Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Watuhumiwa wa Mauaji Kibiti Watiwa Mbaroni

$
0
0
Mkuu  wa Wilaya ya Rufiji, ambaye pia anakaimu Wilaya ya Kibiti, Juma Njwayo,  amesema vyombo vya dola vimewakamata watu wengi wanaodaiwa kuhusika na uhalifu wa kuua watu katika maeneo mbalimbali ya wilaya hizo.
 
Njwayo amesema licha ya watuhumiwa hao kukamatwa, pia vyombo vya dola vinaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo.

“Kuna watu wanaoshukiwa ambao ni wengi wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa, kuna wengine wanatafutwa na wakipatikana watahojiwa, lakini hawajakamatwa kwa maana ya kwamba imethibitika wao ni wahalifu,” alisema.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wa maeneo hayo waendelee kufanya shughuli zao, lakini kwa tahadhari.

“Watu wanalima, wanaofanya shughuli za Serikali wanafanya, lakini haya yanafanyika tunapata uthibitisho kwa mfano wa hawa watu wanne waliouawa huku Rufiji, kwa hiyo hali iko hivyo. Tunaomba watu sasa wafanye shughuli zao kwa tahadhari, wakiona mtu wasiyemjua watoe taarifa katika vyombo.

“Pia kama wanazo taarifa watuambie, sisi tunajua hawa watu wako kwenye jamii, haiwezekani mtu asiyekujua wewe aje akupige risasi jioni, lazima awe anakujua na kama hakujui basi anashirikiana na mtu anayekujua. Hivyo tunawasisitiza hawa wananchi wetu wawe na tahadhari ya kiusalama,” alisema.

Alipoulizwa amebaini nini katika matukio hayo yanayowalenga zaidi viongozi wa Serikali, alisema suala hilo ni gumu na bado haijajulikana sababu ya uhalifu huo.

“Hatujui sababu ni nini, lakini ni kweli watu wote waliopata hilo tatizo wapo askari, wapo viongozi ama ni wa serikali ya vijiji au chama tawala,” alisema.

Awali, Njwayo alikiri wazi kuwa wananchi katika maeneo hayo wanaishi kwa hofu kwa sababu matukio si ya kawaida.

“Lazima uhofu, yaani upo nyumbani kwako unakula mtu anakuja anakupiga risasi, watu nao wanasikia mlio wa risasi lazima wapate hofu, hilo ni jambo la kila mtu mwenye akili yake timamu lazima ahofie.

“Lakini sisi kwa upande wetu wa wilaya halitupendezi jambo hili, tuna hatua nyingi tunazichukua kwa kushirikiana na Serikali Kuu kupambana na jambo hili,”
alisema.

Kauli ya Njwayo imekuja siku chache baada ya watu wasiofahamika kumuua Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Muyui, Iddy Kirungi, huku mtoto wake, Nurdin Kirungi, akipigwa risasi ya tumbo wilayani Kibiti.

Wauaji hao baada ya kutekeleza unyama huo walitokomea kusikojulikana, hali inayotishia usalama wa raia na mali zao, huku wengine wakilazimika kuzikimbia nyumba zao kwa hofu ya kupoteza maisha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema linaendelea kuwasaka wahalifu na kuimarisha ulinzi.

RC Gambo: Tutawadhibiti Wote Wanaoingiza Siasa Misibani

$
0
0
Mkuu wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali itaendelea kuwathibiti watu wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga mbalimbali hasa la vifo vya wanafunzi wa Lucky Vicent na kuwataka watu kufuata utaratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.

Mkuu wa mkoa huyo alisema hayo jana wakati anapokea misaada inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali na kuwataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima.

Mbali na hilo Gambo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria, taratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.

Meya wa Arusha Afunguka Maneno Mazito baada tu ya kuachiwa na Polisi leo

$
0
0
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za rambirambi kwa wafiwa  badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Aidha amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.

Meya, Lazaro aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi leo majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini.

Amesema fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa moja badala ya kwa RC Gambo kwani RC huyo anaonekana kutumia fedha hizo kwa malengo mengine na kumtuhumu kuwa anachukua fedha zinazochangwa na kupeleka kwenye misiba ambayo ilitokea kipindi cha nyuma kama rambirambi.

Amesema wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga  jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni 56 huku akijua kabisa fedha hizo zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.

“Yani hili jambo ni la ajabu sana nimefika shuleni kutoa rambirambi na si mimi bali nimewasindikiza umoja wa shule binafsi na nikaomba viongozi wa dini wafanye sala kwaajili ya kuanza kutoa fedha hizo lakini cha ajabu nakamatwa kwa kosa gani ,na mimi nasema sitaelekeza fedha kwa RC Gambo ambazo ni za rambirambi bali zikija kupitia ofisi yangu nitazielekeza kwa wafiwa ambao wapo kwenye kila Kata,” alisema na kuongeza;

"Mimi ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu, Diwani wa Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo ana familia 6 zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu wahakikishe hizo familia zinakuwepo pale shuleni.
 
