Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Salma Kikwete Awagawa Wabunge Bungeni

$
0
0
Mchango wa Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Salma Kikwete kuhusu kupinga wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo jana ulizua gumzo bungeni kutokana na wabunge kugawanywa na suala hilo.

Hali hiyo ilijitokeza wakati wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha 2017/18 bungeni jana.

Salma amesema anapinga suala la watoto wanaopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo kutokana na mila, desturi, dini na mazingira.

Ameitaka Serikali kutafuta njia nyingine ya watoto hao kupata elimu badala ya kuwaruhusu kuendelea na masomo.

Akitoa taarifa yake kwa mchangiaji Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy alitaka mbunge yeyote ndani ya Bunge ambaye alianza kushiriki mapenzi akiwa shuleni atoe ushuhuda bungeni kama aliweza kuendelea vizuri kimasomo.

Amesema anaunga mkono wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo

Ofisa wa Polisi mwingine auawa Kinyere

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni 
 **
Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala.
 
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni zinasema aliuawa nyumbani kwake. Hata hivyo hakumtaja jina lake.
 
Taarifa zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni.
 
Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye.
 
“Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi tutawapa taarifa baadaye,” alisema.

VIDEO: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 16, 2017

$
0
0
Fuatilia hapa matangazo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma leo Mei 16, 2017, kipindi cha maswali na majibu . 

==>Bofya hapO chini kutazama.

Breaking: Mkuu wa Mkoa Meck Sadiki na Majaji wawili Waandika barua kuacha kazi .......Rais Magufuli Aridhia

$
0
0
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi wafuatao;

1. Ndg. Saidi Meck Sadiki - Aliyekuwa mkuu Wa Mkoa wa Kilimanjaro.

2. Ndg. Aloysius Kibuuka Mujulizi - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

3. Ndg. Upendo Hillary Msuya - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi hao kuanzia tarehe 15 Mei, 2017.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam 
16 Mei, 2017

Maajabu Jijini Mwanza: Mti Wagoma Kung'olewa......Ilikuwa Kila Ukikatwa Unalia Kwa Sauti Kupinga Kung'olewa

$
0
0
Wakazi wa Barabara ya Iloganzala  Jijini Mwanza jana walipigwa butwaa baada ya mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using'olewe. 

Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu. 

Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza. 

Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe  leo imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu

==>Tazama Video hapo chini

Naibu Waziri aliyetishiwa na bunduki jana afikishwa Mahakamani Kisutu

$
0
0
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, na Mbunge wa Mkuranga, Adam Kighoma Ali Malima amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo akituhumiwa kumzuia Polisi kutekeleza majukumu yake.

Malima anatuhumiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2017 eneo la Masaki karibu na Ubalozi wa Canada jijini Dar es Salaam jana majira ya saa sita mchana, ambapo Polisi walikuta ameegesha gari lake sehemu isiyotakuwa na alipotakiwa kulipeleka ‘yard’ alikataa.

Polisi hao walikuwa wameambatana na maofisa wa kampuni moja ambayo ni wakala wa kukusanya madeni, kukamata teksi bubu pamoja na kukamata magari ambayo yanaegeshwa sehemu ambayo si sahihi kisheria.

Licha ya Malima kuelezwa ukweli kuwa hakuwa ameegesha gari sehemu sahihi, lakini alikataa kulipeleka alikoambiwa jambo lililoibua mtafaruku mkubwa.

Baada ya kufikishwa mahakani yeye na dereva wake, wameachiwa kwa dhamana ya TZS milioni 5.

Rais Magufuli Atembelea Shirika La Utangazaji La Taifa - TBC

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake kutajwa alieleza kuwa, Rais Magufuli aliwasili kituoni hapo majira ya saa 5 asubuhi, na miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusikiliza changamoto zinazowakumba wafanyakazi wa shirika hilo.

“Rais alitembelea hapa majira ya asubuhi na alizungumza na wafanyakazi wa TBC. Ujio wake ulikuwa ni kwa lengo la kujua hasa changamoto tunazokabiliana nazo katika eneo letu la kazi,” kilisema chanzo hicho.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 17


Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano Halotel ahukumiwa kulipa milioni 700 kwa Uhujumu Uchumi

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewatia hatiani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya Viettel inayofanya biashara kama Halotel, Do Hong na wenzake wanane, kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuwataka kulipa faini ya zaidi ya Sh. milioni 700.

