Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Samia Suluhu: Kero za Muungano zitatatuliwa kwa mazunguzo ya pande Mbili

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande Mbili kuwa kero chache za Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya kudumisha Muungano huo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Mahojiano na vyombo Mbalimbali vya habari katika kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa tangu Muungano huo uasisiwe umekuwa na manufaa makubwa kwa pande zote Mbili kwani jamii zimefahamiani na kushirikiano vizuri katika shughuli za kiuchumi na za kimaendeleo hasa uimarishaji wa ulinzi na usalama kwa wananchi wa pande Mbili.

Aidha,Amesema hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.

Kuhusu elimu ya Muungano wa Vijana, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande Mbili kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.

Amesema kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.

Makamu wa Rais pia amehimiza makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wastaafu nchini waendelee na jitihada zao katika kuelimisha umma ili kuuelewa vizuri Muungano kwa ajili ya faida ya jamii nzima na ya Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
DODOMA.
25-April-2017

Waziri wa Afya ataja vipimo na dawa za malaria zinazotakiwa kutolewa bure

$
0
0
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku vituo vya Umma kuwalipisha wananchi wanaokwenda kupima maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa kipimo cha MRDT na utoaji wa dawa za mseto (ALUU) zinazotumika kutibu ugonjwa huo kuanzia sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Malaria duniani mjini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema vipimo hivyo ni bure na pia mgonjwa asilipishwe fedha kwa dawa za mseto.

“Napenda kusisitiza vituo vya umma vinavyotumia vipimo vya MRDT kwa wagonjwa wa malaria, vipimo hivyo ni bure na pia mgonjwa asilipishwe fedha kwa dawa za mseto ama yule anayelazwa kuchomwa sindano ya ugonjwa huo….Waganga wakuu wa mikoa na wilaya, hakikisheni kuanzia sasa mnafuatilia wahudumu wote na watakaokiuka agizo hili watachukuliwa hatua za kisheria mara moja”. Alisema Bi. Ummy

Aidha, Bi. Ummy amewataka wananchi kushirikiana na serikali kuwafichua wahudumu wa Afya ambao watawalipisha fedha pindi watakapo kuwa wanapima huduma ya Malaria kupitia kipimo cha MRDT ama watakapohitajika kupewa dawa ya mseto (ALUU), pia amezionya maabara binafsi ambazo  zimekuwa zikifanya kazi zake kwa kuangalia zaidi fedha badala ya maisha ya mtu kama kuwaambia wana maambukizi ya malaria wakati hawana.

Pamoja na hayo, amesema takwimu kutoka katika vituo vinavyotolea huduma za afya zinaonyesha takribani watu milioni 12 wanaugua ugonjwa huo kwa mwaka ambapo katika tafiti hizo mkoa wa Kagera, Geita na Kigoma ziliweza kuonekana na viwango vikubwa vya maambukizo kwa mwaka 2015 na 2016 huku wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kuonekana kuathiriwa zaidi.

Jamhuri Yaomba Kuondoa Kesi Ya Kujifanya Afisa Usalama Aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM Arusha

$
0
0
Upande wa Jamuhuri umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi  ya jijini Arusha kuiondoa kesi ya kujifanya Afisa usalama wa Taifa  na kujipatia chakula  katika hotel moja ya kimataifa jijini Arusha inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo  Bw.

Akitoa ombi hilo Wakili wa Serikali Bi. Grace Madikenya mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha, Mhe. Gwantwa Mwakuga, alisema upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo sababu shahidi mmoja muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18. 
 
 “Sasa tumeona tutamtesa mteja wetu. Hivyo kwa nia njema kabisa tumeamua kuiondoa mahakamani kesi hii, maana miezi hii 18 ni  mwaka mmoja na miezi sita,”alisema. 
 
 Ombi hilo lilipingwa vikali na Wakili wa utetezi, Bi. Edna Haraka na kuiomba mahakama hiyo iendelee na kesi hiyo, kwa madai kuwa upande wa mwendesha mashitaka unatumia Mahakama kama kichaka cha kumnyima haki mteja wao na kumnyanyasa. 
 
Alisema upande huo hauna nia njema na mshitakiwa na kwamba kitendo cha kuiondoa kesi hiyo mahakamani sio mara ya kwanza ni mara ya pili, ambapo ya kwanza waliomba hivyo na mahakama ilipofuta walimkamata mteja wao na kumnyima dhamana. 
 
