Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Unataka kuongeza mwili au unene? Unataka kutengeneza shape ya mwili wako kwa kutumia lishe asilia ? Kama jibu ni ndio basi BOFYA HAPA.

$
0
0

Je ! Unataka  kuongeza  mwili  au  unene?  Unataka  kutengeneza  shape  ya  mwili  wako  kwa  kutumia  lishe  asilia  bila  kulazimika  kutumia  madawa  yenye  kemikali ? Kama  jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako.
 
Neema  Herbalist  &  Nutritional  Foods  Clinic  ni  kituo  cha  tiba  asilia  na  vyakula-lishe. Tunapenda  kuwafahamisha  wateja  wetu  kuwa  tunayo   lishe  asilia  INAYO  SAIDIA  KUONGEZA  SHAPE  YA  MWILI NA  KUNENEPESHA  MWILI ..
 
Pia  inasaidia  kun’garisha ,  kunawirisha  na  kupendezesha  mwili. Lishe   hii  inatengengenezwa  kwa  mimea , haina  kemikali  yoyote  ( pure  herbal)  na  haina side  effects  kwa  mtumiaji.
 
Tunapatikana  jijini  Dar  Es  salaam  katika  eneo  la  Changanyikeni  karibu  na  Chuo  Cha  Takwimu  mbele  ya  Chuo  Kikuu Cha   Dar  Es  salaam.

BEI  YAKE  NI  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU    ( Tshs.50,000/=)
Kufika  ofisini  kwetu  panda  daladala  za  Ubungo-Changanyikeni  kisha  shuka  kituo  cha  Takwimu  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  na  utazame  upande  wako  wa  kushoto, utaziona  ofisi  zetu.
 
Kwa  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  watapelekewa   mahali  walipo  na  kwa  wateja  wa  mikoani  watatumiwa   kwa  njia  ya  mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  Meli  na  kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi  wanatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  DHL  au  POSTA.
 
Pia  tunavyo  vipodozi  mbalimbali  vya  asilia  visivyo  na  kemikali  yoyote vinavyo  saidia  kurefusha nywele  na  kuzifanya  kuwa  zenye  afya  pamoja  na  kuondoa  chunusi  na  mabaka ya  usoni  na  kuufanya  uso  uwe  soft.
 
Kwa  maelezo  zaidi, wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766538384.

Kwa  taarifa   zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tembelea 

AUDIO: Mchungaji akamatwa baada ya kuoa mke wa muumini wake

$
0
0
Mchungaji wa kanisa la huduma katika roho wilayani Karagwe, Jafece Josephat anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kumuoa mke wa muumini wake na kuanza kuishi naye kama mke na mume akidai ameoteshwa na Mungu.

Mchungaji huyo amekamatwa jana baada ya kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya amani na maadili  ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Mheruka kufika kanisani hapo na kupata ukweli juu ya jambo hilo baada ya pande zote akiwemo mchungaji wa kanisa Josephat, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Domina Damian na mme wake wa mwanzo Donath Appolo kueleza ukweli jinsi walivyooteshwa mpaka hatua ya mke kuolewa.
==>Mkuu wa Wilaya Akimhoji Mchungaji
==>Mkuu wa Wilaya akimhoji mume wa huyo mwanamke
==>Huyu ndo mke wa mtu alieolewa na mchungaji

Mheruka alitoa agizo la kukamatwa kwa mchungaji huyo  kutokana na baba wa Appolo aliyenyang'anywa mke kujitokeza mbele ya kanisa hilo na kudai mahari aliyomtolea mtoto wake irudishwe kwani hawezi kuutolea mahari ukoo mwingine kwa kuwa mke ameshaolewa na mme mwingine.
 
"Kwa kuwa, mke ameacha familia yake akaja kuolewa na wewe mchungaji amezini na kwa kuwa wewe unayejiita mchungaji umeiacha familia yako ya watoto watano ukaoa mke mwingine nyote mnazini kwani kinachotenganisha ndoa ya mke na mme ni kifo lakini nyie mmejichukulia maamuzi yenu binafsi,"amesema Mheruka.
 
