Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mke mdogo wa Mzee Yusuf Afariki Dunia

0
0
Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku).

Chiku amefariki usiku wa kuamkia leo  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua.

Mzee Yussuf amesema kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana jana  saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

SORRY MADAM -Sehemu ya 70 & 71 (Destination of my enemies)

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Eddy alipo isikia sauti ya Ranjiti kwenye simu ya raisi Praygod, akasimama kwa haraka kwenye sofa alilo kaa, kisha akaikwapua simu kutoa mkononi mwa raisi Praygod na wafanya watu wote wamshangae.
“RANJITI, SIKU NIKUKITIA MIKONONI MWANGU NITAHAKIKISHA KWAMBA KICHWA CHAKO KINAKUWA MALI YANGU”
“Wee…..weee si Eddy”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa wasiwasi mkubwa
“NDIO MIMI NI EDDY, MUME HALALI WA PHIDAYA”
Eddy alizungumza kwa sauti yanye msisitizo na kuwafanya Rahab na raisi Praygod wote kushtuka na kujikuta wakinyanyuka kwenye sofa na kumshangaa, kwani kati yao hakuna aliye weza kumgundua kwamba kijana huyo ni Eddy, ambaye alikuwa ni waziri wa ulinzi katika serikali yao na ni adui wa mapenzi wa raisi Praygoda, kwani aliweza kugundua Eddy alishirikia tendo la ndoa na mke wake kipenzi Rahab.

ENDELEA
   Simu ikakatwa na kumfanya Eddy kuishusha simu hiyo kutoka sikioni mwake kwa hasira. Hakuhitaji kuujali mshangao wa Rahab na raisi Praygod kwa maana alitambua ya kwamba ni lazima watapata mshangao huo ndio maana hakuhitaji sauti yake iweze kusikika kwa Rahab na mumewe.
“Eddy ni wewe?”
Raisi Praygod alizungumza huku akiendela kumshangaa Eddy aliyesimama, akionekana ni mwingi wa hasira.
“Hilo ni jibu na si swali”

Eddy alizungumza huku akimrudishia simu raisi Praygod. Eddy akamtazama Sa Yoo, na kumpa ishara ya kunyanyuka ili waondoke.
“Ahaa hapana Eddy, tukae tuzungumze”
Raisi Praygod alizungumza kwa busara sana, huku akimtazama Eddy machoni.
“Nikae wakati sifahamu mke wangu ni wapi alipo”
“Ndio maan mke wangu alimfwata huyo binti akimini ya kwamba yupo peke yake na alihitaji anahakikisha kwamba anamkomboa mkeo”
“Eddy, natambua haupo vizuri, hembu kaa basi tuangalie ni nini cha kufanya kwa wakati huu, ili kumuokoa Phidaya”
“Eddy kaa”

Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya upole. Taratibu Eddy akakaa sehemu ambayo alikuwa amekaa kwa mara ya kwanza.
“Ila ninawazo moja. Munaonaje tukaifwatilia simu hiyo kupitia satelaiti”
Sa Yoo alizungumza huku akiwatazama watu wote, Rahab akanyanyuka na kuwaomba wamsubirie. Akaingia chumbani kwake, alipo toka akarudi akiwa amebeba laptop aina ya Apple(macbook air), huku mkono wake mwingine akiwa ameshika karatasi mbili ndogo.

“Kuna namba za simu yangu ile nilizo zinunua, hizi hapa”
Sa Yoo akanyanyuka na kusogea sehemu alipo Rahab, akachukua karatasi hizo na kuzitazama vizuri, akaiziona namba ambazo zimesajiliwa simu hiyo na hata endapo itakuwa imezimwa, kwa kupitia sateleitii ni lazima utaipata. Kwa haraka Sa Yoo akaanza kuifanya kazi hiyo kutokana ana ujuzi wa kazi hiyo.

Kila mtu macho yake akayaweka kwenye kioo cha Laptop hiyo, inayo tafuta kwa kasi ni wapi ilipo simu ya Rahab. Ndani ya sekunde arobaini na moja, tayari ramani ikaanza kujitokeza kwenye lapotop, alama ya kijana ikaanza kujionyesha kwenye ramani hiyo ikiashiria kwamba ndipo sehemu ilipo simu hiyo.

“Hii simu ipo katika mtaa El khaing, na sisi tupo huku Al Kerdas. Ili kuweza kufika sehemu naamini ilipo kambi hiyo ni lazima kupita katika daraja la Qasr al-nil ili kuweza kufika. Na kwa haraka haraka tunaweza kuchukua muda kama lisaa moja na nusu hivi”
Sa Yoo alizungumza huku akiwaonyesha kwa kidole jinsi ramani hiyo inavyo kwenda.
“Ila simu yangu nahisi kama niliipoteza walivyo nitelekeza”
“Ulirudije huku?”
Sa Yoo alimuuliza Rahab huku akiwa amemtumbulia macho
“Nilirudi kwa kukimbia, kutokana huo mtaa walio niacha niliweza kuufahamu kwani ni kwa mara kadhaa ni kichukua mazoezi asubuhi huwa ninapita hapo”

“Ulilipita hili daraja?”
Ikambidi Rahab kuitazama vizuri ramani hiyo.
“Hapana sikupita”
“Basi, inabidi kuweza kuifwatilia simu hii sehmu ilipo”
Sa Yoo alizidi kuzungumza kwa kujiamini na kwa msisitizo mkubwa.
“Sa Yoo unaweza kuitafuta namba ya huyo Ranjiti sehemu ilipo tokea”
“Yaa ngoja mara moja”
Sa Yoo akaaiombanamba hiyo na kuonyeshwa na raisi Praygod, ndani ya dakika moja akafanikiwa kujua ni wapi namba hiyo inapotokea.

“Sehemu ni ile ile kama nilivyo sema”
Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku akiwaonyesha sehemu alama ya simu hiyo inapo onekana.
“Inabidi twende muda huu huu”
Raisi Praygod alishauri, hapakuwa na mtu aliye weza kupinga swala hilo, wakatoka wote huku Sa Yoo akiwa ameibeba laptop. Wakaingia kwenye gari, na Rahab akawa dereva wa safari hiyo.
                                                                                                                    ***
Dokta Ranjiti akakata simu huku mwili mzima ukiwa unamtetemeka, akahisi kitu alicho kisikia labda inaweza kuwa ni ndoto. Adrus akabaki akimtumbuli macho bosi wake huyo asijue ni kitu gani ambacho amezungumza na mtu aliye mpigia simu.
“Bosi”
Adrus aliita, ila dokta Ranjiti hakuzungumza chochote zaidi ya kubaki akimtazama, Adrus aliye jawa na shauku ya kuhitaji kujua ni kitu gani ambacho kimetoka.

“Bosi kuna kitu gani kilicho endelea?”
“Amepokea EDDY”
“Eddy ndio nani?”
Dokta Ranjiti hakujibu kitu chochote zaidi ya kunyanyuka kwenye kiti alicho kalia, akatoka ofisini kwake pasipo kulijibu swali la Adrus, moja kwa moja akaelekea chumbani alipo muacha Phiday, akamkuta akitoka bafuni kuoga.
“Vaa vaaa nguo tunaondoka”
Dokta Ranjiti alizungumza huku jasho likimwagika, mwili mzima. Phidaya akagundua kwamba kuna tatizo ambalo limetokea kwa Ranjiti.

“Tnakwenda wapi?”
“Kwani hapa ni kwako. Vaa tuondoke sasa hivi”
Ikambidi dokta Ranjiti aanze kutafuta nguo za Phidaya alizokuwa amezitupa chini, kipindi akimlazimisha kufanya tendo la ndoa.
“Vaa vaaa…mama”
Ranjiti akaendelea kumsisitiza Phidaya, ambaye akaanza kuvaa huku kichwani mwake akijiuliza ni nini kinacho endelea. Alipo maliza kuvaa nguo zake, dokta Ranjiti akamshika mkono na wote wawili wakatoka kwenye chumba hicho na moja kwa moja dokta Ranjiti akaelekea sehemu kulipo na gari lake.

“Adrus ingia ndani ya gari munisindikize bandarini”
“Sawa mkuu”
Adrus akaingia ndani ya gari, akawasha gari hilo aina ya BMW X5. Wakati wote huo Phidaya, alikaa kimya, ila moyoni mwake akawa anaomba Mungu amsaidie lolote liweze kutokea, ila si kuendelea kukaa mikononi mwa Ranjiti. Wakaondoka eneo la ngome yao kwa mwendo wa kasi hadi walinzi wengine wakabaki wakishangaa.
                                                                                                               ***
Madam Mery baada ya kuamka moja kwa moja akaelekea chumbani kwa Eddy kutazama kama yupo, ila hakumkuta. Hakuwa na wasiwasi wowote zaidi ya kuamua kueleka katika chumba wanapo lala Shamsa na Sa Yo, akaugonga mlango mara tatu, hakusikia kitu chochote, alicho kifanya ni kuusukuma mlango huo na kuukuta upo wazi, akaingia ndani na kumkuta Shamsa akiwa amelala kitandani.

Akamsogelea huku akimuita jina lake, ila Shamsa hakuitika. Akafika kitandani na kuanza kumtingisha, ila Shamsa hakuitika, kitu kilicho anza kumpa wasiwasi madam Mery. Akajaribu kumpima mapigo yake ya moyo na kukuta yakiwa hayafanyi kazi.

“Mungu wangu”
Madam Mery alistuka, kiasi cha kuanza kutokwa na kijasho chembamba usoni mwake.
“SHAMSA, SHAMSA, SHAMSA”
Madam Mery akajaribu kumtingisha tena, ila Shamsa hakujibu chochote, Madam Mery kwa haraka akanyanyuka kitandani hapo, kwa haraka akafungua mlango wa bafuni na kuchungulia kama Sa Yoo atakuwepo, ila hakukuta
mtu.

