Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumannevya June 20


Uamuzi ya Mahakama kuhusu James Rugemalira na Harbinde Seth

$
0
0
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia na Rushwa (TAKUKURU) jana Juni 19, 2017 iliwafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili James Rugemalira na Harbinde Seth watuhumiwa wawili wa kesi za ESCROW na IPTL.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo wamesomewa mashtaka sita yanayowakabili likiwemo la uhujumu uchumi.

Akiwasomea mashtaka yao, Wakili wa Serikali, Paul Kadushi alidai Mahakamani hapo kuwa kosa la kwanza la kula njama linawakabili washtakiwa wote wawili ambapo inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Octoba 18, 2011 na March 19, 2014 katika maeneo tofauti ya DSM, Kenya, Afrika Kusini na India walikula njama kwa ajili ya kutenda kosa, ambapo walijipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Katika kosa la pili, la kujihusisha na mtandao wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida huku shtaka la tatu ni kughushi ambalo wakili Kadushi alieleza kuwa linamkabili Seth ambapo inadaiwa October 10, 2011 katika mtaa wa Ohio, Ilala DSM akiwa na nia ya ulaghai alighushi cheti cha usajili wa makampuni  na kuonesha yeye ni Mtanzania.

Aidha katika shtaka la kutoa nyaraka za kughushi ambalo pia linamkabili Seth ambapo anadaiwa alitoa nyaraka za kughushi katika Ofisi ya Msajili wa makampuni kwa nia ya udanganyifu akiwasilisha fomu namba 14 ya usajili wa makampuni ikionesha ni Mtanzania na mkazi wa mtaa wa Mrikau, Masaki Dar.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, wakili Kadushi alidai linawakabili washtakiwa wote wawili ambapo kati ya November 28 na 29, 2011 na Januari 23, 2014 katika Makao Makuu ya Benki za Stanbic na Benki ya Mkombozi tawi St. Joseph Dar  inadaiwa kuwa, kwa ulaghai washtakiwa hao wote wawili walijipatia Dollar 22,198,544.60 sawa na Tsh. 309b.

Wakili Kadushi alidai kuwa, shtaka la sita ni kusababisha hasara ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya November 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya Dollar za Kimarekani, 22, 198, 544.60 sawa na Tsh. 309, 461,358.27.

Baada ya kuwasomea makosa hayo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka, ambapo wakili Kadushi alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kesi kutajwa.

Mahakama hiyo ilisema upelelezi bado unaendelea na haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa hivyo walirudishwa rumande.

==>Hapo chini kuna hati ya mashtaka 6 yanayowakabiri

Zitto ampongeza Rais Magufuli, “Umeitendea nchi haki, hongera sana”

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemsifu Rais Dkt Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na rushwa ambapo amesema kwa muda wote, leo ameona kuwa vita ya ufisadi ina maana kubwa.
 
Zitto ameyasema hayo jana  kupitia ukurasa wake wa Twitter ambao aliandika jumbe kadhaa kupongeza jitihada hizo za Rais Magufuli ambapo katika moja ya jumbe zake alisema kuwa, kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa sakata la Tegeta Escrow ni moja ya hatua kubwa sana za Rais Magufuli dhidi ya rushwa.
 
Zitto alisema kuwa licha ya kuwa amekuwa akimpinga Rais Magufuli katika mambo mbalimbali na ataendelea kumpinga, lakini katika hili la kukamatwa kwa James Rugemarila na Harbinder Sethi anamuunga mkono na kumpongeza sana.
 
Hapa chini ni jumbe za Zitto alizoandika kupitia ukurasa wake wa Twitter;

Polisi Dar wazungumzia tukio la Walemavu kupigwa mabomu

$
0
0
Jeshi la Polisi Dar  limekutana na Waandishi wa Habari na kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali yaliyojiri na moja kati ya mambo hayo ni swala la  Walemavu waliotawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kuziba Barabara ya Sokoine June 16, 2017 wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa.

Jeshi hilo limesema kuwa halikutumia nguvu kupita kiasi kama inavyodaiwa lakini walitumia nguvu kulingana na watu waliokuwa wakifanya maandamano hayo.

"Hatujatumia nguvu ya kupita kiasi. Tumetumia nguvu kulingana na hali ya watu ambao walikuwa wanafanya maandamano hayo.

"Ulemavu, nataka nitoe rai kwa wananchi ulemavu sio kibali cha wewe kuvunja sheria wala ulemavu haukupi wewe kibali cha kuvunja sheria za nchi. Sheria za nchi zipo kwa mtu yeyote yule – mzima au mlemavu na hasa ambaye anazivunja kwa makusudi akijua.

