Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya April 30


Zitto Kabwe ahoji viwango vya ubora wa ndege inayonunuliwa na Serikali aina ya Dreamliner .......Adai zilikataliwa na mashirika mengine

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amehoji viwango vya ndege inayonunuliwa na Serikali aina ya Dreamliner akisema ndege hizo zilikataliwa na mashirika mengine ya dunia kutokana na ubora wake.

Hiyo ni moja kati ya ndege ambazo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imepanga kuzinunua katika mkakati wake wa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Tayari imeshanunua mbili aina ya Bombardier.

Zitto alisema hayo katika mchango wake wa maandishi kuhusu hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano juzi usiku. Mjadala huo wa siku tatu utaendelea Jumanne ijayo ambapo Waziri Makame Mbarawa atajibu hoja za wabunge.

“Ndege hizi zinaitwa ‘Terrible Teens Dreamliners’ ambazo zilikuwa 12 na zilikosa soko kwa sababu ni nzito na hazina viwango,” alisema.

Alisema pia Ethiopia imenunua ndege hizo lakini kwa punguzo kubwa la bei kwa sababu hazikuwa na soko.

“Wajibu wangu kama mbunge ni kuisimamia Serikali na kuhakikisha fedha za Watanzania zinatumika kwa uwazi na kwa umakini. Hivyo naomba maelezo ya Serikali kuhusu suala hili ili Watanzania wajue kama fedha zao zinatumika vizuri,” alisema.

Alisema mwaka jana, Serikali ilitenga Sh500 bilioni kununua ndege na mwaka huu pia kiasi kama hicho na tayari imelipa asilimia 30 ya dola za Marekani 224 milioni kununua Dreamliner.

Zitto alisema kwa miaka miwili, zimetumika Sh1 trilioni ambazo ni alisema ni uamuzi mgumu wakati hakuna chakula katika Ghala la Taifa na watoto wanakosa mikopo ya elimu ya juu kwa sababu tunanunua ndege.

“Bajeti ya mbolea ya ruzuku kwa wakulima wetu imepungua kutoka Sh78 bilioni mpaka Sh10 bilioni kwa sababu tunanunua ndege, fedha ya vifaa tiba na dawa hospitalini ni ndogo kwa sababu tunanunua ndege. Ni maamuzi. Kupanga ni kuchagua,” alisema.

Taarifa Potofu Zinazomuhusisha Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr Asha Rose Migiro

$
0
0
Ubalozi wa Tanzania London umepokea Habari inayozagaa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa instagram ikiwa na nukuu ifuatayo:

''Binafsi bado sijaona umuhimu na mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zaidi ya vingozi kujikusanyia mali na utajiri mkubwa sambamba na kung'an'gania madaraka kwa nguvu. Mfano uchaguzi uliofanyika mwaka 2015 kwa yaliyotokea Zanzibar ni miongoni mwa Athari mbaya kabisa zinazotokona na Muungano,nadhani kila Mtanzania aliyaona"

Ukurasa huo wenyewe jina la UKUTA inaihusisha nukuu hiyo na jina la Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro.

Ubalozi wa Tanzania London unapenda kutumia fursa hii, kuwajulisha Watanzania Waishio Uingereza na Watanzania kwa ujumla kuwa Balozi Migiro ahusiki na nukuu hiyo kama inavyosambazwa.Hivyo ni wazi kuwa wanayoisambaza wana malengo ya kulichafua jina la Balozi Migiro kwa sababu wanazozijua wao.

Ubalozi wa Tanzania London unaendelea kutoa wito kwa Watanzania Waishio Uingereza kutumia muda wao na mitandao ya kijamii kutoa mawazo chanya yatakayo imarisha Muungano wa Taifa letu na mustakabali wa maendeleo ya Nchi yetu na Watanzania wa pande zote za Muungano.

Ubalozi wa Tanzania London
29 Aprili 2017.


Rais Magufuli Ahudhuria Ibada ya Jumapili Katika Makanisa Mawili Tofauti Mjini Moshi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.

Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.

'' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu'' Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewashukuru waumini wa makanisa hayo mawili na watanzania kwa ujumla kwa kusimama pamoja kuliombea Taifa amani iliyowezesha wananchi kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kutokana na sala zao Mwenyezi MUNGU akamuwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli ametoa msaada wa mifuko 100 ya Saruji kusaidia maendeleo ya kanisa Katoliki na Shilingi Milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo ili irekodi nyimbo zake, halikadhalka katika Kanisa la KKKT, Mheshimiwa Rais ametoa mifuko 150 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kanisa hilo na Shilingi milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuunga mkono Rais Magufuli kwa Kuchangia Mifuko hamsini ya Saruji ambapo Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick amechangia mifuko hamsini ya Saruji na Shilingi laki Tano.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani amemshukuru Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kusali kanisani hapo na kuwataka waumini wa kanisa hilo na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea yeye pamoja na Serikali yake ili iweze kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwa Bara la Afrika.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT, Askofu Dr Fredrick Shoo amewataka waamini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kwa mambo yanayofanywa na Rais hususani katika kupambana na maovu, dhuluma na ufisadi vikiwemo na badala yake Watanzania wabadilike na kujijengea mazoea ya kufanya kazi halali na kuwa waaminifu na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.

Aidha, Askofu Shoo amemuomba Dkt Magufuli kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi hususani kwa taasisi za kidini zinzotoa huduma za kijamii zikiwemo zile za Elimu na Afya.