“Sa Yoo, Sa Yoo”
Madam Mery kwa kuchanganyikiwa, alijikuta akiita huku akimtafuta Sa Yoo hadi ndani ya kabati la kuhifadhia nguo. Hakumkuta mtu, wazo la kuomba msaada katika uongozi wa hoteli hiyo ukamjia kichwani, akataka kukimbia na kutoka nje, ili kwenda kuwaita, ila akahisi kwamba atachelewa zaidi, akaisogelea simu iliyopo mezani na kuminya namba za wahudumu.
“Nahitaji msaada”
Madam Mery alizungumza kwa sauti iliyo jaa wasiwasi mwingi, muhudumu akauliza ni chumba namba, ngapi. Akamtajia namba ya chumba.  Hazikupita dakika tatu wahudumu wawili wa kike walio valia sare zilizo wakaa vizuri mwilini mwao, wakaingia ndani ya chumba hicho.

“Mwanangu hapa anatatizo”
Madam Mery alizungumza huku akiwaonyesha wahudumu hao sehemu alipo Shamsa. Wahudumu hao, wakamsogela Shamsa, wakajaribu kumtingisha, kila mmoja wasiwasi ukamuingia kwani Shamsa hakujibu chochote. Muhudumu mmoja akajaribu kumpima kama ana pumua, ila jibu alilo lipata ni sawa na jibu alilo lipata Madam Mery.

“Piga simu kitengo cha dharura”
Muhudumu huyo alimuambia muhudumu mwenzake, kwa haraka akatoa simu zao maalumu wanazo zitumia wakiwa kazini, akapiga simu kwenye kitengo cha dharura kilichopo hapo hotelini. Muhudumu akaelezea tatizo lililomo ndani ya chumbu hicho.
“Tunakuja”
Sauti nzito ya kiume ilizungumza, na simu ikakatwa.
“Amefanya nini huyu?”

Muhudumu mmoja alimuuliza Madam Mery, ambaye macho yote yalisha anza kutwaliwa na wekundu na machozi kwa mbali yalisha anza kumwagika.
“Mimi sifahamu nimekuja kuwatembela asubuhi, wezake hawapo nay eye nimemkuta hapo kalala, nimemuita ila hakujibu chochote.”
“Mwenzake ameenda wapi?”
Kabla madam Mery hajajibu chochote, mlango ukafunguliwa, wakaingia wanaume watatu huku wote wakiwa wamevalia makoti meupe, mmoja wao akiwa amevalia kipimo cha kupimia mapigo ya moyo shingoni mwake. Kwa haraka haraka Madam Mery akatambu kwamba hao watakuwa ni madaktari.

“Mgonjwa yupo  wapi?”
Dokta aliye valia kipimo hicho alizungumza, muhudumu mmoja akamuonyesha kwa kidole. Pasipo kupoteza muda daktari huyo akaanza kumpima Shamsa kifuani mwake. Madam Mery alipo yatupia macho yake usoni mwa dokta huyo akagundua kwamba kuna tatizo, kwa maana sura ya daktari, ilanza kubadiliika kila alipo jaribu kukihamisha hamisha kipimo chake kifuani mwa Shamsa.
                                                                                                       ***
“Ngoja ngoja mara moja”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakiwa yametoka akiitazama laptop. Alama inayo onyesha simu ya dokta Ranjiti lianza kutembea. Kitu kilicho ashiria kwamba dokta huyo anaondoka katika sehemu alipo kuwepo.
“Kuna nini?”
Rahab aliuliza huku akipunguza mwendo kasi wa gari.
“Anaondoka katika eneo alilo kuwepo”
Sa Yoo aliye kaa siti ya nyuma na Eddy alimuonyesha Eddy kwa kidole.

“Hembu nione”
Rahab alizungumza na kumfanya Sa Yoo kumpa laptop, hiyo. Rahab akasimamisha gari pembani na kuanza kuangalia ramani hiyo. Akashuhudia jinsi alama hiyo inavyo tembea kwa kasi kueleka upande mwingine ambao si ule ambao wanao tokea.
“Honye hembu naomba umpishe Sa Yoo akae hapa mbele”
Raisi Praygod hakubisha, Sa Yoo akapita katikati ya siti baada ya raisi Praygod kushuka, kisha akaka mbele na kuichukua laptop hiyo.
“Naamini unatambua kazi ambayo imekuweka hapa mbele”
“Ndio, twende”

Rahab akawasha gari na kuanza kuondoka kwa mwendo wa kasi kiasi, kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza mwendo kasi wa gari. Sa Yoo kazi yake ikawa ni kumpa maelekezo ya kuweza kukunja katika njia za vichochoro zinavyo onekanana kwenye ramani hiyo ili kuweza kuiwahi gari hiyo.
“Tunaikaribia, ipo kama kilomita moja mbele”
“Usijali”
Kwa muda wote huo, Eddy hakuzungumza kitu cha aina yoyote, akilini mwake akawa anafikiria ni adhabu gani ambayo anaweza kumpatia dokta Ranjiti pale tu atakapo mtia mikononi mwake.

Picha ya jinsi Phidaya akiingiliwa kimwili na dokta Ranjiti ikaanza kumjia kichwani mwake, jambo lililo mfanya hasira yake izidi kumpanda. Raisi Praygod, mara kwa mara akawa anamtazama Eddy kwa jicho la kuiba, akaweza kugundua hasira aliyo kuwa nayo Eddy, kwa maana kwa mara kadhaa, aliweza kuona jinsi kifua chake, kinavyo panda na kushuka kwa kuhema kwa nguvu. Breki za gafla alizo zifunga Rahab, zikamstua Eddy na kumtoa kwenye dibwi la mawazo mabaya aliyo kuwa nayo.

“Fala kweli huyu”
Rahab alizungumza huku akiminya honi, akimpigia dereva wa gari ndogo aliye simama gafla barabarani kwa lengo la kugeuza, pasipo kuonyesha ishara yoyote.
“Pita huko pembeni”
Raisi Praygod alimshauri, Rahab akafanya hivyo, uzuri ni kwamba Rahab, katika swala zima la uendeshaji wa gari yupo makini sana na ni mtaalamu wa kufanya hivyo. Alipo hakikisha gari limekaa sawa barabarani, akaendelea kuongez amwendo kasi wa gari hilo.

TFDA yaunda kikosi kusaka ukweli mchele plastiki Dar

0
0
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeunda kikosi maalum ili kupata ukweli juu ya mchele unaodaiwa kutengenezwa kwa kutumia plastiki baada ya picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa umeanza kutumiwa na baadhi ya mamalishe jijini Dar es Salaaam.

Baada ya picha hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikielezea mchele huo kutumiwa na mamalishe kariakoo jijini Dar es Salaam, baadhi ya wananchi hususan wanaopata huduma ya chakula kwa mama lishe hao, walianza kuingiwa na hofu.

Mkurugenzi Mkuu wa (TFDA), Hiiti Sillo,jana alisema mamlaka imeanza kufuatilia suala hilo na kwamba imeunda timu maalum ili kubaini ukweli wa suala hilo.

Aidha, alisema taarifa za awali walizipata kupitia mtandano wa kijamii na Juni 8, mwaka huu, walitoa taarifa ya ufafanuzi kuwa hapakuwa na mchele wa aina hiyo ingawa wanaendelea kufuatilia.

“Mchele ambao upo na ambao TFDA tunautambua ni wa Basmati ambao huitwa Sunrice. Huu wa kutengenezwa kwa plastiki tunaendelea kufuatilia kama taarifa hizo ni za kweli au la,” alisema.

Alisema timu hiyo imeanza kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kama ni kweli mchele huo uko sokoni. Aliwataka wenye taarifa za ziada kuhusu mchele huo wawapelekee ili kurahisisha uchunguzi.

“Tunaomba wenye taarifa za wapi mchele huu unauzwa, waliotumia watuletee au wapeleke taarifa serikali za mitaa wanakotoka, polisi au kwenye ofisi zozote za serikali ili tuweze kufuatilia jambo hili kwa urahisi,” alisema.
 
Mkurugenzi huyo alikiri kwamba mamlaka yake imepata taarifa juu ya mchele huo ingawa hadi sasa haijadhibitisha kama kweli umeshaingia nchini.

“Tayari nimeshatoa maelekezo kwenye kanda zetu za TFDA zikiwamo Mwanza, Arusha, Mbeya kuanza kufuatilia na ninavyozungumza ni kwamba ukaguzi unaendelea. Kama taarifa hizi ni za kweli tunamwomba huyu aliyetuma ‘clip’ (picha) hii kwenye mitandao ya kijamii ajitokeze ili atusaidie ni wapi alikula mchele huu maana clip inaonyesha mkono tu,” alisema.

Katika ‘clip’ hiyo, kijana huyo anaeleza kuhusu chakula hicho (wali) walioletewa na mama lishe huko Kariakoo huku akifinyanga tonge na kuonyesha tofauti yake na ule wa kawaida.

Sillo alisema taarifa mbaya zinazohusu chakula zinagusa watu na maisha yao kwa ujumla ndiyo maana wanamwomba mtu huyo awape ushirikiano ili wawajue wauzaji na wasambazaji.

“Wito wangu kwa watu wanaponunua kitu chochote wadai risiti hii itasaidia matatizo kama haya yanapojitokeza inakuwa rahisi kumkamata mhusika,” alisema.

Kuibuka kwa taarifa juu ya kuwapo mchele wa plastiki, kumezua taharuki na gumzo kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao asilimia kubwa ndicho chakula chao na wengi hula kwa mama lishe.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Yatoa tahadhari ya kuwepo upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Mwambao wa Pwani Jumapili hii.

0
0
Mamlaka  ya Hali ya Hewa nchini imetoa tahadhari ya kuwepo upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Mwambao wa Pwani Jumapili hii.