“Sasa leo tupo katika kusikiliza shahidi wa tatu na badala ya kuleta shahidi walileta maelezo ya shahidi na leo wanakuja na stori ya kuiondoa ili waendelee kumyanyasa mteja wetu. Hapana! Ofisi hiyo ya Mwanasheria Mkuu inatumika vibaya kwa kivuli cha Mahakama,”alisema Edna
 
Wakili huyo alisema serikali ya sasa inasisitiza mpango wa kuharakisha mashauri kusikiliza wa BRN, sasa wakati inafanyika hivyo wengine wanachelewesha kwa sababu zao. 

Hakimu Gwantwa Mwakuga baada ya kusikiliza pande zote mbili, alisema atatoa uamuzi Aprili 28 mwaka huu, ya  kama anakubali shauri liondolewe au la. 

Bw.  Lengai anakabiliwa na shitaka la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa na kujipatia huduma ya chakula na malazi kwenye Hotel ya kimataifa ya Highway ya jijini Arusha.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 26

LIVE: Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano zinazofanyika Dodoma

$
0
0
Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinafanyika leo April 26, 2017 mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

==>Tazama LIVE Tukio hilo hapo chini

Rais Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa Katika Kuadhimisha miaka 53 ya Muungano

$
0
0
Katika kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-

Wafungwa wote ambao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, wawe wametumikia nusu (½) ya vifungo vyao vilivyobaki, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi).

Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi. Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability). Ulemavu huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-

Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.
Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.

Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangik.

Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji na upokeaji au utoaji rushwa.

Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempt robbery).

Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (fire arms, ammunitions and explosives).

Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti au kujaribu kutenda makosa hayo.

Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki, uharibifu wa miundombinu au kujaribu kutenda makosa hayo.

Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002).

Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.

Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mhe. Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.

Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.

Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).

Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.

Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na nyara za Serikali na ujangili (poachers).

Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.

Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe 16/03/2017.

Wafungwa warejeaji wa makosa/wafungwa waliowahi kufungwa gerezani (Recidivists).

Wafungwa 2,219 watafaidika na msamaha huu na wataachiliwa huru. Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Meja Jenerali Projest Rwegasira
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

26/04/2017

Halima Mdee Aomba Msamaha Kwa Kumtukana Spika Job Ndugai

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Halima Mdee jana amefunguka na kuomba radhi bungeni kufuatia kutoa lugha isiyokuwa na staha bungeni wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Halima Mdee wakati akiomba radhi hiyo anasema kuwa siku hiyo ya uchaguzi kulikuwa na matukio ambayo yalikuwa yakiendelea bungeni ambayo yalimpelekea kutoa lugha isiyokuwa sawa kitamaduni za bunge, ambayo ilimgusa Spika wa Bunge na Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala

"Mhe. Mwenyekiti tarehe 4 mwezi wa 4 wakati wa uchaguzi wa EALA kuna matukio ambayo yalikuwa yanaendelea yakanipelekea kuzungumza lugha ambayo kitamaduni za Bunge si sawa na lugha husika ilimgusa Spika wa bunge na Mhe, Kigwangala kwa namna moja au nyingine

"Kama mbunge mzoefu nilitumia jitihada binafsi kuzungumza na kuomba radhi wahusika katika 'individual capacity'lakini vilevile nikaona ni busara kwa sababu haya maneno niliyasema bungeni hivyo kuzungumza pia hapa na kumuomba radhi Mhe. Spika kwa hiyo niliomba huu muda kwa lengo la kumuomba radhi, kumwambia namuheshimu na kumwambia sitarudia" alisema Halima Mdee

Mbali na hilo Halima Mdee aliendelea kuomba radhi kwa wabunge, watanzania pamoja na wananchi wa jimbo la Kawe lakini pia Halima Mdee alisisitiza kuwa michango yake ya bunge itaendelea kama kawaida yake lakini kwa kutumia lugha za staa.   

Kauli ya Nape Nnauye kuhusu CCM kwenye Sherehe za maadhimsho ya Muungano

$
0
0
Ikiwa leo Tanzania inatimiza miaka 53 toka Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964 na kuunda nchi ya Tanzania Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amefunguka na kusema CCM ndiyo waasisi wa Muungano huo.

Mhe Nape Nnauye anakiri kuwa licha ya mapungufu ya hapa na pale katika chama chake hicho lakini bado kinabakia kuwa chama bora cha mfano barani Afrika, Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter

"CCM bado ni Chama bora cha mfano kwa Afrika! Ni imara na kina historia ndefu, nzuri iliyotukuka sana! Ndio waasisi wa Muungano Wetu, tuudumishe" alisisitiza Nape Nnauye

Rais Magufuli: Atakayethubutu Kuuvunja Muungano Atavunjika Yeye

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.