Akijibu Maombi hayo Rais Dkt Magufuli amewaeleza waamini na watanzania kwa ujumla kuwa Serikali inathamini michango ya huduma za kijamii zinazotolewa na Taasisi za dini na kuahidi kuliangalia suala hilo.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Moshi, Kilimanjaro.
30 Aprili, 2017.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 1

Jinsi Kitambi Kinavyopatikana na Jinsi Kinavyoondolewa na Dawa ya Mkataa Kitambi

$
0
0

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.

 Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i.Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii.Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika  mwili  wa  mwanadamu, hali  inayo  sababishwa  na  mtu  kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA  VINAVYO  CHANGIA KULETA  KITAMBI

Vyakula vinavyochangia  kuleta  kitambi ni  pamoja  na :
i.Vyakula  vyenye  mafuta  mengi  kama  vile  nyama nyekundu  (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama  ya  kuku  wa  kizungu  ( iwe  ya  kuchemsha, kukaanga  ama  kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa  mafuta  (chips) pamoja  na  pizza.

ii.Vyakula vyenye wanga mwingi kama  vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate  mweupe.

iii. Vyakula  na  vinywaji  vyenye  sukari  nyingi  iliyo  ongezwa( added  sugar ), kama  vile  soda  na  keki.

iv. Vyakula  vilivyo  tengenezwa  kwa  ngano  na  sukari kama  vile  keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate  mweupe  nakadhalika

v. Pamoja  na  vinywaji  vilivyo  tengenezwa  kwa  kutumia  ngano  kama  vile  bia  za  aina  mbalimbali  na  kadhalika.

Vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu, vikitumiwa  bila  kuzingatia  kanuni  za  mlo  kamili, huchangia  kuleta  tatizo  la  kitambi.

vi. Sababu nyingine ni  kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo(  physical  exercises  )  kwa  muda  mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40  kwa wanaume na >88 cm au 35  kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO  YANAYO  MUWEKA  MTU  KATIKA  HATARI  YA  KUPATWA  NA  KITAMBI
Tumekwisha  ona  hapo  juu jinsi  kitambi  kinavyo  patikana  na  vyakula  pamoja  na  sababu  nyinginezo  zinazo  sababisha  kutokea  kwa  kitambi, sasa  tutazame  mambo  yatakayo  kufanya  uwe  katika  hatari  ya  kupatwa  na  kitambi.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za kitaalamu, mambo  yafuatayo  huwaweka  watu  katika  hatari  kubwa   ya  kupatwa  na  kitambi :

1. Ulaji  mbovu  wa  chakula; Ulaji  mbovu  wa  chakula  ni  ulaji  usio  zingatia  kanuni  za  mlo  kamili. Hapa  mtu  hufululiza  kutumia  chakula  cha  aina  fulani  pekee  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo  za  chakula.  Mfano; mtu  anaweza  kuwa  anakula  mlo  ufuatao :

Asubuhi :  Mchemsho  ama    supu  ya  ng’ombe , chapatti  tatu  na  soda  moja.  Mchana :   Ugali  nyama  choma anashushia  kwa  maji  na  soda.

Jioni :  Mchemsho  wa  kuku  na  bia  mbili  nakuendelea.

Usiku  :  Chips  mayai  au  chips  kuku  au  chips  mishikaki  na  bia.

Mtu  huyu  akiendelea  na  utaratibu  huu  kwa  muda  mrefu, ni  lazima  atapatwa  na  kitambi.

2. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  mafuta  mengi

3. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye wanga  mwingi  

4.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  sukari  iliyo  ongezwa ( added  sugar  ).

5.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vya  ngano.

6.Ulaji  mfululizo  wa   vinywaji  vyenye ngano  na  sukari.

7.Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na viungo  ( physical  exercises  ).

Mhusika  anapokuwa  katika  makundi  yote  yali yotajwa  hapo  juu, hali  huwa  mbaya  zaidi. 

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini, mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitaji.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasihotika  yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

NJIA  ZA  KUONDOA  KITAMBI.
Unaweza  kuondokana  na  kitambi  kwa  kufanya  diet  pamoja  na  mazoezi ya  mwili  na  viungo.

Vilevile  unaweza  kuondoa  kitambi  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  kuondoa  kitambi  na  kuondoa  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

DAWA   ASILIA  YA  KUONDOA  KIAMBI  NA  MAFUTA  MWILINI.
Hii  ni  njia  ya  uhakika  kabisa  ya  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

 Unaweza  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  DAWA  ASILIA   IITWAYO YA  MKATAA  KITAMBI.

 Dawa   hii  ni  ya asili  kabisa
“  Pure  Herbal “, ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote, haina  side  effect kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kabisa  tatizo  la  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

JINSI  DAWA  YA  MKATAA  KITAMBI  INAVYO  FANYA  KAZI.
1.Huyeyusha  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

2.Husaidia  kupunguza  hamu  ya  chakula.

3.Inazuia  kutengenezwa  kwa  seli  za  mafuta  ( fat cells  ) katika  mwili  wa  mwanadamu. Unapokula  chakula  chenye  mafuta  mengi, dawa  hii asilia  hupambana  kuyafanya  mafuta  hayo  yasitengeneze  seli  za  mafuta  mwilini  mwako. Hali  hii  huuepusha  mwili  wako  kuhifadhi  mafuta   yasiyo  hitajika  mwilini.

4. Husaidia  kupunguza  uzito wa mwili  kwa  haraka  sana  endapo  itatumika  pamoja  na  diet  ya  kabechi.

UFANISI  WA  DAWA.
Ufanisi  wa  dawa  hii  ni  wa  asilimia  mia  moja. Dozi  ya  dawa  hii  hutumika  kwa  muda  wa  siki  ishirini  na  moja.