Hata hivyo, Hong ameachiwa huru baada ya kulipa Sh milioni 479 ambazo kati yake, sh milioni 20 ni faini na sh milioni 459 ni fidia ya hasara anayodaiwa kuitia Serikali. 

Wenzake wamekwenda jela kwa kutolipa. Mbali ya Hong, washitakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob (47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess (48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan, Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka na Viettel Tanzania Limited (Halotel) iliyoshitakiwa pia.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri alitoa hukumu hiyo jana baada ya washitakiwa hao kukiri makosa yao baada ya kusomewa upya mashitaka saba badala ya 10 waliyokuwa wameshitakiwa nayo kwa maelezo ya awali. 

Mashitaka waliyoshitakiwa nayo katika kesi hiyo ni kula njama kutenda kosa, kughushi na kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa. Hakimu Mashauri alisema katika kila kosa mshitakiwa atatakiwa kulipa Sh milioni tano na wanatakiwa kurudisha hasara yote walioisababishia serikali, ya Sh milioni 459.

“Washitakiwa hawa wamekuja kuwekeza nchini na lengo sio kuhujumu uchumi na miundombinu yetu. Ili iwe fundisho kwa wawekezaji wengine na kuonesha kwamba Tanzania ipo makini katika masuala haya, kila mshitakiwa atatakiwa kulipa Sh milioni tano na kuilipa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) fedha walizohujumu,” alisema Hakimu Mashauri katika hukumu. 

Pia Hakimu huyo aliagiza vifaa vyote walivyokutwa navyo washitakiwa wakifanyia biashara, vitaifishwe na serikali na akasema wanayo haki ya kukata rufaa Mahakama Kuu kuhusiana na adhabu pekee.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu, Wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia, alidai hawana kumbukumbu ya makosa ya zamani ya washitakiwa hivyo mahakama iwape adhabu inayostahili kulingana na makosa. 

Katika mashitaka yao, inadaiwa kuwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017, Jijini Dar es Salaam, walitengenezamfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila kibali cha TCRA. Pia wanadaiwa katika kipindi hicho waliendesha hiyo mifumo ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila ya leseni.

Inadaiwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na leseni ambapo katika tarehe isiyofahamika Novemba 2016, walisimika vifaa hivyo ikiwamo sim box yenye namba ya siri 1152000.8.n.t.n na Laptop mbili aina ya Dell bila ya kuwa na kibali cha TCRA. 

Katika kipindi hicho, washtakiwa hao wanadaiwa kuunganisha vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA itakavyo sheria.

Viettel Tanzania Limited (Halotel) na Do Hong, wanadaiwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni, walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kusajili laini za simu 1,000. Pia inadaiwa washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia hasara TCRA na serikali ya Tanzania ya Sh 459,000,000.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 17, 2017

$
0
0
Fuatilia hapa matangazo hayo moja kwa moja ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma leo Mei 17, 2017, kipindi cha maswali na majibu. 

==>Bofya hapo  chini  kutazama

Rais Magufuli aitaka TBC itangaze bila kubagua vyama, dini, kabila

$
0
0
Rais John Magufuli amelitaka shirika la utangazaji la TBC, kutoa taarifa sahihi kwa watanzania bila kujali vyama vyao, dini zao wala makabila yao.

Pia Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na MichezoHarrison Mwakyembe aliyekuwepo katika ziara hiyo kuuangalia mkataba kati ya TBC na Star Times na kuchukua hatua zinazostahili endapo itabainika kuwa mkataba huo hauna manufaa.

Magufuli ameyasema hayo   jana  alipotembelea ofisi za Shirika hilo na kuwataka wafanyakazi wa TBC kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na ubunifu wa hali ya juu ili matangazo ya chombo hicho cha Taifa yawavutie Watanzania wengi, na kiwe chombo kinachoongoza nchini.

Magufuli ambaye hivi karibuni ametoa Sh3bilioni kwa ajili ya kuisaidia TBC amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dk Ayub Rioba kutumia fedha hizo kutatua matatizo ya uhaba na uchakavu wa vifaa vya uzalishaji wa vipindi na urushaji wa matangazo, kununua vyombo vya usafiri na kufanya ukarabati wa majengo.