TANESCO yakanusha taarifa ya kuuza mitambo ya Kinyerezi

0
0
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),limekanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi iliyosema kuwa vifaa vya mitambo ya Kinyerezi hatarini kwa kuuzwa.

Tanesco imekanusha taarifa hizo, kuwa si za kweli ni upotoshaji kwa umma huku shirika hilo likidai linaendele na ulipaji kodi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 19

Ole Sendeka amtumia salamu za shukrani Edward Lowassa kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za nchi

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Acacia.

Ole Sendeka ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesema kuwa baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amempongeza Rais, hana budi kumshukuru na kumpongeza pia kwa kufanya hivyo, na kuwaomba wabunge wote bila kujali vyama vyao kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi.

“Nanyi wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea rasilimali za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha Watanzania, waweze kupata huduma zao za msingi kupitia madini hayo,” Ole Sendeka anakaririwa na Mwananchi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza jana kwenye mazishi ya mama yake mzazi yaliyofanyika katika kijiji cha Losokonoi wilayani Simanjiro.

 Alimuomba mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya ambaye alihudhuria mazishi hayo, kumfikishia salamu na pongezi hizo kwa Lowassa.

Lowassa alimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake baada ya kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini yanayoshikiliwa na Serikali katika bandari ya Dar es Salaam, yalipokuwa katika mchakato wa kusafirishwa nje ya nchi na kampuni ya Acacia.

Mwigulu Nchemba Awavaa Wanaompinga Rais Magufuli na Kuwatetea Wezi wa Rasilimali za Nchi

0
0
Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha Marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu (makinikia), Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzia serikali iache kufatilia sakata hilo.

“Viongozi wetu hawajawahi kuwa mawakala wa wale wanao tuibia, mawakala tumewabaini ni wale wanao watetea wezi,” alisema Waziri Nchemba.

Waziri Mwigulu aliongeza kwa kusema sifa ambayo inafanya viongozi walioko madarakani wasing’ang’anie madaraka ni viongozi wastaafu kuheshimiwa baada ya muda wa uongozi.

”Kwa imani zetu wote, tuendelee kumuombea Rais wa nchi yetu, Rais wetu mpendwa kwa kazi kubwa anazozifanya ambazo zitasaidi hii mipango mingi tunayopanga kwenye majimbo yetu, matamanio na matarajio yetu mengi tunayokuwa nayo katika majimbo yetu.

“Ukizunguka kote jibu lake linakuja mahitaji ya fedha. Barabara mahitaji ya fedha; elimu bure mahitaji ya fedha, maji mahitaji ya fedha, umeme mahitaji ya fedha, Hospitali huduma bure mahitaji ya fedha. Hicho ndicho kinachomuuma Rais mpaka munaona anachukua hatua ngumu zinazohitaji ujasiri kama anavyofanya.

“Kwa Mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu lazima ataunga mkono juhudi hizo lakini kwa ambaye ana mambo yake ya ubinafsi na ametanguliza ubinafsi anaweza asielewe kazi inayofanywa lakini sisi ambao tunahitaji maji; tunaohitaji barabara, tunaohitaji elimu bure, tunaohitaji Hospitalini dawa ziwepo, tunaohitaji umeme, sote kwa maombi na kwa jitihada na hata kwa kusema tumuunge mkono Rais wetu kwa uzalendo na ujasiri mkubwa aliouonesha.” 

Waziri Mwigulu aliyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa ya Ndago katika mwendelezo wa ziara jimbo kwake Iramba Magharibi kuongea na wananchi kuwaeleza alipofikia kuhusu ahadi ambazo walikubaliana kutekeleza hasa suala la umeme kutokufika katika vijiji vingi akieleza kuwa sababu ni mkandarasi aliyekuwepo mkoa wa Singida aliyetolewa baada ya kushindwa kazi lakini sasa ameambiwa na watu wa wizara ya nishati kuwa wakandarasi wawili wameshapatikana hivyo kuanzia sasa zoezi la kuunganisha umeme vijijini utaendelea kwa kasi hasa wa REA awamu ya Tatu.

Kuhusu ujenzi wa zahanati alisema mpaka sasa zahanati katika vijiji vingi alipopita zimefika hatua nzuri ya kupaua na kuwahidi kuwa pelekea mabati na mbao na mifuko ya saruji 100 ili zahanati hizo zikamilike na kuanza kutoa huduma mapema sana.

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

0
0
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?
 
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
 
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

Whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Waziri Mkuu: Taifa la Watu Waadilifu Huanzia Kwenye Familia....Tujenge Mazoea Ya Kuwahoji Watoto Kuhusu Utajiri wa Ghafla

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wazazi wana jukumu la kulea watoto kwenye misingi ya kumcha Mungu ili Taifa liweze kuwa na watu waadilifu na wachapakazi.

“Taifa la watu waadilifu na wachapakazi huanzia katika ngazi ya familia. Kama kaya zetu haziishi kwa uadilifu, ni vigumu sana kuwa na Taifa lenye wananchi waadilifu. Ni muhimu basi familia zetu zihakikishe kuwa tunakuwa na watoto wenye hofu ya Mungu na wenye kumcha Mungu,” alisema.

Alitoa kauli hiyo Jumamosi, Juni 17, 2017 wakati akizungumza na wageni waliohudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa na nyumba ya Paroko katika Parokia Teule ya Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Harambee hiyo ilitanguliwa na ibada ya misa ya shukrani kwa ajili ya marehemu Mzee Xavery Mizengo Pinda, ambaye ni baba yake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Peter Pinda. Mzee Xavery Pinda alifariki Novemba 27, mwaka jana katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na kuzikwa kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, Katavi.

Waziri Mkuu alisema wazazi wanapaswa kujitathmini juu ya malezi ya watoto wao na kujihoji kama wamepata malezi yanayostahili. 

“Kupitia funzo tulilolipata leo, tujitathmini kuhusu makuzi ya watoto wetu. Je watoto wetu wanapata malezi stahiki? Je tunawalea katika misingi ya kutoa kwa ajili ya Mungu au tunawafundisha wajilimbikizie mali? Je, tunawahoji watoto wetu kuhusu utajiri wanaoupata ghafla? Au tunawapongeza na kufurahia bila kujua wanapata wapi utajiri huo?,” alihoji.

“Nitumie nafasi hii kuwasihi wazazi wote kwamba tujitahidi kuwekeza katika malezi ya watoto wetu. Ili tuwe kioo cha aina ya Taifa tunalotaka kulijenga, hatuna budi kuwalea watoto wetu katika misingi ya imani, uadilifu na uzalendo mkubwa kwa nchi yetu,” alisisitiza.

Katika harambee hiyo, Waziri Mkuu na mke wake walichangia sh. milioni 10 ambapo jumla ya sh. milioni 160 zilikusanywa. Kati ya hizo, sh. 111,150,000 zilikuwa ni ahadi, sh. 38,447,000 zilikuwa ni fedha taslimu na sh. 10,403,000 zilikuwa ni vifaa vya ujenzi.

Mapema, akiongoza ibada ya shukrani, Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Padre Chesco Msaga alisema kila mtu anapaswa kumshukuru Mungu kwani hakuna mwanadamu anayeweza kudai kuwa yuko jinsi alivyo kwa sababu ya akili zake. 

“Hata sisi tunasahau kumshukuru Mungu hasa pale mambo yetu yanapotunyookea. Tunadhani ni kwa akili zetu ndiyo mambo yetu yananyooka. Tunapaswa tukumbuke kuwa maishayetu yapo mikononi mwa Mungu, na yeye ndiye anajua njia zetu,” alisema akirejea mfano wa wakoma 10 walioponywa na Bwana Yesu na mmoja tu ndiye alirudi kushukuru.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda alisema harambee hiyo inafuatia uamuzi wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya wa kuiteua Zuzu iwe parokia.

“Sasa hivi tulikuwa na kigango. Kuteuliwa kuwa parokia maana yake tutakuwa na padre anakaa hapa Zuzu saa 24 na tutakuwa na ibada kila Jumapili, na katikati ya wiki kadri ratiba zitakavyoruhusu.

“Kikubwa tunachopaswa kufanya kufuatia uamuzi huo, ni kuhakikisha kuwa mapadre wana nyumba ya kuishi. Sasa hivi, wa kwetu anakaa Dodoma mjini. Kwa hiyo tuna kazi ya kukarabati kanisa, lakini kwanza tukamilishe ujenzi wa nyumba ya mapadri,” alisema wakati akielezea madhumuni ya harambee hiyo.

Jaji Warioba: Tumsaidie Rais Magufuli Kushinda Vita Hii ya Rasilimali za nchi ......Suala la Makinikia sio la Chama wala Siasa ni la Watanzania wote

0
0
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya kwanza na ya pili ya uchunguzi wa makontena 277 ya mchanga wa madini (makinikia) yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi na uchunguzi ulifanyika na kulibaini ndani ya mchanga huo kuna dhahabu na madini mengine kwa asilimia kubwa.


Aidha, Mhe Rais amechukua hatua mbalimbali kulingana na ushauri wa kamati husika, pamoja na maamuzi yake kama Rais. 

Kutokana na sakata la hilo, Idara ya Habari-MAELEZO imepata fursa ya kufanya mahojiano na  Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Mheshimiwa, Jaji Joseph Sinde Warioba katika ofisi zake zilizopo Osterbay Jijini Dar-es-salaam.

SWALI: Ninanukuu maneno ya Baba wa Tafa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kuhusu raslimali za nchi na hususan madini alisema: “Madini yetu tuliyonayo ni vema kuyaacha mpaka Watanzania watakapokuwa na ufahamu wa kutosha wataamua kuyachimba” mwisho wa kunukuu nini maana yake?