Mheruka amemwagiza mwangalizi wa kanisa hilo kuendelea kutoa huduma katika kanisa hilo ndani ya miezi sita huku akitafuta utaratibu wa mchungaji mwingine mwenye maadili mema na kuwa wao kama Serikali watachunguza vizuri kama kanisa hilo limesajiliwa au halijasajiliwa  ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

==>Msikilize hapo chini Mkuu wa Wilaya akimuhoji Mchungaji, mume wa huyo mwanamke na kisha huyo mwanamke

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 9, 2017

$
0
0
Fuatilia hapa matangazo hayo moja kwa moja ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma katika Mkutano wa saba, kikao cha 20  leo Mei 9, 2017. 

==> Bofya hapo chini kusikiliza

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Kwa Mwezi Aprili Haujaongezeka Umebaki Asilimia 6.4

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Sensa za watu na takwimu wa Ofis ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji ilivyokuwa mwaka ulioisha.

Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka 1o2 mwezi April 2016.

"Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi marchi 2017 kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,"alisema

Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi.

Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.

Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Machi.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa thamani ya shilingi, Kwesigabo alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92 na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania Kuanzia Kesho Tarehe 10

$
0
0
1. UTANGULIZI
(i) Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob Gedleyihlekisa Zuma anatarajiwa kufanya Ziara ya Kitaifa ya siku tatu hapa nchini, kuanzia tarehe 10 hadi12 Mei 2017, kwa mwaliko wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(ii) Ziara hii inafanyika baada ya Mheshimiwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Rais Zuma kukutana mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

(iii) Mheshimiwa Rais Zuma anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 10 Mei 2017, jioni na kupokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Magufuli.

(iv) Ziara hii itatoa fursa kwa Viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili, ya kikanda na kimataifa pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara. Ujio wa Mheshimiwa Rais Zuma ni fursa nzuri sana ya kuendelea kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano mazuri naya kihistoria kati ya nchi zetu mbili.

(v) Mheshimiwa Rais Zuma anafuatana pia na wafanyabiashara takribani 80. Hii ni fursa muhimu sana katika kukuza mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Hivyo, tarehe 11 Mei 2017, kutakuwepo na Kongamano la Wafanyabiashara katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JINCC).

(vi) Ziara ya Mheshimiwa Rais Zuma inaenda sambamba na vikao vya Tume ya Pamoja ya Marais (Bi-National Commission - BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Mkutano wa Marais umepangwa kufanyika tarehe 11 Mei, 2017. Mkutano huo utatanguliwa na Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 10 Mei, 2017 na kikao cha Makatibu Wakuu kitafanyika tarehe 8 na 9 Mei, 2017.

2.0. RATIBA

(i) Wakati wa ziara hiyo, tarehe 11 Mei 2017, Mheshimiwa Rais Zuma atakutana na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Magufuli kwa mazungumzo ya faragha kabla ya kushiriki mazungumzo rasmi yatakayowahusisha wajumbe wa pande mbili.

(ii) Aidha, Viongozi hao watashuhudia uwekwaji saini wa Mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali ya ushirikiano.

(iii) Siku hiyo hiyo, Mheshimiwa Rais Zuma atashiriki chakula cha mchana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini katika Hoteli ya Hyatt Regency. Pia, Mheshimiwa Rais Zuma na Mheshimiwa Rais Magufuli watashiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini litakalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

(iv) Aidha, jioni ya siku hiyo, Mheshimiwa Rais Zumana ujumbe wake watashiriki Dhifa ya Kitaifa ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima yake na Mheshimiwa Rais Magufuli.

(v) Tarehe 12 Mei 2017, Mheshimiwa Rais Zuma anarajiwa kufungua rasmi Jengo jipya la Ubalozi wa Afrika Kusini nchini pamoja na kutembelea Taasisi ya Matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

(vi) Mheshimiwa Rais Zuma na ujumbe wake wataondoka siku hiyohiyo kurejea Afrika Kusini.

3.0. MAHUSIANO BAINA YA TANZANIA‎ NA AFRIKA KUSINI

(i) Mahusiano ya Tanzania na Afrika Kusini ni mazuri na ni ya muda mrefu tangu wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini zilizoongozwa na Chama kikongwe cha African National Congress (ANC). Nchi hizi mbili zimeendelea kushirikiana kwa karibu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kikanda na hasa ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika. Kwa sasa, Afrika Kusini ni Mwenyekiti wa SADC na Tanzania ni Mweyekiti wa SADC Organ, hatua inayotoa nafasi ya kushirikiana zaidi.