MATOKEO  YA  DAWA:
Dawa  hii  huondoa  kabisa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

BEI  YA  DAWA :
Dawa  hii  inaoatikana  kwa  kiasi  cha  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU  (Tshs. 50,000/=)

MAHALI  TUNAPO  PATIKANA.
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  karibu  na  SHULE  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

KWA  WATEJA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  Tabata, tunao  utaratibu  wa  kuwafikishia  dawa  mahali  popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  MABASI.

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  tunawatumia  dawa  kwa njia  ya  boti.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  NCHI:
Kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA : 0766  53 83 84

TUTEMBELEE:

Leo ni Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ......Mgeni Rasmi Kitaifa ni Rais Magufuli

$
0
0
Rais John Magufuli leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa. Kwa mujibu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), sherehe hizo zitafanyika kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Rais Magufuli aliwasili mjini Moshi juzi akitokea mkoani Dodoma na jana alishiriki Ibada za Jumapili katika makanisa mawili tofauti, na leo anatarajiwa kuongoza maelfu ya wakazi wa Moshi na miji jirani katika kilele cha sherehe hizo za Mei Mosi, huku wafanyakazi wakililia hali bora makazini.

Akizungumza wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Tucta, Yahaya Msigwa alisema, “Tayari tumemwandikia Rais Dk Magufuli kumuomba awe mgeni rasmi, kimsingi sherehe zote kitaifa mgeni rasmi ni yeye...tunazo ajenda za kumpa Rais, lakini moja ya mambo ambayo ni kero ni hili la mikataba ya hali bora kazini, wafanyakazi wengi wanafanya kazi kama vibarua na hawajui haki zao.”

Kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Taifa lilipaswa kuwa na waajiriwa milioni 3.7 katika sekta iliyo rasmi, lakini waliopo ni 650,000 pekee hali inayoashiria kutokuwa na mikataba.

Alitolea mfano wa watumishi wa mashambani pekee nchini Kenya ni zaidi ya 700,000 na Afrika Kusini ni zaidi ya milioni moja na kwamba ipo haja kwa waajiri Tanzania kutafakari upya suala la maslahi ya wafanyakazi wao na rais anapaswa kulisemea hilo.

Tundu Lissu Akomalia Vyeti FEKI Vya Bashite........Aungana na Wanasheria Wenzake Kufungua Kesi Mahakamani

$
0
0
Wakili Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi.

Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye ni Rais wa TLS, alisema uamuzi huo wa kulifikisha mahakamani suala la Bashite umetokana na maazimio ya baraza la uongozi la chama hicho, lengo likiwa ni kulinda utawala wa sheria na uwajibikaji nchini.

Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu, sakata hilo la Bashite halikupatiwa jibu kutokana na ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wote wa umma iliyokabidhiwa kwa Rais John Magufuli Ijumaa kutowagusa viongozi wa kisiasa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wabunge na madiwani.

Katika kufanikisha nia hiyo ya TLS, Lissu aliyekuwa na viongozi wengine wa chama hicho wakiwamo Makamu Rais, Godwin Ngwilimi na Wakili Stephen Kuwayawaya, alisema miongoni mwa hatua walizochukua ni pamoja na TLS kufungua mashtaka binafsi ya jinai dhidi ya mkuu huyo anayedaiwa kuitwa Bashite.

Aliongeza kuwa mkuu huyo wa mkoa, anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya jinai likiwamo hilo la kutumia vyeti feki na kwamba, kazi ya kumshtaki haitachukua miezi bali ni wiki mbili au tatu.

“Kifungu cha 128(2) cha sheria ya Mwenendo wa jinai, sura ya 20 ya sheria za Tanzania kinaruhusu mtu binafsi (pamoja na taasisi, kampuni au mashirika kama TLS) kupeleka malalamiko kwa hakimu mwenye mamlaka pale anapoamini kuna sababu za msingi zinazoonyesha kuwa kosa la jinai limetendwa,”alisema Lissu, akielezea vifungu wanavyotumia kufikisha suala hilo kortini.

Alisema dhana ya utawala wa sheria ina maana pana na kwamba, pamoja na mambo mengine, siyo tu kwamba hakuna mtu aliyeko juu ya sheria, bali pia kila mtu bila kujali cheo au nasaba na hali yake kiuchumi na jamii, yuko chini ya udhibiti wa sheria za kawaida za nchi na hivyo yuko pia chini ya mamlaka ya mahakama za kawaida.

“Kuna tuhuma za muda mrefu sasa kwamba Mkuu huyo wa mkoa ametumia vyeti vya shule ya sekondari visivyokuwa vyake. Yeye… ni Daudi (Albert) Bashite,” alisema Lissu, akiongeza kuwa jina linalotumiwa sasa na mkuu huyo linadaiwa kuwa mwenyewe yupo na ndiye mwenye vyeti halisi, na kitendo hicho ni kosa la jinai.

Akifafanua zaidi, Lissu alisema kifungu cha 120 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kinasema “Mtu yeyote aliye kwenye utumishi wa umma ambaye, wakati akitekeleza majukumu ya ofisi yake akifanya kitendo cha udanganyifu au ukiukaji dhamana huo ungekuwa ni kosa la jinai kama ungefanywa na mtu binafsi au la, anafanya kosa na endapo atapatikana na hatia atapata adhabu ya kifungo cha miaka saba jela.”

Lissu alisema kwa kutumia vyeti vya shule visivyokuwa vyake, na kwa kutumia majina ya mtu mwingine wakati akiwa mtumishi wa umma, mkuu huyo mwenye jina halisi la Daudi Bashite ameathiri imani ya wananchi kwa serikali yao kwa kuajiri na kulinda watu wadanganyifu na wasiokuwa na vyeti halali.