JIBU: Mara baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokea nchi kama Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru akiwa hana wataalamu zaidi ya madaktari 2 na yeye mwenyewe ambaye alikuwa msomi kutoka chuo Kikuu cha Edinburg Uingereza. Kwa hali hiyo, Mwalimu alikuwa sahihi usingeweza kuruhusu rasilimali za nchi mfano madini kuchibwa na wageni kutoka nje maana yake Watanganyika wangekuwa watazamaji tu bila kufaidika na lolote.

Mwalimu alihakikisha anawekeza katika elimu ambayo ilikuwa bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu elimu ndio msingi wa kuondoa Ujinga Umasikini na Maradhi. Alitambua Watanganyika wakielimika na kupata utaalamu wa madini ikiwani pamoja na uchimbaji watakuja kuyachimba na kufaidika.

SWALI:Tanzania ni kati ya nchi zilizobarikiwa kuwa na raslimali nyingi za kila aina kuanzia madini, gesi, wanyamapori na hifadhi, misitu, milima, maporomoko ya maji, mabonde maziwa makubwa kwa madogo, bahari ya hindi na raslimali za mazao ya uvuvi,  nchi yenye ardhi ya kutosha watanzania wenye uwezo wa kufanyakazi kwa ufanisi . Unadhani nini tatizo letu, nini cha kufanya?

JIBU: Sioni kama kuna tatizo la msingi lakini, ni suala la uelewa mara nyingi kuna watu ambao huamini viongozi wao kwa kila kitu wanachosema. Lazima wananchi wawe makini kwa sababu tatizo la watanzania ni maendeleo kila mwananchi ana kiu ya kutaka tufikie mahala pazuri kama Taifa na mimi nakubaliana nao kabisa.

Tuna rasilimali nyingi, ambazo kimsingi tukiweza kuzishughulikia kwa makini kama lilivyoshughulikiwa suala la mchanga wa madini tutakuwa mbali sana kiuchumi.

Mosi, tuangalie rasilimali ya madini kwa mapana yake na kushughulikia wawekezaji wa ndani na wale wa nje, Barick na Acaccia ni sehemu ndogo sana ya madini, tuangalie wachimaji wa ndani mfano Tanzanite ni aibu madini yanachimbwa Manyara biashara hii inatokaje Mererani na kufanyika Nairobi na New Delhi tujiulize kwa nini sio Arusha na Dar-Es-Salam.

Pili, upande wa rasilimali za maziwa makubwa tuliyonayo Victoria, Tanganyika na Nyasa, Bahari ya Hindi kuanzia Moa mpaka Tanga kwa kiasi gani tumeweza kutumia rasilimali za bahari maharamia wanakuja na meli zao wanavuna tu na kuwatajirisha watu wengine. Mfano ziwa Victoria linategemewa na wananchi wengi na sasa samaki hamna wamekwisha kwa sababu hatusimamii rasilimali zetu ipasavyo. Maana suala sio kuvuna tu tunalindaje hizi rasilimali zetu ili ziwepo leo kesho na vizazi vijavyo.

Tatu, Maliasili zetu za wanayamapori, mbuga za wanyama, vitalu vya utalii unampaje mfanyabiashara kibali cha kuwinda miaka 99 yaani atumie yeye, wanawe na wajukuu zake, watanzania watatumia lini, haya ni masuala ya msingi kabisa ya kuangalia upya.

Nne, Ardhi Mwalimu alisema ili tuendelee tunahitaji vitu vine Watu, Ardhi Siasa Safi na Uongozi Bora. Mwalimu Nyerere aliona ardhi ndio kilakitu hivyo vyote tulivyovitaja vipo ardhini pamoja na sisi wanadamu tunaitegemea kwa kila kitu. Maeneo mengi yaliyotumiwa na watu kwa shughuli za ufugaji aidha , yana matumizi mengine kama nyumba, kilimo cha mashamba makubwa, na idadi ya watu inaongezeka ardhi ni ileile hii imesababisha migogoro ya watumiaji wa asili wa maeneo hayo na wenye matumizi mengine tunatatuaje changamoto hii.

SWALI: Kwa kuwa umebobea katika masuala ya mikataba na sheria, ushauri gani unautoa katika masuala yote ya raslimali za Tanzania? Nani anatakiwa kusimamia raslimali hizi kwa ufanisi?

JIBU: Hii sio suala la mjua sheria au asiyejua, Mwanasheria lazima anazijua sheria ndio maana amepewa dhamana. Linalojitokeza ni ukosefu wa maadili ya uongozi, imani, utiii, uwazi na kutopenda nchi yako na Watanzania ambao wamekupa dhamana ya kusimamia jambo.

Ndio maana Mwalimu Nyerere aliweka miiko ya uongozi, maadili ya uongozi kwenye Azimio la Arusha. Kila mwananchi alikuwa anaweza kujua kiongozi huyu muadilifu au sio muadilifu na anachukuliwa hatua kabla mambo hayajaharibika.

Lakini sio vema kumhukumu mtu kwa jambo lolote lile, ni vema busara itumike kujua kilichotokea mfano hili suala la mchanga wa madini ya makinikia. 

Jambo la msingi ni kutafuta suluhu itakayotupeleka mbele, tuone sera zetu zikoje na zinatusaidiaje kulinda rasilimali za Taifa, tunarekebisha vipi kuondoa tatizo, sheria na utendaji kwa ujumla. Naomba watanzania tutoe maoni na mawazo yatakayoboresha sera, sheria na utendaji au usimamizi wa rasilimali husika. Tunaweza kurudisha miiko na maadili ya uongozi katika kusimamia rasilimali za nchi, kila Mtanzania ajue sio mali yake ni ya Watanzania wote lazima aitunze vinginevyo atahukumiwa kwa hilo.

SWALI: Ni ukweli usiopingika kuwa kosa limeshafanyika kwa hili tuliloliona la mchanga wenye madini ya dhahabu, ambapo mhusika ambaye ni mmiliki wa Kampuni inayobeba mchanga huo tangu 1998 hadi 2017 amewasili nchini kuonana na viongozi wakuu wa serikali, nini maoni yako kuhusu hili?

JIBU Sisi hatukushughulika na uchimbaji wa madini, lakini utafiti tulifanya na kujua madini yapo na kuna maeneo mengi ambayo tumeweza kufanya vizuri tunapata mapato, lakini hatukupata mapato yote.

Lakini hili la mchanga sitaki kulizungumzia sana nadhani watu wanalichukulia kwa mihemko sioni faida kuzungumzia matukio badala ya kuona tafsiri nzima nini cha kufanya.

Ninachokiona na cha muhimu sana, Watanzania wamepata faida kwa mara ya kwanza tumeweza kujua mikataba ya madini ikipitiwa na Kamati zote mbili zimetueleza maeneo yote ya mikataba waliyopitia na kuja na mapendekezo. Tumetambua serikali ilikuwa na hisa au la mrahaba asilimia ngapi, kodi kiasi gani, na mambo kama hayo.

Naomba jambo hili lisibague, tunasema hatupati mapato ya kutosha ni lazima tujue kwa wachimbaji wa nje na wa ndani mfano nani anajua wachimbaji wadogo wadogo wamechimba madini kiasi gani tangu 1998 hadi 2017 na kodi kiasi gani imeimngia. Tumepata nafasi sasa ya kuangalia sera za kulinda rasilimali ya madini na nyingine zote katika nchi, kama maliasili ya bahari tunaitumiaje, gesi, makaa ya mawe, chuma, wanyama pori na mambo kama hayo.

Hii imetufungua macho sera ya aina gani sheria za aina gani, jinsi gani ya kutunza na kutumia rasilimali hizi tulizopewa na mungu.

SWALI: Kwa kuwa wananchi tulio wengi tunaenda kwa mihemko bila kupambanua hoja husika na kutoa mapendekezo au maoni yatakayo isaidia serikali kuboresha sera sheria na utendaji wa rasilimali zetu unadhani tatizo ni nini?

JIBU: Hatujaona uongozi wa Kitaifa katika hili suala la mchanga wa makinikia ninachokiona mimi ni uongozi wa chama na siasa nyingi, sio sahihi kabisa wanafanya makosa hili ni suala la rasilimali za nchi ni la kila Mtanzania.

Viongozi hawawatendei haki wananchi wanaowakilisha, wanakuwa na mihemko wanasema kamata, shitaki, wafunge. masuala ya kitaifa hayaendi hivyo sisi sio Polisi wala Mahakama waachieni wenye kazi yao.

Uongozi wa kulalamika hautusaidii, wananchi wanataka kuona rasilimali zetu zinanufaisha na kuboresha huduma za jamii ambazo wanalalamika kila leo hakuna dawa, elimu isiyowajenga vijana na mambo kama hayo.

SWALI: Mhe. Kutokana na sakata la mchanga wa dhahabu uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi na matokeo yake watanzania tunajifunza nini kwa maoni yako?

JIBU: Kabla ya tuona funzo tulilopata nadhani ni vema nikazungumzia jambo hili, nimeona mjadala katika mitandao ya kijamii ambayo inafanywa kwa mihemko. Ukiangalia vyombo vya habari au viongozi tumejikita katika majina ya watu, nilikuwa nnaangalia Bunge wote wanakwenda kwa wale waliotajwa unakuta kuna wanaochangia na wanaolaumu ama unsahangilia au unalalamika kuhusu watu.

Kubwa ni utaratibu tulionao haitasaidia kulalamika juu ya watu waliofanya kazi huko nyuma, tunaweza kuwauliza wahusika nini kilitokea mpaka kufanya hivyo, lakini hilo sio kubwa, muhimu ni kutafuta ufumbuzi.

Mjadala huu umenikumbusha Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere viongozi wote na wananchi walikuwa wanalalamika kila kitu wanachokikosa ni kwa sababu ya wakoloni. Mwalimu akasema namnukuu: “Ni kweli wakoloni wametuleta matatizo mengi sana lakini haitoshi kulaumu wakoloni bila kuondoa mateso ya wananchi”. Mwalimu akaja na Waraka ambao ulikuwa unaitwa “Act dont Argue” nadhani bado upo.

