Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tamko la CHADEMA Kuhusu Kauli ya Mzee Mwinyi Kwamba Magufuli Awe Rais wa Tanzania Milele

$
0
0
Chadema imelaani vikali kauli ya Rais wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi aliyesema kuwa kama siyo matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote.

Kiongozi huyo wa awamu ya pili ambaye alikuwa akizungumza kwenye swala ya Eid El Fitri alidai pia laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa urais, amengemshauri Rais Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote.

Akizungumzia kauli hiyo katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni, leo (Alhamisi) Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee, Roderick Lutembeka amesema matamshi hayo yanapaswa kukemewa kwa vile yanaashiria kulipeleka Taifa kuandaa viongozi watakopuuza Katiba ya nchi.

“Sisi wazee wa Chadema kwa kutambua madhara ya kauli kama hizi tumeamua tusikae kimya kwani  kauli hiyo inakiuka Katiba ya nchi inayoweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko kama ambavyo imetokea kwa nchi jirani zilizopuuza uvunjifu wa katiba,” amesema.

Amewataka Watanzania kwa ujumla kujitokeza na kupinga kauli za namna hiyo ambazo alisema zinajaribu kuwaandaa wananchi kisaikolojia ili kuwa na viongozi watakaopindisha Katiba katika siku za baadaye.

==>Msikilize hapo chini akiongea

Freema Mbowe: Polisi Msituzibe Midomo

$
0
0
Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelitaka jeshi la polisi nchini kutowafunga midomo na kusema kitendo cha jeshi hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati wakifanya kazi yao si sawa.

Freeman Mbowe amesema hayo leo Alhamisi  baada ya jeshi la polisi kuwafukuza waandishi wa habari ambao walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya Polisi ambapo leo alikwenda kuitika wito wa jeshi hilo baada ya juzi kutoa maelezo na kutakiwa kufika leo tena.

Mhe Edward Lowassa alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi siku ya Jumanne tarehe 27 kufuatia kauli zake alizozitoa ambazo zinasemakana kuwa ni uchohezi

Lowassa juzi alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa muda wa masaa manne, kisha baada ya hapo alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kufika siku ya Alhamisi ya tarehe 29 Julai 2017 ambapo amefika na kuambiwa uchunguzi wa jambo lake haujakamilika hivyo arudi tena tarehe 13 Julai 2017.  


==>Msikilize hapo chini akiongea

Mkurugenzi wa Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amtoa Machozi Rais Magufuli......Ni Baada ya Kufariki Ghafla Akiwa Ofisini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Joseph Pombe Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa benki ya AFDB Dkt Tonia Kandiero kilichotokea usiku wa jana, na kusema kwamba ni mtu aliyechangia maendeleo Tanzania.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo za rambirambi kwa Rais wa benki hiyo Akinwumi Adesina na kusema kuwa Dkt Tonia atamkumbuka kama hodari na mchapakazi katika kipindi cha uhai wake na kwamba kwa kushirikiana kwao kulifanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa iliyokuwa chini ya ufadhili wa AFNB.

Kifo cha Dkt Tonia kimetokea usiku wa jana Juni 28 alipokuwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika kusini.

==>Hapo chini ni taarifa ya IKULU 

CCM Walaani Matamshi ya Lowassa......Waitaka Serikali Imchukulie Hatua

$
0
0
Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kauli za kichochezi na zakidini zilizofanywa na mmoja kati ya mwanasiasa nchini, zenye lengo la kuwafitinisha watanzania.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM ndugu Humphrey Polepole amebainisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, huku akiiomba serikali ikithibitika mtu amekosea serikali isiwe na ajizi kuchukua hatua kwa aina ya mtu huyo.

Siku ya Jumanne na leo Alhamisi,  aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amehojiwa na Jeshi la Polisi kwa kilichodaiwa kuwa ni maneno ya kichochezi aliyoyatoa kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati alipohudhuria Futari iliyokuwa imeandaliwa na Mbunge Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.

Katika hatua nyingine, Polepole amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaunga Mkono Kauli ya Rais Magufuli ya kutorudi masomoni kwa wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shule kwenye mfumo rasmi wa Elimu.

Polepole amesema kuwa wanafunzi waliopata ujauzito hawataweza kurudi shuleni kwenye mfumo rasmi isipokuwa kwenye Mfumo wa elimu ya watu wazima.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 30

Kisukari Ni Ugonjwa Unao Weza Kudhibitiwa Kwa Kutumia Tiba Asilia

$
0
0
Kisukari  ni  tatizo  la  kiafya  linalo wasumbua  na  kuwatesa  mamilioni  ya  watu  duniani. Miongoni  mwa  dalili  za  ugonjwa  wa  kisukari ni pamoja  na

i. Kukojoa  mara  kwa  mara  ( Watoto kukojoa  kitandani )

ii.Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.

iii.Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.

iv.Kupungua uzito  kwa  kasi  au kukonda pamoja na kwamba unakula  vizuri  tena kila  wakati  kwa  sababu  ya  kusikia  njaa kila  wakati  kunakosababishwa  na  maradhi  ya  kisukari

v.Wanawake  kupatwa  na  tatizo  la kuwashwa ukeni.

vi.Kupoteza  uwezo  wa Kuona  vizuri.

vii.Wanaume  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu na / ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  na  wanawake  kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa.

viii.Kupatwa  na  ganzi,  kusikia  hali  ya  kama  kuchomwachomwa au kutohisi chochote  pindi  unapoguswa  kwenye  sehemu za miguu, viganjani na  kwenye  vidole.

ix.Miguu kuoza na hata kupata gangrini.

x.Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.

xi.Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.

xii.Kutokwa  na   Majipu kwenye  sehemu  mbalimbali  mwilini.