(ii) Aidha, ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini umekuwa ukiimarika kila mara kwa Viongozi wakuu kutembeleana na viongozi wa ngazi za juu Serikalini kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi zetu mbili. Kama mtakumbuka Julai 2011, Mhe. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alifanya Ziara ya Kiserikali nchini Afrika Kusini ambayo ndiyo iliyozaa Mkataba wa Ushirikiano wa Tume ya Marais ambayo ndiyo iliyotuwezesha kukutana leo.

(iii) Uhusiano wa Vyama vya Siasa vya CCM na ANC

Vyama vya ANC na CCM vina mahusiano mazuri na Viongozi wa vyama hivyo wamekuwa wakikutana mara kwa mara kwa ajili ya kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati yao.

(iv) Mikataba ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini

Tanzania na Afrika Kusini zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hadi sasa, Tanzania na Afrika Kusini tayari zimetia saini Mikataba ya Ushirikiano (MoU) kumi na tano (15), ambayo inagusa sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, sayansi na teknolojia, uwekezaji, utamaduni na kilimo.

(v) Ushirikiani katika Utatuzi wa Migogoro katika Kanda

Tanzania na Afrika Kusini zimeendelea kufanya kazi pamoja katika juhudi za utatuzi wa migogoro na kuhakikisha kwamba Afrika inakuwa sehemu salama. Nchi hizi mbili zimeshiriki katika kutatua migogoro nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Sudan Kusini. Tanzania na Afrika Kusini zote zimechangia Askari katika Brigedi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia Amani na Usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (United Nation Force Intervention Brigade-FIB) kwa lengo la kutuliza uvunjifu wa amani Mashariki mwa Kongo. Vile vile, nchi hizi mbili kwa pamoja zimekua zikishirikiana katika kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Sudan Kusini.

(vi) Uhusiano katika Nyanja za Uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika Kusini

Ø Uhusiano ya uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika Kusini umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huo mzuri umezidi kuchochea na kurutubisha ushirikiano wetu wa muda mrefu na wa kihistoria.

Ø Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zinazochangia idadi kubwa ya wawekezaji wa kigeni nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre-TIC) kimesajili jumla ya miradi 226 kati ya mwaka 1990 hadi 2016. Miradi hiyo ina thamani ya Dola za Kimarekani zipatazo Milioni 803.15 na imetoa ajira zipatazo 20,916.

(vii) Uhusiano katika Sekta ya Biashara

Ø Kiwango cha biashara (volume of trade) imekuwa ikiongezeka kila mwaka. Mwaka 2007 ilikuwa Tsh Milioni 976,331 na mwaka 2016 ni Tsh 2,402,211.20. Hili ni ongezeko kubwa na linaleta matumaini ya ushirikiano zaidi.

Ø Bidhaa ambazo Tanzania inauza nchini Afrika Kusini ni pamoja na maua, kahawa, wanyama hai, chai, nguo, pamba, vito vya thamani, tumbaku na mafuta ya kupikia. Bidhaa zinazoagizwa kutoka Afrika Kusini ni pamoja na maziwa na mazao yote ya maziwa, matunda aina ya apple, mbegu za mahindi, mafuta ya soya, sukari kwa matumizi ya viwanda, juisi za matunda, mafuta ya kulainisha mitambo, bidhaa za vileo, Acrylic polymers, lami, magari, pampu za maji, bidhaa za chuma, vitabu, mashine, na trela.

(vii) Mchango wa Madawati wa Afrika Kusini kwa Serikali ya Tanzania

Ø Katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kwa kupitia Ubalozi wake hapa nchini, Serikali ya Afrika Kusini iliweza kuchangia jumla ya madawati 1100 kwa shule za Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. Madawati hayo yalikabidhiwa kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Ø Pamoja na hayo, Serikali ya Afrika Kusini inatarajia kuanzisha programu mahsusi ya kubadilishana walimu na uzoefu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuinua sekta ya elimu.

