Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwakyembe Apiga Marufuku Magazeti Kusomwa Redion na Katika Television

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), jana tarehe 03 Mei, 2017 alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, jijini Mwanza. 

Mhe. Mwakyembe alipokea hotuba na matamko kutoka kwa Mabalozi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zikiwemo Umoja wa Mataifa, UNESCO, Umoja wa Nchi za Ulaya, Baraza la Habari Tanzania, Mfuko wa Vyombo vya Habari na Klabu za Waandishi wa Habari Mikoani.

Katika hotuba yake, Mhe. Mwakyembe aliwahakikishia Wanahabari kwamba Serikali itaendelea kuweka mazingira bora, salama na wezeshi ili kuilea na kuikuza tasnia ya habari. 

Mwakyembe aliwakumbusha wanahabari kwamba Serikali tayari ilishakamilisha utungaji wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa na Sheria ya Huduma za Habari ambazo zote zimekamilika mwaka 2016, hivyo wazizingatie katika utendaji kazi wao.

 Mwakyembe pia aliwasihi wanahabari kuwa wakweli na kuzingatia misingi na maadili katika kazi zao. "Mlinzi wa kwanza wa Waandishi wa Habari ni Mungu, Mlinzi wa Pili ni Kalamu ya Mwandishi mwenyewe hasa anapozingatia maadili ya kazi yake," alisisitiza Mhe. Mwakyembe. 

Mhe. Mwakyembe alielekeza Idara ya Habari ya Habari-Maelezo kuwa na utaratibu wa kukutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari mara kwa mara ili kubadilishana mawazo na kutoa taarifa sahihi za Serikali.

Aidha, Mhe. Mwakyembe aliwashauri wanahabari kuzichukulia taarifa za mitandao ya kijamii kama "tetesi" ambazo huitaji utafiti kabla ya kuzitumia. 

Mhe. Mwakyembe alivitaka vituo vyote vya runinga na redio viwe vinasoma vichwa vya Habari tu vya magazeti na visisome habari hizo kwa kina mpaka kurasa za ndani za magazeti kwa kufanya hivyo kunaathiri biashara za magazeti.

Mhe. Mwakyembe pia alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa hakuna uhuru usio na mipaka hivyo wanahabari watimize  wajibu wao bila husda wala mawaa na kuzingatia misingi ya sheria na taaluma. 

Aidha, Mhe. Mwakyembe aliwaahidi wanahabari wote ushirikiano wa karibu kwa wakati wote na aliweka utaratibu wa kukutana nao mara kwa mara ili kutazitatua changamoto zinazowakabili.

Zitto Kabwe:Serikali inaficha jambo kuhusu ununuzi wa ndege, Boeing 787-8 Dreamliner

0
0
Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli. Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Hivi sasa kuna ushindani mkubwa kati ya Kampuni ya GE ya Marekani na Kampuni ya Rolls Royce Uingereza kuhusu nani apate biashara ya injini hiyo.
 
Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi. Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.

Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili. 

Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei. 

Bahati mbaya Sana mazungumzo hayo yalimhusisha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao. Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya.

Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu. 

Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.

Zitto Kabwe
3/5/2017

Vanessa Mdee adai kuna msanii mkongwe anamchafua

0
0
Vanessa Mdee ameshindwa kuyavumilia yanayomtoka kinywani mmoja kati ya vigogo anaowaheshimu kwenye sanaa ya muziki nchini, hali iliyomsukuma kuanika ya moyoni.

Vee Money ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Duasi’ alioshirikishwa na Legendary Beatz ametumia mtandao wa Twitter kuyatoa ya moyoni dhidi ya kigogo huyo, ingawa hakuweka wazi jina lake.

“Inasikitisha kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” inasomeka tweet ya kwanza ya Vee Money.

Hata hivyo, mwimbaji huyo ameamua kuweka heshima yake mbele na kujiepusha na majibishano kwani kufanya hivyo anaamini kutakuwa utovu wa nidhamu.