Kwa  mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu , watu walio katika makundi yafuatayo  wapo katika  hatari  kubwa  ya  kupatwa  na  ugonjwa wa kisukari kuliko watu wengine.  Watu  hao  ni  kama  ifuatavyo :

i. Watu  wenye   uzito uliozidi,

ii.Watu  wanao  toka  katika  familia  zenye  historia  ya  kuwa  na  wagonjwa  wa  kisukari.

iii.Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

iv. Watu   wasio  fanya  mazoezi

v. Wagonjwa  wa  shinikizo la damu,

vi.Watu wenye  kiasi  kikubwa  cha  lehemu  mbaya  ( Bad  Cholestrol ) kwenye  damu.

vii.Watu  wenye   virimba  tumo (  vitambi):  Wataalamu  wa  afya  wanaeleza  kuwa, kuna hatari kubwa ya kupatwa na maradhi  ya  kisukari ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu

viii.Watu  wenye msongo wa mawazo na

ix.Watu  wanao tumia  pombe  na kupita  kiasi  pamoja  na  wale  wavutaji  wa  sigara  kupita  kiasi: Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa  na  tatizo  la  kisukari,kwani kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu, uvutaji  sigara huathiri  moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu.  Tafiti  mbalimbali  za  kiafya  zinaeleza  kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

x. Kundi  jinginge  la  watu  walio  katika  hatari  ya  kupatwa  na  maradhi  ya  kisukari  ni  watu wenye  umri  mkubwa  kuanzia  miaka  55  na  kuendelea

Wataalamu  wa  afya  wanashauri  watu walio  kwenye   orodha  iliyo  tajwa  hapo  juu, kujiwekea  utaratibu  wa  kuwa  wanapima  afya  zao  walao  mara  moja  kila  mwakaili waweze  kuchukua  hatua  stahiki  za  kiafya endapo  watakutwa  na  tatizo  la  sukari.
TIBA   ASILIA   KWA   WAGONJWA   WA  KISUKARI
Zipo  tiba  asilia  mbalimbali  zinazo  saidia  kkupunguza  maradhi  ya  kisukari. Miongoni  mwa  tiba  hizo  ni  pamoja  na  tiba  ijulikanayo  kama  Mkatasukari. Tiba  hii  inasaidia kushusha  na  kudhibiti  kiwango  cha  sukari  kwa  mgonjwa mwenye  sukari  ya  kupanda. Kama  unasumbuliwa na  maradhi  ya  kisukari ( Sukari  ya  kupanda ), unaweza  kujaribu  kutumia  tiba  hii.

JINSI   YA   KUANDAA  TIBA  ASILIA  YA  MKATASUKARI

Mahitaji  ;
i. Nanasi  moja  kubwa

ii. Majani  ya  chai  vijiko vitatu vya  chakula

iii. Maji  lita  tano

iv. Dawa asilia  ya  Mkatasukari  vijiko  vikubwa  vitatu.

MATAYARISHO:  Chukua  nanasi  lako  lililo  iva  vizuri, limenye  kisha  likate  vipande  vidogo vidogo,  kisha  liweke  kwenye  sufuria  halafu ndani  ya  sufuria  hilo, ongeza  lita  tano  ya  maji  safi.  Baada  ya  hapo  weka  majani ya  chai vijiko  vikubwa  vitatu, kisha  ongeza  vijiko  vikubwa vitatu  vya  dawa asilia  ya  Mkatasukari, kisha  chemsha  kwa  muda  wa  dakika  thelathini (30).

Baada  ya  dakika  thelathini, ipua   na  uchuje, makapi  weka  pembeni, kisha  hifadhi  kimiminika  chako  kwenye  chombo  safi.

MATUMIZI  :
Tumia  kunywa  kikombe  kidogo chenye ujazo milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills ) au  robo  lita  kwa  lugha  nyepesi. Utafanya  hivyo  mara  tatu  kwa  siku, asubuhi  mchana  na  jioni  hadi  dozi  yako  itakapo  kamilika.

Baada  ya  kutumia  dozi  hii, unashauriwa  kwenda  hospitali  kupima   tena  sukari  ili  ujue  sukari  yako  imeshuka  kwa  kiasi  gani  pamoja  na  kupata  ushauri  wa  daktari  wako.

Kwa  mahitaji  yako ya  tiba  asilia  ya  Mkatasukari, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM,  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini DAR  ES  SALAAM, ambao  hawawezi  kufika  ofisini kwetu., tunatoa  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY ), kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  watasafirishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti, kwa  wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabasi mbalimbali. Wateja  waliopo NAIROBI  na  MOMBASA  watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  usafiri  wa  mabasi  mbalimbali.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83 84

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu ;

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?
 
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
 
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

Whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Mwalimu Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanafunzi Darasani

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku.

Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.

"Kuanzia wanafunzi waliotimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee kushikiliwa .Huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi" alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge

Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya sanaa.

Jipatie Dawa za Asili za Kuongeza Maumbile, Nguvu za Kiume......Kuondoa Mvi na Mkanda kwa Ajili ya Kupunguza Tumbo

$
0
0
OFFER OFFER OFFER
Natural beauty product inakupa OFFER ya EID kwa punguzo la %10 kwa kila product. 
 
 Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ni kwa watu wengi sana lakin NATURAL BEAUTY imepata uvumbuzi wa tatizo hilo na tiba zake zilizotengenezwa kwa mimea na matunda hazina kemiko wala madhara yoyote.
 
Pata bidhaa hizi uweze kufurahia matokeo mazuri. Tunazo za÷
   🥝🥑🥒🧀🍉🍅🍓🍇
1.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kifaa hiki kinapatikana kwa @180,000/= tuu.
 