''Muungano ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano  kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.

Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.

Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli  na nchi kavu.

Aidha Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.

Kwa mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.

''Niwahahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla  kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na  kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.

Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.

Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii''

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017

Jukwaa la Wahariri (TEF) Lamkaa Koo Profesa Ibrahim Lipumba......Lamtaka Atoe Maelezo Sakata la CUF Kuvamiwa na Waandishi Kupigwa

$
0
0
Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) limelaani kitendo cha waandishi wa habari kujeruhiwa katika tukio la uvamizi lililotokea katika mkutano wa CUF katika hotel ya Vina kata ya Mabibo ambapo waandishi wa habari walipigwa na kujeruhiwa

Katika taarifa hiyo ya (TEF) imemtaka Profesa Lipumba kujitokeza na kukiri na kuomba radhi kwa waandishi wa habari pamoja na Watanzania kufuatia tukio hilo kama alivyofanya Maalim Seif

"Tunamtaka Profesa Lipumba binafsi atoe kauli kuhusu tukio hili kama alivyofanya Maalim Seif ambaye binafsi aliandika barua rasmi kwa uongozi wa TEF akilaani kupigwa kwa waandishi wa habari na kutoa pole kwa wale waliomizwa na kupata mshtuko" Walisema viongozi wa TEF

Taarifa hiyo ya TEF ilikwenda mbali zaidi na kuwatahadharisha waandishi wa habari, wahariri kuwa wanapaswa kuwa makini pindi wanapokuwa wanaitwa na kundi hili la Lipumba kwa ajili ya kutoa habari zao 

Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia ya Tanzania kuingizwa nchini humo.....Zitto Kabwe Aitaka Serikali Ichukue Hatua

$
0
0
Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya linasema ‘ ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania ‘.

Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.

Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.

Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.

Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. 

Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. 

Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017

Marekani yaanza kujenga mtambo kuzuia makombora ya Korea Kaskazini

$
0
0
Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.

Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju

China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

THAAD ni nini?
  • Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
  • Hugonga kombora la kuliharibu
  • Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
  • Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC

Kauli ya Diamond Baada ya Ray C Kutoka na Wimbo wa "Unanimaliza"

$
0
0
Baada ya Mwimbaji Ray C kuachia wimbo wake wa Unanimaliza, Leo Msanii wa BongoFleva, Diamond Platnumz kupitia account yake ya Instagram ameandika ujumbe huu

"Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….

"Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….

"niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku🙏"

Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali.... Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya.... Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita....niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali....InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku🙏 @rayctanzania
A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Kauli ya Waziri wa viwanda kuhusu Kenya Kupiga Marufuku Gesi ya Tanzania

$
0
0
Leo Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amekiri kupokea taarifa za katazo lililotolewa na serikali ya Kenya juu ya uuzwaji wa gesi zinazotumika majumbani zinazotoka Tanzania na kusema wataalamu wa wizara wanazifanyia kazi taarifa hizo.

Waziri Mwijage ametoa taarifa hiyo wakati alipozungumza na mwandishi wahabari wa Azam Two mjini Dodoma baada ya kuzagaa kwa taarifa za serikali ya kenya kupiga marufuku ya gesi zamajumbani za Tanzania kuuzwa Kenya na kukiri kuwa Kenya wamekuwa na chokochoko kadhaa lakini watahakikisha wanakaa chini kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa juu wa nchi hizi mbili.

==>Msikilize hapo chini akiongea

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 27


Je, Umeathiriwa na Punyeto Kiasi cha Kushindwa Kurudia Tendo la Ndoa???.....Bofya Hapa Kupata Tiba, Pia Tuna Handsome Up ya Kuongeza Maumbile

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETIC ni kampuni inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote. Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi. 
 
1.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu. 
 
2.MEN GELY kupaka. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=.  
 
3. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana masturbation. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa @130,000/=tu.     
 
Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.

Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
 
Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
 
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu

TRA Yakamata Mali za Lugumi

$
0
0
Kampuni  ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.
 
Katika operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar.
 
Aliwataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati.
 
Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za Kampuni ya Lugumi zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli ambapo wanashikilia nyumba za kifahari za mfanyabiashara huyo.
 
“Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba za Lugumi zimefungiwa ni kweli, amefungiwa nyumba zake za kifahari na anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa Gm Dewji naye anadaiwa Sh bilioni 1.8, Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan Construction anadaiwa Sh bilioni 45,” alisema.
 
Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao TRA ndani ya siku 14 na kwamba muda huo ukipita watapewa maelekezo na serikali kama ni kuuza mali hizo ili kufidia madeni yao.
 
Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye hakupenda jina lake litajwe alithibitisha kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na mamlaka hiyo na ghorofa la kifahari lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.
 
“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo nyumba mtakuta alama ambazo huwa Yono wanaweka kwa nyumba inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba tunazoshikilia,” alisema

‘Padri’ wa Kanisa Katoliki afunga ndoa Dar es Salaam

$
0
0
Miaka tisa baada ya kuvuliwa upadri wa Kanisa Katoliki, Privatus Kargendo jana alifunga ndoa na mchumba wake Rose Birusya. Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es Salaam katika misa iliyoongozwa na Padri Stefano Kaombe.

Kabla ya kuvuliwa upadri, Karugendo alikuwa Padri wa Jimbo la Rulenge-Ngara kabla ya Papa Benedict XVI kumvua daraja hilo kwa madai ya kukiuka maadili ya kanisa katoliki.

Septemba 14, mwaka 2008 Karugendo alitangazwa kuwa ni muumini mlei asiye na daraja la upadri tena kupitia hati ya Papa yenye namba Protokali 4182/08.

Ingawa sababu za kuvuliwa kwake hazikuwekwa wazi kwa jamii zaidi ya kusema amekiuka kanuni za kanisa hilo, watu wengi walihusisha tukio hilo dhidi ya andiko lake kuhusu UKIMWI na matumizi ya mipira ya kiume (condoms).

Baada ya kuvuliwa cheo hicho, Karugendo sasa ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo gazeti la Mwananchi.

Waumini waliokuwamo katika misa ya ndoa hiyo, walimpongeza Karugendo na kusema kuwa uamuzi wake wa kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki umeonyesha kuwa hana tatizo nalo licha ya kuvuliwa cheo hicho.

Mapadri wa Kanisa Katoliki hawaruhusi kuoa ikiaminika ili waweze kujikita zaidi katika kushughulikia masuala ya kanisa bila kuwa na kitu cha kuwaondoa humo ikiwa ni pamoja na familia.

Hussein Bashe Aipa Makavu Serikali ya Kenya Kwa Kuzuia Gesi ya Tanzania

$
0
0
Mbunge wa Nzega mjini, Hussein Mohamed Bashe amesikitishwa na Serikali ya Kenya kuweka zuio la kuingiza mitungi ya gesi inayotoka Tanzania kwa kusema ni vizuri nchi hiyo ikaheshimu mikataba ya 'East African Community (EAC)' .

Bashe amesema hayo baada ya serikali ya Kenya kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Andrew Kamau kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya kupikia kutoka Tanzania kupitia mipaka ya nchi hiyo.

"Serikali ya Kenya imezuia gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tanzania kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu 'EAC treaty common'......Dar es salaam 'port and Cost' ya gesi inayotoka Tanzania ndiyo 'competetive edge' ya makampuni ya Tanzania dhidi ya yale ya Kenya uamuzi huu si sawa". Ameandika Bashe kupitia ukurasa wake wa twitter.

Chadema Yakanusha kupoke barua ya bunge Inayowataka Wapeleke Majina ya Wagombea ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kuwa hakijapokea barua yeyote kutoka bungeni ikiwataka kupeleka majina ya wagombea ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Owen Mwandumbya, amesema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinasubiri barua ya maelekezo kutoka bungeni lakini mpaka sasa hakijapokea.

Uchaguzi wa wabunge wa EALA uliingia dosari baada ya wagombea wa Chadema, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje kupigiwa kura za hapana hivyo kukosa wawakilishi wa nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa mpaka sasa hawajapata barua kutoka kwa katibu wa bunge Dkt. Thomas Kashililah kuhusu hatua wanazopaswa kuchukua.

“Tangu umalizike uchaguzi wa awali hatujapata taarifa zozote kutoka Ofisi ya Bunge, tunasubiri barua kutoka kwa Katibu wa Bunge mchakato gani ufanyike ili suala hilo lifikie muafaka,”amesema Mrema.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa kama Chadema watapeleka wagombea waliokataliwa basi wategemee majibu yale yale na kwamba atalazimika kutumia utaratibu mwingine.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images