Mwaka huu umeendelea kuwa mwaka wa mafanikio ya kupanda zaidi katika ngazi za kimataifa kwa Vee Money, ingawa amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutajwa kwenye orodha ya wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Msanii huyo ameendelea kukubalika ndani na nje ya nchi ambapo amekuwa akipewa mashavu kadhaa kung’arisha nyimbo za wasanii wa nchi za Afrika Kusini na Afrika Magharibi.

Shilole Ataja Sababu Inayomfanya Abadili WANAUME Kama Nguo

0
0
Msanii wa bongo fleva, Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amefunguka zile tetesi za yeye kubadilisha wanaume kama nguo na kusema siyo kweli kwamba yeye anapenda kufanya hivyo ila wanaosababisha yote hayo ni wanaume wenyewe kutotulia.

Shilole amebainisha hayo kupitia kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook ya EATV.

Shilole baada ya kuulizwa swali na shabiki alidai kuwa yeye anapenda sana kutulia ila wanaume ambao huwa anawapata ndiyo huwa hawatulii jambo ambalo linamfanya yeye aonekane hajatulia.

"Sisi wanawake inapotokea upo katika mahusiano halafu ukaachana na mtu huyo unaonekana 'malaya' lakini kumbe siyo kweli wakati mwingine mtu unakuwa unashindwa kuvumilia matatizo ya mahusiano ukaamua kutoka kwenda kwa mwingine kwa kuwa siyo ndoa sasa ya nini niendelee kuteseka katika mahusiano". Alisema Shilole

Mbali na hilo Shilole amesema kuwa amekuwa na bahati mbaya sana kwenye mahusiano kwani mara nyingi kila mwanaume anayempata huwa yeye amewazidi umri jambo ambalo linafanya watu wahisi kuwa wanapenda kutoka na watoto wadogo.

"Kiukweli saizi siwakubali hao Serengeti boys, ila nina bahati mbaya maana kila mwanaume ambaye huwa ninampata unakuta nimemzidi umri kidogo, lakini kweli sipendi hicho kitu, mimi nampenda mwanaume yoyote yule ili tu anatakiwa awe anafanya kazi, hata kama ni mchota maji, mwanaume ambaye hana kazi sina muda naye kwa sasa maana hatakuwa na thamani ya kuwa mwanaume atakuwa ni 'Marioo' na mimi hao watu saizi hawana nafasi kwangu" alisisitiza Shilole

Nay wa Mitego: Remix ya wimbo WAPO ya Rais Magufuli iko tayari

0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo ‘Wapo’ kwaajili ya  Rais John Pombe Magufuli iko tayari na inaweza kuachiwa muda wowote.

Rais Magufuli  aliufungulia  wimbo huo baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na kumtaka rapa, Nay wa Mitego kuongeza baadhi ya maneno katika wimbo huo ili uwaguse watu wengi zaidi.

Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo huo iko tayari na ameongeza vitu vingi ndani ya wimbo huo.

“Kusema kweli wimbo wa Mh Rais umekamilika na muda wowote unaweza kutoka.

“Nimeongeza mambo mengi ndani yake, kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya moto mwingine kwa sababu bado ‘Wopo’ yenyewe inaendelea kufanya vizuri,”

Rapa huyo amedai hawezi kusema ni lini project hiyo itatoka.

Katika hatua nyingine rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumuunga mkono katika muziki wake pamoja na kujitokeza kwa wingi katika tour yake ya  ‘Wapo’ ambayo imeingia ndani ya jiji la Dar es salaam.
A post shared by NayTrueboy (@naytrueboy) on

Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 4, 2017

0
0
Fuatilia hapa matangazo hayo moja kwa moja ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma katika Mkutano wa saba, kikao cha kumi na saba  leo Mei 4, 2017. 

==>Bofya hapo chini  kutazama

Mbunge amwaga chozi bungeni akizungumzia udhalilishaji wa watoto

0
0
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Faida Bakari amemwaga chozi bungeni akielezea udhalilishaji unaofanywa kwa watoto nchini.