2.MEN GELY YA KUPAKA. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @130,000/=. 
 
3. SHARK POWER. Hii pia ni kwa ajili ya kuongeza maumbile  wastani wa inch 7.5 kutoka size uliopo inapatikana kwa @140,000/=.
 
4.. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana master blashion. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa inapatikana kwa @140,000/=
 
5.DISCREET. Hii ni ya kuondoa mvi na zisiludi tena milele inapatikana kwa @130,000/=
6.MICRO COMPUTER. Huu ni mkanda kwa ajili ya kupunguza tumbo pamoja na nyama za pembeni unapatikana kwa 180,000/=
 
🍅🍇🍉🍅🍍🍓🥒🥑🍒
      Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.
      Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
           Pia bidhaa zetu zote ni guarantee na hakikisha ununuapo bidhaa kampuni hii unapewa risiti.
           Follow us Instagram
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
                            Karibu

Serikali Yatoa siku 7 walimu Wapewe Posho Zao

$
0
0
Serikali  imetoa siku saba kwa ajili ya halmashauri zote kuhakikisha walimu wa hesabu, sayansi na wataalamu wa maabara waliopangwa hivi karibuni wanapewa posho za kujikimu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema). 

Mkundi alitaka kujua ni lini serikali itawalipa stahiki zao walimu wa Hesabu, Sayansi na watalaamu wa maabara waliopangiwa vituo hivi karibuni. 

Alisema halmashauri zote zilizopokea walimu hao zinapaswa kuwapa posho za kujikimu ndani ya siku saba.

Akijibu swali la msingi la Mkundi aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa posho za mazingira magumu kwa watumishi wa maeneo ya pembezoni, alisema, “Katika kutekeleza Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha iliyopitishwa mwaka 2010, mwaka 2012/13 halmashauri 33 za wilaya ikiwemo halmashauri ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo ya kutoa motosha kwa watumishi.”

Alisema kutokana na mpango huo, halmashauri 29 ziliandaa na kuwasilisha katika ofisi ya wizara hiyo miongozo iliyobainisha aina ya motisha inayohitajika.

 “Utekelezaji wa miongozo hiyo kwa halmashauri zote 29 ulikadiriwa kugharimu Sh bilioni 331.087 kwa mwaka na utekelezaji wa miongozo hiyo, ulitarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2013/14 na haukuanza kutokana na ufinyu wa bajeti."

Waziri Mkuu Apigilia Msumari Mwingine Zuio la Kusafirisha Mahindi Nje ya Nchi......Kasema Bora Kusafirisha Unga Lakini Sio Mahindi

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi uko pale pale.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo  jana Alhamisi Juni 29, 2017 Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri  Mkuu wakati akijibu swali la Ritha Kabati  (Viti Maalumu) aliyetaka ufafanuzi kuhusu zuio la kusafirisha mazao nje ya nchi kwa mikoa yenye chakula cha ziada.

“Tumedhibiti na kuzuia usafirishaji wa chakula hasa mahindi kwenda nje ya nchi ili kuliepusha Taifa kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya mikoa kutopata mavuno ya kutosha,

“Kuna maeneo kama ya Sengerema na Geita mahindi yamekauka, hivyo bado tuna upungufu wa chakula. Na hata bei ya chakula ipo juu, hatuna namna nyingine zaidi ya kudhibiti utokaji wa chakula kwenda nje na nawasihi wananchi tushirikiane katika jambo hili,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kama kuna ulazima wa kusafirisha chakula kwenda nje ya nchi wahusika wakaombe kibali kutoka Wizara ya Kilimo,  Mifugo na Uvuvi na kibali kiwe cha kusafirisha unga na si mahindi.

"Nimeeleza sisi tumedhibiti kutoa mahindi nje bila ya kibali na kama kuna umuhimu wa kuyapeleka mahindi nje basi yasagwe ndani ili upelekwe 'unga' maana ukisaga kuna faida zake, pumba tunazitumia kwa chakula cha mifugo lakini pia mashine zetu tunazo sisitiza viwanda zitapata kazi ya kusaga pamoja na kutoa ajira" alisisitizia Majaliwa. 

Ombi la Rais Latimia, Miswada ya Madini Yatua Rasmi Bungeni

$
0
0
Ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya Rais John Magufuli kulitaka Bunge lipitie upya sheria na mikataba ya madini, miswada mitatu inayohusu madini tayari imesomwa bungeni kwa mara ya kwanza jana.

Aidha, ili kutoa fursa ya wabunge kujadili miswada hiyo iliyowasilishwa bungeni kwa hati ya dharura, vikao vya Bunge la Bajeti vilivyokuwa vifikie tamati leo, vimesogezwa hadi Julai 5 mwaka huu ili kutoa fursa kwa wabunge kupitia miswada hiyo. 

Miswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza bungeni hapo ni Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.

Muswada huu unapendekeza kuweka utaratibu ambapo wananchi kupitia chombo chao cha uwakilishi ambacho ni Bunge, kitapitia na kujadili makubaliano na mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi, ambayo imefungamana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujiridhisha na masharti. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya nchi Kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017.

Muswada huu unakusudia kuweka masharti yatakayohakikisha kwamba hatua yoyote inayochukuliwa kuhusu uwekezaji wa rasilimali za taifa, inatambua na kuzingatia haki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama taifa huru lenye mamlaka ya kusimamia na kutumia rasilimali zake kwa maslahi ya taifa. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017.

Wakati anapokea ripoti ya pili ya Kamati Maalumu ya Uchumi na Sheria kuhusu Taarifa ya Makinikia, Rais Magufuli aliliomba Bunge kupitia upya sheria na mikataba yote ya madini na gesi ili kuiepusha nchi kuingia katika mikataba mibovu.