“Mtu huyu amefanya kosa la jinai ambalo kwalo anastahili kushtakiwa mahakamani na endapo atapatikana na hatia anastahili kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria za kawaida za nchi yetu,” alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

Lissu aliongeza kuwa endapo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) atakataa kutoa ridhaa, TLS itamfungulia mkuu huyo wa mkoa mashtaka ya rejea ya kimahakama katika Mahakama Kuu ili alazimishwe kutoa ridhaa hiyo.

Kabla ya kumkabidhi Rais Magufuli ripoti ya uhakiki wa vyeti vya elimu na kitaluma kwa watumishi wa umma nchini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Uatawala Bora, Angela Kairuki, alisema watumishi 9,932 walikutwa na vyeti vya kughushi na kwamba, ripoti hiyo haikuwagusa viongozi wa kisiasa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge na madiuwani.

Hata hivyo, Makamu Rais wa TLS, Ngwilimi, alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Utumishi wa Umma namba 3 na 5, tafsiri ya mtumishi wa umma inawahusisha pia Wakuu wa mikoa na Wakuu wa Wilaya na hivyo kina Bashite walipaswa pia kuhusishwa katika uhakiki huo.


Live: Yanayojiri Moshi katika maadhimisho siku ya wafanyakazi Duniani

$
0
0
Leo ni maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo Tanzania inaunga na nchi nyingine duniani kuadhimisha na Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akiwa ameambatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa.

Bofya hapo chini kutaza tukio hili LIVE kutoka Moshi

Ujumbe wa Diamond Kwa Wasanii Wenzake

$
0
0
Msanii Diamond Platnumz leo Mei mosi ameamua kuwatumia ujumbe wasanii wenzake kwenye bongofleva kwa kuwaandikia kupitia ukurasa wake wa Instagram ushauri wake kwao ili waweze kufanya vizuri kwenye masoko ya nje.
Leo ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa... Siku hizi mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu....pasipo kujua kuwa kila nyimbo ina soko lake na kila mwanamziki anapotoa nyimbo anakuwa na malengo ama plan ambayo kaidhamilia...leo ntakupostia baadhi ya nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na wanaojifanya wajuaji wa Muziki... pasipo kujua kuwa dhamira ama nini yalikuwa malengo yangu....kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani..... sababu yangu kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia...lakini pia kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda, hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina "UKIMUONA" Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine... #SimbaInZambia
A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Rais Dkt. Magufuli aahidi neema kwa wafanyakazi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe Mosi Mei, 2017 amesema Serikali ya  Awamu ya tano imepanga kufanya  nyongeza ya kawaida ya kila mwaka katika mishahara yaani Annual increment, ambayo ilikuwa imesimama kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na promosheni.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema uamuzi wa Serikali wa kuanza kutoa promosheni unatokana na kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa Wafanyakazi hewa  zaidi ya wafanyakzi kumi 19,000 walibainika kuwa wafanyakazi  hewa.

''Yale mambo yote yaliyokuwa pending ikiwa ni pamoja na promosheni kwa sababu tulishindwa,  unaweza kupromoti mfanyakazi hewa hayupo,kwa sababu tungetoa promosheni wakati kuna wafanyakazi 19,000 hewa,maanake tungepromoti na 19,000 na siajabu na watu waliowaandika mule ndio wangeletwa katika mapendkezo ya promosheni'' amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewaonya watumishi ambao wamekuwa wakidanganya umri wa kustaafu ili waendelee kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa siku zao sasa zimekwisha.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amepiga marufuku uhamisho wa Wafanyakazi bila kuwalipa stahili zao kutokana na kuwepo na tabia ya kuwahamisha wafanyakazi bila kuzingatia taratibu hasa za malipo ya uhamisho.

''Sasa niwaombe wafanyakazi yeyote akihamishwa hakuna kuhama mpaka umelipwa pesa ya uhamisho,kuanzia juu mpaka chini,yeyote atakaye kuhamisha mwambie nipe hela yangu ya uhamisho ninapoenda akishindwa usihame kaa hapohapo ufanye kazi'' Amesema Rais Magufuli.

Amesema viongozi wengine wamekuwa wakiwahamisha wafanyakazi  kwa maslahi binafsi au visasi kutokana na maendeleo wanayowapata wafanyakzi

Rais Mgufuli amewahakikishia wafanyakazi kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kuwajali na kuwa  karibu nao katika kutimiza dhana ya utatu ya ushirikiano kati ya Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kwa lengo la kuleta maendeleo.

Aidha, Rais Magufuli amewaeleza wafanyakazi mipango mbalimbali anayofanywa na Serikali katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya ,ujenzi wa Reli ya kisasa, utoaji elimu bila malipo na uboreshaji wa miundombinu katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika mkoa wa Kilimanjaro pia zimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ambapo kauli mbiu inasema,'' Uchumi wa Viwanda uzingatie kulinda Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi''.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Moshi, Kilimanjaro
1 Mei, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 2

Serikali Yatangaza Nyongeza ya Mishahara......JPM Atangaza Ajira 52, 000 Kuziba Pengo

$
0
0
Rais  John Magufuli ametangaza kuwa Serikali yake itatoa nyongeza ya mshahara ya mwaka na kupandisha madaraja ya kazi kuanzia Bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2017/18.

Aidha, amepiga marufuku wafanyakazi wa Serikali kuhamishwa kituo cha kazi bila kulipwa stahiki zake, akisema lengo la hatua hiyo ni kuepusha madai yasiyo na sababu.