“Hawa walemavu walifanya makosa, wamevamia Ofisi ya Mkurugenzi  wa Manispaa lakini pamoja na hivyo wakaziba njia. Tumejaribu kuongea nao kuwasihi kwamba wafungue njia lakini pia wateue viongozi wao kwenda kushughulikia matatizo yao lakini walikaidi. Kwa hiyo, ikabidi tutumie nguvu kidogo tukaenda kuwaondosha tukafungua barabara na wananchi wengine wakaendelea na shughuli zao.”

Hayo yalisemwa  jana  na Naibu Kamishna wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Operesheni za Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lakini kwa sasa anakaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali ambazo zimefanywa na jeshi hilo.

Muhimbili Yanasa Daktari Feki

$
0
0
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwa jina la Dkt. Abdallah Juma.

Aidha, kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu ya Hospitali hiyo huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.

Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye alikamatwa  jana.

Wananchi Bukombe waomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani

$
0
0
Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.

Wananchi hao walitoa ushauri huo jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alivyosimamia sekta ya madini,mkutano ambao ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.

Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,alisema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara.

Urusi Yaionya Marekani.....Yasema Itatungua Ndege Yoyote ya Muungano Unaoongozwa na Marekani

$
0
0
Urusi imeonya kuwa itashambulia ndege za muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria iwapo ndege hizo zitapaa katika maeneo ambayo jeshi lake linahudumu.

Hii ni baada ya ndege ya kivita ya Marekani kutungua ndege ya kivita ya serikali ya Syria.

Muungano huo unaoongozwa na Marekani ulisema ndege yake moja  ilitungua ndege ya Syria aina ya Su-22 baada ya ndege hiyo kuwaangushia mabomu wapiganaji  waasi wanaoungwa mkono na Marekani katika mkoa wa Raqqa, Jumapili.

Urusi, mshirika mkuu wa serikali ya Syria, imesema pia kwamba itakatiza mawasiliano yote na Marekani ambayo lengo lake huwa kuzuia ajali angani.

Syria imeshutumu shambulio hilo la Marekani na kusema litasababisha "matokeo mabaya sana".

"Ndege yoyote, ikiwa ni pamoja na ndege za kawaida na ndege zisizokuwa na rubani ambazo ni za muungano wa kimataifa unaohudumu magharibi mwa mto Euphrates, zitafuatiliwa na majeshi ya kukabiliana na ndege angani na ardhini na zitachukuliwa kama kitu kinachofaa kushambuliwa," wizara ya ulinzi ya Urusi  imesema.

Urusi imekanusha madai kwamba Marekani ilikuwa imewasiliana na maafisa wa urusi kabla ya ndege hiyo aina ya Su-22 kutunguliwa.

Maafikiano kati ya Urusi na majeshi ya muungano unaoongozwa na Marekani ya kushirikiana kuzuia ajali angani na pia kuhakikisha usalama yalifika kikomo Jumatatu, wizara hiyo iliongeza.

Hii si mara ya kwanza mawasiliano kusitishwa kati ya pande hizo mbili.

Aprili, mawasiliano yalisitishwa baada ya Marekani kurusha makombora aina ya 59 Tomahawk katika kambi ya ndege za kijeshi ya Shayrat, nchini Syria.

Marekani ilishambulia baada ya Syria kudaiwa kutekeleza shambulio la kemikali katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi katika mkoa wa Idlib.

Lakini mataifa hayo mawili yalifufua mawasiliano yao mwezi uliopita.

Ndege hiyo ya kivita ya Syria aina ya Su-22 ilitunguliwa na F/A-18E Super Hornet karibu na mji wa Tabqa mkoa wa Raqqa Jumapili alasiri, wizara ya ulinzi ya Marekani imesema.

Inaaminika kwamba ndicho kisa cha kwanza kabisa cha ndege yenye rubani ya Marekani kutungua ndege nyingine ya kivita yenye rubani tangu vita vya Kosovo mwaka 1999.

Waasi wa Syrian Democratic Forces (SDF) wanaoungwa mkono na Marekani, wamekuwa wakihudumu eneo la Tabqa.

Credit: BBC


Nape Nnauye Awataka Wapinzani Waungane Na CCM Kumtetea Rais Magufuli Kwa Kupigania Raslimali Za Nchi

$
0
0
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kuwataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi na wale wa upinzani kuungana pamoja katika kupigania rasilimali za nchi katika vita ambayo imeanzishwa na Rais Magufuli.

Nape Nnauye amesema hayo bungeni na kuwataka watu wa CCM wasipuuze mawazo ambayo yanatolewa na watu wa upinzani na kusema wanapaswa kuyafanyia kazi ili mwisho wa siku nchi iweze kufaidika na rasilimali hizo na kuwafanya kuwa pamoja katika jambo hilo na si kunyoosheana vidole.

"Katika hili tunaweza kugawanyika katika mitazamo wapo wale wanaounga mkono asilimia mia moja, wapo wale wanaopinga kwa namna wanavyowaza wao sasa kelele zisiturudishe nyuma lazima tusonge mbele sababu vita hii ni takatifu.