“Kamati ya uongozi ilikaa jana (juzi) kubadilisha ratiba ambapo sasa mkutano huo wa Bunge la bajeti utaahirishwa Julai 5 mwaka huu, badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa imepangwa awali, miswada mitatu mipya ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza, itapelekwa katika kamati za Bunge,” alisema Spika Job Ndugai, ili kutoa nafasi kwa wabunge kujadili miswada hiyo,.

 Bunge limebadili ratiba kwa Bunge kuendelea na shughuli zake hadi Julai 5 mwaka huu, ambapo bunge hilo litaahirishwa.

Alisema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2017 kwa kuangalia upungufu uliojitokeza itafanyiwa kazi na Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengerwa.

Ndugai alisema pia Bunge limeunda kamati maalumu itakayoundwa na wajumbe wa kamati nne za Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya sheria Ndogondogo na Kamati ya Katiba na Sheria, itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dotto Biseko ambayo itapitia miswada miwili ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017.

Pia kamati hiyo itafanyia kazi Muswada wa Sheria ya Mamalaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017. 

“Kamati hizo zitafanya kazi kuanzia leo (jana) kwa kukutana na wadau mbalimbali na kisha taarifa itawasilishwa bungeni Jumanne, kabla ya bunge kuahirishwa Jumatano (Julai 5 mwaka huu),” 

Baada ya kuwasilishwa kwa miswada hiyo, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliomba mwongozo wa Spika, ambapo aliliomba bunge kuondoa hati ya dharura ya kujadili miswada hiyo.

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa haraka haraka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo,

 “Kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kwa umuhimu wake na maslahi kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, hivyo ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dharura ikaondolewa na kuletwa bunge lijalo.

 “Kwa maelezo uliyotoa wadau wataitwa kwa short notice wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichambue. Huu ni mtego kwa kutufanya tushindwe kuishauri serikali kwa kazi yetu ya kibunge”. 

Akitoa majibu ya serikali kuhusu muongozo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulamavu, Jenista Mhagama alisema masharti ya kutunga sheria na masharti ya jumla, yamewekwa katika fasihi ya nane ya Kanuni za Bunge, masharti yameongezwa na kanuni ya 80 na kanuni nyingine.

“ Muswada ambayo imeletwa imekuja kwa hati ya dharura, ili bunge liridhie kama miswada hii inastahili kujadiliwa na bunge ama la, kanuni 80(4) inasema muswada wowote wa dharura hautaingizwa katika shughuli za Bunge bila kuwa na hati iliyowekwa sahihi na rais kuthibitisha kwamba muswada huo ni wa dharura. 

“Sisi kama serikali tumeshatimiza masharti yote, tumeshakamilisha hatua zote za kufikishwa muswada huo kwa hati ya dharura. Wanaoweza kulishauri Bunge baada ya kuona uzito wa kazi iliyolewa na serikali ni kamati husika itakayopewa kazi ya kujadili miswada hiyo,” alisema.

Alisema sio busara kwa wabunge kabla hawajaona yaliyomo katika miswada husika, kujenga hoja ya kuikataa ndani ya bunge, mana kinachofanyika ni kwa maslahi mapata ya taifa. 

Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai alisema kwa niaba ya wabunge alipokea hati ya dharura huku akiwataka wabunge kulifanyia kazi jambo hilo.

“Tulijadiliana na kamati ya uongozi yenye uwakilishi wa tukakubaliana suala hili lisonge mbele. Wakati Rais (Magufuli) akipokea ripoti ya pili ya mainikia, kwa niaba yenu nilikubali kama kuna mambo yenye maslahi kwa nchi tutayafanyia kazi, mambo yameletwa katika kamati husika, kamati itajadili kama muswada inastahili kuingia bungeni ama la hoja nitatokea huko.

Aliongeza, “kwa muda mrefu tulikuwa tunataka Bunge kuwa na nafasi fulani katika masuala yanayohusu maadini na gesi, liwe na nafasi fulani ili kuzuia nchi kuingia katika mikataba mibovu.

 “Miswada hii kama mtanzania yeyote mwenye kuhitaji ataipata katika tovuti,”alisema Ndugai.

Mjue mgunduzi wa BUNDUKI MAARUFU IITWAYO AK 47

$
0
0
Luteni Jenerali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov wa Urusi ndiye mgunduzi wa silaha maarufu sana katika uwanja wa mapambano duniani kote iitwayo AK 47. Ni bunduki iliyobuniwa na kutengenezwa na kamanda huyu wa Jeshi Jekundu (Red Army) la Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR) wakati huo.

Luteni Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alizaliwa tarehe 10 Novemba 1919 eneo la Kurya, Altai, Urusi, ambalo kwa sasa linajulikana kama Altai Krai, Russia. Alijiunga na jeshi la Urusi mwaka 1938 na kupangiwa kama fundi wa vifaru na baadaye alipanda cheo na kuwa kamanda wa vifaru.

Mwezi Oktoba mwaka 1941 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alijeruhiwa vibaya katika mapigano ya Bryansk na kulazwa hospitalini mpaka mwezi Aprili mwaka 1942. Akiwa hospitalini akitibiwa, aliwasikia askari wenzake wa Kirusi wakilalamikia udhaifu wa bunduki zao za Urusi katika uwanja wa mapambano.

Baada ya kubaini udhaifu huo wa bunduki za Urusi, aliamua kutumia ubunifu wake kutengeneza bunduki bora zaidi za jeshi la nchi yake. Baada ya majaribio yake ya muda mrefu, hatimaye juhudi zake zilizaa matunda mwaka 1947 alipofanikiwa kutengeneza bunduki ya AK 47. Jina hili AK 47 ni kifupi cha maneno "Avtomat Kalashnikova model 1947"; namba 47 inasimama badala ya mwaka wa ugunduzi.