Kuhusu maslahi ya wafanyakazi amewahakikishia kuwa Serikali itaboresha stahili zao kwa mujibu wa utaratibu uliopo na papohapo amemuagiza Dkt. Rioba kulipa mara moja malimbikizo ya posho zote ambazo wafanyakazi hao wanadai kuanzia Oktoba 2016, zilizofikia Sh3.2bilioni.

 “Msemaji wa Serikali mkubwa ni TBC1 na Redio ya Taifa, nyinyi hamuwezi mkawa kama vyombo vingine ambavyo vina malengo yao ya kufanya biashara, nyinyi kazi yenu ni kutoa taarifa sahihi kwa Watanzania bila kubagua vyama vyao, bila kubagua dini zao, bila kubagua makabila yao, huo ndio uwe msimamo mkuu.

“Mmetoa mchango mkubwa sana kwenye Taifa hili, hilo ni lazima niseme,  hata vipindi vyenu ukiviangalia ni vizuri vinaeleza mpaka maisha ya vijijini, na mimi ni shabiki mkubwa sana wa TBC, lakini tatizo lenu mnashindwa kwenda na wakati wa sasa.” amesisitiza Rais 

Upinzani Kenya Yatishia Kususia Uchaguzi Mkuu

$
0
0
Mzozo mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, na vinara wa mrengo wa upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za Urais.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ‘IEBC’ imeijibu mrengo wa upinzani wa NASA kufuatia vitisho vyake vya kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itafaulu kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani dhidi ya uamuzi wa mahakama ulioruhusu matokeo ya kura za Urais kutangazwa katika kituo cha kupigia kura.

Hii ni baada ya viongozi wa upinzani kuishauri IEBC dhidi ya kusaka njia za kubadili mipango hiyo ili kutangaza matokeo ya kura za Urais katika kituo cha kitaifa jinsi ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.

Tume hiyo kupita mwenyekiti wake Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitobadili msimamo wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani kuheshimu mahakama na kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.

Viongozi wa mrengo wa upinzani wakiongozwa na Mgombea wa Urais, Raila Odinga, walitishia kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu matokeo ya Urais kutoka kila kituo kutangazwa kitaifa.

Taifa la Kenya linatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais baadaye mwaka huu huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania kiti hicho kupitia mrengo wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba bendera ya mrengo wa Upinzani wa NASA.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Said Mecki Sadiki Ataja Sababu Zilizomfanya Aandike Barua Ya Kuacha Kazi ya Ukuu wa Mkoa

$
0
0
Aliyekuwa  Muu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki , amesema ameamua kuondoka serikalini baada ya utumishi wa muda mrefu na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki.

Aidha Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana wadogo wamsaidie Rais Dk John Pombe Magufuli kulingana na kasi yake kwani yeye ameepuka kumkwaza rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa mkoa. 

“Uamuzi huu wa kupumzika nilimuomba rais kwa muda mrefu sana, na nikirudi kijijini nitaendelea na ufugaji Samaki maana nilishaandaa bwawa la kufugia, nitaendelea nalo huku nikiwaza jambo lingine la kufanya,” alisema.

Sadiki alisema hayo jana wakati akitaja sababu zilizochangia kumuomba Rais Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro. 

“Namshukuru rais kuridhia ombi langu, nimetumikia serikali tangu mwaka 1999 nikiwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ninapoondoka mwenyewe... nimeona ni wakati muafaka kumweleza aliyeniteua kuwa nahitaji kupumzika nikiwa na akili timamu na afya njema,” alisema.

Alisema Sababu nyingine kubwa ni kuhofia afya yake kutomudu kasi ya rais Magufuli, kwani alifanywa upasuaji mwaka 2012 na 2014 nchini India ingawa hakutaka kuweka wazi maradhi yaliyokuwa yakimkabili. 

“Kama kiongozi muungwana lazma ifike mahali ukiri kwamba wapo vijana wenye uwezo mzuri na kasi ambayo inaendana na serikali ya awamu ya tano... mimi nilishatekeleza wajibu wangu na mchango kwa serikali yangu, sasa inatosha, tupate mawazo na michango ya wengine,” alisema.

Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016 alipoteuliwa na Rais Magufuli, alisema siyo vibaya kwa kiongozi kujitathmini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji kazi imeanza kupungua. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, mkuu wa mkoa Sadiki pamoja na aliyekuwa jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebeisha Sheria Tanzania, Aloysius Mujulizi na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Upendo Msuya waliomba kuacha kazi na rais akaridhia

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 18


Rais Magufuli Ateua Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kabla ya Uteuzi huo Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.