4.0. TAARIFA FUPI KUHUSU TUME YA USHIRIKIANO YA MARAIS (BI-NATIONAL COMMISSION) KATI YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI

Sasa naomba niwape taarifa fupi kuhusu Mkutano wa Tume ya Ushirikiano ya Marais

(i) Tanzania na Afrika Kusini zilisaini Mkataba wa kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano ya Marais (Bi-National Commission-BNC) tarehe 19 Julai 2011 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi. Tume ya Ushirikiano ya Marais imechukua nafasi ya Tume ya Uchumi ya Pamoja ya Marais (Presidential Economic Commission-PEC) iliyoanzishwa mwaka 2005. Kama nilivyosema awali, Mkataba huu ulisainiwa wakati wa ziara ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano, Mhshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

(ii) Mkataba wa kuanzisha BNC umeainisha maeneo kumi (10) ya ushirikiano ambayo ni Biashara na Uwekezaji (Trade and Investment), Maendeleo ya Miundombinu (Infrastructure Development), Kilimo (Agriculture), Elimu, Sayansi na Teknolojia (Education, Science and Technology), Ulinzi na Usalama (Defence and Security), Habari, Utamaduni na Michezo (Infrastructire, Culture and Sports), Afya (Health), Nishati na Madini (Energy and Minerals) na Maliasili na Utalii (Natural Resources and Tourism).

(iii) Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Mashirikiano ya Marais (BNC) unatarajiwa kufanyika kuanzia leo, tarehe 8 hadi 11 Mei, 2017. Mkutano wa Marais utatanguliwa na vikao vya Makatibu Wakuu tarehe 8 na 9 Mei, 2017 ukifuatiwa na Mkutano wa Mawaziri tarehe 10 Mei, 2017. Mkutano wa Marais utafanyika tarehe 11 Mei, 2017 ambapo Mheshimiwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Rais Zuma watakuwa Wenyeviti Wenza wa Mkutano huo.

(iv) Wakati wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Marais, Mikataba ifuatayo inatarajiwa kutiwa saini:-

(a) Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Masuala ya Bio Anuwai na Uhifadhi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini (Memorandum of Understanding between the Government of the United Republic of Tanzania and the Government of the Republic of South Africa on Cooperation in the Field of Biodiversity Conservation and Management);

(b)Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Maji kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini; na

(c) Hati ya Makubaliano katika Sekta ya Uchukuzi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini;

(v) Pia kuna Mikataba mingine inaendelewa kufanyiwa kazi na mara itakapokamilika, Mawaziri wa sekta husika watasaini. Mikataba hiyo ni pamoja na wa Sekta ya Utalii, Sekta ya habari, Sekta ya kilimo, sekta ya afya, niitaje hiyo tu kwa sasa.

(vi) Tofauti na Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC), Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) inashirikisha Marais wa Nchi mbili ambapo katika JPC inaishia katika ngazi ya Mawaziri. Ushiriki wa Marais katika Tume ya Pamoja ya Ushirikiano unatoa uzito wa pekee katika utekelezaji wa maeneo ya mashirikiano yaliyoafikiwa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 
08 Mei, 2017

Tanzania na Afrika Kusini za dhamiria kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

$
0
0
Wataalamu wa Tanzania na Afrika Kusini wapo katika mkutano wa siku nne wa kuandaa mpango bora wa kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi hizo.

Mkutano huo unaojulikana kama Tume ya Ushirikiano ya Marais (Bi-National Commission-BNC) umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima jijini Dar Es Salaam leo.

“Mkutano huu ni muhimu sana kwa kuwa licha ya nchi zetu kuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri tokea enzi za ubaguzi wa rangi, lakini bado utakuwa chachu ya kuimarisha na kuharakisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika maeneo tutakayokubaliana na wenzetu” Balozi Mlima alisema.

Balozi Mlima alieleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zilikubaliana kuanzisha Tume ya Marais ya Uchumi (Presidential Economic Commission-PEC) mwaka 2005 na mwaka 2011 nchi hizo zilisaini BNC ambayo ilichukuwa nafasi ya PEC. Tokea uwekaji saini wa makubaliano hayo, chombo hicho hakikuweza kukutana licha ya kuwa, makubaliano hayo ndiyo yatakuwa mwongozo katika majadiliano yatakayoendelea hadi tarehe 11 Mei 2017.

