Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 29


Rais Mgufuli Akutana na Wataalam Wa Umeme Ehiopia .......Wazungumzia Uzalishaji wa Megawati 2, 100 za Umeme katika Maporomoko ya mto Rufiji

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  jana  tarehe 28 Juni, 2017 amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli alisema timu hiyo inayoongozwa na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele imekuja nchini kubadilishana uzoefu na timu ya wataalamu wa Tanzania ambayo inasimamia utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project).

Katika mazungumzo na timu hiyo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli alielezea nia yake ya kuhakikisha mawazo ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme kutoka maporomoko ya mto Rufiji, yanatekelezwa haraka iwezekanavyo.

“Sasa hivi nchi yetu inazalisha megawatts 1,450 tu, lakini Stiegler’s Gorge itatuzalishia megawatts 2,100 umeme huo ni mwingi na utatusaidia katika viwanda, hivyo Serikali tumeamua kutekeleza mradi huu.

“Najua kutaanza kutokea vipingamizi mbalimbali, lakini naomba Watanzania tuwe na sauti moja, eneo litakalotumia ni Kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa na asilimia 3 tu ya eneo lote la hifadhi ya Selous yenye ukubwa wa Kilometa za mraba 45,000” alisema Mhe. Rais Magufuli na kuongeza kuwa mradi huo utakuwa na faida nyingi zikiwemo uvuvi, maji kwa ajili ya wanyamapori na kilimo.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele alisema Ethiopia ambayo kwa sasa inazalisha megawatts 4,300 za umeme kwa kutumia maji, inayo miradi mingi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji ambayo itaiwezesha kufikia uzalishaji wa megawatts 17,000 ifikapo mwaka 2020 na kwamba yeye na watalaamu wa nchi wapo tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania katika masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Dkt. Medard Kalemani na timu ya wataalamu wa Tanzania wanaosimamia utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project).

Rais Magufuli Akutana na Wajumbe wa kamati za makinikia IKULU na Kuwapongeza Kwa Kazi Nzuri

$
0
0
Rais John Magufuli jana alikutana na wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa mchanga wa madini katika makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.

Taarifa iliyotumwa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu jana umatano ilisema Rais amewapongeza wajumbe hao kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Kamati hizo moja iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, ambaye timu yake ilichunguza kiasi cha madini kilicho kwenye mchanga huo na ya Profesa Nehemia Osoro iliyochunguza masuala ya kisheria kuhusu mchanga huo.

Rais Magufuli alisema timu hiyo imefanya kazi nzuri na yenye maslahi makubwa kwa Taifa na kwamba Serikali itahakikisha inafanyia kazi taarifa zilizotolewa na kamati hizo.

Taarifa Muhmu Toka Ofisi ya Makamu wa Rais

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amewaagiza wapelelezi na waendesha mashtaka nchini waepukane na vitendo vya rushwa bali wafanye kazi kwa bidii kwa kuweka maslahi ya Taifa mbele kwa kuchukua hatua stahiki kwa watu wanaoiba rasilimali za Taifa.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati anazindua mwongozo kwa wapelelezi na waendesha mashtaka wa kesi za wanyamapori na misitu katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema mwongozo aliouzindua utasaidia kwa kiwango kikubwa uboreshwaji wa upelelezi na uendeshaji wa kesi zinazohusu wanyapori na misitu nchini.

“Uwepo wa mwongozo huu ni dhahiri unategemewa kutoa matokeo chanya katika mapambano dhidi ya ujangili na uharibifu wa misitu yetu,” amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kuwa ana imani mwongozo huo aliouzindua utasaidia kukomesha vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikiisababishia Serikali hasara kubwa ikiwemo uharibifu wa rasilimali za Taifa na kupoteza mapato ambayo yangesaidia kuimarisha huduma za kijamii nchini.

Kuhusu sekta ya utalii nchini, Makamu wa Rais amesema pamoja na sekta hiyo kuliingizia Taifa mapato mazuri lakini inasikitisha kuona kuwa uwepo wa wanyamapori ambao ndio nguzo kuu ya sekta ya utalii unazidi kupungua kila kukicha hivyo kuwa tishio kubwa kwa uchumi na nchi.

Amesema vitendo vya ujangili vimeendelea kuangamiza wanyama hasa tembo, hivyo ni muhimu kwa wapelelezi na waendesha mashtaka kutenda haki bila kuonea mtu kwa watu wanaokamatwa kufanya vitendo hivyo ili viweze kukomeshwa nchini.

“Wazee wetu walilinda na kutunza rasilimali zetu kwa faida yetu nasi tuzitunze kwa ajili ya vizazi vijavyo,” ameeleza.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa kazi ya kupambana na ujangili na utoroshaji wa wanyama na viumbe wengine itakuwa endelevu na wale wote  watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.