Luteni Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alifariki hospitalini tarehe 23 Desemba, 2013 akiwa na umri wa miaka 94 huko Izhevsk, mji mkuu wa jimbo la Udmurtia Urusi.

Huyo ndiye MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV, mgunduzi wa bunduki maarufu kwa jina la AK 47 ["Avtomat Kalashnikova model 1947"].

Mawakili 248 waapishwa, Tundu Lissu awataka kutumia taaluma yao kusaidia jamii

$
0
0
Na Eliphace Marwa – Maelezo
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mawakili wapya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uwakili na kutumia taaluma zao kwa kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.

Aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za 56 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 248 iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Aidha Kaimu Jaji Mkuu aliwahimiza Mawakili wapya kujiendeleza kitaaluma kwa sababu kuwa wakili sio mwisho wa taaluma kwani wanahitajika kusoma sheria za nchi mbalimbali Duniani ili kuweza kuingia mikataba ya kimataifa.

Alisema mawakili wapya wanatakiwa washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama na wateja kwani wakienda kinyume haki itapotea.

“Mawakili wote wanatakiwa kuwa waaminifu kwa wateja wanaowahudumia na kushirikiana na mahakama katika kutoa haki na wasiwe mawakala wa rushwa bali wawe mawakala wa kutenda haki,” alisema Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim.

Aidha Kaimu Jaji Mkuu aliwataka mawakili hao kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie upatikanaji wa haki kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya mawakili katika maeneo ya nje ya miji.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Tundu Lissu aliwataka Mawakili hao kutumia taaluma hiyo katika kuisaidia jamii kujua haki zao na utawala wa sheria japo kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya sheria nchini.

“Napenda kuwatakia kila la kheri mawakili hawa wapya ila niwaombe watumie taaluma hii kwa kuisaidia jamii kujua haki zao pamoja na utawala wa sheria,” alisema Mh. Tundu Lissu.

 Idadi ya mawakili walioapishwa  jana imepelekea Tanzania kuwa na idadi ya zaidi ya mawakili 6300.


Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Kuhusu Mauaji ya Watu Huko Kibiti

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe ameonesha kusikitishwa na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia yanayoendelea katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumzia msimamo wa CHADEMA juu ya mauaji hayo ambapo alisema chama hicho kinapingana na kinachotokea Mkoa wa Pwani.

“Kinachoendelea Mkuranga, Kibiti na maeneo mengine ya Mkoa wa Pwani ni kitu kibaya. Hatuungi mkono mauaji ya raia na viongozi.

"Hilo naomba niliweke wazi, sisi kama chama hatuungi mkono mauaji ya viongozi bila kujali wanatoka chama gani au bila kujali wanatoka Serikali ipi au wana wajibu gani wala raia yeyote wa nchi yetu. Hatuungi mkono na tunalaani sana mauaji yanayoendelea.”

Aidha, alisema wanasikitika na namna Serikali inavyolichukulia suala hilo akiwataka viongozi wa kisiasa kuviachia vyombo vya Ulinzi na Usalama vifanye kazi yake.

“Tunasikitika na namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano inavyoshughulika na jambo hili. 

"Kauli za viongozi wetu mbalimbali za majigambo zinaonekana kuwachochea wauaji kwa sababu linapotoka tamko lolote la majigambo anakufa mtu usiku ama anakufa mtu kesho yake. 

"Viongozi wetu wa kisiasa waachie vyombo vya Ulinzi na Usalama vifanya kazi. Matamko mengi yanatolewa na viongozi wetu wa kisiasa. Hatuna hakika ni nini kinaendelea.”

Katika kutafuta suluhisho zaidi juu ya tatizo la mauaji ya Pwani, Mbowe alivitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutumia ujuzi wa ziada kukabiliana na wauaji ikiwa pia kuwashirikisha watu mbalimbali na taasisi mbalimbili.

“Tunataka Majeshi yetu na vyombo vyetu vya Ulinzi na Ulasama vitumie weledi wa ziada. Sio kila wakati nguvu tu inaweza ikasaidia. Busara nyingine zote zitumike; Wazee watumike, Vyombo vya Serikali vitumike, Viongozi wa Kidini watumike.”

Haya ndo Mashitaka 28 Yanayomkabili Rais wa TFF Jamal Malinzi

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi hataweza kutetea nafasi yake hiyo katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

Hiyo inatokana na kushindwa kufika kwenye usaili ulioanza jana na kumalizika kesho kwa kuwa yupo rumande akikabiliwa na kesi.

Mbali ya Malinzi, pia Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais TFF, pia amepoteza nafasi hiyo kwa kuwa naye yupo rumande.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Revocatus Kuuli alisema mgombea ambaye atakosa kufika kwenye usaili katika muda huo atakuwa amejiondoa kwenye uchaguzi.

Malinzi, ambaye aliingia madarakani mwaka 2013 alikuwa akitetea kiti chake ambacho kingemfanya kuwa madarakani kwa miaka mingine minne iwapo angechaguliwa.

Jana, Malinzi (57), Katibu Mkuu wake, Mwesigwa Celestine (46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga (27) walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwamo ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418 (Sh840 milioni).

Malinzi anashtakiwa kwa makosa 28, huku wenzake wakishtakiwa kwa makosa yasiyozidi manne.

Walisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ambaye alidai kuwa katika shtaka la kwanza, Malinzi na Mwesigwa, Juni 5, 2016 wakiwa Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya, walighushi nyaraka zinazoitwa Maazimio ya Kamati ya Utendaji (Executive Committee Resolution) wakionyesha Kamati ya Utendaji ya TFF imebadili mtia saini wa akaunti ya benki ya TFF, Edgar Leonard Masoud kuwa Nsiande Isawafo Mwanga wakati wakijua si kweli.