"Lakini tusipuuze kwani katika kelele nyingi kunaweza kuwa na ushauri mzuri ndani yake, isifike mahali tukapuuza kabisa hii vita ni ya kwetu wote, nchii hii ikifaidika katika jambo hili ni faida kwetu wote bila kujali itikadi zetu za vyama, sasa tusitoboane macho, tusitupiane vijembe visivyokuwa na maana ni wakati wa kuileta nchi yetu pamoja twende pamoja vita hii tushinde, kwa hiyo wapinzani na CCM na watu wengine wote bila kujali itikadi zetu nadhani ni vizuri tukaungana katika hili" alisisitiza Nape Nnauye

Mbali na hilo Nape Nnauye alisema kuwa anachokifanya Rais Magufuli sasa anapita katika msingi ambao watangulizi wake waliuweka hivyo anadai viongozi hao wastaafu walifanya kazi kubwa kulinda rasilimali za nchi kwa uwezo wao, hivyo dhana ya kuona hawakuwa na jitihada za kulinda rasimali hizo si sawa.

"Hizi juhudi za kulinda rasilimali za nchi yetu hazijaanza awamu ya tano, zimeanza toka awamu ya kwanza ya mwalimu Nyerere kuna mambo alifanya kulinda rasilimali zetu hata kama kutakuwa na mapungufu, awamu ya pili ya mzee Mwinyi yapo mambo aliyafanya, awamu ya tatu ya mzee Mkapa yapo mambo aliyafanya, awamu ya nne ya Mhe. Kikwete yapo mambo ameyafanya mazuri tu, kwa hiyo hakuna namna tutapuuza juhudi zilizofanywa na watangulizi wa Mhe. Magufuli kwa sababu nao wana mchango hata kama leo itaonekana kulikuwepo na mapungufu lakini kwa nafasi zao walitimiza wajibu wao" alisema Nape Nnauye

Godbless Lema Atoa Neno Kwa Vijana

$
0
0
Mbunge Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri mwingine mpya kuwa katika nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kila nyumba itakuwa na watu waliomaliza shahada ya kwanza na 'masters' lakini hazitakuwa na tija katika maisha yao na nchi kwa ujumla.

Godbless Lema amesema hayo alipokuwa katika mahafali ya Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO) ambapo amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili na maono katika maisha yao huku akisema hata katika vita ambayo nchi inapigana sasa, watu wanaoturudisha nyuma ni wasomi ambao wameshindwa kutambua wajibu wao.

"Ambalo mimi naliona ni vijana wenye vyeti lakini hawana 'moral authority' nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kutoka sasa utakuta kila familia ina degree, kila familia ina masters lakini zisizona tija. Wasomi wasio na moral authority ni hatari kuliko wajinga wenye moral authority na hata ukiangalia kwenye haya mapambano wanaofanya kazi yetu inakuwa ngumu ni wasomi ambao wameshindwa kujua wajibu wao" alisema Godbless Lema

Mbali na hilo Lema amesema wasomi wengi wa sasa ambao ni vijana wamekuwa ni watu wasiojali mambo ya msingi, wamekuwa wakijali sana mambo yasiyokuwa na tija katika nchi au taifa na kuikacha siasa ambayo ndiyo msingi wa kila kitu.

"Vijana wa sasa hamjali mnajua mambo ya mipira, yaani vijana wasomi wa nchi hii wanajua zaidi mipira sijui 'Premier League' mimi siyajui vizuri hayo mambo, yaani 'commitment' yenu kwenye mambo ambayo hayawezi kuleta tija kwenye nchi imekuwa kubwa kuliko 'commitment' yenu kwenye mambo ya siasa" alisisitiza  Lema

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

$
0
0
Jeshi la Magereza limefanikiwa kumkatamata Ramadhan Nombo mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutaka kuingiza simu tano kinyume cha sheria katika gereza la Keko wilayani Temeke.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustine Mboje jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni katika gereza hilo.

Alisema Nombo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kuanzia 30 na kuendelea alidakwa wakati akifanyiwa upekuzi katika eneo maalumu la ukaguzi wa wageni mbalimbali wakiwamo wanaowatembelea ndugu na marafiki walioko mahabusu kwenye gereza hilo.

“Huyu (Nombo) alikuwa katika foleni ya mstari wa mwisho ya watu wanaokwenda kuwaaona ndugu zao walioko ndani ya gereza hili. Nadhani hakujua kama sisi kama magereza tuna vifaa vya kisasa vya ukaguzi.

“Ilipofika zamu yake askari wetu walimfanyia ukaguzi na kabla haujaisha kifaa hiki maalumu kiliita alamu kuashiria kuna kitu tofauti,” alisema Mboje.

Alisema alibainika kuwa na simu hizo alizozifunga kitaalaamu na kuficha katika mapande ya nyama yaliyopikwa kwa ustadi wa juu na kuchanganywa na viazi aina ya mbatata.