"Moja ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri wa Kanisa Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka Olasiti, kabla ya zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa Polisi walivamia.

"Maswali tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa mkoa? nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali aliyefariki, walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa na Wananchi wangu"

Naye  Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu na wakati Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya hatafika mbali.

Awali jana Mei 19, 2017, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati akipokea msaada uliochangwa na wananchi kupitia tovuti ya  wezesha sasa ambapo alipokea msaada wa takriban shilingi milioni 4 alisisitiza kuwa wanasiasa waache kutumia msiba kwa kuingiza siasa kwani hakuna fedha yoyote ile iliyoliwa na pia wapo katika harakati za kuwatumia fedha wazazi pamoja na timu ya wataalam wa afya walioongozana na watoto wa Lucky Vicent ambao ni majeruhi wanaotibiwa nchini Marekani kama fedha za kujikimu na kiasi kilichobaki hadi sasa ni  zaidi ya Sh, milioni 56 ambazo kunakamati ndogo ya wazazi iliyoteuliwa ambao wataamua zitumikaje kwaajili ya kumbukumbu za watoto hao.

Rais Magufuli akabidhi Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais Museveni wa Uganda

$
0
0
Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.
 
Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani.
 
“Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana.
 
Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.
“Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.
 
Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.

SBL yazindua bia mpya iitwayo Serengeti Premium Lite

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (wa kwanza kulia) akimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika hafla ya uzinduzi wa bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta pamoja na mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma wakishuhudia uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi, Mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta wakionesha bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa bia hiyo itauzwa kwa shs 1500/-.
Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (wa kwanza kulia), Mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma (katikati) na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta wakionja bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa.
Duh...inaradha ya kuvutia eehh! Meza kuu ikifurahia mara baada ya kuonja bia hiyo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi amezinduwa bia mpya ya Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), inayojulikana kama 'Serengeti Premium Lite'.
 
Akisoma hotuba ya Waziri Mwakyembe katika uzinduzi huo, Bi. Kihimbi alisema wizara inaipongeza kampuni ya SBL kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania yaani jina la Hifadhi ya Taifa Serengeti kupitia bia yao. Alisema Bia mpya ya Serengeti Premium Lite iliyopikwa kisasa iliyozinduliwa na SBL inaendelea kulitangaza hifadhi ya Serengeti hivyo kuwataka wananchi wapenzi wa kinywaji hicho kuitumia ili kutangaza nchi.
 
“Programu za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi, watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili ya kuuza mazao yao ambapo SBL hununua mazao yao kama malighafi inayotumika kuzalishia bia,” alisema Mwakyembe.
 
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta alisema SBL, ikiwa ni mojawapo ya kampuni kubwa zinazozalisha bia hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa zaidi ya miaka 20.
 
“Bia ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia utaalamu wa kisasa wa uzalishaji bia. Ina ladha kamili inayoburudisha zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa huuzwa reja reja sokoni,” alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuia ya wanywaji wake ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta bia halisi ya Kitanzania. “Pamoja na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa biaya Serengeti Premium Lite, niseme kuwa ni bia halisi ya kitanzania yenye kiburudisho na ladha nyepesi.
 
Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa muda mrefu. Tuna amini kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishaji bia (bremasters) wa kitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapo kuwa wakifurahia urithi wetu wa aina hii ya bia”, alisema Mehta.
 
Aliongeza kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite ina ubora ule ule wa kimataifa sawa na bia mama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya medali 10 za ubora wa kitaifa na kimataifa.”

Mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma (kulia) akifurahia bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Masoko, Ceaser Mloka (wa kwanza kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia uzinduzi wa bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite'. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa SBL, Anitha Msangi  na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta.

Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (kushoto) kwenye uzinduzi rasmi wa 'Serengeti Premium Lite'.

Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (wa kwanza kulia) akigonganisha glasi na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha (kushoto) mara baada ya kuzinduliwa.

Wageni mbalimbali wakionja na kufurahia bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Wageni mbalimbali wakionja na kufurahia bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Watanzania 11 Watiwa Mbaroni Afrika Kusini Wakituhumiwa Kumbaka Mwanamke Mjamzito

$
0
0
Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii Johannesburg Afrika Kusini .

Radio na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 22 aliyekua akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri.

Mwanamke huyo alikua akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae baadae alifanikiwa kutoroka.

Baada ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu.

Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa Mwanamke huyo aliyekua kwenye hali mbaya ambapo walimpeka Hospitali huku Watuhumiwa wakichukuliwa na kupandishwa Mahakamani siku ya Jumatano.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 21

OFA: Jipatie Kitabu cha Riwaya Kali ya President Wife Toka Kwa Mwandishi Makini Eddazaria

$
0
0
OFA HII SI YA KUKOSA KWA KWELI
Nununa kitabu cha PRESIDENT WIFE kwa sh 10000 upate kitabu cha HARD DAY Bureeeeee kabisa. Kumbuka kitabu hivi hupatikana Whatsapp 0657072588 kwa mfumo wa PDF. Au email eddazariaM@gmail.com


==>"Baada ya utawala wa mzee GODWIN na MANKA kutolewa madarakani na EDDY DODWIN, adui mkubwa wa Eddy, JOHN anachukua madaraka ya Mzee Godwin na kuapa ni lazima ataamuangamiza Eddy aliye kuwa rafiki yake wa kipindi kirefu toka wakiwa sekondari. 

"Rahab anaongoza nchi huku kijana machachari Adrus akiwa mlinzi makini kuhakikisha maisha ya mke wa raisi yanakuwa salama, ila K2 na kaka yake wanajawa na uchu wa madaraka na kuhakikisha kwamba wanauangusha uongozi wa Raahab, ila Eddy anasimama kama ngao na kupigania uongozi wa Rahab je atafanikiwa"
 
Ungana nami muandishi wako Eddazaria G.Msulwa katika hadithi hii ya kusisimua
 
●Wasiliana nami 0657072588 au 0768516188 

KARIBU SANA UZIDI KUNIUNGA MKONO KWENYE KAZI YANGU YA UANDISHI

OFA: Jipatie Kitabu cha Riwaya Kali ya President Wife Toka Kwa Mwandishi Makini Eddazaria

$
0
0
OFA HII SI YA KUKOSA KWA KWELI
Nununa kitabu cha PRESIDENT WIFE kwa sh 10000 upate kitabu cha HARD DAY Bureeeeee kabisa. Kumbuka kitabu hivi hupatikana Whatsapp 0657072588 kwa mfumo wa PDF. Au email eddazariaM@gmail.com


==>"Baada ya utawala wa mzee GODWIN na MANKA kutolewa madarakani na EDDY DODWIN, adui mkubwa wa Eddy, JOHN anachukua madaraka ya Mzee Godwin na kuapa ni lazima ataamuangamiza Eddy aliye kuwa rafiki yake wa kipindi kirefu toka wakiwa sekondari. 

"Rahab anaongoza nchi huku kijana machachari Adrus akiwa mlinzi makini kuhakikisha maisha ya mke wa raisi yanakuwa salama, ila K2 na kaka yake wanajawa na uchu wa madaraka na kuhakikisha kwamba wanauangusha uongozi wa Raahab, ila Eddy anasimama kama ngao na kupigania uongozi wa Rahab je atafanikiwa"
 
Ungana nami muandishi wako Eddazaria G.Msulwa katika hadithi hii ya kusisimua
 
●Wasiliana nami 0657072588 au 0768516188 

KARIBU SANA UZIDI KUNIUNGA MKONO KWENYE KAZI YANGU YA UANDISHI

Serikali Yafafanua Kuhusu Taarifa za Kuzuia Matumizi ya Mkaa

VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli akikabidhi uenyekiti wa EAC kwa Museveni

$
0
0
Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli jumamosi ya Mei, 2o amekabidhi Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. 

Hapo chini ni video ya hotuba ya Rais Magufuli wakati akikabidhi uenyekiti kwa Rais Museveni.

Simba watibua sherehe za Ushindi wa Yanga

$
0
0
Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa Klabu ya Simba imewasilisha malalamiko ya barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga kunyang'anywa pointi 3, hatimaye uthibitisho wapatikana.

Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na kuenea kwa picha ikionyesha vielelezo hivyo, imeanza kuwakwaza mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwakejeli Simba kwa kuwaita “Wazee wa pointi za mezani”.

Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja itatangazwa kuwa bingwa.

Haya ni baadhi ya maneno aliyoandika Msemaji wa Simba aliyefungiwa, Haji Manara;....."Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa, soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA"

Halafu akaendelea;........"Hv unadhani FIFA wana figisu guys?kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu,no way out!!ukizingatia repoti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti!SHUBAMIT"

Halima Mdee Awachana Wabunge wa CCM

$
0
0
Mbunge  wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), amewatibua wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuwashangaa jinsi wanavyoisifu Serikali kutokana na kufuta tozo, kodi na ada katika sekta za uvuvi, kilimo na mifugo.

Tukio hilo lilitokea bungeni jana wakati wabunge walipokuwa wakiendelea na mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 iliyowasilishwa juzi na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba.

Katika maelezo yake, Mdee aliwaambia wabunge hao kwamba pongezi zao katika kuondoa tozo hizo hazitakiwi kutolewa kwa kuwa wakulima hawajandaliwa mazingira mazuri ya kuwanufaisha na kilimo.