Kwa mujibu wa Balozi Mlima, uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaendelea kuimarika kadri siku zinavyokwenda. Kwa takwimu zilizopo takribani makampuni 226 ya Afrika Kusini yamewekeza nchini mtaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 803.15 na kuajiri zaidi ya watu 20,917. Alisema idadi ya makampuni inaweza kuongezeka kwani kuna makampuni mengi mapya kutoka Afrika Kusini yameshaonesha dhamira ya kuwekeza nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, Bw. Edward Makaya alieleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini hazijafanya vya kutosha kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kijamii. Alisema hadi wakati huu nchi hizo zimesaini makubaliano na mikataba takribani 14 ambayo ni michache ukilinganisha na urafiki na udugu uliopo baina ya nchi hizo.

Hivyo, alisistiza umuhimu wa kikao hicho kufanya majadiliano yatakayowezesha uwekaji saini wa mikataba mingi zaidi. Alisisitiza umuhimu wa mikataba hiyo kuzingatia maslahi ya pande zote.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 08 Mei, 2017

Wizara ya Afya Yatoa TAHADHARI Kuhusu Matapeli wa AJIRA

PICHA: Makamu Wa Rais Awatembelea Wanafunzi Walionusurika Katika Ajali Iyoua Walima na Wanafunzi 35 Arusha

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Sadia Isamel Awadhi mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Sadia ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent (Picha na Ofisi ya Maku wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Doreen Mshana mwenye umri wa miaka 13ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Doreen ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent (Picha na Ofisi ya Maku wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Godfrey Tarimo mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Godfrey ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent (Picha na Ofisi ya Maku wa Rais)

Chupa 60,000 za Bia Zatengenezwa kwa Kutumia Lita 50,000 za MKOJO

$
0
0
Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmak kimetengeneza bia mpya kwa kuchanganya ngano na lita 50,000 za mkojo.

Hata hivyo bia hiyo haitakuwa na mkojo wa binadamu.

Mkojo huo ulikusanywa kwa watu waliokuwa kwenye hafla moja kubwa zaidi ya muziki barani ulaya miaka miwili iliyopita

"Wakati habari ziliposambaa kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe, watu walidhani kuwa tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kwenye pombe," alisema Mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus inayotengeneza pombe hizo.

“Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria warsha hiyo ya muziki mwaka 2015.

Lita hizo 50,000 zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.
Mashine iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja kwa kutumia nguvu za miale ya jua.

Chanzo BBC.

Zitto: Nimeomba mkataba rasmi wa ununuzi wa ndege

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuna matatizo makubwa katika manunuzi ya ndege aina ya Boeing jambo ambalo limepelekea Mbunge huyo kuomba mkataba wa ndege hiyo bungeni

Zitto Kabwe amesema hayo baada ya gazeti la Jamhuri kuandika taarifa juu ya ndege hiyo huku likisema kuwa Zitto Kabwe ameshindwa na kudai anapotosha Umma juu ya taarifa za ndege hiyo, jambo ambalo Zitto Kabwe analipinga vikali na kusema gazeti hilo linatumika na watu wanaohangaika kuficha ukweli juu ya manunuzi ya ndege hiyo na kusema watake wasitake watajibu tu ukweli.

"Nimeomba mkataba wa ndege hii rasmi Bungeni. Nitawapa mrejesho. Kuna tatizo kubwa kwenye manunuzi haya. Boeing Airplanes wamepaniki sana na wanunuzi, wamekazana kuficha ukweli kuhusu ununuzi wa Ndege hii. Watajibiwa tu, aste aste" alisema Zitto Kabwe

Sakata la Godbless Lema Kubaguliwa Jana Msibani Latua Bungeni

$
0
0
Wabunge wawili wa Chadema, Peter Msigwa wa Iringa Mjini na Godbless Lema wa Arusha Mjini wameomba mwongozo wa Spika kuhusu ubaguzi wa kisiasa uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jumatatu.

Jana Jumatatu jijini Arusha ilikuwa inaagwa  miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha katika ajali ya gari.

Wa kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa fursa Meya wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa salamu za rambirambi.

Lema kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.

Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.

Mwenyekiti wa Bunge  Najma Giga amesema atatoa mwongozo huo baadaye.