Faida akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni jana mjini Dodoma alisema watoto wanadhalilishwa kwa kufanyiwa vitendo vibaya na watu wazima. Aliiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wanaobainika kufanya hivyo.

“Watoto wanaharibiwa mheshimiwa waziri, naomba mchukue hatua kali za kisheria kwa watu hawa. Nilienda Pemba nililia watoto wanaharibiwa maumbo. Mheshimiwa nasema kwa uchungu,” alisema huku akilia na kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuendelea kuzungumza.

Alisema walimu wamekuwa wakiwadhalilisha watoto huko Pemba na kumuomba waziri ashughulikie suala hilo.

“Tumrudie Mungu, unakuta mibaba mizima inawapa mimba watoto na madevu yao mengi wanawatia watoto wenzao mimba,” alisema.

Faida pia alisema wazee wamekuwa wakinyanyaswa katika jamii na kuwataka Watanzania kuwatunza kwa sababu ipo siku nao watakuwa wazee. “Ukiona nyumba zao unalia naomba  mheshimiwa uangalie katika eneo hili la wazee.”

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Suzan Lyimo yeye alisema wazee wametelekezwa katika kambi za kuwahudumia na kuitaka Serikali kuwaangalia.

“Mwaka jana mlisema mtaleta Sheria ya Wazee lakini mwaka huu haikuzungumzwa, hakuna sheria ya wazazi ndiyo maana wazee bado wanauawa,” alisema.

Mtikisiko wa Uchumi: Benki 3 hatarini kufungwa

0
0
Hali ya mtikisiko wa uchumi uliozikumba taasisi nyingi, hasa za fedha sasa unazinyemelea benki tatu ambazo zinaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyokuwa kwa Twiga Bancorp.

Twiga Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi kiwango kinachotakiwa kisheria.

Hali hiyo inazinyemelea taasisi nyingine tatu za fedh; Benki ya Wanawake (TWB), ambayo pia inamilikiwa na Serikali, Ecobank Tanzania na Efatha Bank, ambayo inahusishwa na taasisi ya kidini ya Efatha, kwa mujibu wa uchambuzi wa The Citizen

Benki hizo tatu zimelimbikiza kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 50 ya jumla ya mikopo iliyotolewa, huku kiwango cha Efatha kikifikia asilimia 63.

Wataalamu wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa kuanguka.

Katika toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanzania, Benki ya Dunia ilitahadharisha kuhusu kukua kupita kiasi kwa kiwango cha NPL, ambacho kilifikia asilimia 9.5 mwaka 2016 kutoka asilimia 6.4 mwaka 2015.

Ripoti hiyo iliitaja TIB Development Bank ambayo kiwango chake cha NPL kilikuwa asilimia 38 katika robo ya kwanza ya mwaka 2017.

Hata hivyo, taarifa za fedha za benki za biashara za robo ya kwanza mwaka 2017 zinaonyesha hali ni mbaya zaidi kwa Efatha, TWB na Ecobank Tanzania.

Hussein Machozi Asimulia Alivyofumaniwa na Mke wa Mtu na Kisha Kupewa Kichapo Nchini Kenya

0
0
Msanii Hussein Machozi ambaye sasa amerudi nchini kutoka nchini Italia amefunguka na kusimulia kisa chake cha kufumaniwa alivyokuwa Kenya na kusema kuwa kama asingekimbia huenda mambo yangekuwa mabaya kwake.

Hussein Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel.

"Kwa hiyo tulipofika hotel tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe yule binti ana mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule jamaa alikuja na magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao.

"Wakatuzunguka pale na kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja pale pale alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa hotel na kukimbia. 

"Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa mbaya kwangu" alisisitiza Hussein Machozi 

Mbali na hilo Hussein Machozi anasema alimua kwenda nchini Italia baada ya kuona muziki unampa mawazo hivyo Mungu akamfungulia mlango  mwingine na kuamua kusepa huko, ambako anadai anasoma na kufanya shughuli zingine zinazomuingizia kipato.