Kwa mujibu wa Mdee, sekta ya kilimo nchini inayohusisha asilimia 65 ya Watanzania, imekuwa ikishuka kila mwaka badala ya kupanda.

“Nashangaa sana waziri anasimama hapa na kutumia robo tatu ya hotuba yake kueleza masuala ya tozo,” alisema na kuongeza:

“Nawashangaa pia wabunge wanaosimama na kupongeza kuondolewa kwa tozo na naamini hizi pongezi zisingekuwapo kama Serikali ingekuwa imeandaa mazingira mazuri kwa wakulima hao.

“Nimesoma bajeti ya Waziri wa Viwanda, ameeleza kuna viwanda 234 vimesajiliwa kuanza, lakini viwanda vyote viko Dar es Salaam.

“Kwa tafasiri nyingine ni kwamba wabunge wa Kanda ya Ziwa ambao wanatoka katika maeneo ya kilimo cha pamba, bajeti hii haikuwaangalia kabisa ingawa mnasimama hapa na kupongeza.

“Kwa hiyo, napenda niwashauri wabunge wa CCM ambao ni wapya katika Bunge hili, kwamba kazi yetu ni kuisaidia Serikali na tunapokuwa tunatoa pongezi za aina hii wakati tukijua hali ni mbaya, tunaharibu nchi.

“Lazima wabunge wa CCM msome ilani ya chama chenu ambayo hata mimi wa chama cha upinzani huwa naisoma ili kupata maarifa na kujua jinsi mlivyojipanga.”

Pamoja na hayo, Mdee aliishutumu Serikali kwa kushindwa kutoa taarifa ya upimaji wa ardhi nchi nzima baada ya hoja yake kuungwa mkono na Bunge mwaka 2011.

Kutokana na maneno hayo, baadhi ya wabunge wa CCM walilazimika kusimama kwa nyakati tofauti na kuomba kumpa taarifa mbunge huyo.

Aliyekuwa wa kwanza kutoa taarifa ni Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, ambaye alimkosoa kwa kusema wabunge wote ni wapya kwa kuwa walipatikana baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi.

Mwingine aliyesimama ni Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya, aliyesema kuipongeza Serikali baada ya kufuta tozo hizo ni jambo la msingi kwa sababu wabunge wanajua jinsi zilivyokuwa zikiwaumiza wakulima.

Kwa upande wake, Mbunge wa Newala, George Mkuchika, alimwambia mbunge huyo kwamba kila mbunge ana uhuru wa kupongeza katika eneo analoona kuna haja ya kufanya hivyo.

Wakati hao wakisema hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisimama na kumwomba Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, amlinde Mdee kwa kuwa anachokizungumza kinatokana na vitabu vya Serikali.

Kutokana na hali hiyo, Chenge aliwataka wabunge wasiendelee kutoa taarifa kwa kuwa mwenye jukumu la kufafanua utendaji wa Serikali ni waziri mwenye dhamana.

“Kuna utaratibu mmeuanzisha hapa wa mbunge kusimama na kuomba kutoa taarifa na anayepewa taarifa hata kama ni nzuri, anaikataa.

“Lakini eleweni kwamba anayechangia hapa ni Mdee ambaye maelezo yake yanatakiwa kujibiwa na waziri mwenye dhamana,” alisema Chenge.

Juzi Dk. Tizeba wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake, alisema Serikali imefuta tozo, kodi na ada 108 zilizokuwa kero katika sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo.

Zitto Kabwe: Kwanini Tanzania ni Masikini Miaka Zaidi ya 50 Baada ya Uhuru? Tumedharau Kilimo.

$
0
0
==> [ Hotuba ya Zitto Kabwe (Mb) kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo 2017/18 ]

Mheshimiwa Spika,
Serikali yeyote makini lazima ihangaike na masuala yanayowahusu wananchi wake walio wengi, na hapa Tanzania watu hao (walio wengi) ni Wakulima. Hivyo basi, kipimo kikuu cha kuondoa umasikini wa Watanzania ni kuondoa umasikini wa wakulima.

Sekta ya kilimo ndio msingi wa Uchumi wa watanzania. Waziri wa kilimo katika hotuba yake hapa ametuambia kuwa 65.5% ya watanzania wameajiriwa kwenye kilimo au wanategemea kilimo kwa kipato chao cha kila siku, kwamba 100% ya chakula nchi inategemewa kutoka kwenye sekta hii. Kilimo kinachangia 29.1% ya pato la taifa (GDP), karibia theluthi moja ya thamani yote ya shughuli za Uchumi nchini kwetu.

