Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Moshi yazuia jeneza la mwili wa Ndesamburo Kutembezwa Barabarani

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia  utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili  aliyekuwa  Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon  Ndesamburo .

 Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.

Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu  kwa watumiaji wengi wa barabarani.

“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.

 Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu alisema  kuwa  mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.

Waziri Mkuu Kutuma Mkaguzi wa Dawa Gairo

$
0
0
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema atatuma mkaguzi aende kuchunguza hali ya upatikanaji wa dawa kwenye zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo, mkoani Morogoro.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Gairo na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Gairo ‘A’.

Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo baada ya kumhoji Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Albert Lyaruu kama anamiliki duka la dawa au laa na kujibiwa kwamba hana duka la dawa ingawa alikiri kwamba baadhi ya watumishi wa idara yake wanayo maduka ya dawa.

“Sasa ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu ili tupate picha halisi kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje. Huyu mkaguzi atakuja kukukagua wewe mwenyewe na kwenye zahanati zako.

“Kwenye mkutano wangu na watumishi wa Serikali nimewaeleza kwamba ninyi ni desk officers (maofisa wa kukaa ofisini tu), wala hamuendi vijijini kuona hali halisi ikoje. Ndiyo maana wananchi hawa wanalalamikia kukosa dawa na wewe wala hujui,” alisema Majaliwa.

Pamoja na hali hiyo alimtaka mganga huyo kuhakikisha anakwenda kwenye vituo vya afya na zahanati  ili kuangalia matumizi ya dawa  na kama hatofanya hivyo anaweza kupata kesi kama ya Mkoa wa Shinyanga ambapo mganga wa kituo cha afya alikutwa na dawa za Serikali nyumbani kwake, baada ya wanachi kumwekea mtego hadi akakamatwa.

 “Serikali haizuii watumishi kuwa na maduka ya dawa, tunachokataa sisi ni kuchukua dawa za Serikali ambazo zinatakiwa kuwatibu wananchi na kuzipeleka kwenye maduka yenu. Tumezuia pia kuwepo kwa maduka ya watu binafsi nje ya hospitali, zahanati au kituo cha afya,” alisema

Waziri Mkuu aliwataka wananchi wa Gairo wawe macho na walinde mali za umma na inapobidi watoe taarifa mara tu wanapobaini kuna mtu anatumia mali ya umma vibaya.

Waziri Mkuu alikuwa alimwita jukwaani, Dk. Lyaruu ili aeleze ni kiasi gani cha fedha amepokea kutoka Serikalini kwa ajili ya ununuzi wa dawa na alipotoa mchanganuo wake, wananchi waliohudhuria mkutano huo walizomea na kudai kuwa siyo kweli.

“Ninapokea shilingi  milioni 109 kila robo mwaka. Na katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho tumepokea shilingi milioni 109 na kati ya hizo tunatoa asilimia 33 ambazo ni sawa na shilingi  milioni 36 kununua dawa na vifaa tiba. Kwa hiyo hadi sasa hali ya dawa ni nzuri na upatikanaji wake ni kati ya asilimia 85 hadi 90,” alisema Dk. Lyaruu.

Kutokana na majibu yake hayo, wananchi walimzomea daktari huyo na kudai kuwa wananunua dawa hizo kwenye maduka ya dawa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano huo kwamba dawa zinazopatikana kwenye zahanati zinatofautiana na dawa zinazopelekwa kwenye kituo cha afya, hospitali ya wilaya au ya mkoa.

Kikwete Aibuka.....Asema Kuongoza Nchi Ni Mzigo Mzito, Amtia Moyo Rais Magufuli

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kusema suala la kuongoza nchi ni kazi kubwa mno na kusema yeye toka amestaafu kazi hiyo saizi anaweza kulala na usingizi ukaisha vizuri lakini kipindi cha nyuma haikuwa hivyo.

Kikwete amesema hayo jana kwenye Futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi nyumbani kwake Msoga, Pwani na kusema saizi mzigo huo ameubeba Rais Magufuli na kudai huwa anamtia moyo kuwa anapaswa kupambana kwani hata wao wamepitia mambo ambayo yeye anapitia.