Breaking News: Basi la Ally's na Isanzu Coaster Yagongana Uso Kwa Uso

$
0
0
Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na Coaster ya Isanzu uso kwa uso iliyokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama

Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa Coaster ya  Isanzu si nzuri.
 
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema  chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi.

Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,  Dk Rashid  Mfaume  amesema amepokea majeruhi  35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili.

Breaking News: Watu Watano Wafariki Dunia Mkoani Arusha Baada ya Kuangukiwa na Mti

$
0
0
Watu watano wamefariki dunia katika kijiji cha Ngiresi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha  baada ya mti mkubwa kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kuanguka kwa mti huo kumetokana na athari za mvua zinazoendela kunyesha.

Amesema kuwa waliofariki dunia ni watoto watatu ambao walikuwa wanafunzi na vijana wa wiwili. Kamanda huyo amesema taarifa zaidi atatoa hapo baadae.

Balaa: Tembo Wanne Wavamia Chuo Kikuu cha UDOM

$
0
0
likuwa  balaa  leo alfajiri katika maeneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya tembo wanne kutinga chuoni hapo.
 
Watu wamefurika chuoni hapo kuwaangalia lakini polisi wamewazuia kusogea karibu na eneo walipo tembo hao.
 
Msemaji wa Tanapa, Paschal Shelutete amesema tayari wameshaita askari wa wanyapori kutoka Manyoni kwa ajili kuwaondoa tembo hao.
 
Shelutete amesema askari hao wanatarajiwa kufika wakati wowote kuanzia sasa.

Taarifa Toka IKULU: Rais Magufuli Amegawa Magari ya kubebea wagonjwa kwa wabunge Watatu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari mapya matatu ya kubebea wagonjwa kwa Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasaidia wananchi wa maeneo yao ya ubunge.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amekabidhi magari hayo aina ya Land Cruiser Hardtop kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Rukwa Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa waTabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Balozi Kijazi amesema Mhe. Rais Magufuli ametoa magari hayo baada ya kuguswa na kilio cha muda mrefu cha Wabunge hao waliokuwa wakiomba wananchi wao wapatiwe magari ya wagonjwa.

“Mhe. Rais ameamua kuwakabidhi nyinyi haya magari kutokana na vilio vyenu ambavyo amekuwa akivisikia mara kwa mara, Mhe. Keissy umekuwa hata ukitafuta miadi ya kuja kumuona Mhe. Rais kwa suala hili, Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakiyazungumza haya kwa muda mrefu.

“Tunafahamu kila Mbunge katika jimbo lake anahitaji kupata huduma kama hii, na huduma kama hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kwa hiyo sisi Serikali kila tunapopata uwezo basi tunasaidia pale tunapoweza kufikia kwa wakati ule, tulishatoa magari mengine matatu kama haya Chalinze na vituo vingine vya Morogoro.” Amesema Balozi Kijazi

Balozi Kijazi amewapongeza Wabunge hao kwa kupata magari hayo kwa ajili ya wananchi wao na amewasihi kuhakikisha yanatunzwa vizuri ili yadumu muda mrefu na yawahudumie wananchi wote bila kujali dini, kabila, itikadi zao za kisiasa wala makundi.

Kwa upande wao Mhe. Ally Keissy, Mhe. Munde Tambwe na Mhe. Lucy Mayenga wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuitikia kilio chao cha kuwasaidia wananchi magari ya kubebea wagonjwa, na wamempongeza kwa kazi nzuri ya kuwapigania Watanzania wote hasa wenye shida na pia kwa juhudi kubwa za kuleta maendeleo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Mei, 2017
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kati) akiwa na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Alphayo Kidata (Kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu  Bw. Charles Mwankupili (kulia) na  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (mbunge wa Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe na Mhe Lucy Mayenga (wabunge viti maalumu)  baada ya kuwakabidhi magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017.

Taarifa toka BUNGENI kuhusu kukamilika uteuzi wa Wabunge wa CHADEMA Bunge la Afrika Mashariki

$
0
0
1.Tarehe 4 Aprili, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya Uchaguzi wa kuwachagua Wajumbe Tisa (9) wa Bunge la Afrika Mashariki watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo. Katika Uchaguzi huo, Wajumbe Sita (6) kutoka Chama cha Mapinduzi na Mjumbe mmoja (1) kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walichaguliwa. Wagombea wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)walikosa kura za kutosha kuwapatia ushindi.