Profesa Lipumba Asema Ilikuwa ni MZIGO Mkubwa sana Kumnadi Lowassa......Akanusha Kutumiwa na CCM Kuivuruga CUF

0
0
Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na msajili wa Vyama vya Siasa Prof. Ibrahim Lipumba leo May 4, 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV amesema hakuwa na namba ya Edward Lowassa wakati anajiunga UKAWA.

Aidha, kwenye mahojiano hayo Prof. Lipumba amesema kuwa amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anaiongoza CUF katika kudai haki za wananchi tofauti na Maalim Seif ambaye mara kadhaa ikitokea suala hilo haonekani akisema:

“Mwaka 2000 baada ya Uchaguzi Mkuu tuliingia kwenye maandamano Zanzibar, lakini Maalim Seif alikwenda Uingereza nilikuwa mstari wa mbele.

Prof. Lipumba amesema pia kuwa Maalim Seif amekuwa akidai kila anapokosana na mtu kisiasa kuwa mtu huyo anatumiwa na CCM akitolea mfano wa Ahmad Rashid, akisema:

“Ni kawaida ya Maalim Seif, akikosana na mtu kisiasa anasema anatumiwa na CCM. Rejea mgogoro na Ahmad Rashid".

Akizungumzia kuhusu kumpokea na kumtambulisha kwa viongozi wa UKAWA aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa wakati anatoka CCM, Prof. Lipumba alisema:

“Mbatia ndiye aliyeniunganisha na Lowassa. Sikuwa na namba zake, na wakati anakuja, nilisema wazi suala la rushwa ni mfumo siyo mtu.

“Mzigo mzito anapewa Mnyamwezi, lakini huu wa kumnadi Edward Lowassa ulinizidi uzito, nisingeweza kuubeba."

Wakai huo huo Prof. Lipumba amebainisha kuwa hakuwa na nia ya kurejea katika nafasi yake ya Uenyekiti wa CUF baada ya kujiuzulu, lakini aliombwa na wanachama wa chama hicho.

“Sikuwa na nia ya kurudi kuwa Mwenyekiti CUF ila wanachama waliniomba nirudi baada ya uchaguzi kumalizika na hali kutulia”

Walioonewa Sakata la Vyeti FEKI Wapewa Nafasi ya Kukata Rufaa

0
0
Serikali, imesema watumishi wa umma walioorodheshwa kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki, wakati hawakutakiwa kuwekwa, wakate rufaa.

Kauli hiyo, ilitolewa jana  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Kama mtakumbuka, uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma, ulihusisha vyeti vya kidato cha nne, kidato cha sita, ualimu na taaluma zingine.

“Baada ya uhakiki huo, iliagizwa watumishi 9,932 waliokuwa na vyeti feki, waondolewe katika ajira, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa maana kwamba vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, wathibitishe vyeti vyao kabla ya Mei 15 mwaka huu na mishahara yao isimamishwe hadi uhakiki utakapokamilika.

“Wale watumishi 11,596 waliogundulika kuwa na vyeti pungufu, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vikaguliwe kabla ya Mei 15, mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua.

“Lakini, wale wanaodai kwamba wamewekwa kwenye orodha ya wenye vyeti feki wakati hawakutakiwa kuwa huko, tunawaomba waandike barua za kukata rufaa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa waajiri wao.

“Waajiri hao, watatakiwa kuwasilisha vyeti hivyo Baraza la Mitihani la Taifa kwa ajili ya uhakiki zaidi kabla ya Mei 15, mwaka huu.

“Pamoja na hayo, ieleweke kwamba, baadhi ya watumishi wakati wanaajiriwa, waliwasilisha vyeti vya matokeo mengine ya sekondari na wakati wa uhakiki, walionyesha vyeti vingine.

“Lakini, naomba ieleweke kwamba, hakuna mtumishi wa umma mwenye cheti halali atakayeondolewa katika utumishi wa umma.

“Kuhusu suala la mafao ya watumishi hao, hilo tunaliangalia namna ya kulifanya kwa sababu kuna sheria zinazolisimamia,” alisema Dk. Ndumbaro.