Mkuu huyo wa magereza, alisema tukio hilo siyo la kwanza katika gereza hilo kwani linatokea katika magereza mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam likiwamo la Segerea.

“Wengine wanatumia hadi mbinu ya kuficha simu hizi katika ugali na mikate lakini tunafanikiwa kuwakamata kutokana na uimara wa vifaa na askari wetu,”alisema Mboje

Mbunge wa CCM Abanwa Bungeni Baada ya Kuwatuhumu Wapinzani Kwamba Wamekula Hela za Rambirambi za Msiba wa Ndesamburo

$
0
0
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Jackline Ngonyani jana alizua kizaazaa bungeni baada ya kuwaambia wabunge wa upinzani wamekosa dira kiasi cha kula rambirambi zilizotolewa kwenye msiba wa Philemon Ndesamburo.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya mwaka 2017/18. Baada ya kuzungumzia hoja zake, Ngonyani alielezea kilichotokea kwenye salamu za pole zilizotolewa wakati wa msiba wa muasisi huyo wa Chadema aliyewahi pia kuwa mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo.

Mbunge huyo alianza kwa kumpongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani ya CCM na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi, akidai utekelezaji huo unawanyima hoja wapinzani.

Aliyafananisha maneno ya wapinzani na miti kuteleza siku ya kifo cha nyani, akisema licha ya kueleza kwamba Rais anatumia sera zao, wapinzani hao wamesahau changamoto zinazowakabili wananchi kwenye majimbo yao.

Mbunge huyo alimshambulia mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari.

Alimshangaa Heche kwa kuomba muongozo kutokana na wananchi wa jimbo lake kuvamia mgodi wa North Mara ulio chini ya kampuni ya Acacia baada ya kukabiliana na askari polisi.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Mussa Azzan Zungu alimtaka kuwasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kupata ufafanuzi wa suala hilo kutoka serikalini.

“Huyu Heche aliongea humu ndani kuhusu wananchi wake kulinda mgodi, leo anajikosha kwa kuomba muongozo. Rais hakusema watu wakavamie migodi, hao wakamatwe kama wahalifu wengine. Huyu naye akamatwe na kuunganishwa pamoja na wavamizi hao,” alisema.

Baada ya kauli hiyo, Heche alisimama na kumpa taarifa mbunge huyo kwa kueleza kwamba jina lake linatumika vibaya. Alikumbusha kwamba wananchi wake walifuatilia uwasilishaji wa ripoti ya kamati na kufahamu kwamba kampuni hiyo ni feki.

“Nilisema sisi tumeumizwa, sasa kama unafikiri naogopa kuunganishwa hebu njoo unikamate wewe,” alisema.

Baada ya taarifa hiyo, Jackline alimwambia Heche: “Usinipotezee muda, nina mambo mengi ya kuzungumza.”

Baada ya kuachana na Heche, mbunge huyo alimvaa Nasari kwa kueleza kwamba alitumia dakika 10 alizopewa kulalamika juu ya uharibifu uliofanywa kwenye shamba la maua la mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

“Hizi ni akili au matope? Wananchi wake hawana changamoto? Ni mambo ya aibu sana,” alisema mbunge huyo akikaribia kuhitimisha mchango wake kwenye mjadala huo.

Kabla hajakaa, sauti ilisikika ikimkumbusha suala la kuliwa kwa fedha za msiba huo, kengele ya kuisha kwa muda wake ikiwa imeshagongwa, alitupa kijembe wa upinzani.

“Nakushukuru sana mwenyekiti, naunga mkono hoja na (wapinzani) waache kula rambirambi za msiba wa Ndesamburo,” alisema Ngonyani.

Kauli hiyo iliwafanya wabunge wa upinzani wacharuke na kumtaka afute maneno hayo.

Alikuwa ni mbunge wa viti maalumu (Chadema), Cecilia Pareso aliyemng’ang’ania baada ya kutoa taarifa kwamba kilichozungumzwa na Jackline si sahihi na kumtaka kufuta maneno hayo au kuthibitisha tuhuma hizo.

Mbunge huyo alikubali kuyaondoa maneno yake kwenye kumbukumbu kutokana na kukosa ushahidi wa alichokisema.

“Mwenyekiti, kwa sababu ni suala la msiba, nayaondoa maneno hayo,” alisema na kuhitimisha suala hilo lililowagusa wabunge wengi wa upinzani waliokuwapo kwenye kikao cha jana asubuhi.

Waziri Nchemba Radhi Sakata la Walemavu Kupigwa na Jeshi la Polisi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba leo bungeni amefunguka na kuomba radhi dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu.

Mwigulu Nchemba amekiri kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kwa watu hao na kusema serikali wamepokea jambo hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili siku nyingine lisijirudie.

"Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie" alisema Mwigulu Nchemba

Mnamo tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuwasilisha malalamiko dhidi ya askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katika jiji. Lakini pia walikuwa wakipigania haki yao ya kuwa na maeneo ya kuegesha vifaa vyao katikati ya jiji.

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo Ammwagia SIFA Rais Magufuli

$
0
0
Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonesha mfano bora katika Bara la Afrika katika kusimamia uchumi na kutetea maslai ya nchi katika uwekezaji.

Mhe. Rais Mstaafu Obasanjo ametoa pongezi hizo leo tarehe 20 Juni, 2017 muda mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Mstaafu Obasanjo amesifu juhudi za Mhe. Rais Magufuli kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali duniani na kusimamia ipasavyo sera ya kuhakikisha nchi inanufaika, badala ya kuacha wawekezaji wakijinufaisha wenyewe na nchi kuambulia kiasi kidogo cha mapato.

“Nimepita katika nchi kadhaa zikiwemo Msumbiji, Malawi na sasa nipo hapa Tanzania, na huko kote nazungumzia masuala ya uchumi na namna nchi zetu za Afrika zinapaswa kunufaika na uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

“Uchumi wa Tanzania unakwenda vizuri sana, na juhudi za Mhe. Rais Magufuli za kuhakikisha nchi yake inanufaika na uwekezaji ni suala muhimu sana na la mfano, ameonesha mfano mzuri kwa viongozi wa Afrika na hii ndio njia pekee itakayotuwezesha kukuza uchumi wetu, hatuwezi kuendelea kuwaacha wawekezaji wananufaika wao na sisi kuambulia kiasi kidogo sana” amesema Mhe. Rais Mstaafu Obasanjo.

Jaji Mwingine wa Mahakama Kuu AJIUZULU......Rais Magufuli Aridhia

$
0
0
Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Mwendwa Judith Malecela amejiuzulu wadhifa wake huo kuanzia leo baada ya Rais Magufuli kukubaliana na ombi la jaji huyo aliyetaka kujiuzulu wadhifa wake.

Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu leo imedai kuwa Rais Magufuli amekubaliana na ombi la Jaji huyo hivyo kuanzia leo tarehe 20 Juni, 2017 Judith Malecela hatakuwa tena Jaji wa Mahakama Kuu. 

Waraka wa David Kafulila kwenda kwa Rais Magufuli

$
0
0
Hatimaye imekuwa! Vinara katika ufisadi wa IPTL/ESCROW Singasinga Seth na Rugemarila watiwa nguvuni. Huu ni uamuzi mkubwa uliosubiriwa sana. Na siku zote sikujua kwanini Mhe Rais alikuwa anahofu kuagiza hatua hii.

Sikujua kwanini, kwasababu wakati wa mnyukano wa hoja hii, Mhe Rais alikuwa bungeni na alikuwa sehemu ya maazimio ya Bunge kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na wahusika watiwe nguvuni..

Nakumbuka nikiwa kwenye kipindi kigumu hata kutishwa kuondolewa kichwa na kuitwa majina ya wanyama, yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri 5, walionidokeza kwamba ESCROW ni dili nikomae tu mpaka kieleweke!

Nampongeza Mhe Rais kwa uamuzi huu muhimu uliosubiriwa siku nyingi kuamua hatma ya ufisadi huu uliomshinda vibaya mtangulizi wake.

Singasinga huyu alinifungulia kesi kunidai Sh300bn Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2014, Agust2015 nikamshinda lakini akaamua kunifungulia upya Mahakama ya Kisutu akidai Sh100m, zote akidai nimsafishe kuwa yeye na wenzake hawakuchota zaidi ya 300bn kifisadi.

Kifupi naomba PCCB na DPP wasituangushe watanzania. Nilipata kuwaza kumwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali anipe kibali niendeshe kesi na hawa majabali wa escrow kwani nina ushahidi wakutosha,Sasa nina furaha kwamba PCCB wameamua kuwaburuza.

Nashauri mambo machache;
1.Mali zote za wahusika hawa ziwekwe chini ya ulinzi kabla hawajahamisha umiliki kwani ni muhimu zikakamatwa kusubiri hukumu ya kesi hii ya Tanzania lakini pia kesi iliyopo Mahakama ya kimataifa ya International Centre For Settlement of Investment Disputes (ICSID). Ambako Septemba 2016, iliamuliwa tulipe Bank ya SCB-HK kiasi zaidi ya 400bn kwa kuwa ndio wamiliki halali wa IPTL na wenye share certificate za IPTL..

Mwaka huu TANESCO imekata rufaa. Najua TANESCO hawajakata rufaa kushinda kesi bali kuomba wapunguziwe hukumu ifanane na uamuzi wa ICSID wa Feb 2014.