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi nanukuu amesema. “Napenda kupata maoni tufanye nini kuhusu suala hili la mchanga wa dhahabu (makinikia).”  Namuunga mkono, sasa tumepata nafasi ya kutoa maoni, mawazo ambayo ni muhimu sana maoni ya wadau katika uundaji wa sera na sheria

Sasa hivi siamini kama hatuna utaalamu, nina hakika tunao wa kutosha  tatizo ni maadili na hilo lazima kutafuta ufumbuzi wake, pia tuunge mkono serikali inachofanya kupambana na rushwa na ufisadi.

“Lakini tusijidanganye bishara ya madini, mafuta ina changamoto kubwa sana duniani hususan Afrika, maana unapambana na watu wenye fedha biashara hii popote utakapo kwenda, ambapo uchumi unategemea mafuta na madini utaona jinsi wakubwa wanavyooneemeka na rasilimali hizo na kuwaaacha wananchi wakiwa masikini mfano mzuri Nigeria”.

Pamoja na kuangalia maadili na nidhamu lazima kuwe na uwazi   katika mikataba ni muhimu sana.

SWALI: Una maoni na mapendekezo yako kwa viongozi wote na Mhe Rais katika kumuunga mkono?

JIBU: Kwanza naliona hili la malumbano yatatugawa, waache tofauti zao hii lawama ya madini ingekuwa ni mwanzo kwa kuleta mawazo na maoni ya kutengeneza nchi yetu katika kulinda na kuzitumia rasilimali zote kwa maendeleo ya taifa letu.

Viongozi msaidieni Rais kulishughulikia kwa pamoja hili si jambo la chama wala Taasisi. Hakuna haja ya kupeana lawama ukishasema tumekosea unatakiwa ueleze tufanye nini, sio kusema serikali ichukue hatua kwani serikali ni nani si mimi na wewe sasa kwa nini hutaki wewe kulitolea maoni?

Tujiamini nimeona katika malumbano hayo, wengine wanaonekana kama hatujiami kama tukifanya hivi tunaweza kushitakiwa, mabadiliko yoyote yana machungu yake. Tusije tukapoteza imani tuliyonayo maana tunaweza tukapoteza mapato yetu lakini ni lazima tufanye kwa kujenga afya ya rasilimali zetu.

Rais amekutana na mmiliki wa Barick na kila upande una msimamo wake, tuiachie serikali na nina imani kabisa serikali itafanikiwa. Kinachonishangaza ni mazungumzo ya baadhi ya viongozi kuwa serikali ihakikishe tunapata hizo fedha walizo taja kwenye taarifa.

 Nadhani hii sio sahihi, tuna imani na Viongozi wet wakuu haswa Rais, lolote litakaloafikiwa tulipokee na kulikubali tusije kuanza kulumbana ripoti imesema trilioni 108 ziko wapi?  Pia nilisemee hili la dalili za kupoteza imani, eti tukifanya hivyo tutashitakiwa,  sababu ya mikataba na wawekezaji hawatakuja mimi naamini watakuja tu rasilimali zipo kwetu hawana jinsi.

SWALI: Msaada wako binafsi kwa Rais au maoni yako kwa Rais

JIBU: Sisi tupo, Uongozi ni suala la kupeana vijiti mimi natoka Mara nimepitia utamaduni wa kabila langu kwa utamaduni wetu unafika mahali unangatuka watu wanadhani kungatuka ni kustaafu hapana sio sahihi. Ukitoka jandoni mzee wako lazima angatuke maana umekuwa sehemu ya jeshi la kabila na yeyote ambaye kijana wake yuko kwenye jeshi yeye anatoka.

Wazee hawaingii katika mambo ya vijana na sisi tupo lakini hatutaki kuingilia utendaji wao kama sisi tulivyoachiwa kuendesha nchi, ila Rais akituhitaji tupo tayari kwa ajili ya ushauri anaweza kuukubali au kuukataa. Nataka nimhakikishie kwa hili tupo pamoja na tutatoa maoni ya kurutubisha Sera, Sheria na Utendaji katika rasilimali za nchi hii.

Jinsi Kitambi Kinavyopatikana na Jinsi Kinavyoondolewa na Dawa ya Mkataa Kitambi

0
0

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.

 Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i.Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii.Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika  mwili  wa  mwanadamu, hali  inayo  sababishwa  na  mtu  kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA  VINAVYO  CHANGIA KULETA  KITAMBI

Vyakula vinavyochangia  kuleta  kitambi ni  pamoja  na :
i.Vyakula  vyenye  mafuta  mengi  kama  vile  nyama nyekundu  (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama  ya  kuku  wa  kizungu  ( iwe  ya  kuchemsha, kukaanga  ama  kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa  mafuta  (chips) pamoja  na  pizza.

ii.Vyakula vyenye wanga mwingi kama  vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate  mweupe.

iii. Vyakula  na  vinywaji  vyenye  sukari  nyingi  iliyo  ongezwa( added  sugar ), kama  vile  soda  na  keki.

iv. Vyakula  vilivyo  tengenezwa  kwa  ngano  na  sukari kama  vile  keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate  mweupe  nakadhalika

v. Pamoja  na  vinywaji  vilivyo  tengenezwa  kwa  kutumia  ngano  kama  vile  bia  za  aina  mbalimbali  na  kadhalika.

Vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu, vikitumiwa  bila  kuzingatia  kanuni  za  mlo  kamili, huchangia  kuleta  tatizo  la  kitambi.

vi. Sababu nyingine ni  kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo(  physical  exercises  )  kwa  muda  mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40  kwa wanaume na >88 cm au 35  kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO  YANAYO  MUWEKA  MTU  KATIKA  HATARI  YA  KUPATWA  NA  KITAMBI
Tumekwisha  ona  hapo  juu jinsi  kitambi  kinavyo  patikana  na  vyakula  pamoja  na  sababu  nyinginezo  zinazo  sababisha  kutokea  kwa  kitambi, sasa  tutazame  mambo  yatakayo  kufanya  uwe  katika  hatari  ya  kupatwa  na  kitambi.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za kitaalamu, mambo  yafuatayo  huwaweka  watu  katika  hatari  kubwa   ya  kupatwa  na  kitambi :

1. Ulaji  mbovu  wa  chakula; Ulaji  mbovu  wa  chakula  ni  ulaji  usio  zingatia  kanuni  za  mlo  kamili. Hapa  mtu  hufululiza  kutumia  chakula  cha  aina  fulani  pekee  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo  za  chakula.  Mfano; mtu  anaweza  kuwa  anakula  mlo  ufuatao :

Asubuhi :  Mchemsho  ama    supu  ya  ng’ombe , chapatti  tatu  na  soda  moja.  Mchana :   Ugali  nyama  choma anashushia  kwa  maji  na  soda.

Jioni :  Mchemsho  wa  kuku  na  bia  mbili  nakuendelea.

Usiku  :  Chips  mayai  au  chips  kuku  au  chips  mishikaki  na  bia.

Mtu  huyu  akiendelea  na  utaratibu  huu  kwa  muda  mrefu, ni  lazima  atapatwa  na  kitambi.

2. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  mafuta  mengi

3. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye wanga  mwingi  

4.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  sukari  iliyo  ongezwa ( added  sugar  ).

5.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vya  ngano.

6.Ulaji  mfululizo  wa   vinywaji  vyenye ngano  na  sukari.

7.Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na viungo  ( physical  exercises  ).

Mhusika  anapokuwa  katika  makundi  yote  yali yotajwa  hapo  juu, hali  huwa  mbaya  zaidi. 

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini, mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitaji.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasihotika  yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

NJIA  ZA  KUONDOA  KITAMBI.
Unaweza  kuondokana  na  kitambi  kwa  kufanya  diet  pamoja  na  mazoezi ya  mwili  na  viungo.

Vilevile  unaweza  kuondoa  kitambi  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  kuondoa  kitambi  na  kuondoa  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

DAWA   ASILIA  YA  KUONDOA  KIAMBI  NA  MAFUTA  MWILINI.
Hii  ni  njia  ya  uhakika  kabisa  ya  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

 Unaweza  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  DAWA  ASILIA   IITWAYO YA  MKATAA  KITAMBI.

 Dawa   hii  ni  ya asili  kabisa
“  Pure  Herbal “, ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote, haina  side  effect kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kabisa  tatizo  la  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

JINSI  DAWA  YA  MKATAA  KITAMBI  INAVYO  FANYA  KAZI.
1.Huyeyusha  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

2.Husaidia  kupunguza  hamu  ya  chakula.

3.Inazuia  kutengenezwa  kwa  seli  za  mafuta  ( fat cells  ) katika  mwili  wa  mwanadamu. Unapokula  chakula  chenye  mafuta  mengi, dawa  hii asilia  hupambana  kuyafanya  mafuta  hayo  yasitengeneze  seli  za  mafuta  mwilini  mwako. Hali  hii  huuepusha  mwili  wako  kuhifadhi  mafuta   yasiyo  hitajika  mwilini.

4. Husaidia  kupunguza  uzito wa mwili  kwa  haraka  sana  endapo  itatumika  pamoja  na  diet  ya  kabechi.

UFANISI  WA  DAWA.
Ufanisi  wa  dawa  hii  ni  wa  asilimia  mia  moja. Dozi  ya  dawa  hii  hutumika  kwa  muda  wa  siki  ishirini  na  moja.

MATOKEO  YA  DAWA:
Dawa  hii  huondoa  kabisa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

BEI  YA  DAWA :
Dawa  hii  inaoatikana  kwa  kiasi  cha  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU  (Tshs. 50,000/=)

MAHALI  TUNAPO  PATIKANA.
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  karibu  na  SHULE  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

KWA  WATEJA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  Tabata, tunao  utaratibu  wa  kuwafikishia  dawa  mahali  popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  MABASI.