Waziri Profesa Maghembe amemwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kuendesha operesheni maalum ya kukusanya silaha zote ambazo zimekuwa zikitumika kwenye ujangili ili kuhakikisha wanyama hasa tembo wanakuwa salama kwenye maeneo ya Hifadhi za Taifa nchini.

Naye, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga amefafanua kuwa katika kipindi cha mwaka 2014-2017 ofisi yake imewafikisha Mahakamani washtakiwa wakubwa wa ujangili ambao walihukumiwa vifungo virefu na faini.

Amesema kuwa washtakiwa 100 walihukumiwa kulipa faini ya zaidi ya shilingi bilioni 1.1 kwa kujihusisha na nyara za Serikali kinyume na sheria na faini hizo zimeshalipwa Serikalini.

Ameeleza kuwa kati ya idadi hiyo watuhumiwa zaidi ya 80 walihukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30 gerezani na faini ya zaidi ya shilingi milioni 164 ambazo bado hazijalipwa Serikalini.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga amesema mafanikio hayo yote yamechangiwa na usimamizi madhubuti wa kesi hizo kupitia dawati la wanyamapori katika Divisheni ya Mashtaka pamoja na Mawakili wa Serikali katika Ofisi zote za mikoani nchini.

Ameeleza kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo kwenye kazi kwa sasa ni dhamana kwa watuhumiwa wakubwa wa vitendo vya ujangili ambapo utafiti uliofanywa Mahakama za mkoa wa Dar es salaam tu katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 unaonyesha kuwapo kwa jumla ya mashauri 13 yanayohusishwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 800 zilizokamatwa ndani na nje ya nchi ambapo watuhumiwa wake walipewa dhamana na kutoweka.

Biswalo Mganga amesema katika mashauri hayo, asilimia 69 walikuwa ni raia wa kigeni na asilimia 31 ni raia wa Tanzania.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikulu – Dar es Salaam.

VIDEO: Msikilize Rais Magufuli Akizungumzia Nia Yake ya Kujenga Bwawa Kubwa la Kuzalisha Umeme

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Juni, 2017 amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tanzania.

== >Msikilize Hapo chini akiongea

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?
 
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
 
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

Whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Wahitimu Wa Stashahada Katika Programu Mbalimbali Wanaokusudia Kuomba Kujiendeleza Katika Ngazi Ya Shahada Katika Vyuo Vya Elimu Ya Juu Kwa Mwaka Wa Masomo 2017/2018

$
0
0
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. 

Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za usajili na ithibati, mitaala na upimaji ili tuzo zitolewazo na vyuo/taasisi ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. 

Kifungu cha 5 (1) (e) na (f) cha Sheria hii kinaipa mamlaka NACTE, kuanzisha tuzo mbalimbali zinazotolewa na kuhakikisha kuwa ubora wa elimu na mafunzo ya kada ya kati yatolewayo na taasisi mbalimbali yanazingatia ubora unaokusudiwa. 

Aidha, Kifungu cha 11, kinalitaka Baraza kuhakikisha kuwa Tuzo zitolewazo na vyuo na taasisi zote zinazoendesha mafunzo ya kada ya kati zinatambuliwa na mamlaka husika. Katika muktadha huu, kila chuo/taasisi inayotoa elimu ya ufundi inatakiwa kuwasilisha Baraza matokeo ya mitihani kila mwisho wa semista.

Hivyo, kwa kuwa Udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Shahada mbalimbali yanayotolewa na taasisi/vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, Baraza linao wajibu wa kuziwezesha taasisi/vyuo hivyo kudahili wanafunzi wenye sifa stahiki.

Ili kulifanikisha hili, Baraza limeandaa mfumo ambao taasisi/chuo kitapata taarifa za muombaji mwenye sifa linganifu (muhitimu wa Stashahada) moja kwa moja.

Hivyo, wahitimu wote wa Stashahada yoyote wanaokusudia kuomba kujiendeleza katika ngazi ya Shahada wanatakiwa kuhakiki taarifa zao Baraza (NACTE) kabla ya kufanya maombi yao kwenye taasisi/vyuo wanavyotaka kwenda kusoma. 

Uhakiki huo utafanywa kwa njia ya mtandao (online) kupitia Mfumo wa Uhakiki wa Tuzo (NACTE Award Verification System - NAVS) kwa kubofya hapa au kupiti tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) kwa kubofya kitufe kilicho andikwa Award Verification. 

Baada ya kuhakiki taarifa zake kuwa kamilifu na sahihi, mhakiki atapatiwa Namba ya Utambulisho (Award Verification Number - AVN) ambayo itaambatanishwa na maombi ya Udahili kwenye taasisi/chuo husika. 