2.Hivyo, Bunge linapaswa kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ili kuwapata wawakilishi Wawili (2) kutoka katika Kundi la Vyama vya Upinzani ambapo  Chama  Cha  Demokrasia  na  Maendeleo  (CHADEMA) ndicho chenye hakiya kujaza nafasihizo.

3.Katika mazingira hayo na kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni zinazotawala  Uchaguzi huo, na  kwa  mamlaka  niliyonayo  kama Msimamizi wa Uchaguzi nilitoa TAARIFA ya Siku ya Uteuzi na Siku ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali Na. 537 la tarehe 21 Aprili,2017. Taarifa hiyo ilitaja Sikuya Uteuzi(nominationday) wa Wagombea kuwa ni tarehe 03 Mei, 2017 Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni na Siku ya Uchaguzi(electionday) kuwa nitarehe 10 Mei, 2017.

Hata hivyo, tarehe 28 Aprili, 2017 Chama cha CHADEMA kiliandikia barua na kuiwasilisha kwangu siku ya tarehe 2 Mei, 2017 Jioni. Barua hiyo ilitoa maelezo kwamba muda waliopewa kuwasilisha majina ya wagombea kupitia kwenye Taarifa hiyo ni finyu kutokana na kuathiriwa na kuwepo kwa siku za mapumziko ya mwisho wa wiki pamoja na Sikukuu ya Mei Mosi iliyoanguakia siku ya Jumatatu hivyo, kuwepo kwa ugumu wa kufanya vikao vyao.

5.Kutokana na sababu hiyo, Chama hicho kiliomba kuongezewa muda usiopungua wiki mbili ili kiweze kukamilisha mchakato wa uteuzi wa wagombea, kupata uthibitisho wa uraia kutoka Idara ya Uhamiaji na uthibitisho wa sifa za kugombea kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 50 (2) ya Mkataba ikisomwa pamoja na Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania,1977.

6.Kutokana na sababu zilizotolewa, niliongeza muda wa siku 4 kuanzia tarehe 3  hadi tarehe 7  Mei, 2017  ili kukiwezesha  Chama  hicho kukamilisha  taratibu  hizo  za  kisheria  na  hivyo  kukitaka  kuwasilisha kwangu majina na nyaraka za wagombea waliowateua tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni ambayo ni Siku ya Uteuzi wa Wagombea(nomination day).

7.Kupitia  taarifa  hii, napenda  kuujulisha  umma  kwamba  Chama  cha CHADEMA kimewasilisha kwangu majina sita (6) ya Wagombea wa nafasi mbili za ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki. Kati ya wagombea hao wanne (4) ni wanaume na  wagombea wawili (2) ni wanawake. Majina hayo yamewasilishwa kwangu jana tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya mudawaSaa 10 Jionikama nilivyokuwa nimeelekeza.

8.Baada ya hatua hiyo,nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa mujibu Ibara ya 50 (2) ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4 (4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5 (2), (3) na Kanuni ya 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge,ToleolaJanuari,2016.

Matokeo  ya  uzingatiwaji wa  masharti hayo  yameainishwa  katika Jedwali lifuatalo:
TANBIHI:

√-Maana yake sharti husika limetimizwa

10.Uchambuzi huo umebainisha kuwa Wagombea wote wamekidhi vigezo  na  masharti yanayotakiwa kwa  mujibu  wa  Sheria. Hivyo, napenda  kutoa TAARIFA na  KUWATANGAZA wafuatao kuwa Wagombea katika Uchaguzi wa Wajumbe Wawili (2) kupitia Kundi la Vyama  vya  Upinzani kutoka  Chama  cha  CHADEMA  uliopangwa kufanyika tarehe10 Mei,2017:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 10

Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent Ambayo Wanafunzi 35 Walifariki Kwa Ajali Akamatwa

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya siku ya Lucky Vincent  Jumamosi huko Karatu, Arusha.

RPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari

"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha

Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.

PICHA: Tembo Waliovamia Chuo Kikuu cha UDOM Waondolewa

$
0
0
Tembo wakiwa wamejificha kwenye vichaka ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana. 