Rais Magufuli alisema hayo jana kwenye sherehe za Sikukuu ya Mei Mosi zilizofanyika kitaifa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alisema Serikali ililazimika kufanya ukaguzi wa watumishi wake wote kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu maslahi ya wafanyakazi na kwamba baada ya kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti vya kughushi atakaa na Baraza la Mawaziri kufanya maboresho.

“Acheni tufagie nyumba kwanza, mlitaka nitangaze nyongeza huku wakiwamo watumishi hewa na wasio na vyeti? … Mwaka huu tutapandisha madaraja ya kazi na kuweka nyongeza ya mishahara kuwa sawa na madaraja stahiki ambayo yapo kisheria,” alisema.

Rais alisema mchakato wa kusafisha watumishi wenye upungufu na hewa ulikuwa mgumu, hivyo ni wakati mwafaka kwa ambao wanastahiki kupata promosheni kunufaika, kwani wangefanya kabla kundi la wafanyakazi 19,000 waliondolewa lingekuwapo.

Magufuli alisema pamoja na kuongeza mishahara na kupandisha vyeo, Serikali inatarajia kuajiri zaidi ya wafanyakazi 52,000 ili kuziba mapengo mbalimbali katika utumishi wa umma.

“Mei Mosi si kwa ajili ya Tanzania bali duniani kote. Ni siku ya kukumbushana na kutafakari mambo kuhusu wafanyakazi na kutatua matatizo yanayowakabili, hivyo nimechukua changamoto zenu na ninaahidi kuzifanyia kazi,” alisema.

Alipongeza viongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), kwa kutambua dhamira ya Serikali, hivyo kuwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano ili kuchangia maendeleo ya Taifa.

Aidha, alisema changamoto za kisheria zinazowakabili wafanyakazi, waziri husika atazifikisha bungeni na zikipitishwa atasaini muda huo huo.

“Nawahakikishia kuwa tunaanza ukurasa mpya. Ndiyo maana mnaona hii siku ni tofauti. Serikali tumeamua kuimarisha maslahi ya wafanyakazi. Na nyie muwe tayari kuchapa kazi,” alisema.

Rais Magufuli alisema wafanyakazi ndio injini ya maendeleo katika Taifa lolote kubwa duniani, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Kuhusu fao la kazi, alisema Serikali inalifanyia kazi na kuna mchakato unaendelea mfanyakazi anapoacha ajira kabla ya kustaafu, alipwe sehemu ya mafao.

Akizungumzia bima, alisema Serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha fao la Bima ya Ajira na wadau wameshatoa maoni, hivyo wakati ukifika watapewa taarifa rasmi.

Akijibu hoja ya uhuru wa wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi, alisema suala hilo lilishazungumzwa mwaka jana na lipo kwa mujibu wa sheria na hakuna mwajiri aliye juu ya sheria.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli ameziagiza wizara na taasisi kuunda mabaraza ya wafanyakazi kulingana na mahitaji na kuwa kwa sasa yapo mabaraza 478.

Aidha, alitaka waajiri kutoa mikataba ya ajira kwani ni jambo la kisheria na si hiari.

Akijibu madai ya wafanyakazi baada ya kuhamishwa eneo la kazi, Rais aliwataka wafanyakazi kutohama eneo bila kulipwa stahiki zao, kwani ni kinyume na sheria.

Rais Magufuli alisema hakuna sababu ya mfanyakazi kuhamishwa bila kulipwa, kwani kinachoendelea ni lawama kwa Serikali, jambo ambalo hataki kulisikia tena.

Aidha, kuhusu mfumuko wa bei, Rais alisema Serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha hali hiyo inadhibitika, huku akibainisha kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zitafanikisha mchakato huo.

Halikadhalika Rais alisisitiza kuwa Serikali ina mpango wa kuboresha na kufufua viwanda hali ambayo itachangia kuongezeka kwa ajira.

Alisema kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii jumla ya dola za Marekani milioni 156 zitatumika kujenga viwanda nchini.

TUCTA yataka Serikali kuharakisha fao la kujitoa

$
0
0
Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeitaka Serikali kuharakisha mchakato wa fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ili wafanyakazi wapate haki yao.

Limeitaka pia kuangalia upya makato ya kodi ya mishahara ili yanufaishe watumishi wote na kueleza kuwa kilichopunguzwa mwaka jana kinalinda wafanyakazi wachache wa kima cha chini cha mishahara.

Katibu Mkuu wa Tucta, Dk Yahya Msigwa, alisema hayo kwenye hotuba ya Shirikisho hilo mbele ya Rais John Magufuli kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro jana.

Alisema kwa muda mrefu wafanyakazi wamekuwa wakisubiri upitishwaji wa fao hilo ambalo litawasaidia kujikimu wanapokosa ajira huku akiongeza kuwa kiwango cha kodi ya asilimia tisa kinachotozwa kinanufaisha watumishi wa mshahara wa kima cha chini.

“Tunaiomba Serikali iharakishe kuanzisha fao la kukosa ajira, ili linufaishe wafanyakazi. Kingine vikokoteo vya mafao ya mifuko ya jamii viboreshwe ili watumishi waone matunda ya kuchangia,” alisema Dk Msigwa.

Aliishauri Serikali kufanya maboresho kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo kuunda mifuko miwili wa umma na wa binafsi ili kuondoa mkanganyiko wa vikokoteo uliopo, wingi wa mifuko ya hifadhi na kupunguza muda wa wastaafu kusotea mafao.