Ajira za dharura
Pamoja na hali hiyo, Dk. Ndumbaro aliwataka wakuu wa idara ambazo huduma zake zimeathiriwa na zoezi la vyeti feki baada ya watumishi kuacha kazi kwa kuwataka kuandika barua kwake ili zitangazwe nafasi za ajira za dharura kwa lengo la kuziba mapengo hayo.

Akizungumzia wizara ambazo taarifa za uhakiki wake hazikutolewa hivi karibuni, alisema zitatolewa Mei 10 mwaka huu baada ya uhakiki wake kukamilika.

Katika hatua nyingine, Dk. Ndumbaro alisema Serikali itaajiri watumishi 1,500 kuanzia sasa hadi mwisho wa Bunge la Bajeti linaloendelea mjini hapa.

Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, ajira hizo zimetolewa ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa umma ulioko katika sekta mbalimbali serikalini.

“Katika hili, waajiri watatakiwa kuhakiki vyeti vya waombaji wote kabla hawajaajiriwa ili kuepuka uwepo wa watumishi wengine wenye vyeti feki,” aliagiza.

Rais Magufuli Ateua Mkurugenzi Mkuu wa TBS

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Egid Beatus Mubofu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Egid Beatus Mubofu umeanza tarehe 02 Mei, 2017.

Prof. Egid Beatus Mubofu aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joseph B. Masikitiko ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Gerson Msigwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Mei, 2017

Chadema wamteua Catherine Ruge kuwa Mbunge

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imemteua Catherine Nyakao Ruge kuwa mbunge viti maalumu kupitia tiketi ya Chadema.

Taarifa iliyotolewa ya Nec imesema kuwa imemteua Ruge baada ya kukamilisha kikao ilichokifanya leo.

Katika taarifa hiyo Nec imeeleza kuwa kikao hicho kilifanywa kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Tanzania 1977 pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Uteuzi wa Ruge umefanyika baada aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Dk Elly Macha kufariki dunia Machi 31, mwaka huu.

Simbachawene Amtetea Rais Magufuli Kuhusu Kauli ya Kuifuta Halmashauri Kama Madiwani Watalazimisha Kumfukuza Mkurugenzi

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Simbachawene amefunguka na kutetea kauli ya Rais magufuli aliyoitoa mkoani Kilimanjaro kuwa atafuta halmashauri hiyo kama madiwani watadiliki kutaka kumtoa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye yeye amemteua.

Akitoa ufafanuzi bungeni Simbachawene amesema kuwa Rais Magufuli alitoa kauli hiyo kwa nia njema kwa kuwa wapo baadhi ya madiwani huwa wanataka kuwaondoa watendaji hao kwa maslahi yao binafsi na kusisitiza kuwa ikitokea hivyo hata kabla ya Rais hajachukua hatua ya kuvunja hiyo Halmashauri yeye ataanza kuivunja.

"Si kweli kwamba kauli ya Rais Magufuli imeleta mkanganyiko, ile kauli Rais amemaanisha pale unapokuwepo mkakati wa Madiwani kutaka kumuondoa Mkurugenzi wa halimashauri kwa maslahi yao binafsi, haya yote huwa yanatokea .

"Rais Magufuli hakusema kauli hiyo kuwalinda wabadhirifu bali pale unapokuwepo mpango mkakati wa madiwani kwa wakurugenzi kwa chuki, ikitokea hivi mimi mwenyewe nitaivunja hiyo halmshauri kabla hata Rais hajafanya maamuzi hayo" alisema Simbachawene

Mwenge Waibua Mzozo Bungeni

0
0

Serikali imesema haina mpango wowote wa kusitisha mbio za mwenge wa uhuru na kwamba dhana ya kutekeleza kitendo hicho kitaendelezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine huku ikiahidi kuwa zoezi hilo litasisitizwa bila kuchoka.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri wa  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde, ndugu Khatib Said Haji aliyekuwa akitaka kujua faida za kuwasha na kuzungushwa kwa mwenge nchi nzima na kama hakuna kwa nini zoezi hilo lisifutwe.