Kwa mujibu wa taarifa za Wahifadhi wa Wanyamapori inaelezwa kuwa sehemu ya eneo hilo litakuwa ni njia ya tembo (maeneo ya mapito ya wanyamapori) ambayo ilipitika kwa miaka mingi iliyopita na kwamba tembo wana kumbukumbu hata kama walipita njia hiyo kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita. 

Imeelezwa kuwa njia hiyo ya mapito ya wanyamapori itakua ilitumiwa na wanyamapori kuhama eneo moja hadi jengine ikiwemo maeneo ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ruaha, Serengeti, Pori Tengefu la Rugwa na maeneo mengine ya hifadhi na kwamba maeneo hayo mengi kwa miaka ya hivi karibuni yameshaingiliwa na shughuli za kibinadamu ambazo hazisababishi tembo hao kusahau njia hizo au kutokuzitumia tena.
Tembo hao wakiwa ndani ya eneo chuo kikuu hicho cha Dodoma jana. Hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa kusababishwa na tembo hao na taratibu za kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi zimeshaanza kuchukuliwa na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Askari wa Wanyamapori wameanza zoezi la kuwafukuza kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa somo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma namna ya kuchukua tahadhari juu ya ugeni wa tembo hao chuoni hapo.

 Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa mazingira ya chuoni hapo yataendelea kuwa salama kwakuwa tembo hao wapo katika njia yao ya mapito na pengine kumewahi kukucha kabla ya wao kufika mwisho wa safari yao, hivyo kwa msaada wa askari wa wanyamapori ambao wamewasili chuoni hapo itasaidia  kuwaondoa tembo hao waweze kuendelea na safari yao hadi kwenye maeneo ya hifadhi.
Wanafunzi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dodoma walikusanyika wakiwa na shauku ya kuwaona tembo hao.
Msafara wa viongozi mbali mbali wa Serikali ukiambatana na Askari Polisi na Askari wa Wanyamapori ukisogelea eneo walilokuwepo tembo hao kwa ajili ya kuanza kuwafukuza kutoka katika maeneo hayo ya chuo kwenda kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (wa pili kulia), Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete (wa tatu kulia) na maafisa wengine wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wakiangalia eneo walilokuwa wamejificha tembo hao chuoni hapo.
Askari wa wanyamapori wakiingia ndani ya eneo walilokuwa wamejificha tembo hao kwa ajili ya kuanza kuwafukuza eneo hilo kuelekea kwenye maeneo yao ya hifadhi. Imeelezwa kuwa pindi tembo hao watakapofukuzwa kwa milio maalum ya risasi hutafuta njia wanazozijua wenyewe za kurudi kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Tembo hao wakianza kuondoka katika eneo hilo baada ya askari wa wanyamapori kuanza kuwaondoa eneo hilo kwa kutumia milio maalum ya risasi. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

Jipatie Riwaya Hii ya Kusisimua Iitwayo MY LIFE Toka kwa Mtunzi Makini Eddazaria

$
0
0
"Jojo msichana mdogo, anaye achwa yatima na kukabidhiwa jukumu la kumlea mdogo wake Judy ikiwa hana uwezo wa kupata pesa anajikuta akijitoa maisha yake sadaka kwa kuamua kujitumbukiza katika biashara ya madawa ya kulevya badala ya kunufaika kwa biashara hiyo, anajikuta akiingia mikoni mwa askari nchini china na ili kuhakikisha kwamba anaishi vizuri gerezani, anaamua kuwa MSAGAJI wa wasichana wezake. 

"Je atafanikiwa kwa tabia hiyo? Ungana nami kwenye muandishi wako Eddazaria G.Msulwa kwenye simulizi hii ya kusisimua"

==>Jipatie kitabu hichi kupitia WhatsApp namba 0657072588 kwa ofa ya sh 10000 tu, katika mfumo wa soft copy.Au kupitia email eddazariaM@gmail.com.

 Wahi sasa ofa hii ni leo tu 10 May 2017. Endelea kuni support na Mungu akubariki.
 
Nunua kwa MPESA 0768516188 JOYCE MBWAMBO AU TIGOPESA 0657072588 AZARIA MSULWA
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images