Hivyo basi, unapowekeza kwenye sekta ya kilimo unawekeza kwa theluthi mbili ya watanzania. Unapokuza kilimo unakuza uchumi wa theluthi mbili ya watanzania, na unapoacha kilimo kishuke maana yake umewafukarisha theluthi mbili ya Watanzania.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Uchumi, ili kupunguza umasikini Tanzania kwa kiwango kikubwa, sekta ya kilimo inapaswa kukua kwa asilimia zaidi ya 8% angalau kwa miaka mitatu mfululizo, na ukuaji huo uendelee kukua kwa wastani wa 6% kwa muda miaka kumi mfululizo.

Hali ikoje nchini? Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri wa Kilimo, kwa miaka hii mitatu mfululizo ukuaji wa Kilimo umekuwa ukishuka nchini (Na hivyo ukuaji zaidi wa umasikini). Mwaka 2014 sekta ya Kilimo ilikua kwa 3.4%, Mwaka 2015 Kwa 2.3% na Mwaka 2016 Kwa 2.1%.

Taarifa ya ya robo mwaka ya Benki Kuu nchini (BOT quarterly economic bulletin) inayoishia Disemba 2016 inaonyesha tofauti na anachosema Waziri. Kwa mujibu wa tarifa ya BOT ni kuwa sekta ya Kilimo ilikua kwa kasi ya 0.6% tu kutoka ukuaji wa 2.3%. 65.5% ya Watanzania wote wamejiajiri katika sekta ya Kilimo, hivyo mdororo huu ya sekta ya Kilimo kutoka ukuaji wa 2.3% mpaka ukuaji wa 0.6% ni ishara mbaya mno kwa ustawi wa zaidi ya robo tatu ya Watanzania.

Kwa Vijijini 78% ya Watanzania wanajihusisha na Kilimo. Hii maana yake ni kwamba wananchi wengi vijijini hawafanyi uzalishaji, jambo hili ni hatari sana, ni dalili kuwa ufukara wa watu wetu unazidi. Ni kwa sababu hii, pamoja na uchumi wetu kukua kitakwimu, 7% kwa mwaka, lakini bado wananchi wetu walio wengi wanaishi kwenye dimbwi la ufukara. Maana ukuaji huo wa Uchumi hauhusishi kilimo, hauhusishi zaidi ya robo 3 ya Watanzania.

Tunajenga uchumi unaowaacha pembeni theluthi 2 ya watanzania wote. Ukuaji huu mdogo wa Kilimo unapaswa kuishtua Serikali kwani ni hatari sana, ni hatari mno. Maana unajenga uchumi unaowaacha karibu zaidi ya robo 3 ya Watanzania kwenye ufukara huko vijijini, ni uchumi unaopanua matabaka ya mafukara na matajiri. Ndio msingi wa umasikini wa wananchi wetu miaka 50 baada ya Uhuru.

Tatizo hasa ni nini? Kwanini ukuaji wa kilimo unashuka na hivyo umasikini wa Watanzania kuzidi? Tatizo kubwa ni sera za Serikali pamoja na utekelezaji wake. Serikali haiwekezi vya kutosha kwenye kilimo, Na hata ikipanga mipango juu ya kilimo haitekelezi kabisa mipango husika.

Katika bajeti ya mwaka 2015/16, bajeti ya mbolea ya Ruzuku katika Wizara hii ilikuwa ni shilingi bilioni 78. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano ilishusha fedha za ruzuku ya mbolea mpaka Shilingi bilioni 10 katika mwaka wa Fedha wa 2015/16. Hii ilikuwa ishara ya dhahiri ya kukipuuza kilimo, kuwapuuza 65.5% ya Watanzania wote, kutokujali chanzo cha 100% ya chakula chote cha Watanzania, kupuuza sekta inayochangia theluthi moja ya uchumi wa Taifa.

Si hivyo tu, katika bajeti ya mwaka 2016/17, Bunge liliidhinishia Wizara hii fedha za miradi ya maendeleo katika kilimo kiasi cha bilioni 100.53. Waziri amelieleza bunge hapa kuwa mpaka Mei 4, 2017 Wizara imepokea shilingi bilioni 3.34, sawa 3.31% ya fedha zote za maendeleo ya kilimo. Jambo hili linasikitisha mno, ni jambo linaonyesha kuwa hatuwajali wanyonge wa Taifa hili.

Watanzania wanyonge walikuwa na matumaini makubwa sana na Serikali hii, Rais Magufuli alisema yeye ni rais wa wanyonge. Wanyonge nchi hii ni wakulima. Matendo ya Serikali anayoiongoza yanaonyesha tofauti, Serikali haiwajali wanyonge, inapuuza uchumi wa 65.5% ya wananchi wetu. Ni vigumu kuondoa umasikini nchini ikiwa tutaendelea kuwadharau wakulima.