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  tunawatumia  dawa  kwa njia  ya  boti.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  NCHI:
Kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA : 0766  53 83 84

TUTEMBELEE:

Chama cha ACT- Wazalendo chalaan Kitendo cha Polisi Kuwapiga Walemavu Dar

0
0
Chama cha ACT Wazalendo kimelaani vikali hatua za jeshi la polisi nchini kutumia nguvu kuwatawanya watu wenye ulemavu ambao walikuwa wameandamana Ijumaa katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Walemavu hao walikuwa wamefanya maamuzi hayo ili kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kwa lengo la kuwasilisha malalamiko yao kutokana na watu hao kukamatwa na kuzuiliwa kuingia mjini.

"Chama cha ACT Wazalendo kinalaani vikali na kwa nguvu zote kitendo cha jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi na virungu dhidi ya watu wenye ulemavu wasio na silaha yoyote. Katika tukio husika lililotokea Juni 16, 2017 jijini Dar es salaam, askari wa jeshi la polisi waliwavamia, kuwapiga, kuwaswaga na kuwaburuza watu wenye ulemavu kwa kisingizio kuwa hiyo ilikuwa njia ya kurahisisha kukamatwa na kutawanywa kwao" Alisema Ado Shaibu

Chama Cha ACT kinasema kuwa wao wanaamini kuwa jeshi la polisi lingeweza kuwakamata au kuwatawanya walemavu pasipo kutumia nguvu yoyote zile kwa kuwa watu hao hawakuwa na silaha zozote zile, ACT wanasema kitendo hiki cha polisi hakivumiliki hata kidogo.

"ACT Wazalendo tunaamini kwa dhati kabisa kuwa jeshi la polisi lingeweza kuwakamata na kuwazuia watu hao wenye ulemavu, ambao hawakuwa na silaha yoyote, bila kutumia nguvu kubwa kama walivyofanya. Pia, badala ya kuwatawanya na kuwakamata, jeshi la polisi lingeweza kuwaongoza walemavu hao hadi Manispaa ya Ilala walikotaka kwenda kuwasilisha kilio chao. Vitendo hivi vya polisi kutumia mabavu na nguvu kubwa hata kwenye mazingira ambayo njia nyingine zingeweza kutumika havivumiliki hata kidogo" alisisitiza Ado Shaibu

Mbali na hilo ACT Wazalendo wamemtaka Waziri mwenye dhamana ya jeshi la polisi kuomba radhi kwa Jumuiya ya watu wenye ulemavu huku Waziri mwenye dhamana ya watu wenye ulemavu wakimtaka kuhakikisha kuwa madai ya walemavu yanafanyiwa kazi.

"ACT Wazalendo tunamtaka Waziri mwenye dhamana ya jeshi la polisi, Waziri wa Mambo ya Ndani, ndugu Mwigulu Nchemba kuiomba radhi jumuiya ya watu wenye ulemavu hapa nchini kwa kitendo cha jeshi la polisi na kuhakikisha vitendo kama hivi havirudiwi tena. Pia tunamtaka Waziri mwenye dhamana ya watu wenye ulemavu, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ndugu Jenister Mhagama kuhakikisha madai ya watu hawa wenye ulemavu yanasikilizwa na kutolewa majawabu" alisisitiza Ado Shaibu

Kwa kumalizia Ado Shaibu ambaye ni Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa aliitaka jamii kiujumla kuzingatia misingi yetu ya Utu, Upendo na Udugu, kusimama pamoja na watu wenye ulemavu kukipinga kitendo hiki cha kuwavunjia utu wao.

Zitto Kabwe: Sitagombea Urais TFF

0
0
Ijumaa ya Aprili 21, mwaka huu, gazeti la michezo na burudani nchini, Mwanaspoti, liliandika habari kwenye ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa: "Zitto ajitosa Urais TFF, Rage amkubali."

Upande wangu, licha ya kwamba habari hiyo ilichapishwa bila kupata maoni yangu, lakini haikuwa ngeni. Hii ni kwa sababu kabla ya habari hiyo nilikuwa nimeshapokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wakubwa wakinitaka nigombee Urais TFF.

Baada ya habari hiyo kuchapishwa na kupata umaarufu mkubwa, nilipokea maombi mengi zaidi pamoja na shinikizo lenye kunitaka muda ukifika wa uchukuaji fomu, nijitokeze nichukue fomu ya kuwania Urais TFF.

Msukumo ni mkubwa na maswali ni mengi kipindi hiki ambacho dirisha la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi TFF limefunguliwa.

Kila ombi na shinikizo ambalo nimepokea, nimelibeba kwa unyenyekevu mkubwa. Bila shaka wanaoniomba na kunishinikiza wanavutwa na mambo mawili; mosi, soka letu kutoleta nuru kwa Watanzania. Pili, imani kubwa kwamba kupitia uongozi wangu nuru ya soka letu itadhihirika.

Hata hivyo, yapo mambo mawili nimeyatafakari; Mosi, mahitaji ya soka letu na nguvu ya maarifa inayohitajika kulikwamua. Pili, nafasi yangu kama mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Kuhakikisha kazi ya kulikwamua soka letu inafanikiwa na nuru inadhihirika kwa wapenda soka wote nchini, inahitaji uwekezaji mkubwa wa muda, vilevile uwekezaji mkubwa wa maarifa ya kiuongozi.

Soka la Tanzania lipo hapa kwa sababu ya uwekezaji usioridhisha wa maarifa ya uongozi, hiyo inatokana pia na viongozi wanaopata nafasi ya kulitumikia shirikisho letu la mpira wa miguu nchini, kutowekeza muda wao barabara kwenye soka.

Nikiwa Kiongozi wa ACT-Wazalendo, ninadaiwa mambo mawili, uwekezaji wa muda na uwekezaji wa maarifa ya kiuongozi ili kukiandaa vema chama chetu kushiriki uchaguzi kati ya miezi 28 mpaka 40 inayokuja.

Mwaka 2019, Chama kitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mwaka 2020, Chama chetu kitashiriki Uchaguzi Mkuu.

Hivyo basi, kwa kuongezea na uwakilishi wangu wa Jimbo la Kigoma Mjini ambako Chama chetu kinaongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, naona kuwa lipo eneo ambalo nitashindwa kulitimizia wajibu wake nikivaa kofia ya tatu ya Urais wa TFF.

Nimetafakari na kuchukua uamuzi kwamba Uongozi wa ACT-Wazalendo na Ubunge ni nafasi ambazo ninazo tayari, wakati Urais TFF ni nafasi mpya.

Kwa hali hiyo na kwa mapenzi makubwa ya soka la Tanzania, nimeamua nisichukue fomu ya kugombea Urais wa TFF, kwani naweza kuomba kazi ambayo nitashindwa kuitumikia kwa muda wa kutosha kutokana na majukumu yangu kwenye Chama na ubunge.

Uamuzi huu umezingatia mapenzi makubwa kwa soka letu. Nikijitokeza kuwania Urais wa TFF leo halafu nikakosa muda mzuri wa kutimiza matarajio ya wapenda soka nchini, utakuwa usaliti mkubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania.

Nawashukuru wote walioniomba na kunishinikiza nichukue fomu. Nawaambia kuwa kwa sasa tujielekeze kupata viongozi bora miongoni mwa watakaojitokeza. Wakati mwingine mazingira yakiruhusu, nitaweza kutii maombi hayo.

Asante sana.

Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa

Kijana Ajinyonga Juu Ya Mti Kwa Ugumu Wa Maisha

0
0
Matukio ya watu kuchukua maamuzi ya kujiua katika manispaa ya Shinyanga yanazidi kushika kasi ambapo  jana  Jumapili June 18,2017 majira ya saa 10 alfajiri kijana aitwaye Paulo Ezekiel (17) mkazi wa mtaa wa Mazinge kata ya Ndembezi alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba juu ya mti jirani na nyumba yao.

Inaelezwa kuwa huenda ni ugumu wa maisha ndiyo umechangia kifo cha kijana huyo kwani enzi za uhai wake alikuwa analalamika kuwa maisha ni magumu.

Baba mzazi wa marehemu Ezekiel Paulo anasema majira ya saa 10 alisikia mlango wa chumba cha kijana wake ukifunguliwa akadhani pengine ametoka kwenda kujisaidia lakini hakurudi tena ndipo alipoingiwa na wasiwasi na kuanza kumsaka.

“Tuliamshana tukaanza kumsaka kila mahali baadaye tukamuona akiwa juu ya mti jirani na nyumba yetu tayari amefariki dunia”, ameeleza Paulo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa tukio.

Matukio ya watu kuchukua uamuzi wa kujiua yameanza kukithiri katika manispaa ya Shinyanga ambapo ndani ya mwezi mmoja huu wa Juni hili ni tukio la nne.

Tukio la kwanza ni la Luhende Lusangija (34) mkazi wa kata ya Ngokolo aliyejiua kwa kamba,la pili ni la Mwenyekiti wa waendesha bodaboda katika manispaa ya Shinyanga Jacob Paul mkazi wa kata ya Ngokolo aliyejiua kwa waya wa simu la tatu ni la Saada Elias mkazi wa kata ya Ndembezi aliyekatisha maisha yake kwa kujichinja kwa kisu na chupa ya soda.

Umoja Wa Vilabu Vya Waandishi Wa Habari Tanzania ( MCT, UTPC na THRDC) Walaani Vikali Serikali Kulifungia Gazeti La Mawio

0
0
TAMKO LA PAMOJA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO NA HALI YA UHURU WA HABARI NCHINI


UTANGULIZI
Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Umoja wa Vilabu vya Habari Tanzania (UTPC) kwa pamoja tunalaani vikali kufungiwa kwa Gazeti la Mawio na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe Juni 15,  2017. Gazeti limepigwa marufuku kuchapishwa na kuwekwa katika mzunguko kwa miaka miwili.