Bw. Clifford Tandari anachukua nafasi ya Dkt. John Ndunguru ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Clifford Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


TANZIA: Dogo Mfaume Hatunaye Tena

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.

Dogo Mfaume  alitumbukia kwenye janga la madawa ya kulevya na baadaye kuanza kupata matibabu ya kuondokana na matumizi ya madawa hayo kupitia kituo cha "Back to Life Sober House" kinachoendeshwa na  Pilli Missana kilichopo Kigamboni Dar es Salaam.

Mungu amlaze mahali pema peponi Dogo Mfaume. 

Jikumbushe na moja ya kazi yake hapo chini

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kupunguza tumbo, Kuongeza nguvu za Kiume na Mvi

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETIC ni kampuni inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote bidhaa zetu zote zimetengenezwa Kwa mimea na matunda
 
🍉🍓🍇🍅🍊🍒🍍🌴🍐🧀🧀🧀🧀🍅🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍐🍍🌳🍏🍐🌶🍉🍆🍆🍒.
Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi.
1. YODI PILLS _ Ni vidonge vya kuongeza hips na makalio @170,000/=
 
2. BOTCHO CREAM_ Ni dawa ya kupaka ya kuongeza shepu (hips na makalio) @150,000/=
 
3. BOTCHO MULT PLUS_ Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza shepu (hips makalio na mapaja) @200,000/=
4. PANNAMAS BREAST_ Ni dawa ya kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walio nyonyesha. Inapatikana kwa Tsh @120,000/=
 
5. DISCREET_Hii ni kwa ajili ya kuondoa mvi milele na zisiludi tena. @120,000/=
 
6. BODY BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza mwili mzima na kukupa hamu ya kula vizuri. Inapatikana kwa Tsh @130,000/=
 
7. LEG BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza miguu kuwa (Chupa ya bia) @120,000/=
 
8. HAIR GROWTH STIMULATOR_ Ni mafuta ya kulefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo. Yanapatikana kwa Tsh @100,000/=
 
9. MICRO COMPUTER_ Ni mkanda wa kupunguza tumbo na manyama uzembe. @170,000/=
 
10.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu. 
 
11.MEN GELY YA KUPAKA. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=.  
 
12. SHARK POWER. Hii pia ni kwa ajili ya kuongeza maumbile  wastani wa inch 7.5 inapatikana kwa @135,000/=.
 
15. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana master blashion. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa inapatikana kwa @130,000/=
🌳🍉🍌🍅🍍🍐🍓🍆🍐🍒🍒🍓🍓🍑🍍🍍🍓🍓🍓🍍🍐🍐🍈🍉
         Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani. 
 
Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
 
                 Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
 
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu

Kiongozi CCM auawa Kwa Kupigwa Risasi Kibiti

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne Iddy Kirungi liliopo katika kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wilayani  Kibiti ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwake.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo.

Amesema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia.

Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.

Mganga wa zamu katika kituo cha afya Ikwiriri, Dk Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.

Alisema majeruhi huyo walimpatia rufaa kwenda Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana.

Mtuhumiwa Aliyetoroka akiwa chini ya ulinzi atupwa jela mwaka mmoja

$
0
0
Mahakama ya Mwanzo Kinondoni,  imemhukumu  Allen Robert (33) kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutoroka akiwa chini ya ulinzi mahakamani.

Mtuhumiwa  huyo anayekabiliwa na kesi ya kujaribu kubaka alitoroka akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza mara baada ya kutoka kusikiliza ushahidi wa kesi  inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Hukumu hiyo imesomwa  na Hakimu Marko Mochiwa baada ya askari magereza mwenye namba B.4296 Koplo John Chale kutoa maelezo ya jinsi Robert alivyotoroka na kukimbia.

Hakimu Mochiwa ametoa hukumu hiyo baada ya kupitia maelezo ya mlalamikaji ambapo amesema kitendo  cha kukimbia akiwa chini ya ulinzi ni kinyume kwa mujibu wa sheria za Jamhuri.

Katika utetezi wake mtuhumiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana kesi nyingine inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Awali mwendesha mashtaka wa polisi alimsomea hati ya mashtaka mtuhumiwa huyo na kudai kuwa wakati alipokuwa akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni baada ya kutoka kwenye kesi ya kubaka akielekea katika chumba cha mahabusu ghafla alitoroka na kukimbia.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images