Lakini kwakuwa Singasinga Seth alisaini hati na Benki Kuu ya Tanzania, kwamba deni lolote lotakalotokana na migogoro ya IPTL atawajibika yeye na wenzake wanaomiliki kampuni PAP, ndio maana nasisitiza Mali za watu hawa zishikiliwe.

2. Mtambo wa IPTL uwekwe chini ya TANESCO kama ilivoazimiwa na Bunge Nov 2014, tuachane kabisa na kulipa matapeli 7bn kila mwezi ambazo ni malipo ya capacity charges walizokuwa wanalipwa na serikali hii bila kujali IPTL imezalisha au haijazalisha umeme.

3. Mwisho watanzania watambue kwamba huyu Singasinga anaetambulishwa kama mmiliki wa PAP iliyopora 300bn za escrow kama mmiliki mpya wa IPTL, mpaka fedha hizo zinaporwa alikuwa anamiliki asilimia50% tu ya kampuni lakini asilimia 50 zilikuwa zikimilikiwa na kampuni ijulikanayo kama SIMBA TRUST, inayomilikiwa na watu wasiojulikana. Hawajawahi kutajwa popote kwenye report zote.

Nilijaribu kutaka majina yao kwenye Kamati ya Viwanda wakati tukiwahoji BRELA na hata baadae bungeni Serikali iliendelea kusisitiza kuwa majina hayo ni SIRI. Hawa ni wahusika muhimu sana wajulikane kwani inawezekana ndio msingi wa serikali ya awamu ya nne kuibeba IPTL kama mtoto!

Naam, hongera Mhe Rais kwa hatua hii, nazidi kuomba Mungu kesi hizi zifike mwisho kwani kwangu leo ni siku muhimu katika kumbukumbu zangu kuliko Aprili 28, 2015, siku niliyopewa tuzo kwa mapambano dhidi ya ufisadi kwa rejea ya sakata la ESCROW, kwani tuzo haina maana kama vita haifiki mwisho.

Mwisho nishauri asiwepo yeyote wakulindwa kwa Kinga yoyote kwani Katiba na Sheria vipo kwa ajili ya watanzania na sio watanzania kwajili ya Katiba na Sheria. Tusipofika huko vita ya UFISADI mkubwa itakuwa ngumu sana kufika mwisho.

David KAFULILA
JUNE19,2017

Sumaye aiangukia Serikali, aomba kukivumilia Chadema

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kuitaka serikali ya awamu ya tano iwavumilie na itambue kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama CCM inavyofanya kazi zake.

Sumaye aliyasema hayo jana baada ya jeshi la polisi kuzuia msafara wao ambao ulikuwa na lengo la kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA.

"Hili si jambo la ajabu kwa sababu hata viongozi wa CCM kwa mfano hata Pole Pole anazunguka halmshauri zote nchini, ila wanapozunguka wao hakuna tatizo ila inapokuja viongozi wa CHADEMA kidogo tayari wanaanza mapambano, tunadhani huu ni uonevu tu unaendelea wa kujaribu kuwafanya watu wengine wajisikie kwamba hawana uhuru na nchi yao hili nafikiri si jambo jema.

"Serikali tunaomba ituvumilie ijue kwamba CHADEMA pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama CCM wanavyofanya kazi kwa hiyo mambo ya kuandamwa CHADEMA kila mahali inatusikitisha sana" alisema Sumaye

Mbali na hilo Sumaye anasema vitendo hivyo vinavyofanywa kwa viongozi wa CHADEMA ni kutaka kukatisha tamaa jitihada zozote zinazofanywa na viongozi wa chama hicho hivyo anadai ni kitu ambacho hakiwezi kuvumilika.

"Kwa jambo hili mimi nataka tu kuimbia serikali kuwa hawatafanikiwa kwani wataleta vurugu pasipo kuwa na sababu zozote zile, wawaache watu wafanye kazi zao hapa hakuna siasa zozote tunazofanya.

"Tunakagua miradi kwani halimashauri hizi ni zetu kama ambavyo wao wanatembea kwenye halimashauri zote nchini kuona namna Ilani yao inavyotekelezwa na sisi tunataka kujua viongozi wetu wa CHADEMA wanatekeleza vipi yale ambayo CHADEMA imewaagiza kufanya katika Ilani yake. Na miradi hii ni kwa wananchi wote" alisisitiza Sumaye   

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya June 21

Rais Magufuli: Hatutaki Umeme wa MATAPELI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Pwani kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla inatekelezwa kama alivyoahidi.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Bwawani Mjini Kibaha akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku 3 Mkoani Pwani.

Mhe. Dkt. Magufuli ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambayo imeanza kujengwa, ujenzi wa barabara ya njia sita kati ya Dar es Salaam na Chalinze yenye urefu wa Kilometa 128, ujenzi wa bandari kavu ya Ruvu itakayopokea mizigo ya kutoka bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) ambao mipango ya utekelezaji kwa kushirikiana na Ethiopia imeanza.