"Sasa nimestaafu muda wa kuwasaidieni ninao tofauti na zamani, zamani mambo mengi kubeba mzigo wa kuongoza nchi kazi kubwa sana saizi anahangaika nao Rais Magufuli wakati mwingine nampa moyo tu bwana wewe pambana, wenzako wote ndiyo hivyo hivyo tulipitia humo humo pale unapodhani unatenda jema asubuhi wanakuponda, ndiyo muziki wenyewe lakini mara kuna hili kuna lile saizi mimi nalala usingizi unaisha kabisa kama kuna watu wananisumbua watakuwa ni wajukuu tu" alisema Kikwete

Mnyika aahidi kumchukulia hatua askari wa Bunge aliyemsukuma

$
0
0
Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema atachukua hatua kwa kitendo cha kusukumwa kilichofanywa na askari wa Bunge mwishoni mwa wiki.

Alisema atafanya hivyo mara baada ya kumaliza msiba wa mmoja wa waasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo.

“Nitatoa tamko na kuchukua hatua nikimaliza msiba, leo (jana) na kesho (leo) nipo msibani huku Moshi, lakini nitafafanua na kuzungumzia hilo nikimaliza,” alisema.

Mnyika alitolewa bungeni kwa nguvu na askari wa Bunge baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwaamuru kumtoa ndani akidaiwa kukiuka kanuni za Bunge wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini.

Pia, mbunge huyo alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao saba vya Bunge, huku askari hao wakimtoa ndani kwa nguvu na kumsukuma.

Ndesamburo, ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15 mfululizo ataagwa leo katika Uwanja wa Majengo mjini Moshi na baadaye mwili wake utapelekwa nyumbani kwake ambako taratibu za mazishi zitafanyika kesho.

Wakati Mnyika akisubiri kumzika Ndesamburo, Chadema Wilaya ya Ubungo imelaani kitendo alichofanyiwa mbunge huyo ikisema hakikuwa cha kiungwana na kilikiuka hadhi yake.

Katibu Mwenezi wa Chadema wilayani humo, Perfect Mwasiwelwa alisema kitendo alichofanyiwa Mnyika kingeweza kumletea majeraha kama angeanguka kutokana na mazingira ya eneo aliposukumiwa.

Mwasiwelwa alisema mwanasiasa huyo anawawakilisha wananchi zaidi ya 78,000 hivyo Chadema inalaani kitendo hicho kwa sababu si cha utu.

“Alitolewa nje katika mazingira ambayo sio ya utu, sio ya Kitanzania, sisi kama chama ngazi ya wilaya tunasema hakikuwa kitendo cha kawaida kabisa,” alisema.

Wakati huo huo, wabunge wawili wa Chadema; Halima Mdee (Kawe) na Esther Bulaya (Bunda Mjini) leo watasomewa hukumu yao baada ya Kamati ya Kudumu ya Maadili ya Bunge kuwajadili na kumshauri Ndugai hatua sahihi za kuwachukulia.

Bulaya na Mdee watasomewa hukumu kutokana na kulivalia njuga suala la Mnyika kutolewa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati spika alipoamuru atolewe na askari wa chombo hicho.

Makamu wa Rais avitangazia hatari viwanda na migodi inayoharibu mazingira

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi ambayo inafanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwemo utitirishaji wa kemikali kwa wananchi kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo tarehe 4-Jun-2017 kijijini Butiama mkoani Mara wakati anahutubia wananchi katika kilele cha siku ya mazingira Duniani.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alisema uharibifu wa mazingira ukiachiwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo kote nchini.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kwa ushirikiano na jamii kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuokoa mifumo ya ikolojia, uhifadhi wa bioanuai, kudhibiti uchomaji miti kiholela ili kurejesha uoto wa asili ambao umeharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo mengi nchini.

“Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo huo na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani”. Alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alisema katika kuadhimisha siku ya mazingira Dunia viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

Kuhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa nchini, Makamu wa Rais aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuruhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa bila kiingilio na kusema mpango huo ni mzuri na unatakiwa kufanyika kila mwaka.