Alifafanua, kwamba baada ya Serikali kupunguza kiwango cha kodi ya mishahara (PAYE) kutoka asilimia 11 hadi tisa, TUCTA imebaini wafanyakazi wanaopokea mishahara ya kima cha chini ndio wanufaika wakubwa, huku wenye kima cha juu wakiendelea kubanwa.

Kuhusu wawekezaji, Dk Msigwa alisema wapo wanaokiuka sheria za kazi na kanuni za ajira, ikiwamo kunyima wafanyakazi haki ya kuunda vyama vya kutetea maslahi yao, pamoja ulipaji mishahara kibaguzi.

Alibainisha kuwa wapo wawekezaji wanaolipa watumishi wenye Shahada kutoka nje ya nchi Sh milioni saba na kuwalipa wazawa Sh 700,000.

Aidha, aliiomba Serikali kuzifanyia maboresho sheria za utumishi wa umma zinazohusu uhusiano wa kazi ili ziwawezeshe kupeleka masuala yao kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Masuala ya Kazi (CMA).

Pia aliitaka Serikali kuwezesha majaji kwenda mikoani kumaliza usikilizaji kesi za wafanyakazi kwa wakati na haki itendeke huku akibainisha kuipunguzia majukumu Wizara ya Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu ili ishughulikie matatizo ya wafanyakazi.

Alisema TUCTA inaipongeza Serikali kwa kupambana na rushwa, ufisadi, kuondoa watumishi hewa, kupambana na dawa za kulevya na uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi.

Rais Magufuli Atangaza Kiama Kwa Waliodanganya UMRI wao

$
0
0
RAIS John Magufuli amesema serikali inawachunguza watumishi wa umma waliogushi umri ili wasibaki kwenye utumishi wa umma kwa muda ambao hawakustahili kuwa kazini.

Kadhalika, amesema kuna watumishi wenye miaka 60 na zaidi ambao hawataki kustaafu huku waking’ang’ania ajira na madaraka, na wengine wakijipachika vyeo vya ukurugenzi.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambazo kitaifa zilifanyika jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Rais Magufuli alisema uchunguzi huo wa umri umeshaanza.

“Wako watumishi ambao wamebadilisha umri wao," alisema Rais Magufuli. "Wamebadilisha miaka yao na unakuta ni mzee kabisa, lakini kabadilisha umri.
 
"Kuna watu ambao ni wazee tena kuliko mimi. Wanasema hawaondoki eti ndio wakati umefika, hao nao tunawachunguza.”

Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisisitiza kuwa wapo watumishi wa umma ambao bado wanafanya kazi wakiwa wameshatimiza umri wa kustaafu kwa lazima wa miaka 60 lakini hawataki kustaafu ili kuachia nafasi wegine waajiriwe.

Watoto wa viongozi 
Alisema katika watu walioghushi vyeti, kuna baadhi ni watoto wa viongozi ambao walijipatia ajira bila uhalali huku watoto wa maskini wamekuwa hawaendi kokote, licha ya kuwa na vyeti halisi.

Alisema kwa sababu hiyo serikali ilisimamisha ajira kwa muda mrefu, kwa kuwa wafanyakazi walikuwa ni wengi wakiwemo hewa na wenye vyeti vya kughushi. 

Rais aliwahoji wafanyakazi, “Hivi mlitaka nipandishe mishahara niwapandishie ndani humo na wale wafanyakazi hewa na watu wa kughushi vyeti, ndio maana nilitaka kwanza nisafishe nyumba.

Alisema kwa sasa mwelekeo ni mzuri na atakapopandisha mshahara atafanya hivyo kwa watumishi sahihi na ndio nia ya serikali. 

Alisema wafanyakazi hewa, sio jipu maana halionekani, ila wafanyakazi wenye vyeti feki wapatao 10,000 ndio majipu na ameamua kuwatumbua, maana ndio walikuwepo. Alisema ameshaagiza watu wote ambao wameorodheshwa kwenye orodha ya vyeti feki, wajiondoe ndani ya siku 15.

“Waondoke hata kama ni mtoto wa waziri au wa rais, yeyote anayehusika aondoke. Akigoma apelekwe mahakamani na huko najua kifungo chao sio chini ya miaka saba,” alisema Rais Magufuli. 

Hata hivyo, alisema kwamba anachojua, watumishi hao wenye vyeti feki watajiondoa tu wenyewe kwa kuwa mishahara hawataendelea kupata. 

Rais Magufuli alisisitiza kuwa viongozi wa juu, hawana nia mbaya kufanya uhakiki huo, bali wana nia nzuri, kwani wanataka watumishi ambao wanadai maslahi yao yaboreshwe, yaende kwa watu sahihi.

Rais Magufuli alisema serikali inataka kila kazi iwe na mfanyakazi mwenye sifa stahiki na kama ni ya darasa la saba, afanye mtu mwenye elimu hiyo na sio kughushi cheti.

Alisema serikali imefanya uhakiki huo ili kama ni mtu wa darasa la saba, aombe kwa sifa ya cheti chake na sio kwenda kufoji cheti cha kwenda kufanya kazi ya uuguzi wakati hajafikia sifa hiyo. 

Rais alisema kuna wakurugenzi wa mashirika na taasisi za serikali ambao wameghushi vyeti, halafu wanawanyanyasa watu wa chini ambao hawana vyeti vya kughushi. Alisema watu hao walioghushi, hawastahili nafasi hizo na ndio maana Serikali imeamua kuwaondoa.