Utambulisho huo utatumiwa na taasisi/chuo kujiridhisha kwamba taarifa alizowasilisha muombaji wa Udahili ni sahihi na hivyo kuweza kudahiliwa na kisha kuchaguliwa kwa ajili ya masomo kulingana na mahitaji ya taasisi/chuo husika.

Aidha, Baraza linapenda pia kuwafahamisha wale wote walio na Stashahada walizopata nje ya nchi (Foreign Diploma Awards), nao waziwasilishe kupitia mfumo huu (NAVS) kwa ajili ya kuzifanyia ulinganifu na kuweka taarifa zao kwenye Kanzidata ya Baraza ili nao waweze kupata Namba ya Utambulisho. Maelezo ya namna ya kuziwasilisha tuzo za kufanyiwa ulinganifu yanapatika kwenye tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).

Ili mwombaji Udahili apate Namba ya Utambulisho atalipa Shilingi Elfu Kumi (10,000/=) kwa njia ya mtandao (Online) kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye Mfumo wa Uhakiki wa Tuzo - NAVS.  

Kwa wale wanaotaka kufanya ulinganifu wa vyeti vyao, watatakiwa kulipa Shilingi Elfu Ishirini (20,000/=) kwa tuzo za ndani ambazo hazisimamiwi na baraza, na Shilingi Elfu Hamsini (50,000/=) kwa tuzo za nje ya nchi (foreign awards).

Baraza linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa wanaweza kufanya uhakiki huo kuanzia leo tarehe 28 Juni, 2017 hadi tarehe 20 Julai, 2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 28/06/2017

Taarifa Kuhusu Tanzania Kuzuiwa Kuingiza Gesi Asilia na Unga wa Ngano Kenya

$
0
0

Tarehe 24 Aprili, 2017 magazeti nchini Kenya yalitoa taarifa ya kwamba Serikali ya Kenya itapiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupikia (Liquefied Petrolium Gas, LPG) nchini humo kutokea Tanzania, na kwamba gesi itakayoruhusiwa kuingia Kenya ni ile itakayokuwa imepitia kwenye Bandari ya Mombasa peke yake. 

Baada ya kusoma taarifa hizi Serikali ya Tanzania iliwasiliana na Serikali ya Kenya ili kupata maelezo kuhusu hatua hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibiashara katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. 

Tarehe 18 Mei, 2017 Serikali ya Kenya ilitekeleza uamuzi wake kwa kuzuia shehena ya gesi isiingie Kenya kutokea Tanzania. 

Hatua hii ina athari kubwa kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia hapa nchini pamoja na watu wote ambao ajira zao zinategemea biashara hii. 

Wakati hatua hizi zinachukuliwa bado Serikali ya Kenya ilikuwa haijatoa maelezo rasmi kwa Tanzania kuhusu uamuzi wake huo. 
 
Katika kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika tarehe 2 Juni, 2017, suala la hatua ya Kenya kupiga marufuku uingizwaji wa gesi kutokea Tanzania lilizungumzwa kwa kirefu na kufanyiwa maamuzi. 

Kimsingi Serikali ya Kenya ilikubali kuondoa katazo la uingizaji wa gesi kupitia Tanzania mara moja, na makubaliano haya yaliingizwa kwenye kumbukumbu za Mkutano ambazo ziliafikiwa na nchi zote wanachama wa Jumuiya kwa kuweka sahihi. 

Pamoja na makubaliano haya, Kenya imeendelea kuzuia gesi isiingie nchini mwao kutokea Tanzania. Serikali ya Tanzania imewasilisha rasmi malalamiko yake Kenya kuhusu suala hili. 





Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Maalim Seif afunguka makubwa.......Atishia Kuishitaki RITA Mahakamani Kwa Kuihujumu CUF

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Wananchi (CUF), kinatarajia kumfikisha mahakamani  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini yaliyofikishwa kwake kama yalipitishwa na kikao halali cha chama kwa mujibu wa katiba.

Kauli hiyo ameitoa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seifjijini Dar es Salaam  jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema wanachukua hautua hiyo kutokana RITA kushindwa kutumia mwongozo na weledi katika kutekeleza majukumu yao na badala yake wamesukumwa na utashi binafsi kwa ajili ya hujuma dhidi ya chama hicho.

“Chama chetu kimepatwa na mshituko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa na nyeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo. RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku. Licha ya kusajili Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza wosia kwa ajili ya mirathi,” alisema Maalim.

Alisema michakato wa kufungua kesi hiyo inaanza leo ambapo alieleza kuwa tayari wamekwisha agiza mwawakili kulishughulikia. 

Kutokana na matarajio ya ufunguzi wa kesi hiyo watawasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote walizofungua kuhusiana na kadhia hiyo hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA  litakapoamuliwa.