Alisema kuwa mkakati huo unalenga kuhamasisha wananchi ili kuwa mahusiano rafiki na mazingira kwa kuzingatia ukweli kwamba jinsi wananchi wanapoona ndipo wanapoamini na kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Alieleza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo inapasa jamii kutafakari mchango wa kila sekta na kila mwananchi katika uhifadhi wa mazingira kwenye maeneo wanayoishi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira January Makamba alisema Serikali imeamua kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kijijini Butiama kama hatua ya kuenzi mchango mkubwa uliofanya na baba wa taifa  mwalimu Julius Nyerere katika uhifadhi wa mazingira.

Alisema baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere alifanya kwa vitendo katika kuhifadhi mazingira ambapo alianzisha msitu wake katika eneo la Butiama hivyo wananchi wote ni lazima waige mfano huo katika kulinda na kutunza mazingira.

Kwa upande wa familia na mwalimu Nyerere wameishukuru Serikali kwa kupeleka maadhimisho hayo kijijini Butiama ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kutambua mchango wa baba wa taifa katika uhifadhi wa mazingira nchini.

Kabla ya Kuhutubia katika Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alipanda miti katika msitu wa Mwalimu Nyerere na kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Ndege ya Kivita ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) uliopo katika msitu wa Muhunda katika kijiji cha Butiama mkoani MARA.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Butiama – Mara
4-June-2017.

CUF Ya Maalim Seif Yazindua Ofisi Magomeni Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Suleiman Msuya
IKIWA ni takribani miezi 10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Buguruni na kundi la Profesa Ibrahim Lipumba chama hicho kimezindua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa, Kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aidha, Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na Profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana sifa hizo kwa sasa.

Akizindua ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge 40 wa CUF, Seif alisema uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni cha kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.

Alisema kwa muda wa miezi 10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande wa Tanzania Bara jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.

Maalim Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya mambo hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa kukutana na wakurugenzi wake.

“Nimekuwa ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi, viongozi mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha kuungwa mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi hiki,” alisema.

Katibu huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa kukutana na wakurugenzi wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.

“Hakuna shaka kuwa huu unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu kwani CUF ni chama imara hakitikisiki,” alisema.

Maalim Seif alisema jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana na misingi ya chama hicho.

Alisema kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza kuwa haki haipotei ila inachelewa.

Katibu huyo alisema anaimani na mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

Aidha, alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inashikilia zaidi ya sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya chamahicho.

Maalim Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.

Kwa upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.

Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu kamahuyo.

Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa CUF bungeni, Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua ofisi nyingine ili wapate mahali pa kukutana wakiwa nje ya Bunge.

Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.

Kwa upande wake Mbunge wa Temeke CUF, Abdallah Mtolea alisema katika ofisi hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za Bunge ili kuwarahisishia katika uchangiaji bungeni.

Alisema katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa sh. milioni 18 kwa mwaka ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania
 
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..
CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?


(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.


Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)


KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.

Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.


Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa 

 
whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Maalim Seif Azungumzia Kitendo cha Rais Magufuli Kuteua Mpinzani Kuwa Mkuu wa Mkoa

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amemkingia kifua Rais Dk. John Magufuli kwa uamuzi wake wa kumteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Maalim Seif alisema Rais Magufuli hajakosea kwa uteuzi huo kwa kuwa hapangiwi nani amweke wapi na nani asimweke. 
 
“Uteuzi ni haki yake, wala hatuingilii maamuzi yake kwa sababu kuteua au kutoteua ni yeye na kuteua ACT na kuacha vyama vingine huenda yeye mwenyewe ana yake moyoni na kwamba hajaamua kufanya hivyo. 
 
“Mimi sikuingia katika moyo wake na kwa kufanya hivyo si jambo geni kwa kuwa wapo waliopita waliwapa wapinzani ubunge, lakini pia ni Rais wa kwanza kuingiza mtu wa chama kingine kwenye serikali katika utendaji…si jambo baya kwa maana linaweza jenga upya Serikali,’’ alisema. 
 
Alisema Rais Magufuli ametumia mfumo ambao pia hutumiwa na nchi za Bara la Ulaya na Marekani, ambapo Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama naye aliutumia. 
 
“Siwezi kushangaa kwani inaweza ikatokea siku akamteua Naibu Katibu Mkuu wangu, Joran Bashange kuwa Waziri wa Nishati na Madini,” alisema Maalim Seif huku waandishi na maofisa wa chama hicho wakiangua kicheko. 