MAKOSA WANAYOTUHUMIWA KUFANYA
Gazeti la Mawio limefungiwa siku ya tarehe 15 Juni 2017, baada ya kutoa toleo lake lenye namba 196 la tarehe 15-21Juni, 2017.Waziri ametumia sheria mpya ya Huduma ya Vyombo vya Habari, 2016 kulifungia gazeti la Mawio kwa madai ya kukiukwa vifungu vya sheria hiyo na “Agizo la Mhe Rais” kuhusu kutowahusisha Marais wastaafu na sakata la uporaji wa rasilimali madini nchini. Gazeti hili limeshutumiwa kutenda makosa mawili; kosa la kwanza chini ya kifungu cha 50 na 59  cha Sheria ya Huduma za Habari Namba 2 ya 2016 na kosa la pili kukiuka  “ Agizo la Rais laTarehe 14/6/2017.. “ kama ifuatavyo;

(ii) Kuchapisha Picha za Marais Wastaafu
Waziri alidai kuwa, gazeti hilo limechapisha picha na majina ya marais waliopita kwa kuwahusisha na kashfa ya rushwa katika mikataba ya madini kati ya Serikali na wawekezaji.
Waziri anasema kuwa hawakufurahishwa na picha za marais wastaafu ambazo ziliwekwa kwenye ukurasa wa mbele.
(i) Kuchapisha Makala Kuhusu Uporaji wa Madini kinyume na Agizo la Rais
Kosa la pili ni kuchapisha makala ambayo ilichapishwa katika ukurasa wa 12 wa gazeti hilo kinyume na “Agizo la Rais la tarehe 14/6/2017.  Linalowataka watanzania kuacha kuwataja au kuwahusisha marais wastaafu na sakata la upoteaji wa rasilimali madini”.

Makala hiyo ni andiko lililosheheni historia ya jinsi viongozi mbalimbali walivyoshiriki katika usimamizi wa uwekezaji katika sekta ya raslimali madini.

UCHAMBUZI KUHUSU TUHUMA HIZI NA HATUA YA KULIFUNGIA GAZETI
Itambulike kuwa hii si mara ya kwanza kwa magazeti na vyombo vya habari kufungiwa na Waziri  katika nchi yetu kwa kutumia  sheria mbalimbali kandamizi hasa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 iliyofutwa mwaka 2016 na kuridhiwa na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya 2016. Magazeti kadhaa yalifungiwa katika siku za nyuma ikiwemo Mwananchi, Mawio, Mwanahalisi na Mtanzania.
Kwa upande wa Gazeti la Mawio hii ni mara ya pili kusimamishwa. Januari 15, 2016 gazeti hili lilipigwa marufuku kabisa kupitia Tangazo la Serikali (GN) Namba 55 la 2016. Hata hivyo gazeti hilo liliishtaki Serikali kwa mafanikio katika kesi namba. 15 ya 2016 na hatimaye likaweza kuendelea na machapisho yake.

 Itambulike  kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukipinga utaratibu wa kisheria wa kumpa Waziri mamlaka makubwa katika sekta ya habari.

Sheria iliyopita na ya sasa havina tofauti yoyote hasa katika mamlaka ya Waziri kulifungia gazeti pekee na kwa makosa atakayoyaona yeye ni kinyume na maslahi ya umma.  Sheria hii mpya imeendelea kumfanya Waziri awe Mhariri Mkuu, Mlalamikaji, Mpelelezi, Mwendesha Mashtaka na Hakimu kwa wakati mmoja. 

Kifungu cha 59 cha sheria ya huduma za habari imetumika kulifungia Mawio kwa madai kuwa kuchapisha picha za viongozi wastaafu ni kinyume na maslahi ya umma.

 Kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania Watanzania wana uhuru wa kutoa maoni na kupashana habari kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao.

Kitendo cha kuzuia watanzania au vyombo vya habari visichapishe picha za viongozi wastaafu hasa katika mijadala ya kitaifa ambayo inahusu mambo yaliyotekea wakiwa madarakani ni kuwaziba watanzania midomo katika sakata la vita dhidi ya wizi wa madini Tanzania.

Katika kosa la pili gazeti hilo lilitumia makala ya Mbunge mmoja na mtaalamu wa sheria za madini nchini yenye maelezo juu ya mambo muhimu katika kumsaidia Mhe. Rais katika vita ya uporaji wa rasilimali madini.

 Vyombo vya habari kama watu wengine wana haki ya kutoa habari kama wanadhani ina maslahi kwa umma ilimradi hazikiuki sheria.  Tumeshangazwa kuona Waziri kitaaluma ni Mwanasheria ametumia Agizo la Rais Kama sheria kitendo ambacho ni hatari kwa mustakabali wa Taifa kama kila kitakachoagizwa na kiongozi mkuu kitachukuliwa kama ni sheria. 

Hata hivyo kwa mujibu wa Mawio, Agizo la Rais kuhusu kuzuia marais wastaafu wasitajwe au kujadiliwa kwenye sakala la madini lilitoka wakati tayari gazeti hilo toleo la tarehe 15/6/2017 lilishakuwa limeshachapishwa na kusambazwa kwa mawakala nchi nzima tarehe 14/6/2017 wakati ambapo ndipo Agizo la Rais lilitoka tarehe hiyo hiyo 14.

Taarifa rasmi ya Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO na msemaji mkuu wa Serikali ilinukuu Kifungu cha sheria cha 50 (a) (b) (c) (d) na (e) kuwa ndicho kifungu kilichokiukwa na gazeti la Mawio kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Dr. Harrison Mwakyembe. Aidha, kifungu kilichotumiwa na waziri kutoa adhabu hakiendani na kifungu kilichotamka kosa lililotendwa na gazeti la Mawio.

Kwa mujibu wa kifungu kilichotumika, mamlaka yenye uwezo wa kutoa adhabu ni mahakama baada ya kumsikiliza mtuhumiwa jambo ambalo katika maamuzi ya Waziri Mwakyembe halikufanyika ukiachilia mbali kwamba yeye sio mahakama.

Ikumbukwe kwamba, mamlaka pekee yenye uwezo wa kutoa haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mahakama kwa mujibu wa Ibara ya 107 (A) (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Hivyo waziri kutoa adhabu kama hii amekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kifungu alichotumia kutoa adhabu hakielezi kosa lililotendwa na gazeti la Mawio na kisheria adhabu haiwezi kutolewa bila kuwepo kosa (no punishment without law kwa kilatini Nullum Criminem Sine Lege). Waziri ametoa adhabu kwa gazeti la Mawio bila kufuata misingi ya sheria ili hali yeye mwenyewe ni mwanasheria.

Ikumbukwe mpaka sasa kwambakuzuia kujadili watu au juu ya masuala ambayo hayakuwekwa katika ripoti mbili za  kamati ya Mhe Rais  juu ya kashfa ya madini,  haiondoi haki na  wajibu  kwa watanzania kama ilivyoanishwa katika katiba ya nchi kama ifuatavyo;

• Kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake Ibara ya 18(a). Makala iliyochapishwa katika ukurasa wa 12 ni maoni ya mwandishi wa makala hiyo kwa mujibu wa kifungu hiki.

• Kila mtu amepewa haki wakiwemo waandishi wa habari kutafuta, kupokea na kutoa taarifa kama inavyoelezwa katika Ibara ya 18 (d) ya  Katiba. Wanahabari ni sehemu muhimu katika maendeleo ya taifa letu na wamekuwa kiungo kizuri cha utekelezaji haki hii.

• Kila Raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na shughuli muhimu kwa wananchi Ibara ya 18 (b).  Suala la Madini ni tukio muhimu kwa maisha ya Mtanzania na gazeti la mawio lilikuwa katika kufikisha taarifa mbalimbali zinazohusiana na sakata hili la madini.

• Katiba ibara ya 27 (1) imempa wajibu kila Mtanzania wajibu wa kulinda rasilimali asili za nchi. Hivyo pamoja na kuwa kuna  ripoti mbili za kamati, bado watanzania wengine wana wajibu wa kumsaidia Mhe. Rais katika kulinda rasilimali za nchi kama gazeti la Mawio lilivyofanya kwa kuruhusu watanzania watoe taarifa wanazoona ni muhimu kumsaidia Rais katika sakata hili.

Tumebaini pia hakukuwa na  utaratibu mzuri wa kuwasikiliza viongozi wa Mawio kwani Idara ya Habari iliwasiliana kwa njia isiyo rasmi na Mhariri wa Mawio bila ya kutoa barua yoyote ya kiofisi.  Pamoja na kwamba hakukuwa na mawasiliano yoyote ya kiofisi zaidi ya simu, Mawio waliandika barua ya kuelezea sababu za kuchapisha gazeti lao na taarifa husika.

 Moja ya sababu ni kuwa gazeti lilipishana na Agizo la Rais. Maanake Agizo liliwafikia wakati tayari gazeti limekwishachapwa na kusambazwa kwa mawakala.

Nguvu kubwa kama hizo alipewa Waziri pia katika Sheria ya Magazeti ya 1976 na sasa imeletwa  katika Sheria ya Huduma za Habari.

Waziri chini ya sheria hii mpya anafanya kazi kama mhariri mkuu, mlalamikaji, mchunguzi, mpeleka mashtaka na jaji.

Kwa mfano, Kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari inasema kwamba, "Waziri atakuwa na uwezo wa kuzuia au kuweka vikwazo kwa uchapishaji wa maudhui yoyote ambayo yanahatarisha usalama wa taifa au usalama wa umma."

 Hiki ni kipengele pekee ambacho Waziri anaweza kutumia kupiga marufuku gazeti. Kifungu hicho kinampa nguvu kubwa mno mtu moja kuamua makosa yanayofanywa chini ya Sheria ya Huduma za Habari na kuwa muamuzi wa makosa hayo pia.  Ni kinyume na misingi ya sheria za utawala bora.