Maalim alisema kusajiliwa kwa bodi hiyo ambayo aliiita kuwa ni bodi feki, alieleza kwamba ni mwendelezo wa kukihujumu na kukidhoofisha chama kunakofanywa dola kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake.

Alitaja mambo manne ambayo yalikuwa msukumo wa kusajiliwa kwa bodi hiyo. Alisema kuwa ni kwa ajili ya kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola, kufungua akaunti mpya ya benki ili kumwezesha Profesa Lipumba kupata ruzuku.

Aliongeza mengine kuwa ni Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao Makuu, Zanzibar pamoja na kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki Wazanzibar kwa maamuzi yao ya Oktoba 25 mwaka 2015.

Hamadi alisema kamwe  haki ya Wazanzibar haitapotea na kuahidi kuwa ndani ya miezi mitatu haki hiyo itakuwa imepatikana.

Watanzania 500 Watimuliwa Kenya

$
0
0
Uhusiano  kati ya Tanzania na Kenya umeanza kuingia dosari baada ya uongozi wa Kaunti ya Kajiado kuwamuru Watanzania zaidi ya 500 wanaoishi kwenye mpaka wa Namanga  kuondoka katika eneo hilo.

Hatua hiyo ya Kaunti ya Kajado  kuwafukuza Watanzania hao imetokana na Serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji kudhibiti raia wa Kenya waliokuwa wakiingia nchini holela kupitia mpaka wa Namanga wilayani Longido Mkoa wa Arusha.

Uamuzi huo wa Kenya unatajwa kuathiri uhusiano wa  jamii za   pande mbili za nchi hizo uliojengewa kwa zaidi ya miaka 60 ambako wananchi wamekuwa wakipita kwenda kila upande  kununua bidhaa bila kuzuiwa.

Baadhi ya Watanzania waliofukuzwa   Kenya  walisema  uamuzi huo wa Kaunti ya Kajiado, umewasababishia hasara kutokana na uwekezaji waliofanya nchini humo.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, alisema akiwa kiongozi na mwakilishi wa Rais Dk. John Magufuli anatekeleza sheria za nchi.

Aliwataka wananchi wanaotaka kuishi nchi yoyote   wafuate sheria za nchi husika na si vinginevyo.

“Ikiwa wazazi wanataka watoto wao wasome   Kenya wafuate sheria za Kenya na Wakenya wakitaka kuingia Tanzania wafuate sheria za Tanzania. Huu ndiyo utaratibu na si vinginevyo,” alisema DC Chongolo.

Raia wa Kenya wanasema hatua ya kufukuzwa kwa Watanzania nchini humo imetokana na Serikali ya Tanzania  kuwafukuza wananchi wa nchi hiyo Machi mwaka huu.

Ndugu Wasimulia Jinsi Viongozi Wawili Walivyouawa KIBITI Huku Mmoja Akitobolewa Macho Yote

$
0
0
Risasi tano zimetumika kuwaua Mwenyekiti wa Kijiji cha Mangwi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, kisha kumjeruhi machoni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo, wilayani Kibiti, mkoani Pwani.

Waliofariki katika tukio hilo ni Ofisa Mtendaji, Mwarami Shamte aliyekutwa na majereha matatu ya risasi na Mwenyekiti wa Kijiji, Hamis Bakari Mkima aliyekutwa na jeraha moja.

Pia wauaji hao walimpiga, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo, Michael Martin risasi ya macho, iliyoharibu macho yake mawili.

Kama hiyo haikutosha, waliichoma moto nyumba ya Martin na kisha kutokomea kusikojulikana.

Mganga wa zamu katika Kituo cha Afya Kibiti, Dk Sadock Bandiko alithibitisha kuuwawa kwa viongozi hao wa kijiji hicho.

Amesema Shamte amekutwa na majeraha matatu yaliyotokana na kupigwa risasi.

“Shamte alipigwa risasi moja kichwani na risasi mbili tumboni,”amesema.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Dk Sadock amesema marehemu alipigwa risasi moja ya shingoni aliyopigwa toka upande wa kulia na kwenda kushoto lakini  haikutokeza.

Pia alisema mwenyekiti huyo alikuwa na jeraha kubwa katika mguu wake wa kushoto lililotokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali.

Mganga Mkuu wa Hospital ya Mchukwi, Dk Zacharia Lukeba alipolazwa Martin, amesema alipigwa risasi moja ya kichwani iliyofumua na kuharibu kabisa macho yake.

Amesema tayari wamempa rufaa kwenda Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mmoja wa ndugu za marehemu hao amesema watu wanne waliokuwa na bunduki wakiwa wamevaa nguo nyekundu na kuficha sura zao kwa soksi walivamia kijijini hapo saa nne usiku wa kuamkia jana.