Kwetu sisi ACT Wazalendo tunaofuata Ujamaa wa Kidemokrasia, Kilimo ndio sekta ya msingi, ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, ni sekta nyeti ambayo hatutaacha kuisemea. Hivyo pamoja na kuonyesha kasoro zote hizo za serikali, tutatumia pia nafasi hii kutoa njia mbadala za kuondoa kasoro hizo ili kuhakikisha uchumi wetu hauwaweki kando wananchi wetu wengi.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
Mei 20, 2017

Sumaye ajiuzulu ujumbe wa bodi CRDB kwa Madai ya Kufuatilwa sana na Serikali

$
0
0
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amejitoa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB kwa madai kuwa familia yake inafuatwafuatwa hivyo kuhofia kuwa anaweza kuathiri benki hiyo.

Baada ya kujitoa kama mmoja wa viongozi wa benki hiyo kubwa nchini, Sumaye amesema kuwa ataendelea kuwa mwanahisa wa benki hiyo ya biashara.

“Sitaki msimamo wangu wa kisiasa uhusishwe na benki yetu” alisema Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.

Sumaye alisema kuwa huenda majukumu yake ya kisiasa yakambana na akashindwa kuhudhuria baadhi ya vikao muhimu vya benki hiyo ambavyo ni muhimu kwa ufanisi na ustawi wa benki.

Akiwa nje ya mkutano huo Sumaye alisema kuwa, familia yake imekuwa ikifuatwafuatwa na serikali na kwamba tayari mtoto wake amepokwa shamba.

Serikali pia alimnyang’anya Sumaye shamba lake lililokuwa Mabwepande kwa madai hakuliendeleza, huku yeye akisema uamuzi wa yeye kupokwa shamba ulikuwa ni wa kisiasa. Sumaye alieleza kwamba hakuweza kulima shamba hilo kutokana na serikali kupiga kilimo jijini Dar es Salaam.

Sumaye amesema uamuzi wake aliuchukua ili CRDB iweze kuendeshwa na watu walioko huru mbele ya jamii kuepusha hisa za wafanyabishara wengine kuathiriwa.

Sumaye anamiliki zaidi ya hisa milioni 7.4 za benki hiyo.

Mawaziri Waliotemwa Wageuka MWIBA Kwa Serikali

$
0
0
Mawaziri  wa zamani, Nape Nnauye na Charles Kitwanga, wamegeuka kuwa mwiba kwa kutoa hoja za kukosoa utendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

Mwenendo wa makada hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuikosoa Serikali, umeanza kuibuka siku za hivi karibuni baada ya wote kwa nyakati tofauti kuenguliwa katika nafasi zao za uwaziri.

Kwa hatua yao ya sasa, wanasiasa hao wanadhihirisha ukweli kwamba wabunge wengi hushindwa kueleza matatizo ya majimbo yao pindi wanapopewa nyadhifa serikalini na wanapotenguliwa wanadai wanapata nafasi zaidi za kuwatumikia wapigakura wao.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai kuwa makada hao walikosa ujasiri wa kuikosoa Serikali walipokuwa wanashikilia nyadhifa zao kutokana na kubanwa na hoja ya uwajibikaji wa pamoja.

Nape Nnauye
Nape ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla uteuzi wake kutenguliwa Machi, mwaka huu baada ya kupokea ripoti ya tukio la kuvamiwa kwa Kituo cha Televisheni cha Clouds, amesikika mara kadhaa nje na ndani ya Bunge akiikosoa Serikali.

Akiwa jimboni kwake Mtama alikoenda kuzungumza na wapigakura wake baada ya kutenguliwa, alisema kama matukio ya kuteka watu yataachwa yaendelee, basi CCM itakuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Nape alitoa kauli hiyo wakati huo kukiwa na tukio la kutekwa kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki.

Wakati akichangia hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wiki iliyopita, Nape alisema kuwa kama CCM isipotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kutowapatia maji wananchi, inaweza kuondoka madarakani.

Kauli nyingine ya Nape aliitoa wiki hii alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, aliposema kuwa wananchi wa mikoa ya Kusini hawatakubali kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana na kile alichodai vita iliyopo kati ya mataifa makubwa.

Aliitaka Serikali isikubali kuona vita hiyo inaendelea kuwaumiza wananchi hao na kuongeza kuwa kama itashindwa kusimamia, wao hawatakubali.

Pia kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii wa twitter, Nape, amekuwa akiandika baadhi ya kauli zenye mwelekeo wa kuikosoa Serikali

Charles Kitwanga
Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alianza kuikosoa Serikali baada ya kutenguliwa mwaka jana, kutokana na ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya Bombardier kutoka Canada ili kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Alisema ndege hizo, si tu hazina mwendo, lakini pia ilikuwa ni ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia.

Kitwanga aliibuka tena wiki iliyopita wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Lwenge kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, akisema atawahamasisha wapigakura wake wakazime mtambo ulioko katika chanzo cha maji cha Iherere.

Alisema jimboni kwake hakuna maji ya uhakika na tangu mwaka 2008 wananchi wamekuwa wakiyasubiri bila mafanikio.