 Nao Umoja wa  Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),  umesema hatua ya Rais Dk. Magufuli kumteua Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ni kitendo cha kijasiri na cha kizalendo kwa sababu  hakuna alipokosea.

Pamoja na hali hiyo, umoja huo umesema uteuzi wa nafasi ya RC Mghwira, ni wazi ataisimamia na kuongoza kwa hekima, busara na uzalendo kwa masilahi ya Taifa.

Kauli hiyo, imetolewa  Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka.

Alisema uteuzi huo, usiibue nongwa na kuonekana kuna jambo limekosewa.

Pamoja na hali hiyo Shaka, alisema Katiba ya nchi hairuhusu mgombea binafsi na kwamba kila mgombea urais, udiwani au ubunge hutokana na chama cha siasa ila anaposhinda urais huwa na mamlaka ya kuteua mtu yeyote ili mradi awe Mtanzania bila ubia.

Alisema Rais Dk. Magufuli, ana haki na wajibu wa kumteua mtu yeyote atakayeona anafaa kushika nafasi atakayomteua ilimradi aliyeteuliwa awe ana hisia za uchapakazi, mpenda umoja na mzalendo.

Shaka alisema katiba ya CCM imetamka ikiwa kutakuwa na mkuu wa mkoa anayetokana na CCM atashiriki vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa wakati wa vikao lakini kwa suala la Mghwira lipo tofauti kwani anatokana na chama kingine na ikiwa ataona kuna haja ya kujiunga na CCM basi naye atapata fursa ya kushiriki vikao hivyo.

“Ila kwa sasa hasa baada ya kuripoti katika eneo lake la kazi hatoweza kuhudhuria vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa kuwa si mwana CCM ila kama ataona kuna haja ya kujiunga na CCM hazuiwi na atakuwa na haki ya kuhudhuria vikao vyote.

“Kwa hili Rais Dk. Magufuli anabaki kuwa nembo ya demokrasia ya kweli nchini kwetu kwa kushirikisha wapinzani kwenye nafasi nyeti za utendaji.


“Viongozi wa Serikali wakiteuliwa hula viapo vya utii ambavyo vimeandikwa kisheria katika medani za uendeshaji Serikali, mteule wa Rais hali kiapo cha kisiasa bali huapa kiapo cha kutumikia nchi na watu wake kwa mujibu wa sheria za nchi na Katiba,”
alisema Shaka. 

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Mwenyekiti Wa Chama Chake Kuteuliwa Kuwa Mkuu wa Mkoa

$
0
0
Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 

Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.

Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.

Aliyeteuliwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, sio mshauri au mwanachama tu. Ni mmoja wa viongozi wa juu wa Chama chetu. Uteuzi wake unahitaji kikao cha Kamati Kuu ya Chama kukaa na kujadili. Nitaweza kutoa Taarifa baada ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama. 

Kwa sasa umma usubiri vikao Kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu.

Adhabu: Halima Mdee na Esther Bulaya Wapigwa Marufuku Kuhudhuria Bunge Hadi mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19

$
0
0

Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.
 
Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo.
 
Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.
 
Hata hivyo, Bunge liliendelea kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe.
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.
 
Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.


Halima Mdee: Porojo za Dodoma haziniumizi Kichwa

$
0
0
Baada ya kupatiwa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge vilivyobakia Mbunge wa Kawe Mh. Halima James Mdee ameibua mapya na kusema porojo za Dodoma hazimuumizi kichwa na badala yake anaangalia zaidi suala la kumsindikiza Muasisi wa chama.

Kipitia ukurasa wake wa twitter Mh. Mdee ameandika kwamba

"Tunamsindikiza jemedari wa mageuzi Mhe. Philemon Ndesamburo kwenye nyumba ya milele!, porojo za Dodoma haziniumizi kichwa" aliandika Mdee kupitia ukurasa wake wa twitter.

Mnyika awaponza askari wa Bunge......Ndugai Kaamua Kuwahamisha

$
0
0
Askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.
 
"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaofaa," amesema Ndugai.
 
Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.
 
Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.
 
Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo. 
 
Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge.

Mbowe Aikana Sauti Inayosambaa Mitandaoni Ikidai Wema Sepetu ni Mpenzi Wake

$
0
0
Habari inayotikisa mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile Audio  (voice note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.