Amesema watu hao walianza kwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho (Hamis Bakari Mkima) (30) ambaye alifanikiwa kuwakimbia kabla hawajamfikia.

Amesema watu hao walimpiga na kitu chenye ncha kali katika mguu wake wa kushoto kisha kumrejesha kwake huku wakimtaka awapeleke kwa viongozi mbalimbali wa kijiji hicho.

Alieleza kuwa baada ya hapo walimtaka awapeleke kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho (Mwarami Shamte) (40) na baada ya kufika huko walimpiga risasi tatu na alifariki dunia papo hapo.

Amesema watu hao bado walimtaka mwenyekiti huyo awapeleke kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo na baada ya kufika kwake walimpiga risasi ya usoni iliyoharibu macho yake.

Amesema baada ya hapo walimpiga risasi moja mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Mangwi, (Hamis Mkima) na alifariki papo hapo.

Pia ameeleza kuwa wakati watu hao wakifanya hayo walikuwa tayari wamechoma moto nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo kwa kutumia mafuta ya petroli yaliyokuwemo kwenye pikipiki yake na kuteketeza kabisa nyumba yake yote.

Mdogo wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo (aliyepofuliwa macho) aliyejitambulisha kwa jina la Paul Martin amesema tukio hilo limetokea usiku wa jana saa 4  ikiwa ni muda mfupi tangu aagane na kaka yake.

“Nilikuwa nyumbani kwake na nimeondoka wakati huo huo  kwenda kulala baada ya dakika chache kupita, tulianza kusikia kelele za watu nisiowafahamu wakiwa kwenye nyumba ya kaka yangu,” amesema.

Paul amesema baada ya kusikia kelele hizo alitoka nje ili ashuhudie lakini kabla hajafanya lolote aliwekwa chini ya ulinzi kwa kumulikwa tochi na kutishiwa kupigwa risasi.

"Niliona watu kama watano wakiwa na silaha ambao waliniweka chini ya ulinzi baada ya kunimulika tochi," alisema.

Amesema baadhi ya watu hao walikuwa ndani ya nyumba ya kaka yake wakiendelea kumhoji huku wakiwa wamefunika sura zao.

Ameongeza kuwa baada ya hapo watu hao waliondoka na kaka yake kwenda kusikojulikana na baada ya muda mfupi walirudi naye.

Amesema watu hao baada ya kurejea naye waliwaamrisha watoto wake waliokuwa wamelala kutolewa nje kisha walichukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye pikipiki ya kaka yake kisha kuyamwaga ovyo kwenye nyumba hiyo na kuichoma moto.

Amesema baada ya tukio hilo waliondoka naye kwa mara ya pili na kwenda naye kusikojulikana kisha wakampiga risasi ambayo imeharibu macho yake yote.

Amesema baada ya kumpiga risasi hiyo walimtelekeza katika barabara iendayo katika kijiji cha Misimbo ambapo walimkuta jana  asubuhi akiwa hajitambui.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea kwa matukio hayo.

Rais Magufuli kufungua maonyesho ya biashara Sabasaba

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kufungua Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sababsaba Julai Mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Rais atafanya ufunguzi huo katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Slaam.

Waziri Mwijage ameeleza katika taarifa hiyo kuwa lengo la maonesho ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na taasisi mbalimbali kutangaza biashara na huduma, kutoa fursa kwa wafanyabisashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza mitandao ya mawasiliano baina yao ambayo itasaidia kukuza biashara na kufikia malengo waliyojiwekeka na pia kutoa fursa ya kuuza bidhaa.

“Maonesho haya yanabeba kauli mbiu isemayo Ukuzaji wa Biasha kwa Maendeleo ya Viwanda, inanalenga kutumia Maonesho haya kama jukwaa la kutangaza biashara na huduma mbalimbali kwa ajili ya ukuzaji wa sekta ya viwanda, ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza uchumi wa viwada hapa nchini,” alisema taarifa ya Waziri.

Aidha Maonesho ya mwaka huu yatatoa fursa kwa wenye viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kukutana na wanunuzi wa bidhaa zao na kutakuwa na kampeni maalum ya kuhamasisha wananchi kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

“Napenda kuwafahamisha kuwa Tan Trade kwa kushirikiana na washirika wake kwa mara ya kwanza imeandaa Siku ya ‘Afrika Mashariki’ ambayo itaadhimishwa tarehe 6 Julai, 2017. Lengo la siku hii ni kuimarisha biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama inavyojulikana nchi hizi zimejaliwa kuwa na rasilimali nyingi hali ambayo itatoa fursa nzuri katika maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo ili kuwe na uchumi endelevu,” ilisema taarifa hiyo.

