suala hilo, muda wa kumaliza Bunge umeongezwa badala ya kumaliza Juni 30 sasa litaenda hadi Julai 5, 2017.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images