Waziri Lukuvi Atishia Kumpasua KITAMBI Mkurugenzi

$
0
0
Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemtahadharisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, John Wanga, kwamba endapo atashindwa kusimamia vema agizo la urasimishaji makazi holela na uandaaji wa hati miliki kwa wananchi, atatumbuliwa.

Alitoa tahadhari hiyo juzi baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa   urasimishaji na uandaaji wa hati za ardhi ambako Halmashauri ya Ilemela imetekeleza kwa asilimia moja kwa kuandaa hati 834 huku viwanja  vingine 16,000  vikiwa vimepimwa bila kuandaliwa hati.

 Lukuvi  ambaye alionekana kukasirishwa na hali hiyo alisema kushindwa kuandaliwa    hati hizo  ndani ya Halmashauri ya Ilemela ambayo ina maofisa ardhi  na watathmini zaidi ya 40 kmeisababishia  hasara   Serikali.

Alisema kazi hiyo ingefanyika ilivyotarajiwa serikali ingepata  mapato ya  Sh bilioni 2.5 kwa mwaka lakini kilichopatikana  ni Sh bilioni 1.3 tu.

“Hakuna halmashauri nchini iliyo na watumishi  wengi wa idara ya ardhi kama Ilemela na Nyamagana mara zote nimekuwa nikifikiria kuwahamishia wilaya nyingine kama Geita kwa Mheshimiwa Rais, Dk. John  Magufuli ambako hakuna hata mmoja.

“Lakini  leo pamoja na wingi wenu mnaandaa hati 834 huku viwanja 16,000 mkishindwa kuvikamilisha kwa muda niliotoa.

“Sasa Mkurugenzi nakuambia kwamba Serikali imewavumilia  vya kutosha na sasa kama hautabadilika kwa muda ambao nimekuongezea kuanzia sasa hadi Juni 30, mwaka huu   tambua kwamba kitambi chako kitapata pancha.

“Wewe mwenyewe utajua namna ya kuiziba pancha hiyo, hatuwezi kuimba wimbo huo huo kila mwaka.

“Kuna  vitu vidogo vidogo vya hapa halmashauri  mnavifinyia kazi lakini suala ambalo ni la muhimu    mnashindwa kukamilisha.

“Nilikuwa namuona mkurugenzi ni mjanja   lakini anachokifanya hapa ni kama kutwanga maji kwenye kinu kwa sababu kodi ya ardhi haikusanywi,” alisema.

 Waziri alisema Halmashauri za Ilemela na Nyamagana  zinatakiwa zikamilishe hatua hiyo  Juni 30, mwaka huu atakapoifunga rasmi na kutangaza ‘masterplan’ ya Jiji la Mwanza ifikapo Agosti.

Aliwataka wananchi kutambua kuwa baada ya kufungwa  urasimishaji makazi haitatokea    tena  fursa ya namna hiyo. 

Alisema wananchi ambao hawatakuwa na hati ya eneo analoishi watahesabika kama wavamizi, hivyo watapoteza haki yao na maeneo hayo yatachukuliwa na Serikali kwa shughuli nyingine. 

Lukuvi alisema Serikali kuu imetenga Sh bilioni 22 kwa ajili ya masterplan ya   Mwanza ambayo itaanza kutekelezwa Agosti mwaka huu,  kazi ambayo  itafanywa na wataalamu kutoka China.

TANESCO: Ni Marufuku Kumtoza Fedha Mteja anayetaka Kubadilishiwa Tarifu kutoka juu kwenda chini

$
0
0
Shirika la Umeme, Tanesco limesema hakuna gharama zozote zinazotozwa kwa mteja anayetaka kubadilishiwa tarifu kutoka juu kwenda chini...

Akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki iliyopita, Kaimu Meneja Masoko wa Shirika hilo nchini, Mussa Chowo alisema mteja anayetaka kubadilishiwa tarifu hatakiwi kutozwa gharama zozote.

Alisema wateja wa kawaida kabisa wanatakiwa kutumia tarifu namba nne ambayo ni lazima matumizi yake ya umeme yasizidi uniti 75 kwa mwezi na gharama za kila uniti ni sh. 100.

Kundi ya la pili ni wateja wa tarifu ya pili ambao hutumia umeme wa uniti sifuri hadi 1,750 ambao hulipia sh. 292 kwa uniti bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

“Tunawaomba wananchi kote nchini kuhakikisha hawachajiwi (hawatozwi) malipo yoyote ikiwa wanataka kubadilishiwa tarifu," alisema Chowo.

"Yeyote atakayetendewa hivyo basi ajue ni kosa la jinai na atoe taarifa kwa ajili ya hatua stahiki kwa aliyetenda kosa hilo.”

Alisema Tanesco imeshatoa elimu kwenye baadhi ya mikoa hapa nchini hasa ile iliyopata miradi ya Rea, lengo likiwa ni kuwapa wananchi elimu ya kutosha juu ya haki zao na matumizi sahihi ya umeme ili kuepuka gharama.

Mbunge Alalamika Baada ya Kutimuliwa na Kuzuiwa Kuingia IKULU Katika Kikao cha Rais

$
0
0
Mbunge wa Moshi Mjini, Japhary Michael, ameeleza kusikitishwa kwake juu ya maofisa usalama kuwazuia yeye na Meya wa Manispaa hiyo kuingia Ikulu ndogo ya Moshi kuhudhuria kikao cha Rais John Magufuli na viongozi wa dini.

Michael ambaye ni wa Chadema, alisema tukio hilo lilitokea juzi baada ya kufika Ikulu kutokana na mwaliko wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kushiriki kikao hicho.

Mbunge huyo alisema aliitika mwaliko huo lakini ghafla akiwa kwenye foleni yeye na Meya wakazuiwa kuingia na kutakiwa warudi walikotoka.