Amebainisha kuwa pamoja na kutekeleza miradi hiyo Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watu wanaolihujumu Taifa ikiwemo kujihusisha na vitendo vya wizi na rushwa na haitakatishwa tamaa na watu wanaolalamika na kubeza juhudi hizo.

“Stiegler’s Gorge mradi ambao ulifanyiwa utafiti tangu enzi ya Mwl. Julius Nyerere, tukautelekeza, nataka tujenge bwawa litakalozalisha umeme utakaotosheleza katika nchi yetu, nchi ya viwanda, ili Watanzania wasilalamikie tena suala la umeme, nataka tuachane na umeme wa matapeli wanaokuja hapa wanawekeza kwa lengo la kutuibia.

“Mimi nachukia wezi, na kwa kweli wezi watakoma tu, awe mwizi wa Tanzania, awe mwizi wa Ulaya, awe anatoka magharibi, mashariki, kaskazini au kusini, mwizi ni mwizi tu” Alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi na wananchi wa mkoa wa Pwani kwa Mkoa huo kutekeleza vizuri sera ya ujenzi wa viwanda na ametaka viongozi wa Mikoa mingine waige mfano huo ili kuwawezesha wananchi kupata ajira na kujiongezea kipato.

Kuhusu mauaji yanayotokea katika Wilaya za Kibiti na Rufiji Mkoani humo, Mhe. Rais Magufuli amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo lakini amesema Serikali imeanza kuwashughulikia wanaowahalifu hao na itahakikisha inakomesha tatizo hilo.

Mapema akitoa taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa humo Mhandisi Evarist Ndikilo amesema mkoa huo una jumla ya viwanda 371 vikiwemo viwanda 9 vikubwa na kwamba ujenzi wa viwanda hivyo unaendelea katika hatua mbalimbali.

Leo  tarehe 21 Juni, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Pwani ambapo atazindua viwanda vitatu ambavyo ni kiwanda cha vifungashio cha Global Packaging Co. Ltd, kiwanda cha matrekta cha Ursus-TAMCO Co. Ltd na kiwanda cha chuma cha Kiluwa Steel Group.

Pia atazindua mradi wa maji wa Ruvu na kuzungumza na wananchi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Kisukari Ni Ugonjwa Unao Weza Kudhibitiwa Kwa Kutumia Tiba Asilia

$
0
0
Kisukari  ni  tatizo  la  kiafya  linalo wasumbua  na  kuwatesa  mamilioni  ya  watu  duniani. Miongoni  mwa  dalili  za  ugonjwa  wa  kisukari ni pamoja  na

i. Kukojoa  mara  kwa  mara  ( Watoto kukojoa  kitandani )

ii.Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.

iii.Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.

iv.Kupungua uzito  kwa  kasi  au kukonda pamoja na kwamba unakula  vizuri  tena kila  wakati  kwa  sababu  ya  kusikia  njaa kila  wakati  kunakosababishwa  na  maradhi  ya  kisukari

v.Wanawake  kupatwa  na  tatizo  la kuwashwa ukeni.

vi.Kupoteza  uwezo  wa Kuona  vizuri.

vii.Wanaume  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu na / ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  na  wanawake  kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa.

viii.Kupatwa  na  ganzi,  kusikia  hali  ya  kama  kuchomwachomwa au kutohisi chochote  pindi  unapoguswa  kwenye  sehemu za miguu, viganjani na  kwenye  vidole.

ix.Miguu kuoza na hata kupata gangrini.

x.Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.

xi.Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.

xii.Kutokwa  na   Majipu kwenye  sehemu  mbalimbali  mwilini.

Kwa  mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu , watu walio katika makundi yafuatayo  wapo katika  hatari  kubwa  ya  kupatwa  na  ugonjwa wa kisukari kuliko watu wengine.  Watu  hao  ni  kama  ifuatavyo :

i. Watu  wenye   uzito uliozidi,

ii.Watu  wanao  toka  katika  familia  zenye  historia  ya  kuwa  na  wagonjwa  wa  kisukari.

iii.Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

iv. Watu   wasio  fanya  mazoezi

v. Wagonjwa  wa  shinikizo la damu,

vi.Watu wenye  kiasi  kikubwa  cha  lehemu  mbaya  ( Bad  Cholestrol ) kwenye  damu.

vii.Watu  wenye   virimba  tumo (  vitambi):  Wataalamu  wa  afya  wanaeleza  kuwa, kuna hatari kubwa ya kupatwa na maradhi  ya  kisukari ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu

viii.Watu  wenye msongo wa mawazo na

ix.Watu  wanao tumia  pombe  na kupita  kiasi  pamoja  na  wale  wavutaji  wa  sigara  kupita  kiasi: Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa  na  tatizo  la  kisukari,kwani kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu, uvutaji  sigara huathiri  moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu.  Tafiti  mbalimbali  za  kiafya  zinaeleza  kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

x. Kundi  jinginge  la  watu  walio  katika  hatari  ya  kupatwa  na  maradhi  ya  kisukari  ni  watu wenye  umri  mkubwa  kuanzia  miaka  55  na  kuendelea