Licha ya ukweli kwamba sheria hii ni mbaya sana na ni hatari kwa uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari kwa ujumla, tunaona hakuna uwezekano wowote kwamba machapisho hayo yameweza kuuweka "usalama wa taifa au usalama wa umma hatarini”.

Badala yake, uchapishaji wa picha za viongozi wastaafu wa nchi na makala iliyoundwa vizuri ikionyesha namna ambavyo sheria mbaya katika sekta ya madini zilipitishwa katika nchi yetu kipindi cha uongozi wao inaweza kutumika vyema na serikali, Bunge na wadau wengine ili kupata ufumbuzi sahihi katika usimamizi wa rasilimali zetu.

Kufungiwa kwa Mawio si tu kumekiuka sheria zetu kuhusu uhuru wa kujieleza lakini pia kimataifa imevunja Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) na Mkataba wa Afrika ambao Tanzania imeridhia.

 Kwa  uzuiaji huu idadi kubwa ya Watanzania wamenyimwa haki ya kupata taarifa na hivyo inapunguza kiwango cha uwazi kwa viongozi wa serikali kwa sababu waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla ni waangalizi  wa utendaji wa serikali.

Kwa ujumla hatukuona sababu kubwa ya kulifungia gazeti hilo kwani tuhuma zote zilikuwa zinazungumzika lakini katika njia ambayo ingehusisha makundi kadhaa katika sector ya habari badala ya kumwachia Waziri awe mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mwamuzi kwa wakati mmoja.

WITO NA USHAURI WETU
• Serikali itengue uamuzi wake wa kulifungia gazeti la Mawio kwani umeenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 ambayo kimsingi haimpi mamlaka waziri kutoa adhabu aliyoitoa.

• Juhudi za serikali katika kuhakikisha uchumi unakua na juhudi za kupambana na rushwa lazima ziende sambamba na viongozi kuwa wavumilivu na kukubali kukosolewa kwa  mambo ambayo ni muhimu katika kufikia malengo na matarajio hayo.

• Ili kutimiza nia ya Rais wetu  ya dhati katika kukabiliana na watuhumiwa wote wa kashfa za madini, yampasa kuruhusu wananchi kuwajadili kwa uhuru wale wote wanaotuhumiwa kuhusika bila kujali kwamba wametajwa katika taarifa ya Kamati au la.

• Tunamshauri Rais atambue kuwa hiki kizuri anachokifanya leo katika kulinda rasilimali asili, kinaweza kuwafanya wananchi kwa nia nzuri kabisa kuhoji  viongozi wa zamani walifanya nini kwa kuwa walikuwa na jukumu kubwa katika kushawishi aina ya usimamizi wa rasilimali wakati wa uongozi wao.

• Ikumbukwe kwamba vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na Magazeti hufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Katiba inasema wazi chini ya Ibara ya 18 kwamba Watanzania wote wana haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari na maoni kwa njia yoyote.

• Kwamba serikali inapaswa kuondoa marufuku yake dhidi ya Mawio kuzingatia kwamba sheria hii inakiuka misingi ya kidemokrasia na inajenga picha hasi ya nchi yetu kwa jumuiya ya kimataifa.

• Ni wakati muafaka sasa kwa Sheria ya Huduma za Habari, 2016 kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kwamba vifungu vyake vinaendana na matakwa ya  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatoa ukakika wa uhuru wa kujieleza.

• Tunamshauri Mhe Rais avione vyombo hivi vya habari kama wabia wazuri katika kupambana na rushwa nchini , na asikubali kuona wasaidizi wake wanachukua hatua za kuwajengea hofu waandishi wa habari katika kuhabarisha mambo yanayohusu ufisadi na uhujumu uchumi.

• Vyombo vyote vya habari na wanahabari waweke tofouti zao pembeni na waamke kupigania uhuru wao wa kufanya kazi zaao kama katiba ya nchi inavyotaka.

• Kwamba waandishi wa habari na wahariri wachukue kwa uzito masuala yenye maslahi ya Taifa na pia kusimamia maadili ya taaluma zao.

• Tunashauri Sheria ya Huduma za Habari ifanyiwe marekebisho ili kuondoa vifungu vinavyompa mtu mmoja mamlaka ya kufungia chombo cha habari na kuweka mfumo shirikishi utakaoshirika wadau wengine wa vyombo vya habari katika kufuatilia makosa yanayofanywa na vyombo vya habari

• Kutokana na kuwa hakuna sehemu yoyote ya kupeleka rufaa dhidi ya maamuzi ya Waziri katika sheria ya huduma za habari ya 2016,  endapo hakutakuwa na mazungumzo na waziri,  tutakwenda mahakamani kwa kushirikiana na Mawio kuonyesha haki zilizokiukwa katika kulifungia gazeti hili.

Imetolewa kwa pamoja kati ya MCT, UTPC na THRDC leo Juni 18, 2017
...............................................................
Pili Mtambalike
Kaimu Katibu Mtendaji  Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Taifa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)

Deogratius Nsokolo,
Rais – Umoja wa  Vilabu vya Waandishi Habari Tanzania-UTPC

Wananchi wa Tarime Wavamia Mgodi wa North Mara

0
0
Siku  chache baada ya Rais Dk. John Magufuli  kukabidhiwa ripoti ya pili ya kuchunguza mchanga wa dhahabu wa Kampuni ya Madini ya Acacia, wananchi wa Tarime wamevamia mgodi wa North Mara kwa siku mbili mfululizo.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni mwendelezo wa kupinga uonevu unaofanywa na wawekezaji hao kupitia Kampuni ya Acacia.

Taarifa kutoka wilayani Tarime zinadai  kuwa wananchi hao walivamia mgodi huo juzi saa 2.00 usiku na jana asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wananchi hao walikwenda hadi kwenye mtambo wa kufua dhahabu na   kufanya uharibifu   huo kabla ya kudhibitiwa na jeshi la polisi.

Hata hivyo shuhuda huyo ambaye hakutaka kutaja jina , alisema vurugu hizo zimetokana na uongozi wa Kampuni ya Acacia kushindwa kuwalipa fidia wananchi waliokuwa na maeneo yao tangu  awali.

Alisema wakati madini yalipogundulika,   wananchi walioondolewa walitathiminiwa mali zao yakiwamo mashamba, nyumba na kuahidiwa kulipwa fidia akini hadi sasa hawajalipwa stahiki zao.

Alisema kwa siku mbili mfululizo  wanachi wenye madai yao walifika katika ofisi za kampuni  na kuona baadhi ya majina ya wanaotakiwa kulipwa fidia yakiwa yamebandikwa katika ubao wa matangazo lakini majina ya wengine yakiwa hayajabandikwa.

“Wale ambao hawakuona majina yao walichukuana na kuvamia   mtambo  wa kufua madini na kuondoka na mawe  ambayo tunahisi mengine yana dhahabu.

“Lakini polisi walifika na kuwatawanya na  mabomu ya machozi,’’ kilisema chanzo cha habari hiyo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga,   alisema alikuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ingawa aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari leo.

“Nimesema hivi, siwezi kuzungumza lolote, sina cha kuzungumza na siwezi kuzungumza na mwandishi hadi hapo tutakapokaa kikao kesho (leo) ndiyo nitasema,’’alisema Luoga.

Alipotafutwa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema)   kujua kama hatua ya wananchi hao inatokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuwa atawaongoza wananchi   kuwaondoa Acacia kwa kuwa wamekuwa wakiwaibia kama ilivyoelezwa kwenye ripoti ya Tume ya Rais Magufuli, alisema kwa sasa yupo  Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge .

Alisema  anachojua ni kuwa wananchi hao wamekuwa wakidai malipo yao kwa muda mrefu.

“Wananchi wamekuwa na malalamiko wakidai malipo yao na tayari mgodi umeshaleta madhara mengi, hilo naweza kusema lakini mengine zaidi ya hayo siwezi kuyajua,’’ alisema Heche.

Marekani yaitungua ndege ya kijeshi ya Syria

0
0
Marekani imeitungua ndege ya kijeshi ya Syria iliyokuwa ikijiandaa kuwashambulia wanamgambo wa IS ambao wamekuwa wakihatarisha maisha ya wananchi wa nchi hiyo huku umoja wa mataifa ukitaka kuwepo na usuluhishi.

Aidha, Marekani imesema kuwa imefikia hatua hiyo mara baada ya jeshi la Syria kuvishambulia vikosi vya Syrian Democratic Force SDF, vinavyoungwa mkono na Marekani  kwa lengo la kupambana na wanamgambo wa Islamic State.

Kwa upande wa Serikali ya Syria imesema kuwa ndege yake ilikuwa katika maandalizi ya kuwashambulia wanamgambo wa Islamic State na si vikosi vya Syrian Democratic Force vinavyoungwa mkono na Marekani.

Vikosi vya Syrian Democratic Force (SDF ) vinaungwa mkono na umoja unaoongozwa na Marekani kwaajili ya kupambana na wanamgambo wa Islamic State ambao wamekuwa tishio katika ukanda huo.

Vigogo wa Escrow (James Rugemarila na Harbinder Sethi ) wafikishwa mahakamani leo

0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) aimewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wafanyabiashara James Rugemarila na Harbinder Sethi kwa tuhuma za uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hao.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa muda mrefu wamekuwa wakiulizwa kuhusu kesi ya Escrow hivyo sasa anaamini ni wakati muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa hao wawili mahakamani.

Mlowola alisema kuwa taasisi hiyo imefanya uchunguzi wa kutosha kwa muda wote ambao ilikuwa kimya, na hivyo wamefikishwa mahakamani kisutu na baada ya hapo mahakama itafanya taratibu za kuhamishia kesi hiyo katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images