Katika shtaka la pili, Wakili Katuga alidai kuwa Septemba Mosi, 2016 katika benki ya Stanbic, tawi la Kinondoni, Mwesigwa aliwasilisha nyaraka hiyo ya kughushi.

Katika shtaka la tatu, inadaiwa kuwa Desemba 17, 2013 katika ofisi za TFF, Malinzi alighushi risiti namba 308 ya Novemba 6, 2013 akionyesha ameikopesha TFF dola za Marekani 9,300 (Sh19 milioni) wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la nne, Malinzi anadaiwa kuwa Desemba 17, 2013 katika ofisi ya TFF, alighushi risiti namba 322 akionyesha ameikopesha TFF dola za Marekani 10,000 (Sh20 milioni) wakati si kweli.

Shtaka la tano, Malinzi anadaiwa kuwa Desemba 17, 2013 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 323 akionyesha ameikopesha TFF dola za Marekani 18,000 (Sh37 milioni).

Katuga alidai kuwa katika shtaka la sita, Desemba 17, 2013, Malinzi kwenye ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 324 akionyesha ameikopesha TFF dola 5,000 (Sh10 milioni).

Katika shtaka la saba, Malinzi anadaiwa kuwa Desemba 17, 2013 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 325 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,032 (Sh2 milioni) wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la nane, Katuga alidai kuwa Machi 26, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1956 akionyesha ameikopesha TFF dola za 40,000 (Sh84 milioni).

Wakili huyo wa Serikali alidai katika shtaka la tisa kuwa, Machi 13, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1957 akionyesha ameikopesha TFF dola 5,000 (Sh 10 milioni).

Aliendelea kudai kuwa katika shtaka la 10, Mei 13, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1624 akionyesha ameikopesha TFF dola 40,000 (Sh84 milioni).

Katika shtaka la 11, Katuga alidai kuwa Mei 16, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1634 akionyesha ameikopesha TFF dola 10,000 (Sh20 milioni).

Shtaka la 12, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 11, 2014, alighushi risiti namba 1860 akionyesha kuwa ameikopesha TFF dola 15,000 (Sh30 milioni).

Katika shtaka la 13, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 11, 2014 alighushi risiti namba 1861 akionyesha ameikopesha TFF dola 3,000 (Sh6 milioni).

Katika shtaka la 14, inadaiwa kuwa Julai 15, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1863 akionyesha kuwa ameikopesha TFF dola 14,000 (Sh28 milioni).

Iliendelea kudaiwa katika shtaka la 15 kuwa, Julai 15, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1866 akionyesha ameikopesha TFF dola 4,000 (Sh8 milioni).

Katuga alidai katika shtaka la 16, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 25, 2014 , alighushi risiti namba 1876 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,000 (Sh2 milioni).

Katika shtaka la 17, wakili huyo alidai kuwa Agosti 19, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1890 akionyesha ameikopesha TFF dola 5,000 (Sh10 milioni).

Kwenye shtaka la 18, Katuga alidai kuwa Oktoba 11, 2014, Malinzi alighushi risiti namba 1568 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,200 (Sh2.4 milioni) wakati akijua si kweli.

Shtaka la 19, Malinzi anadaiwa kuwa Agosti 17, 2015 alikula njama ya kughushi risiti namba 1511 akionyesha kuwa ameikopesha TFF dola 5,000 (Sh 10 milioni).

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akisoma shtaka la 20, alidai kuwa Julai 22, 2015, Malinzi alighushi risiti namba 2981 akionyesha kuwa ameikopesha TFF dola 2,000 (Sh4 milioni).

Swai akisoma shtaka la 21, alidai kuwa Mei 9, 2016, Malinzi alighushi risiti namba 832 akionyesha ameikopesha TFF dola 7,000 (Sh14 milioni) wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la 22, Swai alidai kuwa Juni 16, 2016, Malinzi alighushi risiti namba 931 akionyesha ameikopesha TFF dola 10,000 (Sh20 milioni).

Inadaiwa katika shtaka la 23, kuwa Agosti 2, 2016, Malinzi alighushi risiti namba 947 akionyesha kuwa ameikopesha TFF dola 1,000 (Sh2 milioni).

Akiendelea kusoma hati ya mashtaka, Swai alidai katika shtaka la 24 kuwa Septemba 19, 2016, Malinzi alighushi risiti namba 1029 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,000 (Sh 2 milioni).

Swai katika shtaka la 25, alidai kuwa Septemba 22, 2016, Malinzi alikula njama ya kughushi risiti namba 1071 akionyesha kuwa ameikopesha TFF dola 15,000 (Sh30 milioni).

Kwenye shtaka la 26, ilidaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, 2016 washtakiwa Malinzi, Mwesigwa na Mwanga kwa pamoja, walitakatisha fedha kiasi cha dola 375,418 huku wakijua fedha hizo ni zao la kughushi.

Katika shtaka la 27, Swai alidai kuwa Malinzi na Mwesigwa katika kipindi hicho cha Septemba Mosi na Oktoba 19, 2016 katika benki ya Stanbic, tawi la kati la Kinondoni walijipatia dola 375,418 wakati wakijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

Katika shtaka la 28, Mwanga anadaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, 2016 katika ofisi ya TFF aliwasaidia Malinzi na Mwesigwa kujipatia dola 375,418 kutoka benki ya Stanbic huku akijua upatikanaji wake umetokana na kughushi.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo yanayowakabili Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa aliiambia Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Jopo la mawakili wa utetezi likiongozwa na Jerome Msemwa na Aloyce Komba liliiomba Mahakama iwapatie dhamana washtakiwa hao lakini Mutalemwa na mawakili wenzake wa Serikali waandamizi, Christopher Msigwa na Pius Hilla walipinga dhamana kwa washtakiwa hao kwa madai kuwa mashtaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili hayana dhamana.