Wataalamu  wa  afya  wanashauri  watu walio  kwenye   orodha  iliyo  tajwa  hapo  juu, kujiwekea  utaratibu  wa  kuwa  wanapima  afya  zao  walao  mara  moja  kila  mwakaili waweze  kuchukua  hatua  stahiki  za  kiafya endapo  watakutwa  na  tatizo  la  sukari.
TIBA   ASILIA   KWA   WAGONJWA   WA  KISUKARI
Zipo  tiba  asilia  mbalimbali  zinazo  saidia  kkupunguza  maradhi  ya  kisukari. Miongoni  mwa  tiba  hizo  ni  pamoja  na  tiba  ijulikanayo  kama  Mkatasukari. Tiba  hii  inasaidia kushusha  na  kudhibiti  kiwango  cha  sukari  kwa  mgonjwa mwenye  sukari  ya  kupanda. Kama  unasumbuliwa na  maradhi  ya  kisukari ( Sukari  ya  kupanda ), unaweza  kujaribu  kutumia  tiba  hii.

JINSI   YA   KUANDAA  TIBA  ASILIA  YA  MKATASUKARI

Mahitaji  ;
i. Nanasi  moja  kubwa

ii. Majani  ya  chai  vijiko vitatu vya  chakula

iii. Maji  lita  tano

iv. Dawa asilia  ya  Mkatasukari  vijiko  vikubwa  vitatu.

MATAYARISHO:  Chukua  nanasi  lako  lililo  iva  vizuri, limenye  kisha  likate  vipande  vidogo vidogo,  kisha  liweke  kwenye  sufuria  halafu ndani  ya  sufuria  hilo, ongeza  lita  tano  ya  maji  safi.  Baada  ya  hapo  weka  majani ya  chai vijiko  vikubwa  vitatu, kisha  ongeza  vijiko  vikubwa vitatu  vya  dawa asilia  ya  Mkatasukari, kisha  chemsha  kwa  muda  wa  dakika  thelathini (30).

Baada  ya  dakika  thelathini, ipua   na  uchuje, makapi  weka  pembeni, kisha  hifadhi  kimiminika  chako  kwenye  chombo  safi.

MATUMIZI  :
Tumia  kunywa  kikombe  kidogo chenye ujazo milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills ) au  robo  lita  kwa  lugha  nyepesi. Utafanya  hivyo  mara  tatu  kwa  siku, asubuhi  mchana  na  jioni  hadi  dozi  yako  itakapo  kamilika.

Baada  ya  kutumia  dozi  hii, unashauriwa  kwenda  hospitali  kupima   tena  sukari  ili  ujue  sukari  yako  imeshuka  kwa  kiasi  gani  pamoja  na  kupata  ushauri  wa  daktari  wako.

Kwa  mahitaji  yako ya  tiba  asilia  ya  Mkatasukari, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM,  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini DAR  ES  SALAAM, ambao  hawawezi  kufika  ofisini kwetu., tunatoa  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY ), kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  watasafirishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti, kwa  wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabasi mbalimbali. Wateja  waliopo NAIROBI  na  MOMBASA  watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  usafiri  wa  mabasi  mbalimbali.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83 84

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu ;

Rais Magufuli Atuma Salam Za Rambirambi Kwa Klab Ya Yanga Na CCM Kwa Kifo Cha Ally Yanga

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uongozi wa Klabu ya Yanga na wanamichezo wote kwa ujumla kufuatia kifo cha shabiki mkubwa wa timu ya Yanga Bw. Ali Mohamed maarufu kwa jina la Ali Yanga.

Ali Yanga amefariki dunia jana tarehe 20 Juni, 2017 kwa ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chipogolo kilichopo katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli atamkumbuka Ali Yanga kwa uzalendo wake na mchango wake wa kuhamasisha na kushabikia masuala mbalimbali ya kitaifa na hasa michezo, ikiwemo kuishabikia timu yake ya Yanga, timu ya soka ya Taifa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na shughuli za kiserikali kama vile Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi.

“Nimeguswa sana na kifo cha Ali Yanga, nilikuwa nae wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo alitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi kukipigia kura chama changu cha CCM, na pia amekuwa akiongoza mashabiki wenzake kuishabikia timu ya Yanga na timu ya Taifa bila kuchoka. Kwa kweli alikuwa hodari sana katika ushabiki wake.

“Natoa pole nyingi sana kwa familia yake, viongozi wa timu ya Yanga, wanamichezo wote, wana CCM na wote walioguswa na kifo cha Ali Yanga na namuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kibaha, Pwani.
21 Juni, 2017
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images