Katika maonesho hayo, Waziri anaeleza kuwa Tan Trade imeandaa eneo maalum litakalojulikana kwa jina la ‘Banda la Tanzania’ kwa ajili ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotengenzezwa ndani ya nchi na ‘Banda la Asali’ kwa ajili ya kukuza bidhaa za nyuki na pia kutakuwa na eneo maalum la wazalishaji wa bidhaa za ngozi ambalo washiriki wake watapata fursa ya kuonesha bidhaa bora za ngozi kwa ajili ya kuvutia wananchi wengi kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Katika kuimarisha huhusiano wa kibishara na kuwakutanisha wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao kutoka nje ya nchi, kutakuwa na banda maalum kwa ajili ya mikutano ya kibiashara yaani Business to Business (B2B) na pia banda maalum litakalotumika kwa utoaji wa mafunzo ya kibiashara.

Hadi sasa washiriki zaidi ya 2500 kutoka ndani na nje ya Afrika wamethibitisha kushiriki Maonesho ya mwaka huu. Nchi zitakazoshiriki ni Burundi, China, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Misri, Ujerumani, Ghana, India, Indonesia, Iran, Italia, Japan, Kenya, Malawi na Mauritius.

Nchi zingine ni pamoja na Morocco, Msumbiji, Namibia, Pakistani, Rwanda, Singapore, Afrika Kusini, Sudani Kusini, Syria, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Uganda, Marekani, Uingereza na Vietnam.


Mwanafunzi wa Shule ya DYCCC Ajirusha Toka Ghorofa ya Nne Hadi Chini

$
0
0
Mtoto anayedhaniwa kuwa ni Mwanafunzi wa  shule ya DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam amejirusha kutoka ghorofa ya nne mpaka chini huku chanzo cha tukio hilokikiwa bado hakijafahamika haraka.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto amekiri kutokea kwa tukio hilo ingawa taarifa hizo zipo kwenye mitandao na hazijafikishwa kituoni hapo lakini tayari wameanza kufuatilia ili kubaini nini chanzo cha cha tukio hilo

Hata hivyo Jina na umri wa mtoto huyo bado havijafahamika.

==>Tazama video zaidi ya tukio hilo.

Tangazo la Nafasi za Masomo ya DIPLOMA na CERTIFICATES Toka Chuo Kikuu cha SAUT- Mwanza

$
0
0
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania kampasi ya Mwanza, kinakutangazia nafasi za masomo katika ngazi ya DIPLOMA na CERTIFICATES kwa mwaka wa masomo 2017/2018 utakaoanza mwezi wa 10 mwaka 2017.

DIPLOMA PROGRAMMES:
1.    Ordinary Diploma in Accountancy
2.    Ordinary Diploma in Business Administration
3.    Ordinary Diploma in Psychology and Counseling
4.    Ordinary Diploma in Journalism and Media Studies
5.    Ordinary Diploma in Procurement and Supply Chain Management
6.    Ordinary Diploma in Computing, Information and Communication Technology
7.    Ordinary Diploma in Computer Science
8.    Ordinary Diploma in Law
 
SIFA ZA MWOMBAJI:
i) Mwombaji awe amehitimu kidato cha sita na amepata alama za ufaulu kiwango cha principal pass moja.    AU
ii) Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne na awe amepata alama za ufaulu kuanzia “D” 4 na awe na Astashahada katika fani husika.

CERTIFICATES PROGRAMMES:
1.    Basic Technician Certificate in Law
2.    Basic Technician Certificate in Business Administration
3.    Basic Technician Certificate in Accountancy
4.    Basic Technician Certificate in Health Administration
5.    Basic Technician Certificate in Tourism Enterprise Management
6.    Basic Technician Certificate in Logistics and Supply Management
7.    Basic Technician Certificate in Journalism and Media Studies
8.    Basic Technician Certificate in Computing, Information and Communication Technology
9.    Basic Technician Certificate in Computer Science
 
SIFA ZA MWOMBAJI:
i)    A amehitimu kidato cha nne na awe amepata alama za ufaulu kuanzia “D” 4 katika masomo yasiyo ya dini. Kwa waombaji wa kozi za Accountancy, Computer Science, na Information Technology wanatakiwa wawe na ufaulu wa “D” katika somo la hesabu.

•    Maombi yameanza kupokelewa chuoni kuanzia tarehe 15/05/2017
•    Fomu za maombi zinapatikana chuoni au katika tovuti ya chuo www.saut.ac.tz
•    Unaweza kufanya maombi kwa njia ya kielektroniki (Online application) kupitia tovuti ya chuo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa anuani:
Ofisi ya Msajili
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania                                              
S.L.P: 307
MWANZA, Tanzania 
 
Tel:     028 29 81186, 028 29 81187
Mob:     +255 744 509 110
+255 769 759 622
Email:     admission@saut.ac.tz

Programu hizi pia zinapatikana katika kampasi ya Arusha, Mbeya na Dar es Salaam.