“Kwa hiyo, nitakachokifanya safari hii, sitatoa shilingi kwenye bajeti, bali nitakwenda kuwahamasisha wananchi wa Misungwi wapatao 10,000, twende tukazime mtambo katika kile chanzo cha maji ili wote tukose.

 “Mshukuru nilipokuwa waziri nilikuwa siwezi kusema kitu, sasa nimetoka, tutapambana kwa sababu lazima tuwe na mipango mizuri ya kuwapelekea wananchi wetu maji kama inavyofanyika katika umeme kupitia REA (Wakala wa Umeme Vijijini),” alisema.

Kauli hiyo iliibua hasira za Waziri Lwenge wakati akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, ambaye aliita kuwa ni sawa na uasi.

Kutokana na kauli hiyo, alimtaka ahame chama kama haoni jitihada za kupeleka maji jimboni kwake zinazofanywa na Serikali.

“Kitwanga anaposema atakwenda kuhamasisha wananchi wakabomoe mtambo wa Iherere maana yake analeta uasi au hathamini kazi iliyofanywa na chama chake?

“Kama ni hivyo, sasa ajitoe kwenye chama kwa sababu Serikali imepeleka fedha na kwa maendeleo yaliyofanyika, ni lazima tuwahamasishe wananchi kutunza miundombinu iliyopo badala ya kwenda kuibomoa.’ alisema.

Khamis Kagasheki
Mbali na kina Kitwanga, baadhi ya waliokuwa mawaziri katika Serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete nao pia wamegeuka kuwa wakosoaji wa Serikali.

Mmojawapo ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, anayeikosoa Serikali kupitia akaunti yake ya twitter.

Kagasheki aliyeangushwa katika ubunge wa Bukoba Mjini na mpinzani wake wa siku nyingi, Wilfred Lwakatare (Chadema), aliwahi kusema kuwa kama nguvu ya Ukawa ingemchagua mgombea makini, basi CCM ingekuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi.

Kada huyo wa CCM aliyejiuzulu nafasi yake kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza, aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa twitter: “Kuikosoa Serikali yoyote ile ni jambo la kawaida. Ni vema kuchagua maneno na kulenga hoja bila matusi.”

Philip Mulugo
Naye Philip Mulugo aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati wa utawala wa Kikwete, pia amekuwa akiikosoa Serikali ya Magufuli.

Mulugo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Songwe, amesikika bungeni wiki iliyopita akiikosoa Serikali alipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.

Akichangia bajeti hiyo, Mulugo aliishangaa Serikali kuruhusu vitabu vyenye makosa vitumike shuleni wakati kuna uwezekano wa kuviondoa.

Katika maelezo yake, Mulugo alivitaja vitabu vya jiografia vya kidato cha tatu na kiingereza kidato cha nne, kuwa vina makosa yanayoweza kuharibu misingi ya wanafunzi.

“Haiwezekani mbili mara mbili mtu aseme ni sita wakati sisi tunajua ni nne. Kwa hiyo, hili suala la vitabu mliangalie vizuri kwa sababu haliko vizuri,” alisema Mulugo.

Pamoja na hayo, Mulugo alizungumzia michango inayotozwa na Serikali katika shule binafsi na kusema ni mingi na kwamba inatakiwa kupunguzwa kwa kuwa inawakatisha tamaa wamiliki wa shule hizo.

Kutana na Mtaalamu wa NYOTA Akusaidie.....Huzuia Chuma Ulete, Anatoa Pete za Bahati Nasibu, Anatafsri Nyota na Atakupa Jini la Mali

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. 

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
 
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.

Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. PIA ANATOA POCHI YA MAAJABU ISIO ISHA HELA( Magic Wallet)..Nguvu za KIUME,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidiWhatsapp +255 674 835107 -calls +255746757102
 
Pia Anatibu kwa Njia ya simu popote Pale Ulipo..

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Yahitimisha rasmi zoezi la kupokea rambirambi.....Yatangaza kuhamishia nguvu kwa Majeruhi wanaotibiwa Marekani.

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAPATO NA MATUMIZI YA MSIBA WA AJALI YA LUCKY VINCENT MKOANI ARUSHA
TAREHE 21 MAY 2017
Mnamo tarehe 19 May 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ilitoa taarifa ya mapato na matumizi kuhusu michango ya Rambirambi ya ajali ya basi ya shule ya Lucky Vincent iliyotokea Wilayani Karatu eneo la Rhotia. Ajali hiyo ilitupotezea wapendwa wetu 35, wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1.

Aidha, ajali hiyo pia ilitubakishia Majeruhi 3 ambao hali zao zilikuwa ni mbaya sana. Tunaamini Mwenyezi Mungu ana makusudio yake kuwaacha hai hawa Majeruhi 3 kwenye ajali mbaya kama ile.