Leo kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM  Mbowe ameielezea sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka: 

“Mimi nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema kwa sababu siyo za kweli.

“Timu yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu. 

"Sauti siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za upotoshaji tu."

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 6

Kisukari Ni Ugonjwa Unao Weza Kudhibitiwa Kwa Kutumia Tiba Asilia

$
0
0
Kisukari  ni  tatizo  la  kiafya  linalo wasumbua  na  kuwatesa  mamilioni  ya  watu  duniani. Miongoni  mwa  dalili  za  ugonjwa  wa  kisukari ni pamoja  na

i. Kukojoa  mara  kwa  mara  ( Watoto kukojoa  kitandani )

ii.Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.

iii.Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.

iv.Kupungua uzito  kwa  kasi  au kukonda pamoja na kwamba unakula  vizuri  tena kila  wakati  kwa  sababu  ya  kusikia  njaa kila  wakati  kunakosababishwa  na  maradhi  ya  kisukari

v.Wanawake  kupatwa  na  tatizo  la kuwashwa ukeni.

vi.Kupoteza  uwezo  wa Kuona  vizuri.

vii.Wanaume  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu na / ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  na  wanawake  kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa.

viii.Kupatwa  na  ganzi,  kusikia  hali  ya  kama  kuchomwachomwa au kutohisi chochote  pindi  unapoguswa  kwenye  sehemu za miguu, viganjani na  kwenye  vidole.

ix.Miguu kuoza na hata kupata gangrini.

x.Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.

xi.Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.

xii.Kutokwa  na   Majipu kwenye  sehemu  mbalimbali  mwilini.

Kwa  mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu , watu walio katika makundi yafuatayo  wapo katika  hatari  kubwa  ya  kupatwa  na  ugonjwa wa kisukari kuliko watu wengine.  Watu  hao  ni  kama  ifuatavyo :

i. Watu  wenye   uzito uliozidi,

ii.Watu  wanao  toka  katika  familia  zenye  historia  ya  kuwa  na  wagonjwa  wa  kisukari.

iii.Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

iv. Watu   wasio  fanya  mazoezi

v. Wagonjwa  wa  shinikizo la damu,

vi.Watu wenye  kiasi  kikubwa  cha  lehemu  mbaya  ( Bad  Cholestrol ) kwenye  damu.

vii.Watu  wenye   virimba  tumo (  vitambi):  Wataalamu  wa  afya  wanaeleza  kuwa, kuna hatari kubwa ya kupatwa na maradhi  ya  kisukari ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu

viii.Watu  wenye msongo wa mawazo na

ix.Watu  wanao tumia  pombe  na kupita  kiasi  pamoja  na  wale  wavutaji  wa  sigara  kupita  kiasi: Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa  na  tatizo  la  kisukari,kwani kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu, uvutaji  sigara huathiri  moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu.  Tafiti  mbalimbali  za  kiafya  zinaeleza  kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

x. Kundi  jinginge  la  watu  walio  katika  hatari  ya  kupatwa  na  maradhi  ya  kisukari  ni  watu wenye  umri  mkubwa  kuanzia  miaka  55  na  kuendelea

Wataalamu  wa  afya  wanashauri  watu walio  kwenye   orodha  iliyo  tajwa  hapo  juu, kujiwekea  utaratibu  wa  kuwa  wanapima  afya  zao  walao  mara  moja  kila  mwakaili waweze  kuchukua  hatua  stahiki  za  kiafya endapo  watakutwa  na  tatizo  la  sukari.
TIBA   ASILIA   KWA   WAGONJWA   WA  KISUKARI
Zipo  tiba  asilia  mbalimbali  zinazo  saidia  kkupunguza  maradhi  ya  kisukari. Miongoni  mwa  tiba  hizo  ni  pamoja  na  tiba  ijulikanayo  kama  Mkatasukari. Tiba  hii  inasaidia kushusha  na  kudhibiti  kiwango  cha  sukari  kwa  mgonjwa mwenye  sukari  ya  kupanda. Kama  unasumbuliwa na  maradhi  ya  kisukari ( Sukari  ya  kupanda ), unaweza  kujaribu  kutumia  tiba  hii.