Alisema alifika eneo la tukio saa 6.30 mchana akamkuta Mstahiki Meya akiwa ametangulia kwenye foleni.

“Tulipata mwaliko na tukaheshimu, ila katika mazingira ambayo hayaeleweki tulizuiwa na watu wa usalama na sisi hatukuhitaji kugoma tukaondoka,” alisema.

Alisema jambo la kusikitisha wakati akiwa kwenye foleni na viongozi wa dini, viongozi wa CCM na watendaji wengine wa Serikali, alichomolewa yeye na Mstahiki Meya wakiambiwa hawastahili kushiriki kika hicho.

Alisema Mkurugenzi alijaribu kuwatetea kwa kuwambia ndiye aliyewapa mwaliko kwa maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa, hakusikilizwa kabisa.

“Mimi mbunge sijaumizwa, kwa kuwa nimetimuliwa bali ninasikitika kwa kuwa tunatiwa woga wa kushiriki shughuli za viongozi wetu wa kitaifa hasa wanapofanya ziara katika maeneo tunayowakilisha,”alisema.

Alisema kutokana na tukio hilo, huenda jamii ikawajengea taswira mbaya kwamba hawaheshimu viongozi wa kitaifa pale wasiposhiriki matukio mengine.

“Mimi binafsi nimetafsiri tukio hilo lililonipata kama ubaguzi wa kiitikadi kwa mambo ambayo ni ya kitaifa,” alisema.

Tundu Lissu: Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta) ndo ADAUI Namba Moja wa Wafanyakazi

$
0
0
Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, amesema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta) ndiye adui wa kwanza kwa wafanyakazi.

Lissu ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Nishati na Madini nchini (NUMET) katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani .

Alisema Shirikisho hilo ni mwiba kwa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki za wafanyafakazi kama inavyotarajiwa, badala yake linashirikiana na Serikali kuwanyanyasa.

Kutokana na hali hiyo, Lissu aliwataka wafanyakazi kubadilika katika mitazamo yao ili waweze kudai haki zao na siyo kuziomba kama wanavyo fanya hivi sasa.

“Wafanyakazi badilikeni, haki haiombwi bali inatafutwa, inadaiwa hata ukiona nchi ambazo wafanyakazi wake wanapata raha leo hii walipambana hata kumwaga damu kwa ajili ya kupata haki zao za msingi, acheni kuwa ombaomba wa haki zenu,” alisema.

Alisema ni vigumu kwa wafanyakazi kuomba haki zao kwa watu ambao wamewatesa kwa zaidi ya miaka 50 kwa kuwalipa mishara midogo ambayo pia imekuwa ikikatwa kodi kubwa.

“Wafanyakazo wadogo leo hii wanahangaika na wanahitaji unafuu maana wanakatwa kodi ambayo hupunguza mishahara yao wakati wengine hawatoi hata senti tano katika kodi hali hii inafanya ubaguzi wa hali ya juu,” alisema Lissu.
 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NUMET, Nicodemus Kajungu, alisema kuna haja ya kuundwa wa shirikisho lingine la vyama vya wafanyakazi nchini kutokana na kuonekana kuwa Tucta inawatenga.

“Leo hii sisi vyama ambavyo sio wanachama wa Tucta tumenyimwa nafasi ya kushiriki kule Moshi, hivyo basi ipo haja ya kuwa na shirikisho letu ambalo litasimamia kwa nguvu zote haki zetu na kuboresha maslahi ya wafanyakazi na Tucta iendelee na wanachama wake 12 ilionao sasa,” alisema Kajungu.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kupunguza tumbo, Kuongeza nguvu za Kiume na Mvi

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETIC ni kampuni inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote bidhaa zetu zote zimetengenezwa Kwa mimea na matunda
 
🍉🍓🍇🍅🍊🍒🍍🌴🍐🧀🧀🧀🧀🍅🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍐🍍🌳🍏🍐🌶🍉🍆🍆🍒.
Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi.
1. YODI PILLS _ Ni vidonge vya kuongeza hips na makalio @170,000/=
2. BOTCHO CREAM_ Ni dawa ya kupaka ya kuongeza shepu (hips na makalio) @150,000/=
3. BOTCHO MULT PLUS_ Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza shepu (hips makalio na mapaja) @200,000/=
4. PANNAMAS BREAST_ Ni dawa ya kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walio nyonyesha. Inapatikana kwa Tsh @120,000/=
5. DISCREET_Hii ni kwa ajili ya kuondoa mvi milele na zisiludi tena. @120,000/=
6. BODY BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza mwili mzima na kukupa hamu ya kula vizuri. Inapatikana kwa Tsh @130,000/=
7. LEG BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza miguu kuwa (Chupa ya bia) @120,000/=
8. HAIR GROWTH STIMULATOR_ Ni mafuta ya kulefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo. Yanapatikana kwa Tsh @100,000/=
9. MICRO COMPUTER_ Ni mkanda wa kupunguza tumbo na manyama uzembe. @170,000/=
10.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu.
11.MEN GELY YA KUPAKA. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=. 
12. SHARK POWER. Hii pia ni kwa ajili ya kuongeza maumbile  wastani wa inch 7.5 inapatikana kwa @135,000/=.
15. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana master blashion. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa inapatikana kwa @130,000/=
🌳🍉🍌🍅🍍🍐🍓🍆🍐🍒🍒🍓🍓🍑🍍🍍🍓🍓🍓🍍🍐🍐🍈🍉
         Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani. 
 
Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
 
                 Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
 
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images