Hakimu Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi hiyo, aliiahirisha hadi Jumatatu ijayo atakapotoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana hivyo, walipelekwa rumande. 

Zitto Kabwe Ampinga John Mnyika Sakata la Miswada ya Madini Kujadiliwa Bunge Hili

$
0
0
Jana miswada mitatu inayohusu madini ilisomwa bungeni kwa mara ya kwanza jana. Miswada hiyo iliwasilishwa kwa hati ya dharura kama ambavyo Rais Magufuli aliliomba Bunge  lipitie upya sheria na mikataba ya madini. Bunge pia limeongezwa muda hadi July 5.

Wakati anapokea ripoti ya pili ya Kamati Maalumu ya Uchumi na Sheria kuhusu Taarifa ya Makinikia, Rais Magufuli aliliomba Bunge kupitia upya sheria na mikataba yote ya madini na gesi ili kuiepusha nchi kuingia katika mikataba mibovu.

Baada ya kuwasilishwa kwa miswada hiyo jana, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika(Chadema)  aliomba mwongozo wa Spika, ambapo aliliomba bunge kuondoa hati ya dharura ya kujadili miswada hiyo.

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa haraka haraka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo,

 “Kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kwa umuhimu wake na maslahi kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, hivyo ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dharura ikaondolewa na kuletwa bunge lijalo.

 “Kwa maelezo uliyotoa wadau wataitwa kwa short notice wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichambue. Huu ni mtego kwa kutufanya tushindwe kuishauri serikali kwa kazi yetu ya kibunge”. Alisema Mnyika

Baada ya kauli hiyo ya Mnyika aliyoitoa jana Bungeni, leo Zitto Kabwe(Mbunge wa Kigoma-ACT Wazalendo) amepingana na kauli hiyo  ambapo amesema  Hoja ya hati ya dharura anayoizungumzia Mnyika  ni dhaifu kwa sasa.

==>Huu ni ujumbe wake aliouandika kupitia ukurasa wake Facebook
 
Naelewa Sana wenzangu wanapoongelea hati ya dharura kwenye miswada Hii ya Rasilimali za Nchi. Lakini ukisoma muswada mmoja baada ya mmoja hakuna jambo linalohitaji muda maana yote tumekuwa tukiyasema Kwa miaka 10 sasa tangu Buzwagi Mwaka 2007. Hoja ya hati ya dharura ni dhaifu Kwa sasa na Kwa hili.

- Sheria moja inataka tamko rasmi la kisheria kuwa madini, mafuta na gesi asilia ni mali ya Taifa ya milele na haitahamishwa Kwa yeyote. Tukiongezewa muda tutabadili hili?

- Sheria moja inataka mikataba ya Madini iwe inapitishwa na Bunge. Tukiongezewa muda tutabadili hili?

- Sheria moja inabadili sheria ya Madini ya mwaka 2010 Kwa kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Unataka muda Kwenye hili?

Hebu tukatunge sheria na tuboreshe miswada Hii ili kurudisha rasilimali zetu kwenye mikono yetu. Hoja ya Hati ya Dharura ni hoja nzuri lakini Kwa sasa ni maneno matupu yaani empty rhetoric

Mwigulu Nchemba Ampa ONYO Godbless Lema Kwa Kushabikia Mauaji ya Wananchi Kibiti

$
0
0
Waziri  wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba jana ‘alimkalia kooni’ Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema) kwa kauli yake kwamba wabunge wanaogopa kujadili mauaji yanayoendelea Kibiti wakihofia yatahamia kwao.

Mwigulu alichukizwa na kauli hiyo jana bungeni wakati wa mjadala kuhusu kuridhia   itifaki ya udhibiti wa mazingira ya bahari na ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu.

Nyingine ni    itifaki ya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo sahihi wa faida zinazotokana na matumizi ya rasimali za  jenetiki.

Wakati akichangia, Lema alisema   wabunge wasishangae mauaji yanayotokea Kibiti yakisambaa nchi nzima.

“Kila mtu anaogopa kujadili suala la Kibiti, Bunge linaogopa kujadili wanaona wakianza kujadili jamaa anaweza kuhamia huku,”alisema Lema.

Akijibu, Waziri Mwigulu pamoja na mambo mengine, alisema Serikali haitaacha eneo hata moja la nchi likatawaliwe na wahalifu.

“Tutashughulika na mmoja mmoja, watu wetu watafanya kazi katika mazingira salama.

“Unaongea kimzaha mzaha, taswira iliyoko ndani inahusiana na siasa, leo ukituambia yale ya Kibiti yanaendelea na maeneo mengine tunaendelea kutafuta uhusiano, kama leo kauawa wa CCM, kaacha mwingine kule…. kuna haja ya kutusaidia kwa nini unasema yanaendelea, kwa nini unadhani wanashindwa…

“Katika panga kazi zetu tunahakikisha wananchi wa maeneo yote wanakuwa salama…sentesi kama hizi hata kama zinasemwa bungeni nadhani kuna umuhimu   ndugu zetu hawa wakasaidia kujua kiini ama kinatoka bungeni ama kinatoka wapi, lakini sasa wanahangaika na watu wengine,” alisema.

Wilaya za Mkoa wa Pwani za Rufiji, Kibiti na Mkuranga zimekumbwa na mauaji  ya viongozi wa vijiji na vitongoji tangu Mei  mwaka jana na hadi sasa  zaidi ya watu 30 wameuawa.