JINSI   YA   KUANDAA  TIBA  ASILIA  YA  MKATASUKARI

Mahitaji  ;
i. Nanasi  moja  kubwa

ii. Majani  ya  chai  vijiko vitatu vya  chakula

iii. Maji  lita  tano

iv. Dawa asilia  ya  Mkatasukari  vijiko  vikubwa  vitatu.

MATAYARISHO:  Chukua  nanasi  lako  lililo  iva  vizuri, limenye  kisha  likate  vipande  vidogo vidogo,  kisha  liweke  kwenye  sufuria  halafu ndani  ya  sufuria  hilo, ongeza  lita  tano  ya  maji  safi.  Baada  ya  hapo  weka  majani ya  chai vijiko  vikubwa  vitatu, kisha  ongeza  vijiko  vikubwa vitatu  vya  dawa asilia  ya  Mkatasukari, kisha  chemsha  kwa  muda  wa  dakika  thelathini (30).

Baada  ya  dakika  thelathini, ipua   na  uchuje, makapi  weka  pembeni, kisha  hifadhi  kimiminika  chako  kwenye  chombo  safi.

MATUMIZI  :
Tumia  kunywa  kikombe  kidogo chenye ujazo milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills ) au  robo  lita  kwa  lugha  nyepesi. Utafanya  hivyo  mara  tatu  kwa  siku, asubuhi  mchana  na  jioni  hadi  dozi  yako  itakapo  kamilika.

Baada  ya  kutumia  dozi  hii, unashauriwa  kwenda  hospitali  kupima   tena  sukari  ili  ujue  sukari  yako  imeshuka  kwa  kiasi  gani  pamoja  na  kupata  ushauri  wa  daktari  wako.

Kwa  mahitaji  yako ya  tiba  asilia  ya  Mkatasukari, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM,  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini DAR  ES  SALAAM, ambao  hawawezi  kufika  ofisini kwetu., tunatoa  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY ), kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  watasafirishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti, kwa  wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabasi mbalimbali. Wateja  waliopo NAIROBI  na  MOMBASA  watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  usafiri  wa  mabasi  mbalimbali.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83 84

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu ;


Anna Mgwira kuapishwa leo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mteule Anna Elisha Mghwira leo Juni 6, 2017 saa 3:30 asubuhi hii Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Anna Mghwira anaapishwa leo baada ya kuteuliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Said Meck Sadick aliyeomba kujiuzulu.

Hadi wakati huu hakuna taarifa rasmi iliyokuwa imetolewa na Chama cha ACT Wazalendo kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wao, na wala mteule huyo hajazungumza jambo lolote.

Rose Muhando Atiwa Mbaroni mkoani Singida kwa Utapeli

$
0
0
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani humo.

Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida.

Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwenda Singida yeye na wasaidizi wake, fedha ambayo ilitumwa na mawasiliano yakaendelea kufanyika ili kuakikisha kuwa siku ya tukio anakuwepo.

Chakushangaza, siku ya tukio msanii huyo hakujitokeza na walipata taarifa kuwa yupo Kahama anatoa huduma, walipofanya mahojiano walithibitisha kuwa ni kweli.

Alipofanyiwa mahojiano na Polisi, Rose Muhando alikiri kutenda kosa hilo kwa kutotoa taarifa kwamba hawezi kuja na alieleza si kweli kwamba alikuwa kahama, bali alikuwa na mgonjwa nyumbani hivyo hakuweza kutoka. Muhando amesema kuwa yupo tayari kurejesha fedha hizo alizotumiwa.

Lowassa, Sumaye, Mabata Watema Cheche Msibani

$
0
0
Na Regina Mkonde
Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki ya kisiasa.

 Katika hatua nyingine, wameshangazwa na CCM kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia. “Nawapongeza kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure."

Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “Hata njia za kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai, wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu  ya amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.”

 Wakati akitoa salamu hizo, Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia alisema kitendo cha viongozi wa CCM kutohudhuria kwenye ibada hiyo si cha kiungwana kwani kinalenga kugawa wananchi kwa misingi ya vyama.

 “Walichofanya leo sio cha kiungwana, watanzania tusikubali kugawanyishwa kwa misingi ya imani wala vyama, sijauona uwakilishi wa CCM, tuwasamehe na mimi nimewakilisha CCM wote hapa ili tulete amani ya mzee Ndesa.Ndesamburo alikuwa analeta watu wote pamoja, lakini leo hata njia za kupitisha mwili wake nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai,” alisema.

 Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti CUF Severina Mwijage wakati akitoa salamu za rambirambi alisema amesikitishwa na kitendo cha kuzuiwa uwanja kwani marehemu Ndesamburo alishiriki kuujenga uwanja huo.

 “Siasa za sasa hivi ni hatari, za kupandikiza watu chuki ni mbaya sana, na mimi naomba niongezeee wenyewe wanajua chuki ndio chama chao kitakachosaidia kuchukua dola, sisi tunachaguliwa na wananchi tunajua matatizo ya wananchi, aelewe yule anayewachonganisha itakuaje yeye ambaye aliyemchagua atakuja na kuondoka na yeye atabaki katika mkoa na watoto wake wanaishi na wananchi,” alisema.


Ally Kessy: Wabunge Wanaotusumbua Bungeni Wapimwe Madawa ya Kulevya

$
0
0
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.

"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale"  alisema Keissy na kuongeza;

"Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo"

Rais Magufuli Akutana Na Mjumbe Wa Rais Kabila Wa Kongo, Mjumbe Wa Rais Nyusi Wa Msumbiji Na Balozi Wa Kuwait Ikulu Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa kutoa mkopo wa Dola za Marekani Milioni 51 sawa na takribani Shilingi Bilioni 110 kwa ajili ya kujenga barabara ya Chaya - Nyahua Mkoani Tabora yenye urefu wa kilometa 85 ambayo itaunganisha mawasiliano ya barabara kati ya mkoa wa Singida na Tabora.

Mhe. Rais Magufuli ametoa shukrani hizo  jana tarehe 05 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipofanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem na kupokea msaada wa magari mawili ya kusombea taka ngumu yenye thamani ya Dola za Marekani 200,000/- yaliyotolewa na Serikali ya Kuwait kwa lengo la kuunga mkono kampeni ya usafi hapa nchini.

“Naomba unifikishie salamu zangu kwa Mfalme wa Kuwait, mwambie tunathamini mchango mkubwa wa Kuwait katika maendeleo ya nchi yetu, hizi fedha za barabara mlizotupatia zitatusaidia kumalizia sehemu hiyo ya barabara ambayo ndio ilikuwa imebaki” alisema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli pia aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini ikiwemo msaada wa Dola za Marekani 250,000 kwa ajili ya kununulia vifaa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na visima vya maji safi 27 vilivyochimbwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wananfunzi na wananchi wa maeneo jirani na shule.

 Aidha, Mhe. Rais Magufuli aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kutoa Dola za Marekani Milioni 50 kwa ajili ya kuikarabati hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja iliyopo Zanzibar.

Mhe. Rais Magufuli pia aliiomba Serikali ya Kuwait kuweka alama ya kumbukumbu ya uhusiano wake na Tanzania kwa kusaidia ujenzi wa barabara za Makao Makuu ya nchi Mjini Dodoma na amemhakikishia Mfalme wa Kuwait Sheik Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait hususani katika masuala ya kiuchumi ikiwemo mafuta na gesi ambayo imevumbuliwa kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al- Najem alielezea kufurahishwa kwake na uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya nchi yake na Tanzania na amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa Kuwait ipo tayari wakati wowote kuunga mkono juhudi za maendeleo kulingana na vipaumbele vya Tanzania.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli alifanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Mhe. Leonard She Okitundu na kumhakikishia kuwa Tanzania inaunga mkono juhudi za kumaliza tofauti kati ya pande zinazopinga nchini Kongo.

Pamoja na kukabidhi barua yenye ujumbe wa Rais wa DRC Mhe. Joseph Kabila Kabange, Balozi Leonard She Okitundu alimueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Kongo ni shwari na kwamba mchakato wa mazungumzo kati ya pande zinazopingana nchini humo unaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli alifanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji ambaye ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali Atanasio Salvador Ntumuke.

Baada ya mazungumzo hayo, Jenerali Atanasio Salvador Ntumuke alisema Msumbiji itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa mambo mbalimbali kwa kuwa nchi hizo ni ndugu na zimesaidiana kwa mengi tangu harakati za kupigania uhuru ambapo Tanzania ilitoa mchango mkubwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images