Waziri Mhagama ameendelea kufafanua kwamba Mwenge umesaidia sana katika kukuza ari za maendeleo katika nchi ikiwa ni pamoja na uwekwaji wa mawe ya msingi katika miradi inayoandaliwa na wananchi huku ukiendelea kuhamasisha uzalendo pamoja na umoja ikiwa ni ishara ya kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere.

"Mtanzania yoyote anayemuenzi baba wa Taifa hili halafu akaukataa Mwenge wa uhuru itabidi tumshangae kwa sababu yeye ndiye muasisi na aliuwasha akiwa ana nia umulike wanyang'anyi, wezi lakini pia uangaze maendeleo, kudumisha amani na mshikamano. Mwenge wa uhuru ni tunu kubwa katika uhuru wa nchi yetu hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuuheshimu mwenge" Mhagama alisisitiza.

Pamoja na hayo Waziri Mhagama amefafanua na kuweka wazi pamoja na dosari ndogo ndogo zinazojitokeza wakati wa ukimbizwaji wa mwenge hazitakuwa chanzo cha kusitisha zoezi hilo bali zitatafutiwa ufumbuzi.

"Dosari ndogo ndogo zinazojitokeza tutazitafutia ufumbuzi lakini siyo kusitisha zoezi la kukimbiza mwenge. Mwenge huu wa uhuru utadumu na utakuwa kama chachu ya maendeleao nchini" aliongeza Mh. Mhagama.

LIVE: Tazama Taarifa ya Habari ya TBC Saa mbili Usiku huu wa May 4, 2017

0
0
 Tazama Taarifa ya Habari ya TBC Saa mbili Usiku huu wa May 4, 2017

Meneja Leaders Club apandishwa kizimbani kwa kutotumia mashine za EFD

0
0
Meneja Msaidizi wa Viwanja vya Leaders Club, Emmanuel Chacha (40) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashtaka mawili, likiwamo la kushindwa kutumia  mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Is-Haq Kuppa, wakili kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Kinondoni, Juliana Ezekiel alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 5, 2016 katika ofisi za klabu hiyo zilizopo Ada Estate.

Wakili Ezekiel alidai mshtakiwa kwa kukusudia alishindwa kununua na kutumia mashine hiyo akitambua anafanya kosa kinyume na sheria ya kodi.

Ezekiel katika shtaka la pili alidai meneja huyo akiwa mfanyabiashara wa baa na kukodisha ukumbi kwa kukusudia alishindwa kufuata sheria za kodi.

Wakili Ezekiel alidai upelelezi umekamilika hivyo aliiomba Mahakama kupanga tarehe kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa.

Hakimu Kuppa alisema kwa mujibu wa sheria mashtaka hayo yana dhamana, hivyo alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja anayefanya kazi inayotambulika kwa mujibu wa sheria, ambaye atasaini bondi ya maandishi ya Sh5 milioni.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti, hivyo alipelekwa mahabusu. Kesi imeahirishwa na itatajwa Mei 19.

Binti wa Miaka 35 Ajitokeza Kuwania Urais Nchini Rwanda

0
0
Mwanadada Diane Rwigara, ametangaza azma yake ya kuwania Urais nchini Nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha .

Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.

Amesema, kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha, na kwamba huwezi kusema uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi.

Huyu ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza rasmi nia ya kutaka kugombea urais nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana Mpayimana Philippe aliyetangaza kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green.

Ufafanuzi wa taarifa inayodai Rais Magufuli Ametengua agizo la Waziri Mwakyembe kwa vyombo vya habari kuhusu kusoma magazeti.

Wabunge wa UKAWA waliodaiwa Kumdhalilisha na Kumjeruhi Katibu Tawala wa Dar Washinda Kesi na Kuachiwa Huru

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wa muungano huo baada ya kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.

February 27 2016 katika ukumbi wa Karimjee Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema, mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu walidaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata  mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.

Aidha ameongeza ushahidi wake ulielezea Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi, hivyo hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.

 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images