Mauaji mengi yamekuwa yakifanyika usiku kwenye nyumba za viongozi na watu wengine ambao wamewahi kushika uongozi, idara ya maliasili na polisi.

Bunge jana liliridhia itifaki ya udhibiti wa mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu na ile ya itifaki ya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo sahihi wa faida zinazotokana na matumizi ya rasimali za  jenetiki.

Lowassa: Demokrasi imeshaanza na Itaendelea....Hakuna wa kuizuia

$
0
0
Waziri  Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema gurudumu la demokrasia limekwisha kuanza nchini hivyo ni vigumu  kulizuia.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  alirejea  Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam jana baada Juni 27 kuhojiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Alihojiwa  kwa takriban saa nne juu ya kauli alizozitoa kuhusu viongozi wa dini wa kundi la Uamsho na akatakiwa kurudi  jana saa 6.00 mchana.

Akizungumza ofisini kwake Mikocheni, Lowassa alisema baada ya kuitikia wito wa polisi jana, hakuna mengi aliyoambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa  upelelezi wa suala hilo unaendelea hivyo arejee  ofisini hapo Julai 13.

Alipoulizwa analichukuliaje suala hilo la kutakiwa kwenda  polisi mara kwa mara  alisema: “Njoo kesho, njoo kesho kutwa ni sehemu ya kazi yao (polisi).

“Kuhusu maoni yangu nitawaambia baada ya kumaliza hili, isionekana naingilia.

“Lakini nieleze jambo moja, demokrasia ikishaanza kuizuia ni taabu sana.

“Unaweza ukapunguza spidi ya gurudumu la demokrasia lakini huwezi kuiondoa, demokrsia imeshaanza, inaendelea, ni vigumu kuizuia.

“La pili, nichukue nafasi hii kuwaomba wanachama wa chama chetu na wananchi na wanaotutakia mema wasiwe na  shaka kila kitu kipo chini ya utaratibu mzuri.

“Tuko sawasawa, tuko sahihi na tunatekeleza kama alivyosema (Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe). Tunatekeleza sera ya chama chetu, wasiogope wawe na amani, watulie,” alisema Lowassa.

Alivyoulizwa kama wakati anatoa kauli kuhusu viongozi hao wa Uamsho labda aliteleza, Lowassa alisema, “I stand by what I said” (naisimamia kauli yangu).

Alisema anaamini alichosema ni sahihi kama alivyoeleza Mbowe na kwamba suala la msingi ni kuachiwa kwa Masheikh wa Uamsho.

Lowassa alisema Chadema  kama chama hakisemi kama viongozi hao wa dini wana makosa ama hawana, ila wamekaa ndani kwa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa.

“Wamekaa vya kutosha, hilo ndilo la msingi tunaloomba… katika hotuba yangu nilisema na kwenye magazeti waliandika vizuri, wale walioko madarakani wana mamlaka.

“Mtu mwenye dhamana ya kuwatoa ni Rais. Nikawaeleza wajipange wakaongee na Rais wamwambie ‘mzee, wenzetu tunaomba waachiliwe’.

“Mwenye madaraka ya mwisho ni Rais, mkiendelea na mahakama miaka minne, nane siyo… kwa hiyo narudia, ni vema wakamuombe Rais awaachilie.

“Sintoshangaa akitekeleza (akawaachia) kwa sababu juzi ametekeleza moja ya uamuzi wetu wa kuunda tume ya kuchunguza madini, tulivyokuwa Kahama tulisema tutaunda tume.

“Waendelee na uchunguzi wao (juu ya kauli yake), lakini narudia, gurudumu la demokrasia likianza kulizuia ni  taabu sana.

“Narudia mwenye mamlaka ya mwisho kuombwa na kushawishiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”alisema Lowassa.

Naibu Waziri afanya ziara ya kushtukiza mradi wa umeme Kinyerezi II, atoa agizo

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani ameagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha mradi wa umeme wa Kinyerezi II unazalisha megawati 30 za umeme nchini ifikapo Desemba mwaka huu.

Kalemani amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi huo leo asubuhi (Juni 30) ili kujua hali ya utendaji.

Amesema taarifa aliyopewa tangu alipowasili ni kuwa mradi huo utazalisha megawati 240 utakapokamilika mwakani ila 30 zikamilike Desemba mwaka huu.

"Mradi wa Kinyerezi II tunategemea utupatie megawati 240, lakini lazima tuanze kupata hizo mapema, kwa taarifa niliyosikia tutaanza na megawati 30 sasa niseme megawati hizo tupate ifikikapo Desemba," amesema Kalemani.

Amesisitiza kuwa zitakazobakia apewe ratiba za utekelezaji wake ili hadi kufikia Septemba 2017 megawati zote ziwe tayari.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanesco, Tito Mwinuka ameomba ushirikiano baina ya Serikali na Shirika hilo ili kufika malengo ya agizo la Naibu Waziri.

"Tushirikiane pamoja Tanesco na Serikali kuhakikisha fedha zinapatikana kwa wakati ili kwamba mradi ukamilike kwa wakati," amesema Mwinuka.

Kalemani ameongeza kuwa hakutakuwa na uongezaji wa muda katika miradi yote miwili ya Kinyerezi I na II hivyo kuwataka wahusika kufanya kazi kwa nguvu na weledi ili kumaliza kazi.

Amesema mradi wa Kinyerezi I umefikia asilimia 35 hali ambayo hairidhishi huku ukitegemewa kutoa megawati 185 kufikia Agosti 2017.

"Kufikia Septemba mwakani, tunategemea kuwa na megawati 425 kwa miradi yote miwili bila kupungua, fanyeni kazi sana katika Kinyerezi I," amesema Kalemani.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images