Baada ya Serikali na wadau mbalimbali nchini kushilikiana kufanikisha kuihifadhi miili ya wapendwa wetu ikiwa ni pamoja na kutoa fedha taslimu za rambirambi kiasi cha shilingi 3,857,000 kwa kila familia iliyofiwa kwa familia zote 35. Kwa ujumla tumeona ni vema sasa nguvu kubwa ikapelekwa kwenye kuwahudumia majeruhi ili waweze kupona na makusudio ya Mungu yaweze kutimia.

Tunapenda kuujulisha Umma kuwa hadi Ijumaa ya tarehe 20 May 2017 kutokana na wadau kuendelea kuchangia tumebakiwa na kiasi cha Shilingi 67,993,885. Kwa mantiki hiyo busara imeelekeza kuwa nguvu kubwa sasa ipelekwe kwenye kuwahudumia majeruhi, maana hata tufanyeje kwa wale ambao Mungu kwa mapenzi yake amewachukua hatuna namna tena ya kuwarudisha.

Hivyo, tunapenda kuujulisha Umma kuwa Jumatatu tarehe 22 May 2017 tutazitumia familia za majeruhi pamoja na Madaktari wetu waliojitoa kuwasindikiza majeruhi kiasi cha Dola za kimarekani 20,000 (Sawa na 44,720,000 kwa Exchange rate ya 2,236 , kila familia itapata Dola 5,000 (Jumla ni Dola 15,000 kwa familia 3), Daktari Dola 2,500 na muuguzi Dola 2,500 kama sehemu ya kuendelea kuwafariji na kuwapunguzia changamoto huko ugenini.

Kwa ujumla baada ya yote hayo tutabakiwa na kiasi cha shiliingi 23,273,885 huku tukiendelea kuangalia hali za majeruhi wetu. Kiasi cha fedha kilichobaki kitaendelea kuwekewa utaratibu kupitia timu ya wafiwa 4 walioteuliwa na wafiwa wenzao kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha mapato na matumizi ya suala hili yanaeleweka vema kwa Umma.

Pia tunapenda kuuhabarisha Umma kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imehitimisha rasmi zoezi zima la kupokea rambirambi ili ipate muda zaidi wa kufuatilia Mustakabali wa Majeruhi wetu walioko haspitalini nchini Marekani.

Imetolewa na:
Mrisho Mashaka Gambo
Mkuu wa Mkoa Arusha

TFDA yakanusha soda ya Novida kuwa na virusi vya Ebola

$
0
0
Mamlaka ya Chakula na madawa (TFDA) imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa kwa nyakati tofauti kwenye mitandao ya kijamii  kuwa kuna soda aina ya ‘Novida’ kutoka nchini Nigeria zimeingizwa nchini kinyemela na zina sumu ya virusi vya Ebola na tayari zimesababisha vifo vya watu 180 nchini humo.

Taarifa ya Mamlaka hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni mwendelezo wa taarifa yake ya awali iliyotolewa mwezi Aprili 2017 inabainisha kuwa taarifa zinazosambazwa za kuingizwa soda zenye sumu ya Ebola haina ukweli na inapaswa kupuuzwa.

Kwenye taarifa hiyo, TFDA imeeleza kuwa inatambua uwepo wa soda ziitwazo Schweppes Novida zinazozalishwa na viwanda vya Coca-Cola Kwanza,Bonite na Nyanza Bottlers na soda hizo zinazalishwa kwa kuzingatia mifumo bora ya uzalishaji na zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.

‘’Kama  ilivyo kwa bidhaa nyingize za chakula,vipodozi,vifaa vya tiba na vitendashi,soda za  Schweppes Novida ambazo zimesajiliwa na TFDA zimekuwa zikifuatiliwa katika soko kupitia mifumo liyopo ya udhibiti ili kujiridhisha kuwa zinaendelea kukidhi vigezo vya usalama na ubora kwa lengo la kulinda afya ya mlaji’’inabainisha sehemu ya taarifa ya TFDA .

Soda aina ya Schweppes Novida  kwa hapa nchini ilizinduliwa mwaka 2013, inatengenezwa na kusambazwa na viwanda vya Coca-Cola vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.Soda hizi zinazopendwa na wateja zinatengenezwa kwa ujazo wa ml 300 na ml 500 zipo za aina ya Mandarin Cooler zenye ladha murua ya machenza na Pineapple Breeze zenye ladha ya Nanasi.

Timu ya Ruvu Shooting Yapata Ajali

$
0
0
Msafara wa Timu ya Ruvu Shooting Umepata Ajali mbele Kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea Dar es Salaam.

Ruvu Shooting walikuwa njiani wakiokea Shinyanga walipocheza mchezo wao wa kumalizia msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Stand United  

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wachezaji waliokuwapo zinasema kwamba gari  hilo likiwa katika Mwendo, tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama Njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.
 
Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata Majeraha ya kawaida.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images