Dawa Mpya ya UKIMWI Yaanza Kutumika Kenya

$
0
0
Hatimaye Kenya imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutumia vidonge vya ugonjwa wa Ukimwi ambavyo vinaweza kuboresha afya na kurefusha maisha ya maelfu ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa nyemelezi na ambayo hayakubali tiba nyingine.

Jina la dawa hiyo kitaalamu ni Dolutegravir (DTG), lakini itajulikana kama Tivicay, na inazalishwa na ViiV Healthcare, kampuni ambayo sehemu kubwa ya hisa zake inamilikiwa na GlaxoSmithKline.

DTG imekuwa dawa ambayo ni chaguo la kwanza la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa miaka miwili iliyopita katika nchi za watu wenye kipato kikubwa kwa kuwa ina athari chache, ni rahisi kutumia kuliko dawa za ARV zinazotumika sasa (yaani kidonge kimoja kidogo kila siku).

Kwa kutumia dawa hiyo, kuna uwezekano mdogo kwa wagonjwa kutengeneza usugu, kwa mujibu wa tovuti ya unitaid.eu.

Mwaka 2015, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipendekeza DTG iwe chaguo la kwanza kwa watu wazima na vijana, lakini hadi siku za karibuni watu wanaoishi na VVU katika nchi kama Kenya walikuwa hawawezi kupata dawa hizo.

Vidonge hivyo, ambavyo vilipitishwa kutumika nchini Marekani mwaka 2013, sasa vinagawiwa kwa wagonjwa 20,000 nchini Kenya kabla ya kupelekwa Nigeria na baadaye Uganda, kwa kusaidiwa na Unitaid, ambao ni wakala wa afya.

DTG ni dawa ambayo inatumiwa na watu wenye VVU ambao hawakuwahi kutumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi ya ARV.

“Nilikuwa na tatizo la mara kwa mara la kutokuwa na hamu ya kula,” alisema mkazi wa Nairobi, Doughtiest Ogutu alipozungumza na taasisi ya Reuters Foundation.

Ogutu alianza kutumia dawa hizo mwaka huu kwa sababu tiba nyingine hazikuwa zinamfaa.

“Hamu yangu ya kula imerejea, mwili wangu unafanya kazi vizuri.”

Ogutu, ambaye ameishi na VVU kwa miaka 15, alisema kiwango cha VVU mwilini mwake kimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka virusi 450,000 hadi 40,000 tangu aanze kutumia DTG.

Nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara zimekuwa zikiathiriwa sana na Virusi vya Ukimwi kwa miongo kadhaa na karibu robo tatu ya wakazi wake wana Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi (UNAIDS) linalenga kuwa asilimia 90 ya watu watakaogundulika kuwa na VVU wawe wamepata dawa hiyo ifikapo mwaka 2020.

Karibu asilimia 15 ya wagonjwa wa VVU hawawezi kutibiwa kwa kuwa dawa hazifanyi kazi mwilini mwao, alisema Sylvia Ojoo, mkurugenzi wa Shule ya Afya ya Chuo Kikuu cha Maryland nchini Kenya, ambaye anasimamia dawa hizo.

Tangazo la Nafasi za Masomo ( Bachelor Degree, Masters na PHD ) Toka Chuo Kikuu cha SAUT- Mwanza

$
0
0
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania kampasi ya Mwanza, kinakutangazia nafasi za masomo katika ngazi ya:
• Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree)
• Shahada ya Uzamili (Masters)
• Shahada ya Uzamivu (PhD)
 
Kwa mwaka wa masomo 2017/2018 utakaoanza mwezi wa 10 mwaka 2017
 
UNDERGRADUATE PROGRAMMES:
1. Bachelor of Business Administration
2. Bachelor of Science in Procurement and Supply Chain Management
3. Bachelor of Science in Tourism
4. Bachelor of Arts in Mass Communication
5. Bachelor of Arts in Public Relations and Marketing
6. Bachelor of Arts in Sociology
7. Bachelor of Arts in Economics
8. Bachelor of Arts in Philosophy
9. Bachelor of Philosophy with Education
10. Bachelor of Arts in Religious Studies
11. Bachelor of Science in Electrical Engineering
12. Bachelor of Science in Civil Engineering
13. Bachelor of Laws
14. Bachelor of Arts with Education
 
POSTGRADUATES PROGRAMMES:
1. Master of Sociology, Master of Laws
2. Master of Education Management and Planning
3.Master of Higher Education Management and Development
4. Master of Arts in Linguistic
5. Master of History
6. Master of Business Administration
1. Postgraduate Diploma in Accountancy and Finance
2. Master of Arts in Economic
3. Master of Arts in Mass Communication
4. Doctor of Philosophy in Mass Communication
5. Doctor of Philosophy in Law
 
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Maombi yote yatumwe moja kwa moja chuoni katika ofisi ya msajili.
 
Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi tembelea tovuti yetu: www.saut.ac.tz
 
Au wasiliana nasi kwa anuani:
Ofisi ya Msajili
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania
S.L.P: 307
MWANZA, Tanzania
 
Tel: 028 29 81186, 028 29 81187
Mob +255 744 509 110
+255 769 759 622
Email: admission@saut.ac.tz
 
Programu hizi pia zinapatikana katika Kampasi za Arusha na Mbeya

Lowassa Awasili Polisi na Kuhojiwa.......Atakiwa Kurudi Tena July 13

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa  amewasili katika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo (Alhamisi) kama alivyoelekezwa siku ya Jumanne wiki hii baada ya kuhojiwa kwa saa nne.

Lowassa amewasili saa 5:52 asubuhi akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe huku ulinzi mkali ukiwa umewekwa katika makao makuu hayo.

Kando na hao walikuwepo watu wengine aliombatana nao, lakini walizuiliwa kuingia na askari walioimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Askari hao pia waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo na kuwataka kusogea mbali ya viunga vya makao makuu hayo.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi Lowassa aliondoka katika makao makuu hayo huku Mbowe akieleza kuwa ametakiwa kurudi Julai 13 kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika

Lowassa alitakiwa kufika polisi leo tena kwa tuhuma za kutoa kauli ya kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23 na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.

Jumatatu wiki hii Lowassa alipokea wito wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz kwenda kuhojiwa juu ya tuhuma hizo na alitakiwa kuripoti saa 4 asubuhi siku ya Jumanne.

Lowassa aliwasili Jumanne saa 3:58 asubuhi kama alivyotakiwa akiwa na msafara wa magari manne ambayo yaliyosindikizwa na magari mawili ya polisi.

Alihojiwa kwa saa nne mfululizo kabla ya kuachiwa kwa dhamana saa 8:15 mchana na kuelekea nyumbani kwake, Masaki ambako alizungumza na vyombo vya habari.

Baada ya kuachiwa, wakili wake Peter Kibatala ambaye pia alikuwepo katika mahojiano hayo alisema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena kwa DCI leo saa sita mchana ili kujua taratibu watakazoambiwa.

Kibatala alisema Lowassa alihojiwa kwa kosa la uchochezi kwa kauli yake aliyoitoa Juni 23 na kwamba baada ya kuhojiwa aliandika Maelezo ya Onyo juu ya kauli yake ambayo imetafsiriwa kuwa ni ya kichochezi.

Maelezo hayo ya onyo yanaweza kutumika dhidi ya Lowassa kama akifikishwa Mahakamani.

Waziri Mkuu Ampongeza RC Anna Mghwira Kwa Kuzuia Malori 100 ya Mahindi

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kwa kuyazuia malori zaidi ya 100 yaliyokuwa yanasafirisha mahindi nje ya nchi.

Jumatatu hii, Majaliwa alipiga marufuku usafirishaji wa mahindi alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya Eid el Fitr.

Baada ya agizo hilo, malori hayo yalikamatwa na kuzuiwa. Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni leo  ( Alhamisi) juu ya zuio hilo, Waziri Mkuu amesema uamuzi huo ni moja ya hatua za kuhakikisha Taifa linajihadhari na ukosefu wa chakula hasa ikizingatiwa kwamba kulikuwa na uhaba wa mvua mwaka jana.

"Nampongeza Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa kuyazuia malori hayo," amesema Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  jana Jumatano, Mghwira alisema magari hayo yalikamatiwa eneo la Himo  huku akipiga marufuku usafirishwaji wa nafaka pamoja na sukari kwenda nchi jirani bila ya kuwa na kibali maalumu.

“Baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari na nafaka nyakati za usiku huku wakishirikiana na baadhi ya askari polisi ambao si waaminifu, ni vema askari hao wakaacha mara moja kwani ni kinyume cha maadili ya kazi zao,”alisema mkuu huyo wa mkoa.

IGP Simoni Sirro atembelea Kijiji alichouawa Mwenyekiti na Mtendaji Huko Kibiti

$
0
0
Baada ya  mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa.

IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.
IGP Simon Sirro akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mangwi, Kata ya Mchukwi alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji.
IGP Sirro aizungumza na Wananchi wa Mangwi alipowatembelea baada ya mauaji ya Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji
IGP Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa Wananchi wa kijiji cha Mangwi
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images